Usafirishaji nje haramu wa mkaa unazalisha mapato makubwa kwa al-Shabaab

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Agosti 16, 2012

  • 5 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Biashara haramu ya mkaa huko Somalia ya Kusini inavuma na kuzalisha mapato makubwa kwa al-Shabaab, wachambuzi na waangalizi wanasema.

  • Al-Shabaab inatumia bandari ya Kismayo, Barawe na Marka kusafirishia nje mkaa, wakigharamia shughuli za himaya yao kutokana na tasnia hii haramu. [Saif Dahlah/AFP]

    Al-Shabaab inatumia bandari ya Kismayo, Barawe na Marka kusafirishia nje mkaa, wakigharamia shughuli za himaya yao kutokana na tasnia hii haramu. [Saif Dahlah/AFP]

Al-Shabaab inategemea kwa kiasi kikubwa mapato kutokana na usafirishaji wa mkaa nje ili kugharimia shughuli zao za ugaidi, alisema Sheikh Ahmed Madobe, kiongozi wa kikundi cha Ras Kamboni, ambacho kinashiriki katika kampeni za kijeshi za vikosi vya ushirika dhidi ya al-Shabaab katika maeneo ya Juba.

"Usafirishaji mkaa nje kinyume cha sheria kwa sasa unachukuliwa kama chanzo kikuu cha mapato cha al-Shabaab," Madobe aliiambia Sabahi. "Al-Shabaab ni kikundi pekee ambacho kinaruhusu wafanyabiashara wenye kupokea rushwa kusafirisha mkaa nje kupitia bandari zilizo chini ya usimamizi wao."

Madobe alisema hakuna idadi rasmi ni kiasi gani cha fedha al-Shabaab inapata kutokana na kusafirisha nje mkaa, lakini alisema mapato yanaweza kufikia mamilioni kadhaa ya dola kwa mwaka.

Barua ya Kikundi cha Umoja wa Mataifa cha Ufuatiliaji huko Somalia na Eritrea iliyofichuliwa mwezi Juni ilisema mkaa ni "sehemu moja muhimu sana ya chanzo cha mapato cha al-Shabaab."

Al-Shabaab wanadhibiti bandari kuu tatu huko Kismayo, Barawe na Marka ambako ndiko mkaa unakosafirishiwa kwenda nje.

Wapiganaji wa al-Shabaab wameanza kuondoka kadri Somalia na vikosi vya muungano vinavyolekea Marka , na Viongozi wa majeshi ya Somalia na Kenya wanasema wanadhamiria kuichukua Kismayo mwezi huu.

Al-Shabaab imekuwa ikiondolewa kwenye ngome nyingi huko Somalia kwa miezi kadhaa iliyopita, ikiwa ni pamoja na Beledweyne , Baidoa , Hudur , Afgoye na Balad . Matokeo yake, al-Shabaab "imepoteza sehemu kubwa ya vyanzo vya fedha ambavyo vilikuwepo kwa kukusanya kodi kubwa kutoka kwenye masoko, vyombo vya biashara na wakulima," alisema Mohamed Hassan, mchambuzi wa masuala ya kisiasa ambaye anaifuatilia al-Shabaab.

"Al-Shabaab hivi karibuni imekuwa ikilenga biashara ya mkaa ili kugharamia shughuli zake za mapigano baada ya mapato yake mengine kupunguka polepole tangu kuongezeka kwa kampeni ya kijeshi ya vikosi vya muungano," Hassan aliiambia Sabahi.

"Wakati al-Shabaab ilipokabiliwa na matatizo ya kifedha , ilianza kujielekeza katika kusafirisha mkaa," alisema. "Zaidi ya asilimia 95 za mkaa [kutoka Somalia] unasafirishwa kupitia katika bandari chini ya usimamizi wa al-Shabaab."

Jitihada za kuzuia usafirishaji nje wa mkaa Somalia

Mwezi Februari, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kupiga marufuku usafirishaji nje wa mkaa wa Somalia, likisema biashara yake inatishia amani, usalama na utulivu wa Somalia.

Mwezi Aprili, Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia ilitoa na kutekeleza sheria inayopiga marufuku usafirishaji wa mkaa, ikizuia usipite katika bandari ya Mogadishu.

Licha ya azimio la Umoja wa Mataifa, mkaa kutoka Somalia bado unajaa katika masoko ya nchi za Ghuba, kwa mujibu wa barua ya Juni kutoka katika Kikundi cha Umoja wa Mataifa cha Ufuatiliaji huko Somalia na Eritrea.

"Waagizaji wakuu wa mkaa wa Somalia -- hasa Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia -- zimekuwa zikisuasua kutekeleza upigwaji marufuku huo, na hadi kufikia Juni 2012, kiasi kikubwa cha mkaa kinaendelea kuondoka kwenye bandari zinazodhibitiwa na al-Shabaab za Barawe na Marka kwa ajili ya kuuzwa katika nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba," barua hiyo ilisema."Lakini mashambulizi ya kijeshi ya AMISOM, Ethiopia na Kenya yameinyima al-Shabaab udhibiti wa vituo vya kodi vyenye faida kubwa, ikiwa ni pamoja na masoko na vituo vya mpakani, yakiondoa msingi wao wa mapato."

Mbunge Mohamed Omar Gedi alisema itakuwa vigumu kuamuru kuzuia usafirishaji nje hadi al-Shabaab itakapokuwa imetolewa nje ya bandari inayotumia kusafirishia mkaa. Nchi za ghuba pia ni lazima ziamuru kizuizi cha biashara ya usafirishaji wa mkaa wa Somalia, alisema.

"Kama nchi hizi zitakubaliana kumaliza uagizaji wa mkaa kutoka Somalia, wasafirishaji hawatakuwa na uwezo wa kutafuta soko, na kusababisha kushuka kwa mapato ya al-Shabaab," alisema Gedi.

Uharibifu wa mazingira kutokana na mkaa unatishia kilimo

Kutokana na wanamazingira, tasnia hii isiyo halali inaathiri mazingira na inaweza kuzidisha hali ya ukame na njaa.

"Ukataji wa misitu, matokeo ya uzalishaji wa mkaa, unasababisha uharibifu wa hali ya juu wa mazingira ambao umechangia kuzidisha mgogoro wa kibinadamu nchini Somalia," alisema Farhan Ali, Kaimu Mkurugenzi wa Somali Environment Protection Alliance Network, shirika lisilo la serikali (AISE) lililopo Mogadishu.

"Ukataji wa hali ya juu wa misitu katika baadhi ya maeneo ya Somalia umesababisha jangwa na kupungua kwa ardhi yenye rutuba na kwa ajili ya mifugo," Ali aliiambia Sabahi. "Hili limelazimisha baadhi ya wenyeji hususan wachunga kondoo, kuacha ardhi yao inapotokea ardhi haifai kwa mifugo baada ya kukatwa kwa miti yote"

Wataalamu wanaamini kwamba ukataji wa misitu uliosababishwa na uzalishaji wa mkaa umechangia kuwepo kwa ukame na njaa ya mwaka jana nchini Somalia.

"Uzalishaji wa mkaa nchini Somalia sio tu unaharibu mazingira na kuchangia kukosekana kwa chakula cha uhakika, lakini pia unachangia dhana na uandaaji wa vurugu," ilieleza Programu ya Maendeleo ya UN mwezi Mei. " Uzalishaji wa mkaa unaongeza kasi mchakato wa kusababisha jangwa, unapunguza kiasi cha ardhi isiyofaa kwa kilimo au hata ufugaji, na kuwafukuza wenyeji nje ya eneo kwa kukosa makazi baada ya wachomaji wa mkaa kukata miti yote."

