Septemba 04, 2012
Huzuni zimeenea mji mzima wa Kismayu baada ya wanamgambo wa al-Shabaab kuburuza miili ya wale waliosema ni askari wa Somalia na Kenya katika uwanja mkuu siku ya Jumamosi asubuhi (tarehe 1 Septemba).
Dhofo Saeed Hassan, mwenye umri wa miaka 43 na mama wa watoto wanane, alisema al-Shabaab ilimlazimisha pamoja na makumi ya wakaazi kutoka majumbani kwao katika eneo la Fanole kwenda kuangalia miili iliyokuwa ikiburuzwa kwa gari. Al-Shabaab ilisema miili hiyo ilikuwa wahanga wa vita vya umwagaji damu huko Miido, ambao vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika viliukomboa kutoka kwa wanamgambo siku ya Ijumaa .
"Walituonesha miili minne katika sare za kijeshi -- miwili ilikuwa ya askari wa Jeshi la Taifa la somalia na miwili mengine yalikuwa ya askari wa Kenya," Hassan aliiambia Sabahi.
Ahmed Hassan Garad, muuza juisi mwenye umri wa miaka 26, alisema al-Shabaab iliwalazimisha wakaazi kufunga biashara zao na shule ili kukusanyika katika uwanja mkuu wa Kismayu ili kuwaangalia wanavyoburuza miili mitaani.
Maafisa wa serikali ya Somalia na Misheni ya Umoja wa Afrika Somalia AMISOM) walisema wiki iliyopita kuwa majeshi tayari yamekaribia kuuzunguka mji huo muhimu wa bahari , ambao al-Shabaab imeudhibiti kwa miaka mitano iliyopita.
Garad alisema viongozi wa kikabila wa Somalia, masheikh na wanaharakati wa haki za kibinadamu wamelaani uhalifu wa kikatili wa al-Shabaab kama ukiukaji wa utakatifu wa maisha na heshima ya binadamu.
"Al-Shabaab imeamua kufanya matendo ya kinyama na yasiyo ya kimaadili...ambayo yako mbali na Uislamu na ubinadamu uliostaraabika," Garad aliiambia Sabahi.
Mkaazi wa Kismayu Najma Nuh Ibrahim alisema alimuona mwanachama wa al-Shabaab akichukua video ya gari inayoburura miili inayodaiwa kuwa ya majeshi ya Kenya na Somalia.
"Yalikuwa mazingira ya kutisha na huzuni kwa sababu haimo katika mila zetu kuburuza mwili wa binadamu aliyefariki, iliyo na baraka na neema za Mungu," aliiambia Sabahi. "Kwa kila binadamu ambaye ana maadili yoyote katika uso wa dunia hii, hii ni tanzia ya kuhuzunisha na inayouma na tendo la aibu kutoka kwa kikundi chenye msimamo mkali, kikatili na kilichoachwa nyuma ambacho hakijui maana za maneno "'Binadamu' au 'ubinadamu'-"
"Wakaazi wa Kismayu hawakufurahishwa na uhalifu uliofanywa na al-Shabaab, ambayo ina sifa mbaya katika kumwaga damu ya binadamu na ambayo viongozi wake ni washirika katika mauaji, utekaji nyara na mauaji yanayofanywa na watu wasiojulikana," alisema. "Mara nyengine wahanga wanapotea na hatima yao kuwa haijulikani daima."
Awade Abdullahi Gabane, mfanya biashara mwenye umri wa miaka 52 anayesafirisha bidhaa baina ya Kismayu na kijiji cha karibu cha Bulo Haji, alisema al-Shabaab inawasumbua wananchi wa Kismayu na kuwaingiza katika vurugu zisizochagua, wakijaribu kufikia malengo yao kwa kupitia mbinu potofu na za kihalifu.
Gabane aliiambia Sabahi kuwa Uislamu haihusiki na misimamo mikali kama hiyo, na kuita tendo la kuburuza na kuivunjia heshima miili kuwa ni ukafiri. Uislamu unahitaji mazishi ya watu kwa heshima, alisema, na unalaani matendo ya utesaji na yasiyokuwa ya heshima.
Baada ya mapambano ya huko Miido, AMISOM ilisema iliwauwa wanamgambo 36 wa al-Shabaab wenye mafungamano na al-Qaida.
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) Meja Emmanuel Chirchir alitangaza siku ya Jumamosi kwamba askari watano wa KDF wamepotea, na watatu walisafirishwa Dobley ili kupatiwa matibabu. Watatu kati ya askari waliopotea walipatikana hapo Jumapili, alisema, ilhali wawili wengine hawajulikani walipo.
Mwandishi wa habari Faiza Shire Ali alisema al-Shabaab inalichukulia jeshi la Kenya kama kikosi kivamizi, ingawa Umoja wa Afrika na Serikali ya Mpito ya Shirikisho zilifikia makubaliano hapo mwezi wa Machi wa kuunganisha maelfu ya majeshi ya Kenya kufanya kazi chini ya uangalizi wa AMISOM .
"Maadui wa amani wamekuwa wakipoteza maeneo kadhaa ya kimkakati, ikiwa ni pamoja na mji wa mwambao wa Marka, ambao ni mji mkuu wa Shabelle ya Chini," aliiambia Sabahi. "Pia wamekuwa wakikabiliwa na vikwazo mfululizo pamoja na maafa na machungu yanayowaumiza viongozi wa kikundi ambao wamelazimika kubadilisha sehemu zao za malazi kila usiku wanapohama kutoka kijiji kimoja hadi kingine," alisema.
"Tunaweza kuwaona wakichungulia chini katika kila lindi wanaloangukia, mmoja baada ya mwengine, katika sehemu kadhaa za nchi mpaka watakapokamatwa na vikosi vya usalama na kufungwa katika magereza ya Mogadishu, Beledweyne na Bosaso," Ali alisema.
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
Sampuli ya DNA iliyochukuliwa kwenye mswaki uliokuwemo kwenye begi lililokuwa na risasi lililopat...
Wakenya kumi na wasaba wameshtakiwa kwa kuvunja amani, kufanya ghasia na ukatili dhidi ya wanyama...
Al-Shabaab imedai kuhusika na urushwaji wa makombora kwenye kasri ya rais mjini Mogadishu siku ya...
Wanajeshi wa Uganda wa Kikosi Namba 9+ wanarudi nyumbani baada ya kukamilisha miezi 13 ya ziara y...
Kikosi cha polisi cha Kenya kitaanza uhakiki wa kina wa maofisa mwezi ujao, kikianza na kusaili w...
Ujambazi ulizuiwa katika ofisi za usalama za Wells Fargo huko Mombasa ulisababisha kifo cha watu ...
Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliahidi msaada wa nchi yake katika kipindi cha ujenzi mpya wa ...
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Dunia haitakuwa huru mpaka uislamu ushike hatamu ya kuutawala ulimwengu!! na kuondokana na ukandamizaji na unyonyaji wa wakoloni wa kimagharibi..
Watu wawemakini na viongozi wasio waadilifu
Nyinyi watu wa Somalia, kwanza napenda kuwaomba ikiwa watu hawa watamalizwa au watarejea wakati mwengine. Kwa nini hamkuyachoma moto maficho yao? Kwa nini hamkuwatafuta popote walipo badala yake mmewaachia? Mnawaogopa watu hawa waliopotoka?
Mwenyezi Mungu awe pamoja na askari wote wa Somalia kila siku ili kujua kuwa Mungu wa Israeli amewapa al-Shabaab mikononi mwenu, wasafisheni, ni wakati wa kuvuna kile walichopanda.
Wacha Al-Shabaab ikusanyike upya nchini Kenya au nje. Kila Mkenya mpumbavu aliye mzalendo na anayeenzi utaifa anaweza kufyatua bunduki, kurusha makombora au kuangusha mabomu, yawe ya haradali au la.
Wanaweza kufanya chochote wanachofanya katika njia zao za kishenzi. Kama inavyosemwa "wanaweza kukimbia lakini hawawezi kutoroka". Tutawasafisha na watakabiliwa na sheria ikiwa hili ni kweli. kwa nini hawajifunzi kutokana na historia? Wako wapi Hitler, Saddam, Gaddafi n.k.? Watakumbwa na ghadhabu hiyo hiyo. Heko KDF.
Yote haya kwa jina la Uislamu!!! WENDAWAZIMU UNA MIPAKA YAKE.
Wanadhania wao ni nani? Daima wanatafuta umwagaji damu. Hili litakuwa jambo lililopita miezi michache tu ijayo.
Mungu wetu Mkubwa na Bwana Mwema aziokoe roho za Wakenya wote ambazo zimepotea katika juhudi za kuleta amani ya kudumu na ubinadamu nchini Somalia na eneo letu kuu. Mungu awape amani ya milele Peponi na nguvu kwa familia zao. Ama kuhusu al-Shabaab, maandiko ukutani na Mungu wetu Mkuu atateremsha ghadhabu zake juu yenu, enyi madikteta wapotofu! Hakuna dini ya Mungu duniani inayotetea chuki, mauaji na kuwakosea heshima na kuwanajisi binadamu.
Ninawaambieni nyinyi. Nyinyi sio Waislamu. Msiue kwa jina la Uislamu ilhali Uislamu ni amani, usalama, yenye msamaha na ubinadamu. Nyinyi mko tofauti kabisa. Wakristo na watu wasio na dini ni bora zaidi kuliko nyinyi. Mungu ananitosha kwani Yeye ni Mpangaji Bora zaidi wa mambo!
Ni tendo la kiwoga kuburuza mwili wa mfu.
Mungu, ingilia kati hali hii.
Hongera askari wa Kenya, mtashinda na kushinda dhidi ya majeshi haya ya shetani ambayo hayana kibali kutoka kwa Mungu. Kumbukeni kuwa Bwana Mungu ni moja na havumilii maovu. Hakuna Mungu kwa ajili ya Waislamu na kwa ajili ya Wakristo! Mungu wetu amewahukumu Al-Shabaab kwenda jehanamu!
Nadhani kwa ukombozi wa Somalia, nchi zote jirani zinaweza kufaidi uhusiano mzuri wa biashara na Somalia na hii inaweza kujenga njia nzuri kwa wawekezaji. Semeni Kwaheri al-Shabaab!!!
Jeshi la UA linapaswa kupewa moyo zaidi ili kupambana na wahuni wa al-Shabaab.
HONGERA kwa askari wenzangu, mbele daima nyuma kamwe mpaka misheni ikamilike. Sasa tunajitayarisha kusafisha benki tunayowapa ili kuwafunika ndugu zetu wa Somalia. Lazima kuwepo na amani, Mungu yupo pamoja nasi sote. HONGERA tena na endeleeni kudhibiti uwanja.
Uingereza imepewa kuchagua baina ya vita na aibu. Ilichagua aibu na itapata vita.
Nashangaa ni aina gani ya mawazo waliyonayo wanachama wa mtandao huu wa al-Shabaab. Hawa ni aibu kwa binadamu, ni mawakala wa moja kwa moja wa shetani mwenyewe, lakini hatimaye nia njema itashinda uovu. Mungu Wetu ni Mkubwa!
Hawa watu ni vichaa na hawaelewi maana ya ubinadamu. Hawawezi kuua kila mtu kwa sababu ya imani zao tu. Wanapaswa kufumbua macho yao na kuona ukweli. Heko KDF, wanalofanya ni jambo zuri sana.
Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, vita hivi vitafikia mwisho. Ninamuomba Bwana wetu mwema kuwalinda askari wetu wanaotaka kuikomboa Somalia dhidi ya watoto wa maovu wanaoua wananchi wasio na hatia. Yeyote yule anayeifadhili al-Shabaab atashughulikiwa na Bwana wetu mwema kwa vile kisasi kinatoka kwake.
NASIKITIKA KWA WAKENYA WENZANGU ... NINGEPENDA HILI LITOKEE KWA majeshi ya Ethiopia.
Eeeeh al-Shabaab, shetani yumo ndani yenu, lakini wasubirini AMISOM huko Kismayu…. Mnawaelewa vizuri …. Kutoka Mogadishu …NAOMBA KAZI NZURI YA AMISOM IZAWADIWE IPASAVYO. TUNAHITAJI AMANI NA SIO MACHAFUKO. Al-Shabaab, muingie jahanamu kwa matendo yenu ya mauaji.
Mungu awe pamoja na jeshi la KDF.
Karibuni dunia itasherehekea ukombozi kamili wa nchi ya Somalia kutokana na juhudi za pamoja za KDF, AMISOM NA WAZALENDO WA SOMALIA. Amani na mafanikio ya kudumu yapo karibu. Ama kuhusu kushindwa kwa al-Shabaab kunachukua muda kuzingatia jinsi gani mlivyopotoshwa na ombeni msamaha na Mwenyezi Mungu kwa wema wake wa milele USIO KIASI atawapeni msamaha na huruma zake ili muweze kujiunga na jamii nzima.
Tujuwavyo al-Shabaab walivyo!!.. Wamalizeni.
ANGAMIZA HAO AL SHABAB HAWAFAI KBISA KATIKA DUNIA YA AMANI MUNGU YUPO NASI
Wakati askari wa Kenya wanawapunguza al-Shabaab nchini Somalia, wanachama zaidi wanajiunga nchini Kenya. Kwanza washughulikie wale walioko Kenya.
KDF wanapaswa kuharakisha vita dhidi ya watu hawa wenye akili za uovu ambao hawana heshima hata kidogo kwa maisha ya binadamu. Kuhusu hili, sisi kama Wakenya, wa Afrika Mashariki, Afrika ya kati na dunia yote wanatiwa wasiwasi na vita kwa sababu sote tunahitaji amani, kwa hivyo ikiwa tunaitaka, tunapaswa kuitetea sheria hii ya ugaidi ... fikiria kama mlinzi wa ndugu yako na utaona haja ya kuwepo kwa amani ... amani kwa ajili ya Kenya… amani kwa ajili ya wote.
Asakri wa KDF na TFG ni binadamu. Kaka na dada zetu, naamini watarejea nyumbani na familia zao. Mungu wangu wa peponi awajaalie busara ya kuimaliza vizuri na kurejea nyumbani wakiwa wameshinda. Mchungaji George Osoro Nairobi – Kenya.
Hongera KDF. Endeleeni na kazi nzuri. Familia zenu zinawasubiri, rejeeni nyumbani haraka.
Huu ni unyama kamili. Wacha wahusika wa chombo cha UN wachkue hatua mara moja.
KDF inahitaji kuongeza kasi ya operesheni, pengine kwa kupunguza vifo kutoka upande wetu. Tuko pamoja nanyi na tunaomba kwa ajili ya jeshi letu. Ushindi upo machoni.
AL-SHABAAB MNACHEZA MCHEZO AMBAO TAYARI MMESHINDWA. KWA NINI? KWA SABABU KDF HAWAZUILIKI. KUTOKANA NA MUNGU NA KWA JUHUDI ZETU, SISI TUNASHINDA NA NYINYI MNASHINDWA!!!!!!!!!!!!!!
Kufeni al-Shabaab
Mungu aisaidie Somalia. Al-Shabaab acheni kuutumia Uislamu katika matendo yenu ya kishenzi. Mmelaaniwa. Mwenyezi Mungu awashushie jeshi lake na ili kuwaangamizeni mara moja.
Kucheza na miili ya maiti ni sawa na kucheza na masanamu ya kuchezea, ndio! Kwa nini hamna ustaarabu, vichwa vitupu vijana wa al-Shabaab? Wakabilini wanaume wa kweli wa KDF ana AMISOM ilimuache mbinu zenu za kijinga na zisizo za kitaalamu! Hawa watoto wa al-Shabaab ni wajinga waliozaliwa na mama wa kweli? Hawawezi kuheshimu kazi nzuri ambayo Mungu ameifanya katika uumbaji wa binadamu? VIJANA WA AL-SHABAAB NA WAFUASI WENU, KAPUMZIKENI JEHANAMU!
Dua zenu tu kwa ajili yao.
Mapigano yanachukua muda mrefu. Tulikuwa tunataraji kuwa mwezi wa Agosti 2012 mambo haya yangekuwa yamemalizika. Al-Shabaab inapaswa kujisalimisha na kufikiri juu ya vipi kuisaidia serikali yao.
nina waombea jeshi letu limalize oparesho linda nchi vema
Inasikitisha kuwa nchi kama Somalia kukaa kwa miaka 20 bila ya serikali rasmi. Kenya na nchi nyengine jirani hazikuwa salama kwa sababu ya tishio la al-Shabaab. Wakati umefika wa kuungana na kupambana dhidi ya al-Shabaab. Kwa morali mkubwa tunawaunga mkono KDF wetu na AMISOM kwa jumla katika kazi zao dhidi ya al-Shabaab
Hawa al-Shabaab wamezingirwa na ndio maana wanatuonesha vitendo vyao vya kiwoga. Mungu yasaidie majeshi ya AMISOM na KDF kumaliza kazi hii kwa haraka na watu wa Somalia kuwa huru kutokana na mabaki ya al-Qaida.
Al-Shabaab sio jeshi la ukombozi wa Somalia bali ni maadui wa nchi yao wenyewe. KDF na vikosi shirika, watokomezeni wote.
Kwa mimi Wasomali ni ndugu zangu na ninawatakia mafanikio.
yan hao wakikamatwa wauwa kwasababu wameua vyakutosha nalipongeza jesh la KENYA na UN
Mara zote kuwa upande wa wafanyakazi.
Sitaki kuamini kuwa yule alikuwa jeshi wa Kenya......viatu na rangi yake?????? Hii ni udanganyifu tu na hatutishiki na al-Shabaab. Karibuni watakufa. Ni waoga. KDF, endeleeni.
Ikiwa mtu anafikiri ni mwanaume wa kweli kwa nini atese na kuburuza mwili wa maiti? Na kwa kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, makosa yote haya ya kikatili yanafanywa kwa jina la dini. Tena watu washenzi wanaoishi na kufurahia maisha nchini Kenya wanakubali kuwaunga mkono al-Shabaab bila ya kujali juu ya dada na kaka zetu walioko katika KDF. Hongera KDF na AMISOM, Mwenyezi Mungu yuko upande wenu na tutawageuza al-Shabaab kuwa majivu.
Wanamgambo wa al-Shabaab wanapigana vita vya wasiwasi tu huko Kismayu kwa woga wa kuwa mji karibuni utatekwa tena kutoka mikononi mwao. Mungu wa amani apeleke msaada kwa kazi ya Mkono wake (watu) Somalia yote.
Mungu awabariki baba zetu walioko huko
Ninawachukia al-Shabaab, acheni vita, ikiwa hamtaacha nitawauweni nyote kwa mikono yangu. Mimi ni raisi wa MAREKANI.
Endeleeni KDF na askari wa AMISOM, hicho mnachofanya ni halali na kimaadili ni sahihi. Ni dhamira adhimu sana. Tunajivunia kwenu. Bwana awabariki zaidi wakati mnaandika historia.
Mwisho wa misheni hii itakuwa alama ya mwisho wa migogoro ya muda mrefu miongoni mwa Wasomali, pia kwa upande mwengine wanamgambo wa al-Shabaab wanaweza kuzidisha mashambulio ya ugaidi kwa Kenya na Uganda.
MILELE KDF! MILELE!
Al-Shabaab wataangamizwa. Nadhani ni waoga.
HUO NI UISLAMU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Somalia itakuwa huru, uhuru unakuja kwa Somalia.
Waangalieni punguani na wanyama hawa punguani wanavyoburuza mwili wa mzalendo, shujaa na mpiganaji. Inanikumbusha juu ya mende mmoja ambaye kwa kawaida hutoka gizani ili kukusanya makombo.
Wafu lazima waachwe wapumzike kwa amani. Matendo ya al-Shabaab ni dhidi ya kanuni zilizothibitishwa kimataifa katika masuala ya vita na lazima wawajibishwe kwa makosa yao.
Watu, tuombe kwa ajili ya watu wa Somalia, Mungu anaweza.
Hongera KDF.
Waacheni wamburuze yeyote wanayetaka, awe amekufa au hai lakini hatimaye watasagwa...
KDF...mtaona mwanga mwishoni mwa handaki
Kama unataka amani jitayarishe na vita. Hatimaye kutakuwa na amani nchini Somalia lakini maumivu ya watu waliofariki yatamalizika lini katika nyoyo za Wasomali? Mungu wa Waisraeli aingilie kati na kuiokoa damu ya watu wasio na hatia. Mwenyezi Mungu tunakuomba kwa ajili ya watu wa Somalia. TUNAMPENDA MUNGU; MUNGU ANAKUPENDA, YESU ATAKUOKOENI.
ITIKADI ZAO NI ZA KIWENDAWAZIMU KAMA MATENDO YAO. MAFUNDISHO YA KIISLAMU YANADAI WATU WAYAPINGE HAYA KWA VILE HAYARUHUSU JAMBO HILI. KUNA MENGI YA KUONESHA KATIKA VITA KULIKO KUBURUZA MIILI YA WAFU.
Natumai Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi unaangalia kile kinachotokea kwa kawaida nchini Somalia, ambapo watu wasio na hatia wanakuwa wahanga bila ya wao kuingilia kijeshi kama walivyofanya kwa Libya. Kwa kweli tunahitaji msaada wenu wa kutangaza uhuru kamili wa Somalia wakati huo huo kuwamaliza al-Shabaab na al Qaida.
Watu wote waelewe hakuna kitu kama vita vitakatifu. Tafadhali, sote tujaribu kupenda maisha ya wengine. Al-Shabaab na al-Qaida MUNGU atawaadhibu nyote daima.
KDF, ninawaombeeni dua. Songeni mbele. Kismayu itaanguka! Ni suala la siku tu! Mungu yuko upande wenu.
Mungu alisaidie jeshi letu na askari wa Somalia huku wakifanya kazi ya kuleta utulivu na amani nchini Somalia. Mungu awaongoze na kuwalinda. Mtaweza kushinda na imani.
Kenyans are lovers of peace....that is the sole reason they are in Somalia...unlike AMERICA Kenya is not after any resource...am proud of KDF ....surely you will win...you are infact blessed for you are peacemakers;amani haiji ila kwa ncha ya upanga...lazima Al Shaabab watambue KENYA is great..very great..with great soldiers...GOD SHALL PROTECT KDF;WE NEED NO ARGUMENT.
Hatua kali zichukuliwe kwa yule aliyeburuza mwili
Hebu Al-Shabaab wajiulizetu wao wenyewe kwamba wanachokifanya kipo sahihi kweli? wanataka nini? wanaona ni furaha kuuwa raia bila kosa? nini wataenda kijibu mbele ya haki? Mimi binafsi nina washauri waende wakae mezani na new president wazungumze yaishe ili wakabiliane na jukumu la kuijenga Somalia.
ALSHABAAB PUNGUZENI JAZBA; RUDINI NYUMBANI IJENGENI SOMALIA MPYA YA AMANI NA UPENDO.
Mnastahiki kufa kwa bunduki... nani aliyewapa ruhusa ya kuburuza mwili wa binadamu kama sanamu ya kuchezea. Mtavuna mara kumi kwa kile mnachofanya al-Shabaab na wengine kama wao wanaochukua jukumu la kuua watu kama vile wao ni Mungu ... Bwana alipize kisasi kwa damu ya ndugu zetu wasio na hatia waliouawa kwa njia yoyote ile ... Al-Shabaab, mjaaliwe kushindwa kubaya sana....
Al-Shabaab sio Waislamu, wanawaua watu wasio na hatia, na wanajidai hivyo kwa sababu ya Waarabu. Sisi ni Waafrika na kwa vyovyote vile sisi sio Waarabu, hatutaki kuwa na ngozi nyeupe. Kila mtu aelewe kuwa al-Shabaab ni kikundi tu na wako kule kwa sababu ya maslahi yao binafsi.
Huu sio Uislamu. Uislamu kama dini inaheshimu ubinadamu iwe mwili wa aliyekufa ni Muislamu au la! Uislamu unafuata heshima ya maisha ya binadamu na kuitendea vyema miili ya maiti kwa vile haina uwezo wowote. Waislamu tulifundishwa kuheshimu maisha, kuyaenzi na siku zote kukumbuka hadithi za Mtume Muhammad (Amani iwe juu yake)kama nyenzo yetu ya mwongozo na kile ambacho ninaona katika makala hii ni tendo la kishetani na ni kinyume na mafundisho ya Kiislamu. Al-Shabaab sio wawakilishi wa Waislamu na katu hawatakuwa wawakilishi wao. Watu wa Somalia ambao wanateseka kutokana na matendo ya kikatili yanayofanywa dhidi yao na kikundi hiki cha wanamgambo ni Waislamu. Kuwapigisha kwata na kuwalazimisha waangalie jinsi miili ya maiti inavyoburuzwa mitaani kama walivyofanya ni adhabu tosha na hawawezi kudai kuwa wanawawakilisha Waislamu kwa kufanya hivyo. Sisi Waislamu wa kweli tunawalaani vikali sana.
Kama nchi ya Kenya, tumefanya jambo jema kabisa, jambo ambalo kizazi kijacho kitakuja kufurahia amani. Hawa al-Shabaab ni mashetani na haja yao ni kukandamiza tu.
uislam ni amani si mauaji na udhalilishaji wa viumbe vya ALLAH
Uislamu maana yake ni amani. Je, kuua na kuburuza wafu ni miongoni mwa matendo ya amani?
KDF, NYINYI NI BORA. WAPENI MAFUNDISHO KWA VILE MUNGU YUPO PAMOJA NA NYINYI. HAKUNA MTU ATAKAYE WATISHENI KATIKA DHAMIRA HII.
Ni athari gani ya kuburuza mwili mitaani? Hilo linaonesha upuuzi, uduni wa kufikiri kwa akili. Kuburuza mwili wa maiti hakumaanishi chochote kwetu, tutawapiga hadi mwisho.
Mwash, wewe ni mpuuzi. Kwa kweli naamini kuwa kuna mara ulikuwa upande wa majambazi hawa wapuuzi. Uingie jehanamu kwa kuwasema vibaya vijana wetu, mshenzi!
Jehanamu inaungua moto kutoka kwa KDF. Al-Shabaab wanalijua hili. Kwa kweli wananusa kile ambacho KDF wanapika. Ni suala la wakati tu na Mpishi Mkuu Karangi atatoa amari ya kuwaangamiza wahuni hawa hadi jehanamu. Kwa KDF, mmetufanya sote tujivunie. Mmefanya kile ambacho WENYE NGUVU KUU hawakuweza kukifanya.
Hatimaye ninaiona Somalia inayoongozwa kwa utawala wa sheria. Hongera KDF.
Wauweni al-Shabaab, Kenya itashinda, Kenya shinda.
Daima mbele nyuma jeshi letu. Wapigeni ili kuwaonesha vitendo vyetu.
Kwa nini wakati baba yako ameuliwa wakati wa kuilinda nchi yako unalia kuchezewa rafu. Hapa tunao vijana wanaolinda itikadi zao zinazohusu maisha maisha yao na utamaduni, uhuru katika kutoa maamuzi, kufanya utamaduni pamoja na imani, baadaye inakuja nchi ya kigeni ambayo imeshindwa hata kuwalisha watu wake wanaokufa kwa njaa wala kuwapatia kazi, inakalia viti vya fahari vya walipa kodi 200,000 na kuamua kuivamiaa nchi kwa kutumia pesa watu hao hao masikini. Kuweni na hisia, enyi viongozi waroho. Pesa zote hizo zingeelekezwa kwa miradi ya wakulima kwa taifa linaloendeshwa na uovu kwa makusudi. Hata hivo, vijana wetu walijumuishwa katika AMISOM ambayo iliwalipa vizuri kwa kulipuwa vichwa vya wanyama wapuuzi, lakini bado swali linabaki, ni nani atakayefidia kikamilifu viongozi waliopata kipigo cha nguvu? Pesa zinaweza kufanya hivyo? Nijibuni tafadhali, askari mnaorejea.
KDF mtawabomoa watu hawa kwa sababu wamesabababisha matatizo mengi. Endeleeni! Endeleeni! Endeleeni!
Al-Shabaab wataangamizwa, Mungu akipenda.
Al-Shabaab ni tatizo la Somalia, majeshi ya Kenya yanafanya nini nchini Somalia? Ninachukulia kuingia ndani ya Somalia kama tendo la kihalifu, rejeeni Kenya. Hamkubaliwi katika nchi yetu takatifu. Kenya tayari imechukua sehemu ya kaskazini mashariki kutoka Somalia, sasa wanataka kuichukua Kismayo?
WAISLAMU NA WAKRISTO, SOTE TUOMBE AMANI KWA SOMALIA! SOTE TUNATESEKA!!!
Al-Shabaab ni wapuuzi na hawana nafasi katika jamii. Karibuni Somalia itakuwa huru.
Al-Shabaab, hakuna haja ya kuburuza mitaani mwili wa maiti wenu wenyewe, bado mnao waoga wenu kwa maelfu waliouwawa katika uwanja wa vita.
Makafiri na wanaojipendekeza kwao ambao wameasi dini yao kwa ajili ya fedha wanapaswa kuuliwa na kuadhibiwa popote wanapoonekana. Waueni, mwageni damu yao na wachomeni. Suala ni, kitu gani kilichowaleta hapa? Yeyote anayeua kafiri ataingia peponi. Sisi kwa wakati huo huo tunalinda nchi yetu na heshima yetu na hatutapoteza chochote katika njia mbili hizi- Hatutavumilia wakati wowote kukandamizwa na kutawaliwa na makafiri wa Kiafrika. Somalia itafanikiwa. Uislamu utafanikiwa.
UISLAMU ni AMANI, kile al-Shabaab wanafanya sio cha Kiislamu, na hawapaswi kuutumia Uislamu kwa maslahi yao binafsi. Kupigana na maiti ni ishara ya kushindwa. Ni mateke ya mwisho ya farasi anayekata roho.
last kicks of a dying horse...........watu wachapwe!!!! atlast there shall be peace in Somali
Ikiwa washenzi hawa wa al-Shabaab wanasikia raha kuburuza miili ya maiti mitaani, na wao watakuwa wamekufa hivyo hivyo. Hawana Aibu wote!!!
HONGERA KDF, PIGANENI KAMA NGUZO ZA CHUMA. KWENYE UANDIKISHAJI MAFUNZO YAJAYO NADHANI NITAKUJA KWA MAJARIBIO.
Kwa kweli Somalia inahitaji amani na usalama. Watu wake wanahitaji maendeleo na sio vita. Mungu iokoe Somalia kutokana na wauawaji hawa wasio na hisia wanaoitwa al-Shabaab.
Ninawahurumia al-Shabaab. Wanakufa kama nzi nchini Somalia. Ili kuongeza matusi juu ya jeraha, wote wataishia jehanamu daima milele. Poleni al-Shabaab.
Al-Shabaab inapaswa kujisalimisha na kuachana na vita hivi kwa sababu vinapelekea kwenye vifo vya wanachama wao wengi, wanawake, wanaume na watoto ambao ni viongozi wa kesho, kwa kujihusisha na matendo haya ya kinyama ya kwa majeshi. Je, wana angalau alama za upendo ndani yao?
Haya yanayooneshwa na al-Shabaab ni matendo ya kuchanganyikiwa.
Unapokuwa unapigana na wahuni ambao hawajawahi kuona hata milango ya darasa, hili ndilo unalotarajia kutoka kwao. Kama ni wakweli, basi waoneshe wapiganaji wao waliofariki.
MUNGU AWALINDE WATU WAKE.
Al-Shabaab wanajaribu kupigana na miili. Huo ni upuuzi wa kiwango cha juu. Mnaweza kujipanga na kuwa wanaume bara bara. Hamna aibu!
Kwa ndugu zetu wa KDF WALIOFARIKI ... tunawapongezeni na kuwaunga mkono kikamilifu. Al-Shabaab ni WAOGA!!!
Siku za kuburuza miili ya maiti ili kuonesha ushindi zimepita zamani. Ni wakati sasa kwa wanamgambo kuacha kumwaga damu na kuanza kujenga Somalia kwa watu hao wote walionao. Mambo yamebadilika kutokana na wakati.
ENDELEENI KDF!!!!!!!!!!
guys we realy felt for you but in God we trust atawise morale tuko pamoja
Al-Shabaab hawatafanikiwa ... shukrani kwa juhudi za kila mtu za kuwatoa nje al-Shabaab.
Kupeleka askari wa Kenya au wa nchi nyengine yoyote hakutaweza kutatua hili na hakutatatua jambo lolote ... ni Wasomali tu wanaoweza kutatua matatizo ya Somalia ... kitu pekee tunapaswa kufanya ni kuwawezesha, kwa ujuzi wa kivita na silaha, intelijensia, na mafunzo maalumu .. vita dhidi ya ugaidi ni vita vya muda mrefu na sio vya msimu .. ipatieni serikali ya Somalia vifaa ili wawashughulikie wendawazimu hawa...
Al-Shabaab ni wahalifu wa dunia kama walivyo al-Qaida. Yeyote anayewaunga mkono al-Shabaab anastahiki adhabu ya kifo. Lazima wasagwe kutoka uso wa dunia kwa gharama yoyote ile. Hawana ajenda ya maadili ya kidini, hawa ni watu waliokithiri tu, Waislamu wenzangu tafadhili jitengeni na wahalifu hawa. Uislamu hautetei utekaji nyara wa wanawake wenye ulemavu. Hamna aibu al-Shabaab, siku zenu zinahesabika. Hakuna mwanachama yeyote wa kikundi hiki atakayeachwa atoroke. Hongera UA, Hongera TFG na Mashujaa wa KDF waliofariki.
Kwa Mungu mambo yote yanawezekana. Kwa hivyo tusubiri mipango ya Mungu. Lakini tukumbuke kuwa sisi ni zaidi ya washindi kwa Yesu Kristo.
Kwa nini wanapigana na maiti? Inaonesha jinsi gani walivyokuwa hawawezi kitu ...
Al-Shabaab ni laana tu! Nyote mtamalizwa! Machozi ya watu wasio na hatia mliowaua yawapeleke katika moto wa kudumu jehanamu. Nyinyi si chochote isipokuwa waoga tu!
Tutawasukuma pembeni hata iwe vipi.
KUBURUZA MIILI YA WAFU HAKUWEZI KUATHIRI CHOCHOTE ... HAPANA. NAMBARI 1. NI MWILI WA MFU USIO NA HISIA ZOZOTE 2. DALILI ZA UPUUZI.
... Majeshi yetu daima huvaa viatu Vyeusi!!! ... huyu anaweza kuwa mmoja wa watu wao wenyewe. Acheni kutupumbaza! Siku zenu zinahesabika!
Ni sawa, kwa vile serikali inaonekana imelala.
Hatimaye amani inatawala nchini Somalia. Al-Shabaab waoze jehanamu. Heko KDF na AMISOM.
AL-SHABAAB BORA MJISALIMISHE... GHADHABU ZA KDF ZITAWASHUKIENI KAMA DHORUBA. Kizazi cha mbwa!
KDF endeleeni kulipua vichwa vya al-Shabaab wasio na moyo..... Wanapaswa wawaelewe watu!!!!!
Huyu si mmoja wa askari wetu, labda wa Rwanda au Burundi. Watu wetu hawavai viatu vyeupe na hata magwanda yenyewe yanakuambia kuwa huyu sio Mkenya na ni upuuzi kuwatisha watu kwa kuburuza maiti mitaani. Ili iweje na kijana huyu ameshafariki na hahisi mnachomfanyia? Mmepata nini, bado mtasafishwa tu kama mtaro.
Endeleeni KDF.
hawa magaidi siku yao ikaribu kufika na waombea wana jeshi wetu kdf mungu awalinde nakuwa mlinzi kwa mwenzako mungu wa amani awa linde amen
Waoga.... inahuzunisha kuwa vifaru na magari yetu ya kijeshi yanazidiwa na maiti za watu wa al-Shabaab waliokufa. Pengine tungekuwa wapuuzi sana kufanya kama walivyofanya wao... wafe zaidi mpaka wa mwisho. Tunawadharau kwa kile mnachofanya... mpumzike kwa amani makomredi wetu waliofariki.
La kuchekesha sana wanasema wanafanya hivi kwa ajili ya Mungu. Ikiwa ni hivyo, basi tunafikiri ni aina gani ya Mungu hao al-Shabaab wanao. Mungu anatumikiwa kwa matendo mema lakini sio kwa utekaji nyara na kuwafanya watu waishi katika woga.
Watu wa Somalia wawe huru na kufurahia matunda ya ukombozi kutoka kiini cha mabwana wa kikoloni. Waislamu ni watu wanaomwogopa Mungu na sio wauaji. Wanathamini maisha kwa sababu ni zawadi ya Mungu kwa binadamu kuishi na kumtumikia YEYE. Al-Shabaab sio Waislamu, ni wauwaji. HEKO AMISOM.
Ni lini yatamalizika yote haya? Hawa vijana wa al-Shabaab hawawezi kuishi kwa amani...??
Hongera askari wetu! Tunawaaminieni na tunajua kuwa kujitolea kwenu kutaikomboa Somalia kutokana na genge hili la wauwaji. Hongera!
KDF, MATENDO YA AL-SHABAAB JUU YA ASKARI WETU WATUKUFU LIMEWAPA MAMLAKA MAKUBWA ZAIDI YA KUTUMIA NGUVU ZA SILAHA ZILIZOPO MIKONONI MWENU- NAFASI ZOTE ZA AL-SHABAAB LAZIMA ZICHAKAZWE KWA MABOMU KUSIWE NA ISHARA YA UWEPO WAO.
Wakenya tumesaidia.
Ninashuku kuwa al-Shbabaab sio binadamu wa kweli, kuna kitu hakijulikani.
Ni vyema kuwaheshimu al-Shabaab kwa sababu walikuwa wanaogopa neno ulimwengu {wa Waislamu}.
Al-Shabaab, wacha waende jehanamu.
Al-Shabaab sio tu ni maadui wa watu wa Somalia lakini ni hatari kwa dunia nzima. Mungu awaongeze nguvu zaidi wale wote wanaoshiriki katika kuzima uovu huu.
Kila la heri mabibi na mabwana wetu. Mungu wetu abariki kazi ya mikono yao.
Hizi ni siku za mwisho,kwa hivyo sote tumuombe Mwenyezi Mungu kuiokoa dunia ambayo imejaa watu wenye matendo ya kinyama. Fikiria tendo la kuburuza maiti!
Inatisha kuona na kusikia madai kama hayo. Hawafahamu neno Ubinadamu? Mungu apishie mbali!
WOTE WALIOTENDA HIVYO NI WABAYA NA WANYAMA. NI NINI MWISHO WA KUWA NA NCHI ISIYO NA AMANI? WATU WA SOMALIA WANAPASWA KUFIKIRIA MASLAHI WA NCHI NA WATU WAKE BADALA YA KUWA WAKIMBIZI KILA WANAKOKWENDA.
Ni wanyama wsiostaarabika tu kama mbwa ambao huburuza miili ya wanyama waliokufa. Al-Shabaab sasa imerejeshwa katika hatua ya chini pamoja na mbwa wanaotangatanga. Hawaoni aibu!
KDF inafanya kazi nzuri.
Mungu akubarikini AMISOM kwa juhudi na kujitolea kwenu mnakofanya ili kukuza amani na utulivu nchini Somalia. Vyenginevyo, tunawaombeeni wakati mnafanya shughuli zenu za kila siku. Hongereni nyote kwa operesheni yenu nchini Somalia.
Ni bahati mbaya sana kuwa al-Shabaab hawana heshima kwa maiti. Tunaiombea Somalia amani.
Al-Shabaab Itakuwa ni sehemu ya serikali, Mungu akipenda.
zungumza kile ambacho unakielewa na unauwakika nacho, epuka kusema maneno ambayo huna huwakika nayo, juu ya somalia, yangu macho,
Mungu nakushuru kwa mama, kaka na baba zetu walioko huko, wamewaacha nyuma wanaowapenda zaidi kwenda kupigana kwa nchi yetu. Ushindi ni wako baba!!!!!!!
Al-Shabaab haIna hatima na mwisho wao ni sasa sio kesho. HONGERA AMISOM NA KDF KWA HUDUMA MLIYOTOA VIZURI.
AMISOM wanawakilisha utu wa Afrika, ambapo askari waliofariki ni mhanga kwa matumaini kwa watoto wa Somalia, wanaoishi na ambao bado hawajazaliwa, Mungu atawalipa! Idumu AMISOM. Idumu KDF!
Karibuni nitaweza kusoma katika Chuo Kikuu cha Mogadishu na kupumzika katika fukwe nyeupe za Kismayu. Al-Shabaab ni maadui wa ustaarabu.
Al-Shabaab ni kikundi, kama akina Mungiki na vikundi mengine haramu katika nchi yetu. Hakiwakilishi dini yoyote kabisa. Lazima wauliwe mara moja. Wasilianeni na Obama juu ya mikakati aliyotumia juu ya mfu wao Osama.
Mamlaka ya taifa la Somalia yanategemea kuanguka kwa gengi hili (kikundi cha wezi na watu wasio na maadili wanaoitwa al-Shabaab. Wezi hawa ambao hawana thamani wala maadili yoyote. Kuchezea maiti ni kitu cha mwisho mtu yoyote anahitaji kukiona. Je, kikundi hiki kinawafundisha nini watoto wetu na kizazi kichanga. Mimi ni Mkristo lakini ndugu na binamu zangu ni Waislamu, tunaishi kwa amani na furaha. Naamini kuwa dini ya Kiislamu hufundisha watu kuwa wanyenyekevu, watiifu na wanaomwogopa Mungu. Al-Shabaab wapo kwa dini yao wenyewe, hawaamini wala kutekeleza maamrisho ya dini ya Kiislamu. Tuwamalizeni vichaa na wauwaji hawa. ENDELEENI AMISOM, KDF NA JESHI LA SOMALIA kuwang’oa washenzi hawa.
Baada ya askari wetu kuifanya nchi yenu kuwa na amani, mtapaswa kurejea nchini kwenu.
MAKUBWA HAYA! WAPIGANAJI WAOGA WALIOUA MAITI YA SIMBA.
IFANYENI SOMALIA KUWA NA AMANI NA MLINDE ENEO LETU KWA THAMANI YOYOTE, HILO LILIKUWA KOVU, ENDELEENI!
AL-SHABAAB, TAFADHALI JISALIMISHENI AU MTAKABILIANA NA NGUVU KUBWA YA MAKOMANDO MACHACHARI WA KDF. ANGALIENI HATUA ZAO. HONGERA KDF.
Al-Shabaab imekuwa mwiba katika nyama ya nchi zote na Mwambao wa Mashariki. Kadiri watakavyosafishwa mapema, ndio bora kwa wote.
Al-Shabaab wataangamia!! Tendo hili la kikatili linaonesha tu kwa nini tunapaswa kuwafutilia mbali kutoka uso wa dunia…!! KDF wameifanya Kenya ijivune na kuthibitisha tena ukubwa wa jeshi letu katika kanda hii..!! Wapumzike kwa amani askari wetu mashujaa waliouwawa...bado tunashukuru sana kwa kujitolea huku kizalendo kwa jina la amani katika kanda yote.
KDF ni watu waliojipanga, al-Shabaab lazima wawe na tahadhari kubwa au wajisalimishe na kusahau masuala ya vita na kukubali kushindwa.
Majeshi yetu daima huvaa viatu vyeusi!!!!!!!!!
Mungu ibariki AMISOM kwa kuwafuta al-Shabaab kutoka Somalia. Tuombe kwa roho zilizoondoka za wale waliopoteza maisha yao kupambana na kikundi cha kigaidi na Mungu awarejeshe nyumbani salama ndugu, marafiki na waume.
Al-Shabaab inapaswa kwenda mitaroni. Wamesababisha aibu kwa ardhi yetu nzuri ya SOMALIA.
Ni waoga tu wanaopigana na miili ya maiti kwa vile hawatarajii kuwa maiti atajibu. Kama wangekuwa mashujaa, kwa nini wanakimbia wakati KDF wanaposhambulia. Wanapaswa kuchomwa katika jehanamu. Washenzi!!!!
Inahuzunisha kuona haya yanatokea nchini Somalia. KDF wanapaswa kukusanya nguvu zao kutokana na hofu zilizooneshwa na maadui wa ustaarabu wanaojificha chini ya Uislamu. Uislamu haufungamani na lolote kati ya matendo haya.
wanajeshi wa AMISOM wasife moyo. kila kunapokuja giza linazidi lakini kwa mda mfupi. unyama huu wadhihirisha kuwa ushindi haupo mbali
Ni bahati mbaya sana kusikia mtu akizungumzia kuhusu Kenya na Ethiopia kama maadui zao na bado wanakulana wenyewe kwa wenyewe. Hii inafananna na mtu kuokolewa na baadaye kumtafuna mwokoaji. Ikiwa al-Shabaab wanadai kuwa ni wanaume wa vita, basi wajitokeze uwanjani nakuonesha uanaume wao na sio kujificha. Hamna aibu. Hongera AMISOM.
Al-Shagaga wanapigana na maiti... WAOGA!
Hongera kwa vikosi vyetu vya KDF, pamoja na AMISOM na Jeshi la Taifa la Somalia. Al-Shabaab ni wahalifu na lazima washindwe na kufutwa kutoka uso wa dunia na sio tu kuondolewa nchini Somalia. Mimi ni Muislamu, ni Mkenya na pia ni Msomali- Kaka na dada zangu waliteseka kwa muda mrefu na hii ni fursa nzuri sana na Wasomali wote bila ya kujali wako wapi wanapaswa kuitumia.
Walifikiria kuwa wanaogopwa lakini sasa wanahisi uzito wake lakini kwa kweli, kwanini nyinyi al-Shabaab hamwezi kuwa binadamu?
Kwa kweli al-Shabaab na wafuasi wengine wanahitaji nasaha. Mnafanya dini yenu kuhukumiwa vibaya katika njia isiyofaa, na baadhi ya wafuasi wenu hawako hata kwenye eneo kuona jinsi kile hasa kinachoendelea. Mnakurupuka tu na kusherekehea kitu ambacho hata hamuelewi mizizi au malengo yake. Mmewahi kufikiria utawala wa al-Shabaab ikitawala? Kile wanachofanya sasa ndio kile watakachoendelea kukifanya ikiwa hatimaye watadumu na hawataweza. Mtakuwa wendawazimu kuwaunga mkono, mnafurahi maovu na kumuomba Mungu msaada mkidhani mtajibiwa. MUNGU HUPIGANIA WENYE WATENDAO HAKI SIO WATENDAO DHAMBI!
Al-Shabaab wanapaswa kufutwa ulimwenguni. Jumuiya ya Afrika Mashariki tuungane pamoja na kuwapiga Waislamu hawa wenye siasa kali na kiu ya damu. Wanaua watu wasio na hatia, kwa kweli wanapaswa kuondoka.
Al-Shabaab lazima ipoteze matumaini tu kwa sababu wameshashindwa.
Al-Shabaab ni kikundi kidogo tu, nadhani watu wetu wamewapa wakati, wanapaswa kuwasafisha wote kutoka wale wadogo wadogo hadi kiongozi wao mpenda damu na kuwaacha watu wa Somalia waishi kwa amani.
Yule ambaye anaishi kwa upanga atakufa kwa upanga, biblia inasema. Al-Shabaab imeishi kwa bunduki na kwa bunduki watakufa, Amin.
Ni mateke ya mwisho ya farasi anayekata roho. Enzi ya al-Shabaab zinakaribia mwisho wake sasa au baadaye.
Ni wa kibinafsi al-Shabaab … tunalipiza kisasi kwa vifo vya mashujaa na ndugu zetu.
Kwa kweli nafikiri al-Shabaab hawawakilishi chochote kinachohusu Uislamu. Matendo ya kigaidi na kuleta aibu kwa ubinaadamu si kitu ambacho kinafundishwa na Uislamu. Hili ni kundi la vijana wasiojua kusoma au kuandika waliolishwa kasumba ya kukidhi matashi ya watu wenye ajenda finyu wasio na nafasi katika dunia ya sasa inayopaswa kufurahikia mchanganyiko wa watu wake… jamaa hawa wanachofanya ni kuupa jina baya tu Uislamu. Aibu kwa manabii wa giza na imani zenu za siasa kali…Mungu wa kweli atashinda vita dhidi ya mafasiki na tutawaona Waislamu wa kweli wanaowakilisha Uislamu wa kweli, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu…
HEKO KWA WANAJESHI WETU LAKINI WASIJISALIMISHE.
Mungu aipe Somalia amani na awalinde wanajeshi wetu wa KDF kushinda dhidi ya al-Shabaab.
Jamaa hawa wanajificha chini ya Uislamu kusababisha mateso mengi dhidi ya Wakristo. Tunashangaa Ukristo unahusikaje na siasa zao chafu za mauaji ya maangamizi dhidi ya watu wasiokuwa na hatia, Ukristo unafundisha msamaha lakini inaonekana Uislamu unafundisha visasi na mauaji...
Shukrani kwa taifa kwa sababu sisi ni mashujaa
Wanajeshi wetu kawaida huwa na viatu vyeusi. Mwili huo si wa KDF.
Kwa nini al-Shabaab inatumia mitindo hii ya fadhaa kwenye mapigano? Al-Shabaab inapaswa kujua kwamba jeshi la Kenya liko kwenye hatua zake za mwisho na hakuna kitakachowazuia kukamilisha kile ambacho karibuni watakimaliza, vyenginevyo al-Shabaab wanarusha mapindi yao ya mwisho.
hawa watu ni kubafu tu.. wananafikiri wakitupa grenade na kufanya ukubfu huo wote watafika popote. hakuna, hapana watamalizwa wote, hawana maana kabisa. shidwe
Al-Shabaab-hesabuni upande wenu – sehemu munayoiita NYUMBANI, karibuni itakuwa tofauti, yenye amani na kutakuwa na nuru kila mahala. Kismayo itakuwa kigezo chake yenyewe. Viongozi wa al-Shabaab wataishia jela au kwa mauti...mlifanya kosa la kipumbavu na kitoto mwaka 1993 na kwa hakika mara hii mtakufa tu.. natamani nasi tungelikuwa na michezo yenu hiyo ya kitoto ya kuburuza miili...lakini sisi hatuna kwa sababu sisi ni wakuu.. tunajuwa kinachomfanya mtu kuwa mwanaadamu... hatuwaogopi...tutaendelea kuwafunza wanajeshi zaidi kupigana kwenye ardhi yenu…hisabuni siku zenu tu...punde na hivi punde tu...al-Shabaab itamalizwa Kismayo, karibuni sana...Amin...
Woga wapumbavu. Ama iwe wanakokota, wanapika na kuila miili ya maiti, yote ni mateke ya farasi anayekata roho. Tendo hili liwape nguvu KDF wakati wakiikomboa Somalia.
Jambo hili ni dhidi ya dini yoyote na Uafrika hasa utamaduni wa Somalia. Kwani watu hawa wanatoka wapi?
Siku zao zainahesabika.
Hili ni onyo kwa wale wote wanaodhani kwamba watavunja mamlaka na heshima ya watu wa Kenya, hadharini!! Ukitaka shari utaipata tu. Kenya ni jitu lililolala lenye kiwango cha juu cha uwezo. Mashambulizi mengine yoyote dhidi ya makanisa nchini Kenya yatapelekea hatua za kujilinda katika maeneo ya Wakristo. Tuna uwezo na nguvu za kujilinda dhidi ya Waislamu wenye siasa kali, na hatutadhalilishwa na kutishwa na woga wanaojidai kuwa watu wasio na makosa wakirusha mabomu yao na kukimbia kama wavulana wasiotiwa jandoni. Ushauri wangu kwenu mjiitao Waislamu wa siasa kali, acheni kufanya hivyo kabla hamjakumbana na hatua kali. MANENO YAMETOSHA!!!
Inasikitisha sana, ninahisi huzuni kwa familia yake.
AL SHABAAB...KAMA KWELI NYINYI NI MASHUJAA KWA NINI MPIGANE NA MAITI...AIBU YENU WENYEWE. TUTAWAUA NYOTE....
Mungu tu ndiye atakayeinusuru Somalia na Somalia ikipatikana, bara zima kwa hakika litafurahi. Mungu asikie dua zetu.
Hawa ni majeshi ya kishetani. Ni suala la siku chache kabla hawajamalizwa. Lango la motoni haliwezi kushinda. Hongereni KDF na AMISOM.
Al-Shabaab haihusiani chochote na Uislamu. Hili ni kundi la kigaidi linalowafanyia ugaidi watu na kuwavuta vijana wasio na hatia kuelekea njia isiyo sahihi. Al-Shabaab ni watu wasiojua kusoma an kuandika kabisa wasiojuwa ni nini Uislamu unasema wala wasio hata na hisia ya ubinaadamu. Lengo lolote walilonalo al-Shabaab, KWA IDHINI YA MWENYEZI MUNGU halitatimia kamwe. MWENYEZI MUNGU ALIYETUKUKA atusaidie kuwafurusha al-Shabaab. Wapo hapa kupandikiza chuki, si chengine chochote.
Kuna njia nyingi ya kuonyesha hasira, Wasomalia waliyakokota miili ya wanajeshi wa Marekani na kuwaambia Wamarekani wengine wanunue nyama yao, huko nyuma mwaka wa 1991 wakati hakukukuwa na kitu kama al-Shabaab. Hilo halimaanishi kwamba walikuwa wakipigana dhidi ya ukahaba kufanyika Kismayo, na unajua nini, Jihadi si chochote zaidi ya kuzuia mfumo wa kikafiri kuwepo duniani. Unachopaswa kukihofia kwanza ni kwa nini wanajeshi wenu wako Somalia. Kuwapeleka wanajeshi vitani bila ya sababu ni hatari zaidi kuliko kuiburuza miili ya maiti mitaani, kwa sababu, ingawa hili la mwisho linatokana na hasira, la mwanzo linatokana na upumbavu wa wazi.
Ninamjibu mtu mmoja ambaye anatumia jina la uongo la Uislamu...aibu yako mwenyewe...WAKENYA WALIALIKWA NA INTELIJENSIA YENU WENYEWE NA SASA WEWE NI MMOJA WA waigizaji….Kenya ilikuja kunusuru heshima yake....al-Shabaab waliitisha Kenya eti tutayalipua majengo na kisha wakadhani Kenya haikuwa na jeshi. Mliyataka haya...sasa mnajua kuwa tuna jeshi lenye utaalamu, mlitujaribu sasa TUTAWAFAGIA HADI KWENYE BAHARI YA HINDI MILELE NA kuwaacha Wasomali wa kweli watawale na waishi kwa amani....Mungu wa kweli wa baba yetu Ibrahimu aishi milele...Amin.
Al-Shabaab wataangamizwa kabisa ndani ya wiki mbili.
Naomba radhi kwa mtu ambaye hashukuru na kutambua msaada unaotolewa na KDF kuyaimarisha majeshi ya serikali ya mpito ya Somalia. Nimefurahi sana kusikia kwamba Wasomali wengi wamekombolewa kutokana na matendo mabaya na mateso ya waasi. Ahsante sana kwa msaada huu wa kijeshi. Hongera Wakenya.
Kenya ichukue tahadhari, inaweza kuwa mhanga.
Kenya ichukue tahadhari, inaweza kuwa mhanga.
Al-Shabaab sio adui wa Somalia. Adui wetu ni: Kenya, Ethiopia, Uganda na Burundi. Mungu akipenda tutawashinda vibaya AMISOM.
Itekeni Kismayu tafadhali. Waoga wanapigana na maiti au watu wasioweza kujilinda. Songeni mbele vijana. Ni wito na Mungu awalindeni katika kazi hii adhimu ya kusherehekea Somalia iliyo huru.
Al-Shabaab sio adui wa Somalia. Adui wetu ni Kenya na Ethiopia.
Kenya itashinda vita hivi.
Niko tayari kufa kuilinda Kenya. Watu wa al-Shabaab mnauliwa. Nawaonya kaeni mbali na KDF la sivyo nyote mtakufa.
KITENDO KIBAYA KWELI WELI, WATAKABILIANA NA HUKUMU YA ALIYE JUU ZAIDI.
Al-Shabaab ni waongo na waoga. Nani asiyeweza kuona kuwa yule si askari wa Kenya? Jaribuni ujanja mwengine. Tayari mmekwisha!!!
alshabab endeleeni na kazi!!
kenyan soldiers do not wear white boots. hi ni propaganda ya maharamia.
Hii ni jamii ya mtu kula mtu, naamini kuwa KDF karibuni watarajea nchini kwao salama na amani itatawala tena nchini Somalia. Mungu isaidie nchi hii ya Somalia.
Al-Shabaab, mmekwisha. Mtasafishwa na watu wa Somalia na majirani wataishi kwa amani daima. Vita imara.
Naam, walianza na kuingilia kati eneo la Kenya na kwa kuwa Wasomali wengi wameishi kwa muda mrefu sana, baadaye kama binadamu na ndipo raisi alipoona wamezidi na kuwaambia ni wakati wakulipa… Nchi yangu haihusiki katika mzozo wowote lakini ninauhakika Wakenya wana haki ya kuilinda nchi yao kwa gharama yoyote, kwa hivyo baadhi yetu lazima tuelewe kuwa ni Uislamu tu unawasumbua wasio Waislamu kama kule Irani ambako mhubiri alikuwa anyongwe lakini akaachiwa huru siku chache zilizopita. Kwa hivyo uko wapi Uvumilivu wa kidini. Kwa nini tuna mataifa ya Kiislamu wakati hatuna mataifa ya Kikristo? Ninao marafiki asilimia 40 walio Waislamu na hatukubaliani juu ya baadhi ya masuala lakini tunasaidiana wakati wote bila ya kujali chochote. Kwa hivyo, vituko hivi vilivyomo Somalia, ni wakati wa Afrika sasa kuwasafisha.
KDF hawatani, al-Shabaab ni nusu maiti.
Al-Shabaab wamekwisha kwa hivyo AMISOM endeleeni kuwatwanga hadi dakika ya mwisho. KDF, kazi nzuri, tunawaombeeni.
Wajinga wasio na aibu! Shukrani kwa Mungu kuwa dini yetu ni ya amani, ambapo tunapenda na kuheshimu maiti … Ni balaa gani hili la viumbe hawa wanaoitwa al-shagoons?
Wameshindwa vita, hayo ni mateke ya mwisho ya farasi anayekata roho. Natumai kuwa AMISOM itawauwa wote
Hawa ni waoga. MAITI HAWAPASWI KUTENDEWA HAYA. Kwa nini hamkabiliani na wanaume? Kama KDF wangefanya sawa na hivyo, nadhani barabara zote zingekuwa zimejaa miili ya al-Shabaab.
AL-SHABAAB ni jambo la historia. ENDELEENI KDF na AMISOM na MUNGU WETU Mwenyezi yuko mbele na HATAWAANGUSHENI. Hongera AMISOM na KDF. AFRIKA NI KWA AJILI YENU - AMIN
Asanteni askari wa KDF, mmetufanya tujivunie, tuko tayari kuwasaidieni ikiwa mnatuhitaji. Ni vita ambavyo tutashinda kwa gharama yoyote ile.
Hatimaye shambulio lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu limeanza. Tukae na kuona matokeo yake. Ninawatakieni mema Majeshi ya AMISOM, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.
Askari wa Kenya watawashinda wahalifu hawa kwa sababu ni jeshi lenye nidhamu sana ambalo linasimamia mema katika bara hili. Al-Shabaab ni waoga ambao wanawafanyia ugaidi watu wasio na silaha na kukuza imani kuwa ni askari na wala sio majambazi. Tunawaona na mikono yao hewani wakati wanapolowanisha chupi zao wakati wanapokutana na askari wa kweli. Kuburuza miili mitaani ni tendo la kiwoga na halitawasaidia muda wao utakapowadia.
Mungu aibariki Kenya na KDF kwa jumla. Tunakukumbukeni katika maombi yetu. Kuweni imara na endeleeni mbele, hawa ni kama panzi tu kwenu. Mungu tayari ameshawasalimisha (al-Shabaab) mikononi mwenu. Wamalizeni mara moja kabisa kabisa. Mjaaliwe kurejea nyumbani kwa ndugu zenu baada ya kushinda vita kwa mafanikio. Kila siku tunakuombeeni.
Oh Mungu Wangu! Hili haliaminiki.
@Muislamu. Msitumie jina hili katika blogu hii ili kudhalilisha imani ya Kiislamu, maoni yenu yanaivunjia heshima imani yetu. Uislamu unatetea umoja wa familia na amani kwa Waislamu wenzetu na wengine wote. Mimi ninaishi Kismayu, al-Shabaab na mengi ya matawi yao wanafanya maisha yetu kuwa magumu. Nadhani hamuishi Somalia kama mnawaunga mkono al-Shabaab au nyinyi ni moja wa wanaofaidika kutoka kwao. KDF na majeshi mengine yaimarishe amani pamoja na vikosi vingine, hatuwezi kuwa na amani sisi wenyewe. Wazazi wetu walishindwa, bunge letu linapigana, baadhi yetu tunapigana mabomu tu. Misikiti yetu ina misingi ya koo/makabila. Kitu pekee tunachosikia ni "ukoo, familia, kabila", walichukua kile kilichotarajiwa kuwa chetu na vipi sisi vijana tutapingana kuyakataa wakati tunapokuwa imara. Uislamu haupo kwa ajili ya kulipiza kisasi au kuwa na hamaki, kinyume chake ni dini pekee ambayo inaelezea amani, maelewano na umoja kwa uwazi. Somalia iliyo kubwa
Hawa majamaa ni washenzi na wanapingana na Uislamu. Unapiganaje na maiti na kutarajia kushinda vita? Hili ni tendo ovu, Waislamu wote wanapaswa kukilaani kikundi hiki.
@ Askari wa Kenya .. Mnaudhi kama ilivyo al-Shabaab yenyewe. Hamuoni wanajaribu kupindisha akili za watu ili waamini kuwa hivi ni “Vita Vitakatifu”?. Huu ni ulemavu sana na mnaonekana mmeangukia katika propaganda zao. Vita hivi havihusiani kabisa na itikadi za “Uislamu dhidi ya Ukristo” kama ambavyo al-Shabaab na wafuasi wao wanadai. Wakaazi wa Kismayu na kila inchi moja ya Somalia ambao wamekuwa wakikandamizwa kwa miaka kadhaa ni Waislamu, askari wa TFG wanaopigana kuikomboa nchi yao ni Waislamu, hata baadhi ya askari wa Kenya ni Waislamu. Uislamu unasimamia amani na haiwezekani kwangu kuonesha ni kiasi gani (al-Shabaab) wao wenyewe ni Waislamu. Tunawaombea KDF/TFG/AMISOM bila ya kujali asili, uzawa, rangi, kabila na dini zao. Tunamuomba Mwenyezi Mungu kuwalinda wote, kukomboa na kurejea makwao kama kitu kimoja. Nimewasilisha kesi yangu.
Al-Shabaab inakaribiwa kuanguka miguuni mwake. Askari wa Somalia na Kenya waendelee na mchamchaka. Ushindi upo umbali wa mkono umoja tu na lazima tusiwe wakaidi. Aina yoyote ya vitisho lazima viwekwe kando. Hivi sio vita vya kidini wala baina ya nchi; ni vita dhidi ya uhalifu na matendo ya kinyama na mnyama ni al-Shabaab.
Somalia isimame!
Hongera KDF, AMISOM na serikali ya mpito ya Somalia. Mungu awabariki kwa kujitolea mlikofanya na al-Shabaab waungue motoni. Tumechoshwa na uhalifu wa kikatili na lazima wapelekwe The Hague kwa shehena na Mungu wetu awalaani kwa laana ya milele kwa vitendo vyao vya kipuuzi. Na hawa wanahubiri nini? Ikiwa hiki ndicho wanachohubiri, ni bora nibakie kuwa kafiri, kama wao wanavyotuita.
Ikiwa wanaogopa kupigana na AMISOM, wangejisalimisha kuliko kufanya mzaha na maiti. Hii inaonesha kuwa wanakaribia kujisalimisha. Hamna aibu al-Shabaab!
KISMAYU SISI TUNAKUJA. TUTAUA MABAKI YOTE YA AL-SHABAAB NA KUTUPA MIILI YAO BAHARINI KWA PAPA. IDUMU KDF. ASKARI DAIMA HAWAFI, HULALA KWA SABABU ZA KIMBINU.
Genge la majambazi ni balaa kubwa kwa Afrika ya Mashariki. Ninaomba warejewe na akili zao haraka. KDF, nyinyi ni wenye nguvu kubwa barani Afrika. Mwenyezi Mungu awajaalieni busara za kuwadhibiti al-Shabaab.
ASKARI WA KENYA, NYINYI NI WATAALAMU. MALIZENI KAZI YENU NA MREJEE NYUMBANI
Al-Shabaab hatimaye watashindwa tu na KDF kwa sababu ya matendo yao maovu na Somalia karibuni itakuwa taifa huru.
Al-Shabaab wameandikiwa kuvunjwavunjwa. Ni suala la wakati tu, wote watakuwa wamekwisha.
Mema daima yatatawala mbele ya muovu. Kuburuza mwili wa askari aliyefariki, si lolote bali woga. Hongera AMISOM, TFG na wale wote wanaosaidia vita hivi dhidi ya ugaidi...Subirini, ushindi unakuja na ardhi ya Somalia itajawa na maisha. Mawazo na dua zetu ziko pamoja nanyi katika vita.
Ni sawa, tunavumilia machungu lakini al-Shabaab, mmekufa.
Kwa alkebab, viashiria vya MAPAMBO YA VITA. Bila ya shaka KDF WAMEWAANGAMIZENI. Kumburuza askari mmoja au wawili, au hata kumi katika njia yoyote ile hakutateteresha moyo wa mtu yeyote. Kinyume chake, hii ni sababu milioni zaidi kwa nini al-Shabaab na washirika wao LAZIMA WAFUTWE kutoka uso wa dunia! Tumeshuhudia al-Shabaab wakiogelea kwenye damu zao wenyewe. Huko Kismayu KDF ITAWAVUNJENI na mtavunjwa na KDF. MUNGU AKIPENDA! Kwa wale MASHUJAA walioanguka vitani na FAMILIA zao, tunawaamkieni. Mtaendesha daima pamoja na majenerali ambao wamekwenda kabla yenu. Jenerali Gen Montgomery, Jenerali Romme, Jenerali TsunTzu, Gen Alexander the great, Jenerali Kustov, na wengine. Mungu awajaalie mpumzike katika amani ya milele na nyoyo zenu za USHUJAA ziungane nasi daima na daima zaidi!
Chochote chenye mwanzo kina mwisho wake. Vijana wa al-Shabaab mnafikiri mmeshashinda lakini ni kuwa tu mnakaribia kushinda. Lakini mnafikiri mtaweza kushinda? Mungu walinde askari wetu wapendwa katika kuyashinda matendo haya ya kishetani na kuwaweka jirani wetu wa Somalia katika amani.
Kuburuza maiti ya askari aliyefariki kunaonesha ushindi au upuuzi? Al-Shabaab ni kikundi tu cha mijitu mioga inayojaribu kuwatisha watu wa Somalia kupitia mbinu zao chafu lakini wakumbuke kuwa Ugaidi hauna nafasi katika Karne ya 21 na dunia itaungana ili kuwasafisha. Mungu awaapizeni nyote viongozi wa al-Shabaab na wafuasi wenu!!!!!!!!!
Hayo ni mateke ya mbwa anayekata roho!!!
Kuburuza mwili wa askari wa Kenya hakutatuzuia kumaliza ukatili huu. Tuko nyuma yao kwa asilimia 100. Tuko nyuma ya AMASIM wakati wote.
Sidhani hii ni ukweli kwa sababu al-Shabaab wasingeweza kupata fursa ya kuburuza mwili kutoka kwa majeshi ya KDF au TFG. Ni matendo ambayo yametengenezwa tu katika mtandao.
Hata al-Shabaab wanawaua watu wao na huwavisha sanda. Vita vinaendelea hadi ardhi ya Somalia iwe huru. Hii ni gharama ambayo askari wetu wanalipa kwa ajili ya amani kwa ndugu zetu.
Hawa al-Shabaab wanahitaji kutendewa hivyo hivyo ambavyo wanawafanyia maiti. Hamna aibu, waoga wa karne!
Picha hii inanikumbusha mapango ya Shimoni katika mwambo wa kusini, inaweza kuwa inaungana kitabia na imani baina ya al-Shabaab na Waarabu wawindaji/wafanyabiashara wa watumwa.
Hamuwezi kutuzuwia, bado tunakuja, mmetufanya tuwe imara zaidi. Tutawaleteeni amani kama mbavyo tumefanya kwa nchi nyingi. Ninajuvunia kuwa Mkenya na kupelekea amani ambako amani haijulikani na wengi.
Wa Afrika tutatumiwa mpaka lini?...maana huu ni unyama sana ..Mbona hamsikii wao wazungu wakipigana?...kazi yao kutuchonganisha sisi tuuu...Acheni ujinga.. Pendael (Tanzania)
Inahuzunisha. Ninamuomba Mungu kwa amani ya kudumu nchini Somalia.
Mungu walinde watu wetu wa KDF, lazima tuwasafishe al-Shabaab nje ya Afrika. Msiogope kufa kwa ajili yao kuwa na amani kwa sababu tunawapenda watu wa Somalia. MUNGU KUWA PAMOJA NA ASKARI WETU. Lazima tushinde vita kwa jina la Yesu.
Al-Shabaab ni genge la wahalifu ambao lazima wasafishwe kutoka uso wa Somalia. KDF, ongezeni mwale wa moto. Hakuna huruma hata kidogo.
Kwa askari wote wa Kenya (KDF) na AMISOM yote, Mungu awe pamoja nanyi, awalinde, awaangalie na awarejeshe nyumbani salama. Shalom! Shalom! Shalom!
Al-Shabaab ni waoga katika kinyago cha simba.
Uislamu na ugaidi, al-Shabaab, al-Qaida...vyote hivi ni visawe vya unyama na uwakala wa muovu kabisa (Shetani), lakini ni Utukufu wa Mungu unaotupa ushindi kupitia Yesu Kristo.
KDF, tunawaunga mkono kikamilifu ili kuleta busara nchini Somalia. Mapambazuko ya Somalia yako karibu, Al-Shabaab na al-Qaida tayari wameona machweo. Wameona vita ambavyo daima hawakufikiria maishani mwao. Kwa hili tunaweza kusema tu kuwa linatokea katika filamu kwa nchi zingine lakini kwa Kenya tumeliona katika maisha halisi. Mungu yuko mstari wa mbele, mfuateni Yeye.
Haya ni mateke ya farasi anayekata roho. Tutashinda dhidi ya uovu huu. Mungu ibariki operesheni yetu ya pamoja ya AMISOM na jeshi la Somalia.
Sijawahi kuona au kusikia popote duniani dini inayofundisha wafuasi wake wasiheshimu watu wa dini nyengine. Hatuwezi kuwa sote Waislamu na ikiwa hamtaki kuingiliana na wasiokuwa Waislamu, waacheni kwa amani. Kwa hivyo manasema Kenya imewashambulia huku tukitarajiwa kuangalia tu mnavyowateka watalii na kuharibu jina la letu na uchumi wetu. Wasomali wanapaswa kukua.
Ninatoa hongera kwa al-Shabaab na wafuasi wao na wale walio tayari kufa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Mmewahi kujiuliza wenyewe kitu gani wanafanya askari wa Kenya nchini Somalia? Mnafikiri Kismayu ni ya Wakenya. Ninasema tene na tena, Daima mujahidina wa AL-SHABAAB, na tuko tayari kufa kwa nchi na dini yetu. Lakini ushauri wangu kwa watu wa Kenya, tafadhalini msipotoshwe na viongozi wenu.
Wanajaribu kuwatisha AMISOM, walifanya hivyo hivyo kwa Wamarekani mwaka 1993. Tumaini lao ni kuwa KDF itajitoa kama ilivyofanya Marekani. Lakini nadhani mara hii wamekosea. Tunaomba vita hivi vimalizike. Mungu awarejeshe nyumbani mashujaa wetu wa KDF wakiwa salama na wazima. Msiruhusu tena mwanamme/mwanamke wa Kenya kuburuzwa. Amen.
Jambo zuri ni kuwa wamefunzwa na wamedhamiria kushinda na wanaelewa kuwa vita ni vita na hata kama unakwenda ukiwa umekusudia kushinda inawezekana pia kutorejea nyumbani, lakini ikiwa mmoja anafariki kabla ya vita kumalizika, ieleweke kuwa kuna vitu vinastahiki kupiganiwa kama Dustin Evan anavyosema katika nyimbo yake, ikiwa nitakufa kabla hujaamka.
KDF, tayari mmeshakula ng'ombe mzima, malizeni mkia uliobakia na rejeeni nyumbani kwa fahari _namunyu peter, Mombasa, Kenya.
Huu ni ushenzi.
Kwa hivyo wanafikiri kwa kufanya hivi watatuzuwia tusifike Kismayu? Kismayu, tunakuja huko.
Watu wa Somalia wanapaswa kusaidia kitengo cha vikosi vya usalama vinavyosimamiwa na serikali ya Ethiopia ili kuwakamata maadui hawa wa amani.
Al-Shabaab inapaswa kumalizwa, wanatumia kitabu kitukufu kujaribu kuhalalisha dhamira yao.
Huu unaitwa Woga wa daraja la kwanza, kwa nini wanaonesha miili ya wafu? Kama wangekuwa mashujaa kweli, basi wangezika wanachama wao 150 waliofariki katika mji iliyotekwa.
Tuliyo nayo ni misheni, tunachohitaji ni ushindi, tunachojua ni kuwa tuko imara na tunachodhamiria ni amani. Al-Shabaab wanasukumwa kwenye jabali la majaliwa yao. Sote tusimame imara na askari wetu.
Endeleeni kuwaponda wahalifu hawa wanaofanyakazi kwa jina la al-Shabaab. Waueni bila kuchagua na wasafisheni kutoa uso wa dunia. Hawa wahalifu waache kuingiza Uislamu katika matendo yao ya kihaini. Wanataka Somalia isiyokuwa na sheria ili waendelee kukusanya pesa za kikomboleo kupitia uharamia. Waelewe kuwa hata wakaazi wa Kismayu ni Waislamu na wanachukizwa na matendo yao.
Ikiwa hii ndio gharama ambayo watu wa Somalia na AMISOM watalipa ili kukomboa ubinadamu na watu wa Somalia kutoka kwa kikundi hiki katili, basi na iwe hivyo.
Inahuzunisha. Hata wanajali kwa kile kilichotokea kwa makomredi wao 36 waliokufa katika ugaidi?
Ni wapi duniani genge la washenzi sana kama hawa linaburuza miili ya maiti mitaani mwa mji na watazamaji kulazimishwa kuzunguka na kudai kuwa chochote karibu na serikali? Al-Shabaab ni waovu ambao lazima wasafishwe katika ramani ya dunia na hata katika msamiati wa lugha. Ikiwa ni sawa na ambacho al-Qaida wanakisimamia basi si dunia itaangamia?
kwani hawaishi
Wakati mmoja anapouliwa na kuburuzwa, askari wengine wako wapi kuukoa mwili. Mungu awe pamoja nao popote wanaposhambulia. Amin.
Hawa al-Shabaab lazima wasagwe kabisa. Wanawezaje kuburuza askari wetu mitaani! Mungu awaongoze askari wetu ili wamalize kazi hii ya heshima.
Tutashinda sio kwa mtindo wa kujionesha bali kwa kupitia uvumilivu. Kazeni buti KDF na yote yatakuwa mema kwenu.
Huu sio ubinadamu. Kwa nini mnamtendea mtu aliyekwisha fariki namna hii? Al-Shabaab ni wakatili.
Matendo haya ya kishenzi na kikatili toka kwa al-Shabaab hayatawasaidia, la muhimu ni kuwa katika siku chache zijazo, al-Shabaab hawatakuweko tena na Kismayu itaanguka kwa TFG na watu wa Somalia. Aibu iwe kwenu enyi wafanya biashara wa vifo na uharibifu. KDF na AMISOM nyote daima mko katika dua zetu na mtawang'oa mashetani hawa wauwaji kutoka Somalia.
Waliburuza askari wawili tu, KDF walikuwa na uwezo wa kuwaburuza 73 lakini hilo halina maana. Watachinjwa kama mbuzi na amani itapatikana kwa Wasomali. Mungu ibariki AMISOM. Mungu ibariki Kenya.
Al-Shabaab ni waoga. Inahusu nini mnapigana na miili ya maiti? Kwa kweli karibuni mtakufa na mtakufa kifo kibaya zaidi kuliko MASHUJAA hawa mnaodhani wamekufa. Kwa taarifa zenu, nafsi za askari hawa ZIKO HAI na ndio sababu nyinyi al-Shabaab mtakufa, sio tu kufa lakini KUSAFISHWA. Hongera KDF na MUNGU awabariki.
Waacheni watu wa al-Shabaab wafunzwe somo ambalo linaweza kuwafanya wasisahau kwa maisha. Watu wa Somalia wapewe uhuru ambao wamekuwa wakiupigania muda mrefu.
Yote inahusu maisha na kifo. Haijalishi chochote wanachofanya, mwili wa maiti hauhisi maumivu. KDF, wakabeni kooni hao. Hakuna kurudi nyuma, hakuna kujisalimisha. Mashetani wa al-Shabaab wanaojidai ni Waislamu watakiona cha moto. Kwa kweli hawa sio watu wa Mwenyezi Mungu. Ni mawakala wa Shetani, wakiwa na sifa zote za maisha ya kishetani.
Walifanya hivyo mara tu baada ya kuanguka kwa Siad Barre. Nadhani lugha hii tata ya haki za binadamu inatugharimu sana. Kwa nini wakaazi wa Kismayu hawapewi muda wa mwisho kujitokeza kwa uchunguzi baadaye kuupindua mji chini juu?
Ni maisha yasiyo na hiyana ambayo KDF imejitolea. Wanatakiwa watu kama hawa katika kizazi hiki ikiwa kuna kitu chochote chema ambacho kinaweza kuokolewa Afrika na katika nyanja zote za maisha, hasa, kwa wanasiasa wetu wa Kenya, Waroho Wasiokuwa na Aibu. Hawana aibu, watu ambao wanafikiria yaliyo chini ya Matumbo yao TU.
Wanamgambo wa al-Shabaab wanafanya kama wendawazimu. Ili kuiokoa Somalia kama nchi, lazima mataifa yaungane, kuandaa mpango wa kuwatambua Wasomali safi, wasiomtendea mtu madhara, wafanyakazi hodari na wanaofikiri vizuri. Asilimia kubwa inafanywa na watu hodari sana nje ya nchi. Kwa pamoja yatoeni magenge ya wahalifu yaliyobaki nyuma na wale watakaokataa kujisalimisha.
Hili haliaminiki kwa wahuni hawa kufanya tendo kama hili la kikatili. MUNGU IBARIKI KDF YETU NA AMISOM.
Ninasifia kazi iliyofanywa na majeshi ya pamoja. Al-Shabaab wamevunjika na karibuni watakuwa kitu cha kupita. Marekani inapaswa kutoa msaada zaidi kwa majeshi yetu.
Mbwa aliyezingirwa ukingoni atamtafuna yeyote. Kitu kama hicho kingefanyika kwa ajili ya Al-Shabaab.
Ninaendelea kuomba kwa ajili ya AMISOM na familia zao. Matendo ya al-Shabaab ni ya kishenzi na mateke ya mwisho ya farasi anayekata roho. Mtashinda.
Hawa al-Shabaab hawawezi kuona najisi inayozidi matendo yao ya kinyama. Ninajisikia kuruka hadi Kismayu kwenda kuwasaidia wazalendo wetu wa KDF.
Al-Shabaab ni waoga na waongo kwa dini na watu.
Huu ni ushenzi kweli. Je, makafiri hawa wana heshima yoyote kwa binadamu? Haishangazi, ndio maana hawaungwi mkono na watu, lakini Mungu akipenda, siku zao zinahesabika, na watauliwa na upanga huo huo.
Kwa nini al-Shabaab hawawi washupavu na kuwakabili vijana wetu wa kuogopesha kuliko kupiga wafu. KDF, wasafisheni mara moja. Tunawaungeni mkono.
Waombaji hawana chaguo mbadala bali kujisalimisha! Hawaoni aibu.
Kwa hivyo wanapata nini kwa kuburuza miili? Waoga msio na haya. Jitokezeni mpambane na wanaume wenye sare, ambao wanafanyakazi chini ya mwavuli na kuongozwa na Mwenyezi Mungu.
Wafu wanapigana na wafu. Al-Shabaab ni wafu, ni suala la masaa tu al-Shabaab watakuwa katika vitabu vya historia. Kuburuza miili ya wafu hakuwezi kuvitisha vikosi vyetu, walivyo na ushujaa. KDF, MMESHASHINDA!!!
Waacheni wafe wote kwa sababu wanawashambulia Waislamu.
Waacheni waonje ladha ya risasi; ni vizuri kuona askari Mkristo akiburuzwa katika mitaa ya Kismayu.
Ni vyema kuua askari wa Kenya ambaye anavamia ardhi yenu, ni dhamiri gani wanakuja Somalia, ni nini misheni yao? Wanawaua watu wasio na hatia na kubaka wasichana. Waacheni waonje ladha ya risasi, au sio? Nyinyi ni wavamizi, serikali ya Kenya ilikataa kuwaambia watu wa Kenya Askari wa Kenya waliouawa. Tumegundua kuwa si chini ya 29 waliuliwa katika vita vya mwisho.
Al-Shabaab ni waoga, watasagwasagwa kama Sheikh Rogo.
Kuchezea maiti ni tendo la kishetani. Waacheni wafu wapumzike kwa amani. Siku moja miili yenu itachezewa hivyo hivyo. Walifanya hivyo kwa askari wa Marekani na askari wa Pakistani pia. Kumekuwepo na amani nchini Somalia kutokana na matendo yale.
Binafsi ninalaani kwa maneno makali kabisa tendo la kinyama la kuburuza miili iwe ya KDF au AMISOM hata ya askari wa Mpito. Angalia tofauti baina ya kuteka na kujidai. Kenya itabakia katika historia kwa kile walichofanya. Kwa hakika ni majeshi ya uvamizi. Subirini hadi Kismayu ianguke katika mikono moto ya Kenya!
MUNGU awape watu wetu nguvu ili kuwashughulikia wahuni hawa.
Huyo si askari wa Kenya, hebu angalia viatu kwa karibu.
Hiki ni kitendo kiovu kabisa na kisichokubalika kwa ubinadamu, hakuna dini kubali hili. Hili ni tendo la kishenzi la kulaaniwa na wote. Idumu KDF, tuko pamoja nanyi njiani kote. Mungu awe pamoja na askari wetu shupavu wanaopigana kwa ajili ya uhuru wa majirani zetu wa Somalia.
Wekeni habari za karibuni za duniani – (habari za karibuni za al-Shabaab huko Kismayo).
Ninaomba tu kuwa hili limalizike karibuni. Watu wa Somalia wanahitaji maisha ya kawaida yasiyo na sauti za risasi.
Vita hivi vitachukua muda mrefu na majeshi ya Kenya yatakiona moto.
Kwa maonesho haya ya kiwoga al-Shabaab wanajaribu kuwashtua na kuwatisha askari wa AMISOM. Propaganda zao hazifanyi kazi kwa sababu wameamua kufanya vitendo vya kishenzi. Vifo vyao vitakuwa vya kukirishisha zaidi. Lakini waelewe jambo moja, dunia inaangalia na AMISOM haitasita kwa lolote hadi kuwatokomeza majambazi hawa, Mnakumbuka walipowaburuza askari wa Marekani kabla? Mara hii dunia imeamua na askari waliopata mafunzo ambao hawatatishika wala kupumbazika. Ikiwa hawa sio makafiri basi wabakie Kismayu na kujaribu kulizuwia jeshi letu lililodhamiria na lenye uwezo kwa jina la AMISOM. Hongera AMISOM. Watwangeni mashetani hawa moja kwa moja, TUNATAKA SOMALIA ILIYO HURU NA SHERIA KUREJESHWA
Dua zetu ziko pamoja na watu wa Somalia wanaokandamizwa, na pamoja na ndugu zetu wa Kenya ambao wamekufa kishujaa wakijaribu kuikomboa Somalia.
Al-Shabaab ni watu hatari katika dunia hii ya tatu. AMISOM lazima wawapige na kuwang’oa kutoka Somalia na kuwapa watu wa Somalia nchi yao ili kuiendeleza. Katika picha tunamwona mpiganaji wa al-Shabaab akitoa mwili wa askari aliyeuwawa akisaidia wana raia ili kumtoa na wanadai kuwa mwili ni wa askari wa Kenya. Tunaweza kujua vipi kuwa huyo ni mtu wa Kenya aliyeuwawa. Mwili ule lazima utakuwa wa al-Shabaab ambao waliubadilisha ili uonekane kama ni askari wa kenya. Hiyo siyo ukweli. Wanasema uwongo kuionesha dunia juu ya mauaji ya wapigananji wengi wa Kenya dhidi yao. Tunaelewa askari wa Kenya wana nguvu na mbinu katika vita. Hawauliwi tu kama watu wasio na mafunzo kutoka nchi mbali mbali za kigeni kama vile Israeli, Marekani, Uingereza kwa kutaja chache. Tunaziomba nchi zote za Afrika kuungana na kuwa na lengo moja la kusaidia katika vita vya Somalia dhidi ya wapiganaji wa al-Shabaab ili kuwatoa nje ya Somalia na ikiwezekana kuwafuata kwenye vichaka wanakojificha na kuwang’oa kabisa nje ya Somalia.
Inachukiza, kuhuzunisha na unyama.
Chochote wanachofanya, ufumbuzi wa kurejea katika hali ya kawaida kwa faida kuu ya Wasomali na eneo hili lazima uendelee. Lazima watashindwa na kuwajibishwa kwa uhalifu wao dhidi ya binadamu.
Mara nyengine ni vigumu kukubaliana na habari kama hizo lakini kwa kawaida hiyo ndiyo gharama tunayopaswa kulipa. Mungu atasaidia.
Al-Shabaab ni genge hatari sana ambalo linahitaji kumalizwa bila huruma.
Aibu juu ya Uislamu...mbona mnajiepusha na matendo haya ya kikatili na huku mnawafunza haya katika Madrasa.
Ndio sababu lazima kipigo kiendelee!!
Ni jambo jema sana kuheshimu maiti.
Maisha ya binadamu lazima yaheshimiwe, iwe mtu yuko hai au amekufa. Bora kuiteka Kismayu sasa.
Hili n jambo la kipuuzi kabisa kulifanya na kinyume na Makubaliano ya Geneva, hata kwa Waislamu wenzao wanakubaliana kuwa ni vibaya na ni ukosefu wa maadili. Lazima wasafishwe kutoka uso wa dunia hii ya Mungu.
Ni kitu kinachoudhi kwamba binadamu wanajidhalilisha wenyewe kwa matendo kama hayo. Chochote watakochokuwa wanaamini!
Inasikitisha sana kuona watoto wetu wavulana wanauliwa katika ardhi ya ugenini. Warejesheni nyumbani Kenya.
Wapuuzi al-Shabaab, magaidi nyinyi. Hongera KDF na wengineo kwa kuikomboa Somalia kutoka kwa wahuni hawa.
Mungu anaipenda Somalia, na atawakomboa.
Al-Shabaab LAZIMA WAFE.
Hakika al shaabab ni shetani mwenyewe. Katika dini tunafunzwa mungu kaumba binadamu kwa sura yake mwenyewe. Hivi kuuburuza mwili wa mja aliyefika mbele ya mola wake kwa hukumu ndio uislamu wa al shabaab?
Umoja wa Afrika unafanya kazi ya kuthaminiwa. Kazi nzuri.
Waacheni maadui wa amani waporomoke na kupotea. Dunia haina nafasi kwa itikadi za siasa kali. Hawana aibu al-Shabaab.
Poor kenya tokeni somali please njooni mlinde nchi yenu.
Ni upuuzi wa hali ya juu kuburuza maiti mitaani. Hawa jamaa lazima wafukuzwe nje ya mji wetu na askari wetu shupavu wapo kwa ajili ya kazi hiyo. Mungu wabariki wavulana na wasichana wetu wakati wakifanya kazi yao ya kimataifa kwa niaba yetu sote.
Mateke ya mwisho ya farasi anayekata roho!
Hali gani hii ya kusikitisha! Mkenya kuburuzwa mitaani inauma sana. Ewe Mungu wangu, awe pamoja nanyi K.D.F na AMISOM. KWA MUNGU KILA JAMBO linawezekana. Msife moyo.
Haya ni matendo ya kiwoga yanavyofanywa na wahuni washenzi hawa wanaoitwa al-Shabaab. Haitawasaidia kitu pia. Askari wetu wa Kenya, Somalia na AMISOM kwa jumla hawatishiki, wako mbali zaidi ya kile ambacho al-Shabaab wanafikiri katika fikra zao nyembamba. Wanawajieni, enyi al-Shabaab, mmekwisha, hakuna pa kutorokea.
Al-Shabaab katu haitafanikiwa na matendo yake ya ukatili na matendo mengine maovu ambayo imekuwa ikifanya. Ielewe kuwa siku zake zinahesabika na dada na kaka zetu wa KDF wako tayari kufa ili kurejesha amani nchini Somalia. Siku zao zinahesabika, jambo jema wanaloweza kufanya ni kuokoa maisha yao kwa kujisalimisha tu kwa vile watasagwasagwa kama siafu na mchanganyiko wa vikosi vya AMISOM na KDF.
Vijana wa al-Shabaab wanapaswa kuacha kupigana na wafu. Ama wakabiliane na wanaume na kuuliwa au wajisalimishe. Vijana wasio na aibu!
Hatimaye Somalia na watu wa Somalia watakuwa huru kutokana na al-Shabaab and al- Qaida.