Desemba 18, 2012
Kila siku karibu wanawake 60 hukusanyika nje ya kituo cha gereza la Shirika la Usalama la Taifa la Somalia (NSA) jijini Mogadishu kuona nini kitawatokea wapendwa wao ambao wanashtakiwa kwa ugaidi, uchochezi au kuunganishwa na al-Shabaab.
Wengi wa wanawake hawa, wanaweza tu kulaani, kwani uhalifu ambao waume zao na watoto wao wa kiume wanashtakiwa kwa niaba ya al-Shabaab vimeangamiza familia zao.
"Ninashuhudia kwa dhati kuwa al-Shabaab waliiwatia kasumba vijana na wanajamii wengine muhimu waliowatumia [kubeba] ukatili wao na milipuko," alisema Leilo Adan Agane, mwenye umri wa miaka 25, mke wa Yonis Said, ambaye amekuwa jela kutoka tarehe 11 Oktoba na bado anasubiri mashtaka.
Alisema mume wake alikamatwa katika wilaya ya Hodan ya jiji la Mogadishu katika operesheni ya mapema asubuhi sana. "Alikuwa na maguruneti matatu ya mkononi na bastola katika umiliki wake. Anashtakiwa kwa kupanga shambulio la kigaidi," aliiambia Sabahi.
"Kwa hiyo, ninakiri kwamba al-Shabaab waliharibu familia yangu wakati walipompa mume wangu silaha kwa kutumia fursa ya kukosa kwake ajira, " Agane alisema. "Ninaeleza kwa masikitiko kuwa ninalaumu jambo hili, na ninawataka wazazi wa Somalia kulinda watoto wao kutoandikishwa uaskari na al-Shabaab, ambao wanaharibu matumaini ya familia za Somalia."
Kwa Hibaq Abdirahman mwenye umri wa miaka 29, mama wa watoto watatu mwenye mimba ya miezi nane, uhalifu wa mume wake umemfanya asiwe na matumaini.
"Ninaomba kwamba [mume wangu] aachiwe kwa sababu anaisaidia familia kifedha na siwezi kuwahudumia watoto wetu na mama, na kaka yangu ana matatizo ya akili na siwezi kumudu kumpeleka hospitali," aliiambia Sabahi.
Abdirahman alisema mume wake alikuwa anafanya kazi kwenye duka ndogo katika soko la Bakara huko Mogadishu. Vikosi vya ulinzi vilimkamata pamoja na wapiganaji wengine wengi usiku wa manane katika wilaya ya Hodan, alisema.
"Sijui amepatwa na nini, lakini ninamkosa," alisema.
Faiza Ibrahim, mwenye miaka 27, alisema mume wake alikamatwa tarehe 7 Novemba baada ya kutupa bomu kwa polisi wa doria wa Somalia katika wilaya ya Heliwa kaskazini mashariki mwa Mogadishu, ngome ya zamani ya al-Shabaab.
Anakwenda gerezani kila siku kumpelekea mume wake chakula, lakini hajawahi kumuona au kuongea naye. Anachoweza kufanya Ibrahim ni kusahau fikra zake.
"Nimesikia kwa waliokuwa wafungwa kwamba mamia ya wafungwa wenzao wamefungwa minyororo katika chumba kikubwa chini ya ardhi kisicho na madirisha, mwanga, matandiko au mablanketi ya kulalia," aliiambia Sabahi. "Wanapewa chakula kupitia kwenye uwazi katika mlango wa chuma […] na wanaweza tu kuona jua saa 4 asubuhi."
Shukri Yusuf Omar, mwenye umri wa miaka 49, mkazi wa mtaa wa Yaqshid wa Mogadishu, alisema kijana wake na mke wake wamekamatwa na kikosi cha upelelezi wiki nne zilizopita. Wanakabiliwa na mashitaka ya kuwahifadhi magaidi nyumbani kwao pamoja na kuficha silaha na vitu vinavyolipuka kwenye shimo lililofichwa katika moja ya vyumba vyao, alisema.
Omar alisema aliomba kwamba mamlaka zimwachie huru kijana wake pamoja na binti aliyeolewa na mwanawe au kuwasomea mashtaka bila kuwachelewesha.
"Ninaweza kuwahakikishia kwamba hakuna hata mmoja kati yao atakayerudia kile walichokuwa wakifanya kwa sababu gerezani sio kama kutembelea mbuga za wanyama," aliiambia Sabahi.
Kituo cha kufungia wahalifu cha NSA, ambacho zamani kilijulikana kama Kituo cha Uchunguzi wa tukio la Chama cha Kijamaa la tarehe 21 Oktoba, kipo katika mlima karibu na makazi ya rais huko Mogadishu ya kati.
Jengo hilo lina ghorofa mbili, moja ikiwa ni kwa ajili ya wafungwa wanawake na ofisi kwa ajili ya maofisa wa utafiti, wakati ghorofa nyingine ikiwa ni ukumbi mkubwa kwa ajili ya wafungwa wanaume, alisema Isse Ali, ambaye anafanya kazi NSA katika idara ya uchambuzi wa data na picha.
Ali alisema wachunguzi hawatumii mbinu za mateso dhidi ya wafungwa, lakini wanawatenga na familia na marafiki wakati wanafanya usaili.
"Mwanzoni mwa kuwekwa mahabusu, mahabusu hao wanazuiliwa kuziona familia zao kwa kipindi fulani na kuachishwa kuwasiliana na watu wengine," Ali aliiambia Sabahi.
Wachunguzi wanakusanya taarifa za nyongeza kwa kutumia maofisa wasiojulikana ambao wanajifanya kama wafungwa, alisema.
Baada ya kukamilika kwa uchunguzi, wafungwa wanapelekwa katika jela kuu karibu na Mahakama ya Benadir wakisubiri kusomewa mashtaka, alisema.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Amani iwe juu yenu nyote. Baada ya mamkizi, nadhani kwamba al-Shabaab ni matokeo ya kukosekana kwa mipango na kudharau kwa viongozi wa Somalia. Hii ni kwa sababu al-Shabaab waliibuka kutoka kusikojulikana kutokana na ombwe la uongozi lililoachwa na viongozi hawa. Kwa hivyo, chochote kinachotokea leo Somalia ni kitu ambacho tumekileta sisi wenyewe. Al Shabaab ni watu ambao ni watumishi wa dini lakini wameifahamu vibaya dini na bado wanaamini kuwa wako katika njia sawa. Ukiiangalia Somalia, watu na hata serikali imeundwa na viongozi ambao wameacha haki ya dini na wako nje ya misingi ya dini. Tumuombe Mungu awaokoe watu wa Somalia dhidi yao na awahurumie na kuwaongoza.
Nawapongeza al-shabbaab kwa juhudi zao za kupinga dhulma na kufru katika nchi ya kiislamu wanayotaka ukafiri uenee,Allah awape ushindi. Pia nanyi Sabahi mnaupinga uislam kwa kuwa vibaraka wa America. Kwendeni kuleee
Sheria ya Kiislamu hailiruhusu hilo, kwa hivyo atawajibika kwa kile kinachotokea.
safsana wahukumiwe hili iwe fundisho kwawengine. Mimi sayi. Mwanza tanzania
kwa maoni askar wa NSA waangalie hukumu stahili dhidi ya wafungwa katika kituo hicho kulingana na makosa yao kwani usitake kuhukumu kitabu kwa kuangalia gamba!!!!!!
Amani iwe juu yenu. Al-Shabaab wana elimu na ninamuomba Mungu awalinde dhidi ya watu hawa. .
Ifike mahari tujiulize kwa nini Al-shabaab wanapingana na serikali yao mimi nadhani nimfumo kandamizi ndio umepelekea yote haya pia hata hawa al shabaab wamekosa elimu ambayo ingewasaidia kudai wanachotaka kwa utaratibu mzuri bila kunja haki za kibinadamu kama kuua watoto,wazee na kina mama wasio na hatia.Mungu inusuru Afrika iondokane na matatizo yayo sababishwa na nchi za Ulaya...poleni kina mama ila msifadhaike maana sheria ni msumeno
Mungu hawasamehe hawajui watendalo
Ninawaomba waajiriwa wote wa serikali kumuua yeyote anayetokana na al-Shabaab bila ya kuwa na huruma nao hata kidogo. Hili ni ombi kwa sababu ikiwa tutawapa msamaha, watasababisha matatizo zaidi siku za mbele.
Dini hii hamuiwezi hata muichukue somalia yote dhwarabba seif haito cmama insha allah
Nadhanii kwamba seriklai ya Somalia haiwezi kufanya chochote ambacho kitakuwa cha manufaa au kuwafurahisha raia wote. Kile walichofanya al-Shabaab, ni Mungu tu anayeweza kuwawajibisha na wanaelewa ni kitu gani.
Al Shabaab ni doa jeusi katika jina la Somalia na ninamuomba Mungu atuepushe na laana yao. Amin Amin.
DUNIA HII INGEKUWA PAHALI PAZURI KAMA WANAWAKE WANGETIMIZA WAJIBU WAO. WAKATI WAUME WAO WANAFANYWA VILEMA, KUULIWA, KUPORWA, KUTEKWA NYARA, KUWAKATILI WAUME WA WANAWAKE NA WATOTO ILIKUWA NDIO KAZI YA KILA SIKU NA TAMU KWAO. WAO NI WASHIRIKA KATIKA UHALIFU NA WAWEKWE NDANI PIA
fanyeni mutakav yo,mi cko upande wowote naamini Allah na Quran ndio hukmu yng
Ninasema kuwa al-Shabaab katu hawatamalizika ndani ya Somalia.
Hawa mabwana wanazikosea familia zao kwa tamaa ya hela . Hebu fikiria mama mwenye watoto kadhaa akipitapita mahakamani kila uchao kuja kusikiza maamuzi ya mahakama! Wanaume tusiwe na tamaa za kipuuzi na kutesa familia zetu.
Kile ambacho al-Shabaab wanafanya sio sahihi, Naomba Mungu awaadhibu.
Kwa kweli akina mama wa Somalia wanakabiliwa na changamoto nyingi, kitu kizuri zaidi kwao ni kuwa wawe wavumilivu licha ya changamoto zote hizo.
Ni jambo la kusikitisha sana lakini makosa yalifanywa na hao wanaume wabinafsi wanaoifanyia kazi al-Qaida nchini Somaia wakijua kwamba wanachofanya si sahihi. Kwa hivyo tunawasikitikia akinamama wa Kisomali ambao waume zao wamefanya makosa. Ningelipenda kuwaambia akinamama hawa kuendelea kustahmilia kwani waume wao wataadhibiwa kwa makosa waliyowatendea watu wa Somalia.
Naamini kile kundi hili linalojiita al-Shabaab linachokiamini hakifahamiki kwa sababu wanaua watu wengi mashuhuri miongoni mwa maulamaa wa Somalia. Kwa hakika wanafanya kila wapendacho kufikia umbali wa kuwachukua wanawake bila ya ridhaa zao. Pili wanawaita wanawake waliowateka kutoka mikoa mingine ya Somalia kuwa wahamiaji kwa njia ya Mungu. Ningelipenda kuwaambia watu wa Somalia wapigane na watu hao hadi wawang'oe kutoka Somalia yote. Amani iwe juu yenu.
Nyinyi ni watu mnaouchukia Uislamu. Mnavitukana wapiganaji wa vita vitakatifu na mnayakashifu majina yao. Je, nyinyi si Waislamu????
Ni wewe hasa, hivyo acha kutushambulia, rafiki yangu. Tuko Berbera.
Ninaomba kutoka kwa serikali ya Somalia iwasaidie akina mama kwa kadiri inavyoweza.
NAIPENDA SANA SOMALIA, MIMI NI MTANZANIA NINAYEIPENDA AMANI,WAPO WATANZANIA WASIOPENDA AMANI,WAJAPO KWENU KUJIFUNZA VITA WAFUNDISHENI HASARA ZA VITA.HASA NDUGU ZANGU WAISLAMU WANAODHANI KWAMBA KUONDOA UHAI WA MTU NI KUFUNGULIWA MILANGO YA PEPONI.
makara hi ni nzuri ila nazani si vyema watuhumiwa hao wakachiwa bila uchunguzi wa kina kwasababu wengi kati yao walifanya maamuzi hayo uku wakikiwa na akili timamu, ni haki yao kuchunguzwa kwa makini ili kuakikisha usalama wa inchi yao na inchi jirani pia. i love somaria mungu ibariki somaria
Makala hii sio mbaya lakini tuna hofu kwamba Wasomali walioko Sudani ya Kusini wanaweza kuwa na ajenda ya siri.
maoni yangu ni kwamba serikali iingilie kati swala hili kwani raia wengi hasa wanawake, watoto na wazee ndio wanaodhurika. nawashauri serikali kuuingilia kati kwasababu ndio chombo pekee kinachofanya nchi iwe na amani
Amani iwe kwenu, ninashangazwa na mtu mjinga, anayetoa mawazo yasiyo na msingi, ninaamini mnaelewa maana yake. Al Shabaab ni jaribio tu kwetu sote na ni sawa na kile kilichotokea katika historia ya zamani katika Uislamu wakati khalifa Ali bin Abi Twalib alipouawa na kikundi cha Waislamu waliojitenga kilichojulikana kama Khwariij, waliokuwa na itikadi potofu.
Wajinga wote hawa lazima wachinjwe kama mbuzi kwa sababu ya vifo visivyo hatia walivyosababisha. Nendeni motoni. fakin
Al-Shabaab ni watu wabaya na wajinga kwa sababu wanawaua ndugu zao Wasomali. Ninapenda kuwataka waache kuua watu na kuungana na serikali.
Amani iwe juu yenu nyote. Hamtakwenda popote kwa vile bado hamuelewi. Wapiganaji watakatifu wana msaada wa Mungu na hawatakuwa na tatizo lolote ikiwa watafungwa lakini wataona sehemu tu ya hukumu maishani. Wakati utakapoasi dhidi ya majasusi hawa ambao wamepewa majina ya rais au waziri mkuu. Al-Shabaab wataendelea kuwepo na katu hawatasita. Hawatasita kwa sababu wataendelea kuwepo na hawatasika kamwe, daima. Wao ni watu wetu, watoto wetu na watakwenda popote. Ushindi ni wao, kwa hivyo iogopee nafsi yako tu.
Alshbab hawafai ktk jamii
Kiukweli hali inatisha familia zinaumia ndugu jAmaa wanapata mateso hasa wanawake na watoto inasikitisha
Ninazungumzia kuhusu njia ambayo Waislamu wameharibiwa. Waligawanywa katika vikundi bila ya wao wenyewe kujua. Enyi Waislamu, amkeni kutoka usingizini na mchukue hatua.
Tunapaswa tuwe na tahadhari ya wanawake hawa kwa sababu wameharibiwa na waume wao. Sio wanaume tu ni magaidi bali hata baadhi ya wanawake ni magaidi pia.
Kwa kweli, hiyo ndio sababau wanawake wengi wa Somalia wana matatizo leo na kwa kweli inahuzunisha. Tunathamini kazi inayofanywa na wanawake wa Somalia ambao wamo katika matatizo na mizozo kwa zaidi ya miaka 20 kwa jamii ya Somalia. Nasikitika kuwaambieni kuwa mvumilie na muwazuwie waume wenu kutoka katika itikadi hii mkiweza au kuzungumza nao kwa kadiri mnavyoweza.
Kwanza napenda kutuma salamu zangu kwa wafanyakazi na uongozi wa tovuti hii popote wanapoishi. Ninawapongezeni sana na ninamuomba Mungu awalipe mema, ndugu zangu. Pili, kwa kweli ninapenda maoni yenu na programu zenu. Endeleeni na moyo huo huo au hata zaidi. Asanteni.
kwanza kabisa nawapa pole wanawake hawa ambao waume zao wako gerezan kwa kushinikizwa na wanamgambo wa al shabaab; kimsing coni kabisa msaada wowote wa uwepo wa mwjesh ya umoja wa mataifa inchin somalia kwan n mateso kila kunapo kucha.
Wooo!, Naapa hii ni nzuri sana, Ni njia ambayo watu hao waliozowea kuwalazimisha watu wengine na kujenga magereza mengi duniani ndio walivyoishia? Kuna watu wengi leo ambao hawana hatia walioko gerezani. Makosa waliyotenda lazima yathibitishwe kwa sababu wachache kati ya watu hao wanaoishi Somalia hawakutenda uhalifu wowote. Waliobaki walikuwa katika vikosi. Kwa maoni yangu, nahisi wale wote waliotenda uhalifu wanapaswa kusamehewa baada ya serikali kuichukua nchi yote.
Wale watakaonekana na makosa makubwa lazima wahukumiwe kifungo cha maisha gerezani wale watakaoonekana na makosa madogo madogo wapewe adhabu ndogo. Utoaji huu wa haki haupaswi kutumika kwa kuwaweka gerezani vijana wote ambao ndio tegemeo la Somalia la siku za mbele kwa sababu walipotoshwa na al-Shabaab lakini naamini wanaweza kurekebishwa tabia.
Ninaliona hili kama uvunjaji wa haki za akina mama wa Somali na hii ni bahati mbaya.
Watu hao wanaowanyonya watu masikini lazima watupwe katika shimo la giza na wasiachiwe, kwa mapendekezo yangu.
Ninapenda kuwaambia wanawake hao ambao waume wao walikuwa washukiwa wa wanachama wa al-Qaida, al-Shabaab au magaidi wawe wavumilivu na wasilione hili kuwa ni tatizo kwa sababu watu wema kuliko wao walinyanyaswa kwa masuala kama hayo na yanayofanana nayo. Ni bahati nzuri kwa waume wenu kulaumiwa kwa kuwa Waislamu wa kweli ambao wamejizuwia kutoka kila kitu kibaya kwa sababu hao wanaojiita serikali hawatamkamata yeyote hadi watakapothibitisha kuwa ni mtu wa dini. Watamtia mikononi mwa makafiri pale tu watapothibitisha. Waombeeni na msiwaombe makafiri na vibaraka wao. Kutoka kwa kaka yenu mpendwa.
Kwa jina la Mungu, nina furaha kuhusu hilo.
09-02-2013 Ni vyema kupata amani na sheria kwa ajili ya serikali kuweza kufanyakazi. Ni Kusema kuwa wakati amani ambayo serikali itaweza kujivunia na serikali inaweza kuwazuwia watu hawa wanaojidai kuwa ni kikundi cha dini. Hawa ni mashetani wasiomti Mungu, Mungu anasema, yeyote anayemuua Muislamu bila ya sababu atapata moto wa jehanamu kama zawadi yake ambako ataoza na atakumbana na ghadhabu za Mungu, Ndio hivyo. Kwaherini.
Kwanza, napenda kupeleka salamu zangu kwa watu wa Somalia. Pili, napenda kutuma salamu zangu kwa watu wanaoishi ambako mimi ninaishi, Somaliland, ambayo kwa siku za karibuni imekuwa ikitoa habari ambazo zinaidhalilisha nchi yetu na ambazo zitaharibu maisha ya vijana wengine ikiwa hakukufanyika kitu kwa haraka kuhusu hilo. Wale wanaoongoza nchi leo wamekuwepo madarakani kwa muda mrefu, kwa hivyo wasiishushie nchi heshima yake leo kwa mikono yao. Waacheni vijana warithi mustakabali mwema kutoka kwenu kwa kuwapa uongozi mzuri vyenginevyo mtajiua nyinyi wenyewe kwa mikono yenu.
Ninasikitishwa na suala hili.
SIKUBALIANI NA MAWAZO KWAMBA LAZIMA MUWASUMBUE WATU KWA SABABU [MAISHA] DUNIANI HAPA NI SIKU CHACHE TU.
Ninafurahishwa sana na kazi hii. Kikundi cha waasi kilikataa kwenda na watu na sasa wanastahiki kukaa mapangoni, wanyunyiziwe petroli na kuwashwa moto. Kwa kweli wananuka na ninawachukia. Mbwa hawa hufumbua macho yao pale tu wanapodai kuwa wao sio wahalifu baada ya kukamatwa. Na tena wanawake wanapobeba magunia makubwa wanapokuja kwenye maeneo ambayo waasi hawa wameshikiliwa. Wanawake wanafanya kazi ngumu sana siku hizi na wao ndio wasafirishaji wa mabomu na bastola. Wanawake hawa wanaonuka ambao hubeba magunia makubwa katika mabegi yao wanapaswa kukamatwa na kuchomwa moto pia. Ndio wao waliokuwa wanatumiwa kwa kuwatia madawa ya kulevya maiti, kwa hivyo wanapaswa kuchomwa ili kusahihisha makosa waliyofanya dhidi ya wanawake na watoto wengi, ambao wamewaulia waume na baba zao. Naomba ghadhabu za Mungu ziwashukie wale wanaowaunga mkono kwa kuandika habari za uongo. Hatujui kama hawa ni Waislamu au makafiri. Jina langu ni Baashi Deeq.
Mungu ailaani kikundi cha Al Shabab Mungu amlaani kila mtu anayewaunga mkono, kuwatia moyo na kushirikiana nao. Mungu amlaani yeyote ambaye hatakilaani kikundi cha al-Shabaab.
Kwa jina la Mungu, mwingi wa Rehema na mwingi wa kurehemu. Jina langu ni Mohamed Abdullahi Nuh. Mimi sio mtu ninayeiogopa serikali inayoongozwa na Ethiopia na ninapenda kuwashambulia wale miongoni mwenu mnaosema tovuti imefutwa au al-Shabaab wameshindwa. Hatujashindwa na karibuni tutakutana tena. Tutapigana mpaka sheria ya Kiislamu itumike Somalia na mnaojipendekeza kwa nchi za magharibi wanapaswa waijue hili. Huyu anayeitwa raisi anatafuta umaarufu lakini hataupata. Kamwe msiote juu ya kushindwa kwa wapiganaji watakatifu na wale miongoni mwenu mnaoandika takataka kuhusu vita vitakatifu mtaadhibiwa karibuni. Waacheni wapiganaji watakatifu na mazungumzo yenu maovu kabla hatujawajieni.
Shetani; Al-Shabaab walifikwa na balaa kama lile la Umoja wa Mahakama za Kiislamu. Mungu tuepushe na wao.
Al shabab wako katika haki na haitatokea hata siku moja batil ikaishinda haki, ninaamini vijana wanajua wanachokifanya na kamwa hawatajuta kwa lolote linalowakuta duniani na akhera. watakaojuta ni wale wanaopigania batil wanaovamia ardhi za waislam kwa maslah ya mabwana zao wamagharib na kwa sababu ya njaa zao na chuki dhidi ya uislam. kuuawa, kufungwa kwa sababu za dini ni ushindi kwetu hata mitume waliuawa na wengine walifungwa mfano nabii Yusuph (as).
noanelea kwamba ata wafungwa wapewe nafasi ya kupiga kura kama ilivyopendekezwa kwani ata nao pia ni wakenya kwani wasna haki zao kama binadamu....... asante kwa haya machache
Ninapenda kuiambia tovuti hii ya Kishetani inayoitwa Sabahi inawaangalieni katika tovuti nyengine bila ya nyinyi kuitafuta, kuwa al-Shabaab itawashinda makafiri na wafuasi wao na kwamba watafutwa duniani. Mungu ametuahidi hilo.
Watu wangapi wameuliwa na watu hawa? Ni maafa gani waliyosababisha? Ni siku za kulala bila kukosa usingizi ambazo wanawasababishia wanaume na wanawake? Hivyo waacheni wapate mgao wao.
Nashangaa na njia ya ukatili na vitisho ambavyo mnalishughulikia suala la wanawake wa Somalia wa Kiislamu ambao wana watoto na wanaume wao katika jela. Ndugu, hayo hayatawaleta watu karibu, hivyo njooni na kitu ambacho kinaweza kuunganisha watu. Asante.
Hili suala la kuhuzunisha kweli ambalo linaweza kusababisha mkwamo mkubwa!
Inaelimisha, tafadhali toeni kopi ya maandishi na kuiuza mjini Nairobi.
Wafungwe maisha
Ninafuraha kwamba mchakato wa ulinzi wa amani ya Somalia unafanyakazi na wahalifu sasa wanajutia yale waliyofanya huko nyuma. Napenda kuwaomba ombi lao lisikubaliwe na wanapaswa waadhibiwe kwa makosa waliyotenda.
Kwa hakika, hili ni suala la kuhuzunisha.
Ole wenu na vyombo vyenu vya habari. Al-Shabaab itaishi na kupata ushindi licha ya nyinyi, Mungu akipenda.
Ninafuraha kuhusu nguvu zilizopatikana na vikosi vya usalama vya Somalia kwa jinsi kinavyoonekana. Ninapenda pia kupendekeza wanaomaliza shule za elimu ya juu kuajiriwa katika jeshi la polisi au wale wazuri ambao kamwe hawako katika makundi ya majambazi au wawatumiaji wa madawa (Mirungi). Kikosi cha watumiaji Mirungi kipelekwe makambini na viongozi wao waangaliwe kwa makini. Asanteni. Mafanikio kwa Somalia.
Nadhani wanapaswa kufikishwa mahakamani na kuchujwa na kupatiwa mafunzo. Pia wanapaswa kufanyiwa uchunguzi wa kiakili na kimaadili.
Mimi ni mvulana wa Kisomali ambaye mwanzoni nilinyanyaswa na al-Shabaab lakini walitaka kuniua wakati wa vita na serikali lakini niliwatoroka mwanzoni mwa mwaka 2011 lakini ninaishi katika nchi ya kigeni tangu wakati huo. Watu hao hao walitaka kuniua kabla ya hapo wakati nilikuwa nikifanya kazi na vyombo vya usalama. inawezekana wao kuniua au kunifunga, napenda kuuliza? Ninauliza swali hili kiukweli kabisa kwani ninaogopa kurejea Somalia.
Wanawake hao walikuwa wanawasubiri waume na watoto wao kuangamiza maisha yao na wengine kabla ya kuweza kuzungumza nao waache matendo yao!?
Hata kama ni bahati mbaya ambayo imeifikia jamii ya kusini mwa Somalia, ni vyema kwetu kufanya kazi kwa pamoja juu ya usalama wa jumla wa nchi na kuzilinda zile jamii dhaifu za Somalia ili tuweze kuwamaliza watu wenye maslahi binafsi nchini Somalia. Ni vyema pia kukumbuka haijawahi kutokea kwa watoto wa mtu ambaye yeye ni mwanachama wa al-Shabaab ambaye ameshiriki katika vita, ni vizuri pia wakati huo huo kufikiria mbali zaidi. Vivyo hivyo. wanawake ambao waume zao ni wanachama wa a-Shabaab ambao ama wamekamatwa au la, ni muhimu kwao kuwasahihisha waume wao kwa sababu ukosefu wa kazi ni bora kwao kuliko kufungwa gerezani au kuacha dini.
Makala nzuri.
Watu wanapaswa kutofautishwa kwa sababu kuna wale ambao hawakutenda uhalifu wowote na wale ambao wameshiriki katika ugaidi.Kwa hivyo, maafisa wanaoielewa kazi hii lazima wafundishe sheria kwa sababu sheria za kimataifa zinasema mtu anapaswa kufikishwa mahamani ndani ya saa 24 tangu akamatwe.
kuhusu al-shabaab wakae chini wazungumze ili wamalize matatizo yao watagombana mpaka lini kama wameshindwa kuelewana un iingilie kati kwani kazi yao un ni nini????
Ninapenda kumfafanua mtu ambaye amelitendea vibaya taifa la Kiislamu kwa ajili ya fedha chache anazopewa na Wakristo. Wale wanaousema vibaya Uislamu wako karibu na makafiri kama vile Abdullahi Yussuf, Siyad Mohamad, Sharif Sheikh Ahmed na wengineo. Leo hii wako katika mikono ya Mungu na Mungu katu hasahau ahadi Yake. Wamewekwa katika moto wa jahanamu unaowaka. Na nyinyi pia ni marafiki zao na ninawaambieni, nyinyi Waislamu au wale waliobarikiwa na Mungu, wasiogope na hawana haja ya kuwa na wasiwasi duniani hapa au kesho akhera. Ikiwa wanamwamini Mungu kwa hivyo hawaoneshi kuwa na tabia unazosema. Waislamu wanajulikana lakini kwa kweli umesema uongo dhidi yao. Ningependa kukuambieni mtakufa kwa chuki zenu. Mmeuza dini yenu na kupata dola 50 za kuwalea watoto wako kutokana na uovu unaosema kuhusu Waislamu wanaofanyakazi katika njia ya Mungu. Naomba Mungu akufikisheni mbele ya sheria karibuni.
Walisema uongo sana.
Kitu ninachosikia kwa kweli ni suala la kuchekesha na si sahihi kwa njia tatu; Kwanza, wanawake wa Somalia wanatarajia kuangalia pale ambapo wataamini juu ya mustakbali wao. Pili, wanamgambo; Al-Shabaab wamekuwa wakiwachukua kwa nguvu wanawake hawa masikini wakati wakielewa kuwa walikuwa wanafanya maovu. Kwa kweli hili ni tendo lisilo huruma la kuharibu mustakbali wa wasichana masikini wakati ukielwa kuwa unaangukia katika shimo. Mwisho, inahitajika kutoka serikalini kuwa dhamana ya watu hawa ambao walidharauliwa kufikiri njia za kuwaelimisha ili wahisi kupata suluhisho kutoka kwa serikali. Huu utakuwa mfano mzuri wa kuonesha kuwa al-Shabaab wameshindwa. Watu wanapaswa wafanye waichukie al-Shabaab na kurekebisha maovu waliyofanya katika njia za kijeshi. Haya ni mafanikio ambayo yanahitajika kujulikana. Hii ni kusema kuwa ikiwa serikali iliyo katika mikono ya wageni itakuja kulielewa hili. Ningependa kumalizia kwa kusema kuwa wanawake wa Somalia wanapaswa kufanywa waelewe kuwa wanaume wao wanabaki katika njia waliyokuwa lakini bado wanapendwa.
Amani iwe juu yenu. Nimefurahi kweli juu ya taarifa yenu kuhusu utendaji kazi wa jeshi jambo ambalo ni sahihi kabisa. Kuna kijana anayesumbuliwa na matatizo ya figo ambaye walimuacha katika mji wa Marka baada ya kuugua. Alichukuliwa kwa gari ya punda na baada ya kufika mjini Mogadishu aliwaona watu ambao alidhani wangemsaidia lakini akafariki siku ile ile ndugu yetu, mwandishi wa habari wa Universal TV; mtoto wa Abdulle aliyeuliwa Medina. Shughuli kama hizo hazina mizizi katika Uislamu. Tunasikitishwa sana juu ya athari za masuala kama haya kwa watu wa Somalia.
Natumai al-Shabaab watamalizwa kabisa. Wacha wote wafariki.