Red_arrow

Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |

Al-Shabaab kuwaua wanachama wake kunaashiria matatizo makubwa

Na Mahmoud Mohamed huko Mogadishu

Julai 30, 2012

  • 178 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Uamuzi wa Al-Shabaab wa kuwaua wanachama wake watatu kwa tuhuma za kupeleleza kwa ajili ya serikali za kigeni kunaonyesha ukosefu wa imani ndani ya vyeo vya kikundi cha wapiganaji, wachambuzi wa kisiasa na waangalizi wanasema

  • Mpiganaji wa al-Shabaab amesimama akilinda wakati mamia ya wakazi wakiangalia adhabu ya kukatwa viungo hadharani. Al-Shabaab hivi karibuni iliwaua wanachama wake watatu kwa tuhuma za kupeleleza kwa niaba ya serikali za kigeni. [Mustafa Abdi/AFP]

    Mpiganaji wa al-Shabaab amesimama akilinda wakati mamia ya wakazi wakiangalia adhabu ya kukatwa viungo hadharani. Al-Shabaab hivi karibuni iliwaua wanachama wake watatu kwa tuhuma za kupeleleza kwa niaba ya serikali za kigeni. [Mustafa Abdi/AFP]

Al-Shabaab ilisema watu watatu -- Ishaq Omar Hassan,miaka 22, Yasin Osman Ahmed,miaka 23, na Mukhtar Ibrahim Sheikh, miaka 33 -- walikuwa wanapeleleza kwa ajili ya Shirika la Upelelezi la Marekani na Shirika la Upelelezi la Uingereza MI6.

"Hassan na Ahmed wote wawili walihusika na vifo vya Bilal al-Berjawi na wengine watatu [wanachama wa al-Shabaab]," shirika hilo linalohusiana na al-Qaeda lilisema katika mtandao wake wa Twitter tarehe 22 Julai. "Wawili hao waliweka vifaa vya ufuatiliaji katika magari ya al-Berjawi & kaka zake ambayo waliyaongoza makombora yaliyoshambulia vitongoji vya Mogadishu."

Al-Berjawi, mwenye uraia wa nchi mbili za Lebanon na Uingereza ambaye alivuliwa uraia wa Uingereza, aliuawa katika shambulio la kombora mwezi Januari nje ya Mogadishu. Iliripotiwa kuwa alikuwa kamanda msaidizi wa al-Qaeda nchini Somalia.

Waliyoshuhudia huko Marka walisema watu hao watatu waliuawa na kikosi chenye silaha katikati ya mji.

"Wapiganaji wa al-Shabaab ilitumia vipaza sauti vilivyofungwa katika malori kuwaita watu kushuhudia mauaji na watu walipokusanyika uwanjani, dazani ya wapiganaji waliyofunika nyuso zao waliwafunga vitambaa machoni watu hao watatu na kisha kuwapiga risasi, wakiwaua hapo hapo," mkaazi wa Marka Mohamed Said, miaka 34, aliiambia Sabahi

Tatizo la Al-Shabaab la kujiamini.

Omar Dahir, mkurugenzi wa Kituo kilichopo Mogadishu cha Marekebisho na Mjadala, alisema matatizo ya al-Shabaab yanatokana na kuongezeka kwa mgawanyiko miongoni mwa wanachama na kunaweza kusababisha kusambaratika kwa haraka kwa kikundi katika siku karibu zijazo.

"Kuna kutojiamini ndani ya al-Shabaab, kwa kuwa kikundi hakiwaamini wanachama wake na sasa viongozi wake hawaaminiani," Dahir aliiambia Sabahi. "Uamuzi wa al-Shabaab kuwaua wanachama wake watatu huko Marka unaonyesha ukosefu wa imani ambao unakikabili kikundi."

"Hii inaweza kuwa mwanzo wa kuvunjika kwa mipango ya mapigano iliyoandaliwa ndani ya kundi hilo, ambalo tayari linasumbuliwa na mgawanyo mkubwa," Dahir alisema.

Alisema al-Shabaab inaweza kukimbilia kuwaua kwa siri wengi wa wanachama wake kwa kuogopa kuwa kufanya mauaji mara mingi mbele ya wananchi kunaweza kuyumbisha umoja wa kundi hilo.

"Kundi hili litamuua mwanachama yeyote anyeshukiwa kuwa na uhusiano na pande za nje kwa sababu wanaogopa kuwa mashirika ya upelelezi ya Ulaya yanaweza kupenyeza kwenye kundi hilo na kuwalenga viongozi wao wanaotakiwa," Dahir said.

Al-Shabaab ilisema katika mtandao wa Twitter kuwa imezindua kampeni kubwa ya kukabili upelelezi ili kusafisha nchi kutokanana na majasusi hao .

Mwaka uliopita , kiongozi wa al-Shabaab Mualim Hashi Mohamed Farah alisema Kitengo cha upelelezi cha Ulaya kimepenyeza kwenye safu ya maaskari wa al-Shabaab, na mawakala wa pande mbili wanaojifanya kuwa wapigananaji wa vita vitakatifu.

Huu sio muda pekee kwa al-Shabaab kuwaua washirika wake waliotuhumiwa kwa kupeleleza kwa niaba ya mawakala wa upelelezi wa Kimagharibi. Al-Shabaab ilimuua makamu wa kiongozi wao mkuu wa upelelezi, Ahmed Ali Hussein, pia anajulikana kama Ahmed Keyse,mwaka 2010 kwa "upelelezi " wa serikali za kigeni.

Tarehe 27 Julai, al-Shabaab ilisema iliwakamata "wapelelezi watatu wa TFG" ambao kwa sasa wanahojiwa. "Kama watatiwa hatiani watu hao watatu watauawa hadharani," al-Shabaab ilisema katika Twitter.

Tuzo yazidisha tatizo ndani kati ya al-Shabaab

"Vurugu za kujiamini zimetawala katika sura ya nchi ndani ya kundi la al-Shabaab,ambazo zimesababisha mauaji ya washirika wake," alisema Abdirahman Mohamud, mwangalizi wa makundi yenye msimamo mkali.

Tangu Marekeni ilipotangaza tarehe 7 Juni kwamba itatoa zawadi ya hadi Dola za Marekeni milioni 33 kwa taarifa zinazowahusu wapi walipo viongozi saba wa ngazi ya juu wa al-Shabaab, viongozi wanaotafutwa wamejificha dhidi ya sio tu kikosi cha upelelezi lakini pia dhidi ya macho ya jamii na washirika wao.

"Viongozi wa al-Shabaab sasa wana wasiwasi kwamba Marekeni kutoa tuzo ya fedha kutasababisha kutoa msukumo kwa baadhi ya washirika wa kundi, ambao watahamasishwa na uroho waa pesa, kuwasaliti viongozi wao na kutoa taarifa kuhusu walipo ili wajipatie zawadi za fedha," Mohamud aliiambia Sabahi.

"Kwa maoni yangu huo ni motisha kwa uamuzi wa al-Shabaab hivi karibuni kuwaua washirika wake watatu kwa tuhuma za kufanya upelelezi kwa niaba ya mawakala wa kipelelezi wa Marekani na Uingereza," alisema.

Mohamud alisema al-Shabaab imegawanyika katika kambi mbili, na kila moja "itafanya ukatili" dhidi ya nyingine.

Mwezi Machi, kiongozi wa al-Shabaab Hasan Dahir Aweys alilaumu kikundi cha wanamgambo kwa kuwaua wananchi bila ya malengo kwa jina la kiislamu na kwa kushirikishwa kwake na al-Qaeda. "

Kundi lenye msimamo mkali la al-Shabaab lilifanya mauaji mengi katika miaka michache iliyopita, yakilenga sio tu washirika wake lakini pia na wananchi wengi wa Somalia waliotuhumiwa wakifanya kazi na upelelezi kwa ajili ya mawakala wa upelelezi wa Kimagharibi au wakishirikiana na majeshi ya serikali ya Somalia au Umoja wa Afrika," alisema Abdullahi Osman, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mtaalamu katika masuala ya vikundi vya waislamu wenye msimamo mkali nchini Somalia.

Osman aliiambia Sabahi kwamba al-Shabaab wanawafanyia ugaidi wananchi wa Somalia na wanatishia kuwaua wale ambao wanashirikiana na serikali au Umoja wa Afrika waliopo nchini Somalia.

Alitoa wito kwa serikali ya Somalia kuimarisha jitihada zao ili kuyakomboa maeneo yaliyobakia chini ya udhibiti wa al-Shabaab kumaliza uhalifu wa kuchukiza unaofanywa na kikundi hicho.

"Al-Shabaab itaendelea kufanya vurugu za kutokuwa na hadhari na kutochagua kwa uangalifu dhidi ya wananchi wa Somalia hadi kundi hilo litakapotolewa nchini," alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 314)

Dislike_icon(69)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • المعتصم بالله الصومالي
    May 17, 2013 @ 03:26:06AM

    Wacha niseme - kutafuta msaada wa Mungu - kwamba taifa la Kiislamu la Somalia limeathiriwa na gengi hili la wahalifu ambalo linajificha chini ya mwavuli wa Uislamu na kurejesha nyuma misingi mikuu ya dini zote zinazoamini Mungu mmoja ambayo wamekubaliana. Kikundi hiki kinafuata mkabala ule ule ambao umekuwa ukifuatwa na Kharijit, ambao wanathubutu kutoa maisha ya watu wasio na hatia kutokana na shutuma zisizo sahihi tu. Ina maana gani kudai kwamba Uislamu umeasisiswa kwa kuwakata vichwa watu wasio na hatia? Kwa ajili ya Mungu, mnapaswa kujifunza historia ya Umma huu mtukufu (taifa la Waislamu) ili kujihakikishia wenyewe juu ya uhalifu wa al-Shabaab na jinsi unavyoupaka matope Uislamu kwa njia ambayo ni tafauti na sura yake ya kweli. Wacha nimalizie kwa kusema hili: kile kinachotokea miongoni mwa al-Shabaab sasa ni mwanzo wa kisasi cha Mungu kwa taifa la Kiislamu. Utokomeaji wa al-Shabaab uko karibu, na waumini watafurahia siku hiyo na kuwa na furaha juu ya uokozi wa Mungu.

  • Jacub. P. Amidu
    October 22, 2012 @ 01:01:20PM

    Hivi uislamu ni kumsaidia Mungu kuwaua watu wenye dhambi kama wao Al Shabaab wanavyowaita mkafiri, Hivi huyo ni mungu wa namna gani anayehitaji msaada wa binadamu aliye muumba ili amfanyie kazi ya mauaji, basi Mungu huyo wa waislamu hana uwezo na kama ni hivyo kuna sababu gani ya kufuata kitu kisicho na uwezo.hivi ndivyo Quran ifundishavyo ni aya zipi hizo ambazo Mtume Mohammed na Mola wameziteua zifundishwe kwa watu kuwa makatili. Hivi kweli hata kwa akili ya kibinadamu mtu mwenye utashi anaweza kufanya mambo ya kijinga kama hayo, halafu eti Mwenyezi Mungu anafurahia huko ahera? Dini hii ni dini yenye tatizo la kisaikolojia kama sio dini yenye muongozo washetwani .Angalieni sana enye waja wa mwenyezi Mungu mnaotaka ahera na huko mnau a ndugu zenu kwa faida zenu binafsi upo wakati Mwenyezi Mungu atasema na ninyi

  • sakaja manasae
    October 18, 2012 @ 01:47:44PM

    kumbuka kuuwa ni dhambi ngugu zetu waislamu mzoea kuuwa kwa kisingzio kuwa mnatetea imani yenu. naamini kuwa mungu ni mwema kwa wote pia ni wa amani. imani ya shetani ndio ya kuuwa sio mungu.kuuwa watu wasio na hatia haipendezi machoni pa mungu na watu. sasa hivi alipo mwislam anadhaniwa kuwa ni gaidi au jambazi au mwizi,ona wanavyochoma makanisa kule tanzania

  • jamaal
    October 17, 2012 @ 11:24:36AM

    Ninamuomba Mungu awaongoze katika njia iliyonyooka kwa vile wamepotea.

  • sheekha
    October 13, 2012 @ 10:51:53AM

    Niliangalia filamu iliyochezwa na watu watatu. Kwa kweli ni wanaume, nashangaa na vipi waliicheza. Wote watatu walihojiwa na walisema ukweli. Nimeogopeshwa na jinsi gani wamefanya vitu hadi sasa. Hata hivyo hadithi yao ilitoka baada ya kumaliza mtu wa tatu, Mukhtar. Walilipwa dola 7000 tu kwa masuala yote mawili lakini sasa wameshafariki. Naomba Mungu atulinde. Kwa kweli watu hawa wanafuatwa fuatwa.

  • Axmed Juqaal
    October 8, 2012 @ 10:12:25AM

    Al-Shabaab watashinda na hivyo hawafai kuwa na pupa. Utawala huu mpya ni tawi la kisiasa tu la Al-Shabaab na hamfai kudanganyika kwa kuwajua.

  • ccm
    October 6, 2012 @ 10:17:36AM

    Mungu ailinde jamii ya Wasomali kutoka kwa kundi hili potofu. Amin!

  • prof canshur
    October 3, 2012 @ 06:31:54PM

    Al-Shabaab ndio tatizo pekee linalojaribu njia mbaya kwa maisha ya Wasomali. Wasomali wanapaswa kufikiri kama watu waliostaraabika na hawapaswi kujali juu ya Msomali yeyote anayeabudu dini nyengine kama vile Ukristo. Kila mtu anapaswa kupewa uhuru wa dini na uhuru wa kuabudu. Ikiwa unahisi wazo hili ni baya kwa hivyo wewe utakuwa mwanachama wa al-Shabaab na huwezi kujificha.

  • DFADFSD
    September 30, 2012 @ 05:00:10AM

    SABAHI NI YA KENYA NA HILO LINAJULIKANA. NYINYI NI MAKAFIRI NA WAUNGAJI MKONO WA MAKAFIRI. TOKENI, NYINYI WEZI MNAOFANYAKAZI KWA AJILI YA MAKAFIRI.

  • abdulahi
    September 17, 2012 @ 01:47:53PM

    Mungu atuongoze katika njia iliyonyooka, Mungu akipenda. Hali ya sasa inahitaji maombi yetu kwa Mungu ili atuokoe. Tujiepushe na kile ambacho Mungu amekataza tusikifanye. Mungu anawajua maadui wa dini na waumini pia wanawajua maadui. Ukweli utakuwa wazi kwa sababu Mungu amewaumba watu na Yeye atawatenganisha. Mungu tayari alisema mahali ambapo atawatenganisha watu wake. Jaribu kwa bidii na kuweka imani yako kwa Mungu na kuwa na imani kwake Yeye, Mungu akipenda. Maadui wa Mungu hawatakuambia chochote.

  • khadar cismaan
    September 10, 2012 @ 07:09:14PM

    Wakati wa al-Shabaab umemalizika, serikali mpya imezaliwa usiku huu na tumshukuru Mwenyezi Mungu.

  • fiita waraari
    September 10, 2012 @ 12:03:33PM

    Binafsi nadhani ikiwa suala la al-Shabaab lingekabiliwa kwa makini, watu waliotafrika ambao walidharauliwa wangekuwa wameshakombolewa muda mrefu na mtu huhisi kuwa suala hili ni mchezo tu kwa sababu kwa karibu ya mwaka majeshi ya serikali yameshindwa kuigusa Kismayu. Kwa hivyo, ikiwa suala hili ni sahihi, kitu gani kinazuwia? Binafsi sina jawabu kwa swali hili.

  • JAMES
    September 6, 2012 @ 05:32:23AM

    KAMA WAPO WAISLAMU WA KWELI WANAOELEWA VYEMA DINI YAO, KWA NINI HAWAJI JUU KUPINGA VITENDO HIVI VYA KISHENZI VYA AL-SHABAAB? BADO SIJAONA JINSI UISLAMU UNAVYOFAHAMIKA KUWA WA AMANI. WALA MTUME WAO AU KORAN HAILAANI VURUGU. TENA, NI WAOGA WANAJIHUSISHA NA VURUGU KWA NJIA AMBAYO MTU SHUJAA HAFANYI. NINAUDHARAU UISLAMU NA KILA KITU KINACHOKISIMAMIA.

  • kithetu
    September 5, 2012 @ 02:45:56PM

    Kinachowafanya watu watofautiane na wanyama ni kitu kimoja, “Binadamu anaweza kufikiri” kwa hivyo ni kufikiri kumruhusu kaka/dada/mama/baba…n.k. kuteseka wakati wewe ndio sababu ya tendo hilo? Wanaume na wanawake, tudumishe amani na upendo.

  • Gilly
    September 4, 2012 @ 09:16:50AM

    Asante Sabahionline kwa kuripoti kuzuri. Al-Shabaab wanatokana na mfalme wa ukatili; Shetani. Lao ni wizi, mauaji na uharibifu. Yesu alikuja kupeana maisha na maisha kwa wingi. Wasomali tafadhalini, mwelekeeni Yesu kwa kutibiwa ardhi yenu na maisha kwa wingi. Mtawazeni kuwa mfalme wa nchini yenu, Amin.

  • Nyangi nyateko
    September 3, 2012 @ 07:32:55AM

    Maombi ya amani kwa watu wote. Kwa muda mrefu nilikuwa ninadhani kuwa neno UIslamu linamaanisha amani ... sasa linaonekana kama vitisho. Watu wangapi wanahisi hivyo hivyo wanapoona mwanamke aliyevaa buibui anaingia dukani? Kinachotokea ni watu kununua kwa haraka haraka na kuondoka kabla ya kushuhudia umwagaji wa damu, hiyo ni kama utakuwa na bahati ya kutosha.

  • REAGAN AGUKO
    September 3, 2012 @ 05:34:36AM

    Naamini kuwa sote kwa umoja wetu tutawashinda maadui. Kila kitu kinawezekana kwa Mungu.

  • otwori
    September 3, 2012 @ 04:40:46AM

    Kuna tatizo gani katika ulimwengu wa Kiislamu? Kutokuwepo na utulivu duniani kote siku zote kunasababishwa majamaa hawa Waislamu kuanzia nyakati za Goliath wa Palestina hadi leo. Nyinyi watu mnataka nini? Mmeifanyia ugaidi dunia nzima kwa kisingizio cha kupambana na Marekani na washirika wake kwa sababu ya kiburi, kwa hivyo? Samahani, mnatumiza baadhi ya tabiri katika Biblia licha ya ukweli kwamba mmepiga hatua ya propaganda. Ni za asili lakini subiri kwa kupepesa jicho, nyinyi ulimwengu wa Kiislamu na wengine kama binadamu mtateketea daima kwa sababu kwa kuifanya dunia ambayo Mungu aliimba kuwa ikalike kwa amani lakini mmeifanya kuwa motoni kabla ya wakati ulioteuliwa. Angalieni kile mnachofanya kwa jina la Jihadi, mauaji ya watu wasio na hatia kupitia kujitoa muhanga kwa sababu ya itikadi za kishenzi za kuingia peponi. Nani aliwaambia kuwa kuwaua watu wasiokuwa Waislamu kama mnavyouita ulimwengu wa wasiokuwa Waislamu ni makafiri (neno lisilo na maana) kwamba mtazawadiwa pepo ya maisha?. Waungwana, Mungu ni mmoja ambaye aliumba dunia hii nzuri na kwa hivyo hamna haki ya kuwahukumu watu wengine kwamba vita vyenu ni kuwaona wakazi wa dunia yote wanasilimishwa. Kitu mnachokosea sana, mtajuaje kama nyinyi ndio mnaofanya mema mbele ya Mungu, kwa vile ni yeye tu. Acheni kuwahukumu watu wengine kwa kuwaua wakati nyinyi hamjui mustakbali wenu. Angalieni wale kwa jina la Uislamu, vijana na elimu yao yote, walifanya tarehe 9/11. Ni aibu, waliangamia na pia waliangamia watu wengine wengi wasio na hatia na ajali nyingi. Asanteni.

  • PKOFA
    September 2, 2012 @ 08:00:46PM

    Mungu isaidie Somalia ili kushinda mateso.

  • shykal
    September 2, 2012 @ 02:07:45AM

    Sasa niwazi kuwa al-Shabaab wameshindwa na hii ni kutokana na juhudi za watu wa Somalia pamoja na majeshi. Tangu kushindwa, maisha yanarejea kuwa ya kawaida na sasa watu sasa wanashughulikia kuijenga upya nchi yao. Serikali pia imeimarika kwa usalama.

  • RUTHU
    September 1, 2012 @ 10:40:21AM

    Mungu rejesha amani SOMALILAND.

  • Heaven sent
    August 31, 2012 @ 03:42:07AM

    Mungu Mwenyezi umewaumba binadamu wote katika sura yako mwenyewe. Jaalia busara zako katika nyoyo zetu na tusaidie kukumbuka kuwa sisi ni kaka na dada bila ya kujali tofauti zetu za imani.

  • abdulrahman
    August 31, 2012 @ 03:18:17AM

    Ugaidi wa Somalia unaendeshwa na al-Shabaab ambao wamekuwa wakitenda baadhi ya matendo ya uangamizaji na yasiyo ya kimaadili kwa watu wa Somalia na majirani zao. Walikuwa wanakata viganja vya yeyote aliyejaribu kutokukubaliana nao na pia kama njia ya kuwadhibiti na kuwatawala. Lengo lao kuu lilikuwa maeneo ya umma na mikusanyiko ya kijamii ambapo walifanya mauaji ya mabomu ya kujitoa muhanga na kuua mamia ya watu wakiwemo watoto wadogo. Kikundi hiki cha kigaidi kiliendelea kuteka nyara meli bahari kuu na wakati wa utekaji baadhi ya mabaharia waliweza kuuliwa, na baadaye kuomba kikomboleo. Al-Shabaab ilikuwa inazuwia kwenye miji iliyokuwa inayadhibiti isifikiwe na msaada wa chakula na madawa, kulikopelekea mateso yasiyosemeka na vifo vya maelfu ya watu nchini Somalia. Utekaji nyara wa watoto na kuwafanya askari kulikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Magaidi waliwageuza Wasomali kuwa wakimbizi na watu wa ndani waliokimbia makazi yao na kuwasababishia mateso na machungu. Walivunja viungo vingi vya familia kutokana na kuhamahama na mauaji, na watoto wengi kubaki mayatima na wanawake kubaki wajane. Kulikuwa na umwagaji damu mkubwa katika nchi ya wasio na hatia wakati kikundi wakiteketeza na kuua kila kitu njiani kwao.

  • KUSH KUSH
    August 30, 2012 @ 02:42:58AM

    NAAM! MAISHA NDIO KWANZA YAMEANZA. KARIBUNI VITA VITAMALIZIKA NA VYENGINE VITAANZA. SISI NI BINADAMU AMBAO KIMAUMBILE TUNAANDAMWA NA MIZOZO. UTAWALA MBOVU WA SOMALIA NDIO SABABU YA VITA. SOMALIA INAHITAJI KUTAWALIWA KWA WAKATI FULANI, KABLA YA KUPEWA UHURU.

  • ANITHA
    August 29, 2012 @ 04:12:53PM

    al-shaababu kama mungu anatenda miujiza sasa miujiza inatendeka kwenu hakuna damu inamwajika isiyokuwa na hatia isiume sasa niwakati wa kulipa kila baya na jema mlilolifanya enyi wANA WA MUNGU OGOPENI ZAMBI ZA MAUAJI ZISIZO NA HATIA

  • kijumbe Allen
    August 29, 2012 @ 01:03:30AM

    Kila chenye mwanzo kinamwisho,enyi wasomali mkiona mateso yanazidi,jueni hakika kuwa ukombozi un akaribia. sasa hapo fale inafitinika. alshababu wekeni silaha chini,muogopeni Mwenyezi Mungu!

  • JOHN EMM
    August 28, 2012 @ 11:11:31AM

    ABADANI ASILANI USIUWE KWA JINA LA DINI ... MTAANGAMIZWA NA KUWA HAMNA MAANA!!!!

  • Abdi
    August 28, 2012 @ 09:38:25AM

    Sabahionline ni CHOMBO CHA HABARI CHA MAREKANI na kinadhibitiwa na AFRICOM huko Djibouti. Kwa hivyo, makala zake hazina msingi wowote na ni za uongo. Wantumia madondoo yasiyo ya ukweli kutoka watu wasiokuwepo. Makala zake hazitayarishwi kwa maadili na kanuni za vyombo vya habari juu ya kutopendelea upande wowote.

  • ym
    August 28, 2012 @ 01:06:59AM

    Endeleeni, AL-SHABAAB

  • Mwongela
    August 27, 2012 @ 01:03:31PM

    Baba yetu uliye Mbinguni jina lako lisifiwe. Somalia ni nchi yetu, ewe Mungu iokoe dhidi ya hatari hii. Nguvu na Uwezo wako utawale. Viharibu na vifadhaishe vikosi vya waovu na watu wabaya na imarisha nguvu zote za wenye haki na sheria na katika ardhi ya Somalia. Hii ni dua yangu pamoja na Wasomali wazalendo kwa jina lililo juu ya majina yote mengine, jina la YESU KRISTO, Amen!

  • charles
    August 27, 2012 @ 11:10:54AM

    Al shabaab ni adui mwoga ambaye katu hatatokeza hadharani ana kwa ana na kulala hadi kila kitu kimetulia ndio wanashambulia tena. Kushindwa sio chaguo na hakuna njia, wakubali tu kuwa wameshindwa. Napenda kuwashauri wote wawe na tahadhari wakielewa kuwa shujaa daima hafi pekee yake. Hata kama kikundi kinaonesha kushindwa kidogo wanaweza kufanya kitu kikubwa wakati hatimaye watasalimu amri. Al-Shabaab hawatashindwa, bado hadi kila kitu kimalizike. Tunaweza kuyaamini maneno hayo ikiwa yatatoka kwa jeshi linalowapiga al-Shabaab na sio kutoka kwa al-Shabaab wenyewe. MWISHO. "TUTARAJIE MEMA ZAIDI LAKINI TUJITAYARISHE KWA BAYA ZAIDI".

  • Andrew
    August 27, 2012 @ 09:12:52AM

    Je kuna mtu anaweza kutuambia historia ya "al-Shabaab"? Kwa nini wanapigana, na nani hasi?

  • JAPHET BULEMELA
    August 27, 2012 @ 05:38:52AM

    Wale walio katika upande wa haki watashinda. Mungu analinda na kuonesha huruma kwa waja wake kwa uwezo wote na hakutakuwa na nguvu za kutosha kulizuia hilo.

  • Yasir
    August 26, 2012 @ 10:54:06AM

    Ni jambo la kuhuzunisha wakati wale mabwana wa vita wakitaja sisi ni vikundi vya Kiislamu.

  • mbecha
    August 26, 2012 @ 01:06:37AM

    Hongera al-Shaabab, hivi karibuni tutaungana nanyi na tutashinda vita Mungu akipenda, sio tu katika Somalia bali Afrika ya Mashariki yote. Hamna chochote cha kupoteza. Mwenyezi Mungu (SW) awalinde na kuwaongoza kuelekea ushindi.

  • MARV
    August 25, 2012 @ 12:13:15PM

    WAJINGA WA KUTUPWA, AL-SHABAAB, MWAKANI MTASHINDWA

  • Kaburu
    August 25, 2012 @ 04:09:39AM

    Al shaabab ni hatari, wanafahamu ufumbuzi wa tatizo ni kuua, mafundisho mengine yana madhara na haya ni baadhi ya madhara hayo . Ni vyema dunia ikaungana kumaliza kundi hili pamoja na mshirika wake al qaida

  • hussein felix musau
    August 25, 2012 @ 02:51:07AM

    Yesu tu ndiye anayeweza kuleta utulivu katika nchi ya Somalia. Amri inasema: USIUE, kwa hivyo kwa nini basi kuua. Hii ni moja ya sababu zilinifanya kutoka katika Uislamu na kujiunga na Ukristo.

  • ligimilo
    August 24, 2012 @ 12:27:58PM

    Mungu ni Mkubwa, mwisho unakaribia, kwa hivyo Mungu tusaidie

  • benard
    August 24, 2012 @ 11:43:39AM

    Sisi watu walio karibu na Somalia na wananchi wa Somalia tunahitaji kuungana mkono kwa sababu kikundi hiki kilikuwa tishio kwa kanda hii. Hongera TFG

  • Juma Salum
    August 24, 2012 @ 10:27:55AM

    Ingekuwa bora kuacha vurugu kwa sababu hata Mungu wetu haipendi hali kama hiyo kwa watu wake.

  • Juma Salum
    August 24, 2012 @ 10:27:51AM

    Ingekuwa bora kuacha vurugu kwa sababu hata Mungu wetu haipendi hali kama hiyo kwa watu wake.

  • jabez churu
    August 24, 2012 @ 09:09:38AM

    Jah Mwenye Uwezo awazawadieni kwa kazi nzuri mnayofanya.

  • AMIRKEY
    August 24, 2012 @ 04:20:18AM

    AL-SHABAAB, SIKU ZENU ZA DAMU ZINAHESABIKA. MNAUA WAISLAMU NA MNAJIITA WENYEWE WAISLAMU. MTAKWENDA JEHANAMU MOJA KWA MOJA ...... HAKI ITATAWALA.

  • ismael
    August 23, 2012 @ 11:43:28PM

    Natamani kuwa ndugu zetu wa Somalia watawafuata wale wanaotetea siasa za wastani, ambao wanauelewa kwa upana juu ya Uislamu. Wanazuoni lazima pia watoe hotuba misikitini ili kueneza Sharia halisi ya Kiislamu na kukabiliana na kuibuka kwa wahubiri wa itikadi kali ambao wanahimiza ghasia katika hotuba zao. Hata hivyo, hatua hii haitafanyika kama serikali na hasa vikosi vya usalama havitaamini kwamba kuna tofauti kubwa kati ya Uislamu na huruma zake na kuvumiliana kwa upande mmoja na mawazo ya msimamo mkali kwa upande wa pili. Napendekeza kuanzishwa kwa kozi za kuwaelezea watu wa vikosi vya usalama mtazamo sahihi kuhusu msimamo mkali na kuwafundisha kwamba wao ni kama wagonjwa ambao wanahitaji matibabu badala ya kuwashughulika kama wahalifu. Mitazamo tofauti itakuwa msingi wa matibabu tofauti. Kama tutawaona wao kama wahalifu, basi tutakuwa tunataka kuwatendea ukatili na unyanyasaji na tunapaswa kuwaadhibu. Hata hivyo, kama tunaona wanahitaji mazungumzo na kutibiwa, matibabu yatakuwa tofauti kwa sababu tabia zote za mtu ni msingi juu ya imani yake. Tabia mbaya hutokana na imani potofu na hawatabadilika bila kujali ni kiasi gani wanakabiliwa na shinikizo la kimwili au kisaikolojia. Kufungua mlango kwa wanaotubu na huruma na kuwapa hisia kwamba yeyote anayetaka kutubu atasamahewa bila kushinikiza wengi wa watu hao watarudi katika njia iliyonyooka. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema (maana yake): {Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na Rehema ya Mwenyezi Mungu, Ambaye husamehe dhambi zote. Kwa hakika! Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}. Kwa hivyo, waja wa Mungu wanapaswa kutenda katika njia hii kwa sababu kubwa zaidi. Hii pia inawahusu wasamehevu na watenda maovu na hii lazima iwafanye kuacha kurudia makosa hayo hayo.

  • IRON MAN
    August 23, 2012 @ 03:36:32PM

    Nitakwenda kupambana nao!

  • Dr Simba Iddi
    August 23, 2012 @ 10:08:09AM

    Allah awafanyie wepesi wasomali amani ya kweli ipatikane na madhalimu wote washindwe.

  • lamech M Nyariki
    August 23, 2012 @ 08:30:57AM

    Sisi ni dunia ya wazima moto. Tunashughulikia matatizo tuliyoyasababisha wenyewe. Kwa vyovyote vile, hata hivyo, uhalali wa KDF nchini Somalia una sababu lakini ukweli ni kuwa Somalia itakuwa huru kutokana na vitisho vya al-Shabaab iwapo Taifa lote litaelekeza juhudi zake katika kuelimisha na sio katika silaha kwa halaiki. Tumai kuwa kila kitu kitakwenda vyema karibuni sana kwa ajili ya maisha ya binadamu. Dini ni kisingizio, kwa kweli daima haikuwahi kuzaa ugomvi hapa lakini...

  • JJ
    August 23, 2012 @ 03:11:10AM

    Mungu anataka kuwa nusuru na maafa makubwa acheni hizo

  • john joseph
    August 22, 2012 @ 07:28:53PM

    Siamini kama watu hawa ni Wasomali kwa sababu hawajali hatima ya Somalia. Watu hawa ni wauaji. Baadhi ya Watanzania wanaamini katika itikadi za al-Shabaab, hii ni hatari, hawako tayari kujifunza kutoka Somalia. Sisi huku Tanzania mara nyingi tunapokea Wasomali waliokimbia nchi yao, lakini siwafahamu baadhi ya Waislamu wa Tanzania, kwa nini hawajifunzi kutoka kwa wa Somali?

  • mapesamohamad
    August 22, 2012 @ 05:39:32PM

    kumbuka enyi waislamu acha kuuwa watu ovyo. mungu ni mwema na mungu ni wa wote lakini ninyi mnauwa watu eti ndipo mtafika mbinguni.kama ni hivyo basi mungu angeumba wailamu peke yao.lakini hakufanya hinyo.anajilipua au kulipua wengine atambue mungu ndiye wa kutoa uhai si bndamu.tumechoka kuuwa watu ovyo

  • AMOS
    August 22, 2012 @ 01:25:09PM

    SIKUBALIANI KABISA NA WALE WANAOSEMA KUWA AL-SHABAAB WANA HAKI YA KUUWA YEYOTE AMBAYE HAKUBALIANI NAO....

  • ACM
    August 22, 2012 @ 10:12:16AM

    Sio watu wa Somalia tu wanaoteseka bali hata fisi pia ambapo al-Shabaab imefanya ulaji wa fisi ni halali hadharani.

  • oscar barasa awory
    August 22, 2012 @ 08:12:38AM

    Kikundi hiki lazima kisafishwe kutoka uso wa dunia.

  • Caleb Mutambi
    August 22, 2012 @ 06:04:25AM

    HONGERA KDF, sasa tunahisi tunalindwa. Maisha yetu kama Wakenya yamo mikononi mwenu. Tunawaamini. Tafadhalini endeleeni.

  • 0787792745
    August 22, 2012 @ 04:25:45AM

    there is and wahat you fori of mimi wewe by weot na makumbati nyangi mara

  • Jama
    August 22, 2012 @ 03:26:32AM

    Katu al-Shabaab hawatashinda.

  • bush
    August 22, 2012 @ 01:42:52AM

    Siku zao zinahesabika.

  • Ndzovu
    August 22, 2012 @ 01:30:42AM

    Wanafiki hawana nafasi katika Jihadi au katika Uislamu. Wakithibitika kuwa ni watu wabaya, waacheni wachinjwe. Wale walio imara tu lazima wabakie katika vita.

  • Kitti
    August 22, 2012 @ 12:32:13AM

    Hii inaashiria mwisho wa kila kitu. Al-Shabaab, siku zenu zimekwisha. Nyinyi msalimu amri TU kwa ajili ya maisha yenu na maisha ya kaka na dada zenu kwa sababu wakati umefika na ni WENYE KUMCHA MUNGU tu watakaosimama.

  • qadar mumin
    August 21, 2012 @ 06:45:17PM

    Serikali lazima ilisimamie suala hili na kuingilia kati wakati hali itakapokuwa mbaya zaidi ili kulinda maisha ya watu, mali na maendeleo yaliyokwishafikiwa na jamii. Kwa kuhitimisha, tunahitaji kuunganisha juhudi zetu katika kuzileta familia pamoja.

  • Kalulu
    August 21, 2012 @ 09:51:52AM

    Majambazi hawa wamechanganyikiwa kwa sababu majeshi yetu yanawakaribia, sasa badala ya kupigana kama walivyoanza kuichokza Kenya kwa kufikiria kuwa askari wetu hawawezi kupigana, sasa wameshughulika kuuana wao kwa wao na kuiweka mikakati yao kuwa mchafukoge kabisa! Kwa kweli Mungu anawahukumu. Kikundi hiki cha majambazi kitamalizwa, ni suala la wiki chache tu kwa ndugu zetu wa Somalia kupata uhuru wao.

  • Dovick
    August 21, 2012 @ 06:12:42AM

    Kwa kweli kitendo cha Hao jamaa kuuana nfikiri ni neema kwa Wasomali maana kila kukicha Wasomali wanakimbia mapigano na kuingia Nchi za jirani kama wahamiaji haramu, hivyo basi ni bora hao elshabaab wauane ili iwe rahisi kuwakamata wakishapunguzana ili sheria ifuate mkondo wake

  • Kagame -Dar Young African
    August 21, 2012 @ 05:46:04AM

    Kwakweli hakuna ambae haoni wala hasikii jinsi ndugu zetu somalia wanavyoteseka na ugaidi na mauajia ya raia wa somalia -ombi langu tumeona Tanzania umekomboa nchi nyingi sana ningeomba Tanzania ijaribu kuikomboa somalia kwa hawa jamaa al-shabaab najua Tanzania inaweza.

  • Muslim Mubarak
    August 21, 2012 @ 04:45:44AM

    Mi nadhani wa kulaumiwa si alshabab wa kulaumiwa ni mataifa ya kimagharibi,ambayo yamepandikiza chuki dhidi ya uislamu na waislamu,waislamu na wakristo wameishi kwa karne nyingi wakitofautiana imani,nakushirikana katika mambo mengi na si VITA vita ya somalia imekuja pale mataifa ya kimagharibi yakiongozwa na marekani kusaidia waasi kuidondosha Serikali Halali ya kiislamu.Sasa mdadhara yake ndo haya wanakufa watu wasio na hatia mataifa haya yamekaa kando na kuzidi kufanya biashara za silaha,na majaribio ya silaha zao mpya walaumiwe WAMAREKANI NA WASHIRIKA WAKE HII NI JIHAD WALA HAINA SHAKA, MUNGU ATASAIDIA AMANI ITAPATIKANA NA HESHMA ITAKUWEPO TU.

  • JOHN
    August 21, 2012 @ 03:43:25AM

    Dada na kaka zetu katika jeshi watuondolee majangili hawa mara moja. Waendelee na kazi nzuri kwani inayoonesha mafanikio mazuri. Tuko nyuma yenu kwa asilimia 100. Shukurani zetu za dhati na dua zetu kwenu. Tuwasafishe kabisa duniani.

  • kim
    August 20, 2012 @ 03:53:39PM

    MUNGU, ubarikiwe.

  • Abdi Dhahir Malik
    August 20, 2012 @ 06:49:43AM

    Tutashinda vita hivi, Mungu akipenda. Mungu yuko upande wetu.

  • com
    August 20, 2012 @ 02:16:07AM

    Search Al-Shabaab kuwaua wanachama wake kunaashiria matatizo makubwa - Sabahionline.com

  • jahideen
    August 19, 2012 @ 01:22:51PM

    Ninaamini sana kuwa Serikali ya Mpito ya Shirikisho itashinda mapigano kwa vile Mungu daima yuko pamoja nayo. Wanachama mashetani wa al-Shabaab wataangamizwa motoni.

  • mahamudi mpoja
    August 19, 2012 @ 10:12:11AM

    kama kuna dini inayoruhusu kuuwa hiyo ni dini ya shetani. mara nyingi watu wajiita waislamu na wanauwa watu bila huruma, kwa kujilpua kwa kuwachinja, kuwatwanga mawe hadhrani.mtu anapojilipua huuwa hat wasio na hatia tumeshuhudia kenya, nigeria, uganda n,k.naomba nifahamshe mtume mhamadi alihubri kuuwa watu ovyo na je kuna tofauti gani kati ya ugaidi na uislam?je mungu wetu ni wa kuuwa au wa kuponyesha

  • kims job
    August 19, 2012 @ 10:02:36AM

    Asanteni vikosi vyetu vya Kenya kwa kazi nzuri mnayofanya.

  • Jonas Jack
    August 19, 2012 @ 08:20:30AM

    Kamwe al-Shabaab hawatashinda. Naipongeza serikali ya kenya kwa maamuzi yao kuisaidia somalia katika vita ili kuing’oa al-Shabaab na kuokoa maisha ya watu wa Somalia. Nadhani hii ni changamoto kwa nchi zingine za Afrika kuwa na mwamko kama huo kuungana na kuzima mapigano hayo kwa hali na mali. Poleni wasomali kupoteza ndugu zenu.

  • Lovemore kwanjiwa
    August 19, 2012 @ 08:04:24AM

    Lini mtaacha tabia ya kuuana wenyewe kwa wenyewe? Angalieni mnatoka wapi na mnakwenda wapi...sitisheni mapigano!!!!!!!!!!!!!!!!

  • waithaki
    August 19, 2012 @ 07:28:18AM

    Shukurani kwa Mungu kuwa mara hii sio Muhamed, Muhamed Kamau, Muhamed Njoroge, Muhamed Mutizo au Muhamed Otieno. Tafadhalini vijana wetu rejeeni nyumbani katika vijiji vya Kangema, Masako na Siaya na mtubu tu vyenginevyo vijana hawa wendawazimu wanaoitwa al-Shabaab wataendelea na kukata tamaa kwao na watawauweni nyote wanaowaiteni majasusi. Tumeshawasameheni licha ya kuwa mliwapiga mabomu mama, dada zenu, n.k.

  • samuel
    August 19, 2012 @ 06:03:08AM

    Hawa maalshabbab bana si wajikate tu ama wajitie kitanzi coz wanalose n its my hope they lose.

  • SEIDU
    August 19, 2012 @ 04:40:09AM

    Al-Shabaab huwa wanapata silaha kutoka wapi? Naamini kuwa wanapata msaada kutoka mataifa yenye nguvu ambayo hayana haja ya amani nchini Somalia. Mataifa haya yanafaidika katika uuzaji wa silaha. Uislamu unafundisha wazi kuwa yeyote anayeua mtu lazima na yeye auliwe. Sifahamu Al-Shabaab wanayatafsiri vipi mafundisho haya.

  • SEIDU
    August 19, 2012 @ 04:40:09AM

    Alshabab wanatoa wapi silaha? Mimi naamini kuna mataifa makubwa yapo nyuma ya Alshabab na Koo za kisomali.Mataifa haya yanafaidika kwa kuuza silaha.Islamic teachings inaeleza bayana kuwa,Atakayeua mtu basi naye auawe.Sijui Alshabab wanatafsiri vipi mafundisho haya.

  • king feisalali
    August 19, 2012 @ 04:15:32AM

    Kwa mimi sio wazuri kwa sababu wanawaua watu wasio hatia kila mara.

  • willy
    August 19, 2012 @ 02:28:18AM

    Dini na imani za kidini, na utekelezaji wake ni mambo ngumu, wote na baadhi wanahitaji kutambua na kufahamu kuwa dini ni suala binafsi na la ushirikiano na kwamba kila mmoja wetu anahitaji kuelewa la sivyo tutaangukia katika uchoyo na mafundisho hatari na yanayopotosha, fikra potofu ambayo itamchukua mtu milele. Binadamu wazingatie upana huu wa dini hata kama tunaachagua kuabudu muumba wa kweli wa pepo, ardhi na vyote vinavyoishi na visivyoishi. Binadamu wote pia wakubali ukweli kwamba mwisho wa maisha yetu hapa duniani utakuwa mmoja juu ya Mungu mmoja na kwamba binadamu wote kwa jumla mafundisho yanayokubalika kwa jumla katika dini zote za ulimwengu. Kwa hivyo, sote tuna jukumu la kuhakikisha kuwa sisi ni watu wa dini ya kweli iliyojikita katika imani binafsi na sio katika mafundisho ya watu wengine na kufahamu dini na udini unahusu nini.

  • Dr.Ngonyani
    August 19, 2012 @ 01:18:31AM

    Nashindwa kujua hasa kinachopiganiwa ni kwa maslahi ya WASOMALI au watu wengine waroho na wasio na huruma ya masikini wa somali land!!!watu hawa wamuogope mungu,watu wanaoteseka sana na hali ilivyo sasa somalia hawana hatia hata kidogo,na wala hawafahamu lolote kuhusu serikali,na tena hawafahamu vita!!ANGALIA WATOTO WALE WANAKUFA KWA NJAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  • xuseen
    August 18, 2012 @ 05:24:08PM

    Karibu kila kitu kimemalizika kwa Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia. Viongozi wa dunia wameipa muda serikali ya Somalia kuanza uchaguzi tarehe 20 Agosti 2012. Hata hivyo, tutaona kile kitakachotokea mjini Mogadishu siku zijazo. Na kuhusu al-Shabaab, majeshi ya AMISOM yameshakiteketeza kikundi cha al-Shabaab, bado kumebakia ngome moja tu imara kutekwa ya Kismayo. Jirani yetu Kenya ilisema ndani ya wiki moja litakuwa ndani ya Kismayu, kwa hivyo jambo pekee ninaloweza kusema ni kutumai bora zaidi hapa ambapo ninatoka.

  • JUMA MANASE
    August 18, 2012 @ 03:04:24PM

    SIDHANI KAMA NI BUSARA KUUA WATU KAMA HIVYO. NINAJIULIZA MWENYEWE KWA NINI WAISLAMU WANATAKA KUUA WATU WASIO NA HATIA? WAO WANAMUABUDU NANI? JE, MUHAMMAD ALIWAAELEKEZA KUUA? NI AINA GANI YA DINI INAYORUHUSU KUUA? TAFADHALINI TUMECHOSHWA NA MAUAJI YA WATU WETU NA NYINYI MNAICHAFUA DINI YA KIISLAMU.

  • cabdiqani cabdilaahi aadan
    August 18, 2012 @ 02:43:51PM

    Inatia wasiwasi kweli. Mungu awaongoze njia iliyonyooka vijana hawa waliopotoshwa na kufanywa wajiingize katika matendo ya dhambi kwa jina la jihadi (vita vitakatifu)? Ndugu zangu, vita vitakatifu vina masharti yake ambapo vinaweza kupiganwa. Muogopeni Mungu wenu na mtubu kwa vile toba inakubalika. Kama kweli mnataka kupigana vita vitakatifu, subirini kwani Mungu ataleta vita vitakatifu vya haki na acheni kuua watu wenu. Watu hao waliotangaza vita vitakatifu kwa maslahi yao wenyewe na kuwaambia vijana wawe wauwaji wa mabomu ya kujitoa muhanga au kupigana kwa jina la Mungu, mmoja wao akiwa mtu anayejulikana kama Hassan Hussein, hawakuwahi kuonekana hata mara moja akipigana kwa kile wanachokiita vita vitakatifu na waliobakia ni sawa na yeye. Hakuna yeyote kati ya hao wanaojiita viongozi aliyetekeleza uuaji wa bomu la kujitoa muhanga. Kwa nini badala ya kuwapotoa vijana, hawashiriki wao katika kujitoa muhanga kwa mabomu kama ni kweli watazawadiwa pepo? Muogopeni Mungu wenu, ndugu zangu.

  • haarun
    August 18, 2012 @ 06:53:47AM

    Ripoti hii sio ya kweli. Yule aliyeiandika na watu wanaoiunga mkono wote ni wamoja.

  • Sam
    August 18, 2012 @ 04:00:19AM

    HUKUMU ILIPITISHWA KWA AL-SHABAAB WOTE SIKU WALIPOUA BINADAMU WA MWANZO ASIYE NA HATIA, IWE MUISLAMU, MKRISTO, KAFIRI AU MWENGINE YOYOTE. WATAKUWA WAO WA KUPIGWA RISASI YA MWISHO IJAPOKUWA WENYEWE KWA WENYEWE WAKATI MTU WA MWISHO ATAKAPOKAMATWA NA KUSEMA WALITOKEA WAPI. SOMALIA ITAKUWA HURU. SOMALIA ITAFANIKIWA.

  • ikon mwalo
    August 18, 2012 @ 02:31:45AM

    Hongera kwa K.D.F. Tunaelewa kuwa al-Shabaab ni waoga na watu wanaoangalia maslahi yao na tumefurahi kwamba kikundi hiki sasa kinavunjika… Tunatarajia amani kubwa.

  • Muema katavi
    August 17, 2012 @ 03:42:42PM

    Lini watu wa Somalia watafaidika na dakika moja ya utulivu? Upotelee mbali uoga wa Marekani na Waislamu wenye siasa kali waliopotoshwa. Wanaishi kwa kupigana na wanaowaona tu ambao daima wanapiga mikono chini katika makutano yoyote?

  • alex mwanake
    August 17, 2012 @ 02:20:35PM

    Sisi Wakenya tunajua tunachokifanya kuwatoa Al-Shabaab ndani ya nchi yao. Inasemekana ikiwa diplomasia inashindwa, nguvu itatumika. Askari wa Kenya endeleeni hivyo hivyo.....mpaka watakapopotea.

  • james protace
    August 17, 2012 @ 02:16:43PM

    Al-shabaab wanatakiwa kufutika kwenye uso wa dunia

  • kabatha
    August 17, 2012 @ 01:46:03PM

    Matatizo ni Wamarekani walioingilia baina ya Kenya na Somalia ambayo ilikuwa ni kazi ya ndani kama ile iliyotokea katika World Centre ambako Wayahudi na Wamarekani walihusika na milipuko ambayo iliufanya ulimwengu uamini kuwa yalikuwa ni mashambulizi ya kigaidi. Watakuja na kila aina ya mbinu za kibinadamu lakini siku moja watakuja kulipa.

  • rome ngetich
    August 17, 2012 @ 09:19:10AM

    Mungu ndiye pekee aliyeumba na anayechukua maisha yetu.

  • sam
    August 17, 2012 @ 08:08:49AM

    Hongera KDF...Siku zote tunawaoombeeni. Zidisheni vita mpaka wote (al-Shabaab) watakapo sagwasagwa!!!!!!!!!

  • Saido Omar
    August 17, 2012 @ 07:51:53AM

    Kuna watu wengi katika kikundi cha al-Shabaab waliojitoa na kujiunga na vikosi vya serikali, na kujitoa huku ni ishara muhimu ya kuwepo kwa haki kwa machafuko na mgawanyiko ndani ya kikundi. Kujitoa huku ndani ya kikundi cha al-Shabaab karibuni kumetokea katika njia mbaya kutokana na mafanikio ya vikosi vya Umoja wa Afrika katika kudhibiti miji ya kimkakati nchini, ambayo ilikuwa inadhibitiwa na kikundi, na ambayo imejitenga na viunga vya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Mwisho wa al-Shabaab uko karibu, kwa vile imekabiliwa na upotevu mkubwa katika kipindi kilichopita.

  • Diini
    August 17, 2012 @ 06:49:57AM

    Kwa mawazo yangu, naamini uongozi wa nchi hii lazima upewe kikundi chochote ambacho kinaweza kuwasaidia watu, iwe al-Shabaab au serikali ya mpito ya shirikisho, lakini tunapendelea kikundi ambacho kitatawala kwa kutumia sheria ya Kiislamu kwa vile sisi ni Waislamu.

  • Ngash
    August 17, 2012 @ 06:40:09AM

    Vita gani hivyi vitakatifu? Kama wao ni wanaume wa kutosha, basi wajitokeze hadharani.

  • adesh
    August 16, 2012 @ 01:33:07PM

    Mnaota, hamtawashinda al-Shabaab. Mtakufa nyote kwani wao ni jeshi la Mungu, Mungu akipenda watawasaga. Niko katika wilaya ya Kerugoya nchini Kenya.

  • STEVE
    August 16, 2012 @ 11:36:02AM

    Hongera kwa KDF, Amerika na nguvu zote zinazowapiga NGURUWE hawa WAPUUZI,WASO FADHILA..N.K..!

  • steve
    August 16, 2012 @ 11:31:16AM

    Wote al-Shabaab na wafuasi wao nchini Kenya na popote pale ni WAPUUZI. Ningekuwa rais wa nchi hii, ningekuwa nimeshawatokomeza wote kwa sababu ni watu hao hao ambao wanafanya mashambulizi haya ya mabomu nchini hasa makanisani. Kwa nini wasiende kuwashambulia Waislamu wenzao misikitini?..

  • Evance Komu
    August 16, 2012 @ 09:09:59AM

    Kwanza inatakiwa ijulikane hawa Al Shaabab wantoa wapi hizi silaha nzitonzito na inafanyika hivyo kwa maslahi ya nani? mimi siamini kama kuuwa watu kwa migongo ya dini ni kwenda mbinguni au kuepuka hukumu kali siku ya mwisho. Al Shaabab ni kundi tishio sana na halitakiwa hapa duniani!!

  • moses Nganga
    August 16, 2012 @ 07:11:29AM

    Iwe kulikuwa na dhuluma ya kihistoria iliyofanywa kwa mtu yeyote ikiwa ni pamoja na wale masheikh haiwapi nafasi wa kuua wananchi wasio na hatia. Tumekwenda mbali katika eneo lao na tutaweza kwenda mbali zaidi ikiwa tu mlingano utakuwa na uwiano. Hata hivyo, serikali na mataifa ambayo yamekuja kusaidia Wasomalia lazima wafanye hivyo kwa mioyo safi na sio kwa matakwa ya kichoyo. Wawe al-Shabaab au raia wema, wote wana haki ya kuishi!

  • abuarafat
    August 16, 2012 @ 04:40:37AM

    Mimi skielewi hiki kikundi kwa nini iwauwe wanachama wake hadharani? Ikiwa ni hukumu ya kijeshi si wangechinjana huko kambini kwao badala ya kuwaaaninka hadharani? This scaring even to normal wananchi Somalis

  • TIM
    August 16, 2012 @ 04:40:28AM

    Hawa ni waoga wanaojificha nyuma ya dini ili kumwaga damu.

  • john
    August 16, 2012 @ 02:21:32AM

    Al-Shabaab na imani zao za kipuuzi wako nyuma kiteknolojia. Badala yake wanatakiwa kuendelea kila wakati teknolojia inapoendelea. Kama msemo unavyosema, "Kama msemo unavyosema "kama utaanguka kikamilifu utakuwa mpumbavu". Vijana wale wenye tamaa lazima wafunzwe tabia njema ya kutoendeshwa na mapenzi ya fedha bali waendeshwe na sifa za kibinadamu. Wanapaswa kutofuata viongozi wao kwa upofu kwa kumwaga damu ya binadamu ovyo....

  • Mudus
    August 16, 2012 @ 01:47:34AM

    Hao majamaa WATAANGAMIA kabisa!!!!!!!

  • عادل
    August 16, 2012 @ 12:24:20AM

    Umasikini na njaa ambavyo Somalia inatesekea navyo kutokana na vikundi vya ugaidi ambavyo vimeiba kila kitu nchini, ikiwa ni pamoja na msaada na ruzuku zinazotolewa kwa Somalia. Vikundi vimeiba hivyo ili kuongeza mateso ya wananchi wasio na hatia ambao wamevumilia sana kwa sababu ya kuwepo kwao. Ni lazima kuvizuia vikundi hivi, na kuzuia vitendo vyao dhidi ya wananchi. Ni mara ngapi vikundi vimepigana wenyewe kwa wenyewe, na kusababisha kuanguka kwa wahanga wengi wakati wa mashambulizi yao? Ilikuwa ni lazima kwamba vikosi vya usalama kupambana navyo tangu mapema vikundi hivi, kwa sababu mashambulizi wanayolenga dhidi ya wanajeshi na kuua watu wake. Vikundi hivi vya kigaidi vimechafua sura ya Somalia ulimwenguni. Zaidi ya hayo, wanaifanya Somalia itengwe na dunia yote. Lakini, mpango wao huu haukufanikiwa na vikosi vya usalama vimeweza kukabiliana nao, kwa kushirikiana na mifumo mengine ya usalama.

  • kindege
    August 15, 2012 @ 06:56:41PM

    ikopoa

  • hamis suleman
    August 15, 2012 @ 03:23:46PM

    alshabab kamwe hawata shinda ni ujinga tu wakuto elewa imani na kudanganywa na waarab!! stupid!!

  • izo
    August 15, 2012 @ 07:53:27AM

    Siku zao zinahesabika. Mungu mwenye uwezo mkubwa ulimwenguni atawasaga mmoja mmoja.

  • lyn
    August 15, 2012 @ 05:18:04AM

    Mungu atawalaani na katu hawatakuwa kama walivyokuwa. Hawawezi kuendelea kuua watu wwa Mungu kama wanavyofanya. Hili lazima lisitishwe, kwa Mungu wa Mbinguni! Ikiwa wao ni Ibilisi na wanatafuta damu, waende kuua wanyama kama ni lazima kuua viumbe hai.

  • DENNIS YEGON
    August 15, 2012 @ 02:59:28AM

    Ikiwa wanaamini katika vita, kwa nini wanawaua majasusi? Inaelekea kama kitengo chao cha intelijensia ni dhaifu na kuwaua ndio chaguo lao. Kwa vyovyote vile, Mungu yupo kwa kuiokoa hali hii, Amin, Amin.

  • DENNIS YEGON
    August 15, 2012 @ 02:31:03AM

    Ikiwa wanaamini katika vita,kwa nini wanawaua majasusi? Inaelekea kama kitengo chao cha intelijensia ni dhaifu na kuwaua ndio chaguo lao. Vyovyote vile, Mungu yupo hapo kuiokoa hali hii, Amin, Amin.

  • jackson Jerome
    August 14, 2012 @ 04:02:17PM

    kila kitu kina mwisho kama osama ameshindwa hata wao watashindwa,marekani na mataiifa mengine yasaidie na ziongeze wapelelezi wa kutosha na wawawezeshe mawasiliano yenye nguvu na masafa marefu bila mitambo ya al shababi kunasa.vile vile serikali ya sudani iunge mkono hadi mwisho.

  • christine mutula
    August 14, 2012 @ 08:42:22AM

    Naamini Mungu amekuja kuikomboa Somalia kutoka mikononi mwa washirika hawa wa Shetani ambao wameinakamisha nchi na kuua watu wasio na hatia. Hebu dunia yote isimame na kuiokoa Somalia.

  • parachute
    August 14, 2012 @ 07:08:49AM

    Kimbieni al-Shabaab...Kimbieni!

  • Alshabaabi
    August 14, 2012 @ 05:14:40AM

    Idumu al-Shabaab, magaidi nambari 1 wa ulimwengu? Ninawapenda kwa sababu wanawafanyia ugaidi magaidi wakuu ambao ni Wakristo... kwa mfano Marekani, Uingereza, Ethiopia na Kenya pia.

  • Anna Msuya
    August 14, 2012 @ 03:26:43AM

    hiyo ni laana tosha kwa Alsabaab kwani mwisho wao wakutawala umefika kwa hiyo watamalizana wenyewe kwa wenyewe kwani mtenda dhambi hujilaani mwenyewe kwanza mfijana wenyewe wanaoshiriki hiyo vita niwadogo kiasi kwamba hawawezi kuhimili vita visivyo kuwa na mwisho ndio maana wanataka kutoa siri ya viongozi wao marekani big up

  • RAMADHANI MUHIDINI SHABANI
    August 14, 2012 @ 02:33:46AM

    ILA MI NAAMINI NJIA BORA SI YA KUUANA.ILI WATU WANATOFAUTIANA.NI SAWA NA KUSEMW UNAMUUA MGONJWA WA UKUIMWI ILI ASIENDELEE KUAMBUKIZA.ILA HUKUMU YA MUNGU NI YA MWISHO..SI SOLUTION

  • عبد الرحمن الدسوقي
    August 14, 2012 @ 02:28:17AM

    Wananchi wa Somalia wameshateseka sana kutokana na ugaidi. Hizi harakati zina dhamiri ya kuyumbisha usalama wa Wasomali na kufifisha hatima yao. Magaidi wengi wamefanya uhalifu mbaya sana ili kukamata udhibiti wa sehemu nyingi za Somalia; hasa kwa sababu Somalia haina mfumo imara wa usalama. Hii imerahisisha kuenea kwa vikundi vya magaidi nchini Somalia na kuigeuza nchi kuwa uwanja wa vita baina ya wananchi wasio na nguvu na harakati za magaidi na kusababisha fujo nchini Somalia. Nchi hii iliyo nzuri imekumbwa na njaa na uchumi mbaya sana. Umasikini na njaa vimeivamia Somalia, kwa sababu harakati hizi zimekuwa zikiiba misaada inayoingia katika ardhi ya Somalia kabla ya kuifikia serikali. Hili linafanya hali kuwa mbaya zaidi ndani ya ardhi ya Somalia.

  • Hussein Rajabu Sendaro
    August 13, 2012 @ 08:00:20AM

    Wengi wa wachangiaji hawajui historia ya wanachokieleza.Somalia ilikuwa imetulia chini ya Mamlaka ya Kiislamu na wasomali walikuwa wanaishi kama ndugu.Kwavile Marekani ni adui mkubwa wa Uislamu akachokonoa mambo na hatimaye alichokitaka ndicho kinachoigharimu Somalia mpaka sasa.Kaiondoa serikali halali ya kiislamu na kuweka mapandikizi ambayo yameshindwa kuendesha nchi na mpaka sasa hakuna dalili za amani,Insha allah !Mungu mkubwa siku moja amani itarejea kwa uwezo wake yeye na wala sio Marekani wala Mapandikizi yake

  • ME
    August 12, 2012 @ 02:30:29AM

    Ikiwa waoga hawa wanamwamini Mungu kwa nini basi wanawaua watu wasio na hatia katika kanisa nchini kenya, kwa mfano walirusha maguruneti ndani ya kanisa na kuwauwa waumini na kuwajeruhi wengine. Ikiwa wana matatizo na serikali ya Kenya ambayo inaongoza OPERESHENI LINDA NCHI nchi Somalia, basi watoe malalamiko yao kwa njia nyengine lakini sio kulenga dini. Wakristo na Waislamu wamekuwa wakiishi pamoja kwa miaka mingi na wataendelea hivyo kwa karne nyingi zijazo. Kenya sio taifa lililoshindwa kama Somalia na KDF litawasafisha na kuwatoa wote. Waendelelee kuwaua watu wengine lakini wasiwaletee Wakenya UPUUZI WA JIHADI….

  • Cabdikarim Awes
    August 11, 2012 @ 04:19:28PM

    Ni vizuri kusikia habari hii

  • Adrian Mbwambo
    August 11, 2012 @ 09:45:03AM

    tunashukuru kwa hilo..........

  • Aman Suleiman
    August 11, 2012 @ 09:18:43AM

    Ni upuuzi kufata imani isiyokuwa na taswira, yoyote yule amwagaye damu ya bin adam mwenzake lazima ajue kuwa ni mfuasi wa shetani na sio Allah, na waumini wa kikundi au dini yoyote inayoamini kwa kuuwa bin adam wenzake eti watapata thawabu kwa mwenyezi Mungu ni upuuzi mtupu, God is not stupid like that. Damu waliyoimwaga itawalilia na kuwamaliza wenyewe kwa wenyewe na kizazi kwa kizazi, na pia wakazi wawapuuze kwa kutokwenda kushuhudia mauaji hayo ya kinyama

  • Idd Kitambi
    August 11, 2012 @ 05:15:17AM

    Aluta Qontinua

  • geeddi
    August 11, 2012 @ 03:38:32AM

    Sijawahi kuzungumza nyuma ya simba ninayemuona.

  • xildhibaan gacma dheere
    August 11, 2012 @ 02:19:31AM

    Al-Shabaab ni wavunjaji wa haki za binadamu.

  • john nyangala
    August 10, 2012 @ 11:30:18AM

    ukiua kwa upanga nawe utauwawa kwa upanga na ndicho kinachotokea sasa kwa hao magaidi mungu sasa anawaadhibu

  • mubarak
    August 10, 2012 @ 09:42:57AM

    Al-Shabaab kimeundwa na watu ambao ni wapigananji wa vita vitakatifu na wanapigana na maadui wa Mungu na wale wanaoipiga vita dini ya Kiislamu na mtawaona wakiitawala Somalia yote, Mungu akipenda.

  • libale
    August 10, 2012 @ 09:24:32AM

    Al-Shabaab yenyewe imeandikisha watu kwa kutoa fedha kwa vijana. Uongozi wake usilalamike pale ambapo zawadi ya dola milioni 33 imewekwa juu ya vichwa vyao.

  • ezgard
    August 10, 2012 @ 08:07:07AM

    kila ovu lina mwisho wake, naamin mkonno wa mungu unafanyakazi

  • judy
    August 10, 2012 @ 06:21:36AM

    Wote watakufa vifo vyenye uchungu.

  • marigah
    August 10, 2012 @ 04:53:27AM

    Nadhani hiyo itakuwa ya kipekee kabisa

  • JEAN
    August 10, 2012 @ 03:10:03AM

    ALSHABAB NI WAKALA WA SHETANI

  • furaha mabeva
    August 10, 2012 @ 01:33:05AM

    alshabab nawaomba muwe watuliv katika nchi yenu kwasabab hamuna mtu atakaye kuja huko somalia kuleta aman ni ninyi mtakaye hakikisha amani inakuwapo huko somalia, pia hao vibaraka wa kimarekani na uingeza wao hawana nia ya kuleta amani bali machafuko, nia yao kubwa ni kuhakikisha amani afrika inatoweka kabisa. ninachoshauli ni kwamba afrika tuwe na umoja wa kutafuta suluhisho sisi wenyewe.

  • FADHIL KHATIB
    August 8, 2012 @ 12:26:23PM

    Kinacho waua wasomali mpaka leo hii ni damu ya (mashekhe) waliochinjwa kama mbuzi hapo nyuma. Hivyo, suluhisho la matatizo ya somalia ni kuruhusiwa kuwa chini ya serikali ya kiislamu kama ilivyokua awali, mbali nahivyo mapigano yataendelea mpaka Qiyama.

  • Bakilana Paschal Bashange
    August 8, 2012 @ 05:34:26AM

    Mwenyezi mungu hakutoa haki kwa binadamu kumuua mwenzie, ni yeye tu mwenye kufanya hivyo kwa namna anavyotaka kumuadhibu mtu ambaye anamkosea, Hivi hawa Al-Shaabab wamepata wapi amri ya kuua watu wasio na kosa/hatia mbele ya haki? Dhambi zao zinawarudia na wataagamizana wao kwa wao kwa sababu wote ni wauaji na mungu hataki kiumbe chake alichokiumba kihukumiwe na mwanadamu mwenzie, hiyo ni raana ya mwenyezi mungu

  • jeff japheth
    August 8, 2012 @ 04:46:53AM

    Hakuna ubaya unaoweza kuepuka adhabu! Utukufu uwe kwa Mungu!

  • jimmy
    August 8, 2012 @ 04:42:10AM

    Hivo ndivyo njia inavyotakiwa, lazima al-Shabab ijue kwamba huu ni wakati wao wa kuondoka.

  • Ignas mutalemwa
    August 8, 2012 @ 02:35:33AM

    Poleni sana ,kuna ndugu zenu wanateseka sana huko msumbiji, wanaishi kama wanyama sababu kukimbia hiyo vita. malizeni vita ndugu zenu walejee kwao,

  • Muumin
    August 8, 2012 @ 01:36:59AM

    Walio katika njia sahihi watashinda. Allah huwalinda na kuwarehemu waja wake kwa nguvu yote na kwamba hakuna mwenye ubavu wa kuzuia.

  • hashil ally
    August 7, 2012 @ 08:29:38AM

    Alshabab bado wana nguvu na watashinda kwani ninavyoamini katika vita yoyote kuna kushindwa halafu baadaye mapambano yanaendelea, kwa hiyo hao vibaraka wa mmarekani na uingereza wajue watapata shida baadaye.

  • samuel m opingo
    August 7, 2012 @ 04:29:27AM

    Matayo 10:28 Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Badala yake, kuwa na hofu na yule awezaye kuangamiza mwili na roho katika moto wa Jehanamu. Waebrania 10:31 Ni jambo la kuogopa kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.

  • xyk
    August 7, 2012 @ 04:21:28AM

    Al-Shabaab ni zao la ujinga wa Waislamu wengi na hawawezi kuushinda uhuru, wengi wa watu hawa wanatoka Somaliland.

  • Albert Njoroge
    August 7, 2012 @ 02:41:24AM

    Aibu kwa wanaowaunga mkono na kuwapatia fedha al-Shabaab, wanaofikiria kuwa wanamtumikia Mungu kwa vitendo vya kishetani. Mungu wao ni dhaifu, anahitaji ulinzi wa binadamu.

  • walter
    August 6, 2012 @ 03:24:22PM

    inapendeza mnavyotupa habari kama hizi endeleeni kutuletea na nyingine zenye uchambuzi wa kina

  • salaad
    August 6, 2012 @ 07:40:19AM

    Al-Shabaab ilikuwa inajulikana tangu mwanzo kwa kutoijali Somalia na wanachama wake karibu wote walikuwa wageni wenye itikadi potofu ya vita vitakatifu akilini mwao lakini wengi wao sasa wameijua al-Shabaab, isipokuwa wachache tu ambao watajua karibuni.

  • Charles Mwangi
    August 6, 2012 @ 04:28:27AM

    Ni nzuri, kuwa fisi ameanza kula utumbo wake mwenyewe. Ahadi ya kutoa zawadi nono kwa vichwa vyao inafanya maajabu kwa vile wengi wao wanahamasishwa na pesa, na sio itikadi. Itakuwa nafuu kubwa sana (hasa kwa Wasomali) wakati kikundi cha al-Shabaab kitakapomalizwa daima.

  • Jeexlibaax
    August 6, 2012 @ 02:42:59AM

    Al-Shabaab wanakuwa dhaifu kama jua linalotua lakini tahadharini na wale Wasomali walio na maslahi mamoja wakati fulani watapigana wenyewe kwa wenyewe baada ya al-Shabaab kutokomezwa kwa sababu lengo lililowaunganisha lilikuwa kupambana na al-Shabaab. Kuweni na tahadhari juu ya ukweli huo na mlitie akilini.

  • baabaa
    August 5, 2012 @ 01:14:41PM

    Inaeleweka kwamba watu sio waaminifu wa dini wanayodai kuilinda kwa hivyo kuitumia ili kukidhi maslahi yao ya kichoyo kwa kuwapotoa wengine kwa itikadi zao potofu. Hili linanisikitisha sana. Ningependa kuwaomba Wasomali kuasi waziwazi dhidi ya watu wanaoua wengine bila ya sababu yoyote wakati wote.

  • nb
    August 5, 2012 @ 09:49:36AM

    Kwa kuwa Mungu anawapenda watu wake waacheni waadhibiwe mara mbili kwa sababu walimfanyia makosa. Ni wakati wao sasa wa kuteseka kama ambavyo wamekuwa wakiwaangamiza na kuwaua watu wasio na hatia.

  • EMMANUE LOI
    August 5, 2012 @ 07:25:28AM

    Big up mwandishi wa makala hii, unatuhabarisha mambo muhimu

  • Macherino
    August 5, 2012 @ 06:33:01AM

    Tukitaka tuinusuru Somalia basi ni lazima turejee nyuma kidogo,Siadbare alifanya makosa ambayo hadi sasa yanaizuru Somalia, lakini inawezekana kabisa, unajua Wasomali ni Waislam na waislam si wakaidi basi ni bora Somalia ipewe mamlaka kama ilivyokuwa pale mwanzo, ikiongozwa kwa sharia hii ndio (solution)

  • lwidiko Mgalilwa
    August 4, 2012 @ 03:05:41PM

    Kilicho na mwanzo hakikosi mwisho. Mungu yupamoja na wasomali wapenda haki.

  • ceel daar
    August 4, 2012 @ 01:34:49PM

    Sawa.

  • jacob kabaya
    August 4, 2012 @ 12:36:45PM

    Nina imani na serikali ya mpito ya shirikisho.

  • mwaura ndura
    August 4, 2012 @ 12:07:22PM

    Dua zangu ni kuwa siku moja wanawake, watoto na wanaume wa Somalia waishi kwa amani kama mtu yeyote duniani. Al-Shabaab lazima waondoke sasa. Asanteni Jeshi la Ulinzi la Kenya, askari shujaa wa TFG na AMISOM.

  • xabsa maxamed
    August 4, 2012 @ 09:34:32AM

    Naamini ikiwa serikali ya shirikisho ya mpito iko sahihi, itafanikiwa kwa kupata imani ya wananchi.

  • philip makungu
    August 4, 2012 @ 07:16:25AM

    ni bora wasomalia woote wakaungana na kupigania nchi yao maana ni bora muwe na umoja wa nchi maana wanaoteseka ni wao na hasa watoto na wanawake nawashauri wasiikimbie nchi yao wakae wapambane

  • dr.marm
    August 4, 2012 @ 04:20:46AM

    tatizo la makundi ya kigaidi ni kutoaminiana na kwakuwa wanachokifanya ni dhambi mwisho wa siku huukizana wenyewe kwa wenyewe'na hapo ndo kusambaratika kunapokuja na mwisho wa magenge ya waovu hao ndo unafika,nai-penda.

  • Albert Wanjofu
    August 4, 2012 @ 04:14:17AM

    Nimefurahi kuwa hili ni mwanzo wa njia kuelekea dunia iliyo salama zaidi. Ninaunga mkono juhudi za kupunguza uwepo wa kikundi hiki cha kigaidi ambacho kimesabababisha maangamizi na woga kwa watu wote duniani.

  • rASHID
    August 3, 2012 @ 10:14:49AM

    HATIMAYE WATASHINDWA

  • sosopi pa
    August 3, 2012 @ 06:53:11AM

    iko poa!

  • MURACHAANA
    August 3, 2012 @ 05:38:25AM

    Ni wazi sasa kwetu sote kuwa watu hawa wenye imani dhaifu wanasema kwaheri kwa kuuwana mmoja wao. Dunia ina kila sababu ya kutabasamu juu ya hili. Tuombe sana kwa ajili yao kwa kumaliza vizuri na si iliyo mbaya.

  • Harmaton collins
    August 3, 2012 @ 05:09:38AM

    Tunaishurkuru dunia yote kwa kukubali kuingilia kati Somalia hasa Wamarekani ambao daima huwepo pale amani inapopiganiwa. Mungu ibariki Marekani.

  • ali khalid
    August 3, 2012 @ 04:50:52AM

    Shukrani kwa jeshi la Uganda. Lilikuwa la kwanza kupeleka jeshi lake kule. Watawaondoa waoga hao.

  • sety willison
    August 3, 2012 @ 02:50:54AM

    alshabab wanapowauwa wanachama namnahiyo wanategemea wakati wa uchaguzi ninani atawapigia kura wagombea maana wananchi ndio hawo wanaisha

  • shiks
    August 3, 2012 @ 01:45:58AM

    Vyenye nataka kiwango cha kuaminiana kishuke ili kikundi cha wanamgambo kidhoofike.

  • mimi
    August 2, 2012 @ 10:32:04AM

    Hongera intelijensia ya Kenya kwa kuwatoa nje wanaharamu hawa….Nchi nyenye nguvu ya Afrika ya Mashariki.

  • qorane
    August 2, 2012 @ 10:00:20AM

    Al-Shabaab ni harakati iliyotumwa na Mungu kuwaadhibu Wasomali baada ya kutupa serikali yao na kuwa na tabia kama ya wanyama. Namuomba Mungu atulinde kutokana na vikundi vinavyoleta shida hii chini ya jina ya dini. Wakati wao wa kuvunjika umefika.

  • Grace
    August 2, 2012 @ 07:21:50AM

    Somalia itanawiri tena na kuongozwa vizuri. Hilo ndio tunalotegemea. Al-Shabaab kwa sasa wanakaribia mwisho wao. Ubaya haujawahi kuushinda wema. Muda wote ambapo Mungu yuko katika kiti chake.

  • slovadan
    August 2, 2012 @ 03:23:04AM

    makala makini sana

  • Saka w.Maurice
    August 1, 2012 @ 12:33:21PM

    Wameua watu wengi wasio na hatia na sasa wanageukiana wao kwa wao. Hatimaye wote watajiua wenyewe. Hii inadhihirisha kuwa hawana dhamiri yoyote wanayoipigania.

  • Lucas Eleyo
    August 1, 2012 @ 09:44:18AM

    Al-Shabaab lazima watolewe na vikosi vya AMISOM. Kikundi hiki kimewatesa na kuwaua watu wengi nchini Somalia. Nchi imeharibiwa kabisa ambapo itaichukua serikali ya Somalia muda mkubwa kuiimarisha. Wengine duniani wanaombwa kusaidia katika kuijenga upya Somalia wakati vita vitakapomalizika. Serikali ya kenya imeisaidia sana Somalia katika vita ili kuing’oa al-Shabaab na tunaishukuru Kenya kwa juhudi walizojitolea kuokoa maisha ya watu wa Somalia. Pamoja na hayo, Kenya isaidie kwa njia zote kwenye vita vya Somalia na maisha ya watu kwa vile sasa AMISOM inakaribia Kismayu kuwang’oa al-Shabaab nchini. Afrika inapaswa kuungana na kuibuka pamoja kusaidia kuwatoa al-Shabaab kwa namna yoyote ile. Tunataka watu wa Somalia waishi katika amani na kuendeleza nchi yao ambayo imekwama kwa muda wa miaka 24 sasa.

  • Lisa m
    August 1, 2012 @ 08:32:24AM

    Nayapenda sana.

  • cabdifataah mouse
    August 1, 2012 @ 08:28:57AM

    Nadhani kudhoofika kwa uaminifu baina ya vikundi vya al-Shabaab ni habari nzuri sana kwa Msomali yeyote ulimwenguni. Hongera nyingi kwa Wasomali na Wasomaliland na kwa heri al-Shabaab, mpo kwenye hatua zenu za mwisho!!!

  • Dr Mohamad Farah
    August 1, 2012 @ 07:17:12AM

    Ni mara ya mwanzo kujifunza au kukishambulia kikundi hiki kwa kusema kitu kuhusu wao na kunao matatizo mengine mengi yanayoikabili kikundi hiki ndani ya wao wenyewe au kutoka kwa watu.

  • raashid ali
    August 1, 2012 @ 03:35:03AM

    Naamini kuwa Serikali ya Mpito ya Shirikisho iko sahihi, itafanikiwa kwa kupata imani ya wananchi na itapata uwezo wa kuwashinda maadui kupitia njia zifuatazo: 1. Watu kuiunga mkono. 2. Eneo la kijiografia ambapo ipo. 3. Imani ya kufa kwa kile inachopigania.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo