Jeshi la Somalia latembea kuelekea Buurhakaba na Diinsoor

Na Adnan Hussein huko Mogadishu

Agosti 06, 2012

  • 5 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vikosi vya Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia vinatembea kuelekea miji ya Buurhakaba na Diinsoor katika mkoa wa Bay , na vinatarajia kupata upinzani usio na nguvu kutoka kwa wanachama wa al-Shabaab waliojificha katika vijiji vinavyozunguka miji hizo.

  • Askari wa jeshi la taifa la Somalia wachukua nafasi za ulinzi huko magharibi mwa Mogadishu. Vikosi shirika kwa sasa vinaelekea kuchukua vijiji vya kimkakati katika mkoa wa Bay. [Na Stuart Price/AFP]

    Askari wa jeshi la taifa la Somalia wachukua nafasi za ulinzi huko magharibi mwa Mogadishu. Vikosi shirika kwa sasa vinaelekea kuchukua vijiji vya kimkakati katika mkoa wa Bay. [Na Stuart Price/AFP]

Vyanzo vya usalama vinasema kwamba vikosi vya Somalia na Ethiopia vilikwishatoka katika ngome ya jeshi ya Deeynunay na tayari vimewasili katika viunga vya Buurhakaba, kilometa 60 kusini mwa Baidoa, mji mkuu wa mkoa huo. Mashuhuda waliiambia Sabahi kuwa vikosi vya pamoja vimebakiza kilometa 10 kufika katikati ya Buurhakaba.

Kadri vikosi shirika vinavyokaribia, wanamgambo wa al-Shabaab wameachia nafasi zao katika vituo vya ukaguzi magharibi mwa kijiji hicho kwa kuogopa kuzingirwa, vyanzo vya jeshi la Somalia vimesema.

Ali Osman, ofisa wa jeshi la Somalia aliyeweka makao Baidoa, alisema vikosi hivyo vinaeleka Buurhakaba kuwaondoa al-Shabaab na wanamgambo wanaofanya nao kazi pamoja. Alisema anatarajia vikosi shirika kuukamata mji huo mapema, kwani kwa sasa wanafanya kazi kuuzuia katika sehemu kadhaa za mbele

"Watoto wa Somalia katika maeneo ya kati na kusini ya nchi wanapinga ugaidi katika hali yoyote na muundo wowote na wangependa kuuharibu kuliko kuwepo pamoja nao," aliiambia Sabahi. Ugaidi unalenga wasomi na yeyote anayepinga itikadi yake isiyo ya kawaida ili kufanya ugaidi katika mkoa huo na katika dunia. Vikosi vyetu viko tayari kugeuza matamanio ya viongozi wa al-Shabaab kuwa ya majonzi na kukata tamaa."

"Inaendelea pasipo kusema kuwa Somalia ina uwezo wa kuzuia jitihada za yeyote anayejaribu kulazimisha madhara kwa Somalia na watu wake na kuondoa uthabiti wa nchi," Osman alisema. " "Somalia siyo milki ya al-Shabaab au al-Qaeda. Somalia ni ya Wasomali na watasimama imara dhidi ya kugeuza nchi yao kuwa bandari salama kwa magaidi kwani wanajaribu kuchochea hofu na kuleta kero kwa nchi za Afrika mashariki."

" "Somalia siyo milki ya al-Shabaab au al-Qaeda. Somalia ni ya Wasomali na watasimama imara dhidi ya kugeuza nchi yao kuwa bandari salama kwa magaidi kwani wanajaribu kuchochea hofu na kuleta kero kwa nchi za Afrika mashariki."

Kama makabiliano yatazuka huko Buurhakaba, vikosi shirika vitatumia roketi na mota kushambulia wapiganaji al-Shabaab na ngome zao, alisema mchambuzi wa masuala ya usalama Muhsin Mohamed.

Mohamed aliieleza Sabahi kwamba al-Shabaab watatumia milima midogo ambayo inazunguka Buurhakaba kama makazi isipokuwa kama jeshi litaharakisha kutengeneza mpango wa kina kwa ajili ya eneo.

Meya Msaidizi wa Baidoa Sandheere Mohamed Istin alisema wakaazi wa Buurhakaba wanateseka na kuharibika kwa hali ya maisha na huduma mbovu za jamii, hususani maji, umeme, afya na elimu.

"Hatuwezi kuwaacha watu wetu wafe kwa kiu na njaa huko Buurhakaba. Tutawashinda al-Shabaab , ambayo inaporomoka na kusambaratika kadri mgawanyo wa ndani unavyokua ," aliieleza Sabahi. "Tunaandaa vikosi vyetu ili kupata mafanikio ya kijeshi katika vijiji vyote vya mkoa wa Bay, baadhi yake bado vinashikiliwa na maadui wa amani."

"Tunapigania kuleta amani katika ardhi yetu, kudumisha utulivu na umoja, na kurejesha muundo wa serikali. Hatutaki wapiganaji wa kigeni kukaa katika nchi yetu ili kusababisha vurugu na kusambaza ugaidi," Istin alisema. "Tutapambana hadi katika maficho yao makuu na tutalisaka genge hili la wahalifu linaloitwa al-Shabaab na uongozi wake ambao unaonyesha kiburi cha kuweka chini silaha na kujisalimisha kwa vikosi vyetu."

"Ushindi uko karibu na tutaona kwa macho yetu wenyewe kuanguka kwa wakuu wa kundi hilo kadri tunavyowasaka kama panya," alisema. "Tutawaumbua kuonyesha uchafu wao na nyuso zenye aibu na tutaondoa wito wao wa uongo na mabango yao meusi, bila ya kujali itachukua muda gani.

Abdullahi Geellow, dereva wa lori la biashara anayefanya shughuli kati ya Buurhakaba na Baidoa, alisema Buurhakaba imekuwa ikiteseka na bei za juu, kukatika kwa umeme na uhaba wa maji. Alisema wakaazi wa mji wameanzisha uhamaji wa makundi kuelekea vijiji vya Buur Eylo na Leego ili kukimbia mgogoro unaotarajiwa.

Geellow aliiambia Sabahi aliona mamia ya vikosi vya Wasomali na Waethiopia wakiwa na silaha nzito za vita wakitembea kuelekea Buurhakaba. "Katika barabara kuu inayounganisha Baidoa na Buurhakaba, niliona vikosi vikisonga taratibu na kukamilisha mikakati yao ya vita. Pia niliona misafara ya kijeshi ikipeperusha bendera ya bluu ya Somalia yenye nyota nyeupe katikati," alisema.

Al-Shabaab inatarajiwa kupoteza Diinsoor

Wanajeshi wa Somalia wakisaidiwa na jeshi la Ethiopia nao pia wapo njiani kuelekea Diinsoor, kilometa 100 Magharibi mwa Baidoa.

Siku ya Jumamosi (tarehe 4 Agosti), wanajeshi wa Somalia waliulinda Qansah Dhere , kilometa 29 lutoka Diinsoor, dhidi ya shambulio la al-Shabaab, Garowe Online ya Somalia iliripoti. Meya wa Qansah Dhere Adan Abdi Adan alisema wapiganaji 13 wa al-Shabaab na wanajeshi wawili wa Somalia waliuawa katika mapambano hayo.

Gavana wa Bay Abdifatah Hasan Gesey aliyaita mapambono hayo "kipigo kikubwa" kwa al-Shabaab.

Kamishna wa Diinsoor Osman Mohamed Abdi ameahidi kufanya mapigano ya wazi dhidi ya al-Shabaab ili kuwatoa nje na kuruhusu majeshi ya serikali kuchukua udhibiti kamili wa mji.

"Majeshi yetu yanakaribia Diinsoor na tutashambulia isipokuwa kama wanamgambo wa al-Shabaab na wapiganaji wao wa kigeni wataachia nafasi zao," Abdi aliiambia Sabahi. "Tutavunja migongo yao na kuwazuia kuendelea kuishi au kuungana katika kundi."

Alisisitiza umuhimu wa kuwapeleka wanajeshi wa upelelezi kati ya wanaochunga mifugo, kwani wanaweza kukusanya taarifa kabla wanajeshi hao hawajashambulia mji. Abdi alisema hili litadhoofisha miundombinu ya kijeshi ya al-Shabaab, ambayo ilijaribu kuzuia uchumi kwa wakaazi wa jimbo la Bay kwa kufunga njia za ardhini zinazoelekea Mogadishu.

Abdi alitoa wito kwa wanamgambo wanaoishi katika Mkoa wa Bay na Bakool kuanzisha mazungumzo na kuweka silaha zao chini ili waweze kuungana na familia zao kwa usalama.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 39)

Dislike_icon(3)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • الكتبي
    August 7, 2012 @ 04:40:53PM

    Jeshi la Somalia na vikosi shirika lazima waisafishe Somalia na al-Shabaab ili watu wa Somalia walioathiriwa hatimaye waweze kufurahia usalama na utulivu.

  • Nelson buberwa
    August 7, 2012 @ 02:36:12PM

    napenda kutoa maoni yangu kama ifuatavyo 1.makala hii ni nzuri sana nimeipenda naomba ipatikane na kwenye mitandao nyingine!

  • xasan cabdi cali
    August 7, 2012 @ 01:48:04PM

    Ndugu zangu, ninawaamkia na ningependa muwasiliane nami.

  • lisu rashid
    August 7, 2012 @ 07:13:43AM

    asili ya wasomali ni uasi so umoja wa mtaifa angalieni kwa macho tu na tuzid kumwomba mola kwan mbio za sakafun huwa zina mwisho kama ilivyokuwa kwa muasi kunda.by lisu wa singapoo

  • PAGIKUWA MAHENGE MJENGWA
    August 7, 2012 @ 02:31:12AM

    MUNGU AIJALIE SOMALIA IPATE AMANI AMBAYO ITAWATOA KATIKA SHIDA ZA KISIASA,KIUCHUMI NA KIJAMII

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo