Agosti 10, 2012
Kutoka Bunge la Katiba ya Taifa la Somalia kuthibitisha rasmi katiba ya muda tarehe 1 mwezi Agosti, kumekuwa kukiongezeka tofauti za maoni miongoni mwa wakosoaji wa katiba na waunga mkono ambao wanaiona kama hatua ya kihistoria kwa Somalia.
Ingawaje katiba inaeleza kuwa sheria za Sharia zitakuwa chanzo kikuuu cha sheria katika nchi hiyo, baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wanaupinga sehemu kadhaa za waraka huo.
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Somalia cha Wanazuoni wa Kiislamu Shekhe Nur Barud amesema baadhi ya vifungu vya katiba hiyo havilingani na mafundisho ya Kiislamu.
"Katiba hii mpya haitoi uhakikisho wa uhifadhi wa dini na maadili ya taifa ya watu wa Somalia, hivyo tunaomba ipitiwe tena," alisema.
"Tunataka katiba hii mpya kuwa na ulinganifu na sharia za Kiislamu na vifungu virekebishwe ili viendane na sheria za Sharia, hususani zile zinazohusiana na uhuru wa [watu] na hasa [kipekee] jukumu la wanawake," Barud aliiambia Sabahi.
Kuna ukosoaji mwingine ambao umetokea katika vyanzo visivyo vya dini kuhusiana na mgawanyo wa rasilimali miongoni mwa maeneo, hadhi ya mji mkuu wa Mogadishu, na mipaka ya Somalia -- masuala yote haya hayakushughuhulikiwa katika katiba hii mpya.
"Hadhi ya makao makuu na suala la mipaka ya nchi haliko wazi katika katiba mpya," alisema mchambuzi anayeishi Mogadishu Mohamed Nur Osman. "Masuala haya yanahitaji ufafanuzi zaidi kwa sababu utata katika mambo kama hayo haukubaliki."
"Tunapaswa kutatua masuala haya kwa sababu hatuwezi kukubali waraka ambao unapuuza hadhi ya makao makuu ya nchi na mipaka yake," Osman aliiambia Sabahi.
Osman alisema rasimu ya katiba haikuonyeshwa kwa sehemu zote za jamii ya Somalia kabla ya kupelekwa kwenye Bunge la Taifa la Katiba, na bunge halikuwa na madaraka ya kubadilisha chochote, hivyo liliidhinisha rasimu bila ya marekebisho au nyongeza yoyote.
Mohamud Hussein, mtaalamu katika sheria ya katiba anayefundisha katika vyuo vikuu kadhaa huko Mogadishu, haoni kwamba yaliyomo katika katiba mpya inafaa kuleta ulaghai na mabishano hayo.
"Kwa hakika makosa yanafanyika wakati wa kuandika katiba mpya kwa sababu mchakato huu unafanywa na binadamu," aliiambia Sabahi. "Hata hivyo, jambo muhimu sana ni kusahihisha makosa, popote yalipo na kuendelea mbele."
"Hii bado ni katiba ya muda na haitakuwa ya mwisho hadi itakapowekwa katika kura ya maoni ya taifa," Hussein alisema.
Alisema bunge linalokuja litawajibika kushughulikia masuala ambayo hayakujumuishwa katika rasimu ya katiba, na kisha yatapelekwa katika kura ya maoni ya kitaifa haraka kadri mazingira ya usalama yanavyoruhusu.
"Katiba hii mpya inakaribiana na sharia za kiislamu kuliko zilizotangulia na ni katiba inayozingatia kanuni za uhuru, usawa na haki, na kueleza kuunga kwake mkono kwa taifa la Somalia lisilogawanyika na lililounganishwa," Hussein alisema.
"Tatizo linatokana na ukweli kwamba Wasomali wengi hawajasoma kabisa katiba mpya na hivyo kudhania ya kwamba iko mbali na mafunzo ya sharia ya Kiislamu," alisema, akiongeza kwamba Wasomali wanapaswa kusoma na kuielewa katiba mpya kabla ya kuikosoa.
Omar Abdirahman, mwanafunzi wa ualimu wa Kiislamu huko Mogadishu, alisema kitabu kitakatifu kinatosha kuhudumia katiba ya Somalia.
