Septemba 07, 2012
Wananchi wa Somalia wamekaribisha kuundwa wa bunge jipya la Somalia na kuwataka wabunge kuimarisha hali nchini na kuchagua baraza la mawaziri lenye uwezo na raisi.
Wasomali wengi wanaiangalia hatua ya mwisho ya mpito kama hatua kubwa kuelekea kubadilisha hali ngumu zinazoikabili nchi.
Mwisho wa kipindi cha mpito kilianza kwa kuwaapisha wabunge wapya hapo tarehe 20 Agosti . Tarehe 28 Agosti, Wasomali walikesha ili kujua nani angekuwa spika mpya wa bunge katika uchaguzi wa kwanza wa bunge ndani ya Somalia kwa miongo.
"Ukweli kwamba Profesa Mohamed Sheikh Osman Jawari alishinda kuwa spika wa bunge ni ishara kwamba nchi imeingia katika awamu mpya, na matumaini ni kwamba wasomi watatawala uwepo wao katika vyombo vyengine kufuatia hiki cha kwanza," alisema Mohamed Farah Ahmed, mwenye umri wa miaka 41 mkaazi wa Garowe. "Maoni yetu ni kuwa tutaweza tutaweza kuendelea kuyapita matatizo ambayo tumekumbana nayo."
Ahmed Sheikh Ali, mwenye umri wa miaka 52 na baba wa watoto tisa kutoka Mogadishu, alisema kuwa ana matumaini makubwa katika uchaguzi wa raisi uliopangwa kufanyika tarehe 10 Septemba .
Ali alisema kuwa ana matumaini kuwa uchaguzi utakuwa chanzo cha maendeleo na kutoka katika hali ya machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimewameza Wasomali na kuchukua maelfu ya maisha yasiyo na hatia kwa miongo miwili iliyopita.
"Tarehe 25 Agosti, wabunge walichagua wataalamu kuongoza asasi ya sheria, na natumai kuwa tarehe 10 mwezi huu wataweza kuchagua mtu bora zaidi miongoni mwa wagombea wanaoshindania uraisi kuiongoza nchi," alisema.
"Ukurasa mpya katika historia ya nchi hii umefunuka, na nchi ina haja ya uongozi wa taifa katika kipindi hiki cha kihistoria. Kwa sababu hii, tunawaomba wabunge kuchukua fursa ya dirisha hili la matumaini ili kuiokoa nchi," aliiambia Sabahi. "Lazima wamchague raisi mzalendo na mwaminifu atakayetumikia maslahi ya umma, kuliko maslahi yake binafsi na kushughulikia kutumika watu wake na nchi yake."
Bisharo Hassan, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 30 katika Taasisi ya Uongozi katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Puntland huko Garowe, alisema hatimaye kuondokana na serikali ya mpito kutarejesha amani miongoni mwa Wasomali katika serikali kuu inayofanya kazi.
"Asasi za Serikali ya Mpito ya Shirikisho, ambazo zilifanya kazi kwa miaka kadhaa iliyopita, zilizuwia uwezo wa serikali. Kuondokana nazo kutaiwezesha serikali [kufanya shughuli za nchi] katika jukwaa la dunia." Hassan alisema.
Mabadiliko ya karibuni pia yamekaribishwa na watu wa ndani waliotawanyika (IDPs) ambao wanataka kurejea majumbani kwao walikoondoka kwa sababu ya vurugu zinazoendelea, kwa mujibu wa Isaac Abdi Hassan, kiongozi katika kambi ya wakimbizi huko Garowe.
"Swali la kila mara katika akili zetu ni lini tutapata serikali yenye itatuokoa kutoka uwepo wetu wa kuhuzunisha na matatizo mfululizo yanayowakumba wakimbizi, aliiambia Sabahi, na kushangaa kuwa lini IDPs wataweza kurejea makwao.
Baadhi ya Wasomali waliotawanyika wanaoishi makambini wanasema wana matumaini ya hatima iliyo bora zaidi na hali zao za maisha kubadilika baada ya uchaguzi ujao wa raisi na kuundwa kwa serikali mpya.
"Tunatumai kuwa serikali ijayo itaangalia kwa ufanisi masuala ya wananchi," alisema Hassan Osman, IDP mwenye umri wa miaka 49 katika Kambi ya Barwaqo kwenye Wilaya yaWaberi huko Mogadishu.
Osman, aliyekimbia Shabelle ya Chini mwaka jana na kuacha nyuma vitu vyake, alielezea kuwa IDPs wanaishi katika hali ngumu sana. Alisema chakula na madawa pamoja na misaada mengine inayotolewa na mashirika ya kibinadamu imekuwa ikiporwa na wanamgambo wenye silaha jijini.
"Tumekuwa tukiishi katika kambi hii kwa miezi 13 na hatuna kazi, shule wala vyoo," aliiambia Sabahi. "Tunahisi kwamba serikali haikushughulikia kutosha hali zetu, lakini tunatarajia hatima bora zaidi na kuimarika kwa hali za maisha baada ya kuundwa kwa serikali mpya."
Mohamed Aden, IDP anayeishi katika Kambi ya Tawakal kusini ya Mogadishu, alisema kuwa ana matumaini makubwa kwamba serikali itaanza kazi mara moja baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa raisi.
"Baada ya uchaguzi ujao. Somalia itatoka katika serikali ya mpito kuingia katika serikali iliyotulia na dunia yote itatuunga mkono na kutusaidia. Tunatumai kuwa mambo yatabadilika kuwa bora zaidi na kwamba tunaweza kupata utulivu na kuishi kwa heshima."
"Tunatarajia kuwa tendo la ukarimu kutoka kwa serikali ijayo na mabadiliko katika ukweli huu tunaoishi sasa," aliiambia Sabahi, na kuongeza kuwa anataka serikali kuwasaidia IDPs kurejea katika shamba zao. "Tulipoteza imani na serikali iliyopita, lakini kwa mara hii, tuna matumaini na mabadiliko makubwa."
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
Sampuli ya DNA iliyochukuliwa kwenye mswaki uliokuwemo kwenye begi lililokuwa na risasi lililopat...
Wakenya kumi na wasaba wameshtakiwa kwa kuvunja amani, kufanya ghasia na ukatili dhidi ya wanyama...
Al-Shabaab imedai kuhusika na urushwaji wa makombora kwenye kasri ya rais mjini Mogadishu siku ya...
Wanajeshi wa Uganda wa Kikosi Namba 9+ wanarudi nyumbani baada ya kukamilisha miezi 13 ya ziara y...
Kikosi cha polisi cha Kenya kitaanza uhakiki wa kina wa maofisa mwezi ujao, kikianza na kusaili w...
Ujambazi ulizuiwa katika ofisi za usalama za Wells Fargo huko Mombasa ulisababisha kifo cha watu ...
Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliahidi msaada wa nchi yake katika kipindi cha ujenzi mpya wa ...
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Ndugu rais wa Somalia, ninamkaribisha kwa vile ni mtu ambaye tulikuwa tunamsubiri kwa miaka 22 na tumefurahika naye sana. Hongera hongera hongera!