Agosti 03, 2012
Shughuli za kisiasa ambazo zimeiangukia Mogadishu kama dhoruba zinawafanya wamiliki wa hoteli wawe na furaha sana.
Mkutano wa Bunge la Taifa la katiba, ambao uliidhinisha katiba mpya ya muda ya Somalia hapo Jumatano (tarehe 1 Agosti) , ulileta idadi kubwa ya wageni mjini, kujaza hoteli na kupanda kwa bei.
Vivyo hivyo, uteuzi unaokuja wa wabunge, uchaguzi wa raisi bungeni na kuteuliwa kwa nafasi za mawaziri ambako kumepangwa kumalizike tarehe 20 Agosti, kunatarajia kufanya vyumba vya hoteli jijini kuwekezwa kwa wiki chache zijazo.
Mogadishu inarejea katika hali ya kawaida kutoka katika vurugu na vita ilivyovimulia kwa miongo miwili, waangalizi wamesema. Jiji kwa sasa linachukua hatua madhubuti za kurejesha utukufu wake uliopita baada ya amani na usalama kurejea jijini kote.
Meneja wa Hotel Shamo Mohamed Ahmed Mathana alisema maisha ya biashara yamerejea mjini Mogadishu. Uwekaji vyumba katika hoteli yake umeongezeka kutokana na mkutano na watu wanaorejea kutoka uhamishoni. Alisema anatarajia vyumba zaidi kuwahiwa siku zijazo.
"Natumai kuwa matukio ya sasa ya kisiasa ambayo yamewavutia maelfu ya watu kutoka mashirika ya kikanda na ya kimataifa kutainua shughuli za kiuchumi, ambao umekuwa katika hali ya kwamo kabla ya kuimarika kwa usalama mjini Mogadishu," alisema.
Mathana alisema hoteli yake, ilioko karibu na makutano ya Kilomita 5 jijini, inatoa usalama wa hali ya juu na huduma nzuri nsa ina matumaini ya kurejea kwa shughuli za utalii na biashara. Huduma hizi ni pamoja na huduma za udobi, uoshaji wa magari na chumba cha kufanyia mazoezi chenye vifaa vya kisasa.
Alisema ana matuamini chanya kuhusu kurejesha upotevu wa miaka iliyopita. "Mtu hawezi kuurejesha wakati. Yaliyopita yamepita, lakini sisi tuna matumaini chanya kuwa soko linaelekea njia sahihi katika kurejea hali yake, hasa kwa vile karibuni hivi Wasomali na wageni wamekuwa wakiekeza vyumba, ikiwa na maana kuwa imani imerejea," Mathana alisema.
Hotel Shamo, iliyojengwa na marehemu Abubakar Amiin Shamo mwaka 1997, ni moja miongoni mwa hoteli zinazojulikana sana. Wateja wake ni pamoja na waandishi wa habari, maafisa wa serikali na Wasomali waliokuwa uhamishoni. Vyumba vyake vina viyoyozi, vyakula vya moto na vinywaji baridi vilivyotengenezwa kutokana na matunda yanayolimwa kusini mwa nchi.
Mwandishi wa Habari Mohamed-deeq Botan alisema kuna mabadiliko ya wazi kuanzia mwaka jana, yaliyokuwa yamezuiwa na hali ya kutokuwepo kwa utulivu. Sasa, wageni na watu wanaorejea kutoka nje wamejaza vyumba vya fahari, kuongezeka kwa idadi ya uwekaji na kwa hivyo kupanda kwa bei.
"Sasa haiwezekani kupata bei isiyobadilika katika vyumba vya hoteli kwa vile hoteli za Mogadishu zimekuwa zikibadilisha bei kwa mujibu wa uwekaji wanaopokea," aliiambia Sabahi.
Botan alisema matukiio ya kisiasa nchini yamehamasisha soko lote kutoka usingizi na kukuza mauzo katika hoteli, mikahawa na magari ya taxi. Shughuli hii kubwa ya kiuchumi imezipelekea baadhi ya hoteli kutoa masharti ya idadi ya uwekaji vyumba kuwa isiwe chini ya usiku mitano kwa kiwangocha kuanzia cha dola 120 hadi 150.
Mohamed Ali Wariri, mfanyabiashara wa Uingereza, aliiambia Sabahi kuwa ni muhimu kukamilisha ujenzi wa majengo na hoteli mpya karibu na maeneo ya Barabara ya Maka al-Mukarama ili kupunguza ukiritimba wa wamiliki wa hoteli.
Mkurugenzi wa Hotel Sahafi International, Mohamed Hassan Gafaa, alisema hoteli yake inatoa uzoefu wa kiwango cha juu na raha za kukaa hapo ni za kipekee. Hoteli yake imepata kuaminiwa na wafanyabiashara wa ndani na wanasiasa tangu kufunguliwa upya mwaka 1998. Hoteli hiyo ipo karibu na maungano ya Kilomita 4 na ni iliyo karibu sana na uwanja wa ndege.
Hotel Sahafi International inavyo vyuma 70 vyenye televisheni, intaneti, vyumba vya kukogea vya raha na mapokezi. Mkahawa wa hoteli pia unahudumia vyakula mbali mbali vya kimataifa siku nzima.
Gafaa aliiambia Sabahi kuwa sekta ya utalii ya Somalia inapaswa kuanzisha kampeni za biashara. Sekta ya utalii itabidi kuinuka tena baada ya kusimama kabisa kutokana na kuanguka kwa serikali kuu miaka 21 iliyopita, alisema na kuongeza kuwa utalii huwanufaisha masikini na matajiri, kwa vile mikahawa itapata wateja wengi zaidi na kuajiri wafanyakzi wengi zaidi kutokana na uingiaji wa watalii nchini.
"Kukiwa na uimarikaji wa usalama mjini Mogadishu, mikahawa ya jijini, Cafés na maisha ya usiku yameshuhudia wateja wengi, hasa miongoni mwa familia ambazo zimeanza kutoka nje na kukaa hadi saa nyingi za usiku katika maeneo ya kusini mwa mji, kama vile Waaberi na Hamar-Jajab," alisema. "Tunawataka watu wapinge utamaduni wa vurugu ambao umeikumba Somalia kwa muda mrefu.
Wizara ya Usafiri wa Anga ya mkoa wa Somaliland siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni) iliikataza ndege...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata makamu wanne wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Ma...
Watu wenye silaha kwenye Kaunti ya Wajir walimuua polisi mmoja wa akiba wa Kenya siku ya Jumanne ...
Japan inaipa Tanzania dola milioni 49 (shilingi bilioni 80.4) kama msaada na mkopo kwa ajili ya k...
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo yeye pekee yake amewateua na kuwapangia kazi maafisa wa...
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumanne ilimkubalia Makamu wa Rais wa Kenya Willia...
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji