Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |
Agosti 07, 2012
Al-Shabaab wanatumia gazeti la mtandaoni ili kuwajaza hofu Wakenya na kuwahamasisha wapiganaji wake waliokata tamaa baada ya kukabiliwa na msururu wa kushindwa na kuasi , maafisa usalama na wachambuzi wa Kenya wasema.
"Gaidi Mtaani" kwa Kiswahili, lilianzishwa mwezi Aprili na limekwishachapisha matoleo mawili ya Kiswahili na Kiingereza. Mhariri wa gazeti hili alisema limepata msukumo kutokana na kutiwa moyo na gazeti la mtandao wa tovuti la Kiingereza lililochapishwa na al-Qaeda katika Rasi ya Uarabuni.
Katika toleo lake la kwanza, Gaidi Mtaani lilidhihaki operesheni Linda Nchi ya Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), maana yake "Linda Nchi" kwa kuigiza operesheni yao hiyo kuwa ni "Linda Uislamu"
Kundi hilo liliapa kupata ushindi mkubwa juu ya vikosi vya Somalia na vya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM), likiweka kwenye jalada katika toleo lake la kwanza picha ya mtu anayetazamana na Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Kenyatta jijini Nairobi, akiwa ameshikilia maguruneti mawili nyuma yake.
Maofisa usalama waliiambia Sabahi kuwa wanafuatilia gazeti hilo na watawasiliana kupitia vyombo vya habari vya ndani kuondoa uongo wowote unaoshapishwa na kundi hilo.
Serikali imewataka raia kuwa waangalifu zaidi na kufanya kazi kwa kushirikiana na vikosi vya usalama kukabili vitisho hivyo, alisema Ofisa wa Wilaya ya Dadaab Bernard Ole Kipury.
Hakuna kilicho kipya katika maudhui ya gazeti hili la mtandao wa tovuti, alisema, al-Shabaab inarejeleza vitisho vya kushambulia majengo ya serikali na raia. "Baada ya matoleo mawili au matatu, wataondoka kwenye mawazo hayo na watatapika ujumbe wa aina hiyo mara kwa mara," alisema.
Kipur aliambia Sabahi kuwa al-Shabaab haitafuti tu kupata askari wapya na wanaowaonea huruma, lakini pia kufanyia watu ugaidi katika nchi zinazozungumza Kiswahili, kama vile Kenya, Tanzania, Uganda na sehemu za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.
Alisema gazeti hilo linaonyesha kuwa al-Shabaab imedhibitiwa na inakimbilia hatua zisizo na matumaini kutafuta hatma.
Al-Shabaab inachapisha kwa Kiswahili kuvutia hadhira kubwa baada ya kukabiliwa na kushindwa kwa mfululizo Somalia, Kipury alisema.
Al-Shabaab wamepoteza ngome nyingi nchini Somalia kwa miezi mingi iliyopita, ikiwa ni pamoja na Beledweyne , Baidoa , Hudur , Afgoye na Balad. Zaidi ya hayo, serikali ya Somalia ilitoa msamaha kwa wapiganaji wa zamani waliohimizwa uharibifu mwingi kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabaab.
Matukio mengi ya hivi karibuni katika magazeti yanaonyesha barabara iliyoharibika katika vichwa vya habari, "Barabara ndefu kuelekea Kismayo".
Majeshi ya Somalia na AMISOM yanatarajiwa kukamata jiji la kimkakati la Bandari ya Kismayo wakati wowote ndani ya mwezi Agosti.
"Kutekwa kwa jiji la Kismayo hakutahitimisha mujahedeen ya al-Shabaab, lakini badala yake kutakuwa mwanzo wavita vya muda mrefu vya kidini dhidi ya Kenya," gazeti lilieleza.
Wachambuzi wanasema uamuzi wa al-Shabaab kutumia matukio ya suala la pili katika kuzuia upotevu wa ngome yao kuu ya mwisho unaashiria kwamba kundi hilo limepatwa na msukumo mkubwa. David Ochami, mwandishi wa habari anayeishi Mombasa anayeandika kuhusu vitendo vya kundi la wanamgambo katika Afrika ya Kati na Pembe ya Afrika katika gazeti la The Standard, alisema al-Shabaab hawawezi kuamini kwamba wametupwa nje ya ngome yao na wanajeshi ambao awali waliwatoa kwa dharau.
"Kismayo ni kambi pekee iliyobaki na kundi linajaribu kugeuza mtazamo. [Kismayo] ni mahali ambapo [al-Shabaab] wanatunza silaha zao na kama itatekwa, [al-Shabaab] itaishiwa nguvu," aliiambia Sabahi.
Mgawanyiko wa ndani umedhoofisha kundi kwani limepoteza wapiganaji wengi ambao wametoroka kwa usalama wao au kwa sababu ya kudhoofika kwa vivutio vya kifedha, alisema Ochami.
Mashambulizi ya kijeshi dhidi ya al-Shabaab hayatakiwi kusimama sasa, licha ya mashambulizi ya kikundi kwa wananchi, alisema.
Katika miezi ya hivi karibuni, al-Shabaab wamekuwa wakiwalenga wananchi katika mfululizo wa mashambulizi ya mabomu ya ardhini na ya kutupwa kwa mkono, ikiwa ni pamoja na mashambulio ya makanisa mawili huko Garissa tarehe 1 Julai ambayo yaliua watu 17 na kujeruhi zaidi ya watu 60. Tarehe 18 Julai, i al-Shabaab walivamia kinyozi na hotel huko Wajir, na kujeruhi watu wanne .
Ochami alisema Wakenya wanapaswa kutoruhusu al-Shabaab kuwazuia katika kazi zao za kila siku.
"Kwa sasa, Wakenya wanajua vizuri kuhusu madhara ya vita hizo lakini mashambulizi ya mabomu ya ardhini na ya kutupwa kwa mkono kwa wananchi na waumini ni kiashiria cha wazi kwamba al-Shabaab ni jeshi lililochoka," alisema.
Meja mstaafu wa KDF Bashir Hajji Abdullahi alisema al-Shabaab wanatumia magazeti kujaribu kuokoa nyuso zao na kuandaa wapiganaji wao waliovunjika moyo kwa uharibifu wa baadaye wa Kismayo.
"Dunia inajua kwamba KDF [imesaidia] kukomboa Afmadow na majeshi ya Somalia na AMISOM wamekomboa miji mingi na majiji. Kundi limetegwa na linajaribu kuongeza morali," alisema.
Abdullahi aliiambia Sabahi kwamba kundi linawapotoa wananchi kwa madai ya kupigana kwa jina la dini. Alisema kundi hilo linapaswa kufukuzwa kwa dharau.
Katika toleo la kwanza la Gaidi Mtaani, al-Shabaab walisema Kenya wamekuwa maadui wa Uislamu mara ilipoamua kuwapeleka wanajeshi Somalia.
Lakini Abdullahi alisema wanamgambo wa al-Shabaab hawawezi kudai kuwa Waislamu wa kweli wakati wanaua wananchi wasiokuwa na hatia na Waislamu wenzao.
Alisema viongozi wa kisiasa wa Somalia, majeshi ya kutumia silaha ya Somalia na wananchi ambao wanamgambo wanawalenga ikiwa ni pamoja na Waislamu ambao wameungana dhidi ya vitendo vya kutisha. KDF pia inao Waislamu katika jeshi lake, aliongeza.
Kamishna wa Jimbo la Magharibi James ole Seriani alisema al-Shabaab hawawezi kudai kuitetea Somalia kutokana na tuhuma za kigeni kwa kuwa inaunganisha wageni katika ngazi zake ambao wanaua Wasomali wasiokuwa na hatia.
Wasomali wanakaribisha ushirikiano na AMISOM baada ya kupata shida kwa muda mrefu, alisema. "Kama [al-Shabaab] wanatetea Uislamu dhidi ya makafiri kama wanavyodai, hatutegemei kuona matukio ya shangwe yanayofanywa na Wasomali katika mijiji mikuu na miji midogo iliyokombolewa kutoka kwa magaidi," alisema.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Uko wapi udugu ikiwa al-Shabaab wanaua Waislamu wenzao? Jihadi sio kuua wasio na hatia.
Hawa al-Shabaab wanataka kujenga hofu kwa Wakenya na pia kuwarubuni vijana kwa kuwaonyesha kuwa wao bado ni imara, ambayo si ya kweli. Kwa kweli ni watetezi wao.
Al-Shabaab lazima walipe ghali sana kwa kuwaua mashujaa wetu. Hongera KDF, AMISOM na TFG. Endeleeni kijeshi.
Waw,Alishabaab wanaume washoka,nchi ngapi zimepeleka majeshi Somalia?Mbona mnazungumzia Kenya tu.Waulizeni wamarekani walifanyiwa nini huko leo wameogopa kichapo,wanawatuma vibaraka kama Kenya,burudi,Uganda na kadhalika.Ninyi mnao lalamika bila shaka mmeanza kuonja keki ya wanaume Alshabaab.Wambie viongozi wenu warudishe majeshi nyumbani.Alshabaab itawapa hasara.
Kama ikiwa hawa al-Shabaab ni wanaume wa kweli kweli, wajitokeze na kupambana na KDF kuliko kujificha mashimoni kama mapanya. Wasafisheni.
Tunachotaka ni amani tu.
Wenye misimamo mikali na magaidi wanapaswa kuelewa kuwa wanapigana vita ambavyo tayari wameshindwa.
Hili ni suala kwa nchi zote za Afrika ya Mashariki ambazo zipo karibu na Kenya na tafadhalini, ACHENI.
NINGEPENDA KUWASHAURI ASKARI WA KENYA KUSITISHA MAPAMBANO DHIDI AL–SHABAAB KWA SABABU WATALETA MATATIZO MAKUBWA NDANI YA TAIFA LA KENYA NA WATU WASIO NA HATIA BADO WATAULIWA AMBAPO KIONGOZI WA JUU HUJIFICHA TU. ACHENI KUFANYA HIVYO.
NZURI, BAADHI YA MAONI YAMEANDIKWA KIHESHIMA. HATA HIVYO, UISLAMU AU UKRISTO SIO WA KULAUMIWA. LAWAMA NINAZIPELEKA KWA KILA BINADAMU ANAYEJARIBU KUMUUA RAIA, IWE NI ISRAEL AMBAYO INAUA WAPALESTINA MASIKINI. SIMAMISHENI VITA.
Al-Shabaab kwa sasa ni farasi anayekata roho. Karibu itakuwa wakati uliopita.
Waacheni wote waingie motoni. Hawana nafasi hapa duniani.
Niiwachukia al-Shabaab kwa matendo yake ya uuaji. Kufikiria kuwa watarithi utawala wa mbinguni kwa kuua watu wasio na hatia, ninawaahidi jehanamu. Waelewe kuwa wao ni walioshindwa.
Hatutatembea pekee yetu.
NI BAHATI MBAYA KUWA KIKUNDI HIKI KINATAKA KUGEUZA AJENDA YAO YA UCHOYO KUONEKANA KAMA VITA VYA KIDINI BAINA YA WAISLAMU NA NDUGU ZAO WAKRISTO. NILISOMA KATIKA SHULE YA KIISLAMU NA NINAWAELEWA KWA KWELI NDUGU WA KIISLAMU WANAHESHIMU MAISHA NA KILE MWENYEZI MUNGU ANACHOSEMA WANAKITEKELEZA. TUUNGANE PAMOJA KATIKA UNDUGU WA KWELI LICHA YA TOFAUTI ZA DINI ZETU.
