Afrika ya Mashariki kufaidika na pendekezo la jina la umiliki wa wavuti la bara la Afrika

Na Sargajan bin Kadii, Nairobi

Agosti 16, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Umoja wa Afrika unafanyakazi kuanzisha jina la wavuti kwa bara zima ambalo litayawezesha mashirika binafsi na ya serikali kutumia jina moja la umiliki wa wavuti- -kama .africa -- kutumika katika tovuti zao.

  • Wakaazi kutoka kijiji cha Embakasi, kilomita 25 kutoka Nairobi, wanaelekea katika cafe ya wavuti inayotembea na inayotumia umeme wa jua, iliyotengezwa kwa kutumia kontena la mizigo.  [Na Tony Karumba/AFP]

    Wakaazi kutoka kijiji cha Embakasi, kilomita 25 kutoka Nairobi, wanaelekea katika cafe ya wavuti inayotembea na inayotumia umeme wa jua, iliyotengezwa kwa kutumia kontena la mizigo. [Na Tony Karumba/AFP]

Mpaka sasa, nchi 44 za Afrika kati ya 54 zimeukubali mpango huo, zikiwemo Tanzania, Kenya na Djibouti, kwa mujibu wa shirika linalosimamia kampeni hiyo, UniForum Association.

Mpango huo utaliwezesha bara la Afrika kupata kuonekana zaidi katika wavuti lakini sio lazima upelekee katika ukuaji wa uchumi, wachambuzi wasema.

"Kuanzisha jina moja la umiliki wa wavuti kutasaidia mtiririko wa habari barani Afrika kwa vile hakutakuwa na vikwazo vya kiufundi katika kuwasiliana kutoka jina la taifa moja kwenda jengine," alisema Charles Ryoba, mshauri wa teknolojia ya habari (TEKNOHAMA) aliyeko Nairobi.

"Pia itazisaidia nchi ndogo kama vile Sudani ya Kusini ambazo miundombinu yao ya TEKNOHAMA bado haijaendelea kwa vile programu nzima itahamasisha mwamko na ukuaji wa teknolojia," aliiambia Sabahi.

Mara tu jina la umiliki wa wavuti la kanda litakapoanzishwa, majina ya umiliki ya taifa yatafuata jina la umiliki la bara katika anuani za tovuti zao. Kwa mfano, ikiwa .africa itachaguliwa kama jina pekee la umiliki la bara hili, tovuti za Kenya zitaishia na .africa.ke, Tanzania zitashia na .africa.tz, Ghana .africa.gh, n.k.

Tiberius Barasa, mkurugenzi mwendeshaji wa Kituo cha Utafiti wa Sera cha Kenya, anasema kuwa na jina moja kutazisaidia serikali kupambanana na uhalifu.

"Tofauti na mfumo wa sasa ambapo maeneo tofauti yanaingiliana katika mtiririko wa data kusaidia kuipata anuani asilia, kukiwa na jina moja, chanzo kinaweza kufuatiliwa kwa urahisi zaidi, na kuisaidia serikali kupambana na wanaoghushi na wadanganyifu," aliiambia Sabahi.

Barasa alisema mashirika yanayouza vitu vinavyodaiwa kuwa ni ubunifu kutoka Afrika watakuwa na wakati mgumu kwa vile njia moja la umiliki litabeba saini ya mtandaoni duniani kote kwa kila kitu kinachotoka Afrika.

"Pia itakuwa rahisi kwa serikali za Afrika ya Mashariki kupatanisha huduma za teknolojia ya habari," alisema.

Licha ya kukubaliwa kwa jumla wazo la jina moja la umiliki wa wavuti, Francis Bett, mhandisi wa programu za kompyuta aliyeko nairobi, anasema mpango huo sio lazima ulete faida kubwa sana za kiuchumi kwa Afrika.

"Dunia inakuwa moja na biashara zinataka kufuata vitambulisho vitakavyoziwezesha kuonekana kuwa za kimataifa tofauti na [kupatikana] kikanda," Bett alisema. Jina la umiliki [la bara zima] litakuwa na faida za kisiasa kwa vile litawapa Waafrika utambulisho mmoja mtandaoni, zaidi ya hilo, uwepo wake utakuwa unakwenda kinyume na moyo wa wavuti, unaoufanya dunia kuwa kijiji cha ulimwengu."

Ingawaje Ulaya na Asia zinayo majina yao ya umiliki wa wavuti wa kikanda, hayo hayajapelekea kuwapo na athari kubwa kiuchumi katika uwanja wa kimataifa, Bett aliiambia Sabahi. Jina moja la umilki wa wavuti kwa Afrika linatarajia kuwa la tatu baada ya .eu kwa Ulaya na .asia kwa Asia.

Sera za Shirika la Wavuti kwa Majina na Nambari (ICANN) zinaeleza kwamba kampuni yoyote inayoomba kutumia jina la kikanda lazima likubaliwe na angalau asilimia 60 ya nchi zilizopo kanda hiyo.

UniForum na shirika la Kenya lisilo la kifaida DotConnectAfrica ni mashirika mawili yaliyobakia katika zabuni ya kusimamia wavuti wa kanda ya Afrika. Kampuni hizo ziliomba kwa ICANN kupatiwa leseni na mshindi atatangazwa robo ya kwanza ya mwaka 2013, wakati uandikishaji unapotarajiwa kuanza.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 6)

Dislike_icon(2)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Gitonga F.M.
    August 23, 2012 @ 09:30:19AM

    Nzuri sana.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo