Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |
Agosti 29, 2012
Somalia ilishuhudia tukio la kihistoria hapo Jumanne (tarehe 28 Agosti) wakati uchaguzi wa bunge ulipofanyika nchini kwa mara ya kwanza kwa muda wa miaka 20.
Wabunge wapya walimchagua Mohamed Sheikh Osman Jawari kuwa spika wa nchi wa bunge, hatua inayochukuliwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa na maafisa wengi kama ni uzoefu wao wa kwanza katika historia ya karibuni ya Somalia.
"Najisikia heshima kwa kuchaguliwa kama spika wa kwanza wa [Somali] wa bunge ambalo si la mpito na natumai tutaweza kuwa na bunge ambalo litatumikia watu linaowawakilisha," Jawari alisema baada ya kuahirishwa kwa kikao cha bunge hapo Jumanne. "Uchaguzi ulifanyika kwa njia ya uwazi na ninatumai kuwa Somalia itaendelea na chaguzi ziitakazofanyika kwa njia ya kidemokrasia."
"Nina imani kuwa bunge hili litaisaidia Somalia kufikia mabadiliko chanya katika masuala ya usalama na utawala," alisema.
Jawari aliwaambia waandishi wa habari kuwa kikao cha bunge kitaendelea tena siku ya Alhamisi wakati chombo hicho kitakapojadili vipi na lini uchaguzi wa rais utafanyika .
Pia waliochaguliwa ni manaibu spika wawili: Jaylaani Nur Ikar, waziri wa zamani wa kazi za umma na ujenzi upya katika serikali ya mpito ya shirikisho, alishinda nafasi ya naibu spika wa kwanza , wakati Mahad Abdalle Awad alichaguliwa kuwa naibu spika wa pili.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na profesa wa chuo kikuu Abdullahi Mohamed Aden alisema Somalia imepiga hatua muhimu katika uanzishaji wa asasi za kudumu kikatiba baada ya miaka mingi mfululizo ya serikali za mpito.
"Kwa mara kwanza baada ya miongo kadhaa, Somalia ilishuhudia uchaguzi wa haki ndani ya nchi," alisema. Majaribio yote ya nyuma ya kuunda serikali yalifanyika nje ya nchi kutokana na matatizo ya kiusalama.
"Kwa uchaguzi huu uliofanyika katika mtindo wa kidemokrasia na uwazi, manaibu wapya wamewathibitishia watu wa Somalia na ulimwengu kuwa wana uwezo, ustadi na mafungamano," "Tunatumai uchaguzi ujao wa raisi pia utafanyika katika hali ya haki na uwazi kwa ajili ya kutimiza matumaini ya watu wa Somalia na kuithibitishia dunia kuwa Somalia imeingia katika enzi mpya."
Raisi wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed aliusifia uchaguzi, na kuuelezea kama tukio la kihistoria ambalo litadumu katika kumbukumbu za kila mwananchi.
"Katika wakati huu wa kihistoria ambao Somalia imeshuhudia, ningependa kumpongeza spika mpya wa bunge pamoja na wabunge," Ahmed alisema katika mkutano wa habari baada ya kuchaguliwa kwa spika mpya.
"Leo ni siku ya kihistoria kwa watu wa Somalia kwa vile bunge jipya la kudumu limepiga hatua muhimu kutimiza matumaini ya watu wa Somalia na ninatumai kuwa hatua hii ni ya kwanza kuelekea ujenzi wa Somalia mpya ambayo ina amani, utulivu na mafanikio," alisema.
Mbunge Isaac Mohamed alisema, "Mchakato wa kumchagua spika wa bunge na manaibu wake wawili ulifanyika kwa uwazi kwa vile wabunge wote waliheshimu matokeo ya kura na ninatarajia kuwa uchaguzi wa raisi utafanyika haraka iwezekanavyo."
"Somalia imemudu kupata mafanikio makubwa ya kisiasa ikiwa ni pamoja na kufuata katiba mpya na kuchagua wabunge ambao, badala yake, wamemchagua spika wao na manaibu wake wawili," alisema. "Katika siku chache zijazo, tutamaliza kazi zilizobakia za kufanikisha kipindi cha mpito nchini kwa ufanisi."
Mohamed Sheikh Osman Jawari alichaguliwa spika wa bunge baada ya kupata wingi wa kura katika duru ya kwanza na kujitoa kwa wapinzani wake katika kura ya duru ya pili.
