Agosti 27, 2012
Mhadhiri wa Kiislamu wa Kenya Aboud Rogo Mohammed, ambaye alikuwa kwenye orodha ya kimataifa ya watu waliowekewa vikwazo kwa kuliunga mkono kundi la al-Shabaab lenye mafungamano na al-Qaeda, alipigwa risasi na kuuawa hapo Jumatatu (tarehe 27 Agosti) akiwa garini mwake mjini Mombasa.
Mashahidi walisema kwamba gari hilo lilitobolewatobolewa kwa risasi. Picha iliyosambazwa na wafuasi wake iliionesha maiti yake ikiwa imerowa damu nyuma ya usukani wa gari.
"Alikufa wakati tukimuwaihisha hospitali," alisema mjane wake, Haniya Said, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP kabla ya yeye mwenyewe na watoto wake kupelekewa hospitalini.
Kifo cha Mohammed kilichochea maandamano ya maelfu ya waandamanaji wenye hasira kukusanyika katika msikiti ambao alikuwa akiutumia kutoa hotuba zake mara kwa mara, waliotia moto magari na kupiga mayowe ya kumuunga mkono kiongozi huyo, iliripoti AFP.
"Imamu alipiga kelele kupitia spika ya msikitini "damu kwa damu", na mara moja vijana wakaanza kuyarushia mawe magari," alisema shahidi Dennis Odhiambo, ambaye gari yake iliathirika na akalazimika kukimbilia kituo kimoja cha polisi kwa usalama wake.
Mkuu wa Polisi wa Mkoa huo, Aggrey Adoli, alisema: "Mtu mmoja ameuawa, alikatwa kwa mapanga hadi kufa wakati wa maandamano."
"Kuna vurugu mjini sasa, na maafisa wetu wako huko kuwatawanya waandamanaji kurudisha amani," alisema Adoli.
"Mji mzima uko kwenye hali mbaya, kuna waporaji mitaani, gari zimevunjwa, mengine yamechomwa moto," alisema Francis Auma kutoka Jumuiya ya Waislamu kwa Haki za Binadamu.
Mohammed alikuwa amewekwa kwenye orodha ya vikwazo ya Marekani mwezi Julai "kwa kujihusisha na vitendo ambavyo ama moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja vinahatarisha amani, usalama au utulivu wa Somalia," hasa hasa kwa kuwapa mafunzo na kukusanya fedha kwa ajili ya al-Shabaab.
Mohammed" aliwataka watu wanaomsikiliza kwenye mihadhara yake kusafiri kwenda Somalia kujiunga na al-Shabaab kupigana dhidi ya serikali ya Somalia," ilisema idara ya Hazina ya Marekani.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliweka vikwazo vya kusafiri na kuzuia mali za Mohammed hapo Julai, likisema alikuwa ametoa "msaada wa kifedha, vitu, mafao au ufundi kwa al-Shabaab."
Alikuwa "kiongozi mkuu wa kiitikadi" wa kundi la Hijra la Kenya, ambalo pia linajulikana kama Kituo cha Vijana wa Kiislamu," ulisema Umoja wa Mataifa. Kundi hilo linachukuliwa kuwa mshirika wa karibu wa al-Shabaab kwa Kenya.
Mohammed "alilitumia kundi hilo lenye msimamo mkali kama njia ya kupandikiza siasa kali na kuwapa mafunzo Waafrika wanaozungumza Kiswahili ili kushiriki mambo ya uasi nchini Somalia," kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Katika ukusara wake wa Twitter, Kituo hicho cha Vijana wa Kiislamu kilitoa onyo kali kwamba "makafiri (watu wasioamini Mungu) watalipa" kwa kifo cha Mohammed. Wakiweka picha ya bomu la kwenye gari likilipuka barabarani, Kituo hicho kimesema, "Mwanzo tu wa kile kijacho au sio?"
"Kituo cha Vijana wa Kiislamu kimepeleka ujumbe kwa mujahidina wa Tanzania kuhusu ripoti za kifo cha Sheikh Rogo," lilisema kundi hilo, likionesha kwamba linaweza kutanua kisasi chake hadi nje ya Kenya.
Kiongozi wa kituo hicho, Sheikh Ahmad Iman Ali, alisema katika ujumbe uliotumwa kwenye Twitter, "Tupo kwenye njia sahihi pale viongozi wetu wanapopata shahada (wanapokufa mashahidi)."
"Atabakia nyoyoni mwetu daima," kiliongeza Kituo cha Vijana wa Kiislamu.
Polisi nchini Kenya walimkamata Mohammed mwezi Januari, wakishikilia silaha, milipuko na vifaa vya kutegea mabomu. Alipelekwa mbele ya mahakama ya Mombasa tarehe 14 Agosti kwa mashitaka ya kupanga mashambulizi katika maeneo ya umma.
Mohammed alishitakiwa kwa mashitaka sita yanayohusiana na kumiliki silaha isivyo kihalali, ambayo aliyakana na baadaye akaachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 (dola 60,000). Kesi hiyo iliahirishwa na ilikuwa imepangwa kusikilizwa tena tarehe 15 Oktoba.
Wakati huo huo, Kamati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imemuwekea vikwazo vya kusafiri na kuzuiwa kwa mali zake dhidi ya Abubakar Sharif Ahmed, mmoja wa viongozi wa Kituo cha Vijana wa Kiislamu na "mshirika wa karibu" wa Mohammed.
"Ahmed ni muwezeshaji na mtoaji mafunzo mkuu wa vijana wa Kiislamu wa Kenya anayewatayarisha vijana hao kufanya vitendo vya uasi nchini Somalia," ilisema kamati hiyo katika ripoti yake iliyotolewa tarehe 23 Agosti.
"Anatoa msaada wa vitu kwa makundi yenye misimamo mikali nchini Kenya (na kwengineko Afrika ya Mashariki)," ilisema taarifa hiyo. "Kupitia safari zake za mara kwa mara katika ngome za al-Shabaab nchini Somalia, ikiwemo Kismayo, ameweza kuwa na mafungamano makubwa na wanachama wa ngazi za juu wa al-Shabaab."
"Ahmed amehubiri katika misikiti ya Mombasa kwamba vijana wa kiume lazima waende Somalia, kufanya matendo yenye mtazamo wa siasa kali, kupigana kwa ajili ya al-Qaeda na kuwaua raia wa Marekani," kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Hadi mwaka 2010, Ahmed amefanya kazi kama mtoa mafunzo na muwezeshaji kwa ajili ya al-Shabaab katika eneo la Majengo mjini Mombasa, ilisema ripoti hiyo.
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Mimi ninachotaka sio amani bali serikali ya Kiislamu kwa kutumia sharia ya Kiislamu kuwatawala watu.Vita havitamalizika mpaka tupate serikali ya aina hiyo, Mungu Akipenda. Nataka kuwambia wale wanaosubiri amani waamke kutoka usingizi wao kwa sababu hawatapumua na kupata Sharia ya Kiislamu hadi Wamarekani na wapenzi wao wamalizwe na watamalizwa, Mungu Akipenda.
Unajua kila mtu anafanya jambo kutokana na utashi wake Sasa tuwe makini katika hilo tujaribu kuwa makini katika kuamua. Na tunapotaka kuamua turudi nyuma katika kitabu chetu kitukufu kuran. Utapata jibu jinsi ya kuamua Hilo ndio Nionavyo mimi
Mabaya mawili hayafanyi jema moja. Kumwaga damu ya watu wasio na hatia hakuwezi kutatua matatizo. Tujifunze kutoka vurugu za baada ya uchaguzi.
Ni wakati wa majaribio lakini tunachohitaji ni amani tu.
Inakirihisha, watu masikini wanakufa bila ya sababu yoyote. lakini ni hali isiyofichika kuwa serikari ndo wafanya mauaji ya viongozi wakidini wakishilikiana na baadhi ya viongozi wanafiq wakiislaam.
Nadhani vijana hawa waliochoma makanisa na kumwaga damu ya watu wasio na hatia wataishi kujuta kwa sababu Mungu hajaribiwi daima. Suala ni rahisi, jifunzeni kufanyakazi kwa bidii nyinyi vijana wavivu mnaodai kuwa watakatifu sana kwa Rogo kwa sababu hakuna unga tena ameshakufa. Hamna aibu wanaharamu nyinyi. Mkue! Acheni kuwa watoto wa mama na fikirini kwa makini. Sawa? Sina furaha hata kidogo.
Hampaswi kulipiza kisasi kwa raia wasio na hatia na sehemu za ibada. Hili litasaidia tu kutengwa kwa dini yenu. Je, ikiwa Wakristo watalipiza kisasi mashambulizi hizo? Mnaonesha rangi zenu za kweli: nyinyi wenyewe ni magaidi! Mtabaki nyuma sana daima kwa kunajisi sehemu za ibada na kuua na kulemaza wananchi wasio na hatia.
Ni wakati sasa kwa Wakenya kukaa pamoja kama taifa lililokomaa. Kile kilichotokea kuhusu kifo cha Sheikh Mohamed sio kizuri hata kidogo lakini bado imeonesha ulimwengu jinsi gani Waislamu walivyo wagomvi na wapenda vurugu tofauti na dini yao- Matendo kama haya yanawafanya waonekane kama Boko Haram na al-Shabaab. Tuache amani itawale miongoni wwa Wakenya na Wakenya waendelee tena kama taifa la kisekula na lililoungana.
Afadhli ameondoka. Aboud Rogo alikuwa jambazi hatari aliyekuwa hataki kutofautisha baina ya maadili ya kimagharibi na Ukristo. Kwa yeye Ukristo ulikuwa maadili ya kimagharibi na ndani ya moyo wake alichukia makanisa na Wakristo. Kama ajenti wa al-Qaida na al-Shabaab alifikiria kuwa njia nzuri ya watu kuishi ni kufuata utamaduni wa Kiislamu na Kiarabu. Hili lilithibitishw ana wafuasi wake kuchoma makanisa na kuwashambulia Wakristo ambao daima walikuwa hawajui kuwa walikuwa maadui.
Msipigane vijana kwa vile hili linaweza kuathiri uchumi wetu. Tunzeni amani, sote ni wamoja.
@mimi, mara nyengine unapaswa kufikiri kabla ya kuandika kwa ajili ya kuandika tu. Unaposema damu kwa damu, damu ya nani unakusudia kuimwaga? Ikiwa umehamaki kwa sababu mtu mmoja alimuua Rogo, kwa hivyo uelewe kuwa mtu mmoja pia atahamaki kwa damu ambayo una hamu ya kumwaga. Mungu ajalie yeyote aliyemwaga damu ya Rogo akabiliane na ghadhabu ya Mungu.
Umesema vizuri Moss hata wakosaji wa Kanisa la Kiambaa walilipa ghali sana. Kisasi ni cha Bwana. Sio Waislamu wote walichoma makanisa, ni wahalifu wachache tu na hawataepuka, sio chini ya jua.
NI MUNGU TU MWENYE UWEZO WA KUAMUA KIFO CHA MTU, NDUGU ZETU WAISLAMU,MAKANISA HAYA YAMEWAFANYANYIA NINI MPAKA MYACHOME MOTO? MUNGU ATAWAHUKUMU WAKOSA.
NINAWAOMBA NDUGU ZETU WA KIISLAMU KUANDAMANA KWA AMANI IKIHITAJIKA NA KUEPUKA VURUGU. SERIKALI TAYARI IMESHAAHIDI KUCHUKUA HATUA. TUSUBIRINI!!
Tangu lini mabaya mawili kufanya jema moja? Acheni uhuni na acheni matendo ya kishenzi. Iacheni sheria itawale.
Mimi ni Muislamu na nimeishi Kenya maisha yangu yote. Marafiki zangu wengi ni Wakristo na ukweli ambao unavunja moyo ni kuwa Waislamu wote si magaidi lakini magaidi wote ni Waislamu. Nadhani ni wakati kwa sisi (Waislamu) kufikiria upya itikadi zetu kuhusu kukubali na kuheshimu imani za watu wengine. Samahani kwa Wakenya wenzangu ambao wamepoteza maisha na mali zao kwa matendo haya ya aibu na ya woga yanayofanywa na ndugu zangu wanaojidai kuwa "watukufu"...
Upuuzi mtupu! Huu ni mtazamo wa kabla tu, picha inakuja karibuni.
Enyi ndugu zangu Waislamu, ni vibaya sana kufanya kisasi kwa Mkristo na watu wasio na hatia, badala ya taftunei njia bora ya kutatua tatizo. Kumbukeni kuwa watu wasio na hatia ambao mnawalazimisha kulipa deni ambalo hawana habari nalo hawatawasahau, hata Mungu ambaye mnajidai kumuabudu hatasikiliza dua zenu kwa sababu ni upuuzi.
Alikuwa katika Orodha ya Magaidi wa Kimataifa! Nani anayejua kuwa hakupigwa risasi na magaidi wenzake? Kuchoma Makanisa, kuua Wakristo, kwa jumla ni matendo ya kihuni!Askari wa Kenya wawazuwie kabisa...
Tendo lenyewe lilikuwa la kusikitisha na aibu iwe juu yenu. Serikali inapaswa kuchukua hatua haraka ili kuzuwia matendo haya.
Makosa mawili hayafanyi jema moja wapendwa marafiki Waislamu. Kwa kuchoma makanisa, uadui zaidi unajengwa baina ya Waislamu na Wakristo. Kwa nini yote hatuyaachii serikali kuyatafutia ufumbuzi badala ya kujichukulia sheria mikononi mwetu. Kwa hisani zenu, jizuieni na uchomaji wa madhebahu ya Mungu.
@Moss, tayari umeshaisema! Mungu wetu atapigana vita na yeye ni mwingi wa kusamehe kwa wale wanaotubu.
Kisasi kimethibitishwa kihistoria kuwa hakitatui masuala ya dunia. Ukweli ni kuwa tishio la sasa la kigaidi limekuwa likitumia maguruneti yale yale yanayotumiwa kwa ajili ya damu kwa damu. Ni mjinga gani anayehitaji kuhukumiwa kwa misingi ya kidini kuliko mwengine. Wakenya Wakristo, Waislamu, wenye dini za asili na wasio na Mungu kwa pamoja lazima wawe juu ya msimamo mkali kwa lengo moja.
Mpendwa Bwana, jioneshe mwenyewe ulivyo na NGUVU kwa niaba yetu. Vita hivi sio vyetu. Pigana kwa ajili yetu Mungu wa Israeli. Amen.
Imani ni kitu kimoja kinachoweza kumsababishia mtu kufanya jambo ambalo katika mazingira mengine asingeweza kufanya. Adui wenu sio wao, adui yenu ni nafsi zenu. Tunapaswa kujifunza kukubaliana kutokubaliana, sisi ndio tunayoyafanya maisha yetu wenyewe yawe ya matatizo. Unaweza kuamua matendo yako lakini huwezi kuamua matokeo ya matendo yako. Fikirini kwa makini kabla ya kutenda.
Ni aibu kuwaona Waafrika wanauwana wenyewe kwa dini za Waarabu na nchi za magharibi...Mungu, walaani watu walioleta Uislamu na Ukristo Afrika....
Sheikh Rogo na wafuasi wake lazima waelewe kwamba," anayeishi kwa upanga, atauwawa kwa upanga." Na huu upuuzi wa "Damu kwa Damu" unakera. Ukristo kwa kweli ni bora kuliko Uislamu. Wakati Wakristo walipouliwa katika Makanisa ya Kenya, Wakristo hawakulipiza kisasi. Waislamu waelewe kuwa sio pekee yao wanaojali Dunia hii.
Asante kaka/dada kwa makala hiyo hapo juu. Mwenyezi Mungu akujaalie busara na ufahamu zaidi. Inasikitisha kuwa Waislamu kuchoma makanisa kwa jina la kisasi. Tunawapenda na tunajishirikisha nao, kwa hivyo kwa nini kugeukia makanisa ambayo hayakuwafanyia chochote?
Naamini watu kama Rogo ni maadui wa Waislamu kwa sababu hakuna njia yoyote unaweza kumuita Rogo Muislamu baada ya kutetea waziwazi mauaji ya watu wasio na hatia. Uislamu unatetea maisha wazi, kuua mtu asiye na hatia ni sawa na kuua ubinadamu wote!! Mashehe hawa wenye siasa kali lazima wafungwe jela maisha. Kitu gani chema Rogo amefanya kwa Muislamu yeyote? Hawa wanaojiita leo Waislamu wanataka kulipiza kisasi kwa kifo chake, alipata kile alichostahiki. Hakukamatwa huyu na kiwango kikubwa cha silaha za mauaji? Kama angefanikiwa kuua Wakenya wengi zaidi wasio na hatia, wahubiri hawa wangefurahi? Kolego tuliite kolego na Rogo hakuwa chochote zaidi za mueneza chuki na hakuna nafasi ya waeneza chuki katika Uislamu. MUNGU AMJAALIE ABOOUD ROGO AUNGUE MOTONI MILELE, AMIN, AMIN!!
Msikiti ni pahali pa kuabudia kama lilivyo kanisa, kwa nini mnapoteza heshima kwa kutangaza matendo ya kigaidi dhidi ya watu katika mahali patakatifu? Mnataka tubadilishe jina la pahali hapa patakatifu na kupaita kambi ya kijeshi?
“Damu kwa Damu” katu haitaweza kufumbua tatizo hata kidogo. Kuchoma moto makanisa hakutasaidia, fikirieni mara mbili. Vijana hawa wanaoshiriki katika kuchoma moto makanisa watakufa tu bila ya sababu yoyote, kwa nini basi wasihubiri amani? Vipi kanisa limehusika katika suala hili? Wapendwa Waislamu, fikirieni mara mbili. Mmewahi kusikia Wakristo wakichoma Misikiti?
Hatuhitaji kuwa Waislamu au Wakristo kulaani mauaji ya raia wa Kenya, wala hatuhitaji mapambano ya wananchi ili kulimeza taifa letu. Sote tunatoka kwa Mungu mmoja mwenye majina Mengi kwa mfano Allah, Ngai, God, Mwiyai, Jile, Jah.... vijana, msipigane.
Inakirihisha, watu masikini wanakufa bila ya sababu yoyote.
Damu kwa damu, au je serikali inaweza kujitokeza na kutuambia kwa nini walimuua?
Wapendwa Waislamu wa Kenya, kwa nini mnachoma moto makanisa? Mmewahi kuona kanisa likikamata bunduki ili kumdhuru mtu yeyote? Watu wetu wamepigwa mabomu makanisani. Sisi hatuchomi moto misikiti. Hiyo si damu? Kwa nini kuwa na ghadhabu na watu wasio na hatia? Kanisa lilimjua Rogo na linaweza kumuombea. Kanisa halifurahishwi kwa kuuliwa kwake. Kwa nini mnaingia kwenye madhahabu na kuyachoma? Kwa nini hamumtafuti aliyekuwa na bunduki na kumuua. Sisi tunawasameheni. Watu waliohusika na uchomaji moto makanisa, TUBUNI. Mmekwenda mbali sana. Sisi hatutapigana. Mungu wetu hujipigania mwenyewe. YEYE ana nguvu. Hahitaji mtu kupigana kwa ajili yake. ANAWAPENDENI SANA.