Agosti 02, 2012
Waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu wanasema wanahofia kuongezeka kwa ukandamizaji dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza katika Somaliland.
Mohamed Rashid Muhumed Farah, katibu mkuu wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari ya Somaliland (SOLJA), anasema hiki ni kipindi kibaya kabisa kwa uhuru wa kujieleza kwenye Somaliland.
Katika miezi mitano ya mwanzo ya mwaka 2012, serikali ya Somaliland iliwakamata waandishi 63, alisema Farah. Alisema hakuna hata mwandishi mmoja aliyefunguliwa mashitaka, na kwamba wote waliachiliwa baadaye. Katika mwaka mzima wa 2011, SOLJA ilirikodi kukamatwa kwa waandishi wa habari 51, jambo ambalo Farah anasema ni dalili kwamba vyombo vya habari vinalengwa isivyo haki.
Akilitaja mfano wa kesi ya mwandishi wa habari wa Somaliland, Mohamed Abdirahman Ismail, aliyeomba hifadhi nchini Yemen.
Katika mwezi Februari, Ismail anayefanya kazi na mtandao wa habari wa Subulaha, alikamatwa mjini Borama na kuteswa na vikosi vya usalama. Alitibiwa mjini Addis Ababa kwa kutumia fedha za msaada alizopewa na Kituo cha Uhuru wa Habari cha Doha, alisema Farah.
Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari, ambayo ni shirika lisilokuwa la kiserikali lenye makao yake makuu jijini New York inayopigania uhuru wa vyombo vya habari duniani, iliandika barua kwa Rais wa Somaliland, Ahmed Mohamed Silanyo, hapo tarehe 13 Juni kuelezea khofu juu ya kuongezeka kwa ukandamizaji dhidi ya vyombo huru vya habari huko Somaliland.
Katika mkasa mwengine, Mahakama ya Mkoa ya Hargeisa ilimhukumu Boqor Osman Aw Mohamud, aliyejuikana kama Bur Madow, hapo tarehe 8 Julai kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumkashifu rais na maafisa wa ngazi za juu wa serikali.
Hukumu hiyo ilizua malalamiko kutoka jumuiya za kimataifa za haki za binadamu na serikali ikasalimu amri kutokana na shinikizo hilo na kumuachia huru Mohamud siku hiyo hiyo, mwanasheria Osman Ibrahim Dahir aliiambia Sabahi. Alishakuwa kizuizini tangu katikati ya mwezi Machi.
Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International lilitoa taarifa hapo siku ya tarehe 12 Julai ikisema kwamba kesi ya Bur Madow inaonesha kuongezeka kwa vikwazo dhidi ya uhuru wa habari Somaliland.
Hukumu kama hizo zinaathiri katiba ya Somaliland, ambayo inalinda haki za raia kwa uhuru wa kujieleza, alisema Mohamed Said Hirsi, katibu mkuu wa Jumuiya ya Wanasheria wa Somaliland.
"Uhuru wa kujieleza upo kisheria Somaliland," Hirsi aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba mahakama za huko haziko huru kama vile katiba inavyoagiza.
Kitivo cha sheria katika Chuo Kikuu cha Hargeisa kiliandaa warsha siku ya tarehe 17 Julai kujadiliana mapungufu ya sheria ya habari ya Somaliland, iliyoanzishwa mwaka 2004.
Warsha hiyo ilihudhuriwa pia na Waziri wa Habari wa Somaliland, Bobe Yusuf Duale, mkuu wa kitivo cha sheria, Mohamud Hussein, wanasheria, wanafunzi na zaidi ya waandishi 30 wa habari.
"Uhuru wa habari ni sawa na uhuru wa kutembea," alisema Duale. "Vyombo vya habari havipaswi kutafuta kuwa na uhuru usio mipaka, ila kila kikwazo lazima kiwe cha kisheria."
Hata hivyo, Farah alisema hakuna haja ya kuonyesha mapungufu ya sheria kwani serikali haizitekelezi bali badala yake hutumia sheria ya uhalifu kuwalenga waandishi wa habari.
"Hatukubali marekebisho ya sheria hii, kwa sababu madhali serikali haifuati sheria, haiwezi kuhojiwa kwamba ina mapungufu," alisema Farah. "Ni pale tu sheria itakapofuatwa ndipo mapungufu yake yatakapoonekana. Kwa sasa serikali ina ajenda tofauti na sisi kama vyombo vya habari hatuwezo kuikubali."
Ismail Mohamed, mkuu wa kitengo cha kuimarisha vyombo vya habari kilichopo Hargeisa - Somalia Media for Peace and Development, alisema kukosekana kwa makubaliano kati ya pande mbili hizi kutatuliwe kuondoa vikwazo dhidi ya uhuru wa kujieleza.
"Vyombo vya habari haviwezi kuiamini serikali ambapo mahakama hazitekelezi sheria zinapotokea kuwa dhidi yao," alisema Mohamed.
Rasimu ya Sheria ya Utangazaji na Uchapishaji ipo bungeni, ilitarajiwa kutanua uhuru wa vyombo vya habari, alisema. Sheria hiyo itawaruhusu kwa uundwaji wa Kamisheni ya Vyombo vya Habari ya Taifa, inayowajumuisha wadau ambao watakuwa kama wapatanishi kati ya vyombo vya habari na serikali.
Malalamiko dhidi ya vyombo vya habari yatapungua ikiwa waandishi wa habari wamepatiwa mafunzo mazuri, alisema mwenyekiti wa SOLJA Hassan Mohamed Yusuf.
Hakuna nchi iliyoendelea bila ya vyombo vya habari makini na huru, alisema Duale. Alisema ili kufanikisha hilo, ni muhimu kuwa na mashirikiano kati ya serikali na vyombo vya habari.
"Serikali ya Somaliland inaheshimu uhuru wa habari na imejitolea kuhakikisha uhuru huo," alisema.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Somaliland imekuwa karibuni ikiingilia kati uhuru wa vyombo vya habari. Kwa mujibu wa vifungu vya katiba yake, vyombo vya habari lazima vifanye kazi kwa uhuru wa kifikra, kuandika na kujieleza. Nadhani serikali hii inachukia ripoti kuhusu upungufu yake. Ningependa kuwahimiza walinde haki zao kama zilivyoelezwa katika katiba.
Ikiwa vyombo vya habari vinakuwa na matusi na uchochezi, kitu ambacho kwa kweli sio kizuri, kitaadhibiwa na kufungwa. Kuna popote ulimwenguni ambapo kuwatukana wengine kunakubalika? Tulipigania uhuru wa vyombo vya habari na kulipia kwa damu yetu na mali zetu kwa ajili hiyo. Lugha ya matusi si sehemu ya uhuru wa vyombo vya habari. Mtu unayemtukana anaweza kuchukua sheria mikononi mwake ikiwa hawezi kuvumilia matusi yako. Haya ni baadhi maadili yanayokosekana katika vyombo vya habari. Rashid Hassan Ali
Makala nzuri. Mwandishi yeyote anayehitaji anaweza kuwasiliana na Kituo cha Uhuru wa Vyombo vya Habari ili kusaidiwa. Habari zaidi: