Agosti 07, 2012
Mwaka mmoja baada ya Jeshi la Taifa la Somalia, kwa msaada wa Misheni ya Umoja wa Afrika (AMISOM), liliwalazimisha al-Shabaab kutoka vituo vyao maalumu mjini Mogadishu, wakaazi walisherehekea uimarikaji wa usalama na maendeleo katika miundombinu ambayo jiji limenufaika navyo.
Mwaka jana ulikuwa ndio kipindi kirefu zaidi cha amani kamili tangu kuporomoka kwa serikali ya shirikisho hapo mwaka 1991, AMISOM ilisema katika taarifa iliyotolewa hapo Jumanne (tarehe 7 Agosti), siku moja baada ya sherehe za maadhimisho.
Wananchi wa Somalia. wanasiasa na washika dau mbalimbali walisherehekea mwaka mmoja wa kuondolewa al-Shabaab hapo Jumatatu kwa maonesho ya muziki na watu kupeperusha bendera ya rangi bluu na nyeupe ya Somalia.
Katika maandamano ndani ya uwanja wa Michezo wa Konis, Raisi Sheikh Sharif Sheikh Ahmed aliishukuru AMISOM na majeshi kutoka Ethiopia " kwa kutusaidia kumponda adui yetu pamoja".
Siku ya Jumatatu usiku, Ahmed aliandaa chakula cha usiku katika kasri la rais mjini Mogadishu kwa makamanda wa juu wa jeshi la Somalia, baraza la mawaziri na Naibu Waziri Mkuu Hussein Arab Isse, ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi.
Alisisitiza mafanikio ya Somalia, na kutaja usalama unaonenea mjini Mogadishu, kuidhinishwa kwa katiba mpya na uteuzi uliobakia wa bunge jipya, Radio ya BAr-Kulan inayofadhiliwa na UN iliripoti.
Nur Ali Kulmiye, mmiliki wa duka katika soko la Suqa Bakaraha, aliiambia Sabahi kuwa mambo mengi yamebadilika tangu tarehe 6 Adosti 2011.
"Al-Shabaab ilisabababisha dhiki na huzuni kwa wananchi wakati ilipokuwa inaidhibiti Mogadishu," alisema. Soko lilikuwa kitovu cha fedha kwa operesheni za al-Shabaab mjini Mogadishu wakati huo. Tangu walipoondolewa, usalama umeimarika vya kutosha na biashara inanawirika.
"Kwa kweli, unaweza kuona tafauti kubwa baina ya [maisha] sasa na wakati al-Shabaab ilipokuwepo hapa," Kulmiye alisema.
"Wakati Somalia inaadhimisha siku hii muhimu na inajitayarisha kumaliza kipindi cha mpito, Misheni ya Umoja wa Afrika Somalia utaenedelea kufanya kazi na viongozi wa Somalia kuweka mazingira yatakayopelekea kuzidisha mjadala wa kitaifa na machakato wa maridhiano," alisema Mwakilishi Maalumu na Msemaji wa Kamisheni ya Umoaja wa Afrika Somalia Balozi Boubacar Diarra, akithibitisha tena juu ya wajibu wa Umoja wa Afrika katika mchakato wa amani ya Somalia.
"Katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi, na kwa vile vikosi vya AMISOM vinaendelea kusaidia kuyakomboa maeneo zaidi ya nchi, tunawataka viongozi wa Somalia kuendelea kuwa na umoja na kuweka maslahi ya taifa kwanza," alisema.
Al-Shabaab ikiwa haidhibiti tena, Mogadishu imeshuhudia ongezeko la ujenzi kwa vile Wasomali walioko uhamishoni wanarejea kujenga upya nyumba zao, hoteli na biashara .
Masoko yamekuwa yakifunguliwa upya, shule na hospitali kuanzishwa na taa za umeme wa jua kuwekwa katika barabara kuuza Mogadishu . Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde umekarabatiwa na wasafirishaji wa kimataifa kama vile Shirika la Ndege la Uturuki, yanaendesha safari za kawaida ndani na nje ya jiji.
"Siku ya terehe 6 Agosti ni muhimu sana ambayo itakumbukwa na kusherehekewa," alisema Yusuf Abdi Roble, mkazi wa Mogadishu mwenye umri wa miaka 42 , aliiambia Sabahi. "Ni siku ambayo Mogadsihu iliepukana na al-Shabaab, adui wa amani ya Wasomali."
Roble alisema sasa wanamgambo wako katika pumzi zao za mwisho na vikosi vya usalama lazima viendelee na shinikizo la kijeshi ili kuikomboa nchi yote.
"Al-Shabaab karibu itamalizwa. Wamekuwa wakiondolewa kutoka maeneo mengi ya nchi," alisema. Sasa operesheni lazima zizidishwe dhidi yao ili kuikomboa Somalia yote."
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
Sampuli ya DNA iliyochukuliwa kwenye mswaki uliokuwemo kwenye begi lililokuwa na risasi lililopat...
Wakenya kumi na wasaba wameshtakiwa kwa kuvunja amani, kufanya ghasia na ukatili dhidi ya wanyama...
Al-Shabaab imedai kuhusika na urushwaji wa makombora kwenye kasri ya rais mjini Mogadishu siku ya...
Wanajeshi wa Uganda wa Kikosi Namba 9+ wanarudi nyumbani baada ya kukamilisha miezi 13 ya ziara y...
Kikosi cha polisi cha Kenya kitaanza uhakiki wa kina wa maofisa mwezi ujao, kikianza na kusaili w...
Ujambazi ulizuiwa katika ofisi za usalama za Wells Fargo huko Mombasa ulisababisha kifo cha watu ...
Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliahidi msaada wa nchi yake katika kipindi cha ujenzi mpya wa ...
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Kuna vitu muhimu vya kupambana na ugaidi kwa kuimarisha uwezo wa vikosi vya usalama, na kusababisha pigo linalouma kwa magaidi na kuharibu mitandao yao. Pamoja na kufuata mpango wa kuzawadia pesa kila mtu anayechangia kutoa habari kuhusu magaidi, na kujenga utamaduni, elimu, uchumi, na uungaji mkono kimorali na ujenzi wa jamii kiimani. Serikali ya Somalia leo inadai kuzihusisha asasi zote za jamii katika utekelezaji wa mkakati wa kupambana na ugaidi, kila mtu katika uwanja wake unaomhusu. Hata katika ngazi ya elimu, kungekuwa na aina ya elimu katika viwango vyote vya shule inayolenga juu ya ubaya wa vitendo vya kigaidi na kulinda utakatifu wao katika ngazi ya dini na jamii na taifa. Pia ielekezwe katika kuimarisha usalama wa kitaaluma, kwa sababu ugaidi ni matokeo ya mawazo yalioachana na maadili. Magaidi mara nyingi hutegemea kueneza mawazo ambayo yanaathiri msimao wa jamii ili kutaka waungwe mkono.
Kukiwa na utumiaji nguvu ambao unashuhudiwa ndani ya nchi jeshi nguvu zake hujaribu kuzuia watumiaji nguvu hao na hutoa muhanga roho za wanajeshi wake kwa ajili ya utulivu na usalama na amani na kila siku tunasikia kwenye vyombo vya habari vya kusikiliza kutazama na kusoma kile ambacho wanatoa thamani yake wanajeshi na kupoteza roho na zana na uokoaji wa kila siku wa wale waliotekwa nyara na maharamia na magaidi, kwa hivyo salam ya heshima iwaendee wanajeshi wa Somali.
nimefarijika sana kusikia habari hizi,muda sio mrefu hali somalia yote itakuwa imekombolewa kutoka kwenye makucha ya maadui
Naamini Somalia inao uwezo wa kukua na hatima yake inaonekana kunawiri zaidi kuliko ilivyokuwa miaka kumi iliyopita. Kuna sababu kadhaa za kuwa na matumaini chanya kuhusu hatima ya Somalia. Kitu cha kwanza ni kuwa serikali inafanya kila iwezacho ili kuhakikisha kunakuwa na amani nchini. Pia inajaribu kukimaliza kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab ambacho kimekuwa kikwazo katika uchumi wa nchi. Watu wa Somalia pia wanataka kuijenga upya nchi yao na wakimbizi wanarejea nchini kwao kwa shughuli za kuinua uchumi wao. Serikali ya Somalia pia inayataka mashirika ya kimataifa kuja kuwekeza nchini, ambao baadaye utainua uchumi. Kumekuwepo na shughuli nyingi zinazoendelea za kuimarisha miundombinu kama vile ujenzi wa barabara, shule, hospital na huduma zingine za kijamii. Mawasiliano yanaimarishwa na Somalia inaungana na dunia na wataweza kufanya biashara duniani kote.
Sisi huku Kenya tunawatakia majirani zetu, watu wa Somalia, kila la heri katika juhudi zao za kurejesha amani na mafanikio katika nchi yao iliyoharibiwa na vita. Amani, utulivu na mafanikio siku moja vitafaidiwa katika Jamhuri ya Somalia ambapo wanawake na watoto wa Somalia wataishi na kutembea bila ya kuogopa mauaji yasio na hisia.
Inafurahisha kusikia hivyo.
Ni habari njema sana kusikia ndugu zetu wa somalia wakiishi kwa amani baada kuondoa maadui wa amani,E Mwenyezi Mungu wabariki majeshi ya umoja wa Afrika(AMISOM).majeshi ya Ethiopia na majeshi ya serikali ya Somalia mmefanya kazi kubwa sana
Kwanza, natamani Somalia kuwa na kurejea katika njia yake ya maendeleo lakini hili litaweza kufikiwa kwa kutubu kwa Mungu, kuepuka dhuluma na kutoa haki sawa kwa wote. Lazima tutubu kuwagawa watu, ukabila na kuacha masuala yote mengine maovu. Tulilinde taifa letu katika umoja. Wale waliopewa dhamana lazima wazitekeleze kwa niaba na kwa kumuogopa Mungu na sisi pia tuwatii wao. Somalia inapaswa kujali maslahi yake na kuwazuwia wageni kujihusisha katika masuala ya Somalia. Ikiwa tutakuwa wakweli baina yetu wenyewe, hakuna mtu atakayetukosea. Asanteni.