Hebu hebu! Muislamu, Mkristo, Msomali, Vikosi vye Silaha na Visivyokuwa na silaha ... Zingatieni hili, "YULE AMBAYE AMEKAMATA KAA LA MAWE MKONONI MWAKE NA KUJARIBU KUMRUSHIA ADUI YAKE, HUUNGUZA MKONO WAKE MWENYEWE." Ninaiangalia Somalia kwa jicho kali kama kitovu cha kiuchumi katika kanda hii ya mashariki. Hatutakuwa na haja ya kusafiri kwenda Dubai, Somalia ina uwezo ambao haujatambuliwa kutokana na bandari zake na kuungana kwake na Ghuba na Mashariki ya Kati na Asia kwa njia ya bahari. Ninataka kuona barabara kuu imefunguliwa kwa Wakenya wanaothubutu, Wakikuyu, mfanyabiashara wa Meru na mabasi ya Somalia yanayosafiri kila siku kutoka Garissa, Wajir kupitia Korbio, Kiunga hadi Ras Kamboni na miji mingine ya jirani nchini Somalia. Dira hii inakwamishwa na tatizo sawa na vita vinavyotugharimu sana za AMISOM na Oparesheni Linda Nchi. Kile kilichomo katika ubongo wako ndio hicho hicho unachoweza kutoa, kwa vile safu za Al-Shabaab wana vita na mafundisho ya Koran kwa Kiarabu. Ikiwa unafikiri kwamba elimu ni ghali, hebu jaribu ujinga, ndivyo utakavyoona (ujinga) katika safu zao. Elimu huwapa watu uhuru na uwezo wa kufikiri. Ni ujinga gani huu wa kuitawala dunia na waumini wa Kikristo? Mungu wangu!Ni nani anayeendeleza ujinga huu? Wewe utakuwa nani kati utawala huo? Na baadaye itakuwaje? Na bado mnawafundisha za waumini kuenda peponi kutoka katika utawala huu? AMISOM au njia nyengine bora zaidi wanahitaji kubakia huko hadi akili hizi zikombolewe kutoka ujinga huu. Watawaleni na mlazimishe elimu nchini Somalia ili akili hizi masikini ziweze kuwa za maana kuliko njia ya wanavyohasarishwa na ujinga na kutusababishia matatizo haya.
Al-Shabaab, ni kikundi kizuri cha wanajihadi. Siku moja wataiteka Kenya na ardhi ya Ethiopia, watawaadhibu wanajeshi wote waliopigana dhidi ya jamii ya Waislamu. Kwa upande mwengine, kwa nini watu wasio na hatia wa Palestina wanauliwa kila siku na serikali ya Israel bila ya kuuita uhalifu?!! KDF hawatawakomboa al-Shabaab kutoka Somalia, bali wataiteka Somalia. Kwa hivyo Wasomali wote watasimama bega kwa bega na al-Shabaab ili kuilinda nchi yao kutoka kwa adui wao Nambari 1 (Kenya na Ethiopia).
Uelewe ukweli na ukweli utafanya uwe huru.
Al-Shabaab sasa wanasagwa. Ni suala la wakati tu kwa Kismayu kuangukia kwa KDF na AMISOM. Vitengo vya kiitelijensia pangeni tu mchezo na amani itatawala. Katika vita kama mtaua wanawake na watoto mtalazimika kushindwa.
Naona al-Shabaab wanakabiliwa na jaribio la damu yao. Walifikiria KDF kilikuwa kikosi kisicho na uzoefu, lakini sasa wanalipa, matendo yao yanawatokea puani. KDF na AMISOM ongezeni kasi ya kuwatoa al-Shabaab ndani ya Somalia na kurejesha amani katika nchi iliyoharibika kwa vita.
alshababiin sare gur chira
Mtu anayeruhusu umwagikaji damu na anayeendeleza mdundo wa mauaji ya mwanamke na mtoto asiye na hatia, na baadaye anadai anafanya hivyo kwa misingi ya Uislamu au Ukristo, huyo ni mpotoshaji asiye na malezi yoyote ya kidini. Hakuna dini inayoruhusu kifo kwa watoto na wanawake wasio na hatia na viumbe vya Mungu. Inalinda maisha. Haijalishi kama ni damu ya Mkenya au Msomali. Mimi ni mmoja ambaye nisingepoteza usiku hata mmoja bila ya kulala ikiwa watu kama hao watakamatwa, kushitakiwa kwa haki, kuhukumiwa kifo na kunyongwa hadi roho zao za uovu itoke mwilini mwao.
Waliahidi kuwa watakuwa nazi ngumu kuweza kuivunja kwa kutilia maanani kuwa vita walivyopigana huko nyuma vilionesha kuwa watu wenye uzoefu. Kwa nini wanaendelea kuwakimbia wenzetu wanaosonga mbele kuelekea mstari wa mbele?
Mojawapo ya maamrisho kumi inasema kuwa usiue, kwa nini al-Shabaab wanaua watu wasio na hatia? Hawataingia katika Ufalme wa Mungu. Wamepotea. Mungu awaoneshe njia iliyo sahihi.
Siwapendi al-Shabaab kwa matendo yao ya kinyama ya kuua watu wasio na hatia kwa jina la dini. Mwenyezi Mungu aziguze nyoyo zao ili waache kuwadhuru watu wasio na hatia.
NI WAKATI SASA KWA WATU WA SOMALIA KUWA HURU KAMA NCHI NYENGINE YA KIAFRIKA. NI WAKATI WA KUIJENGA NCHI YAO KAMA WATU WA RWANDA NA SIO KUKIMBILA NCHI NYENGINE. NI WAKATI WA KUANGALIA NINI CHA KUFANYA BAADAYE NA SIO KWENDA MAREKANI NA AUSTRALIA. SIKU ZOTE UTAWAONA KATIKA HIZI MASHIRIKA KAMA I.O.M WAKITAFUTA VIZA. NI WAKATI WA KUJENGA NCHI YENU. ACHENI.
Sio rahisi kuimaliza al-Shabaab hii, wanavaa kama mwanamke/mwanamme yeyote wa Kiislamu lakini wana silaha kwa hivyo kuwa na faida dhidi ya AMISOM ambao siku zote wanavaa magwanda kwa hivyo kuwatambua kirahisi.
Mungu kamuumba binadamu katika ardhi ili kuiimarisha na kuishi kwa usalama juu yake na watu wengine kwa mapenzi na huruma na kwa usalama na amani na utulivu, lakini kujitokeza kwa baadhi ya vikundi mbalimbali vinavyojiita magaidi ili kuweza kutia hofu katika mioyo ya watu huu sio usalama kabisa hivyo lazima mlinganiaji wa kiislamu anaye waongoza watu na kuwakumbusha mambo ya dini yao lazima awaongoze katika njia sahihi isiyokuwa na madhara wala isiyodhuru wingine na pia awalinganie katika kusamehe na amani kati yao.
Ugaidi ni jambo jipya ambalo lilikuwa halijulikani hapo mwanzoni, wapi limeanza? na limeundwa vipi? na nani analifadhili? hakuna mtu anayejua, lakini kinachofahamika ni kwamba ugaidi hauna dini wala nchi, ni jambo lilionea ambalo wanatoa thamani yake watu wasio na hatia wa kila jinsia ulimwenguni kutoka kila nchi ya dunia na mfano wa karibu zaidi ni kile kilichotokea Sinai kushambuliwa kwa wanajeshi wema wasio na hatia wamepoteza maisha yao kwa ajili ya kuumaliza ugaidi kwa hivyo kila siku kunatokea utumiaji nguvu na uvunjaji sheria na ugaidi na utekaji nyara na unyanyasaji ambao wanalipa thamani yake wanajeshi wa Somali na wanainchi wa Somali kwa hivyo pongezi nyingi kwenu wanajeshi wa Somali kwani kwa jitihada zenu kubwa za usiku na mchana kwa uwezo wa Mungu mutaweza kurejesha usalama na amani nchini mwenu Mungu akubarikini na akunusuruni na ukupeni nguvu na aimarishe nia zenu na kwa mapenzi yenu Somali itarudi tena inachomoza jua la matumaini ya maisha musiache kufanya haki na uadilifu kwa kuogopa lawama za atakayelaumu ni roho ngapi zimeangamizwa na magaidi hawa hivyo mshikamano wenu unaongeza ulinzi wenu dhidi yao na mutaishi kama nchi nyingine duniani kwa usalama na amani.
Magaidi wana uchu wa kuua, uharibifu na uteketezaji. Magaidi wanachukia maisha; kwa wao, kuishi maana yake ni mauti. Magaidi wanafurahia kuwaua wananchi wote wasio na hatia ambao wanatafoutiana nao katika fikra au imani. Magaidi wanaona rahisi kumwaga damu ya watu wasio na hatia kwa kisingizo kuwa watu hawa wasio hatia ni makafiri. Magaidi wanawachukulia watu wengine wanaojaribu kuishi maisha mazuri kama walio nje ya dini; wanawachukulia watu kwa mujibu wa dini yao wenyewe, na sio kama binadamu wanaoishi pamoja. Wana akili finyu, kama walivyo watu wenye itikadi kali. Ndio wao waliotaka kuanzishwe sharia, lakini waliitekeleza vibaya. Magaidi wanafurahia kuchoma moto sehemu zozote wanazoziona, kuwua wananchi na kuwaangamiza, wakidai kuwa ni makafiri na wasio na maadili. Magaidi hawa wote wana itikadi kali, kiakili na kimwili, na hata kama hawako na kikundi chochote, wote wana akili sawa chafu.
Waacheni wauliwe hadi mwisho, jahanamu unawasubiri, wasafisheni wote.
Ninawaomba al-Shabaab kuachana na matendo haya. Si haki hata kidogo kuua wasio na hatia. Tafadhalini, tafadhalini, acheni hayo ili tuendelee kufaidi amani kama tuliyokuwanayo kwa miaka mingi.
Mim ni Mkenya mwenye asili ya Kisomali. Ninao marafiki zangu Oduori, Gaceri, Muthoni, Shikanga, Baraza and Abdalla (kwa kutaja wachache). Watu nilioenda nao shule, kula pamoja na hata kugawiana shati na mkate(na pea),(kumbuka shule za elimu ya juu)kama marafiki zangu na washikaji zangu kutoka utoto hadi sasa. Dini yangu inanifunza kuwa mwenye amani. Uislamu maana yake ni salaam au salama (amani kwa Kiswahili). Kwa hilo la al-Shabaab kuniua mimi au marafiki zangu kwa kukusudia au "kwa vya pande zote" kwa jina la Uislamu (amani) ni kinyume na kile baba yangu alinifunza na yeye alikuwa mwalimu wa dini. Nina hakika alikuwa mtu wa dini zaidi kuliko nyinyi mnaokamata bunduki na kuua wanawake wasio na hatia na kuwatoa kule wanakokuita nyumbani kwao, kwa hivyo kuwafanya wawe wakimbizi na kubakwa katika makambi...Kwa jina la Uislamu! Tafadhalini niacheni pekee yangu, iacheni nchi yangu pekee, iacheni pekee KICC yangu, waacheni pekee marafiki zangu, waacheni pekee wanawake na watoto wasio na hatia... Mmewafanya watu wateseke. Wananchi wanabaki hawana elimu, wengi wakiwa vilema, mmezuia watu wanaowatakia mema wasitoe hata madawa kwa watu dhaifu na masikini na bado mnajiita Waislamu? Hata watu wasio kuwa Waislamu wanaelewa kuwa mnasema uongo!!! Naomba huo mkaa huko Kismayu ukwishe na karibuni mtaangushwa.
Mazungumzo na diplomasia ni njia pekee za kumaliza mzozo kwa kweli. "Haiwezekani kupeana mikono na mpinzani wako, iwapo umekunja ngumi zako!!"
Nadhani serikali yetu haichukui hatua za kutosha ili kulinda watu wake kama nchi. Kwa kweli tumechoshwa na maneno matupu, tunahitaji vitendo zaidi. Hatukuwachagueni kwa hizo ofisi za juuu ili kuwasikieni mnasema nini. Tunataka vitendo. Ikiwa mngetupa ulinzi kama ule mnaojipa wenyewe, tusingekuwa tunahesabu idadi ya maiti tunazohesabu leo. Walindeni raia wenu.
Serikali iliwezeshe jeshi letu ili kuwaondoa hawa magaidi kwa ajili ya taifa lenye amani.
Waislamu watafaulu na makafiri Wakristo watatokomezwa kama ilivyoahidiwa na Mungu. Hakuna yeyote anayeweza kusimama katika njia ya jeshi la Mungu (Sifa zote kwa jeshi letu). Ikiwa Wakenya watashindwa kuwasaidia Waislamu, wao watakuwa watumishi wetu. Mungu akipenda. Makafiri watashindwa vita.
Kwa wale wanaounga mkono majeshi ya Afrika, ninawatakia maisha marefu ili muweze kufaidi matokeo ya kazi nzuri. Na kwa vikosi vya Misheni ya Umoja wa Afrika, ninasema bila ya kuwepo kwenu na msaada wenu kwa Somalia, Somalia kamwe isingefika ilipo sasa. Wasomali wote lazima waungane na kusimama pamoja dhidi ya wahalifu. Kila heri na naomba amani itawale, ili watu wajue vipi kuwa na imani kwa Mungu na sio kwa watu au mawazo.
Maandishi yapo ukutani. Al-Ashabaab inashindwa, kilichobakia ni jinsi gani ya kushughulikia mabaki yao ambao yatakuwa yanafanya shughuli zao bila ya utaratibu na pia yatataka kugawanya silaha zao. Wanaweza kusababisha kuwaletea madhara mengi raia, hata hivyo, hilo lisituzuie. Tuko kwenye vita na matokeo ya vita ni kifo. AMISOM wanapaswa kuichukua Kismayu haraka sana.
MWENYEZI MUNGU (ALLAH) AWAONGOZE WOTE KATIKA NJIA SAHIHI - MUNGU AKIPENDA.
Je, majambazi hawa kweli wanamwabudu Mwenyezi Mungu au shetani? Vipi unaua hadi watu wasio na hatia kabisa na watu dhaifu na baadaye kumshukuru Mungu kwa tendo hilo? Mnamkumbuka Sadam Hussein? Aliwaua kwa sumu ya gesi watu wake na kuliahidi jeshi lililoongozwa na Marekani kuwa vitakuwa "mama wa vita" ikiwa wataivamia Iraki na walipofanya hivyo alikimbia na kujificha kwenye shimo la mbweha. Hatimae alikuwa kwa uchungu baada ya hukumu ya mahakama. Al-Shabaab watakabiliwa na majaliwa kama hayo popote walipo na yeyote waliye pamoja nao.
Maoni mazuri. Kwa vile nina uchungu na al-Shabaan mimi pia nimevunjwa moyo na serikali yetu kwa kuruhusu Wasomali wengi kujipatia ardhi nchini Kenya hasa Mombasa, na ndio maana ni vigumu sana kuwatoa magaidi ndani ya makazi yetu... Tutawaambia nini ikiwa wataanza kukamata viti bungeni... wakati umefika wa kuanza hatua mpya ndani na warejee nchini kwao, wametumia vibaya ukarimu wetu...na wema wetu...na uchumi wetu uko chini...Rais wetu ajaye lazima atuambie anakusudia kuwafanya nini wageni hawa...
Jua ukweli kwani ukweli utakufanya uwe huru.
Hadi lini al-Shabaab watajihusisha na vita? Ni aina gani hii ya dini ambayo inawafanya watu wawe watumwa maisha yao yote? Inawezekana ni ulokole na uongo wa kidini.
Tuna imani na KDF. Itekeni Kismayu na amani itatawala nchini Somalia. Mungu yupo kwa ajili yetu na tunawaombeeni.
Kenya inatoa nafasi ambayo bado inawawezesha al-Shabaab kukamata mabua wakiwa wamekata tamaa, kwa nini msiwape kipigo cha mwisho (kuikamata Kismayu) tendo ambalo litawapelekea kutoweka kabisa.
Sababu pekee ya KDF ni kuhakikisha amani inakuwepo nchini Somalia na Kenya, hilo kwangu mimi linakubalika kwa Mungu. KDF mnashinda karibuni
AL-SHABAAB NI WAOGA KWELI.
KDF... mtu akiwa askari daima ataendela kuwa askari. Kismayu ipo karibu,...al-Shabaab wanakimbia kwa woga...Wasageni, wasageni kabisa. Tunahitaji Somalia yenye amani ya kudumu. Hatutaki al-Shabaab!
Huwezi kumuua binadamu mwingine na kuhubiri kwamba unafanya hivyo kwa jina la Mungu. Ni upuuzi. Kushindwa kwa al-Shabaab iwe somo kwa vikundi vingine vyenye akili kama hizo. KDF, wamalizeni...karibuni.
KWA MUNGU KILA KITU KINAWEZEKANA.
Haijawahi kufikiria kuwa kikundi cha al-Shabaab kwa njia yoyote ni kikundi cha dini. Sielewi ni dini gani inayoisimamia kwa sababu imani ya kweli ya Uislamu haipo kwa ajili ya kuua ndugu wenza. Wapenda amani ambao hawatetei matumizi ya nguvu pia wanakubali kuwa kikundi hiki ni sawa na Unazi na kwa hivyo lazima watakiwe kujifunza kwenye historia na kuona matokeo ya vita vya pili vya dunia. Katika jamii iliyostaarabika kwenye karne ya ishirini na moja tunaweza kushinda vita zaidi kwa upendo kuliko bunduki- Lakini bado, mtu anayeua kwa kutumia upanga, mwisho wake atakufa kwa upanga kwa kutumia sheria ya kuadhibu
Wamemalza mipango yao yote wanayoweza kufikiria. KDF muendee maeneo yao ya mwisho wanayoyashikilia.
Ni tishio kubwa lakini watafagiliwa kwa masekunde tu...
Wakati umefika wa kuipiga al-Shabaab kipigo kizito. Endeleeni KDF na vikosi vya washirika!
Bado sijajua kama kung'olewa kwa al-Shabaab ni sehemu ya DIRA YA ILIYOPOTEA YA KENYA 2030...Kwani hadithi hii ya OPERESHENI LINDA NCHI INACHUKUA MUDA GANI????????
Al-Shabaab ni sababu pekee inayowafanya Wakenya wengi wauchukie Uislamu. Vipi mnaweza kuua watu wasio na hatia kwa jina la Mungu? Hiyo sio dini. Mnasukuma ajenda yenu ya uovu tu na mumeshashindwa. KUBALINI AU KATAENI.
HATUWATAKI AL-SHABAAB.
KATIKA YOTE HAYA MWANAMKE WA KISOMALI NDIYE ANAYEPOTEZA, WANALAZIMISHWA KUZAA KILA MWAKA ILI KUFIDIA MAISHA YALIYOPOTEA VITANI NA AL-SHABAAB. WANAWAKE WANAOLEWA WAKIWA NA MIAKA 15 ILI KUZAA ZAIDI TU NA MUNGU ATUEPUSHE NAYO, IKIWA LOLOTE LINATOKEA WANAKUWA WAJANE HATA KABLA YA KUJIFUNGUA NA MARA BAADA YA KUOLEWA KWA JINA KWA SABABU WAUME HAWAONEKANI TENA. NINASHANGAA KUWA HUU NDIO MCHANGO WAKO KATIKA VITA, KWA HIVYO HII NI GHARAMA KUBWA WANAYOLIPA DADA ZANGU. NATUMAI HILI NI BORA ZAIDI. WALA SIVYO WEWE UNA NGUVU YA KUCHUKUA HATUA. WAKOMBOENI WATOTO WENU WA KIKE.
Ukweli wa mambo ni kuwa wanamgambo wa al-Shabaab ni wahalifu tu ambao wamefaidika na machafuko na kutokuwa na sheria. Fikiria juu ya kikombozi na mamilioni waliyopata kwa kutumia uharamia. Kwa hisani zenu, msidanganye yeyote kuwa wanapigana kwa jina la Mungu. Abadan! Sio Koran wala Biblia inayotetea machafuko. Ningependa wenzetu hodari wanaoandika vitisho mitandaoni wawashauri wajisalimishe, warejee shule na kujiunga na Jeshi la Somalia wakati utulivu na amani utakaporejea. Pia natumai ulimwengu umeshajifunza usiruhusu tena kutokuwepo kwa utawala usio wa kisheria kwa vile kuna majangili wengi wanaosubiri kutumia fursa hiyo -- wananchi wasio na hatia wamekuwa wakiteseka bila ya matakwa yao.
BAADA YA AL-SHABAAB, KILA MKENYA NA MSOMALI WAPENDA AMANI LAZIMA WAWE NA TAHADHARI NA MAADUI WA NDANI, KWA VILE NINAELEWA NA NIMESIKIA BAADHI YA MASHEIKH WAKIHUBIRI KWA JINA LA DINI. VIJANA WETU WALIJAZWA KASUMBA NA WATU KAMA HAO WAOVU KUVUKA KWINGINE ILI KUPIGANIA DHAMIRA AMBAYO NI DHIDI YA BINADAMU NA HAIHUSIANI CHOCHOTE NA MUNGU.
Kwa maoni yangu, nadhani wanawake wasishiriki katika siasa. Hakuna chochote kizuri zaidi kwao kuliko watoto wao na nyumba zao kwa sababu wao ni viongozi wa familia zao.
Wasenge wote wanatoa mawazo hapa. kwa nini wasenge wote wanaeleza maoni yao katika tovuti hii au ni yao? Ikiwa mnataka niwaambie, hakuna mjadala kama al-Shabaab ni wanaume au la kwa sababu siwajui wanaume wengine isipokuwa wao mpaka sasa.
Asanteni KDF kwa kazi nzuri. Kwa hakika al-Shabaab wako katika hali ya kutoamini kwa vile hawakutarajia kabisa hilo kutoka kwa KDF. Kwa upande mwengine, angalizo moja muhimu, wananchi wa Kenya lazima muwe waangalifu na kushirikiana na vikosi vya usalama ili kutoa habari yoyote ya yeyote anayeonekana kutiliwa shaka na hatari ili hatua zifaazo ziweze kuchukuliwa. Kumbukeni, kumripoti mtu kwa sababu unamshuku sio kosa.
Kwa upande wangu sikubaliani na baadhi ya maoni hapa. Linapokuja suala la kuleta amani nchini Somalia, badala yake ningesema kunapaswa kuwa na njia mbadala ya kuwa na amani kuliko kupeleka mamilioni ya majeshi nchini Somalia kwa jina la kuleta amani kule. Ni aibu kwa akili za Waafrika. Ni karibu miaka mitano sasa na hatuoni chochote, kumbukeni kuwa kua msemo unaosema ikiwa huwezi kuwashinda, ungana nao. Nakusudia kuwa njia pekee ya kuleta amani ni kupitia mazungumzo na matumizi ya demokrasia na sio kwa bunduki. Na kwa tarifa yenu, mnaelewa kuwa Marekani pia inawapa fedha al-Shabaab kwa lengo la kuwamaliza Waislamu. Ikiwa ni suala la kuleta amani ni rahisi sana lakini hapa tunafahamu kuwa hakuna nchi yenye hamu ya amani nchini Somalia. Kwa hivyo ujumbe wangu kwa watoa maoni wote wasiojua kusoma ni kuwa mnapaswa kuwa na akili zaidi kuliko hivi kwa ajili ya nchi yenu masikini.
Al-Shabaab ni majambazi wanaohitaji kung'olewa kwa gharama yoyote ili watu wa Somalia waishi kwa amani. Miaka ishirini bila ya serikali ni pigo kwa Wasomali wote wapenda amani.
katu al-shabaab hawataweza kenya. they are just joy riding around and wasting their time and resources.but as for kenyans,we must pray hard to God for a win.
Hatutaki kuhusishwa na watu wasio tukufu maisha. Uislamu ni dini ya amani na Muislamu wa kweli atakuambia hilo. Magaidi ni watafuataji wa nafsi zao ambao hawataki kuona ustaarabu wowote na wanachukia amani. Waislamu wanapaswa kusimama pamoja dhidi yao na kuwatoa nje ya mipaka. Tuwasafafishe pia wafuasi wao na kuripoti habari kwa polisi ya mtu yoyote asiye wa kawaida au mwenye uso wa kutenda kosa kwa ajili ya uchunguzi. Waislamu wamechoka kutumiwa kama kisingizio wakati mambo yanapokuwa mabaya na ni wakati sasa kwa Waislamu wanaojali juu ya amani, maendeleo na utukufu ya maisha ya binadamu kusimama na kusema HAPANA, INATOSHA! Rejeeni kwa wanaowapeni fedha nje na mkaanze fujo kwenye nchi zao na sio nchi ya amani!!!!
Waulizeni askari wa miguu, watawaambieni vyema jinsi isivyowezekana kuelezea “kwa nini vita” inachukiza kuona wananchi wasio na hatia, familia za askari waliofariki wanavyolia na pembezoni kuna makampuni yasiyo na haya yanavyofaidika kutokana na tenda na mikataba ya ulinzi...lakini inakuja kuamuliwa mema waliyofanya dhidi ya yale maovu waliyofanya. Natuma dua zangu kwa askari wote wakuweko nyuma ya M16, Heckler, Koch au Kalashnikov zao, endeleeni kupigana hadi tusahau kuwa vita ni jehanamu.
Waoga hao wanaomwaga damu lazima na wao wamwagwe damu!!! wao wanayo damu pia!!! Zaidi ya hayo watuambie wapi watakuwa Osama, Saddam Hussein, na karibuni Jeshi la Mapinduzi la Irani!!!
Sote tutaendelea kuwaombea kwa ajili yenu na Mungu wa Jacob na Abraham, Mungu wa kweli na muumbaji wa mbingu na ardhi daima atawakumbukeni. Mwenyezi Mungu azikumbuke familia zenu, wazazi wenu, wake zenu, dada na kaka zenu bila ya kuisahau Kenya yote.
Tunahitaji kuwa na tahadahri sana na tusilegee katika ulinzi. Operesheni za usalama zinaweza nchini kwetu kuungana na operesheni za Marekani na Mossad kwa ajili ya uwazi na mbinu zaidi juu ya kuzuwia uvamizi na propaganda kama hizo? Lakini siku zote endeleeni kumuamini Mungu kwa vile yeye ni Mlinzi bora zaidi kuwahi kuwepo duniani. Ninajivunia kuwa MKENYA NA DAIMA SITOTISHWA NA CHOCHOTE! TUNAMWAMINI MUNGU!
Al-Shabaab ndio Watetezi Pekee wa Heshima ya Somalia dhidi ya mashambulizi ya wasioamini.
mm kwa maoni yangu vita sio kumaliza tatizo somalia malizeni vita jamani?
Habari ya al-Shabaab inaendelea kukua kila wakati inaposikika. Kama ilivyotokea inawezekana ya kuwa wanapigana kuwalinda Waislamu baada ya vita vitakatifu kumalizika na kusahaulika. Tafadhali tujulishe barua pepe ili nitume habari zaidi inayokua kuhusu mashambulizi ya al-Shabaab.
MWENYEZI MUNGU KWETU SISI SOTE.
Majeshi ya Kenya wana nguvu zaidi uwanjani ndiyo maana al_Shabaab iliondoka. Ni ukweli kuwa hii ni "Mgogoro ambao umeleta mgogoro katika jamii yenye mgogoro nchini Somalia". Vurugu hizi zote imesababishwa na al-Shabaab....Kuingilia kati kwa Kenya katika mgogoro huu kutabakia kama mafunzo kwa watu Wasomali kwa kuwa watalindwa na kuhudumiwa. Lakini kwa nini al-Shabaab inawalenga Wakenya? Kwa sababu Kenya ina mpaka mrefu isiyovukika kwa kuwezekana kwa mipango zao za kutishia eneo ya Pembe na Afrika Mashariki.DAIMA KENYA........MAPAMBANO YAENDELEE!!
Serikali ya Kenya lazima izingatie kwa makini ukweli ya kwamba watu wasio na hatia wamepoteza maisha yao na Wakenya wanaishi kwa hofu kubwa kila siku kwa sababu ya hawa wateteaji wa al-Shabaab waoga walio huru na wanaozurura mitaa zetu kila siku..Lazima wakaze ulinzi na wape Wakenya usalama..
Al-Shabaab ni mnyama mdogo anayetishia maisha ya watu wasio na hatia. Karibuni watasafishwa na askari wetu wenye nguvu na mbinu. Kwa sasa wamepooza kabisa. Kwa sababu hawataki kuonesha kusalimu kwao amri, mwishowe askari wetu watafanikiwa kuikamata nchi yote. Lakini ninawashauri kujifunza kuweka sheria za kuwaongozeni (Wasomali) hapa duniani. Kwa vile sisi ni Waislamu, hakuna shaka Mungu atawaongoza kubuni sheria kwa taifa hili na Wasomalia popote walipo Mwenyezi Mungu alibariki taifa hili na watu wake wazuri.
Swali ambalo linapaswa kuulizwa ni kwa nini serikali ya Kikristo ya Kenya inatoa tahadhari za usalama kuhusu mashambulizi yaliyopangwa kwa watu wake na viongozi wake wanalindwa na makomando wa kijeshi wenye vifaru na mizinga mikubwa mikubwa ikiwa kweli al-Shabaab wameshashindwa? Ikiwa wapiganaji wa vita vitakatifu (al-Shabaab) walishashindwa, vipi tena wanaishambulia Kenya? Nadhani habari hii inatolewa na mtu ambaye amepokea madola na kuiuza dini yake. Angalieni nyuma katika historia ya Pembe ya Afrika, ilikuwaje? Wasiokuwa Waislamu wanaelewa kuwa Uislamu utakuja kutawala ulimwengu lakini wanaogopa Waislamu wapiganaji wa vita vitakatifu kuwashinda wasiokuwa Waislamu katika nchi za Kiislamu bila kujishughulisha na vita hata kabla ya nchi zao kushambuliwa. Huu ni ushahidi nchini Kenya ambako ikiwa utawaambia watu kuwa mtu huyu ni al-Shabaab unapotembea mitaani wote watakimbia. Hii ni kwa sababu ya hisia za kuwa katika tishio siku zote. Kwa uwezo wa Mungu, tutauteka ulimwengu wa wasiokuwa Waislamu bila ya kuingia nao vitani na kwa hivyo tunawaambia wanafiki wajifiche popote wanapoweza kujificha.
Ni lazima tuwashinde hao wanamgambo.
Hapana. Naamini kuwa wanawake wasingepaswa kushiriki katika uongozi wa Somalia kwa sababu Mungu aliamrisha sauti zao zisikike mtaani, kwa hivyo iweje watu kama hao wapewe dhamana.
KAZI NZURI KWA JESHI LETU LA ULINZI LA KENYA! SISI KAMA RAIA TUNA WAJIBU MKUBWA WA KUTEKELEZA. KUWA WALINZI NA KUTOA HABARI YOYOTE ITAKAYOSAIDIA KUOKOA MAISHA KWA KUSAIDIANA NA VYOMBO VYA USALAMA. HII SIYO VITA VYA KIDINI. BALI NI VITA VYA KUSAFISHA VIKOSI VYA GIZA (VYA AL-SHABAAB) NCHINI KENYA!!!! TUPAMBANE NA AL-SHABAAB PAMOJA. TUFANYE KAZI PAMOJA NA VYOMBO VYA USALAMA, TUTOE RIPOTI YA WASHUKIWA WOTE WA KIKUNDI HIKI NA SHUGHULI ZAO. NA MIMI... NA KAMA MKENYA. DAIMA NITAKUWA MLINZI NA TAYARI KUFANYAKAZI NA VIKOSI VYA USALAMA ILI KUPAMBANA NA UGAIDI. WEWE JE?
Kwa maoni yangu nafikiria kikundi hiki cha kigaidi kinajaribu kutupa mateke za mwisho kabla ya kutenganishwa mara ya mwisho. Ni silaha ya mwisho ya kujaribu kuwahofisha wanaanchi na kujaribu kuhalalisha madai yao. KDF mapambano yaendelee. Wakenya wote na Wasomali wapenda amani wako nyuma yenu kikamilifu.
Je unakumbuka kilichofanyika wakati Yesu alipowatupia nguruwe mapepo? 'Nguruwe' hao walikimbia chini bondeni lisiyokuwa na mwisho. Vivyo hivyo kwa hawa 'nguruwe' wanaotishia maisha ya watu wa Mungu. Itakuwa kuwa vema kama hawa NGURUWE WADOGO WANAOKUFA AU MAFUKO, AU MACHINDI, AU NUNGU KWA KUKOSA NENO ILIYO BORA KWA SABABU YA TABIA YAO YA KUJIFICHA kujua umuhimu ya kusalimu amri mapema la sivyo AMISOM iliyoimarishwa itawatia adabu zaidi hawa kondoo waliyochanganyikiwa!
inahuzunisha ya kuwa dini inatumiwa kwa jinsi yoyote ile mbaya, kipengele muhimu ya ubinadamu ni uvimilivu, hakuna anayedai kufurahishwa na tabia yote ya mtu mwingine yeyote lakini mungu tusaidie hii ni dunia tunayoishi na basi tunafaa kuishi kwa amani na umoja.
Vita lazima ushindwe kwani hivyo tu ndivyo kutahakikisha ulinzi wa nchi yetu.
MATEKE YA FARASI ANAYEKATA ROHO – AL-SHABAAB IMEKWISHA!!! KDF ITEKENI KISMAYU KARIBUNI. NINAJIVUNIA KUWA MKENYA.
Kwa upande wangu nadhani mgogoro unaoendelea nchini Somalia, diplomasia zaidi unahitajika kuliko matumizi ya nguvu. Natumai ni wakati sasa wa kukaa na al-Shabaab na kuangalia uwezekano wa suluhisho la pamoja kwa kuzingatia matakwa yao makuu. Taratibu na masharti yatawekwa katika mazungumzo. Mungu ibariki Somalia na Afrika kwa jumla.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, aibu iwe juu yao, hawa ni wakosefu. Ni kitu gani hiki cha kuwatisha watu kwa kutumia magazeti hayo ya kipuuzi? Al-Shabaab imepoteza vita kwa muda mrefu, sasa wanafanya kila kitu ili waonekane katika vyombo vya habari. Enyi al-Shabaab, muombeni Mwenyezi Mungu msamaha na kila ambaye hakutenda uhalifu mkubwa arejee katika jamii ya Somalia na kujaribu kufanya kitu chema kwa watu badala ya kupoteza wakati katika kukifuata kikundi hiki cha wauaji wapuuzi. Mwenyez Mungu atawasamehe ikiwa mtajaribu kubadilisha mfumo wa maisha yenu. Asante mwandishi wa habari uliyeandika makala hizi nzuri kuhusu ugaidi. Mwenyezi Mungu akusaide katika kila jaribo la kufichua ukweli katika nyuso za chuki za al-Shabaab.
TUMUOMBE MUNGU SANA MAMBO HAYA YASIFIKE TANZANIA ''EEEEEHHH M/MUNGU MWINGI WA REHMA UNAYE TUWAZIA YALIYO MEMA TUEPUSHE NA HAYA'' amen!!!!!!!!!!!!!
Nyinyi ni takataka na wachafu. Fuateni mfumo kama ulivyowekwa. Nyinyi sio chochote, mbwa nyinyi.
Hii ni sauti ya kushindwa ya mwenzetu aliekata tamaa. Nina imani kuwa AMISOM itashinda na kuleta amani katika vita vilivyolichana taifa la Pembe ya Afrika. Tusiogope vitisho vya mtu ambaye karibuni atakufa, kwa vile karibuni atakuwa hayupo tena.
Ni kwa wasiwasi mkubwa nilisoma makala hii, al-Shabaab inaonekana kudhoofika lakini hilo linaweza kuwa nguvu yao, wanatoa picha ya uongo (habari za uongo) katika chapisho lao la Gaidi Mtaani kwa kuzungumzia kuhusu kuipoteza karibuni Kismayu kwa vikosi vya AMISOM. Intelijensia ya Kenya lazima iuelewe mchezo wao.
Al-Shabaab haina nguvu tena, kwa kweli wamepooza kabisa. Sababu hasa hawataki kuonyesha kujisalimisha kwao na kukubali kushindwa, ndio maana wanavaa vinyago vya kutorejea nyuma kwenye nyuso ili kufunika tu machozi na aibu yao.
Kwa kweli al-Shabaab wamewekwa kwenye pembe ya ulingo. Kuua wanawake, watoto wa shule ya Jumapili na wa madrasa hawawafanyii jema lolote.