Kenya yaharakisha upatikanaji wa mashine ya usajili wa wapiga kura kieletroniki.

Na Bosire Boniface huko Garissa

Agosti 09, 2012

  • 3 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kenya iko katika harakati za kutekeleza mfumo wa usajili wa wapiga kura kieletroniki kwa mara ya kwanza katika nchi hiyo katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao , uliopangwa kufanyika tarehe 4 Machi, 2013 .

  • Mawakala wa Uchaguzi nchini Kenya wanahesabu kura katika kituo cha Michezo cha Kimataifa cha Moi jijini Nairobi. Kenya itatekeleza hivi karibuni  mfumo  mpya wa usajili wa wapiga kura kieletroniki. [Simoni Maina/AFP].

    Mawakala wa Uchaguzi nchini Kenya wanahesabu kura katika kituo cha Michezo cha Kimataifa cha Moi jijini Nairobi. Kenya itatekeleza hivi karibuni mfumo mpya wa usajili wa wapiga kura kieletroniki. [Simoni Maina/AFP].

Serikali imekubali kukata utepe mwekundu unaozuia upatikanaji wa kivunge cha Usajili wa Wapiga kura Kibiometriki (BVR) kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Uingiliaji kati huo umekuja baada ya EABC kusimamisha zabuni ya shilingi bilioni 3.9 (dola milioni 47) ili kupata kivunge cha BVR, ikiweka kipingamizi cha muda, taratibu ngumu za ununuzi na kuingilia kati kisiasa.

Mfumo huu mpya utabadili usajili wa wapiga kura kwa mkono kuhakikisha uchaguzi wa amani, huru na wa haki, Rais Mwai Kibaki aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu (tarehe 6 Agosti) baada ya kufanya mkutano na maofisa wa IEBC Ikulu. Waziri Mkuu Raila Odinga na maofisa wengine wa serikali wa ngazi ya juu pia walihudhuria mkutano huo.

Kibaki alisema serikali itaharakisha mchakato wa kupata kivunge cha BVR kutoka kwenye nchi ambazo tayari zilisharidhia mfumo huo.

Tangazo la serikali limekuja siku moja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton kuwashauri Wakenya kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha uchaguzi wa rais unakuwa wa wazi na wa haki, na kuepuka kurudia vurugu zilizosababisha mauaji za uchaguzi uliopita wa mwaka 2007.

"Hii sio muhimu kwa watu wa Kenya tu, lakini macho yote duniani yatakuwa katika uchaguzi huu. Na nina imani kubwa kwamba Kenya ina nafasi ya kuwa mfano kwa mataifa mengine, sio hapa Afrika tu bali duniani kote," Clinton alisema.

Katika uchaguzi mkuu ujao, Wakenya watamchagua rais, maseneta, magavana wa majimbo, wabunge, wakuu wa kata na wawakilishi wa wanawake wa majimbo.

Mwenyekiti wa IEBC Ahmed Issack Hassan alisema mashine ya uandikishaji wa kielektroki itachukua data za sehemu muhimu za mwili kuhusu raia, kama vile sura, jiometria ya kiganja, mboni na alama za vidole.

"Wakati wote tumekuwa tukipigania teknolojia mpya lakini tunazuiwa na urasimu wa ununuzi na ushindani wa zabuni ambavyo vinazuia muda wetu tuliopanga, lakini tunafurahi serikali imekubali kupata kifaa cha kielektroni kwa niaba yetu," aliiambia Sabahi.

Hassan alisema serikali inakutana na makampuni kutoka nchi mbalimbali, ikiwemo Kanada ili kupata kifaa hicho, ambacho anatarajia kitapatikana mwezi huu ili uandikishaji uweze kuanza mapema mwezi ujao.

Mchakato mpya utaondoa kadi za mpiga kura zinazochosha ambazo ni gharama kupata na rahisi kuzibadilisha, Hassan alisema. IEBC inatarajia kuandikisha watu zaidi ya milioni 10 kupitia mfumo mpya, alisema.

"Tunatumaini serikali itapata vifaa kwa wakati ili kuwahi muda wa mwisho wa uandikishaji wa wapiga kura. Hata hivyo, tumeiomba serikali kuongeza kipindi cha uandikishaji ili kila mtu mwenye kitambulisho apate nafasi ya kushiriki kupiga kura kama haki yake," alisema.

Harakati za kufunga uandikishaji wa wapiga kura siku 45 kabla ya kura

Katiba inaonyesha kwamba uandikishaji wa wapiga kura unatakiwa kukamilika siku 90 kabla ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utekelezaji wa Katiba Abdikadir Mohammed aliiambia Sabahi kwamba wiki lijalo ataanzisha marekebisho ya sheria za uchaguzi ili kuongeza muda wa uandikishaji wa wapiga kura.

"Tutaomba muda wa kufunga uandikishaji wa wapiga kura kupunguzwa kutoka siku 90 hadi 45 ili kuruhusu IEBC kuandikisha wapiga kura wengi iwezekanavyo," aliiambia Sabahi.

Mohammed alisema Wakenya wengi wanaunga mkono uandikishaji wa kielektroniki kama njia ya kuzuia uandikishaji unaokiuka sheria na kuzuia mwanya wa kiusalama katika mfumo wa usio wa kielektroniki.

Khalif Abdi Farah, Mratibu wa Northern Forum for Democracy, aliiambia Sabahi kwamba ingawa mfumo wa kielektroniki unakaribishwa, utaweza kuwa hasara kwa jamii za wafugaji.

"Tunaamini IEBC itatafuta njia ya kuanzisha mfumo wa uandikishaji kwa njia ya simu ya mkono kutafuta familia za wafugaji wanaohamahama na mifugo yao," alisema.

Alisema pia kwamba IEBC ni lazima kuongeza idadi ya vituo vya uandikishaji kuhakikisha kwamba watu wengi iwezekanavyo wanajiandikisha.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 11)

Dislike_icon(1)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Hector Ruzaro
    October 4, 2012 @ 09:54:47AM

    Uchaguzi wa Kenya...Inawezekanaje kwa kampuni iliyoshitakiwa kwa rushwa na bado inatoa vifaa? Sagem 'Canada' (ambayo pia ni Safran) inatoa teknolojia hiyo. Mungu wangu!

  • john okumbe
    August 13, 2012 @ 04:15:34PM

    Ninakubaliana ma mwenzangu Bwana Jeremy. Kwa nini hatuongei na nchi kama Ghana badala ya kuenda Canada?

  • JeremyP
    August 10, 2012 @ 03:34:45AM

    Kuna mgongano katika maelezo ya Rais Mwai Kibaki na Ahmed Issack Hassan wa IEBC. Kibaki alisema:- “serikali kwanza itaharakisha mcchakato wa kukipata kifaa cha BVR KUTOKA NCHI AMBAZO ZIMESHAFUATA MFUMO HUO,” Hassan alisema:- “Serikali inakutana na MAKAMPUNI KUTOKA NCHI KADHAA, IKIWEMO KANADA ILI KUVIPATA VIFAA HIVYO.” Inaonesha Serikali inaonelea bora kupata kifaa ambacho tayari kipo kutoka nchi nyengine ya Kiafrika. Ikiwa ndio hivi, nafikiria hii itakuwa ni Ghana ambako wamefanikiwa vizuri sana kutayarisha uandikishaji wa wapiga kura na kifaa chenyewe hakihitajiki tena kwa hivyo kifaa kitapatikana mara moja. Ikiwa IEBC inafikiri wanao wakati wa kukinunua, kukipata na kukiweka na programu zake itachukua muda mrefu zaidi. Je, Hassan hafikiri kuwa “kampuni ya Kanada aliyoizungumzia ni Code Inc NA KWAMBA KAMPUNI HII (iliyopedekezwa na Hillary Clinton Jumamosi iliyopita) INAFILISIKA?

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo