Wanachama wa al-Shabaab wakimbia kwenda Barawe baada ya kukumbana na vizuizi.

Na Adnan Hussein, Mogadishu

Agosti 27, 2012

  • 7 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wanachama wa al-Shabaab na viongozi maarufu walikimbia kuelekea mji wa Pwani wa Barawe, kilometa 170 kusini mwa Mogadishu, wakaazi waliiambia Sabahi.

  • Vikosi vya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia vinajiandaa kuchukua nafasi katika mwelekeo wake wa kwenda Marka, kama kilometa 80 hivi kaskazini mwa  Barawe, baada ya kusonga mbele katika maeneo yaliyokuwa yanadhibitiwa na al-Shabaab hapo awali tarehe 4 Agosti. [Mohamed Abdiwahab/AFP]

    Vikosi vya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia vinajiandaa kuchukua nafasi katika mwelekeo wake wa kwenda Marka, kama kilometa 80 hivi kaskazini mwa Barawe, baada ya kusonga mbele katika maeneo yaliyokuwa yanadhibitiwa na al-Shabaab hapo awali tarehe 4 Agosti. [Mohamed Abdiwahab/AFP]

Vikosi vya Somalia, vikisaidiwa na Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM), viliwaondoa al-Shabaab katika ngome zake kuu huko Somalia ya kati na ya kusini kwa kipindi cha miezi michache iliyopita, ikiwa ni pamoja na Beledweyne , Baidoa , Hudur , Afgoye and Balad .

Siku ya Jumatatu (tarehe 27 Agosti ), vikosi shirika vilikamata mji wa bandari wa kimkakati wa Marka, mji mkuu wa mkoa wa Lower Shabelle ulio takriban kilometa 80 kaskazini mwa Barawe.

Tumeichukua Marka, tuliingia tukiwa pamoja na vikosi vya serikali ya Somalia asubuhi hii ," alisema msemaji wa AMISOM Colonel Ali Aden Hamud, kwa mujibu wa AFP. "Kulikuwa na mapambano kiasi, lakini hayakuwa makali, wengi wa [wapiganaji] wa al-Shabaab walitoroka.".

Meja Jenerali Bashir Mohamed Jama, mkurugenzi mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa, alisema mji huo hivi karibuni umeshuhudia uingiaji kwa wingi wa watu ambao wanafuata itikadi za takfiri za kuwatuhumu Waislamu wengine kwa kuwa waasi.

Maida Dahir, ambaye anauza maziwa ya ngamia na ng'ombe katika soko la mji, alisema aliona foleni ya wapiganaji wa kigeni wakisalisha sala ya Idd huko Barawe.

Dahir alisema aliwaona mwanachama mwandamizi wa al-Shabaab Shekhe Hassan Dahir Aweys, makamu kiongozi wa kikundi hiki Shekhe Mukhtar Robow Ali, ambaye pia anajulikana kama Abu Mansur, kiongozi mwandamizi Shekhe Fuad Mohamed Qalaf, ambaye pia anajulikana kama Fuad Shangole, na viongozi wengine ambao hakuweza kuwatambua , kwa kuwa walikuwa wamevaa barakoa au walijifunika kwa vitambaa vyeusi.

"Mji wetu, ambao ni maarufu kwa vyakula vyake vya mikate na samaki wa kubanika, umekuwa ni kimbilio salama kwa magaidi na wenye siasa kali kutoka duniani kote," aliiambia Sabahi. Alisema wapiganaji walianza kuja katika mji baada ya wake na watoto wao kupata hifadhi huko Barawe kutokana na mashambulizi ya anga yaliyowalenga al-Shabaab.

Mustafa Abubakar Haji Aweys, mkaazi mwingine wa Barawe, aliiambia Sabahi kwamba al-Shabaab imeanzisha vituo vya ukaguzi na kujenga maboma katika vijiji vyote vya jirani kwa hofu kwamba mawakala wa upelelezi wa Somalia wanaweza kujipenyeza Barawe.

Aweys alisema anangojea vikosi vya serikali kuchukua mji wa pwani, kuwafukuza wapiganaji na kurejesha hali ya kawaida.

Itikadi ya takfiri ya Al-Shabaab ni 'tishio kwa jamii'

Iidow Jeylani, anayeendesha basi dogo la abiria, aliiambia Sabahi kwamba wenye siasa kali huko Barawe wanawapa mafunzo wapiganaji kutembea kwenye eneo la mji kando ya bahari na kuwapa mafunzo vijana wengi katika eneo ili wajiunge na operesheni zao za upiganaji.

Diidi Omar Shobow, anayeuza mkaa kwenye soko la eneo hilo, alisema viongozi huko Barawe wana uhusiano na kiongozi wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane, anayejulikana pia kama Mukhtar Abu al-Zubair.

Aliiambia Sabahi kwamba Godane ameleta wapiganaji wa kigeni katika mji ambao wanajiona kama "kikundi cha wanusurika" na kuamini kuwa wale wanaohoji tafsiri yao ya Uislamu wanastahili kuuawa.

Shobow alisema wenye siasa kali ya itikadi ya takfiri wanaleta vitisho kwa jamii ya Barawe na Somalia nzima. "Wanatulazimisha kulipa kodi isiyo halali na kuingilia masuala ya familia kwa kuwaachanisha watu waliooana na kueneza machafuko," alisema.

Habib Nurani, mvuvi mwenye umri wa miaka 62, alisema raia wenyeji hawana silaha na hawajihusishi katika migogoro ya kikabila.

"Hatuna nguvu za kujitetea dhidi ya mashambulio ya al-Shabaab kwa sababu hatuna kawaida ya kuwa na silaha ili kupigana vita au kuwaua watu wasio na hatia," aliiambia Sabahi.

Tunachoweza ni kuangalia tu jinsi wenye siasa kali wanavyoongeza udhibiti wao katika mji wetu hadi jeshi la [nchi] litakapokuja na kuusafisha mji wetu kwa kuwaondoa wageni hao na washirika wao Wasomali, ambao wanajaribu kuubadilisha mji huu kuwa eneo lao jipya la kuzindulia operesheni zao," alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 50)

Dislike_icon(2)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • hamza
    October 11, 2012 @ 12:48:53PM

    Potelea mbali al-Shabaab na naomba Mungu aziangamize nyumba zao….Wataingia jehanamu, Iishi maisha marefu Barawe…Ninaupenda mji wa amani wa Barawe.

  • Mustafa Kifofo
    September 27, 2012 @ 10:16:51AM

    SNA na AMISOM, tafadhalini, tafadhalini! Wachomeni moto wajinga hawa (al-Shabaab) wakiwa hai.

  • abdirahman
    September 9, 2012 @ 05:25:07PM

    Hatutaki al-Shabaab!

  • jimmy mwai
    September 9, 2012 @ 06:29:33AM

    Wanaweza kukimbia, lakini katu hawataweza kujificha!! Siku zao zinahesabika!!

  • ماريا
    August 29, 2012 @ 05:03:07PM

    Mungu aishinde (al-Shabaab) kwa vile ni adui mchungu.

  • kingsley
    August 28, 2012 @ 05:54:33AM

    Hiyo ndiyo njia nzuri ya kwenda, hongera AMISOM.

  • خالد
    August 27, 2012 @ 06:25:55PM

    Mungu siku zote huwa pamoja na mema na huwa dhidi ya maovu, na Wasomali hatimaye watafanikiwa katika kudhibiti ugaidi, bila ya kujali itachukua muda gani. Mungu siku zote yuko pamoja na wenye haki, na YEYE hafurahishwi kuona watu wasio na hatia wanauliwa. Kwa hivyo, Mungu siku zote huwahakikishia ushindi wema na sio waovu, na kikundi cha al-Shabaab kiangamie motoni.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo