Wasifu wa wagombea wakuu wa urais wa Somalia

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Agosti 17, 2012

  • 188 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Zaidi ya wagombea 35 wanapigania nafasi ya juu kabisa nchini humo. Ufuatao ni muhtasari wa wasifu wa wagombea urais maarufu kabisa:

  • Kutoka juu kushoto: Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, Sharif Hassan Sheikh Aadan, Hassan Sheikh Mohamud, Abdiweli Mohamed Ali, Abdirahman Abdullahi Baadiyow. [Jalada]

    Kutoka juu kushoto: Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, Sharif Hassan Sheikh Aadan, Hassan Sheikh Mohamud, Abdiweli Mohamed Ali, Abdirahman Abdullahi Baadiyow. [Jalada]

  • Sheikh Sharif Sheikh Ahmed. [Jalada]

    Sheikh Sharif Sheikh Ahmed. [Jalada]

  • Abdiweli Mohamed Ali. [Jadala]

    Abdiweli Mohamed Ali. [Jadala]

  • Sharif Hassan Sheikh Aadan. [Jalada]

    Sharif Hassan Sheikh Aadan. [Jalada]

  • Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo. [Jalada]

    Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo. [Jalada]

  • Abdirahman Abdullahi Baadiyow. [Jalada]

    Abdirahman Abdullahi Baadiyow. [Jalada]

  • Hassan Sheikh Mohamud. [Jalada]

    Hassan Sheikh Mohamud. [Jalada]

  • Yusuf Garaad Omar. [Jalada]

    Yusuf Garaad Omar. [Jalada]

Sheikh Sharif Sheikh Ahmed

Sheikh Sharif Sheikh Ahmed ndiye rais wa sasa wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho (TFG), ambayo muda wake unamalizika tarehe 20 Agosti.

Ahmed alizaliwa mwaka 1964 karibu na mji wa Jowhar, ambako alipata elimu yake ya msingi. Baadaye alihamia Mogadishu na kumaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Sheikh Sufi.

Mnamo mwaka 1992, Ahmed alijiunga na Chuo Kikuu cha Kordofan nchini Sudan na miaka miwili baadaye alipelekwa kwenye Chuo Kikuu Huria cha Libya, akahitimu katika Chuo cha Sharia na Sheria mnamo mwaka 1998. Alifundisha Jiografia, Kiarabu na Masomo ya Dini katika Skuli ya Sekondari ya Juba hadi mwaka 2004 alipoteuliwa kuuongoza Umoja wa Mahakama za Kiislamu (ICU).

ICU ilikuwa ni umoja wa mahakama za sharia za mikoa ambao ulidhibiti sehemu kubwa ya kusini mwa Somalia.

Mwaka 2007, Ahmed aliondoka ICU na akiwa na wanachama wengine wa zamani waliunda kundi la upinzani lililoitwa Umoja kwa Ukombozi Mpya wa Somalia. Baadaye aliingia kwenye mazungumzo yaliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa na serikali ya mpito chini ya marehemu Rais Abdullahi Yusuf Ahmed, na kujiunga na bunge la mpito la Somalia.

Ahmed alichaguliwa kumrithi Yusuf baada ya Yusuf kujiuzulu Disemba 2008. Ahmed alianza rasmi wadhifa wa urais tarehe 31 Januari 2009.

Rais Ahmed anazungumza Kisomali na Kiarabu.

Abdiweli Mohamed Ali

Abdiweli Mohamed Ali alizaliwa mwishoni mwa miaka ya 1950. Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, alijunga na Chuo Kikuu cha Taifa cha Somalia alikohitimu shahada ya kwanza katika fani ya uchumi mwaka 1984.

Alikuwa mkurugenzi wa idara ya kodi katika Wizara ya Fedha na Mapato kuanzia katikati hadi karibu na mwisho wa miaka ya 1980. Kutoka mwaka 1988 hadi 1991, alikuwa mkurugenzi msaidizi katika Idara ya Utafiti na Takwimu kwenye Wizara ya Fedha na Mapato.

Baada ya hapo, alihamia Marekani kuendelea na elimu yake ya juu.

Alipata shahada yake ya pili kutoka Chuo Kikuu cha Vanderbilt cha Nashville, Tennessee mwaka 1998 na kisha kupata tena shahada nyengine ya pili katika fani ya utawala kutoka Chuo Kikuu cha Havard mwaka 1999.

Alipata shahada ya juu ya udaktari wa falsafa katika fani ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha George Mason cha Virginia mwaka 2000.

Mwaka 2003, Ali alifundisha uchumi katika Chuo Kikuu cha Niagara, New York, hadi alipojiunga na serikali ya mpito ya Somalia kama naibu waziri mkuu na waziri wa mipango na ushirikiano wa kimataifa.

Aliteuliwa kuwa waziri mkuu Juni 2011 baada ya Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo kujiuzulu.

Ali ana uzoefu wa hali ya juu katika masuala ya taaluma na tafiti za kitaalamu, maendeleo na siasa ya uchumi na vile vile fedha na utawala. Alifanyia kazi mashirika kadhaa ya kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Kabla ya kurejea Somalia mwaka 2010, Ali alikuwa mwanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Marekani na Jumuiya ya Uchumi ya Atlantic.

Ali anazungumza Kisomali, Kiingereza na Kitaliano na ana uraia wa nchi mbili, Somalia na Marekani.

Sharif Hassan Sheikh Aadan

Sharif Hassan Sheikh Aadan alizaliwa mwaka 1946 mjini Bardaale katika familia ambayo kiasili ilitokea mikoa ya Bay na Bakool.

Aadan aliingia kwenye siasa mwaka 2004 alipochaguliwa kuwa spika wa bunge la mpito la Somalia. Alishikilia wadhifa huo hadi mwaka 2007 alipoondolewa kwa kufanya mazungumzo yasiyoidhinishwa na wajumbe wa Umoja wa Mahakama za Kiislamu.

Aadan aliteuliwa kuwa naibu waziri mkuu na waziri wa fedha wakati Rais Ahmed alipochukuwa madaraka mwaka 2009, na akawa mmoja wa viongozi wakubwa kabisa katika baraza la mawaziri la waziri mkuu aliyepita Omar Abdirashid Ali Sharmarke.

Mwezi Mei 2010, bunge la Somalia likamchagua tena Aadan kama spika wake.

Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo

Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo alizaliwa mwaka 1962 mjini Mogadishu katika familia kutokea Gedo kusini magharibi mwa Somalia.

Mwaka 1985 alichaguliwa katibu katika ubalozi wa Somalia huko Washington DC.

Mwaka 1989 aliacha kazi hiyo kwa ajili ya kuchukua shahada ya kwanza katika fani ya historia kutoka Chuo Kikuu cha Buffalo jijini New York. Katika kipindi hicho, Farmajo aliomba hifadhi ya kisiasa nchini Marekani baada ya serikali kuanguka mwaka 1991.

Aliendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Buffalo na kupata shahada ya pili katika fani za sayansi ya siasa na mahusiano ya kimataifa.

Baada ya kupata uraia wa Marekani, alifanya kazi kadhaa katika jimbo la New York, ikiwemo kwenye Mamlaka ya Makazi ya Manispaa ya Buffalo, Kitengo cha Fursa Sawa za Ajira katika wilaya ya Erie na Idara ya Usafirishaji ya Jimbo la New York.

Rais Ahmed alimteua Farmajo kuwa waziri mkuu Oktoba 2010 kumrithi Omar Abdirashid Ali Sharmarke aliyejiuzulu baada ya mzozo kati yao.

Farmajo alijiuzulu wadhifa wake Juni 2011 chini ya shinikizo la jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya Mkataba wa Kampala kati ya Rais Ahmed na Spika Aadan, ambapo muda wa mwisho wa serikali ya mpito uliongezwa hadi tarehe 20 Agosti mwaka wa 2012.

Mwaka 2011, Farmajo alianzisha chama kipya cha siasa, Haki na Usawa, ambacho pia kinajuilikana kama Tayo.

Farmajo kwa sasa ni katibu mkuu wa Tayo, ambacho mwenyekiti wake ni Dk. Mariam Qasim, aliyekuwa waziri wake wa masuala ya wanawake. Tayo ni chama cha kwanza cha kisiasa nchini Somalia kuongozwa na mwanamke.

Farmajo anazungumza Kisomali na Kiingereza na ana uraia wa Somalia na Marekani.

Ali Mohamed Ghedi

Ali Mohamed Ghedi alizaliwa Mogadishu mwaka 1952.

Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari, alijiunga na Chuo Kikuu cha Taifa cha Somalia mjini Mogadishu na kuhitimu shahada ya kwanza katika fani ya sayansi ya mifugo. Baadaye alikwenda Italia kwa elimu ya juu chini ya ufadhili wa masomo wa miaka miwili kwenye Chuo Kikuu cha Pisa mwaka 1979.

Mwaka 1981, Ghedi alirejea Mogadishu ambako alifundisha kwenye Kitengo cha Madawa ya Wanyama katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Somalia, na ambako mwishowe akawa mkuu wa kitengo hicho hadi serikali ilipoanguka mwaka 1991.

Ghedi alitumikia wadhifa wa uwaziri mkuu katika Serikali ya Mpito ya Shirikisho chini ya utawala wa Rais Abdullahi Yusuf kutoka mwaka 2004 hadi 2007 alipojiuzulu.

Hii ni mara ya pili kwa Ghedi kupigania urais; mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2009, lakini aliondoa jina lake.

Ghedi anazungumza Kisomali, Kiingereza na Kitaliano.

Abdirahman Abdullahi Baadiyow

Abdirahman Abdullahi Baadiyow alizaliwa mwaka 1954 katika mkoa wa Galguduud katikati ya Somalia.

Baadiyow alijiunga na Jeshi la Taifa la Somalia mwaka 1971 alikofikia hadi cheo cha Luteni Kanali na kubakia akihudumu hadi mwaka 1986, alipoamua kuondoka jeshini kutokana na hatua ya kijeshi ya Rais Siyad Barre dhidi ya makundi ya kikabila yenye silaha yaliyokuwa yameanza kuupinga utawala wake.

Baada ya kuondoka jeshini, alijiunga na Chuo Kikuu cha McGill nchini Canada alikosomea shahada ya pili na shahada ya juu ya udaktari wa falsafa katika fani ya Masomo ya Kiislamu.

Alirudi Somalia mwaka 1993 akiwa kama mkurugenzi wa kanda ya Afrika ya Mashariki wa shirika la msaada na maendeleo la Marekani, Mercy, linalofanya kazi ya kutoa misaada ya dharura na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kielimu. Akiwa na Mercy, Baadiyow alifanya kazi kwenye miradi ya afya na elimu hadi mwaka 2007, akianzisha skuli za msingi na sekondari na pia vituo vya afya kwenye eneo hilo.

Mwaka 1996 alishirikiana na wenzake kuanzisha Chuo Kikuu cha Mogadishu ambapo hadi sasa ni mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya chuo hicho.

Mwaka 2000, Baadiyow alishiriki Mkutano wa Amani wa Taifa wa Somalia uliofanyika Djibouti na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Wataalamu iliyopewa jukumu la kusimamia mkataba wa Serikali ya Mpito ya Taifa.

Baadiyow anazungumza Kisomali na Kiingereza na ana uraia wa Somalia na Canada.

Ahmed Ismail Samatar

Ahmed Ismail Samatar ni mwanataaluma maarufu ambaye ameishi marekani kwa zaidi ya miaka 30.

Kwa sasa ni Profesa James Wallace wa Masomo ya Kimataifa katika Chuo cha Macalester huko Saint Paul, Minnesota, ambako pia aliwahi kufanyakazi kama Mkuu wa Maomi ya Kimataifa na Mipango, na Mkuu mwanzilishi wa Taasisi ya Uraia wa Dunia.

Uzoefu wa Samatar ni katika maeneo ya siasa ya uchumi wa kimataifa, mawazo ya kijamii na kisiasa na maendeleo ya Afrika. Ameandika vitabu vitano na amechapisha zaidi ya makala 30. Alipata shahada yake ya udaktari wa falsafa mwaka 1984 katika Chuo Kikuu cha Denver.

Amehadhiri katia vyuo vikuu kadhaa ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Taifa cha Somalia, Shule ya Uingereza ya Uchumi na Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Coronel, Chuo Kikuu cha Havard, Chuo Kikuu cha Amsterdam ma Chuo Kikuu cha Otago.

Samatar anatokea eneo la kaskazini mwa nchi na anapinga kujitenga kwa Somaliland na sehemu nyengine za nchi bila ya makubaliano.

Kwa sasa ni kiongozi wa chama cha siasa cha Hiil Qaran, na ni mmoja miongoni mwa wagombea 13 waliounda mseto unaoitwa Jumuiya ya Taifa kwa Maendeleo. Kikundi kimefikia muafaka wa umoja na kitachagua mmoja wa wanachama wake kwa ajili ya kugombea uraisi.

Samatar ana uraia wa nchi mbili, wa Somalia na wa Marekani na anazungumza Kisomali, Kiarabu na Kiingereza.

Hassan Sheikh Mohamud

Hassan Sheikh Mohamud ni mwanataaluma, mwanasiasa na mwanaharaki wa kiraia aliyewahi kufanya kazi katika mashirika kadhaa ya kitaifa na kimataifa ya amani na maendeleo.

Mohamud alihitimu katika Chuo Kikuu cha Taifa cha somalia mwaka 1981 na kwenda kusoma India ambako alipata shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Bhopal mwaka 1988.

Mwaka 1993, Mohamud alifanya kazi katika Mfuko wa Dharura wa Watoto wa Umoja wa Mataifa kama afisa wa elimu kusini na kati ya Somalia mpaka kuondoka kwa Operesheni ya Umoja wa Mataifa katika vikosi vya Somalia mwaka 1995.

Mwaka 1999, alishiriki katika kuanzisha Taasisi ya Somalia ya Uendeshaji na Maendeleo ya Utawala, ambayo baadaye iligeuka kuwa Chuo Kikuu cha Simad, ambako alikuwa mkuu wa chuo hadi mwaka 2010.

Mwaka 2011, alianzisha Chama cha Amani na Maendeleo na hadi sasa ndiye mwenyekiti wake.

Mohamud anazungumza Kisomali na Kiingereza.

Yusuf Garaad Omar

Yusuf Garaad Omar ni mwandishi wa habari mkongwe na mkurugenzi wa zamani wa Idhaa ya Kisomali ya BBC London.

Omar alizaliwa mwaka 1960 katika wilaya ya Hamar Jajab mjini Mogadishu na kumaliza elimu yake ya sekondari mjini Mogadishu. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Taifa cha Somalia ambako alisomea Kifaransa na kuhitimu shahada ya kwanza ya sanaa katika fani ya Isimu.

Alijiunga na Radio Mogadishu mwaka 1984 ambako alifanya kazi hadi kuanguka kwa serikali kuu.

Mwaka 1990, Omar alihamia Italia na kujiunga na Chuo Kikuu cha Siena kwa masomo ya juu ya taaluma ya Elimu ya Binadamu. Alijiunga na Idhaa ya Kisomali ya BBC mwaka 1992, akianzia kama mwandishi wa kujitegemea kutokea Italia. Alikuwa mkuu wa Idhaa hiyo hadi mwaka 2000.

Omar ana uraia wa Somalia na Uingereza na anazungumza Kisomali, Kiingereza, Kitaliano na Kifaransa.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 178)

Dislike_icon(55)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • ducaale saciid xasa oo ku magac dheer warside
    February 7, 2013 @ 04:05:24AM

    Makala niliyosoma leo hapa tarehe 7/2/2013 ni nzuri sana, kwangu mimi. Kwa heri.

  • ع؟
    December 26, 2012 @ 02:46:58AM

    Kama ingekuwa katika uwezo wangu, basi ningemteua Mohammad Ahmad bin Hadan kwa vile ninamhusudu kwa kuwa ni mtu wa kimataifa, mfanyabiashara na Muislamu. Naomba Mungu awarehemu wale waliofariki.

  • ahmed
    September 19, 2012 @ 06:50:06AM

    Tunamshukuru Mungu kwa kuipa Somalia rais ambaye hafanyi kazi na watu wachoyo ambao watakwamisha maendeleo ya nchi na watu wetu. Ni aina ya rais ambaye tulikuwa tunamtaka.

  • cabdi cali
    September 13, 2012 @ 10:25:07AM

    Nimefurahi sana kuwa Wasomalia watamaliza ubunifu na matatizo ikiwa tutaunga mkono mageuzi yanayotokea nchini, ili kumaliza matatizo. Na hilo ni jambo zuri. Ninamkaribisha rais mpya na nina imani kubwa kwamba kwa yeye kutakuwa na mabadiliko.

  • samira hussin
    September 11, 2012 @ 02:44:22PM

    Ewe Mungu, mjaalie rais mpya wa taifa la Somalia na watawala wetu kufuata haki. Enzi mpya imeanza kwa taifa. Ninamuomba Mungu kuifanya nchi yetu na zote za wenye kuamini kuwa salama. Tusifikirie juu ya yaliyopita. Kwa sababu hayatarejea tena. Hatuna chochote isipokuwa sasa na hatima. Ninamuomba kila mtu kutuma baraka bilioni 15 kwa Mtume wetu, amani iwe juu yake. Natumai kuwa kila mtu ataungana nasi. Tuma baraka zako kwa Mtume.

  • abdirashiid osmaan
    September 10, 2012 @ 11:17:05AM

    Ningetoa dhamana wa urais kwa Hassan Sheikh Mahomud, ndugu yangu ambaye ana uzoefu.

  • Abdirazak Idriss Jama
    September 10, 2012 @ 02:59:49AM

    Ningependa kuonesha kuunga mkono kwangu wa Mheshimiwa Mohammad Abdullahi Mohammad Farmajo ambaye nina matumaini makubwa kuwa ataiongoza Somalia kwa hatima bora zaidi. Sidhani mtu mwengine anaweza kurejesha amani nchini Somalia isipokuwa Farmajo

  • Cali Mahdi maxamuud Yuusuf
    September 10, 2012 @ 12:52:05AM

    Ningependa kuzungumzia juu ya Mheshimwa Abdiweli Ali Gas. Yeye ni msomi wa chuo kikuu aliyefanya kazi nchini Somalia hivi karibuni na aliyeiinua nchi kufikia hali yake ya sasa. Nadhani angeweza kuiongoza nchi kwa njia ya haki na kuipeleka kwenye maendeleo kwa sababu mnaweza kuona kile alichofanikiwa wakati wa kipindi chake cha uwaziri mkuu nchini Somalia, isipokuwa mtachagua kwa kuziba macho yenu kwa makusudi. Ninamuomba Mungu amsaidie awe rais wa Somalia.

  • ibraahim cabdi
    September 9, 2012 @ 09:24:52AM

    Amani iwe juu yenu. Ningependa kutuma salamu zangu kwa Wasomali wote popote walipo. Sijawahi kuona serikali inayofanya kazi au utulivu nchini Somalia maishani mwangu kote. Mtu ambaye atapewa dhamana, anasubiriwa na mambo mengi ya kufanya. Mungu amjaalie atakayekuwa rais wetu, awe mtu mzuri ambaye atatuongoza kulingana na dini yetu kama ilivyobainishwa na Mtume wetu (Amani Iwe Juu Yake). MUNGU MJAALIE AWE MTU WA DINI. AMIN

  • أحمد عبد الكريم عمر
    September 8, 2012 @ 07:39:54PM

    Kwanza; Amani, Baraka na rehema za Mungu ziwe juu ya kila mmoja. Pili, sioni tafauti yoyote baina ya uchaguzi wa sasa wa urais na uliotangulia. Tatizo sio kuhusu wagombea kama Sheikh Sharif na wengine, bali uongo wa wale wanaoongoza kama vile (Augustine) Mahiga na wale waliotuchagulia Ahmed kama rais. Uchaguzi ungekuwa na faida kama ungefanyika bila ya kuingiliwa na wageni kwa vyoyote. Nadhani mtu pekee miongoni mwa wagombea anayeweza kupata tena usalama na utulivu nchini ni Mohamed Abdullah Mohamed Farmajo; ikiwa Wasomali ni watumwa wa utii wa ukabila wangekuwa wamelijua hilo. Natumai kuwa wabunge hawatakuwa mamluki wanaofanyakazi kwa maslahi yao binafsi na kuomba pesa kutoka kwa wagombea. Natumai watachamchagua yule anayeweza kuongoza taifa na kufanya kazi kwa mageuzi

  • Jelle kenya
    September 8, 2012 @ 10:33:28AM

    Kila mtu aliteseka nchini Somalia. Wengi walikufa, wengine wako katika kambi za wakimbizi wakati waliobakia ni matakfiri na al-Shabaab, Hakuna wa kutawaliwa.

  • Jelle
    September 8, 2012 @ 10:01:14AM

    Hakuna yeyote kati yao anayeweza kuibadilisha Somalia. Bora ije serikali ya kijeshi.

  • xaji maqoste
    September 8, 2012 @ 02:35:27AM

    Kwanza, ningependa kutuma salamu zangu kwa wafanyakazi wote wa habari wa Sabahi. Pili, nadhani Somalia ilikuwa haina sheria na haikuwa na serikali kuu kwa zaidi ya miaka 20. Kwa hivyo, haihitaji mpiga kampeni mtaalamu bali kiongozi mwenye manufaa. Haihitaji viongozi mafisadi bali kiongozi mwenye mwelekeo wa mafanikio. Haihitaji viongozi matajiri mafisadi bali uongozi mpya. Nadhani Ali Badiyow anaweza kuleta mabadiliko.

  • Mohamed
    September 7, 2012 @ 06:46:57PM

    Ninamwamini Yusuf Garad ni mgombea bora zaidi na ninamuunga mkono.

  • Hassan Said
    September 7, 2012 @ 10:41:33AM

    Nawatakia kila la kheri ndugu zangu huko Somalia katika mchakato wa kupata kiongozi bora,mzalendo,mwenye kujali maslahi ya wananchi wa Somalia,waishi kwa amani pasipo umwagaji wa damu inshallah Mola yu pamoja nanyi.Nashukuru sana Sabahi kwa kutoa sifa za wagombea,wapo wenye elimu nzuri kama Dr Baadiyow.Imefika kipindi tuseme umwagaji wa damu umefika kikomo nchini Somalia

  • fuqdinley
    September 6, 2012 @ 06:12:55PM

    Tumchague Samatar halafu tutangaze vita na wanaotaka kujitenga wa Isaac na kuiunganisha Somalia yote.

  • Dawid
    September 3, 2012 @ 10:45:34AM

    Makala hii ni nzuri. Kwa kusema kweli tumepoteza muda mwingi na sasa tuombe kwa mwanzo mpya, Naamini kuwa mtu yeyote ambaye hana fikra za kial-Shabaab anayo fursa ya kufanya vizuri zaidi.

  • in Mooge
    September 2, 2012 @ 07:53:13AM

    Watu hawa wamejieleza na kujitangaza sana. Ninaweza kusema aina hii ya maelezo hayahitajiki kwa sababu yanaonesha masilahi yao binafsi na kwa sababu hii tunapaswa kumpa dhamana katika bunge yule ambaye hakujieleza mwenyewe kama tulivyoambiwa na mtume wetu (Amani Iwe juu yake). Nadhani, tutapata mtu aliye bora zaidi kwa kutumia njia hii. Vyenginevyo, ninachoona kinaendelea kinaweza kuitwa kujiuza mwenyewe au kuwaibia wengine pesa zao.

  • suldaan aadan cali
    September 2, 2012 @ 06:57:12AM

    Kwanza, ningependa kuwashukuru kwa kuturuhusu kuelewa juu ya maelezo binafsi ya wagombea. Pili, ningempigia kura Prof. A/weli Mohammad Gas kama raisi, mtu wa kuchaguliwa kwa sababu ni mpenda haki. Nilipoangalia kile ambacho amefanya, ninaona anastahiki kuwa raisi wa Somalia. Kama ningeambiwa kumpigia kura mtu, ningempigia kura Gas.

  • Borqor bashiir cali cabdi madoobe
    September 2, 2012 @ 04:47:26AM

    Kwanza, ningependa kutuma heshima zangu kwa Wasomali wote. Ningependa kuwashukuruni sana kwa njia nzuri mliyotayarisha wasifu wa wagombea. Mimi binafsi ninamuunga mkono Farmajo.

  • ilyas ahamed
    September 2, 2012 @ 04:27:41AM

    Amani iwe juu yenu. Wagombea wote ni wananchi lakini wanatofautiana katika vipengele vya uwezo wao na ujuzi wa kupatanisha dunia na kujisalibia. Kwa hivyo, ningewaambia Wasomali kuwapigia kura watu wawili hawa: Profesa Ahmad Samatar au Dr. Badiyow. Mungu atuongoze kwa yule aliye bora zaidi.

  • moh fanah
    September 2, 2012 @ 02:58:55AM

    Mchakato wa kisiasa unaimarika na kwa sasa watu wa Somalia watakuwa na mfumo wa kisiasa ambao daima wamekuwa wakiutaka. Kila mtu ana wajibu wa kuona kuwa mchakato huu unafanikiwa na watu wa Somalia wanakuwa tena na utulivu wa kisiasa baada ya miongo kadhaa ya kutokuwa na utulivu huo. Wanatekeleza na kufanyia marekebisho katiba yao ambalo ni jambo zuri kwa mchakato wa kisiasa.

  • kiinka
    September 1, 2012 @ 01:29:51PM

    Nikitoa maoni yangu, ningempa kura yangu Waziri Mkuu Mohammad Abdullahi Farmajo.

  • mohamed Abdi Hasan Dhaqane
    September 1, 2012 @ 10:32:16AM

    Ripoti hii imetayarishwa vyema. Ninamuunga mkono A/weli Mohammad Ali kwa sababu ni mtu msomi anayejua mengi kuhusu Somalia na ameonesha kazi yake ya haki na uwazi wakati alipokuwa waziri mkuu.

  • Hassan salaad calli AHLU-SHARAF
    September 1, 2012 @ 09:49:42AM

    Ninapenda kutoa heshima zangu kwa wagombea uraisi wote wa Somalia. Mimi kama Hassan, ninamuunga mkono YUSUF GARAD. Ninasema anaweza kufanya kitu kwa sababu alifanya kazi katika serikali na ana uzoefu katika siasa. Tafadhali mpigie kura YUSUF GARAD na muombeeni.

  • jamac ali obsiiye
    September 1, 2012 @ 07:33:24AM

    Shukurani kwa mwandishi wa makala hii. Ningependa kuwaombeni kumchagua Sheikh Sharif kwa sababu amefanya mambo mengi ambayo waliomtangulia hawakuweza kuyafanya na hayataweza kufanywa na wengine wengi baada ya yeye. Ni yeye aliyefanya ugombeaji wa uraisi kufanyika Mogadishu leo jambo ambalo halikufanyika wakati nchi ilipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Alifanya mji mkuu wa nchi yetu kuwa salama. Kwa hivyo ningewashauri kumchagua yeye kwa mara nyengine tena.

  • mohazakir
    September 1, 2012 @ 05:27:20AM

    Kwa kweli ningewahimiza mwachague wanawake badala ya wanaume kwa sababu wanaweza kufanya vizuri zaidi.

  • Asad Yare
    August 31, 2012 @ 04:21:53AM

    Mnaweza kupata Maelezo yao Binafsi sahihi katika Facebook.

  • cumar axmed jaamac
    August 31, 2012 @ 03:21:53AM

    Mimi niko Hargeisa. Mungu anaelewa aliye bora zaidi kwa Wasomali lakini kuna mtu ambaye juhudi na uwezo wake viliwavutia watu wengi na mtu huyo ni Farmajo. Ninamuomba Mungu kuwasaidia Wasomali kuchagua kiongozi bora zaidi. Mimi ni Msomaliland lakini ninataka ndugu zangu wa Somalia wapate mambo mazuri. Ninawaombea kila wakati na kwa kweli huwa ninahisi maumivu ninaposikia kitu fulani kimetokea.

  • cabdikariim.m
    August 30, 2012 @ 03:07:28PM

    Amani kiwe juu enu. Ningependa kusema Prof. Ahmad Ismail Samatar anapaswa kuchaguliwa kwa sababu Wakusini walikuwa wanaitawala nchi kwa miaka 20 iliyopita na hawakufanya chochote muhimu mpaka sasa. Mtu pekee anayeweza kuunganisha Somalia ni Samatar.

  • Dayow
    August 30, 2012 @ 11:48:37AM

    SA, kwa kweli hili ni la kupongezwa kwa vile wananchi wana haki ya kujua aina ya viongozi wanaowachagua. Inashangaza uwezo ambao nchi hii unao katika kipengele cha rasilimali watu na watu wenye elimu lakini kwa huzuni….wanaweza kukubaliana na kuisaidia nchi na watu. Mwenyezi Mungu aijaalie Somalia viongozi wa HAKI.

  • Abdirizak
    August 30, 2012 @ 10:38:47AM

    Tumefurahishwa sana na jinsi mlivyotutayarishia historia fupi ya maisha ya wagombea.

  • maxamed maxamuud
    August 30, 2012 @ 10:01:19AM

    Amani iwe juu yenu. Ninashangazwa na watu hawa ambao maelezo yao binafsi mmeandika na yule ambaye mnataka aiongoze jamii hii iliyoathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na njaa. Hakuna hata mmoja miongoni mwao ambaye ana shahada ya dini. Vipi ataweza kuilinda jamii? Ewe Mungu, tuchagulie kiongozi anayeelewa uwepo wako.

  • WESLEY KIMUTAI BII
    August 30, 2012 @ 09:48:01AM

    KAMA MNATAKA KIONGOZI MWENYE UWEZO WA KUONA MBALI, TAFADHALINI MCHAGUENI DR. ABDIRAHMAN ABDULLAHI BAADIYOW KWA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA SOMALIA. CHOCHOTE ANACHOSEMA ANAKITEKELEZA. UWEZO WAKE WA UONGOZI UMEONESHWA KWA KUKUZA ELIMU AMBAYO NI UFUNGUO WA MAENDELEO NA USTAARABU ULIMWENGUNI.

  • siciid dable
    August 30, 2012 @ 09:28:47AM

    Nadhani unapaswa kutathmini ujuzi kutegemea na kazi ya kufaywa bila ya kujali eneo, kabila au kumpendelea mtu mmoja. Nadhani Prof. Ahmad Ismail Samatar ni mtu mwenye uzoefu zaidi.

  • mustafe Ali hassan
    August 30, 2012 @ 04:23:34AM

    Ninamuunga mkono Yusuf Garad Omar kwa sababu ni mwanasiasa mwenye uzoefu.

  • eng yacquub nuux
    August 30, 2012 @ 04:01:10AM

    Ni nzuri kweli kama watu wasomi leo wanagombania uraisi wa Somalia. Ninamuunga mkono Profesa AHMAD ISMAIL SAMATAR kuwa raisi wa Somalia.

  • fayroor
    August 30, 2012 @ 02:56:13AM

    Ndugu zangu, mpigieni kura mzalendo wa Somalia; Profesa Smatar kutoka mkoa wa Awdal; eneo linalojulikana kwa kuiunganisha Somalia na watu wake ambao ni wazalendo wanaopenda kuisaidia nchi na watu wake.

  • rooble
    August 30, 2012 @ 02:41:29AM

    Ningempigia kura Sharif kwa sababu alihusudu dhamana.

  • sharmal al sheikh
    August 30, 2012 @ 12:57:51AM

    Hakuna yeyote atakayeisaidia Somalia kwa sababu hakuna yeyote, awe awaye, anayefaa kwa uraisi kwa wakati huu. Kila mmoja anataka kujaza pochi lake lisilo kitu alilokimbilia kuja nalo Somalia.

  • hanaan ali obsiiye
    August 29, 2012 @ 10:29:23PM

    Nyote mna mawazo ya kikabila. Wale walioanzisha machafuko nchini Somalia na waliokuwa wapelekwe The HAGUE. Walichaguliwa kwa nguvu kama wabunge ambapo walidai kuwasilisha na baadaye mnatuambia kuwapigia kura fulani na fulani. Nahisi, hakuna jema lolote linalokuja kutokana na mpambano huu lakini waacheni waichukue wakati sisi tunaiunganisha nchi kwa miaka mitano hii. Wanatafuta pesa tu. Angalia hii: Sharif Sakiin alisemekana kutokuwa na elimu lakini hawakuweza kusema kuwa Kanyare ni bwana wa vita. Wanasema Sheikh Sharif anastahiki uraisi lakini yeye ni mmoja wa wale walioiharibu Mogadishu. Hiyo ni sawa? Huo si ukabila? Kwa nini Wasomali wanababaishwa? Hii inahuzunisha kweli.

  • threejayz
    August 29, 2012 @ 08:45:31PM

    Hii ni nzuri. Watu wote hawa wamesoma na wana uwezo wa kuwa raisi lakini ninataka ama Abdiweli au Farmajo kuwa raisi ikiwa Sheikh Sharif atashindwa kupata uraisi. Waliobakia vile vile wanastahili lakini watu watatu hawa ambao tumeona kile walichofanikiwa wanastahiki zaidi kuliko mwengine yeyote yule. Ikiwa tutachagua mtu mpya itatulazimu tumpe muda wa kujizowesha siasa lakini watu hawa tayari wana uzoefu na kile kinachotokea na namna ya kikitatua. Shukrani kwa watu wote wenye akili huru. Na Threejayz Jabka.

  • maxamedqalbinuur
    August 29, 2012 @ 03:29:58PM

    Mimi ni mvulana kijana na mwanafunzi. Kwa kutoa maoni yangu, ninapenda Farmajo awe Raisi kwa sababu aliisaidia nchi na watu wake. Ningependa kumuomba mzazi yeyote anayewatakia hatima nzuri watoto wake kumpigia kura Farmajo. Farmajo. Farmajo. Farmajo. Ninamtakia mafanikio. Mungu awajaalie maadui wako wote washindwe. Ninakuunga mkono kwa sababu ya jinsi ulivyowasaidia ndugu zako Wasomali.

  • askar
    August 29, 2012 @ 01:27:43PM

    Hahahahaha Acha walane wao kwa wao,kama wamekataa kuungana. Somalia haitapata rais bora zaidi ya Siyad Bare, iongozwe na Gedi, Farmajo,au Sharif wawili. Mungu aisadie Somalia. Sikufikiri daima kama Wasomali watalia kwa ajili ya Siyad Bare lakini nimejifunza kuwa alikuwa mzalendo na mbwa aliokuwa akiwatumia kuilinda dhidi yao nchi sasa wamepata fursa.

  • maxamuud xasan cali
    August 29, 2012 @ 12:47:32PM

    Ningempigia kura mtu mwenye busara na uzoefu; Mohammad Abdullahi Mohammad Farmajo.

  • Awaadam
    August 29, 2012 @ 10:25:03AM

    Hahahaha Hawa sio watu wale walioacha dini zao na kuwafuata makafiri walioivamia dini yao? Na huu sasa ni mradi wa makafiri. Tutasubiri uamuzi wa MUNGU.

  • Awaadam
    August 29, 2012 @ 10:22:28AM

    Hili lisiwatie wazimu kwa vile haitatulia daima mpaka Shariah ya MUNGU itekelezwe nchini.

  • muscab haji mohamed
    August 29, 2012 @ 10:11:21AM

    Kwa maoni yangu, ningempigia kura Dr. Mohammad Abdullahi Farmajo. Ninamtakia mafanikio.

  • bulshaaaaawi
    August 29, 2012 @ 09:53:26AM

    Amani iwe juu yenu. Ninapenda kupeleka heshima zangu kwa Wasomali wote. Ninapenda kumshukuru sana mwandishi wa makala hii kwa sababu ametuwezesha kujua mambo mengi kwa uwazi. Kwa uwazi ameonesha ukweli uliopo hasa katika masuala yanayohusiana na elimu. Kama muungaji mkono na mzalendo, ningependa kumpigia kura ama Profesa au yeyote kati ya Madokta wawili; Prof: Ahmed Ismail Samatar au Dr. Mohamed {bashiir} Abdullahi Farmaajo au Dr Abdiweli Ali Gas na ninamuomba Mungu awasaidie Wasomali kumchagua yeyote kati ya watu watatu hawa. Hata hivyo, ningependa Abdiweli kuwa kiongozi wetu kwa sababu amesaidia kwa kweli katika miezi michache aliyokuwa Waziri Mkuu. Naamini anaweza kuitoa nchi hii kutoka tatizo hili. Shukrani kwa watu wote wa Somalia.

  • mohamednoor duweysh
    August 29, 2012 @ 09:26:37AM

    Farmajo anatosha kwa Somalia ikiwa mnafikiria sawa. Ninazungumza juu ya uzalendo. Shukrani kwa wale wote ambao wana busara.

  • Ismael Yare
    August 29, 2012 @ 09:16:21AM

    Mtu amesafiri kwa usalama wake mwenyewe wakati wale wengine walikuwa pamoja nanyi mkijaribu kutatua matatizo. Mungu awasaidieni.

  • SAHRO
    August 29, 2012 @ 08:40:57AM

    AMANI IWE JUU YENU. NINGEMPIGIA KURA BADIYOW KWA SABABU ANA ELIMU.

  • rama
    August 29, 2012 @ 06:49:33AM

    nzuri.nimeipenda

  • farmajo
    August 29, 2012 @ 06:05:31AM

    Zahra Ahmed Hassan Warfa.

  • dhanto
    August 29, 2012 @ 05:52:11AM

    Ninamuomba Mungu ampe uongozi wetu mtu bora zaidi miongoni mwa wagombea. Hata kama mtu ambaye hamuogopi Mungu atadhamiria kuchukua nafasi hiyo, ninamuomba Mungu awarahisishie. Ningependa kuwaambia Wasomali kuwa ukabila ndio uliojenga uadui nchini mwetu na kwa hivyo tumchague mtu ambaye tunadhani ni wa kuaminika, mtenda haki, mzalendo, mwenye uzoefu, aliye wazi na aliyeelimika. Ewe Mungu, tuongoze katika ukweli, awasaidie Wasomali kushinda matatizo yao na kuwa na huruma kwa ya Waislamu wote.

  • SACAD AXMED
    August 29, 2012 @ 02:52:33AM

    SAAD AHMED YASIN, MAELEZO BINAFSI YA WAGOMBEA WA URAIS WALIO NA DHAMIRA ZAIDI WA SOMALIA. SABAHIONLINE.COM – MOZILLA FIREFOX.

  • Sweet Nana
    August 29, 2012 @ 01:30:12AM

    Tunataka mafanikio kwa kila mmoja ambaye katika moyo ana mapenzi kwa nchi yake na wananchi wenzake. Mungu akipenda, tutaishi kwa furaha na amani.

  • mahamuud
    August 28, 2012 @ 05:36:04PM

    Ningependa kumuunga mkono mkuu wa zamani wa BBC Somali; Yusuf Garad Axmed.

  • Abdrizak S. Ibrahim
    August 28, 2012 @ 03:12:43PM

    Kwa kweli ninathamini MAELEZO BINAFSI ya viongozi lakini ninamuunga mkono kikamilifu FARMAJO kwa sababu ameotuonesha harufu ya serikali. Ninaliomba bunge jipya lisipige kura tu bali lipige kura kwa busara.

  • fu.aad
    August 28, 2012 @ 01:45:27PM

    Kwa marafiki zangu wote, rais ni Ahmad Ismail Samatar.

  • MUSTAPHA DHEREEYE
    August 28, 2012 @ 11:30:28AM

    NINAPENDA AMANI ITAWALE SOMALIA YOTE.

  • mudug boy
    August 28, 2012 @ 08:27:43AM

    Amani iwe juu ya wote wale waliotoa maoni yao. Pili, Ni Sharif wawili au Abdiwelli na Farmajo? Sharif wawili sio wazuri wala hawafai kugombea ingawa Sharif ambaye sasa ni raisi anayeondoka ni bora zaidi. Lakini Sharif mwengine hana chochote cha kufanya bungeni na hatafanya chochote kwa watu na nchi. Achilia mbali kumteua kwa ajili ya nafsi hii, ninaweza kuwambieni kuwa haaminiki. Abdiweli Mohammed Gaas ana akili za kikabila na ukabila na ndio lililoifanya Somalia kuwa kama ilivyo leo. Hatutaki kiongozi mwenye akili za kikabila na lazima ukabila tuung’oe. Mwisho, Farmajo ni mtu alielimika anayependa kuisaida nchi na watu wake na ushahidi ni mafanikio aliyopata miezi michache ambayo alikuwa Waziri Mkuu. Kwake yeye uzalendo ni kuzaliwa nao na sio kwa sababu ya kiga; kwa hivyo ningewaombeni kumpigia kura Farmajo ikiwa sisi ni wazalendo na tunataka mtu wa kututoa kutoka hali ya ukimbizi. Mpigieni kura Abdiwedi Gaas kama mnataka ukabila. Mpigieni kura Sheikh Sharif wa bunge ikiwa mnataka mwizi. Mpigieni kura Sheikh ikiwa mnataka kumfanya awe mbunge.

  • cumar yusuf
    August 28, 2012 @ 08:14:32AM

    Makala hii sio sahihi kwa sababu haioneshi mambo mengi ambayo yalitarajiwa kuandikwa kuhusu mgombea kama Dr. Badiyow. Haikuandikwa mengi kumhusu yeye. Anazungumza Kiarabu, Kiingereza na Kisomali. Pia, Sharif Hassan anazungumza Kiingereza, Kisomali na Kiarabu lakini hamkuandika. Haya ndiyo baadhi ya makosa niliyoyaona katika makala yenu. Iandikeni tena makala hii.

  • Ahmed Omar shine
    August 28, 2012 @ 08:11:39AM

    Ninawaamkieni. Mimi ni mmoja wa wasomaji wa kurasa hizi. Ningependa muelewe kuwa, kama binadamu mumemsahau Dr. Abdullahi Ahmad Adow kama mmoja wa wagombea wenye dhamira miongoni mwa wagombea. Vivyo hivyo, mumesahau kuandika habari kuhusu mfanya biashara ambaye hana elimu. Ahmed Omar Shine, Nairobi Kenya.

  • Aliis yusuf
    August 28, 2012 @ 07:52:16AM

    Amani iwe juu yenu. Ningependa kutoa shukrani zangu kwa Wasomali wote popote walipo. Ningependa kuwaomba muungane na kumuunga mkono mgombea ambaye siasa zake zinazhusu amani na maendeleo. Ningependa mfahamu yale aliyofanya katika mji wa Mogadishu katika miezi sita iliyopita. Mhe. Sheikh Sharif hajawahi kunigawia chochote lakini ninataka achaguliwe tena, Mungu akipenda. Ninamuomba Mungu kwa kuchaguliwa kwake tena kwa sababu yeye ni mzalendo anayeipenda Somalia. Umewahi kumwona Raisi anayewasaidia masikini yeye mwenywe? Somalia itaangamia ikiwa itatawaliwa na mtu mpya. Mungu ampe uongozi wetu Raisi Sheikh Sharif Sheikh Ahmed kwa sababu ni kiongozi tu. Mungu ampe uongozi wetu Raisi Sheikh Sharif mara zote kwa sababu tunakuabudu milele? Ninamuomba Mungu atulinde dhidi ya watu ambao waliuza au kusaini ili kukatisha mwendo katika pwani ya Kusini na kuwa mbunge au askari katika nchi yetu na nchi kuifanya jangwa. Mungu ajalie awapunguzie umri wa kuishi wale walioiuza nchi yao au kufuata amri kutoka nchi nyengine. Amani iwe juu yenu. Naomba mnisahihishe kwa vile uandishi wangu ni mbaya, mabibi na mabwana.

  • Omr Mohamed
    August 28, 2012 @ 05:26:59AM

    Hii makala ni nzuri sana kwa vile inatuwezesha kujua hasa nani tunayeshughulika naye. Hongera kwa kugawana nasi habari hii yenye thamani sana. Baada ya kujua kila moja na tabia zao basi tunaweza kufikia hatimisho juu ya uongozi unaohitajika pamoja na uzoefu na mtu kwa ajili ya kazi hiyo anaweza kutambulika kirahisi.

  • abdiaziz
    August 28, 2012 @ 05:18:41AM

    Ni rahisi kuvunja kuliko kutengeneza. Ndugu zangu tunajua na tumeona kwa macho yetu nani anaweza kuifanya nchi yetu ya Somalia kuwa na amani, nani mwengine zaidi ya Mohamed Abdullahi Farmajo na tafadhalini. Na tafadhalini ninawaomba kama wabunge msipokee hongo.

  • xassan aden lodon
    August 28, 2012 @ 04:27:58AM

    Amani iwe juu yenu. Mungu atuongoze sana kwa vile Yeye anajua ukweli lakini mtu ambaye hajafanya uhalifu dhidi ya nchi na watu wake tokea miaka ya 60 na ambaye anawapenda Wasomali popote walipo ni Prof Samatar. Wengi wa wagombea wengine pia sio wabaya pia. Ni hayo tu. Kwaherini!

  • abubakar mohamed
    August 28, 2012 @ 04:15:03AM

    Ijapokuwa wagombea uraisi wana uwezo, mtu pekee ninayedhani anaweza kuleta maadiliko ya maana ni MOHAMED FARMAJO kwa sababu ni mtu ambaye uwezo wake wa kuleta mabadiliko ulionekana kwa kipindi kifupi wakati alipokuwa Waziri Mkuu. Kwa hivyo tunapaswa kumuunga mkono na kumpigia kura.

  • Ali
    August 28, 2012 @ 02:50:43AM

    Kwa ajili ya Somalia iliyo ungana, mchague Samatar. Ewe Mwenyezi Mungu, tuunganishe.

  • Seefta-banaanka
    August 28, 2012 @ 12:54:50AM

    Ndugu zangu, ikiwa mtoto wa Samatar haungwi mkono na jamii yake, basi hawezi kutuongoza hapa Mogadishu. Anapaswa kutafuta ukoo wake wa Isack.

  • ca
    August 27, 2012 @ 12:27:24PM

    Mtu ambaye atafanyakazi kwa maslahi ya Somalia anapaswa kuchaguliwa. Uongozi lazima upewe mtu mpya na Somalia sasa inafanikiwa kutoka katika uongozi wa mpito kwa hivyo inahitaji kiongozi mzuri anayejali nchi na dini.

  • kinuthia
    August 27, 2012 @ 09:39:06AM

    Furahieni amani, enyi Wasomali. Mafanikio daima.

  • maxamed shirey
    August 27, 2012 @ 08:53:24AM

    Ningependa kutuma heshima zangu kwa wagombea wote wa uraisi wa Somalia. Ningependa kumpigia kura mtu mmoja tu anayetaka kufanya kazi kwa manufaa ya watu na nchi na mtu huyu ni Mohammad Abdullahi Farmajo. Amani iwe juu yenu. Kwa heri.

  • dr muhamed hassan hagaa
    August 27, 2012 @ 07:30:18AM

    Amani iwe juu yenu. Ninamuunga mkono Prof. Ahmad Ismail Samatar. Mungu amsaidie kushinda. Amin. Binadamu hawana uwezo wa kuchagua bali Mungu ndiye anayechagua. Mungu amjaalie ashinde.

  • Shukri Ibrahim Hashi
    August 27, 2012 @ 06:04:47AM

    Kwa kweli, ninamuomba Mungu kumsaidia yeyote ambaye anajali kuhusu maslahi ya Wasomali. Nikiangalia kwa undani wagombea ningempa uraisi Yusuf Garad kwa sababu ya uzoefu wake kuhusu masuala ya Somalia kitaifa na kimataifa. Ni maarufu na si mtu mwenye mawazo ya kikabila. Huyu ndiye mtu pekee mwenye sifa tunazotaka kama Wasomali.

  • boqor...axmed
    August 27, 2012 @ 05:36:10AM

    Mmeandika maelezo mazuri binafsi ya wale waliowapeni pesa lakini hamkuandika chochote kwa wengine waliobakia. Ndio nini hiyo? Pili, mmetumia majina yao ya ukoo kama makafiri. Ndio nini hiyo?

  • Abdullaahi
    August 27, 2012 @ 02:58:08AM

    Sharif Hassan hana usuli wa elimu. Nani anaweza kutuelezea kwa nini? Nadhani mambo mengi yanaweza kubadilika ikiwa tutampa uongozi yeyote kati ya wafuatao: Baadiyow, Ahmed Said, Farmaajo au Yusuf Garad, kwa sababu kila mmoja wao ana ujuzi wake, uzoefu na uwezo wa kuongoza.

  • bashir abdillahi skeikh ibrahim
    August 26, 2012 @ 06:34:51PM

    Ninamuunga mkono sana Ahmed Ismail Samatar kuwa raisi nikiweka uungaji mkono wangu katika maelezo yake binafsi na uwezo wake wa kufanya kitu kwa ajili ya nchi hii na watu wake. Ningependa yeye awe raisi wa Somalia. Pili, naamini kuwa anaweza kufanya chochote kuhusu matatizo kama vile vita vya kisiasa, uporaji, mauaji, kutengana, udungu, ukabila, kujipendekeza na tatizo la watu waliokimbia makazi yao nchini Somalia na anaweza kulilinda eneo letu kutovamiwa na wageni kama vile Ethiopia, Kenya na wengine wengi. Mwenyezi Mungu ampe ushindi. Amin.

  • abubakar
    August 26, 2012 @ 01:49:11PM

    Watu wote hawa ambao maelezo yao binafsi yameandikwa katika makala hii ni watu muhimu ambao wana uwezo wa kuongoza. Naamini kuwa kila mmoja kati yao anaweza kutimiza wajibu wake kwa ufanisi. Ninamuomba Mungu kutuchagulia aliye bora zaidi miongoni mwao. AMIN.

  • yaasiin
    August 26, 2012 @ 12:54:27PM

    Kwa maoni yangu, Prof. Samatar anapaswa kuchaguliwa kuwa raisi kwa sababu ni mtu mwenye uzoefu ambaye uwezo na dira yake inajulikana na wote. Anatoka eneo la Kaskazini, hasa eneo la Awdal la Somalia na anatokana na ukoo pekee ulio safi katika uhalifu wa kisiasa, Ningependa kuwashauri mumchague Prof. Samatar kama mna matumaini na Somalia kwa sababu ni mtu pekee anayeweza kuongoza kuelekea amani, umoja, maendeleo ya kiuchumi na mafanikio katika elimu, Asanteni.

  • حسين عبد يوسف
    August 26, 2012 @ 11:13:54AM

    Tungependa kwamba Profesa Abdirahman Muallem Abdullahi (Baidoa) ashinde urais ili kuwapa nafasi wasomi kufanya kazi, kutumikia na kuiongoza nchi yao; wakati umefika wafanye hivyo. Nafasi ya mabwana wa vita imeshamalizika.

  • Ahmed-nuur Osman Daahir
    August 26, 2012 @ 10:37:51AM

    A.S.C? JENGINE NI KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU NA BAADAYE WAANDISHI WA HABARI WA SABAHIONLINE. KWA KWELI MMETUPATIA KILE TULICHOKUWA TUNATAKA KUJUA KUHUSU WAGOMBEA WA URAIS SOMALIA. MUNGU NDIYE ANAYEJUA NI NANI KWELI ANAFAA KWA NAFASI HII YA JUU. LAKINI KAMA MIMI NI MMOJA WA WAPIGA KURA KATIKA BUNGE NINGEMPIGIA KURA PROF. AHMED ISMAEL SAMATAR KWA VILE NI MWENYE KUONA MBALI NA MZALENDO MWELIMISHAJI.

  • Nuurdiin Cali Maxamed (Nuur Cade)
    August 26, 2012 @ 08:16:52AM

    Jina langu ni Nurdin Ali Mohamed. Ninaishi Mogadishu na ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Somalia. kwa maoni yangu urais angepewa Mohamed Abdullahi Mohamed (Farmajo) ambaye ni mgombea anayependwa zaidi na Wasomali. Ninaamini kuwa Bw. Farmajo anaweza kufanya kitu kuhusu matatizo sugu ya Somalia, Mungu akipenda na anaweza kurejesha utukufu wa Mogadishu uliokuwa unajulikana, ikiwa Mungu ataamua hivyo.

  • Caaqilsomali
    August 26, 2012 @ 05:41:17AM

    Naamini zama mpya imefika Somalia,,,,Dada na kaka zangu wa Somalia tafadhali acheni ukabila na kumchagua Profesa Abdi Ismael Samatar. Anaweza kufanya mengi zaidi.

  • mohamad maalim hasan
    August 26, 2012 @ 05:14:13AM

    Wezi hao wanapaswa kufukuzwa na uongozi mzuri ulioko Kismayu kuhamishiwa Mogadishu ikiwa mnataka amani kwa ajili ya Somalia. Haya ni mawazo yagu na lazima yachukuliwe. Amani iwe juu yenu.

  • c/laahi
    August 26, 2012 @ 05:08:55AM

    Ninaanza kwa jina la Mungu. Ningependa kutoa heshima zangu kwa wasomaji na waandishi wa makala hii. Wakati ninasoma maelezo binafasi ya wagombea walioandikwa katika makala hii, nigependa kuwaombeni kumpigia kura Prof. Gaas, waziri mkuu wa sasa kwa sababu ana kumbukumbu nzuri za mafanikio kuliko mgombea mwengine yeyote. Aliikomboa nchi kwa mwaka mmoja na ikiwa tutampa uongozi kwa miaka kadhaa hakuna shaka atafanya mengi. Simsifu lakini ninasema ukweli unaojulikana na Wasomali wote kuhusu yeye. Mhe. Waziri Mkuu, ninakutakia ushindi na utashinda, kwa mapenzi ya Mungu. Asanteni nyote. Ninasema ninakutakia heri Pro. A/wali Mohamed Ali Gaas.

  • mohamad maalim hasan
    August 26, 2012 @ 04:46:09AM

    Je, watu hawa wanastahiki nafasi wanazogombania? Wote wangepaswa kufukuzwa na kuitwa kwa viongozi wa Kiislamu.

  • AXMED AADAN MOHAMED
    August 26, 2012 @ 04:17:34AM

    Ningependa kuwaambia wabunge wasiwachague watu wanaowajua; kama rais wa sasa na Waziri Mkuu [Gaas].Ningependa kuwaomba Wasomali kumchagua Mohamed Abdullahi Farmajo ambaye ni mtu shujaa wa Somalia.

  • axmed m keke
    August 26, 2012 @ 01:49:34AM

    Amani iwe juu yenu. Kama ningekuwa mpiga kura leo ningempigia kura Mohamed Abdullahi Farmajo kama rais kwa sababu ya aliyowafanyia Wasomali wakati alipokuwa Waziri Mkuu.

  • Farah
    August 26, 2012 @ 01:37:08AM

    Nisingempigia kura yeyote kati ya watu hawa kwa sababu hakuna hata mmoja kati yao anayestahiki nafasi wanazogombania.

  • Yusuf Bashir Caliyow
    August 26, 2012 @ 12:12:46AM

    Inavunja moyo kweli kwa sababu mtu aliyezungumza vibaya kuhusu Sheikh Sharif ni Habar Gidir na adui mwengine yoyote. Nina hakika yeye ni bora zaidi mara 1000 kuliko Hassan Dahir. Nyinyi habar Gidir mumechanganyikiwa na msiingie motoni kwa sababu ya chuki mnazojenga dhidi ya Abgaal.

  • asma sh mahomed
    August 25, 2012 @ 03:12:02PM

    Ahmed Ismail Samatar ni mtu mwenye uzoefu. Sio tu ana uzoefu bali ni mtu wa nyanja zote. Mwacheni aiongoze serikali ya Somalia.

  • shiine
    August 25, 2012 @ 05:12:47AM

    Si makala sahihi kwa sababu inasema Prof. Ahmad Ismail Samatar anatoka mkoa wa Kaskazini, ambapo wengine wote wanatoka katika maeneo mengine. Inajaribu kujenga picha ya kaskazini kuwa ni sawa na Banadir. Bado wanaendelea kulidharau eneo la Kaskazini. Kwa kuhitimisha, ningependa kuwahimiza mumpigie kura Prof. Ahmad Ismail Samatar.

  • Dr.Abdullah daher
    August 25, 2012 @ 05:06:59AM

    Tafadhali piga kura kwa Prof. Ahmad Ismail Samatar kwa vile anaweza kuiongoza nchi na watu wake.

  • liban
    August 25, 2012 @ 04:30:33AM

    Ni makala nzuri ambayo inaweza kuwasaidia Wasomali. Kwa maoni yangu, Wasomali wanapaswa kuongozwa na Dr. Bariyow kwa sababu ni mtu aliyesoma sana anayejua kile Wasomali wanataka na ambaye amefanya mengi kwa ajili ya Wasomali. Ninamuomba Mungu amuibue mshindi. AMIN.

  • khadar
    August 25, 2012 @ 03:35:10AM

    Somalia itaanza maisha na matumaini mapya. Tulikuwa tunasubiri muda mrefu wakati huu. Ninamuomba Mungu kuifanya ndoto hii kuwa ya kweli. Ninamuunga mkono YUSUF GAARAD OMAR; ni kiongozi mzuri.

  • cabdi kariim
    August 25, 2012 @ 03:23:13AM

    Sisi kama watu wa Somaliland tunamuunga mkono Mohammed Abdullah kama tuna haki ya kueleza maoni yetu.

  • Abu Mohamed
    August 25, 2012 @ 01:23:33AM

    Somalia inaweza kuongozwa na mtu ambaye alikuwa hajishirikishi na siasa za kikabila ambazo zilikuwa zikiendelea nchini kwa miaka 20 iliyopita.

  • Mohamed
    August 25, 2012 @ 12:50:40AM

    Ningependa kuwaambia Wasomali kuwa kura zenu hazitafika kule mlikotarajia kwa sababu wapiga kura watachaguliwa na MAHIGA na WAZEE wa Somalia ambao hawataangalia kwenye uteuzi wao juu ya ELIMU na UWEZO. Ningependa kuomba msubiri mpaka mtakapoweza kupiga kura nyinyi wenyewe kwa mtu mnayemtaka. Mungu atuongoze katika njia iliyonyooka.

  • ABDIRIZAK S. IBRAHIM
    August 24, 2012 @ 05:25:36PM

    Farmajo anastahili kuiongoza Somalia. Ametuonesha mengi. FARMAJO AWE RAISI.

  • xaaji mire
    August 24, 2012 @ 04:53:05PM

    Nililipoangalia maelezo yao binafsi na namna yao ya uongozi, niliamua kuwaombeni mumchague Sheikh Sharif Sheikh Ahmad ambaye ninaweza kusema amefanya mengi muhimu nchini Somalia baada ya kuwa rais na kabla ya hapo wakati alipokuwa ndani ya Umoja wa Mahakama za Kiislamu.

  • shire
    August 24, 2012 @ 04:42:33PM

    Amani iwe juu yenu. Asanteni kwa kutoa maoni yenu wapendwa wasomaji. Ningependa kuwashukuru waandishi wa habari waliotayarisha makala hii. Baada ya hayo, ningependa kumwambia rafiki yangu Abdi Sahal Ale kutubu kwa kumuambia Muislamu ghadhabu za Mungu ziwe juu yake jambo ambalo ni dhambi kweli. Huwezi kuandaa maelezo mazuri ya kielimu ya Sharif Hassan na maelezo ya kielimu ya kila mtu yalioneshwa, yawe marefu au mafupi. Kuanzia wakati Sharif Hassan alipoteuliwa mpaka wakati huu, sijawahi kuona mahali popote maelezo ya elimu yake yameandikwa. Ikiwa unataka kutumia silaha kuwalazimisha watu kuandaa maelezo ya elimu kwa ajili ya Sharif Hassan basi samahani kwani wazo hilo wakati wake umepitwa. Kama nitaongea juu ya wagombea hawa ningependa kumuomba Mungu kumchagua aliye bora zaidi kwetu kwa vile Yeye anamjua aliye bora zaidi miongoni mwa wagombea. Ikiwa elimu inaweza kupatikana kupitia chuo kikuu, watu wengi wameipata lakini linapokuja suala la mafanikio mgombea mwenye nafasi zaidi miongoni mwa Wasomali, awe kijana au mzee, popote walipo, ni Farmajo kwa sababu tunaangalia mafanikio yake. Hakupata kuungwa mkono na watu kwa sababu ya kumbukumbu za mafanikio yake bali kwa kitu chengine chochote. Ikiwa kuna mtu aliye bora zaidi tunamuomba Mungu basi atuchagulie, na tumuombe Mungu asituchagulie kiongozi mbaya. Mungu anisahihishe pale nilipokosea. ASANTENI.

  • umu sudais
    August 24, 2012 @ 02:34:15PM

    Amani iwe juu yenu. Ikiwa watu wanaweza kupiga kura basi Mungu awaongoze kupiga kura. Ni vyema kwetu kumchagua kiongozi anayestahiki ABDI RAHMAN BAADIYO. Ninakutakia ushindi.

  • khalid
    August 24, 2012 @ 01:56:58PM

    NINAMUUNGA MKONO MOHAMED ABDULLAHI FARMAAJO KWA SABABU NI MTU SHUPAVU. MWENYEZI MUNGU AKUIBUE MSHINDI.

  • Mire
    August 24, 2012 @ 01:00:50PM

    Naam. Tunapaswa kuweka mtazamo wetu katika hisia za ukoo lakini jambo muhimu ni uzalendo. Wakati umefika kwa Wasomali wote lazima wawe na rais mmoja bila ya kujali anatoka kabila gani. Taifa hili LINAHITAJI kiongozi mzalendo ambaye atawaongoza Wasomali wa makabila yote. Farmaajo alipata msaada wa Wasomali duniani kote hata baadhi yao walikuwaa makaburini kutokana na msaada waliomwonyesha. Kumbukeni kuwa Farmaajo alikuwa ni kiongozi pekee ambaye hakuitembelea Ethiopia wakati alipokuwa katika ofisi ya waziri mkuu wa Somalia. Anaamini Utawala Bora unaweza kupatikana tu kwa njia ya kuwa mzalendo kwa taifa lako na ndio maana alitimuliwa ofisini na mataifa ya nje. Ningependa Farmaajo achaguliwe kuwa raisi. Daima huwa nafikiria mipaka kuwa wakati yetu itakapokuwa salama kutokana na uvamizi wa Afrika, tutafikiria kujenga Jeshi Letu la Taifa letu. Farmajo alikuwa kiongozi wa kwanza wa Somalia aliyepanga mishahara Jeshi na sekta nyingine za serikali. Tafadhali, mfanyeni Farmajo kuwa rais wa Somalia yetu tunayoipenda. Ni wakati bora kwa ajili ya Somalia kwa sababu Melez ameshakufa, shetani yule aliyekuwa akichochea matatizo yetu. Kila la heri.

  • Roble
    August 24, 2012 @ 12:22:21PM

    Dr. Abdulkassim Salat anapaswa kuchaguliwa kama rais na Farmajo kama Waziri Mkuu. Waliobakia wanapaswa kupewa nafasi nyengine. Nadhani Mahiga anajua nyumbani kwake iko wapi.

  • Samatar
    August 24, 2012 @ 09:29:26AM

    Wengi wa wagombea hawa ni watu wa aina tunayohitaji lakini nataka kusema jambo moja kutoka hapa na mnaweza kuandika kutoka kwangu, Mungu akipenda. Mtu ambaye alikuwa mkuu wa chuo kikuu atakuwa raisi wa Somalia. Sharif atafadhaishwa na ulimwengu. Nina siri kubwa sana ambayo siwezi kuisema sasa.

  • mustapha
    August 24, 2012 @ 08:27:03AM

    Kazi nzuri iliyofanywa ya maoni mengi ya watu tofauti kutoka sehemu tofauti za dunia. Tunamshukuru na kumuomba MWENYEZI MUNGU ili kuiona Somalia kubwa zaidi kama ambavyo ilipaswa iwe. MWENYEZI MUNGU aifanye Somali kuwa ya amani. Maoni yangu kwa mgombea wa uraisi wa Somalia ni mtu mmoja tu na huyu ni Mohamed Farmajo, mtu pekee anayeangalia maslahi ya taifa la Somalia, msafi na mfanyakazi kwa bidii, waliobakia wanatafuta maslahi yao tu. Ninawaomba wabunge wamchague Farmajo.

  • zakaria
    August 24, 2012 @ 07:41:27AM

    Watu wawili: 1 - Yusuf Garaad Omar 2 - Ahmad Ismail Samatar.

  • salman Ali
    August 24, 2012 @ 04:47:08AM

    Nadhani tunahitaji kufuata hekima zilizoandikwa na raisi wa kwanza wa Kenya ambapo alisema (Kenya haina haja ya mtu na magazeti matupu. Leo nimemechukua na kuokoa mengi kadiri ninavyoweza. Nimeweka akiba ya kutosha ya kula maisha yangu yote lakini Kenya inahitaji) alichaguliwa tena na yeye ambaye aliyefanya Kenya kuwa kama ilivyo leo. Ningependa kuwahimiza mumchague Sheikh Sharif leo kwa sababu nyingi. Sitoki katika kabila moja, mkoa, wala chama kimoja na yeye, lakini ninatoa maoni yangu kama mtu wa Somalia. Namuomba Mungu kutusaidia katika kuchagua. Ni juu yenu na utu wenu kuchagua!!!

  • adan irad
    August 24, 2012 @ 02:58:45AM

    Asante kwa kutupa wasifu wa ndugu zetu. Swali linalonijia akilini mwangu kila mara ni, lini tutaondokana na ukabila, wakati wenzetu waliosoma wanahiari kabila kuliko SIFA? Mimi kama Msomali, ndugu wa Wasomali wote, ningependekeza kuwa tusielekeze akili zetu wakati huu bali tufikirie nyuma na mbele yetu. Ikiwa nitawakumbusheni mwaka jana, je mlihisi vipi kama binadamu wakati mlipowaona watoto, wanawake na wazee wamelala maiti barabarani? Si suala la kucheka. Kwa wale waliokuwa katika makambi wanaelewa hasa. Nchi hii ni yenu na inaweza kututosheleza kikamilifu. Kwa wagombea, leo ni zamu yenu, na kesho mtawajibishwa kwayo, kwa umoja wa nchi yetu. Iacheni sheria itawale, kwani heshima, nguvu na utukufu ni wa Mwenyezi Mungu, Mitume wake na waumini. Asanteni kwa maoni mazuri.

  • DALMAR
    August 24, 2012 @ 02:37:25AM

    KWA HAKIKA WOTE WAMEONESHA KAZI YA BIDII KATIKA MASOMO YAO LAKINI HIYO HAIFAI KITU. AKILI ZAO HAZIONESHI MAELEZO YAO KWA SABABU WOTE NI WAFUASI WA UKABILA. 1 - LUGHA YA ABGAAL INAZUNGUMZWA KATIKA MAKAAZI YA RAIS. 2. LUGHA YA RAHANWEYN-INASEMWA BUNGENI. 3 – UKIENDA NYUMBANI KWA ABIWELI UTADHANI UKO GALKAYO. TATIZO HILI LINAHITAJI KUTATULIWA.

  • jaamac axmed wali
    August 23, 2012 @ 05:41:18PM

    Ndugu zangu, ningependa kusema kuwa siyo vibaya kwa mtu yeyote kutuongoza lakini vipi ataweza kuwaongoza watu na nchi? Je, ataongoza kwa kufuata demokrasia au Sharia ya Kiislamu? Mcheni Mungu kwa vile mtawajibika kwa kila mlifanyalo katika dunia hii mbele ya Mungu. Si jambo nzuri kugombea uongozi. Kuweni makini na suala hili.

  • sudeis abdulkhadir
    August 23, 2012 @ 04:38:20PM

    Amani iwe juu yenu. Asante kwa kutuonyesha habari ya watu hawa. Kama mtu ambaye ana mapenzi kwa Wasomali moyoni bila kujali ukabila, ningependa kuwahimiza kumchagua Muhammad Abdullahi Farmajo. Mimi nitapiga kura kwa ajili yake kama mgombea anayependwa zaidi na Wasomali. Amani iwe juu yenu.

  • Abuu Cali
    August 23, 2012 @ 03:47:35PM

    Nadhani Wasomali sasa wamechoshwa na kutoa nafasi kama ya waziri mkuu na uraisi kwa makabila mawili makubwa; Hawiye na Darood ili kuwaridhisha wao kwa kuwa mkakati huu ulishindwa kuleta utulivu wa kisiasa na kuundwa kwa serikali ya nguvu ya kutatua matatizo yanayoikabili nchi na watu wake. Tunapaswa kuiga ufumbuzi uliotumiwa na Somaliland baada ya kifo cha Rais Ibrahim Igali ambapo urais alipewa Ina Riyale aliyetoka ukoo wa wachache ili kuzuia migogoro kati ya makabila makubwa na hivyo kuiongoza Somaliland hadi kufikia mabadilishano ya kisiasa kwa amani. Aidha, tunaweza kuiga chama tawala cha Ethiopia ambacho kimechagua naibu waziri mkuu kutoka ukoo wa wachache, ambaye anaweza kuiongoza nchi kwa amani katika kipindi cha mpito kutokana na kifo cha waziri mkuu kama tunavyoweza kuona leo. Kwa hivyo, Sharif Hassan anafaa kupewa fursa hii ili kutatua matatizo katika nchi yetu leo? Nadhani yeye ataongoza vizuri zaidi kwa sababu atakuwa haungwi mkono na kabila lolote na hivyo kuwa hapendelei upande wowote. Atakuwa na uwezo wa kuitetea nchi yetu bila ya kuburudisha itikadi za kikabila.

  • siciid jirde
    August 23, 2012 @ 02:58:42PM

    Nadhani huu ni wakati muafaka kwa Wasomali kuweka kando ukabila, migogoro, na kuoneshana vidole na badala yake kushughulika na ujenzi wa amani, utulivu na kuunda serikali ya kitaifa yenye nguvu. Ningependa kumuomba mgombea yoyote ambaye anataka kufanya kazi kwa maslahi ya Wasomali bila kujali ukabila kuchukua urais. Ningependa kuiambia Jamhuri ya Kusini ya Somalia kuwa umefika wakati wa kuitambua Jamhuri ya Somaliland baada ya kukamilisha masuala yenu. Ni bora zaidi kila mmoja kuwa huru kuliko jinsi mambo yalivyo sasa baina ya Kusini na Jamhuri ya Somalia. Asante.

  • abdeeq maxamed abyan
    August 23, 2012 @ 02:43:25PM

    Kwa maoni yangu, nadhani Sheikh Sharif anafaa kuchaguliwa tena kwa sababu yeye anaijua dunia.

  • mohamed bashiir
    August 23, 2012 @ 02:36:39PM

    Ningependa kusema kuwa Farmajo anaweza kubadili mambo mengi nchini Somalia iwapo atachaguliwa. Ningependa kupendekeza achaguliwe yeye.

  • ibraahim
    August 23, 2012 @ 02:07:10PM

    Ningependa kumchagua Ahmad Ismail Samatar kwa sababu yeye ni mtu mwenye busara anayeweza kuiunganisha Somalia lakini Mungu anajua ni nani bora zaidi wa kutuongoza.

  • maxamed mursal sulub
    August 23, 2012 @ 01:14:25PM

    Kwa hakika, nadhani watu hao ambao wanagombea urais wa Somalia kama vile Profesa Samatar na Prof Farmajo ni wenye elimu. Wawili hawa ni watu wakubwa. Tunamuomba Mungu amsaidie yeyote kati ya wawili hawa kushinda urais ili kutuongoza.

  • abdulkadir ahmed
    August 23, 2012 @ 12:54:12PM

    Amani iwe juu yenu. Hebu tusisite kuhusu nani wa kumchagua. Mtu pekee mwenye ujuzi, uzoefu na mipango mizuri ya kuongoza ambaye anaweza kuiokoa nchi kutoka machafuko kwa msaada wa Mungu, ni PROF AHMED ISMAIL SAMATAR. Naomba Mungu atusaidie kumchagua yeye kama raisi wetu, Mungu akipenda.

  • Adam
    August 23, 2012 @ 12:28:46PM

    Ningependa tuipe kipaumbele jinsi mtu alivyo safi kutokana na ukabila, rushwa na undugu kabla ya kumpigia kura mgombea kutoka wagombea kadhaa wa rais. Kama tutamchagua mtu ambaye ana mapenzi kwa Wasomali katika moyo, yeye pengine atakuwa mtu ataikomboa nchi yetu ambayo imekuwa ikikabiliwa na kutokuwa na sheria na maafa pamoja na kuwa makazi ya ugaidi.

  • A Gurey
    August 23, 2012 @ 10:50:21AM

    Tunawashukuru sana kwa njia nzuri ambayo mmetayarish makala hii. Hili linahitajika kweli ili jamii ifahamishwe.

  • cabdulkadir
    August 23, 2012 @ 10:47:07AM

    Hiyo ni nzuri. Tunataka kuimarisha amani na utulivu tulioupata kwa msaada wa Sheikh Sharif Sheikh Ahmad (Mungu amuhifadhi). Tumuombee kama jinsi tunavyomuombea pia. Tumepata uhuru sasa. Tumshukuru Mungu. Tulinganishe kile tulichopitia na tulipo sasa.

  • axmed adan maxamed
    August 23, 2012 @ 10:21:35AM

    Amani iwe juu yenu. Kwanza, napenda kutuma salamu zangu kwa Wasomali wote popote pale walipo. Kama nitatoa maoni yangu juu ya makala hii muhimu inayoonyesha habari za ya wagombea wa urais wa Somalia, naweza kusema ni wawili tu kati ya wagombea urais hao wanaostahili hoja yangu ikiwa kwenye sifa zao kisiasa na kielimu. Hawa wagombea wawili ninaosema wanastahili uraisi ni; Sharif na Farmajo. Somalia haina haja ya mtu ambaye leo anaanza kazi yake ile aliyoiacha mwaka 2007 lakini inahitaji mtu kuendelea kutoka hapa ambapo tupo wakati huu. Wagombea wawili hawa ninaopendekeza wanajua vizuri sana kuhusu siasa ya kisasa ya Somalia. Hasa ninampendekeza rais wa sasa; Sheikh Sharif Sheikh Ahmad kwa urais. Ningependa kuwaomba Wasomali wasiruhusu watu wasio na elimu kutuongoza. Pia tunapaswa kujifunza kuachaa urais kwa mtu mwingine kwa sababu kuwa na njaa ya utawala kwa gharama ya mafanikio hakutatusaidia tena, lakini Usomali utatusaidia.

  • prof omar hassan osman
    August 23, 2012 @ 10:01:48AM

    Yussuf Garaad Omar awe rais, kwa kweli anastahiki kuchaguliwa. Ni mtu mwenye uzoefu na anapenda kupiga vita ufisadi pamoja na ubaguzi wa rangi. Sote tumpigie kura Yussuf Garaad Omar

  • abdulkadir hassan warsame
    August 23, 2012 @ 09:38:25AM

    Hukuandika ukweli kuhusu maelezo ya maisha ya Sheikh Sharif. Alipelekwa masomoni mwaka 1992 na makamu wa raisi Salbalaar Hilowle Iman Omar. Hakuweza kuendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Khartoum na kwenda Libya baadaye ambako alijifunza itikadi za Libya, Kitabu cha Kijani. Kuweni na tahadhari na hilo.

  • Moslim Ahmed Kan
    August 23, 2012 @ 06:31:37AM

    Ninaanza kwa jina la Mwenyezi Mungu. Sifa zote ziwe juu yake. Amani na baraka za Mungu ziende kwa Mtume wetu Mohammad. Baada ya hayo, Mungu ajaalie ghadhabu zake zimwendee Ibilisi. Kama nitazungumzia kuhusu ugombea wa uraisi, ni Mungu tu anayejua atakayekuwa raisi wa Somalia, lakini hakuna shaka kuwa hatuwezi kumchagua mtu tunayetaka sisi kama Wasomali kwa sababu tunapangiwa. Ikiwa uchaguzi wa Raisi utakuwa wa kupiga kura kwa uhuru na kwa matakwa ya watu, hakuna shaka tungewachagua wapiganaji wa vita vitakatifu waliopigana na al-Shabaab ambao waliua watu wasio na hatia kwa jina la dini. Mtu huyo ni Mhe. Farmajo. Asanteni. Ndugu yenu Muislamu. (kumbukeni kuwa unakuwa Muislamu wa kweli ikiwa utachukia kile ambacho ndugu zako Waislamu wanakichukia).

  • maxamed cali cabdule bidaaye
    August 23, 2012 @ 06:12:15AM

    Ni vizuri sana kwa wasomi kugombea uraisi wa Somalia. Ninamuomba Mungu aifanye Somalia kuwa ya amani.

  • ahmedzaki
    August 23, 2012 @ 04:54:17AM

    Kwanza, ningependa kuwapongeza wafanyakazi wote wa Sabahionline, amani iwe juu yenu. Pili, ninataka Mhe. Bw. Mohammad Abdullahi Farmajo ashinde urais. Yeye ni msomi, mwanasiasa mwenye uwezo na anayewapenda Wasomali. Ninamuomba Mungu amsaidie ashinde. Tatu, ninawaomba wabunge wamchague Bw. Farmajo kwa vile anaweza.

  • jeex
    August 23, 2012 @ 04:38:14AM

    Wasomali tunapaswa kuacha masuala ya ubinafsi na kuwategemea wageni kwa msaada ili tusihatarishe mamlaka ya nchi yetu ikiwa tunataka amani.

  • Yaasiin
    August 23, 2012 @ 04:21:20AM

    Abdirahman Baadiyow anafaa kuwa rais. Wasomali wanapaswa kumchagua Baadiyow kama rais wa Somalia ikiwa wanataka utawala bora kwa sababu anaonekana ni kiongozi mzuri kama anavyooneshwa kwenye TV. Ni mpya, si fisadi na ni mcha Mungu.

  • MTABAZI SHEU
    August 23, 2012 @ 02:13:09AM

    Ni juu ya Wasomali pekee, na sio jumuiya ya kimataifa.

  • cabdisalaan
    August 23, 2012 @ 12:37:29AM

    Naamini kuwa Yussuf Garaad anastahiki uras miongoni mwa wagombea wote kwa sababu ni mwandishi wa habari mwenye uzoefu.

  • ADDOW
    August 22, 2012 @ 11:16:48PM

    Mimi namchagua Dr. Samatar kwa ajili ya amani.

  • mahadkaka
    August 22, 2012 @ 08:02:30PM

    Nyote mnajidai kuwa Wasomali kwa sababu hamtaki amani bali fedha na tatizo lenu ni la haki. Tunamuomba Mungu awaangamizeni ili Wasomali wapate amani kwa sababu wamepatwa na matatizo mengi. Mungu awasaidie Wasomali. Amin.

  • mahad
    August 22, 2012 @ 07:28:24PM

    Ningependa Somalia iungane kwa sababu sioni ishara yoyote ya serikali au juhudi zinazofanywa za kuiunda. Ninamuomba Mungu kutusaidia kuchagua kiongozi mzalendo anayemwogopa Mungu na kuwapenda watu na nchi yake. Pia ninamuomba Mungu aiunganishe Somalia. Amin.

  • salmaan
    August 22, 2012 @ 03:15:16PM

    Hii ni nzuri kweli. Somalia inao wasomi wengi lakini ni kitu gani kilifanya nchi kuwa katika matatizo kwa miaka 22 wakati ina wasomi kiasi hiki? Kama ningekuwa mbunge, ningemchagua Profesa Samatar hata kama baba yangu angekuwa mgombea mwengine. Mimi sitoki kabila moja na yeye. Yeye anatoka kaskazini ya Somalia, mimi kusini lakini ninashawishika kwa maelezo ya elimu yake. Ewe Mungu, tusaidie kumchagua kiongozi mzalendo ambaye ana maslahi ya watu na nchi katika moyo wake.

  • maxamad axmed
    August 22, 2012 @ 01:04:55PM

    Hii ni makala nzuri. Ningependa kuwashauri Wasomali kumchagua Mohammad Abdullahi Farmajo kwa sababu ana uzoefu.

  • jamal
    August 22, 2012 @ 09:17:32AM

    Watu wote walioelimika wapewe fursa ya kuthibitisha uwezo wao wa kielimu na sio udhaifu wao.

  • shamsadin suleiman abdilahi
    August 22, 2012 @ 04:29:27AM

    Hakuna aliye bora zaidi kuliko Sheikh Sharif kwa sababu amani na usalama vilionekana katika mji na matumaini ya amani katika maeneo mengine yalikuwa makubwa katika vipindi viwili vya urais wake, kwa hivyo Sheikh Sharif anapaswa kuchaguliwa.

  • al Nuuru
    August 22, 2012 @ 04:07:20AM

    Abdirahman Badiyow anapaswa kuwa rais wa nchi hii.

  • yaser ali
    August 22, 2012 @ 03:39:07AM

    Ninamuunga mkono Farmajo kwa asilimia 100 achaguliwe kwa vile anajulikana na uwezo wake kujaribwa. Ningependa kusema kuwa Farmajo ni Meles wa Somalia na lazima aungwe mkono. Mimi sitoki Somalia, ninatoka Hargeisa na raia wa Somaliland. Ninamtakia maisha marefu Silanyo. Mungu ni Mkubwa. Chagueni viongozi wenu na wala msiwe na uchache katika kura zenu ili mjenge taifa lenu.

  • abdi sahal
    August 22, 2012 @ 03:11:24AM

    Kumbuka, mtu ambaye ameandika makala hii ameitayarisha vyema lakini yote haina maana kwa sababu inasema hivi juu ya Sharif Hassan: “Alizaliwa mwaka 1946 katika mkoa wa Bardaale kutoka familia ya mikoa ya Bay na Bakool.” Angalieni nami habari hii kuhusu Sharif hassan na kile alichoandika kuhusu wagombea wengine. Anasema Alizaliwa Bardaale. Anamfanya Sharif Hassan kama mgeni na kukataa asili yake ya Kisomali. Wewe, mwandishi wa habari mpendwa, nilisoma maadili ya vyombo vya habari na hiki unachokiandika lazima kiwe na mantiki na kuonesha maadili ya vyombo vya habari uliyojifunza. Kama nikiangalia jinsi ulivyoandika habari hii, naweza kuelewa wazi kuwa wewe ni mwandishi wa habari unayechochea nyongo. Digil na Mirifle hawaishi Bay na Bakool bali Shabelle ya Chini na mkoa wa Juba. Unaweza kusema kuwa maeneo ya Gedo badala ya kusema eneo ambalo makabila haya hayajawahi kuishi ndani ya Somalia. Tutajie mikoa hiyo sita, ongeza na Banadir ikiwa hutaki tuishi pamoja na kufanya kazi pamoja. Ghadhabu za Mungu ziwe juu yako.

  • maxamed cali
    August 22, 2012 @ 02:58:25AM

    Ninaipongeza BBC. Naamini kuwa mmoja yeyote kati ya watatu wafuatao anafaa kuiongoza nchi. 1 - Sheikh Sharif Sheikh Ahmed. 2 - Mohammed Abdullahi Mohamed Farmajo 3 - Ahmed Ismael Samatar.

  • C/caziiz
    August 22, 2012 @ 02:15:58AM

    Amani iwe juu yenu. Ninamuomba Mwenyezi Mungu afanye mmoja achaguliwe kama rais wa Somalia, ili awe bora zaidi miongoni mwa Wasomali ambaye atatuongoza kwa kutumia Sharia ya Kiislamu na ambaye ataiharibu katiba ambayo si halali na isiyo na maslahi kwa Waislamu wa Somalia. Sisemi kwa asilimia 100 kuwa fulani ni mzuri kwetu lakini ninamuomba Mungu kutuchagulia yule ambaye atatuongoza katika njia iliyonyooka ya Kiislamu. Mungu atusaidie katika kuchagua.

  • Qareen C/Xakiin Cabdale X Cali (Macsaro)
    August 22, 2012 @ 01:36:26AM

    Farmajo angepaswa kuwa rais wa Somalia kwa sababu anaelewa zaidi kuhusu siasa na Somalia kama nchi. Ni mtu ambaye anaweza kuiunganisha Somalia kama nchi nzima kwa sababu alikuwepo katika siasa za Somalia kwa muda mrefu iliyo ngumu. Amefanya mambo mengi muhimu na alikuwa anasifiwa pale alipoonekana kuwa ni mfanisi. Alisimamishwa kuendelea na kazi yake ngumu ya ufanisi nchini Somalia. Kwa maoni yangu, ninaamini kuwa Farmajo anaweza kuiongoza Somalia bora zaidi kuliko Sheikh Sharif ambaye ameshindwa.

  • abuuyusuf almu haajir
    August 22, 2012 @ 01:32:46AM

    Farmajo ni mwanasiasa mzuri anayejua juu ya utawala bora na kanuni. Anaelewa juu ya utawala na uwazi kutegemea na kile tulichokiona wakati wa miezi sita aliyokuwa anaongoza serikali. Tunamsifu kwa aina yake ya uongozi.

  • dheeg
    August 22, 2012 @ 12:57:12AM

    Sijaridhika kwa sababu katibu wa chama cha Farmajo ni mwanamke. Mtume (Amani Iwe Juu yake) alisema jamii inayoongozwa na mwanamke daima haitafanikiwa.

  • hidaya
    August 21, 2012 @ 11:31:48PM

    Changamoto za kijamii na kiuchumi zinaleta changamoto kubwa kwa rais mpya wa Somalia, hasa masuala ya watu waliokimbia makazi yao. Takriban watu milioni tatu wanaishi katika hali mbaya sana ya kijamii, kibinadamu na kiuchumi kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Wasomali wanategemea misaada ya nje hasa ya chakula na madawa, jambo linalohitaji kuanzisha upya miundombinu ambayo inakabiliwa na uharibifu mkubwa na kuongeza mzigo kwa rais mteule. Ikiwa atakuwa na haja ya uaminifu wa watu wa Somalia ili kumuunga mkono katika kukabiliana na pande zinazopigana, itambidi aanze kutafuta sera ambayo itatoa huduma za msingi, hasa ikiwa tutaangalia msaada wa kifedha unaotolewa kwa pande zinazopigana na kikundi cha al-Shabaab ili kuzishawishi kujiunga nao. Kwa hivyo, kufikia matokeo ya kweli ya kujenga upya huduma na uchumi na asasi za kijamii ni suala muhimu kwa Wasomali ili kuitambua serikali mpya na kiwango cha mafanikio yake.

  • Hajjy
    August 21, 2012 @ 04:20:49PM

    Mtu kama Sharif Hassan hana sifa za kuwa mgombea wa urais kwa sababu ya wasifu wake wa kielimu...nafikiria Somalia inahitaji mtu inahitaji mtu wa kuiongoza na sio mtu anayehitaji kuongozwa.

  • hassan jaamac daahir
    August 21, 2012 @ 01:12:47PM

    Kama kuna haja ya kuunda serikali nchini Somalia, Profesa Samatar achaguliwe kuwa rais.

  • jaalle khaatumo gaane
    August 21, 2012 @ 01:10:06PM

    Ninamuunga mkono Farmajo kwa sababu ni mtu wa haki, mzalendo na kiongozi mwenye uzoefu.

  • ibraahim cilmi daxir
    August 21, 2012 @ 11:13:41AM

    Ningependa kusema mchagueni Sharif Hassan Sheikh Adan kama rais wa Somalia kwa sababu yeye ni mtaalamu wa masuala ya Somalia.

  • FM
    August 21, 2012 @ 06:55:36AM

    SAWA SAWA

  • MR FRANCIS
    August 21, 2012 @ 06:44:28AM

    YUSUF AWE RAISI

  • hussein
    August 21, 2012 @ 05:33:37AM

    Asante kwa historia ulizoandika kuhusu wale wanaogombea urais wa Somalia. Wakati niliposoma historia ya wagombea nimeona watu watatu wanaostahiki. Ningependa kuwachuja tena watu watatu hawa. Watu hawa ni Sheikh Sharif, Farmajo na Abdiweli. Nikiangalia historia ya elimu, kujiamini na kuunganisha watu, Farmajo ndiye anayeongoza. Sheikh Sharif anaweza kuleta imani kwa watu na majeshi. Abdiweli ni mtu mzuri lakini ni mzuri katika masuala ya uchumi na uongozi. Nchi hii inahitaji kiongozi anayeweza kuitoa katika matatizo. Kwa sababu hii, Abdiweli si mmoja wa wanaotegemewa kushinda urais. Farmajo ni simba na amejenga imani kwa jeshi na wananchi. Kumbukeni kuwa ikiwa mtu atapata kuungwa mkono na jeshi atafanikiwa kushinda katika chochote anachojaribu. Asante.

  • Miskiinow
    August 21, 2012 @ 05:16:44AM

    Nadhani tusisite kwa ajili ya mtu wa kuiokoa Somalia kutoka matatizo iliyopitia tokea mwaka 1991. Ni Mungu pekee anayeweza kuiokoa lakini nadhani rais mzuri kwa Somalia ni MOHAMMAD ABDULLAH FARMAJO ambaye tuliona kabla anachoweza kufanyia nchi yake. Yeye alikuwa mwanga uliong’ara mara moja kwa Wasomalia lakini hakuonekana tena kama Umoja wa Mahakama za Kiislamu. Aliituliza nchi japokuwa kidogo kama ya Umoja wa Mahakama za Kiislamu.

  • geesay
    August 21, 2012 @ 05:08:47AM

    Kwa maoni yangu, ningependa kuwaambia Wasomali kumteua Yusuf Garad kwa sababu ni msafi na amesoma. Ndugu zangu, ningependa kuwaomba wabunge kumchagua mtu ambaye hakufanya uhalifu dhidi ya nchi na aliyesoma kama Yusuf Garad. Utafanikiwa mara zote, Mungu akipenda. Tulinde na rais ambaye anaweza kugeuzwa kirahisi na yule ambaye anawapenda watu wa nje. Kumbukeni, pia mnasubiri kuja kuwa maraisi kwa hivyo walindeni wananchi kwa kuwa mtakuja kuwahitaji wakuchagueni. Huu ndio ushauri wangu. Muogopeni Mungu wenu. Asante sana.

  • Saleban Saed Ogle
    August 21, 2012 @ 05:03:38AM

    Kwa kweli niliangalia maelezo ya kielimu na niliwahi kuwajua wote waliotajwa hapa katika kugombea urais, sikumuona yeyote ambaye anastahiki nafasi hii. Sidhani kama kuna mtu miongoni mwao wa kuisaidia Somalia kutoka katika matatizo. Hakuna aliye bora zaidi ya Sheikh Sharif ikiwa tutamkosa mtu mwengine.

  • dahircaawiye
    August 21, 2012 @ 04:26:00AM

    Kwanza, ningependa kumuomba Mungu kuisaidia Somalia itoke katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na matatizo yaliyoikumba kwa muda mrefu. Ningependa kuwashauri Wasomali kumfukuza mtu huyu ambaye ametenda uhalifu dhidi ya nchi yake; Somaliland (Mtoto wa Ismail Samatar) KWA SABABU TAYARI NI MTU ALIYESHINDWA NA HAWEZI KUWASAIDIA WENGINE. Anafanya kazi kwa kuchochea na kujenga chuki baina ya jamii.

  • ABDIKADAR
    August 21, 2012 @ 04:05:56AM

    HABARI HII NI MUHIMU SANA NA NILIIPENDA. ASANTE.

  • Abdulahi
    August 21, 2012 @ 03:57:22AM

    Kwa kweli nimeipenda. Ninamshukuru sana mwandishi aliyeandika habari hii hata kama amewaacha wagombea wengi lakini amechagua wale wanaotarajiwa zaidi kushinda.

  • Leo
    August 21, 2012 @ 03:54:47AM

    Makala ni ya kuvutia na ni nzuri

  • amd
    August 21, 2012 @ 03:51:38AM

    Nadhani Mohammad Abdullah Farmajo anapaswa kuteuliwa kama rais wa Somalia.

  • Abdullahi Issa
    August 21, 2012 @ 03:50:03AM

    Ninamuona Profesa Ahmed Ismail Samatar kama mtu pekee anayeweza kuisaidia Somalia kutoka katika matatizo leo.

  • Elmi mahamoud Ysin
    August 21, 2012 @ 03:27:04AM

    Amani iwe juu yenu. Ripoti hii imejikita zaidi katika historia ya elimu za wagombea lakini nadhani wawili wa wagombea wanaweza kufanya vitu vingi kwa nchi yetu ikiwa watapewa uongozi. Wagombea waliobakia wametenda uhalifu dhidi ya watu, nchi na dini. Watu wawili hawa niliosema waneweza kuleta mabadiliko kwa Somalia ni Preofesa Ahmed Ismail Samatar na Dr. Mohammed Abdullahi Farmaajo. Farmaajo ni kiongozi ambaye Wasomali waliandamana kwa ajili yake ili kumzuia asijiuzulu.

  • haaji ade
    August 21, 2012 @ 03:01:56AM

    KIPINDI CHA SHEIKH SHARIF KWENYE OFISI KIMEKWISHA.

  • Abdulkadir M Ahmed
    August 21, 2012 @ 02:43:24AM

    Ni habari muhimu iliyokusanywa na mtu anayefanya kazi kwa bidii.Kwa nini hamkusema chochote kuhusu historia ya elimu ya Sharif Hassan Sheikh Adan ili watu waelewe kama hakusoma? Asanteni na Muogopeni Mungu.

  • maxamed cumar maxamed
    August 21, 2012 @ 02:30:14AM

    Ninamshukuru Mungu aliyetuumba. Wale miongoni mwenu mnaogombea mtakabiliwa na kazi ngumu ya kufanya huko mbele. Yaani, mtalazimika kuwaambia watu ukweli kuhusu dini ya Kiislamu ambayo mnadai kuifuata, kufanya haki na usawa kwa wote. Lazima mjiamini katika nchi yenu ma kuilinda kutoka chochote kitakachokiuka dini. Lazima muaminiane baina yenu na kuelewa kuwa hamuwezi kuwajibishwa na mgeni isipokuwa mjiwajibishe wenyewe. Tunahitaji kulinda heshima ya dini yetu, watu na chi yetu na itatubidi tujitahidi sana kuiimarisha tena kwa mara nyengine tena. Jitahadharini kuwa ni muhimu kuwaunganisha Wasomali kwa dhamiri ya kufanikisha maslahi yao ya pamoja. Wasomali wanahitajika kuungana ili kumaliza machafuko haya. Wasomali walenge katika maslahi yao ya pamoja badala ya ukabila, undugu na uchoyo wa kibinafsi ambayo yanakwamisha kufanyakazi kuelekea umoja wa kitaifa na maendeleo. Lazima tutazame nyuma tuone kile kilichotokea huko lakini tufanye kazi kwa nguvu ili kuleta umoja miongoni mwa watu. Sio muhimu kwako kuwa rais bali kuwaunganisha na kulijenga upya taifa letu ndio kitu muhimu. Nchi si ya raisi bali ya watu waliozaliwa na ilinde. Kumbukeni, rais ni mtumishi wa watu na kuwaunganisha wananchi ndio kitu muhimu. Tusaidiane katika kuitafuta nchi yetu ambayo ninapenda kuona imejengwa upya kwa milele.

  • PuntlandGeezer
    August 20, 2012 @ 06:14:19PM

    Ahmed Ismail Samatar, Farmaajo au Abdiweli Mohamed Ali washinde, watatu hawa watafanya kazi kubwa lakini hawa masheikh, yaani, Sharif Sheikh Ahmed na Sharif Hassan Sheikh Aadan lazima watimuliwe kutoka siasa za Somalia milele.

  • abdfatah dahir abdilahi
    August 20, 2012 @ 05:12:17PM

    Inasisimua kuona wasomi wanagombea urais wa Somalia. Wanahitaji kukumbushwa kuwa siasa za Somalia zimewafedhesha mabwana wa vita, majenerali wa kijeshi na wasomi wa kidini. Je, wasomi wataaibishwa pia?

  • abdirahman adde
    August 20, 2012 @ 02:15:47PM

    Tafadhalini, malizeni historia ya wagombea mlioandika. Pia,nigependa kuuliza kwa nini MHE. Abdullah Ahmad Adow alitolewa katika ugombeaji wakati mnajua kuwa yeye ni kiongozi wa Somalia? Tafadhalini, jirekebisheni. Asanteni.

  • maxam
    August 20, 2012 @ 01:40:18PM

    Ningependa kusema kuwa wewe ni mwandishi wa habari maarufu unayependwa na wengi wa watu. Viongozi wa Somalia walijulikana kwa kuwa na hatima mbaya. Unadhani utasilimika na hilo? Na ni ipi MIPANGO yako ikiwa utasalimika? Hakuna yeyote atakayekupenda utakapokuwa kiongozi kwa hivyo ninawaomba Wasomali wasisahau sehemu sawa ya ndugu zao wa kaskazini ya Somalia. HONGERA

  • SAYIDCADHO
    August 20, 2012 @ 12:35:06PM

    SISI NI AL-SHABAAB KWA HIVYO MNAPASWA KUJILINDA NA MASHAMBULIZI YETU

  • AMIIN-YARE
    August 20, 2012 @ 10:25:38AM

    Ni wazo zuri. Watu hawa ni raia licha ya uraia wa nchi nyengine walionao na kila mmoja wao anadaiwa na pesa alizosomeshewa wakati alipokuwa anaishi nchi hii, isipokuwa baada ya kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita vya wenyewe viliwasababisha watu wasiyakabili matatizo yaliyokuwa yanatokea nchini kwa hivyo kuharibu hatima yetu kiasi kwamba sasa hatuwezi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Ili kumaliza matatizo yaliyoiharibu nchi yetu kutoka mwaka 1991 hadi 2012, sasa tunawachunguza wagombea leo ili tuweze kuchagua viongozi wanaofaa na kuunda serikali yetu ambayo itakuwa huru na uingiliaji kutoka nje na kututoa kutoka serikali ya mpito, kusimamia elimu yetu, mahitaji ya afya pamoja na kuandaa kazi kwa watu 4500 ambapo watu wanaweza kufanya kazi lakini walishindwa kutokana na utawala mbaya au ukosefu wa utawala. Pia watu hawa wanakabiliwa na ufisadi wa hali ya juu na kujitwalia fedha isivyo halali, kwa hivyo wanahitaji kutumikiwa, kusimamiwa na kurejeshwa katika hali ya kawaida kutokana na mazowea haya mabaya waliyojifunza kutokana na matokeo ya kukosekana kwa serikali na ukabila, ambao uliiharibu na kuivunja nchi yetu kwa miaka 21. Ningependa kuwaambieni nyote kuwa utawala wa haki ni wa Mungu pekee lakini tulikataa na kuwa walamba viatu na watu tusioamini. Ikiwa hao wanaogombea watakuwa pamoja na kumchagua mmoja wao kwa ajili ya kumaliza mzozo huu, nadhani tutasahau makabila na majimbo yetu ambayo kila mmoja wetu hujitambulisha nayo. ACHENI MAJIGAMBO HAYA NA KUPOTEZA MWELEKEO kwa vitu ambavyo vimetufanya tuwe hatuna maana na kukubali kushinda au kushindwa na kufanya kazi na marafiki zetu walioshinda ili muweze kuilipa nchi hii kile inachowadaini, Mungu akipenda.

  • libaax koriye
    August 20, 2012 @ 03:55:03AM

    Hii ni nzuri lakini mtu yule mnyenyekevu (Ina Buuba) alisalimu amri? Sisikii kwamba anagombea au hamkumuweka katika orodha kwa sababu haungwi mkono na watu kutoka eneo lake?

  • aaliya
    August 20, 2012 @ 02:51:59AM

    Kwa kusoma makala hii, na kuelewa serikali ya sasa, tunajua mpaka lea nini serikali ilifanya. Mkuu wa nchi, Sheikh Sharif Sheikh, hakujenga hata shule wala barabara moja ya Mogadishu, lakini kujijengea nyumba zake/zao na mahoteli ndani na nje ya nchi) na kutumia mali za taifa kama pesa zake/zao, na hawakuwa na hata athari chanya kwa taifa, isipokuwa kwa kabila/makabila yake/yao. Ningempokea sana Abdirahman Abdullahi Baadiyow,au Hassan Sheikh Mohamud. Ninaweza kukosea, lakini kwa mujibu wa makala hii kuna watu wawili tu, ambao, wamekuwa sehemu ya ujenzi wa shule na wanaojaribu kurekebisha maendeleo ya wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, (Elimu ni uwekezaji bora zaidi), hao wengine wamefanya nini kwa taifa hadi sasa zaidi ya kuwa sehemu ya serikali bila ya mabadiliko bali ufisadi zaidi? Asanteni kwa fursa hii.

  • setywillison
    August 19, 2012 @ 03:10:32AM

    makala hii inafundisha kutokana na kupata habari mbalimbali za ulimwengu

  • ajaihsfjhaiofcjhqaio
    August 18, 2012 @ 09:50:13AM

    Ikiwa Wasomali wanataka raisi ambaye atafanya kazi kwa maslahi bora ya taifa na asiyetafuta kujaza mifuko yake kwa dola, wanapaswa kuchagua baina ya watu wawili: Dr. Ahmed Ismail Samatar au mwandishi wa habari Yusuf Garaad Omar. Ama kuhusu makala, nakubaliana na yaliyomo ndani yake.

  • mahad
    August 18, 2012 @ 08:30:33AM

    Uteuzi wa bunge la Somalia.

  • mustafe
    August 18, 2012 @ 08:19:31AM

    Kwa kweli, taarifa hii ni nzuri kwa sababu Wasomali wanapaswa kuelewa sifa za mtu wanayetaka kumteua. Hii itatusaidia kuwatambua wale watu wenye sifa hizo na kumchagua yule aliye bora zaidi miongoni mwao. Kwa kweli taarifa hii ni muhimu.

  • ibrahim Mohamed Abdi
    August 18, 2012 @ 04:35:19AM

    Farmaajo kwa urais wa Somalia.

  • Kaamil
    August 17, 2012 @ 10:22:12PM

    Lazima kumaliza kila kitu kinachofanya uharibifu na maangamizi kukamilika kwa katiba mpya ya Somali ndio kumalizika kwa ugaidi na kuanza kwa zama mpya za demokrasia nchini.

  • Muxyadiin Muumin Caateeye
    August 17, 2012 @ 09:56:59PM

    Kama tunaona iko haja ya Somalia kuwa na utulivu na kuwa na wajibu mkubwa kwa Afrika na ulimwengu wote, ningependa kuwashauri watu wamteue Profesa Ahmad Ismail Samatar kwa vile ni mwanazuoni mtenda haki na mzalendo ambaye anaipenda nchi yake na watu wake.

  • Diini
    August 17, 2012 @ 07:53:32PM

    Zimefika zama mpya nchini Somali baada ya kusubiri muda mrefu kuwekwa kwa katiba mpya kwa furaha kubwa ya wajumbe wa tume ya uanzilishi ambayo imechunguza kazi yake kwa kila juhudi na heshima na uadilifu kwa ajili ya ndugu zetu wananchi wa Somali.

  • Aweys Haji
    August 17, 2012 @ 07:11:39PM

    Hii ni makala nzuri. Ninampenda sana Dr. Baadiyow kwa sababu ni mwanazuoni ambaye hakufanya uhalifu wowote kitambo na anapendwa na watu. Naamini anaweza kuliongoza taifa hili kupata maendeleo na mabadiliko tunayoyahitaji. Ninamuomba Mwenyezi Mungu amfanye kuwa rais wa Somalia.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo