Agosti 19, 2012
Watoto wa Mogadishu wanasherehekea Eid al-Fitr kwa furaha kubwa kwa mara ya kwanza baada ya al-Shabaab kuondoka jijini mwezi wa Agosti 2011.
"Baada ya kusubiri kwa miaka sita, sasa tunaweza nyuso za furaha na bashasha za watoto wetu wasio na hatia wakisherehekea Eid al-Fitr bila ya vurugu au mapambano ya umwagaji damu jijini," alisema Abdiqani Yusuf, mkaazi wa Mogadishu. "Vijana wa Somalia wanajiuguza madonda yao yaliyosababishwa na mijeledi ya magaidi wa kigeni na Wasomali watiifu kwa al-Qaida, wenye uchu wa mauaji na umwagaji damu."
Yusuf aliiambia Sabahi kuwa watoto wanatabasamu tena huku wakiaga ukatili wa al-Shabaab.
Magaidi ni maadui wa watu wetu na nchi yetu na hakuna kikomo cha ukatili na uhalifu wao," Yusuf alisema.
Taysir Jama Abdulqadir, baba wa watoto wanne, aliiambia Sabahi ya kuwa mwaka jana, watoto hawakuweza kutembelea fukweni, maeneo ya kucheza na sinema kwa sababu walikuwa katika hatari ya kukumbana na magari yaliyotegwa mabomu na vifaa vya milipuko vya kutengeneza haraka haraka.
Pia wakaazi wa Mogadishu hawakuweza kutembelea jamaa na marafiki zao walioko Balad, Afgoye, Beledweyne, Baidoa, Hudur na Garbaharey kwa sababu al-Shabaab wangewashambulia na mara nyengine kuwaua. Lakini tangu wakati huo, miji mikuu na midogo imekombolewa na vikosi vya Somalia na washirika wake.
"Huko nyuma, sherehe mjini Mogadishu zilikuwa ni jukwaa la maumivu na moshi ulijaa angani kutokana na mashambulizi ya kigaidi," Abdulqadir alisema. "Lakini sasa, mwanga wa matumaini unachomoza katika nyuso za wenyeji wanaojaribu kusahau wasiwasi, maumivu, dhulma, ugumu wa maisha, mateso na huzuni zilizokuwa zimewajaa."
Hoda Dahir, msichana mwenye umri wa miaka 13, alikuwa na hamasa ya kuvaa nguo zake mpya kwa ajili ya Eid.
"Ninahamu ya kutoka nje na kusherehekea siku kuu na bibi yangu anayeishi katika mji wa mwambao wa Marka," aliiambia Sabahi. "Bila ya shaka, sitasahau kwenda kupokea pesa kutoka kwa jamaa zangu siku hiyo."
Bashir Harid, mvulana mwenye umri wa miaka 12, aliiambia Sabahi kuwa anataka kucheza na marafiki zake na kutembelea nyumba za jamaa na marafiki wa familia ili kupokea zawadi za pesa za Eid na vitu vitamu.
Tafouti na siku za nyuma, mitaa ya Mogadishu, Afgoye na Balad ilikuwa uwanja wa vita vya kuigiza vinavyochezwa na watoto wakitumia silaha za plastiki za kuchezea. Watoto huenea mitaani na vichochoroni, wakilipua fataki wakati wa sherehe.
Kabla ya Eid, masoko makubwa mjini Mogadishu, ikiwa ni pamoja na yale ya Bakara, Hamar Weyne na Suuq Baad, yalijaa wanunuzi waliokuwa wanajitayarisha na Eid, kwa kununua nguo mpya, viatu na vitu vitamu.
Mudey Ibrahim Dhere, mfanya biashara ya nguo katika soko la Hamar Weyne, aliiambia Sabahi kuwa kuna mahitaji makubwa ya nguo za watoto wa umri wa miaka 3 na 15, ikiwa ni pamoja na mashati, jeans, suruali na kanzu. "Bei za bidhaa kutoka nje zimepanda," alisema.
Asubuhi ya siku ya Eid al-Fitr, washerehekeaji hupeana mikono na kumuomba Mungu msamaha na baraka zake. Watu huenda kwenye sala ya Eid, ambayo huanza baada ya jua kuchomoza.
Imam Hassan Fidow, mhutubu wa msikiti katika Wilaya ya Wardhigley, aliiambia Sabahi kuwa kupeana mikono ni mila ambayo wanaotakiana mema wa Somalia huamkiana na kukumbatiana wakati wa Eid.
Ni mila wakati wa Eid kuwakumbuka wale wenye shida, kama vile mayatima, watu wa ndani waliokimbia makazi yao na watu waliopatwa na athari za kukosekana kwa utulivu na njaa.
Raaliyo Sheikh Abdiaziz, mwanaharakati wa Jumuiya ya Kiraia mjini Mogadishu, aliiambia Sabahi kuwa baadhi ya watoto huomba pesa ili kuwapa watoto wenzao katika makambi za watu waliokimbia makazi yao mjini Mogadishu, ambao hawana chochote isipokuwa nguo kongwe, ili na wao wahisi uchangamfu wakati wa Eid na wawe na furaha.
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
Moto kwenye soko kubwa la Garissa uliharibu zaidi ya maduka 100 usiku wa Jumatatu (tarehe 17 Juni...
Waziri wa Umoja wa Kitaifa wa Djibouti Zahra Youssouf Kayad alisaini mikataba ya miradi miwili ye...
Kamati ya bajeti ya Bunge ya Kenya imekataa pendekezo la kununua ofisi mpya kwa aliyekuwa Rais Mw...
Moto ulifanya uharibifu mkubwa katika mji wa Balbala huko Djibouti siku ya Jumapili (tarehe 16 Ju...
Picha ambazo al-Shabaab ilizituma siku za Jumapili (tarehe 16 Juni) kwenye mtandao wa Twitter za ...
Polisi nchini Kenya walimuua mtuhumiwa wa ugaidi, Kassim Omolo Otemo, mjini Mombasa wakati uvamiz...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Kuna ulazima wa kusisitiza haja kuwakinga vijana dhidi ya mawazo ya siasa kali na maoni yasiyokuwa na nidhamu yaliyowapelekea katika ugaidi na siasa kali, na kwa kueleza wazi maadili na mafunzo ya Kiislamu kuhusu kuwa na wastani kushughulikia na wengine pamoja nakuwepo pamoja kwa dini zote kihistoria katika nchi za Kiislamu. Kuna mitanziko mingi na shinikizo kuhusu Uislamu kwa sababu ya tabia za uzembe, na hapa lazima tuhakikishe wajibu wa viongozi wa Kiislamu katika kukuza maadili ya upendo, uvumilivu na uwastani katika mzunguko wa jamii. Vile vile kuna ulazima wa kuonesha umuhimu wa jukumu la viongozi wa Kiislamu katika kueneza utamaduni wa majadiliano, kuvumiliana na kufafanua nafasi ya Uislamu kwa misingi ya majadiliano na wengine kupitia nafasi za ushahidi wa Mtume Mtukufu na Makhalifa wake baada yake katika kujadiliana na wasiokuwa Waislamu. Umuhimu wa wajibu wa viongozi wa dini kama madaktari wa kiroho wa mioyo na akili na jamii.
Nimefurahi kuona mabadiliko ya kweli mjini Mogadishu na maeneo mengine yaliyokombolewa.