Jawari alizaliwa mwaka 1945 katika mji wa Afgoye, uliopo kilomita 30 magharibi ya mji mkuu, Mogadishu. Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari, alipata digirii ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Somalia.
Wakati wa serikali ya Mohamed Siad Barre, Jawari alikamata nafasi ya Waziri wa Uchukuzi na baadaye kuwa Waziri wa Kazi mwaka 1991. Baada ya kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini, aliondoka kwenda Norway ambapo alirejea karibuni Somalia.
Mwezi wa Septemba 2011, Jawari alichaguliwa kuongoza kamati ya wataalamu waliopewa dhamana ya kuandaa katiba mpya ya Somalia ambayo iliidhinishwa na Bunge la Taifa la Katiba. mwanzo wa mwezi huu.
Wizara ya Usafiri wa Anga ya mkoa wa Somaliland siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni) iliikataza ndege...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata makamu wanne wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Ma...
Watu wenye silaha kwenye Kaunti ya Wajir walimuua polisi mmoja wa akiba wa Kenya siku ya Jumanne ...
Japan inaipa Tanzania dola milioni 49 (shilingi bilioni 80.4) kama msaada na mkopo kwa ajili ya k...
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo yeye pekee yake amewateua na kuwapangia kazi maafisa wa...
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumanne ilimkubalia Makamu wa Rais wa Kenya Willia...
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Nimefurahishwa sana na mabadiliko yanayotokea bila ya kutegemewa. Ninamuomba Rais kumchagua Waziri Mkuu mwenye uwezo na ujuzi wa kuoongoza na ambaye anaweza kudhibiti matatizo ya usalama nchini Somalia.
Mazungumzo ya leo ni kuhusu siasa za sasa za Somalia.
Ni mtu mzuri na nimefurahi sana kuhusu yeye. Ninamuomba Mungu atuongoze katika nji iliyonyooka.
Kwanza, ningependa kumpongeza Raisi Hassan Sheikh Mohamud. Pili, ningependa kumwambia raisi kuwa Somalia ina matumaini ya kujengwa tena tangu wakati ilipoporomoka. Wasomali hawajapata nafasi ambayo wanayo leo katika utawala wa maraisi wote waliotangulia. Somalia leo inaweza kurejeshwa katika njia ambayo ilivyokuwa lakini hili linawezekana kutokana na uwajibikaji wako, serikali yako na wananchi wa Somalia popote walipo. Kuna haja ya kuwaunganisha Wasomali ili tuweze kuleta mabadiliko katika nchi yetu. Hayo ndio yote.
NINGEPENDA KUWAPONGEZA WASOMALI POPOTE WALIPO. PIA, NINGEPENDA KUWAPONGEZA WOTE WALE WALIOSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI ULIOFANYIKA NCHINI SOMALIA, HASA WABUNGE, HATA KAMA TULIHISI KUWA BAADHI YAO WALIPOKEA FEDHA LAKINI MATOKEO YA UCHAGUZI YALIMPA USHINDI MTU ASIYETARAJIWA. NINGEPENDA KUWATAKA WOTE WATAKAOFANYA KAZI NA RAISI WAKIWEMO SPIKA WA BUNGE NA WAZIRI MKUU YEYOTE ATAKAYEKUWA, KUFANYA KAZI NA RAISI KWA DHAMIRA MOJA NZURI KWA WASOMALI. NINGEPENDA KUWAOMBA VIJANA WANAONYANYUKIA AMBAO WALIKULIA KATIKA NCHI YETU ILIYOCHANIKACHANIKA KWA VITA, AMA WALIKUWA NCHINI AU WALIKIMBIA KUTOKA NCHINI, KUCHUKUA FURSA YA HALI YA SASA KWA VILE TAYARI WANA FURSA NA NGUVU LEO. SASA KWA KUWA WANAWAKE WAMEPEWA DHAMANA KATIKA SIASA HAIMAANISHI KUWA WATAKUWA HURU KUTOKA MIKONO YA WAUME ZAO, DADA ZAO AU SOMALIA KAMA NCHI YAO. WANATAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KUJENGA UPYA TAIFA LAO. NINGEPENDA PIA KUWAOMBA VIONGOZI WA KIJAMII, WAKUU WA DINI NA WALE WOTE WALIO TAYARI KWA AJILI YA MAENDELEO YA TAIFA LETU KUFANYAKAZI KWA PAMOJA. ASANTENI. NA ABDIRIZAK SAYUUN.
Hili ni jambo kubwa. Kwa kweli ni furaha kubwa ikiwa raisi alichaguliwa nchini kwetu leo. Hii ni fursa ya wazi kwa Wasomali na wanatakiwa kuitumia fursa hii ili kumaliza matatizo ambayo yamewaathiri watu na nchi.
Ninataka tovuti mpya.
Ninahisi furaha kwa uchaguzi wa raisi utakaofanyika Somalia. Ninahisi furaha sana.
Vipi vikundi cha wachache vinakuwa tofauti na watu wengine? Wasomalia wote ni wamoja.
Mimi, Abdihakiin Adan Ali ambaye ni kutoka Jamhuri ya Djibouti, nadhani uchaguzi uliofanyika usiku huu jijini Mogadishu unaingiza matumaini kwa vijana wa Somalia na tuna imani kuwa bunge jipya ni bunge ambalo litaibadilisha Somalia kutokana na uchaguzi wa spika wa bunge, Jawahir. Ni wazi kuwa usiku huu imetimia haja ya mabadiliko ambayo watu walikuwa wanayataka. Ninampongeza raisi mpya Hassan Sheikh Abdi. Hongera. Asanteni
Bunge la Somali limechagua rais mpya. Nashangaa kwa nini watu wa Somalia waliwachukia Sharif wawili? Kwa kweli kwangu mimi limekuwa suala zuri sana na njia ambayo lilifanyika. Ninakaribisha mabadiliko yaliyofanywa nchini Somalia. Lakini jinsi gani amani itaweza kupatikana. Suala ni ikiwa wapinzani wa ndani wenye silaha wataangamizwa au kufikiwa makubaliano. Ikiwa makubaliano hayakufanikiwa, kutatokea nini? Zitadumu furaha zilizoanza usiku huu au itakuwa ni mpito unaounganisha mwaka mmoja baada ya mwengine?
Nimefurahi sana na uchaguzi wa rais wa Somalia ulioshindwa na Bw. Hassan Sheikh Mahomud. Ninamuombea kwa Mungu amsaidie. Amin.
Nadhani Sheikh Shariif Sheikh ataibuka mshindi kwa sababu Hassan ni mhafidhina kidogo kwa vile wote ni watu wa dini na tena nafikiri juu ya mawazo yangu, Sheikh Shariif.
Binafsi ningesema kuwa uchaguzi huu ndio uliotegemewa sana kwa sababu umefanyika katika njia ya haki na uwazi.
Kuna matumaini kwamba Sheikh Sharif Sheikh Ahmad atachaguliwa tena lakini suala ni, je, atabadilisha chochote kutokana na siasa zake, atabakia kama alivyo au atakuja na siasa mpya?
Hii uchambuzi ni kuhusu uchaguzi wa rais.
MUNGU akipenda Farmaajo kwa urais.
Ninaupokea uchaguzi unaofanyika ndani ya Somalia. Sisi kama watu wa Somaliland, tunawatakieni mafanikio.
Wasomali lazima wamchague kiongozi ambaye ataisaidia nchi, Mungu akipenda.
Naamini kuwa Wasomali hawatapata nafasi nyengine ikiwa wataipoteza fursa hii. Kwa hivyo ni lazima kuwaheshimu viongozi wanaogombania urais. Nina matumaini kuwa tutampata kiongozi msomi Prof. Samatar, Farmajo au wengine miongoni mwa wagombea.
Sidhani kama tutakuwa na matumaini ya kuijenga upya Somalia ikiwa wasomali watamchagua tena Sheikh Sharif .
Mimi ni mvulana ninayeitwa Abdiaziz.
Ali-Sabih, tarehe 10 Septemba, 2012: Amani na Baraka za Mungu ziende kwa bunge la Somalia. Mimi ni Mdjibouti mwenye asili ya jamii ya Wasomali wa Kaskazini ya Djibouti. Ninaishi katika ndoto za kuwa na Somalia kubwa. Nimefurahi sana kuhusu kuzaliwa upya kwa Jamhuri ya Somalia leo. Tunaweza wakati huo huo kuifanya leo kama siku ya kuzaliwa kwa Somalia kubwa kutokana na sababu nyingi ambazo ninadhani Wasomali wengi hatuhitaji kuzieleza. Sababu hii ni pamoja na: Kupeleka hali ya mpito kwa Ethiopia kufuatia kwa kifo cha mtu (Meles Zenawi) ambaye alikuwa na tabia ya kuigawa na kuwatawala Wasomali. (Kwa sisi hili ni utukizi lakini kwa Mungu ni jambo lililopangwa vizuri). Kuenea leo rasmi kwa utawala wa serikali halali ya Somalia kutoka Ras-Kamboni kupitia Lowya’do hadi Ras-Asyr. Somali ya DDS leo itakuwa na nafasi kubwa za kuwa huru ikiwa uongozi wa Ethiopia utaanguka kama Tigres na Amharas na Tigres wanatangaza kutengana na Ethiopia kwa vile walishatabiri tangu mwanzo lile ambalo lingetokea, Mungu akipenda. Hili litatupa eneo la Somalia ndani ya Ethiopia fursa ya kujitenga moja kwa moja. Wasomali wa eneo la Kaskazini ya Kenya pia watapata fursa ya kupigania uhuru wao baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kulipuka baina ya serikali ya Kenya na jamii ya Waswahili katika mwambao wa kenya hivi karibuni. Hii ni ikiwa Kenya itaepukana na vurugu sawa na zile zilizoshuhudiwa katika uchaguzi wa mwaka 2007 katika uchaguzi ujao ambapo kila Msomali wa Kenya anatumai kulipuka kwa aina mbaya sana ya vurugu.
Hongera kwako kama spika, ndugu yangu.
NINAPAZA SAUTI YANGU KUTOKA HAPA KWA KUCHAGULIWA TENA SHEIKH SHARIF SHEIKH AHMAD KWA VILE AMEFANIKIWA KUREJESHA AMANI NCHINI SOMALIA. NI SHEIKH PEKEE ANAYEWEZA KUIONGOZA SOMALIA NA HATUMHITAJI ABDIWELI AU MWENGINE YEYOTE.
Ewe Mungu wangu, tusaidie kuelekea kwa amani katika uchaguzi wa rais utakaofanyika kesho ili tuweze kumaliza tatizo hili sugu.
Amani kwa ndugu wote wa Radio KNN na hasa kwa Fatma Abdi Warsame. Kwa kweli, tunahitaji mtu ambaye anaweza kuwaokoa watu wa nchi. Kwa sababu hii, tunapaswa katika uchaguzi wetu huu tusizingatie ukabila au imani juu ya uwezo wa mtu kutuokoa. Mtu ambaye anaweza kutuokoa kulingana na mtazamo wangu ni mtu mzuri kutoka kwa Mungu. Nina matumaini makubwa na ninaitakia Somalia mafanikio.
Ningependa kuwapongeza wote waliogombea urais wa Somalia lakini ninaomba kujiondoa haraka kwa Ahmad Ismail Samatar kwa sababu hakuna uwezekano wowote wa yeye kuwa rais ajaye wa Somalia. Ningependa kumshauri badala yake. Kurejea mji wake wa Borama na kuwa Mkuu wa Wilaya huko badala ya kuaibishwa katika kinyang’anyiro hiki cha urais.
MIMI NINAMUUNGA MKONO BWANA FARMAJO
Nimefurahi sana kwa Somalia kutoka katika utawala wa mpito na kuunda serikali halali wenyewe. Ninawapongeza wabunge wapya na spika wa bunge la taifa; Prof. Jawari. Ninawatakia mafanikio kuchagua rais wa haki na mpenda dini kwa niaba yetu. Asanteni VOA.
Hii ni nzuri sana. Ninapenda Somalia itulie ili matatizo yamalizike.
Huu ni wakati wa urais. Hadithi yote inahusu Prof. Samatar. Rafiki zangu, tumchague Prof. Samatar ili kutufanya tufikie maendeleo........ kkkkkkkkkkkkkkkk
Lazima tupate serikali yenye kutenda haki ambayo italeta masuluhisho kwa matatizo yetu na kuweza kuondosha mgawanyiko wa watu kama vile ukabila na masuala ya 4.5 ambayo Wasomali wanapaswa kuyarekebisha.
hongera jawari,tenda haki kwa manufaa ya wananchi na kwa nchi yako ya somalia.HONGERA SANA
Ni kazi nzito na ya kuthaminiwa iliyofanywa na viongozi wetu na tunatarajia mengi zaidi kutoka kwao (Mungu akipenda).
Bunge jipya nchini Somalia litawapa watu wa Somalia nafasi ya kupata amani na kuendeleza miundombinu na uchumi. Bunge jipya litafanya kazi na watu ili kujenga upya taifa lao na wakati huo huo kuja na sheria za kulinda na kukuza wale walio wachache nchini Somalia.