"Watu wa Somalia ni Waislamu kwa asilimia 100 na wana katiba kamili ya kimbingu, ambayo ni Qur'an takatifu, na sidhani kama kuna haja ya kufuata katiba hii yenye utata," alisema.
Abdirahman aliuliza, "Kwanini hatuamui Qur'an kuwa msingi wa utawala badala ya kujishughulisha na katiba ambayo inasababisha utata huo mkubwa"?
Lakini Omar Abdiqadir, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na profesa wa chuo kikuu anayeishi huko Mogadishu, alisema ridhaa ya katiba mpya ni hatua ya kihistoria kwa siku zijazo za Somalia.
"Ninatumai kwamba katiba hii inaipeleka Somalia katika mwelekeo unaofaa na hivyo inahudumia kama ufunguo wa kujenga Somalia yenye mafanikio ambayo wananchi wake wameumia kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, vurugu, ugaidi, na uharamia na sasa ndiyo tu wanafurahia ladha ya amani na utulivu," alisema Abdiqadir.
"Umuhimu wa katiba mpya unajikita sio tu katika kuongoza katika kipindi cha siasa mpya katika nchi hii baada ya awamu ya mpito inayokaribia kuisha, lakini pia ni mkataba mpya wa kijamii ambao unarekebisha uhusiano kati ya wananchi na serikali katika maeneo yote -- ukweli ambao lazima uchukue nafasi katika akili za Wasomali wote," aliieleza Sabahi.
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Viongozi wa Somalia wamekubaliana kuunda bunge jipya na kufuata katiba mpya kwa ajili nchi kwa mujibu wa Mpango Mkuu ili kumaliza tatizo la sasa la kisiasa nchini kwa kukimaliza kipindi cha mpito mwezi ujao wa Agosti, ambapo sehemu zilizotiliana sahihi zilikubaliana juu ya kile kinachojulikana kama mpango mkuu wa kumaliza awamu ya mpito nchini Somalia ambapo kikundi cha wakuu kitachagua bunge. Mikutano yalikuwa muhimu sana na kutawaliwa na mijadala katika hali nyingi, lakini mwishowe wakafanikiwa. Baada ya miongo ya vita, Somalia inapitia katika awamu ya makubaliano ya kitaifa na amani, na kutumika kwa asasi za mpito za serikali katika mpango mkuu uliokubaliwa, na kuamua hatua za utekelezaji kabla ya mwisho wa kipindi cha mpito. Bunge liko katika mikutano mfululizo kufuata misingi ya kikatiba na watachaguliwa wabunge wanaosaidiwa na kamati ya ufundi ili kuhakikisha kuwa wagombea wanatimiza viwango vilivyowekwa katika Mpango Mkuu. Somalia iko katika siku chache tu kufikia wakati muhimu sana katika historia yake, ambapo hakuna wakati tena wa kupoteza. Somalia na Wasomali lazima wafanye kazi kwa mashirikiano na washirika wao ili kuhakikikisha kuwa mchakato ni halali, unaowajumuisha watu wote na wa wazi na chini ya uongozi wa Somalia.
Kuidhinishwa kwa katiba mpya ya Somalia ni jambo la umuhimu mkubwa kwa Somalia, na kuiongoza nchi kutoka awamu ya mpito. Miaka ishirini iliyopita, Somalia imefanikiwa kuandika katiba ambayo inaweza kuchukuliwa kama katiba ya pili ya Somalia tangu ilipopata uhuru. Katiba mpya inayochukuliwa kama ni sheria ya muda baada ya kuidhinishwa na Bunge la katiba, ambapo kutakuwa na kura ya maoni baada ya miaka minne ili iwe katiba rasmi, na kuchukuliwa kuwa ndio sheria ya nchi. Viongozi wahusika walioandika rasimu ya katiba mpya walikabiliwa na changamoto muhimu wakati wa kipindi cha matayarisho, na wamefanyakazi kwa makini ili kuvuka vikwazo hivyo na kufikia mwisho.
Ni hatua ya mbele. Hakuna katiba ulio nzuri asilimia 100. Hivyo utarekebishwa baada ya wakati kupita. Sehemu mbaya utabalidishwa na ulio nzuri.