Agosti 22, 2012
Kituo cha Vijana wa Kiislamu (MYC) kilicho na ushirika na al-Shabaab kina nia ya kusababisha vurugu za madhehebu nchini Kenya, maofisa wa usalama na wachambuzi wamesema.
MYC ,ambacho pia kinajulikana kama Pumwani Muslim Youth, kimesema Kenya inaendeshwa na wasio na imani na kutoa wito kwa jamii ya Kiislamu kuasi dhidi ya dola hiyo.
Kwenye sehemu ya tovuti yake ya tarehe 14 Januari, kikundi hicho kiliapa kufanya " mashambulio dhidi ya makafiri wa Kenya [wasiokuwa na imani] kwa ndugu zetu al-Shabaab hadi nchi itakapoondoa vikosi vyake kutoka Somalia".
Mwaka 2011, Kikundi cha kusimamia Eritrea na Somalia cha Umoja wa Mataifa kilitaja MYC kwa kuandikisha askari wapya, kuchangisha fedha, kutoa mafunzo na kusaidia harakati za jihadi kwa niaba ya al-Shabaab nchini Kenya.
MYC kilianzishwa mwaka 2008 na kinaongozwa na Ahmad Iman Ali , pia anayejulikana kama Abdul Fatah wa Kismayo, ambaye amekuwa akiendesha shughuli hizo nchini Somalia kutoka 2009, Kwa mujibu wa ripoti ya UN.
Kutoka kuanzishwa kwake, MYC imeanzisha mtandao imara wa wanachama na wanaowaonea huruma huko Kenya, na Ali anatoa amri kwa wapiganaji wa Kenya hadi 500, ambapo wengi wao ni watoto, huko Somalia.
" Mafanikio ya Ali katika kuandikisha askari wapya na kuhamasisha upatikanaji fedha kumefanya aonekane kuwa nyota imara ndani ya al-Shabaab," tarifa ya UN ilisema. " Kundi hili linadhamiria kufanya mashambulio ya kiwango kikubwa nchini Kenya, na bila shaka mahali pengine Afrika Mashariki."
Baada ya makataa ya awali, kundi hili lilithibitisha uhusiano wake na al-Shabaab.
"Kuinushwa kwa Ali na kuwa kiongozi mkuu wa al-Shabaab kwa Kenya kunatambulika kutoka kwa ndugu zetu wa Somalia ambao walipigana bila kuchoka dhidi ya wasioamini kuhusu umuhimu wa Wajahidina Wakenya nchini Somalia," kikundi hiki kilisema katika blogi yao na mtandao wa Twitter.
Tangu ripoti ya UN ya mwaka jana, MYC imekuwa ikifanya kazi kwa bidii ikijaribu kuiunga mkono al-Shabaab kwa kutumia mkakati wa kugawanya makundi mawili kwa kuchapisha ujumbe wa vitisho ili kueneza hofu miongoni mwa wananchi na kuchochea mapigano ya kidini nchini Kenya.
Katika maandiko ya Tarehe 30 Julai kwa Twitter, kikundi kilisema, "Kafiri anahema na kujigamba lakini hana uwezo wa kubakia madarakani, tutaleta machafuko kwenu nyote".
Katika maandiko ya Tarehe 3 Agosti kwa Twitter, MYC kilitoa hoja za wito wake wa vurugu kwa kuchapisha "Maswali ya msingi kuhusu jihadi yajibiwa".
Swali moja, "Nitarajie nini ninapojiunga na jihad?", MYC kilisema, "kwa akina kaka na akina dada wenye fursa wanaojiunga na jihad wanapewa mafunzo katika kila kitu kuanzia katika maana ya kweli ya Uislamu hadi kutumia RPG, AK-47 na silaha nyingine."
Swali jingine, "Je, nitapambana na Waislamu wengine?", kituo kinajaribu kutoihusisha dini kwa mashambulizi ya raia: "Mwislamu yeyote anayeunga mkono kuffar dhidi ya Waislamu wenzake hawezi kujiita Mwaslamu."
Katika kujibu "Ninapaswa kwenda wapi kujiunga na jihad?", MYC kiliwaeleza wafuasi wake, "Kama uko nchini Kenya zingatia hijra kuelekea Somalia."
Baadaye siku hiyo hiyo, Twitter ya MYC ilitoa jinsi ya kupata video iliyoandaliwa na aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda wa Rasi ya Uarabuni marehemu Anwar al-Awlaki, ambamo inaeleza njia 44 ambapo wafuasi wanaweza kuunga mkono jihad iliyo na vurugu.
Mkuu wa Wilaya ya Garissa Maalim Mohamud alisema wafuasi wa dini zote lazima wawe walinzi dhidi ya watu wanaotaka kuanzisha mapigano ya kidini.
"Ni mbinu ambayo kituo kinaonekana kuichukua kutoka kwa Boko Haram ya Nigeria ambao wameleta mgogoro kati ya Waislamu na Wakristo," Mohamud aliiambia Sabahi. "Lakini raia wameeleweshwa mbinu hizo na wameombwa kutovutwa na vishawishi."
Kikundi kinachochea hisia za kidini ili kuivuta jamii ya Waislamu kwenye nia yao ya kuchukiza, Mohamud alisema, akinukuu habari katika Twitter ya tarehe 30 Julai ambayo ilisema, "ndege za aina ya drone zinawaua Waislamu wasio na hatia wakati Mujahidina wanawachinja makafiri".
Wapiganaji wanajua malengo yao yanaweza kufanikiwa tu katika hali ya vurugu, na baada ya kushindwa kuishawishi jumuiya ya Waislamu kwamba vita vya al-Shabaab ni vita vya kidini, wanabadilisha mbinu kujielekeza katika mkakati wa zamani wa kugawanya na kutawala, alisema. .
David Ochami, mwandishi wa habari anayeishi Mombasa anayefuatilia kundi la wanamgambo huko Mashariki ya kati na Pembe ya Afrika kwa ajili ya gazeti la The Standard la Kenya, alisema kundi linajaribu kuteka mioyo na mawazo ya jamii ya Waislamu kwa kuanzisha ukandamizaji unaotambulika.
Wakati wanajaribu kutumia teknolojia mpya na vyombo vya habari vya kijamii kusambaza maoni yake, MYC iliwalipua na kuwadhibiti wafuasi katika akaunti yake ya Twitter ambao walishuku au kupinga mbinu zao.
Kwa mfano, alipokataa mtumiaji tweet ya MYC kuhusu ndege aina za drone kuua Waislamu wasiokuwa na hatia, kundi hilo lilijibu kwa vitisho "Wewe ni msaliti na tutakukamata".
Viongozi wa usalama wa ngazi zote wameagiza jamii ya Waislamu nchini Kenya kupuuza wito wa MYC kwa ajili ya vurugu za kidini, ambazo zinaweza kutishia amani na utulivu ambao Kenya imefikia kati ya watu tofautitofauti.
Kaimu Waziri wa Usalama wa Nchi Yusuf Haji aliiambia Sabahi kwamba pamoja na majaribio ya MYC, ni wazi kwamba vita dhidi ya al-Shabaab sio sababu ya dini, lakini badala yake ni vita dhidi ya magaidi na itikadi za wakereketwa.
"Wakereketwa wa MYC ni tishio hata kwa jamii ya Waislamu kwa sababu wanataka kuendeleza vita vya kidini," alisema Haji. "Unawezaje kudai eti serikali ya Kenya inaendeshwa na Wakristo wakati tunajua kwamba kuna Waislamu wengi waliopo katika ngazi za juu ikiwa ni pamoja na mimi ?"
Haji alisema atafanya kila linalowezekana kuwamaliza magaidi nchini Kenya.
Alisema jamii ya Waislamu inapaswa isidanganyike kwa kuwajibika na uhalifu wa baadhi ya watu. "Hakuna yeyote atakayefanya uhalifu kwa jina la dini na kutarajia kuachiwa huru'" alisema.
Waziri ameanza mikutano kadhaa ya mji kuhusisha umma na kuomba ushirikiano katika jitihada za usalama. Alifanya mikutano na jamii huko Garissa na Ijara na amepanga mengine mengi wiki zijazo.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Kama rafiki yangu Khalid anavyosema kwenye maandiko yake, njia ambayo Walter Joseph alivyosema, hakuna njia ya kufikiria kuwa Wakenya wanaweza kuwa na VITA vya kidini ... huu ni upuuzi mtupu. Yeyote anayejaribu kwa juhudi zake zote kuwatenganisha Wakenya kutoka Wakenya, Waislamu kutoka Wakenya, kujenga migogoro miongoni mwa makabila ya Kenya kutashindwa. Wengi wa marafiki zangu ni Wakristo, wanakwenda kanisani. Ninakwenda msikitini. Kwa hivyo ACHENI biashara hii. Wapumbazeni watu kwa muda fulani, lakini msijaribu kuwapumbaza watu muda wote...
Ninachoweza kusema ni kitu rahisi, sote ni Wakenya, tudumishe amani kama tulivyokuwa. Tuna taifa la kuendeleza na juhudi zetu zielekezwe huko.
Nusu ya marafiki zangu ni Waislamu, watu wanaowajibika sana, kwa hivyo magaidi ni wahalifu, sio Waislamu.
Ninaanza kwa kusema kuwa serikali yetu imeshindwa kwa niaba yetu sote Wakenya na ndio maana tunakabiliwa na hali ya aina hii. Nchi hii yenye kitengo cha kutosha cha kiintelijensia, ninakumbuka miaka 15 nyuma Kenya ilikuwa miongoni mwa nchi zenye intelijensia ya usalama bora zaidi na sasa ninashangaa waliishia wapi au kuna mtu anasinzia kazini. Sasa tukubaliane na ukweli, ni kwa sababu ya uroho tutakabiliana na vifo zaidi kwa vile wageni wanapata Vitambulisho vyetu vya Taifa na tunauza mali zetu kwa watu hawa kama ambavyo imetokea katika mtaa wa Luthuli Mboya. Karibuni watu wa asili wa eneo hilo watahamishwa kutoka Nairobi kama ilivyotokea Sudani wakati walipowaruhusu wafanya biashara kuwatawala na kama mnavyoweza kukumbuka wanakuwa wakitendewa vibaya na uongozi wa Kiislamu.
Ni wazi kabisa kuwa kikundi hiki kinatumia kila njia za kuwagawa watu kwa misingi ya dini. Hii ni hatari sana ambayo watu wanatakubali kuzamishwa kwayo. Lazima sote, Wakristo na ndugu zetu Waislamu kuungana na kulaani na kukikataa kikundi hiki. Kila mtu abebe mzigo wake kuliko kujihusisha na vitendo visivyokuwa vya sheria na matokeo yake kuyatupa kwenye dini. Tunathamini ukweli kwamba viongozi wa Kiislamu wamejitokeza kulaani vikali vurugu hizi na kuhakikisha kwamba hivi sio vita vya kidini. SOTE TUWAUNGE MKONO NA SERIKALI YETU IWASAIDIE KWA VILE WANATAKA SANA KUPAMBANA NA KUKIONDOSHA KIKUNDI HIKI. Mwisho, tusiige kile kianchotokea Nigeria. MWENYEZI MUNGU NI MKUBWA. WAKENYA TUISHI KWA AMANI. MWENYEZI MUNGU IBARIKI KENYA.
its high time now that everything should come clear we can not keep quiety and look our Churches gose on Fire like a kiosk no way Is this the war of Alishababu or Christian vas Muslims let them know that wasione simba ame nyeshewa wakafikiri ni paka the Govement should real work so fast and in time otherwise things will not be the ame again. We a tired as christian. KACHONJO
Wakenya wote wanaopenda amani, bila ya kujali dini zao lazima waamke na kupambana na uovu unaoitwa al-Shabaab na wafuasi wake. Kwa kweli MRC ni washirika wa kikundi hiki na lazima kikataliwe kabisa.
Amani ndugu zangu, tudumishe amani.
Inauma sana kuona watu wachache wanataka kuigeuza nchi yetu ya amani kuwa taifa la machafuko kwa jina la dini. Ewe Mwenyezi Mungu, tafadhali liangalie taifa letu na yatokomeze mawazo yasiyokuwa ya kitakatifu.
Ni bahati mbaya. Nchi masikini zimenasa katika vita vinavyosababishwa na nguvu za wabeberu. Kuibuka kwa itikadi kali katia Afrika ni majibu ya wale wanaofikiria kuwa serikali ni vibaraka wa NATO. Viongozi wetu wanaojitongozesha kwa wenye msimamo mikali kwa jina la kutafuta kura lazima wachunguzwe kwa makini. Waambieni wahalifu kukaa kimya na msiahidi majadiliano kwa sababu zisizothibitika. Kwa kaka na dada zetu wa Kiislamu, msikubali kudanganywa. Kenya yenye amani ni bora kuliko ikiwa na vita.
Ni kwa muda gani Wakristo watavumilia mateso ya kutisha? Tumeshawapa mashavu yote.
Wakati umefika kwa sisi kujua kuwa ni nani Mungu wa kweli. Vita vimo katika mikono ya Mungu kupigana kwa ajili a Ukristo. Wapenzi ndugu Waislamu lazima mjifunze kutokana na machafuko ya mashariki ya Kati, Israeli ni nchi ndogo ambayo haijawahi kushindwa licha ya kuzungukwa na nchi za Kiislamu zenye uwezo. Kwa nini? Kwa sababu Mungu anapigana vita vyao. Wakristo wanabakia kimya na kuona Mungu mwokozi wetu akionesha uwezo wa nguvu zake. Kenya ni ya Yesu, na tunaongozwa na Roho Mtakatifu. Wakati umefika mnapaswa kujua ukweli huu na badilisheni njia zenu na kuzaliwa upya.
MYC inapaswa kuweka akilini kuwa suluhisho la matatizo yao sio vita wala kutangaza vita vya kidini kwa wananchi wenzao (Wakristo). Tumekuwa tukiishi kwa maelewano tangu uhuru, Waislamu na Wakristo ni wamoja. Serikali lazima ichukue hatua kali juu ya vikundi hivi vya vijana vinayojiimarisha katika kufundisha vijana mafundisho ya kidini. Jihadi ilikuwa inatumika zamani sana wakati Muhammad (Amani iwe Juu yake) alipokuwa akieneza Uislamu.
Kwa nini mtu afikirie kuwa aliuliwa na Serikali ya Kenya? Vijana wanapaswa kufikiria zaidi juu ya hili. Kwa kweli sote lazima tuwatafute wauwaji ili watueleze zaidi kuhusu al-Shabaab. Francis.
Kwangu mimi, inaonesha kuwa ni ripoti yenye mapendeleo ya upande moja tu.
Amani kwa Wakenya wote: Wakristo na Waislamu kwa pamoja. Ndugu zangu, tusiwasikilize wachache waliopotea na waliokata tamaa kama ambavyo shetani anataka kujenga utengano na machafuko. Ninawapenda ndugu zangu Waislamu na sitomruhusu shetani kwa jina la al-Shabaab kutuweka chini ya mamlaka yake.
Ni wakati kwa ndugu Waislamu kufungua macho yao na kuona kuwa wanapotoshwa na al-Shabaab kwa jina la dini. Ninaiheshimu dini ya Kiislamu na wao wanapaswa kwa njia hiyo hiyo kuheshimu Ukristo. Sote tunamwomba Mungu mmoja ila tuna imani tofauti. Kwa hivyo tujifunze kama dini kuheshimu imani za wengine bila ya upendeleo. NAMASTE... Heshimu Mungu wangu nami nitaheshimu Mungu wako. Tujifunze kuishi pamoja kwa amani. Hatutaki kuigeuza Kenya kuwa nchi ya vita. Tunaipenda nchi yetu ya kenya. Amani itawale kwa wote bila ya kujali imani zao za kidini na maandiko yao.
Je, kuchinja binadamu wengine ni kwa ajili ya wale wanaodhaniwa kuwa ni Waislamu? Kwa nini hawawezi kuja na mpango ambao utawanyanyua wale wanaodhaniwa kukandamizwa kupitia elimu, kujipatia mali na afya pamoja na umwagiliaji maji katika ardhi kame za Majimbo ya Kaskazini Mashariki ambao zimekumbwa na umasikini wa kutisha. Kwa njia hii wanaweza kunyanyua hadhi za kaka na ndugu zao wapendwa na kuheshimiana kila mmoja kwa kiasi cha kuwaalika wengine kuungana nao. Uislamu ni amani na lazima iwe hivyo. Acheni kupotosha jina zuri la dini. Sote ni binadamu.
Kuna MUNGU PEPONI, VITA VYA JERICHO VILISHUKA BILA YA MTU YEYOTE KUIGUSA.
Waislamu wanapaswa kuhubiri amani misikitini na kuwaelezea wafuasi wao haja ya kuishi pamoja bila ya kujali dini ya mtu. Watu wote ni sawa mbele ya Mungu. Inasikitisha kumpiga kaka/dada yako kwa msingi wa usuli wa kabila au dini. Waislamu lazima waongoze katika njia ya amani na kuonesha kweli wako dhidi ya matendo haya ya kikatili!!
Kikundi kikubwa cha Twitter!
...Waislamu wote hawapaswi kuwekwa kundi moja. Ni wale wajinga, wavivu na wasio fikiri miongoni mwao ambao wanasababisha ugomvi ndani ya jamii kama tunavyojua kwa ajili ya kuikoa jamii kutokana na makafiri. Tuombe, ni nani kafiri? Kuhus yeyote anayehusika, hilo litakuwa neno lisilo na maana maalumu...kila mtu anapaswa kuamini kile anachotaka...halimuradi tu iwe kwa amani na kuweza kuishi kwa maelewano na wengine...
Sote ni kaka na dada na Mungu anatuita watoto wake bila ya kujali njia ambazo tunazifuata kueleka kwake na kumwabudu, lakini mwisho wa yote sote tunamwabudu Mungu mmoja na maoni yangu ni kuwa hakuna kitabu chochote kitakatifu kinachoruhusu vurugu. Kwa hivyo, dada na kaka zangu wapendwa tushikilieni amani. Ningependa kuwaomba vijana, wa Kiislamu, Kikristo, Kihindi na dini nyengine yoyote tujihusishe na shughuli za kujenga ambazo zitaifanya nchi hii yetu kuwa bora zaidi na pahali pa kusifiwa duniani. Tuna kazi ya kujenga amani na upendo miongoni mwetu na lazima tufahamu kuwa hatima nzuri imo katika majaliwa yetu.
Wakristo, Waislamu, Wahindu, Singasinga, Budha, Wayahudi na dini zote za kweli, hampaswi kusikiliza au kusoma kuhusu watu wenye msimamo mkali na njia zao za uovu. Hakuna hata dini moja kati ya hizo hapo juu inayofundisha kuwa mauaji ya watu – wanawake na watoto - wasio na hatia ni jambo jema. Wafundisheni watoto maadili mema na sio njia za uovu. Sisi kama Wakristo tutasimama pamoja na Waislamu wema wenye akili na sisi tutafundisha amani.
Hawa MYC ni akina nani hata kutoa vitisho kwa serikali?! wana nguvu kuriko serikali?! wanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka kabla ya hawajaleta madhara makubwa na kukomaza nguvu zao nchini Kenya. na Kenya haipaswi kufanya mzaha na watu hawa hatari. mimi naona ni mikakati ya Magadi kujitanua wanavaa mavazi ya aina tofauti lakini lengo lao ni moja. mavazi ya Magaidi hao ni kama El-Shababu(Somali) Boko Haram (Nigeria) Uamusho(Zanzibar) Mombasa Republican(Kenya) nk. na wote ukichunguza kwa umakini, utakuta msingi wao ni Al-queeda. haya makunda yanayojiita ya kidini lakini yakikana Imani za kidini kwa vitendo vyao, mimi naona kuwa ni hatari. kwani hakuna dini hata moja unayofundisha mauaji na vurugu, hivyo kigezo hicho kinayanyima uhalali wa kuitwa vikundi vya kidini vinavyofanya kazi ya Mwenyezi Mungu. kwani Mungu ni wa Amani siyo Mungu wa machafuko.
Siasa kali za kidini katu hazitafanikiwa hapa Kenya. Waislamu wenzangu, tujaribu kitu kingine.
Ni kweli kabisa. Hii inaonesha kuwa al-Shabaab wanapoteza udhibiti nchini Somalia shukrani kwa KDF na kwa hivyo wameamua njia nyengine kama vile kuua watu wao wenyewe na kuilaumu serikali ili kuchochea fadhaa za kidini. Ninawatahadharisha Wakenya wasije kunaswa katika mtego wao.
Nchi za Afrika ya Mashariki lazima zihakikishe kuwa amani na maelewano yanakuwepo katika nchi zetu. Watawala na viongozi lazima wawajibike kutekelza wajibu wao. MANENO YANGU KWA MARAISI ni kuwa wawe watawala na viongozi imara. WAISLAMU ACHENI SASA KUWASHAMBULIA WAKRISTO. Kwa nini? Muishi kwa amani wenzenu, Wakristo.
Asante kwa habari hii muhimu. Siku zote imekuwa hakika, tangu lile lililojulikana AZIMIO LA ABUJA, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakipanga njama za kuleta Uislamu wenye siasa kali katika Afrika ya Mashariki na hasa nchini Kenya. Ndio sababu nilishangaa sana pale Bw. Odinga alipotangaza karibuni kuwa lugha ya MRC ilikuwa kama lugha yake mwenyewe. Kabla ya kutoa kauli kama hizo, viongozi wetu lazima kwanza wafanye utafiti kwanza ili kupata ukweli uliopo nyuma ya baadhi ya vikundi vya kidini vyenye mashaka, shirika visivyo vya kiserikali na wanaharakati wanaofanya kazi zao nchini Kenya.
Nadhani ndugu zetu Waislamu wameanza kuchanganyikiwa na wanaanza kuiamini al-Shabaab. Kwa upole tunawaomba kurejea nyuma na kufikiri kuhusu mateso ndani ya Somalia ... watu wanakufa ...ukosefu wa chakula ...vita ...bunduki kila pahali ...Mateso MATUPU.
JM...Vijana wa leo wana habari zaidi kuliko miaka iliyopita. Wanapaswa kutojihusisha wenyewe na matatizo ambayo hayapo. Vijana, hebu tujihusishe na mawazo yetu wenyewe ambayo yataongeza thamani wakati wa kizazi chetu na kuepuka upotezaji wa wakati.
Inashangaza kweli yale ambayo Waislamu wanayofanya, na sio Kenya tu lakini duniani kote. Kila mtu ana haki ya kuabudu dini yoyote ambayo anahisi amani moyoni mwake. Swali moja linalohitaji jawabu kutoka kwa Wakenya, mtumishi huyo wa Kiislamu aliuliwa kanisani? Aliuliwa na mchungaji au kasisi? Dada na kaka zangu, nia zenu mbaya hazitazaa matunda.
Tunamtumikia Mungu anayeishi wa Kweli, Mungu wa Elijah. Hajawahi kushindwa na hata kwa hili tunaelewa kuwa Atashinda vita hivi kwa vile Mungu ana nguvu kuliko kitu na mtu yeyote duniani.
Inasikitisha sana jinsi tunavyojaribu kwenda mbele wakati watu wengine bado wanataka kushikilia ya nyuma kwa misingi ya dini. Hatuwezi kuikabili kesho ikiwa hatuwezi kuiona leo, kwa maneno mengine, hatupaswi kugeuza mabega yetu kwa ndugu zetu na kufuata mabadiliko licha ya ukweli kwamba hilo mara nyengine linauma, ikiwa tunataka hatima njema kwa sote na marafiki zetu.
Jeshi la ulinzi la Kenya linafanya kazi nzuri; hatutatishwa na kikundi chochote cha kigaidi.
Upuuzi.
Hii ni mbaya sana. Kwa nini wanataka kufanya hivyo nchini Kenya? Hatupo hapa ili kupigana wenyewe lakini Wakristo wanaomba amani katika nchi hata kama raisi wa nchi hii na Waziri Mkuu wanajaribu kuomba amani kwa ajili ya taifa hili.
Huu wote ni upuuzi mtupu.
Ninakubaliana kabisa na Khaalid. AMANI ni suala la kufuatiliwa. Baada ya yote, mimi sikuzaliwa Mkristo, lakini ni dhana ambayo niliikubali kwa hiari yangu. Kwa hiyo, mimi sipaswi kumlazimisha kila mtu aingie katika Ukristo, hata kama ningependa sana tungekuwa Wakristo.
Serikali za Afrika Mashariki lazima ziwe na tahadhari juu ya Al-Shaabab na wafuasi wao katika kanda hii. Usalama ambao ni msingi kwa maendeleo unaweza kutoweka katika kanda ikiwa uvumilivu wa kidini utamomonyoka . Al-Shaabab ni kama wendawazimu kwa kudhani kuwa wanaweza kulazimisha Uislamu wao kwa kupitia kooni mwa wale ambao kiroho hufuata madhehebu tofauti na wao.
Natumai "wanajihadi" hawa wameingiwa na akili zao halisi ... Bahati mbaya wanajiita Waislamu. Hawa ni bunduki za kukodi, mamluki wasio na huruma. "anatikisa kichwa"
Ningependa kuwaambia Waislamu wa kweli wa Kenya kwa pamoja kujilinda wenyewe dhidi ya wale wanaowapotosha watoto wao kwa jina la dini. Mrengo wa mawazo ya Kiislamu kama ya MYC yanachukua fursa ya wale wanaosilimu na wasioelimika ambao hawana uelewa wa kisekula wala wa kidini. Waulizeni watu wa Somalia kama al-Shabaab ni Waislamu au waliletwa kuwaharibu Waislamu. Hawafanyi chochote kwa wasioamini kwa sababu waliletwa na Israel.
Jembe tuliite jembe si kijiko kikubwa
Waislamu wanakatazwa na Mwenyezi Mungu wasiwe na msimamo mkali katika kitabu kitakatifu {Koran}. Vitendo ambavyo al-Shabaab walitumia kuchagua jihadi si kama wao walivyofikiria. Al-Shabaab ni magaidi ingawa watu wengi wa dini wanawaita magaidi wa Kiislamu, lakini kila kitu hakiwezi kuwa kama ilivyopangwa. Kuna mara walisema kuwa vidole vyote si sawa. Kwa hivyo katika dunia hii tutaona vitu vya kushangaza. WAUNGWANA ACHENI kuwalaumu wengine bila ya sababu yoyote, ........... WAISLAMU SI MAGAIDI.
Siiamini kwa sababu venye ninavyoona mambo yanavyokwenda, watu hawataamini.
Wakenya waishi pamoja kwa amani bila ya asili zao za kidini. Sote ni ndugu. Kama nitajikata damu yangu ni nyekundu. Watu wote ni muhimu. Mtu anapokuwa ndani tumbo la mama yake anakuwa na dini gani?
Wakati umefika wa kutofautisha ukweli na njozi. Vita havimnufaishi yeyote mwishowe!
Hii ni ishara mbaya kwa eneo hilo. Ikiwa hatua hii itasambaa Afrika Mashariki yote itakuwa katika matatizo. Ninaitaka jamii bila ya kujali dini yao kuondokana na mawazo hayo na kuyavunja moyo. Viongozi wa kidini lazima wasimame imara kuvunja moyo hoja hiyo.
Upuuzi, hawaelekei popote.
Hii si haki kwa alshabab
Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Mungu. Waislamu na Wakristo tuishi kwa amani nchini Kenya. Ni nchi ya kila mtu. Suluhisho kwa Afrika kwa jumla ni kueneza misingi ya amani na upendo mara nyengine tena na kueneza dhana ya kuwakubali wengine bila ya kuwakataa. Bila shaka, hii ni kazi ya watu walioelimika na sio kazi ya watu wasio na akili. Ikiwa watu wenye fikra kupitia kwenye maneno yao wanaeneza kuwa na hisia za kutowavumilia wengine, hivyo kushindwa kunatusburi sote kwa sababu mtindo huu wa kigaidi usiopimwa wala usiochunguzwa hautaweza kubadilisha akili sugu, zinaweza kuwafanya kuwa sugu zaidi. Kwa kuvitokomeza vikundi hivi, utulivu utarejeshwa nchini. Kutakuwepo na mabadilishano zaidi ya kibiashara na usalama katika maeneo yenye mafuta. Kwa hivyo, utokomezaji wa vikundi vya kigaidi kunaambatana na amani na usalama wa kimataifa.