Makundi ya haki za kibinadamu yaonya kuhusu hatari ya vurugu za hali ya juu katika uchaguzi wa Kenya

Na wafanyakazi wa Sabahi

Februari 08, 2013

 • 16 Maoni
 • Chapisha
 • Panga upya Punguza Ongeza

Hatari ya vurugu za kisiasa nchini Kenya ni "kubwa sana" kuelekea uchaguzi wa mwezi ujao, Human Rights Watch (HRW) ilionya katika ripoti iliyotolewa siku ya Alhamisi (tarehe 7 Februari).

Ripoti ya kurasa 58 kikundi hicho, "Hatari Kubwa: Vurugu za Kisiasa na Uchaguzi wa Kenya 2013", inasema uhaba wa maendeleo ya serikali ya Kenya juu ya mageuzi iliyoahidi na kushindwa kushughulikia ukiukwaji wa haki za kibinadamu zinaoendelea na uliopita vimechangia kuzua mivutano Kenya yote kabla ya uchaguzi mkuu wa tarehe 4 Machi.

Ripoti ya HRW imetokana na kuwasaili watu 225 Kenya nzima, kukiwa na wengi zaidi katika mikoa ya Kati, Pwani, Mashariki, Kaskazini Mashariki, Nyanza na Bonde la Ufa.

Ripoti hiyo inapendekeza kwamba viongozi wa Kenya wachukue hatua za haraka, ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kuwashtaki kwa haki wale wanaohusika moja kwa moja katika kuchochea au kuandaa vurugu, ili kuhakikisha ufanyikaji wa uchaguzi wa amani na haki.

"Vurugu haziepukiki, lakini ishara za tahadhari ziko wazi sana kiasi cha kutostahiki kupuuzwa," alisema Mkurugenzi wa HRW Afrika Daniel Bekele. "Serikali imeshindwa kushughulikia sababu za vurugu ambazo zimezikumba chaguzi za vyama vingi tangu mwaka 1992, na hasa mauaji ya 2007-2008, kwa hivyo hatua za haraka zinahitajika ili kuwalinda Wakenya."

Kiasi cha watu 1,200 waliuawa na kiasi cha 300,000 kukimbia makazi yao wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-2008, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Ripoti inataja mambo ya kawaida Kenya yote kuwa ni: serikali kutokuwa na ari, mfumo wa sheria, na mamlaka mengine kufanya mageuzi ya vikosi vya usalama, kushughulikia ufisadi, kuvunja vigenge vya wahalifu, na kuwawajibisha wale wanaohusika na vurugu. Inasema kuwa, "hali inayokaribia kutojali kabisa sheria" kwa vurugu ambazo zilitokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 imewaacha huru watu waliofanya uhalifu ule kufanya uhalifu mwengine.

"Wahanga wa vurugu wanahisi kuwa haki imewapitia upande, na watu waliosababisha vurugu zile wanahisi wanalindwa dhidi ya sheria," Bekele alisema. "Huu ni mchanganyiko wa hatari sana kwa uchaguzi unaokaribia."

Ripoti nyengine iliyotolewa tarehe 30 Januari na shirika la kimataifa la haki za kibinadamu Amnesty International ilitoa madai kama hayo.

Ripoti hiyo,"Mageuzi ya Polisi Kenya: Tone moja katika Bahari Kuu"; inataja matukio kadhaa ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na polisi wakizilenga jamii maalumu, na inadai kwamba serikali ya Kenya imefanya machache ili kuwawajibisha maafisa wa polisi wanaohusika.

"Moja ya mfano unaoonekana kwa wingi ni kuwa ongezeko la ubaguzi wa kipolisi na unyanyasaji wa watu wenye asili ya Somalia nchini kote, nchi ikiwa inakumbwa na kukua kwa ubaguzi wa wageni nchini," ripoti ilisema.

Polisi pia wameshindwa kuzuia mashambulizi mfululizo ya Tana River Delta, jambo linalozua "wasiwasi mkubwa kuhusu utekelezaji wa vikosi vya usalama katika hali kama hizo na uwezo wao wa kulinda haki za binadamu za watu wa Tana," kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Kikundi hicho kilionya kwamba kushindwa kwa mageuzi ya polisi kutamaanisha kuwa mfumo ule ule wa polisi uliotumika tangu uchaguzi wa mwaka 2007 ndio pia utakaokuwa na dhamana ya usalama katika uchaguzi ujao.

Mivutano inaizunguka kesi ya ICC

Ripoti ya HRW ilisema kuwa mivutano imekuwa ikiongezwa na kesi inayokuja ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inayowahusu mgombea wa urais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza mwenzake William Ruto kwa madai ya nafasi yao katika kuandaa vurugu za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Kesi hiyo, iliyopangwa kuanza tarehe 11 Aprili, inaweza kugongana na duru ya pili ya uchaguzi wa urais, utakaofanywa ndani ya mwezi ikiwa mgombea atashindwa kupata jumla ya asilimia 51 ya kura zote katika duru ya kwanza.

Msaidizi wa Wizara ya Nchi kwa Masuala ya Afrika Johnnie Carson siku ya Alhamisi aliwaonya Wakenya kuwa "uteuzi una matatizo yake", kama tahadhari ya wazi juu ya uwezekano wa ushindi wa Kenyatta na Ruto, kwa mujibu wa gazeti la The Standard la Kenya.

"Wakenya wanapaswa kujua kwamba watu binafsi wana heshima na pichwa zilizomo katika historia yao na lazima wawe na tahadhari dhidi ya kufanya maamuzi yanayoweza kuathiri kwa njia hasi kwa uchumi wa taifa na mikoa," alisema.

Mwezi wa Disemba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwaonya Wakenya kutochagua viongozi wanaokabiliwa na mashtaka huko ICC, na kusema hatua hiyo inaweza kuathiri mahusiano ya Kenya na nchi za nje.

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

 • fred asienga
  July 17, 2013 @ 05:33:03AM

  Mungu ibariki Kenya. Amin.

 • Reason
  March 25, 2013 @ 02:20:51PM

  There comes a time when what you want does not apply, at that time it is time to accept what is best for your children, now and in the future. Choose peace, say no to any form of loose rapport on the internet. the eyes of the Almighty is squarely on Kenya, His peace is our fortress, after all even the fathers of demoracy like Mandela Nelson had a lot hold on to power but relinquished it to allow others to lead. Whatever the outcome of the case, to most of us who love peacefull coexistance and tolerance, Mungu atabaki kuwa Mungu. All leadership is ordained by God. The good: for a blessing, and the bad as a purnishment, whomsoever triumps, that is the will of God.

 • Dr nthahena
  March 25, 2013 @ 07:07:21AM

  Maoni yangu nikwamba waandishi wahabari huchangia pakubwa kueneza chuki kwa wanasiasa na wana nchi. Hawana dogo kitu kidogoi wanakigeuza kuwa jambo kubwa,waonywe na wakome.

 • joe
  March 21, 2013 @ 06:06:09AM

  Wacheni kasheshe koti itaamua

 • prisca
  March 15, 2013 @ 10:18:02AM

  Kwa mimi, uchaguzi uliibwa

 • Kamau
  March 15, 2013 @ 05:32:37AM

  Enyi watu, kwendeni huko. Kwa nini hamuwezi kuripoti kitu kule kinakotokea. Acheni dhana katika vyombo vya habari...ni ghasia gani mmeona. Hamna aibu, watu nyinyi hamna aibu....

 • Leakey Mutie
  March 14, 2013 @ 11:08:08AM

  huo uchaguzi ulitendeka kwa uwazi na ubainifu wa hali ya juu. Hata hivyo, wakenya wapaswa kuwa na subira na kuingoja mahakama ya juu itoe uamuzi wake kuhusiana na malalamishi kutoka upande huo mwingine. Hii ndio njia mufti kabisa ya kulinda demokrasia yetu.

 • A sang
  March 13, 2013 @ 08:29:33AM

  Kwa mujibu wangu mimi, uchaguzi ulikuwa mzuri na wa haki.

 • Christine
  March 13, 2013 @ 06:55:14AM

  Haha, mlikuwa mnatarajia vurugu lakini hamkupata chochote.

 • Peris
  March 11, 2013 @ 06:14:05AM

  Makala hii ni aibu ka watu wanaotarajia ghasia nchini Kenya na tumevunjika moyo sana. Tunakujueni na hatuwaheshimu,

 • Maina George
  March 10, 2013 @ 10:20:23PM

  Huu ni upuuzi mkubwa...propaganda za Shirika la Ujasusi la Marekani

 • Axmed yasin
  March 5, 2013 @ 06:55:04PM

  Sidhani kama kutakuwepo na mfumo mpya wa kuzingatia haki.

 • jamaal
  February 20, 2013 @ 02:53:44AM

  Napenda kuwaambia watu wa kenya walilinde taifa lao, kwa umoja na sio kwa kujiingiza katika vurugu. wanapaswa kuheshimu katiba ya nchi yao.

 • MOSES .N.FUNDI
  February 19, 2013 @ 11:43:51AM

  Uvumilivu wa kisiasa ni muhimu katika mfumo wowote wa kidemokrasia, pia haki za mtu binafsi lazima zilindwe kwa gharama yoyote.

 • cuma jaamac cabdi yey
  February 17, 2013 @ 03:06:45AM

  Napenda kuwaambia watu wa Kenya kuwa wanapaswa kupewa uhuru wa kushiriki katika uchaguzi pamoja na kuchagua wale wanaotaka kuwachagua. Pia napenda kusema kuwa watu wa Kenya wanapaswa kuwa na tahadhari juu ya kitu chochote kinachoweza kupelekea vurugu na uharibifu katika nchi hiyo, tunajua kilichotokea katika uchaguzi wa 2006.

 • Adam wamahuwa.niko tabora tanzania
  February 11, 2013 @ 09:44:40AM

  Wakenya wachaguwe wamtakae wazungu hakna mwafrika anae waingilia ktk maswala yao ,wao kwani niwasafi?wazungu niwauwaji wakubwa tena hawafai ,tulisha pata uhuru watuache tujitawale

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo