Agosti 01, 2012
Wajumbe wa Bunge la Taifa la Katiba ya Somalia walipiga kura kwa wingi kuunga mkono ufuataji wa katiba mpya hapo Jumatano (tarehe 1 Agosti), na kuisogeza Somalia hatua moja zaidi karibu na kumaliza kipindi cha mpito.
Kura hiyo ilikuja baada ya vikosi vya serikali kuzuia majaribio mawili ya mabomu ya kujitoa mhanga ili kuvuruga mkutano huo.
“Watu wawili waliokuwa wamevaa nguo na mabomu ya kujitoa mhanga walijaribu kushambulia eneo la mkutano. Lakini walizuiwa mlangoni, na kujilipua wenyewe,” afisa polisi Abdullahi Mohamed alisema, kwa mujibu wa AFP.
“Vikosi vya usalama vilizuia dhamira zao za mashambulizi…walipigwa risasi na baadaye kulipua mavazi yao,” Waziri wa Mambo ya Ndani Abdisamad Moalim aliwaambia waandishi wa habari, na kuongeza kuwa mlinzi mmoja wa usalama alijeruhiwa katika mlipuko huo.
Hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo, linalofuatia mfululizo wa milipuko ikiwa ni pamoja na mabomu ya kutega pembeni ya barabara na maguruneti mjini Mogadishu, mengi yao yakitekelezwa na kikundi cha al-Shabaab chenye uhusiano na al-Qaida.
Viongozi wa kisiasa wa Somalia walisifia kuidhinishwa kwa katiba ya muda kama wakati wa kihistoria na mwisho wa serikali ya mpito.
“Tuna furaha hapa leo kuwa mmemaliza kwa uwajibikaji utaratibu wa kupiga kura kwa ajili ya katiba,” Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali aliwaambia wajumbe baada ya kuidhinisha rasimu ya katiba kwa asili mia 96 ya kura zote.
“Ninatangaza kuwa kuanzia leo Somalia imetoka katika kipindi cha mpito,” alisema.
Kati ya wajumbe 645 waliohudhuria mkutano wa Jumatano, 621 walipiga kura kukubali rasimu ya katiba, 13 waliikataa na 11 hawakupiga kura, alisema Abdi Aden, mmoja wa makatibu wa Bunge la Taifa la Katiba na mwanachama wa kamati iliyokuwa na dhamana ya kusimamia mchakato wa upigaji kura.
“Bunge la Taifa la Katiba limeidhinisha rasimu ya katiba mpya ili itumike kama katiba ya muda kwa Somalia mpaka hapo kura ya maoni itakapopigwa kitaifa baada ya kipindi cha mpito,” Aden aliiambia Sabahi.
Aden alisema NCA haikubadilisha kifungu chochote cha katiba mpya, lakini imetoa mapendekezo na maangalizo ambayo yatajadiliwa katika Bunge jipya.
NCA – iliyochaguliwa na viongozi wa kikabila katika mchakato ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa – ilichukua siku nane kujadiliana na kuipigia kura katiba mpya.
“Hii ni siku ya kihistoria – leo tumeshuhudia kumalizika wa kazi ambayo imekuwa ikifanyiwa kazi kwa muda wa miaka minane,” alisema Waziri wa Somalia wa Katiba na Maelewano, Hoshi Jibril, baada ya kupigwa kura.
Ikiwa kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa, viongozi wa kikabila 135 watachagua wajumbe 275 kwa ajili ya bunge jipya katika siku zijazo, na baadaye wabunge watamchagua spika na manaibu wake wawili hapo tarehe 4 Agosti. Wabunge baaye watamchagua raisi mpya wa Somalia ifikapo tarehe 20 Agosti.
Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia Augustine Mahiga aliwataka wazee wa kikabila kuzingatia viwango vya juu vya mshikamano katika uteuzi wa wabunge.
Alisema wale wanaotoa hongo na kuwatisha wabunge “watachukuliwa kama ni waharibifu” na "vitendo kama hivyo hupelekea kukwamisha mchakato wa amani".
“Kumekuwepo na taarifa za kuudhi juu ya ushawishi usiofaa kwa wanasiasa wagombea katika nafasi zilizopita na za sasa. Ushawishi huu umo katika njia nyingi ikiwemo ubadilishanaji na utakaji wa fadhila, hongo na vitisho,” Mahiga alisema katika taarifa iliyotolewa Jumanne.
“Tusikubali viti vya bunge kuwa bidhaa ya kuuzwa katika mnada kwa anayetoa dau kubwa wakati tunatafuta na kudai hadhi ya kweli ya heshima na taifa linaloheshimiwa la Somalia." alisema.
“Watu wanaotumia vitisho na mbinu za matumizi ya nguvu wanajulikana,” alisema. Ninawataka kwa nguvu waache tabia hizi na waheshimu haki za wanawake kushiriki katika mchakato wa kisiasa.
Mahiga aliwasifu viongozi wa kikabila kwa kuchagua wajumbe wa NCA na kuwahamasisha kuendeleza heshima kwa mchakato wa mpito kwa vile unakaribia kufikia mwishoni.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Ni ya muhimu sana