Ali alisema al-Shabaab wameweka vipingamizi kwa tukio lolote la wenyeji na mawakala wa kulinda mazingira kupanda tena miti.

"Kama wakaazi wenyeji au AZISE za kulinda mazingira zitajaribu kutekeleza miradi ya kupanda tena miti katika maeneo yaliyong'olewa miti kwa ajili ya ulinzi wa mazingira, wanamgambo wanaanza kufikiria kwamba wanafanya kazi kwa ajili ya mashirika ya kigeni na hivyo kupinga jitihada hizo." alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 10)

Dislike_icon(3)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Mohamed Sheikh Hussein Mohamed
    August 17, 2012 @ 05:48:57PM

    Kwanza kabla ya yote, ninakishukuru kikundi cha Sabahionline ambacho kinaripoti kila wakati yale yaliyo nyuma ya matatizo yetu. Mada hii ni muhimu, muhimu sana kwa watu wa Somalia na hasa kusini ya Somalia kuangalia miti inavyomomonyoka. Mimi mwenyewe ningependa na ninatarajia kutekelezwa kwa kupigwa marufuku ya mkaa moja kwa moja.

  • dev
    August 17, 2012 @ 01:51:01PM

    waache ugaidi

  • Ali maow
    August 17, 2012 @ 08:19:57AM

    Al-Shabaab wamewaua watu wengi ambao hawakufanya uhalifu wowote. Waliwaua watu hawa kwa sababu tu ya itikadi yao lakini kwa madai ya kidini yanayoshikiliwa na kikundi ambacho bila ya shaka hakina msingi ya kidini. Baadhi ya matendo yaliyofanywa na kikundi hiki kilicholaaniwa ni pamoja na mauaji ya wanafunzi wengi ambao walikuwa ndio kwanza wamehitimu kutoka vyuo vya tiba na kikundi kudai kuwa sherehe za mahafali zilikuwa kinyume na mafundisho ya kidini. Suala hili lilisababisha upotevu katika sekta ya elimu mbali ya upotevu wa watu kwa sababu kitendo hiki kiliwanyima watu msaada ambao madaktari hawa wapya wangetoa kwa jamii. Pia al-Shabaab iliua wanafunzi wengi waliokuwa wamehitimu kutoka shule za sekondari, miongoni mwao, wanafunzi hodari sana ambao walihakikishiwa nafasi za masomo nchini Uturuki. Wanafunzi hawa walikufa kwa sababu ya gari lililokuwa limefungwa chombo cha mlipuko. Pia kuna vitendo vyengine vilivyofanywa na kikundi hiki ambavyo vinaweza kumfanya mtu aote mvi hapo hapo. Mungu ajalie ghadhabu zake zikiendee kikundi chochote ambacho kinataka kujenga chuki katika jamii, na tunamuomba Mungu awafikishe katika hukumu wauaji hawa na kuwaadhibu hapa duniani na akhera.

  • abdifitah
    August 17, 2012 @ 05:42:37AM

    Vikundi hivi vimesababisha kukwama kwa maisha nchini Somalia kwa sababu wanasababisha hisia za vitisho na woga kwa watu. Suluhisho pekee la kuifanya Somalia itulie ni kuvitokomeza vikundi hivi na natumai hilo litatokea kwa sababu ugaidi ni chanzo cha matatizo yote kama vile utengano wa watu na ukatili.

  • jama
    August 17, 2012 @ 03:25:07AM

    Ikiwa nchi za Ghuba hazitapiga marufuku uagizaji wa mkaa kutoka kwa al-Shabaab kwa hivyo haitamlaiza chanzo cha al-Shabaab kujipatia fedha na kuondoshwa katika kambi zilizobakia kama vile Kismayu. Jeshi la Kenya na Somalia lazima ziiteke bandari kuu ya Kismayu ili kuking'oa kikundi cha kigaidi.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo