Agosti 28, 2012
Al-Shabaab wameshuhudia kuongezeka kwa migawanyiko ya ndani wakati majeshi ya Somalia na washirika wake wakiendelea kuking'oa kikundi kutoka maeneo yaliyobakia katikati na kusini ya Somalia,maafisa na wapiganaji walioasi wasema.
Kanali Adan Shire Rufle, afisa wa jeshi la Somalia huko Juba ya Chini, alisema wapiganaji 50 walikiasi kikundi hicho hapo tarehe 24 Agosti na kwa hiari yao wakajiunga na jeshi baada ya kushuhudia ukatili wa wanamgambo na aina kali sana ya sheria ya Kiislamu.
Rufle alisema, waasi hao wakiwa wamebebba bunduki aina ya Kalashnikov,maguruneti ya kurusha kwa makombora na bunduki za rashasha, kwa amani walijiunga na vikosi vya Somalia huko Afmadow baada ya kutoroka mavamizi ya al-Shabaab.
"Tunarajia waasi zaidi na migawanyiko ya kiitikadi ndani ya uongozi wa al-Shabaab, kwa vile baadhi yao wameonesha hamu yao ya kujisalimisha na kutafuta hifadhi kwetu kutoka kwa matakfiri wasaliti," aliiambia Sabahi.
Wakisaidiwa na majeshi ya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM), majeshi ya Somali yameanza kukaza fundo katika shingo za wanamgamnbo waliobakia kwa kushambulia majeshi ya al-Shabaab huko Afmadow huku wakiendelea kuelekea ngome imara ya kikundi hicho ya Kismayu.
Katika wiki kadhaa zilizopìta, vikosi vya washirika vimekuwa vikipiga mabomu maeneo yaliyokuwa yakitumiwa na al-Shabaab na wafuasi wa al-Qaida huko Gedo na Juba ya Chini, kwa mujibu wa jeshi la Somalia.
Wakati wanamgambo wa al-Shabaab wamechanganyikiwa kutokana na mafanikio ya kijeshi ya vikosi vya washirika huko Juba ya Chini, kukakataliwa hadharani miongoni mwa kikundi kumekuwa kukiongezeka.
Mpiganaji wa zamani Kamal Mohamed Yarow alisema wanamgambo wa al-Shabaab si chochote zaidi ya genge la mafia wajinga wanaoiba, kunyang'anya kwa nguvu na kuua -- mambo ambayo yanalaaniwa katika Uislamu. Alisema heshima ya al-Shabaab ni ndogo sana miongoni mwa watu wa Somalia ambao ni wahanga wa matendo yao, ambao damu yao imemwagwa na nyumba na biashara zao kuharibiwa.
Yarow aliiambia Sabahi kuwa katu hatakamata tena silaha kwa ajili kikundi hiki, kwa sababu al-Shabaab inahusika na utesaji, ukataji watu viungo vichwa na mauaji.
"Walikuwa wananichukua katika mapambano ya vurugu na mauaji na kuweza kujigamba mbele ya wasichana mijini," alisema. "Hii sio jihadi ya kweli. Ikiwa sasa wanafanya yale wanayohubiri linapokuja suala la jihadi kwa nini viongozi wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane, msemaji wa kisiasa Sheikh Ali Mohamud Rage na Sheikh Fuad Mohamed Qalaf, ambao wanadhamana ya utetezi na propaganda, lakini hawajitolei wao kufa kishahidi?"
Yarow alisema al-Shabaab ilikuwa ikimpelekea pesa za kuihudumia familia yake, lakini fedha hiyo ilikuwa haitoshi, jambo linalothibitisha kuwa upungufu wa fedha katika kikundi .
Kwa mujibu wa Said Sheikh Abdiweli, mpiganaji mwengine alaiyeikimbia al-Shabaab, mgogoro unavukuta miongoni mwa viongozi wakuu wa kikundi, kulikopelekea idadi yao kubwa kuuliwa, kujikuta wakikabiliwa na mgogoro wa ndani na kutokuwa na mipango. Kikundi pia kiliwaua wanachama wake wenyewe kwa madai ya kuhusika na ujasusi kwa serikali za kigeni.
Abdiweli aliiambia Sabahi kuwa baadhi ya wapiganaji waliwauwa makomredi wao waliojeruhiwa kwa kuwa kuwapiga risasi vichwani wakati wa mapigano huko Mogadishu, Hudur, Adale, Rama Adi, Diinsoor na wilaya ya Dhuumale.
"Hali imekuwa mbaya zaidi miongoni mwa wanamgambo wenye msimamo mkali, kufifia kwa mapato kutokana na wizi, utekaji nyara na kuiba kwa nguvu katika magari ya mizigo," alisema. "Hii ni kwa sababu kupelekwa kwa jeshi la Somalia, linalosaidiwa na AMISOM, kumemudu kuchukua udhibiti na kuondosha vikwazo, na kuyafunga maeneo. Matokeo yake ni kukwama kiuchumi [kwa al-Shabaab] katika Juba ya Chini na Juba ya Kati."
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
Watu watano walikamatwa siku ya Jumanne mjini Dar es Salaam wakiwa na vifaa vya kulipua katika mi...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliwataka wabunge kuweka kando madai yao ya kuongezwa mishahara kwa ...
Majeshi ya serikali ya Somalia waliwaua wanamgambo tisa wa al-Shabaab wakati wa mapambanao hapo J...
Mtu asiyejulikana alimpiga kwa risasi na kumuua ofisa wa kitengo cha usalama cha kijeshi huko kas...
Muungano wa Jubilee tawala cha Kenya kilichukua uongozi wa kamati mbili muhimu za bunge Ijumaa (t...
Chama cha Wafanyabiashara na Asasi ya Chakula na Kilimo ya Umoja wa Mataifa vinatoa mafunzo kwa w...
Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya nchini Tanzania Filiberto Ceriani Sebregondi aliwahamiza waandis...
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
kwa kweli hii ni propaganda tu ya kukipaka matope kikundi hichi cha Al-shabaab,kwa kweli Al-shabaab wako katika njia ya haki na INSHA ALLAH kikundi hichi kitashinda tuzidi kumuomba Mungu awape ushindi wapiganaji hawa wa vita vitakatifu visivyo pendwa na Makafiri.na Mungu akipenda watashinda watashinda tu hata makafiri wakichukia kama Mwenyezi Mungu anavyo tueleza katika Aya zake nyingi tu,kwamba yuko pamoja na wanaomtegemea.
Hivi kwa nini sisi afrika ndo tuna migogoro sana kuliko nchi za ulaya, hebu tubadilike jamani waafrika tutauana hadi lini?
Al shabaab hawana Uisilamu dani yao.
Kwa kweli tunahitaji kuomba sana kwa kushindwa kwa al-Shabaab kwa sababu ni hilo tu ndilo litakalohakikisha amani ya kudumu katika kanda hii.
Hii ni propaganda
Al-Shabaab wako katika njia ya haki. Wamefanya kosa kwa kuwatawaleni kwa kutumia dini kwa sababu fedha na ukabila vimekuwa dini yenu? Kuweni na tahadhari kwamba al-Shabaab ni kikundi cha kikabila kwa sababu kinaongozwa na mtu kutoka ukoo wa Isack. Yeye si mgeni bali anaimiliki nchi pamoja nanyi na anaweza kufanya chochote anachotaka.
"Amani iwe juu yenu"....ni amani gani ambayo wanafiki hawa wanaizungumzia? Ungueni motoni.
Abu Mucad, Sarqaawi,Zubayr....nafsi zilizopotea. Vurugu sio jambo la Waislamu. Tafuteni njia za kweli kwa kusoma kwa ukweli mafundisho ya Mtume Muhammad. Amani iwe Juu yake.
Nyinyi watu muelelewe kwamba Mungu ni msimamizi mkuu wa kila kitu. Nyinyi si lolote, iwe al-Shabaab watashindwa au kuondolewa na Mungu sio mlinzi mkuu wenu kwa sababu mnaunga mkono vurugu na mambo yote yaliyokatazwa na Mungu ikiwemo ubakaji. Ninamuomba Mungu kutuongoza katika njia iliyonyooka. Makafiri mnaowaunga mkono hawatafaidieni kwa njia yoyote isipokuwa kuwatia katika matatizo zaidi na kuwachukilieni watoto wenu wa kike. Mungu alituambia kuwa Wayahudi na Wakristo hawatawaruhusuni chochote isipokuwa kwa kututumia ili kufikia malengo yao. Ningependa kuwaomba wale wanaopenda kuwa wema watubu kwa Mungu.
Naamini kuwa mambo hayaendi katika njia sahihi kwa sababu kwa karibu ya mwaka, vikosi vya serikali havikuweza kufika Juba hasa Kismayu na kuna nyakati , nahisi kuwa kuna jaribio la makusudi la kutowamaliza al-Shabaab; jina lao na uwepo wao vingeshapotea zamani.
Nafikiri al-Shabaab itakuwa kitu ya zamani kwa vile sasa wanashindwa vitani kutokana na kulaaniwa na jamii ya Somalia.
Kwa kweli, inaweza kusemwa kuwa mambo yote haya yamefikia mwisho kwa sababu tuna matumaini ya kuunda serikali halali, Mungu Akipenda.
Al-Shabaab wapuuzi wako ukingoni wa kutokomezwa. Katika siku chache, wengi wao hawatakuwa miongoni mwa wanaoishi.
Huu ni uongo mkubwa na mbali sana na mambo yote mabaya. Kama kijana niliyezaliwa Qorahey, ningependa kuwaomba wale wote waliopotea kutubu kwa Mungu na kuufahamu ukweli. Mungu awaongozeni katika njia iliyonyooka. Pili, hakuna shaka kuwa Waislamu, hasa wapiganaji wa vita vitakatifu, watashinda popote walipo. Ningependa kuwaomba watu walioandika makala hii na kufanyakazi katika wavuti huu kumwogopa Mungu. Msipotee kwenye akhera yenu. Mwenyezi Mungu amebainisha aya fulani katika Koran Tukufu za kujibu habari kama hizi mlizoandika au kitu kinachokaribiana nazo, zinazotolewa na wanafiki. Muogopeni Mungu na acheni kuwakashifu wapiganaji wa vita vitakatifu.
Wakati umefika kwa matendo yao ya kishenzi kufikia mwisho.
Amani iwe juu yenu. Mazungumzo ni sawa lakini wamegawanyika kuhusu hilo.
j aime faire ça [Napenda kufanya hivyo]
Katika makala hii kuna baadhi ya uongo. Watu hawasemi ukweli kuhusu al-Shabaab.
Somalia inateseka na inaweza kutibiwa iwapo tu itapata mzalendo ambaye ni jasiri vya kutosha wa kuisaidia nchi yake.
Wakati umefika kwa Waafrika kuchagua viongozi wenye kuona mbali na hatima bora zaidi kwa watu wao badala ya wale wanaotaka kujifaidisha wenyewe.
Hatutaki al-Shabaab. Mahali pao ni mto wa jehanamu.
Wanajihadi wataoza katika jehanamu!
haki itasimama!zubayr upo sahihi.hizo ni propaganda kwa watu wenye uelewa mdogo.
Marafiki zangu, uongo unakatazwa. Wapiganaji wa vita vitakatifu daima hawataanguka. Muogopeni Mungu.
Uchaguzi wa bunge umefanyika vema na tunapenda uchaguzi wa raisi kufanyika katika njia hiyo hiyo.
Serikali zote lazima zifanye kazi kupambana na misimamo mikali na uhalifu wa kikatili yanayoweza kusababisha. Lazima zifanye kazi kuwatayarisha watu kuweza kuishi katika mazingira yao na katika jamii wanayoishi na kufuata sheria za Mwenyezi Mungu Mwenye uwezo katika njia ambayo itamfurahisha. Kwa kweli, lazima watilie makazo Uislamu kama dini ya uvumilivu, inayofaa, maelewano na kutokuwa na kisasi katika matendo yake. Pia zinapaswa kufanya kazi katika kusisitiza kuwa Uislamu unakataza misimamo mikali na kupitiliza katika masuala yote, pamoja na kuonesha arifa ya sheria za Kiislamu yanayokuza mema na kujiepusha na maovu na kuwakemea wakosaji. Vilevile lazima zifanye kazi kuwasaidia wananchi kutofautisha baina ya mema na mabaya, kuwezesha umuhimu ya jamii na hasara kutoonesha utiifu kwa watawala, kufahamishwa misingi ya Uislamu na kuyaelewa malengo na dhamira zake na kujifunza mafundisho yake. Kwa kweli, kutokuwepo kwa elimu ya dini na kuenea kwa ujinga ni sababu kubwa za kuenea kwa uchochezi. Kwa hivyo, lazima tushughulikie zaidi mafunzo ya dini kuhusu vyanzo vyake halisi, vinavyotuonesha Uislamu kama ujumbe wa dunia kwa watu wote. Haya yaliletwa na Mtume wetu (amani iwe juu yake), ambaye alisisitiza na kufanya kila aliloweza kuwataka watu wajiunge na dini yake. Mtume Muhammad alivumilia madhara na mashaka kwa ajili ya Uislamu na kuwa mtu wa kuigwa kwa taifa lake. Kwa hivyo, watu lazima waungane na viongozi na wanazuoni wa taifa na kurejea kwao kwa masuala mbalimbali ya maisha. Hawa wa mwisho wanachukuliwa kama sababu ya sifa, heshima, ushindi, utulivu, usalama na matunda yote yaliyobarikiwa na matokeo mazuri.
Wanamgambo hawa hawawezi kumshawishi yeyote kuwa mauaji haya wanayofanya ni jihadi. Mtu awakumbushe kuwa jehanamu inawasubiri watakapofariki.
Amani iwe juu yenu. Habari iliyomo katika ukurasa huu inaonekana kama ni habari iliyokusudiwa watu wale ambao hawana uelewa kuhusu uongozi, kazi na nguvu za kikundi cha al-Shabaab. Mwisho, ningependa waongo na wale wanaozungumza vibaya kuhusu kikundi hiki wamuogope Mungu. Amani iwe juu yenu.