Red_arrow

Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |

Watoto wasio na makazi huko Mogadishu watishia utulivu wa kijamii

Na Majid Ahmed, Mogadishu

Novemba 07, 2012

 • 6 Maoni
 • Chapisha
 • Panga upya Punguza Ongeza

Kama waathirika waliosahaulika wa vurugu na njaa nchini Somalia, watoto wa mitaani jijini Mogadishu wana uwezekano wa kupata matatizo makubwa kama vile magonjwa, matumizi ya dawa za kulevya na unyanyasaji wa kingono -- tatizo ambalo wachambuzi wanasema linatishia utulivu wa kijamii.

 • Kijana akiwa amekaa kwenye lundo la takataka jijini Mogadishu. Watoto wa mitaani mara nyingi hulala kwenye majengo mabovu ya mji mkuu na katika kona za mitaa. [Majid Ahmed/Sabahi]

  Kijana akiwa amekaa kwenye lundo la takataka jijini Mogadishu. Watoto wa mitaani mara nyingi hulala kwenye majengo mabovu ya mji mkuu na katika kona za mitaa. [Majid Ahmed/Sabahi]

 • Watoto wengi wa mitaani wana uwezekano wa kutumia dawa za kulevya na kuwa waathirika wa uhalifu. Kijana aliye katikati akivuta harufu ya gundi. [Majid Ahmed/Sabahi]

  Watoto wengi wa mitaani wana uwezekano wa kutumia dawa za kulevya na kuwa waathirika wa uhalifu. Kijana aliye katikati akivuta harufu ya gundi. [Majid Ahmed/Sabahi]

Wakati kukiwa hakuna takwimu rasmi kuhusu idadi ya watoto wa mitaani, Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) na mashirika ya misaada ya ndani yanakadiria kuwa watoto wapatao 5,000 wanaishi kwenye mitaa ya Mogadishu.

"Inaonekana kuwa idadi yao inaongezeka siku hadi siku," alisema Mohamed Nur Salad wa Mtandao wa Ulinzi wa Mtoto, kikundi cha uhamasishaji kwa watoto. "Kwa sasa kuna maelfu ya watoto wenye umri kati ya miaka saba na 16 ambao wanaishi kwenye mitaa ya Mogadishu, wengi wao ni wavulana."

"Wengi wa watoto hawa wanaishi katika hali ya taabu, wakati wote au kwa baadhi ya nyakati wanajihifadhi katika mitaa na katika majengo yaliyohamwa," aliiambia Sabahi. "Wengi wanatumia dawa za kulevya, ambayo yanawaletea tishio la usalama na kijamii."

Kupata mahitaji yao ya kila siku, watoto wengi wa mitaani wanafanya kazi za utumishi kama vile kupiga viatu rangi na kuosha magari, wakati wengine wanakusanya taka au mabaki ya mirungi na kuwauzia tena waraibu.

Salad alisema watoto wa mitaani wana uwezekano wa kupata mashambulio ya kisaikolojia na kimwili, kutendewa vibaya, na kuonewa wakati wanapolala kwenye mitaa usiku. "Lakini hatari zaidi ni ukweli kuwa kwenye mitaa, watoto hawa wanakuwa na urahisi wa kudanganywa na vikundi vyenye siasa kali ambavyo vinawaandikisha uaskari kwenye shughuli za kigaidi," alisema.

Salad alitoa wito kwa serikali na asasi zisizo za serikali kumakinikia haki za watoto kuchukua hatua za haraka kutatua tatizo hili kabla ya kuleta madhara zaidi.

Umasikini na familia zilizovunjika vinawalazimisha watoto kwenda mitaani

"Kawaida ya kupoteza makazi, kutokuwa na makazi, umasikini na kuvunjika kwa familia ni miongoni mwa mambo makuu na ya moja kwa moja ambayo yamewalazimisha watoto kuishi mitaani kwa miaka michache iliyopita," alisema Abdisamad Abdullahi, mwanaharakati wa haki za watoto huko Kalmo, asasi isiyo ya kibiashara iliyoko Mogadishu.

Alisema yatima wengi wanalazimika kuishi mitaana. Umasikini na kuvunjika kwa familia pia vinachangia kwa kiasi kikubwa kuifanya mitaa kuwa "kimbilio la mwisho na mbadala wenye mantiki kwa watoto".

"Watoto hao wanapokulia mitaani, wana uwezekano mkubwa wa kujiunga na makundi ya uhalifu au kuwa waathirika wa madawa ya kulevya," alisema, akiongeza kwamba lazima wajumuishwe katika jamii ili kuzuia mambo hayo.

Mohamed Deeq Hassan, mwenye umri wa miaka 14, alisema alianza kuishi mtaani baada ya kupoteza wazazi wake wote wawili miaka mitano iliyopita.

"Nilipoteza wazazi wangu nikiwa na umri wa miaka tisa na hakukuwa na mtu wa kunitunza, hivyo nilianza kuishi mitaani," aliiambia Sabahi. "Maisha ya mtaani ni mabaya sana lakini siwezi kupata mahali pengine popote pa kuishi."

Hassan alisema ananusa gundi kwa kuwa inampa faraja kwa mateso anayoyapata. "Ninaponusa gundi ninaweza kusahau kwa muda mazingira magumu ninamoishi na ninahisi aina fulani ya furaha ya kufikiria," alisema. "Ninaweza kufikiria niko mwezini na wakati mwingine ninaota kuwa niko Ulaya au Marekani na ninasahau matatizo yote niliyonayo Mogadishu."

Makazi ya kwanza kwa watoto wa mtaani

Ili kupunguza mateso ya watoto wa mtaani, Shirika la Maendeleo ya Jamii lililoko Mogadishu, kikundi cha dini ambacho kinalenga katika kutoa msaada na huduma kwa Wasomali waliopoteza makazi, kimefungua kituo cha kwanza huko Mogadishu ili kuwasaidia watoto wa mtaani.

Kituo cha Mawahib kinahifadhi watoto wa mtaani takribani 80, wengi wao ambao ni yatima wenye miaka kati ya saba na 14, na kinawapa huduma za matibabu, chakula, nguo na elimu, kwa mujibu wa mkurugenzi wa kituo Omar Ahmed.

"Tulipogundua kwamba tatizo linakuwa kubwa, tuliamua kufungua kituo ili kuwahifadhi na kuwarekebisha watoto wa mtaani," alisema mkurugenzi Omar Ahmed. "Hii ni hatua ya kupunguza athari ya kutokuwa na makazi na kupotea kwa watoto hao."

"Wasomali wote -- wananchi na serikali -- wanapaswa kushirikiana katika kuokoa maisha na mustakabali wa watoto hao ambao wanapatikana katika mitaa yote ya Mogadishu," aliiambia Sabahi. "Sote tunawajibika na tunapaswa kutimiza wajibu wetu wa dini na wa kitaifa wa kuwajumuisha katika jamii na kuwabadilisha kuwa watu wazuri badala ya kutengeneza bomu ambalo linaweza kulipuka wakati wowote."

"Kama watoto hawa watarekebishwa, watakuwa viongozi wa baadaye," alisema. "Lakini kama tukiwaacha mitaani, tutakuwa na kizazi cha wananchi wa Somalia kilichopotea."

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

 • naadiya
  December 12, 2012 @ 08:36:13AM

  Ninamuunga mkono ndugu yangu Khadar, kijana aliyeandika katika ukurasa wa mwisho. Watoto wa mitaani wapo kila mahali duniani lakini hatutii chumvi wakati tunapokuwa na maslahi maalumu kwa watoto hawa wa mitaani. Ndugu zangu, Mungu husaidia lakini pia tutawasaidia kwa kadiri tunavyoweza. Napenda kuwaambia wale miongoni mwenu mlioweka picha hizi muache kufanya vitu kama hivi kwa watoto kwa sababu sio kitu kizuri kwa maadili ya watoto.

 • Somalische Komitee Germany
  December 2, 2012 @ 06:42:26AM

  Amani iwe juu yenu! Kaka na dada tunatafuta kusaidia kwa pamoja watoto wa Somalia wanaoteseka mjini Mogadishu. WASILIANA NASI KWA AJILI HIYO MUNGU AKIPENDA

 • jared
  November 9, 2012 @ 07:03:54AM

  Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. Kwa hivyo serikali na Wakenya mwisho wake wanapaswa kufanya kazi bega kwa bega ili kuondosha hili kwa vile vichwa viwili ni bora zaidi.

 • burhaan maxamed 0025290706555
  November 8, 2012 @ 10:12:24AM

  Nadhani hii ni makala halisi ambayo inabeba maana. Hiyo inaonesha kwamba bado kuna watu wanaofanyakazi katika programu za uhamasishaji. Asante na Mungu akutukuze kama mwandishi.

 • Samwel Lupimo
  November 8, 2012 @ 04:16:15AM

  Selikari ya Mogadishu inabid ijitahid kurejesha furaha na amani ndan yahao watoto nasio jukumu la mogadishu pee hata dunia ilitazame kwa makin sana hilo swala la watoto wa mitaan katika inch mbalimbali

 • magacaygu waa khadarbaashe (abwaan)
  November 8, 2012 @ 03:28:36AM

  Hao waliotuma picha za watoto wa mitaani kwenye tovuti ni wendawazimu kwa sababu mlipaswa kufanya chochote kwa ajili yao kama wanaweza; kwa hivyo msituaibishe. Serikali ambayo inatuma picha za watu wake kwenye tovuti haijawahi kuonekana dunia hii na sio jambo zuri kwetu sisi kama Wasomali. Asanteni.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo