Agosti 06, 2012
Kuna matumaini mapya nchini Kenya kuhusu vita vya kupambana na kansa, moja ya magonjwa yanayoongoza kwa vifo nchini humo.
Bunge la Kenya liliidhinisha Sheria ya Kudhibiti Kansa hapo tarehe 24 Juni ambayo itaruhusu kuundwa kwa Taasisi ya Taifa ya Kansa ili kuhakikisha uanzishwaji wa hospitali, matibabu ya kitaalamu na vituo vya matunzo kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa kansa.
"Ili kuishughulikia kansa na magonjwa mengine yasiyokuwa ya kuambukiza kwa mapana zaidi, wizara yangu, kwa kushirikiana na mashirika mengine ya serikali na washirika wa maendeleo, wameungana kwa pamoja kurahisisha kuanzishwa kwa Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti Kansa, ambao utarahisisha kuanzisha kwa vituo vya uchunguzi wa kansa nchi nzima," alisema Waziri wa Afya Anyang Nyongo.
Waziri huyo, ambaye mwaka jana alitangaza kuwa amegunduliwa na kansa ya prostata, aliiambia Sababhi kuwa kila moja la majimbo 47 ya Kenya litakuwa na kituo cha kuchunguza na kutibu kansa chenye vifaa kamili katika hospitali za serikali. Alikadiria kuwa huduma hizo zitagharimu kiasi cha shilingi milioni 200 (dola milioni 2.4).
"Asilimia themanini za kesi za kansa nchini Kenya zinachelewa kuripotiwa, wakati huo ikiwa haiwezekani tena kuzitibu. Lakini tuna imani kuwa, kwa kupitia vituo vilivyopendekezwa, tutaimarisha uchunguzi na utambuzi ili kuepuka kuzigundua kesi hizo mapema na hivyo kuimarisha matokeo ya afya," Nyongo alisema.
Kansa ni gonjwa la tatu linalosababisha vifo nchini Kenya baada ya maambukizi na magonjwa yanayohusiana na moyo, kwa mujibu wa Taasisi ya Kenya ya Utafiti wa Tiba (KEMRI), shirika la utafiti wa tiba linalomilikwa na serikali.
"Kuna kesi nyingi za kansa zinazoripoti sasa kuliko ilivyokuwa miaka 10 iliyopita. Kwa kuhuzunisha, kesi nyingi za kansa zinaripotiwa zikiwa katika hatua za mwisho, wakati ambapo hakuwezi kufanywa lolote la maana la kutibu," KEMRI ilisema katika ripoti yake bungeni.
Raisi wa Kenya Mwai Kibaki alisema kesi za kansa nchini zinaongezeka kwa kiwango cha kutisha, hasa zile za maziwa, za kizazi na prostata. Mwaka jana kulikuwa na kiasi cha kesi 28,000 na vifo 22, 000," alisema hapo Julai katika hotuba yake ya kufungua Hospitali binafsi ya Kansa mjini Nairobi na Kituo cha Matibabu ya Kansa.
Geoffrey Mutuma, mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Patholojia na Kansa cha KEMRI, alisema kuwa mabadiliko katika vyakula, maisha ya kivivu na kukosekana kwa mazoezi ya viungo ni sababu zinazochangia kukua kwa kesi za magonjwa na vifo vinavyotokana na kansa.
Kukosekana kwa uchunguzi na matibabu ya kansa ni moja ya vikwazo vinavyowakabili wagonjwa wa kansa nchini Kenya, maafisa wa afya na serikali waliiambia Sabahi.
Kwa sasa kuna vituo vinne tu vya uchunguzi wa kansa nchini Kenya -- vyote vikiwa Nairobi -- na vitatu kati ya hivyo ni vituo binafsi. "Hii huwafanya wagonjwa masikini wasiweze kulipia gharama za matibabu na usafiri ikiwa wanaishi nje ya Nairobi," alisema Daktari David Eseli simiyu ambaye anafanyakazi katika kamati ya bunge ya afya.
Gharama za wiki moja za matibabu ya mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta (KNH) ni shilingi 2,000 (dola 24), wakati katika hospitali binafsi kama vile Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan, MP Shah Hospital na Nairobi Hospital, mgonjwa analipia shilingi 40,000 (dola 475) kwa ajili ya matibabu, alisema Anselmy Opiyo, mkuu wa kitengo cha kansa katika KNH.
KNH ni kituo pekee cha umma chenye kitengo cha kansa ambapo watu wengi wanaweza kumudu, na kuifanya kuwa ngumu kukidhi mahitaji kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa, Opiyo aliiambia Sabahi.alisema wagonjwa wanalazimika kusubiri kwa mua mrefu sana kabla ya kupatiwa matibabu kwa sababu kitengo cha hospitali kimezidiwa.
"Mpaka sasa, tuna kiasi cha wagonjwa 450 walioko katika orodha ya kusubiri kwa sababu mashine inaweza kuhudumia watu 100 kwa wiki sita, muda ambao baada ya hapo wagonjwa wengine 100 watakuwa wanatumia mashine hiyo kwa kipindi hicho hicho. na mzunguko unaendelea," alisema.
Rose Nyakina, muuguzi katika hospitali, alisema vipindi vya kusubiri vinaweza kuvunja moyo. "Wakati mwengine, unawaangaliwa wagojwa waliokata tamaa unaingiwa na huzuni kwa sababu huwezi kufanya chochote kuwapunguzi mateso yao," aliiambia Sabahi.
Kwa mujibu wa maafisa wa afya, Sheria Mpya ya Udhibiti wa Kansa itashughulikia hili la kutopatikana kwa vituo vya uchunguzi na matibabu. Taasisi Mpya ya Taifa ya Kansa pia inatarajiwa kushirikiana na washirika wa maendeleo na wafadhili kukusanya fedha kwa ajili ya kuuendeleza mradi huu.
"Kazi ya mwanzo tutakayofanya ni kuanza uchunguzi katika hatua ya kituo cha afya na [kushughulika na] na kupigania kuwaarifu watu, hasa wanawake, kuhusu jinsi ya kugundua kansa ya uzazi na maziwa," Waziri wa Afya ya Umma Beth Mugo aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano mwezi uliopita.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Ni programu nzuri sana lakini kabla hatujaanza uchunguzi wa saratani tufahamishwe sababu za saratani, kitu gani cha kuepukwa katika maisha yetu ya kila siku na jinsi ya kugundua gonjwa lenyewe. Elimu itawasaidia watu wengi kusalimika na hili.