Jeshi la Somalia lazingatia Kismayo

Na Adnan Hussein, Mogadishu

Julai 23, 2012

  • 106 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Jeshi la Somalia, likiungwa mkono na vikosi vya Misheni ya Umoja wa Afrika Somali (AMISOM), vinajiweka sawa kuichukua miji na vijiji huko Juba ya Chini vikisonga mbele kuelekea mji wa kimkakati na ngome kuu ya al-Shabaab huko Kismayo.

  • Vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika vyaelekea mji wa bandari wa Kismayo unaodhibitiwa na al-Shabaab. [Na Stuart Price/AFP/AU-UN IST]

    Vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika vyaelekea mji wa bandari wa Kismayo unaodhibitiwa na al-Shabaab. [Na Stuart Price/AFP/AU-UN IST]

Meja Jenerali Abdikarim Yusuf Dhegobadan alisema anatarajia majeshi yake kuisafisha Kismayo, mji mkuu wa tatu kwa ukubwa wa Somalia ulioko kilomita 500 kusini ya Mogadishu, wa al-Shabaab ifikapo mwezi Agosti .

Dhegobadan aliiambia Sabahi kuwa magaidi wamekuwa wakikimbia kutoka mafichoni mwao huku majeshi ya Somalia yanasonga mbele.

Alitoa wito kwa wakazi kuhama maeneo yalipo chini ya udhibiti wa al-Shabaab na kuondoka kabisa kutoka maeneo yenye maficho ya silaha.

"Kismayo ni ishara kwa Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia (TFG), na ndio maana inajaribu kuuchukua mji huo," alisema.

Kwa mujibu wa mbunge Mohamed Omar Gedi, siasa kali za al-Shabaab na uhalifu dhidi ya binadamu, ambao ni pamoja na uuaji wa wanazuoni wa Kiislamu, wasomi na yeyote anayepingana nao, umepitiliza sana.

Gedi alisema jeshi la Somalia karibuni litawapondaponda magaidi na kwamba washirika wa al-Qaeda, al-Shabaab, wako katika saa ya kifo.

"Vikosi vyetu vimepiga hatua katika mapambano ya mwisho na viongozi wa wakuu na wanamgambo wao wamejawa na hofu," aliiambia Sabahi. "Tutachukua udhibiti wa Kismayo wakati mapigano mapya yatakapoanza na moto wa risasi kuwazunguka [maadui]. Tutashinda na amani itapatikana."

Maafisa wa kijeshi wa Somalia walisema operesheni za kijeshi zinategemewa kuenea hadi Juba ya Chini baada ya TFG kuwa kuwaandaa wanajeshi wake kuelekea Marka, mji mkuu wa Shabelle ya Chini na Jowhar, mji mkuu wa Shabelle ya Kati .

Naibu Waziri wa Usafiri wa Anga, Bahari, Ardhini na Bandari Abdirahman Kulmiye Hirsi alisema kuwa kukamatwa kwa Kismayo, ngome kuu ya al-Shabaab iliyobakia, kutakuwa pigo la mwisho kwa kikundi.

"Vikosi vyetu vitazidisha kampeni za usalama na mashambulizi kuyalenga makambi ya vikundi hivi katika maeneo kadhaa kwenye mikoa ya Gedo, Shabelle ya Chini, Shabelle ya Kati na Juba ya Chini ili kulinda bandari, viwanja vya ndege na barabara na kuruhusu upokeaji wa misaada na usaidizi wa afya kwa watu walioathirika kwa matumbo ya kuharisha na kipindupindu , ambayo hivi karibuni yamekuwa maradhi," aliiambia Sabahi.

Msemaji wa zamani wa AMISOM Meja Paddy Akunda alielezea mpango kabambe wa kuitekea Kismayo ili misaada iweze kusambazwa na wakazi kuweza kuendelea na maisha ya kawaida.

Akunda aliwaambia waandishi wa habari mjini Mogadishu kuwa watu karibuni watapokea habari njema kuhusu Kismayo.

Al-Shabaab wanawasumbua wakazi wa Kismayo

Wakazi wa Kismayo wanasema wanasumbuliwa na matatizo ya kifedha, uhaba wa maji, kukatikwa kwa umeme, upungufu wa chakula na madawa kutokana na al-Shabaab kuukamata mji huo, na huishi kwa uoga kwamba kikundi kitafanya mashambulizi ya kulipiza kisasi wakati majeshi ya Somalia na AMISOM yatakapokaribia.

Anab Mohamed Musa, mwenye umri wa miaka 36, alisema alikimbia Kismayo miaka mitano iliyopita baada ya al-Shabaab kumzuia kuuza miraa, ambayo ni halali nchini Somalia, ili kuwalea watoto wake watatu.

"Madaktari, wafanyakazi wa misaada, waandishi wa habari na hata wanafunzi wengi waliosoma Kiiingereza mjini walishutumiwa kuwa wanafanya upelelezi kwa mashirika ya kiintelijensia ya Magharibi, hivyo iliwabidi kukimbia," aliiambia Sabahi. "Kikundi cha waasi kilisimamia simu za mikononi kupitia makampuni ya mawasiliano ya wenyeji ili waweze kusikiliza mazungumzo na kuendesha mauaji na kuzuia mipango dhidi ya kikundi."

Mkazi wa Kismayo Abbas Mohamed aliiambia Sabahi kuwa wapiganaji wa al-Shabaab waliwazuia idadi ya wananchi wazee wasisafiri kuelekea Mogadishu kupata matibabu muhimu kama sehemu ya juhudi za kikundi kuzuia wakazi wasikimbilie maeneo ychini ya udhibiti wa TFG.

Alisema pia al-Shabaab wanawasumbua wanawake, wakilazimisha kanuni kali za mavazi na kuwazuia wasifanye kazi.

Mohamed alisema al-Shabaab wanawalazimisha karibu wanaume wote wa Kismayo kubeba silaha na kuwapa mafunzo ya vita vya msituni, kulazimisha mtindo wao wa mavazi ili kusiwe na tofauti yoyote baina ya wananchi na wanamgambo.

Al-Shabaab pia wamewafunza wanawake na wasichana kufanya mashambulizi, alisema, na kwa muda wa miaka mitatu iliyopita, wamekuwa wakitoa zawadi za bunduki aina ya Kalashnikov na mabomu ya kurusha kwa mkono kwa wanafunzi wanaohifadhi Koran.

Mohamed alisema watu wamekuwa wakichukia tabia za al-Shabaab na uchokozi wao.

"Wanamgambo wa kikundi chenye mafungamano na al-Qaeda kilipanga na kutekeleza matendo ya kutisha ambayo yanauaibisha ubinadamu, kama vile kumpiga kwa mawe msichana hadi kufa kwa uzinifu, ambapo hajabaleghe bado," akisema. "Hili lilifanyika bila ya hata kuendesha uchunguzi wa kina wa makosa [dhidi yake] na bila kufanyiwa vipimo vya kiafya ili kuthibitisha uzima wa akili na mwili wake."

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 197)

Dislike_icon(29)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • said ibrahim
    August 31, 2012 @ 04:57:31AM

    Ni wazi sasa kuwa al-Shabaab imeshindwa na hii imekuwa ni kutokana na juhudi ya watu wa Somalia pamoja na vikosi. Kwa kuwa baada ya kushindwa maisha yanarejea taratibu katika hali ya kawaida na watu wanashughulikia kuijenga upya nchi yao- Serikali pia inaimairisha usalama.

  • muhammad Attaya
    August 31, 2012 @ 03:29:02AM

    Al-Shabaab inajukikana duniani kote kama kikundi katili kabisa ndani ya Afrika ya Mashariki na Afrika kwa jumla. Kikundi hiki cha kigaidi kimesababisha matendo yasiyosemeka ya kikatili na uvunjaji wa haki zabiandamu. Wale waliokuwa hawakubaliani nao waliadhibiwa vikali ama kwa kifo au kukatwakatwa sehemu za miili yao. Kikundi hiki cha ugaidi kimechukuwa dhamana wa upigaji mabomu na mauaji ya kujitoa muhanga nchini Somalia na nchi jirani. Watoto wadogo walitekwa, kuteswa na kugeuza kuwa askari bila aina yoyote ya mafunzo; hii ilipelekea wengi wao kuuwawa vitani na vikosi vya serikali. Al-Shabaab pia wamekuwa dhamana wa ugaidi katika bahari kuu na kuathiri biashara ya kimataifa pamoja na utalii wa Afrika ya Mashariki. Watu wengi wa Somalia wameteseka sana na wamekuwa hawajajua amani kwa muda mrefu; wamegeuzwa kuwa wakimbizi wakilazimika kuvumilia njaa na magonjwa.

  • Faith mumo
    August 31, 2012 @ 02:55:40AM

    Mwenyezi Mungu awalindeni nyote wakati mnaendelea kufanikisha kazi hii ya heshima.

  • ESOLOM NGARI
    August 30, 2012 @ 11:41:20AM

    Tumeona mkono wa Mungu kwenu. Sasa shindeni na shindeni na shindeni. Tunawaungeni mkono KDF kwa sala zetu. Tunawatakieni mafanikio.

  • gegema
    August 30, 2012 @ 07:12:49AM

    Tunaomba kwa KDF na TFG na yeyote mwanye dhamira njema kwa Wasomali, kushinda vita hivi ili kuleta amani nchini na duniani kwa jumla.

  • john muturi
    August 30, 2012 @ 05:12:37AM

    Walinde amani kwa ajili ya kaka na dada zetu, wameteseka kwa miaka mingi.

  • margie
    August 30, 2012 @ 04:10:38AM

    Nzuri sana, ni furaha kwa Wakenya kuona majirani zetu wanaishi kwa amani.

  • joseph
    August 29, 2012 @ 05:37:29AM

    Kutekwa kwa Kismayu kumechelewa sana. Msimamo mkali lazima utokomezwe na daima usiruhusiwe kustawi popote ulimwenguni.

  • jeff m mbune
    August 28, 2012 @ 09:23:32AM

    Huu ni wakati wa kumaliza tishio la lililokithiri muda mrefu la al-Shabaab ambalo limefanya uhalifu dhidi ya binadamu kwa jina la Mwenyezi Mungu. TFG na KDF endeleeni kwa ujasiri na kumaliza misheni hii; watu wa Somalia wameshateseka vya kutosha.

  • NAADIYE
    August 28, 2012 @ 07:00:04AM

    Tatizo ni kuwa mkaidi. Mungu akusaidie kumaliza tatizo hili ambalo lilikuwa linawaathiri Wasomali kwa robo karne.

  • olgidsureman
    August 28, 2012 @ 05:47:36AM

    Ninapenda na kutarajia tu kuwa siku moja nchi jirani zetu zitakuwa katika amani kutokana na tishio hili la kila mara kutokana na ugaidi na kwa hivyo kuweza kufaidi matunda ya nchi zao ambazo wamezipigania sio tu tangu miaka mingi nyuma bali kutokana na mashambulizi haya ya kigaidi dhidi ya watu wasio na hatia. Amani ya Bwana wetu iwe pamoja nanyi.

  • don mcngonje odhiambo.
    August 27, 2012 @ 03:43:32AM

    Ninamuomba Mungu awasamehe kwa maovu wanayofanya na awabariki KDF kwa kazi yao ya kuuteka upya Kismayu. Asante.

  • ngeno
    August 26, 2012 @ 04:19:26PM

    Si hiari ya watu wa Somalia kuwa wateseke lakini walijikutia katika mapigano, lakini ni kwa sababu watu wachache wasioridhika wanaojiita al-Shabaab ambao hawana hatima kwa nchi yao achia mbali wao wenyewe. Wanapaswa kufahamu kuwa kadiri watakavyoacha mapema kupigana ndivyo itakuwa bora sio kwa wao tu bali kwa watoto wajukuu na vizazi vijavyo.

  • gogie
    August 25, 2012 @ 07:52:40AM

    LAKINI WATU WANGU, WAKATI UTASEMA AMBAPO MTASIKIA KUWA WENGI WA ASKARI WETU WA KDF WAMESHINDWA KUTOKA NJE YA SOMALIA. NAAMINI BAADA YA MUDA BAADHI YA KDF WETU WATACHINJWA. TUSUBIRI.

  • John Kituu
    August 25, 2012 @ 04:54:37AM

    Wasiwasi wangu mkubwa ni kwa vijana hawa juu ya imani yao ya Kiislamu dhidi ya kuua raia wasio na hatia.

  • flipo
    August 24, 2012 @ 06:11:38AM

    Umeweka majenereta? Mimi niko huko kama fundi mitambo. Lol.

  • Timothy M. Kimaru
    August 24, 2012 @ 04:44:31AM

    Tuko pamoja katika maombi. Mungu awajaalie ushindi na kuiteka Kismayu, mko huko ili kuwakomboa watu wake. Kumbukeni kuwa nyinyi ndio Musa wa leo. Natamani ningejiunga na kufanyakazi ya kutumia nguvu iliyoko mbele yenu lakini ninawaombea nyinyi na familia zenu.... malizeni misheni na mrejee nyumbani .... Hongera....

  • Warugongo
    August 24, 2012 @ 02:15:12AM

    Msisahau kuwaambia juu ya Mungu na mtoto Wake, Yesu. Enezeni Neno la Mungu bila ya woga. Komboeni nafsi zenu pia, na hiyo ni misheni yenu vile vile.

  • mwangangi kyalo
    August 23, 2012 @ 10:39:43AM

    Ewe Mungu! Wasaidie viumbe vyako vipendwa!

  • V. ANDANDE
    August 23, 2012 @ 07:49:32AM

    Mungu atawafanyieni njia KDF. ENDELEENI BILA KUCHOKA HAKUNA KURUDI NYUMA.

  • FESTUS MURIIKI
    August 23, 2012 @ 03:49:27AM

    Endeleeni na moyo huo huo KDF na AMISOM kwa ajili ya misheni ya kuokoa maisha.

  • Wllie Mwangi
    August 23, 2012 @ 01:53:58AM

    Matakwa yangu, Matumaini, Imani na Dua ni kuwa Mungu atawapeni hisani ya kuwateka na kuwasafisha al-Shabaab/al-Qaida kutoka eneo lote la Somalia mara moja na kwa matokeo mazuri, na Afrika itakuwa na ladha ya amani. Tuunganishe juhudi zetu na kuanza kusherehekea kwa vile naelewa Mungu ni mwaminifu, anachotaka pekee ni kwa sote kumuamini yeye. Amin. Amin.

  • paul kariuki
    August 21, 2012 @ 09:25:33PM

    Bwana wetu mwema awasaidieni nyinyi majamaa kushinda vita hii. Sio rahisi lakini Mungu akiwa pamoja nanyi mtashinda.

  • mkenya asili
    August 21, 2012 @ 07:48:13AM

    HONGERA KWA KDF, NENDENI, NENDENI MKAUTEKE MJI

  • DOMINIC M. KAINDI
    August 21, 2012 @ 05:55:23AM

    MUNGU aonekane katika misheni hii ya kuwakomboa watu wa Somalia kutoka ukandamizaji.

  • Njagi Berns
    August 20, 2012 @ 02:12:54PM

    Kazi nzuri imefanywa, lakini (AMISOM) usimamizi wa wakati wenu unasubiriwa Kismayu na wakaazi wa eneo lote kwa ajili ya uhuru.

  • Dan Omondi
    August 20, 2012 @ 11:06:19AM

    Ikiwa shinikizo endelevu litawekwa kwa makabwela hawa, kikundi cha wanamgambo wa kupiga na kukimbia, bila ya shaka ushindi utapatikana kwa KDF na washirika wake na matokeo yake ni ukombozi kamili wa Somalia. Binadamu wa Somalia wanastahiki haki ya kuwa huru kama watu wengine popote pale duniani. Kitu muhimu kwa KDF na wengineo lazima wakumbuke kuwapa motisha wa kuwakomboa wale wanaokandamizwa. Zaidi ya hayo, tunawatakia askari wetu kila la heri.

  • Nixon
    August 20, 2012 @ 08:32:40AM

    Hatimaye tunapumua kwa sababu mashambulizi ya al-Shabaab yatakuwa historia.

  • PASTOR ISAIAH WELLINGTON
    August 20, 2012 @ 05:59:06AM

    Kumbukeni kuwa sio al-Shabaab wote, al-Qaida, KDF,UDF, TFG na kile mlichonacho, HAPANA bali ni mamlaka ya taifa la Somalia. Ndani ya Afrika yote, kwa nini nchi huangukia katika mtego wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ni utawala mbaya, uchoyo na mtikisiko wa wakuu wa makabila ambao baadaye hugeuka Mabwana wa vita kwa jina la 'watu wangu', kwa hivyo, ili kujaribu kutatua matatizo ya majirani zetu lazima kwanza tuweke utaratibu katika nyumba zetu. ASKARI WA KENYA MKO KATIKA MIKONO YA MUNGU AMBAYE ATAWAZAWADIA KWA KUJITOLEA KWENU NA WAJIBU WENU KWA TAIFA LENU NA RAIS WA KENYA.

  • EMMANUEL LOSURU
    August 20, 2012 @ 04:21:21AM

    NDANI YA SIKU SABA, MJI WA JERICHO ULIHARIBIWA NA NDANI YA SIKU SABA MJI WA KISMAYU UTATEKWA NA TFG NA KDF, HONGERA! UHURU UPO KARIBU KWA WAKAAZI WA KISMAYU.

  • ELIJA
    August 20, 2012 @ 03:47:57AM

    Ninahuzunishwa sana na watu wa Somalia ambao wamefanywa mateka na al-Shabaab na kulazimishwa kufanya yasiyofikirika!, lakini itafika siku ambapo Somalia itakombolewa. ENDELEENI AMISOM, NENDENI KISMAYU!

  • mawe
    August 19, 2012 @ 04:52:57PM

    Katika maisha hakuna kitu muhimu sana kama unapoelewa kuwa ni wewe tu unayepaswa kumuauni binadamu wenzako wanaokandamizwa. Kwa hivyo HONGERA KDF HINGERA AMISOM, msiangalie nyuma mpaka mfike huko, nakusudia KismayO. Mungu ayasikie maombi yetu na kuwaokoeni na kila aina ya moto huko, Amin!

  • Paul.
    August 19, 2012 @ 07:21:22AM

    Sawa sawa. Amani inakuja nchini Somalia, Mungu akipenda.

  • jacob
    August 19, 2012 @ 05:37:54AM

    Heko vikosi vya pamoja, tusafishe uuaji ndani ya Somalia, MUNGU yuko pamoja nanyi.

  • GEOFREY OGORA
    August 19, 2012 @ 03:34:23AM

    TUWAOMBEA NYINYI WATU, MNAFANYA KAZI NZURI

  • Beany George
    August 17, 2012 @ 09:09:45PM

    Wapanguzeni wote wenye akili za kishetani ili kusafishia njia mfumo mzuri wa maisha kwa jamii ya Somalia isiyo na hatia. Ni Mungu tu atakayelidhibti taifa zuri kama hili.

  • Nixon kibet
    August 17, 2012 @ 07:13:59AM

    Hongera vikosi vya washirika.

  • نزار عبد الله
    August 17, 2012 @ 07:05:33AM

    Tunapaswa kueneza mwako wa fikra sahihi na mawazo ya dini kupitia elimu yenye ubora na vyombo vya habari vyenye uelewa, na kwa kutokomeza umasikini, ambao ndio sababu kubwa inayowapelekea watu kufuata itikadi kali. Watu hawa masikini wanajihisi kukandamizwa na kuchanganyakiwa. Lazima tutatue tatizo la ukosefu wa ajira, ambalo huwapelekea vijana kujisikia watupu, jambo linalosaidia kuleta mazingira yanayowafanya vijana washawishike na mawazo ya wanamgambo. Hili pia ni pahali jukumu la asasi za kidini linapoingia. Wanasaidia kueneza mfumo wa kuwaza kwa wastani, wanawaelimisha vijana kuhusu hatari ya kujishughulisha na fikra za siasa kali; wanasambaza utamaduni wa utofauti na ubadilishanaji mawazo kwa uhuru wa kusema na kupata uhuru wa umma na wanaanzisha mfumo wa maisha ya kidemokrasia katika jamii, kunakoruhusu uhuru zaidi unaoeneza mawazo ya kuvumiliana zaidi na kuwasaidia watu wawe wazi zaidi kwa wengine.

  • anonuye
    August 16, 2012 @ 10:03:36AM

    KDF wako wapi? kwa nini TFG wanataka kuiteka Kismayu sasa? Tusubiri tena mwaka mmoja au mlifanya hivyo? Nadhani mngewaachia KDF wapigane na muje baadaye kujiunga. Niko sahihi?

  • edward kirimi
    August 15, 2012 @ 09:50:26AM

    Wasafisheni wanamgambo hao na safisheni njia kwa utawala bora nchini Somalia...tufanye biashara pamoja (Kenya na Somalia).

  • felix memba
    August 14, 2012 @ 10:20:56AM

    Al-Shabaab wako njiani kutoweka. Watasahauliwa kabisa kama walivyosahauliwa Sadam Hussein, Osama bin Laden, Muammar Gadaffi na Hosni Mubarak.

  • JARED
    August 14, 2012 @ 07:32:11AM

    Ijulikane kwamba JEHOVAH, YEYE NDIYE MUNGU. Shalom.

  • beast de fist
    August 14, 2012 @ 05:27:19AM

    Bwana Jah, tafadhali irejeshe Somalia kama tulivyofanya Wakenya. Asante.

  • MOSES
    August 14, 2012 @ 03:04:44AM

    Ronald, wewe ni nani, Mkenya au al-Shabaab unayejificha?

  • gichana.o
    August 13, 2012 @ 03:23:43PM

    Endeleeni kuwasha moto,... hongera KDF, kusiwe na huruma linapokuja suala la kupambana na maadui wa amani. MUNGU atawasaidieni kuwaokoa wananchi wasio na hatia wa ardhi ya Somalia.

  • daniel musyoki
    August 13, 2012 @ 07:54:55AM

    Nadhani hawa al-Shabaab wamekuwa maumivu ya kichwa kwa KDF. LAKINI NILIDHANI kuwa hawa al-Shabaab huko Kismayu walikamatwa mwezi uliopita.

  • Ronald
    August 10, 2012 @ 06:32:12AM

    Nilidhani KDF ilitarajiwa kuiteka Kismayu mwaka jana, kilitokea nini? Sasa makala hii inatuaambia kuwa ni TFG itakayoiteka Kismayo. KDF kuweni wabunifu, tafadhalini.

  • steve
    August 10, 2012 @ 12:47:51AM

    Kwa kweli inauma sana kuona kikundi cha watu kuwaweka watu wengine kizuizini kwa sababu za uchoyo ambazo hazina maana kwa jina la Mwenyezi Mungu. Mungu mwenyewe ni upendo. Wamekuwa wakiwakandamiza watu wa Somalia kwa miongo mingi. “Ujinga umwatawala hawajui kuwa huu ni uovu,” sasa kwa vile wale waliokuwa wakikandamizwa wanapata nafuu wao wanafikiria kuwa hilo ni baya na wanataka waendelee kua watu wasio hatia. Tuwaombee wakombozi na tuwaombee watu wa Somalia. Amani itawale Afrika na Mungu ibariki Afrika.

  • WAMBULWA .B. WAMBULWA
    August 9, 2012 @ 06:23:29AM

    Ni vizuri mumeondolewa nyinyi magaidi. MJAALIWE MUSAGWE KWA NGUVU NA VIKOSI VYA SERIKALI, ILI KUWEPO NA SHERIA NA KANUNI NCHINI SOMALIA.

  • lopusile
    August 7, 2012 @ 04:46:10PM

    Vizuri! Hadithi ya al-Shaabab itakuwa hadithi ya kuwasimulia kizazi kijacho na ni kweli kwamba jamii inakuwa kubwa pale wazee wanapopanda miti ambayo kivuli chake wanajua wazi hawatakikalia chini yake. Hongera KDF, UPDF na jeshi la Ethiopia ambao kwa moyo safi wanapanda miti ambayo pengine hawateza kupumzika kivulini pake lakini ni kwa faida za siku za mbele za wavulana na wasichana wa Somalia yenye amani tunayoitaka.

  • benard
    August 7, 2012 @ 10:09:34AM

    Ninawatakia kila la heri kwa vile wanadhamiria kuisafisha al-Shabaab. Tunatumai wanafanya vizuri sana.

  • SILVANOS MADILANE
    August 6, 2012 @ 09:23:37PM

    Bila shaka wakenya tuko nyuma ya KDF.Kazeni kamba vivyo hivyo.

  • William Bett
    August 6, 2012 @ 10:59:24AM

    Hongera KDF; Bwana yuko pamoja nanyi. Mtashinda kwa niaba ya wananchi wanaoteseka wa Somalia. Wenye hekima wote wa dini ikiwa ni pamoja na Yesu Kristo (mwokozi wetu), Mitume wote ikiwa ni pamoja na Muhammad (Amani Iwe Juu yake) wangefurahia kazi yenu leo. Mnawakomboa watu wanaoteseka kutokana na watu wanaotumia dini ili kuwakandamiza. Tutawaombeeni mpaka mtakapoikomboa Kismayu na Somalia yote.

  • wilson methuselah
    August 5, 2012 @ 09:27:59PM

    Bwana awe pamoja na timu ya AMISOM, na una moyo kwamba karibuni watahukumiwa.

  • GEORGE
    August 3, 2012 @ 11:01:29AM

    NGUVU ZA MOTO WA KDF UENDELEZWE. ENDELEENI KDF, TUNAJUA KAZI HII SIO RAHISI LAKINI TUNAJUA PIA KUWA NYINYI MMEUMBWA KWA KWA AJILI YA KAZI HII KWA HIVYO HAKUNA KUANGALIA NYUMA. MUNGU AWE PAMOJA NANYI.

  • koech simion
    August 3, 2012 @ 08:00:06AM

    Kazi nzuri vijana, Mungu awabariki.

  • kawira
    August 2, 2012 @ 09:32:32AM

    Kwa kweli ninaishukuru KDF na MUNGU awape NGUVU na UJASIRI, tuko pamoja katika maombi.

  • peter wahome
    August 2, 2012 @ 09:32:28AM

    Bunduki za Kalashnikov haziwezi kuzuia mashambulizi ya anga na gari za KDF ambazo zinaweza kuhimili milipuko ya al-Shabaab. Isipokuwa ukosefu wa busara unapompata yeyote, kwa kweli sioni kwa nini kukiunga mkono kikundi hiki cha wanamgambo wapuuzi.

  • Tariq ally
    August 2, 2012 @ 02:15:24AM

    Tuna waomba muongeze kasi ya kuwadhibiti waasi hao.

  • Obado
    August 2, 2012 @ 12:57:51AM

    Nadhani wakati KDF ilipoingia katika kuwasaka al-Shabaab ilionekana kama ndoto isiyowezekana, lakini kutokana na mtandao mzuri wa upelelezi na msaada kutoka kwa TFG na AMISOM, adui sasa anakimbia na muda mfupi itakuwa furaha huko Kismayu kwa vile mji huu utakuwa huru kutokana na tishio la al-Shabaab, ambao walikuwa wameuteka nyara kwa muda mrefu. Zaidi ya hayo, ninawatakia kila la heri na Mungu awalinde.

  • A. Sande
    July 31, 2012 @ 09:48:10AM

    Mungu alipe jeshi letu lote nguvu za kumuaibisha shetani kwa kushinda vita.

  • philip
    July 31, 2012 @ 09:34:37AM

    Hongera kwa KDF na AMISOM yetu. Tuko nyuma yenu. Endeleeni na kuwatokomeza wakatili hao.

  • Nyamogi
    July 31, 2012 @ 08:42:47AM

    Dada na kaka zetu wapondeni maadui hawa hadi roho ya mwisho. Ninawaungeni mkono sana. Hongera.

  • Mtumwema
    July 31, 2012 @ 07:29:36AM

    Wasomali msifanye tena makosa baada ya kukomboa nchi yenu kutokana na propaganda za magaidi chini ya kivuli cha dini. Kumbukeni sio mara ya kwanza nchi yenu kukombolewa toka mkononi mwa magaidi halafu wenyewe kuikabidhi tena kwa hao hao magaidi. Waethiopia waliwasaidia kuwaondoa magaidi halafu mkaambiwa hao ni makafir hawana sifa ya kuwasaidieni kuleta utulivu kwenye nchi yenu mkafanya 'jihad' mkairejesha nchi mikononi mwa magaidi kwa mara nyingine. Kumbukeni dini inamfaa mtu kwa binafsi yake kwenda mbinguni na kamwe haipaswi kuchanganywa na siasa. Hapa Ulimwenguni kinachohitajika ni 'reason and logic' Mkizingatia hilo hakika Somalia iliyokua na heshima tele itarejea.

  • hesbon
    July 31, 2012 @ 06:40:42AM

    Kazi nzuri, Mungu awabariki KDF, AMISOM na TFG. Tunaomba Mungu mrejee nyumbani nyote baada ya kumaliza kazi.

  • daudi
    July 31, 2012 @ 06:30:50AM

    Kuweni wenyewe kwa vile mnaenda kuwatokomeza al-Shabaab watoke Kismayu na tunawafuateni kwa dua zetu.

  • stephen Barasa
    July 31, 2012 @ 06:12:33AM

    Nyinyi ni wajumbe wa amani katika Afrika ya Mashariki. Sote tunawaombea. Nyinyi ndio washindi. Endeleeni.

  • francis
    July 31, 2012 @ 04:58:21AM

    Mungu awabariki askari wetu wa Kenya na askari wenzao kwa vile wanapigania amani ya Afrika. Mungu awabariki nyote kwa kwenda na kurejea kwenu. Amani, amani, amani, Amin...

  • mdudu kadumas
    July 31, 2012 @ 04:56:40AM

    JAMANI WATANZANIA ULAFI NA UBINAFSI WA VIONGOZI WA KADA ZOTE ZA UMMA NA SEREKALI KUU ZINATOKANA NA MTU MWENYEWE NA SI CHAMA .CHAMA KINACHOANGALIA UKABILA, UDINI HIVI HAVITUFAI KABISI NI KHERI TUKABAKIA HIVYO HIVYO KAMA TULIVYO ACHWA NA MWALIMU NYERERE KULIKO KUKIPA CHAMA KINACHAO ANGALIA UKABILA NA UDINI KUSHIKA HATAMU.INCHI YETU UKIANGALIA SYSTEM ILIYOACHWA NA MWALIMU ,VIUONGOZI WA NGAZI ZA JUU WANATOKA KATIKA JAMII YA KWAWAIDA SANA KULIKO HAYA YANAYOTOKEA KWA CHAMA HIKI KINACHOKUJA KWA KASI YAANI CHADEMA .HIKI CHAMA KIINA UKABILA NA UDINI NA UKIANGALIA SOURSE YA CHAMA HIKI KIMETOKE KWENYE UZAO WA KINA MANGI SINA.nI VIZURI VIONGOZI WACHACHE WENYE KUJILIMBIKIZIA MALI WAKACHUKULIA HATUA KULIKO KUNGOA MTI ULIOTA KWENYE JANGWA WAKATI MATUZO YAKE TULIYAKUZA KWA SHIDA SINA CHAMA ILA NI MWONO WANGU. wATANZANIA TUWE MAKINI .........

  • Bosire Rogers Nyakundi
    July 31, 2012 @ 02:38:57AM

    Bwana Mungu wetu awe pamoja nanyi ili kuwasafisha al-Shabaab moja kwa moja. Sote tumo kwa maombi.

  • JOSEPH SHIKUKU MUNG'ALA
    July 31, 2012 @ 12:20:01AM

    KAZI NZURI KDF, AMISOM. ENDELEENI NA MOYO WA KUPAMBANA ILI KUWEPO NA AMANI NCHINI KWETU NA JIRANI YETU SOMALIA. WAKENYA TUOMBE KWA WATOTO HAWA WANAOPIGANA NA MAGAIDI HAWA. JOSEPH SHIKUKU MUNG'ALA-ELDORET

  • suzan john
    July 30, 2012 @ 11:20:55AM

    Eee Mungu kumbuka familia, wanawake na watoto waepushe na vifo.Yeyote anayetaka kuona kile kinachoendelea au kile mnachofanya, watakeni wawe wavumilivu. Kwa hali yoyote ile, walikuweko wapi wakati al-Shabaab ilikuwa ikiwachinja watu. Mashirika ya kiraia hawafai kutoa maoni Tuwasaidie pale inapowezekana lakini tusilaani kazi nzuri ya AMISOM na KDF asanteni kwa kazi yenu. Endeleeni . Mwenyezi Mungu awe pamoja nanyi katika hali zote.

  • imwene noah
    July 30, 2012 @ 11:01:40AM

    Mungu awe pamoja nanyi vijana (KDF) waukamate mji huo na warejee nyumbani!!! Hongera!!

  • tracy sialo
    July 30, 2012 @ 08:52:47AM

    Wapendwa askari wetu kuweni na ujasiri wa kuwashinda hao al-Shabaab. Na mimi hapa ninaomba kwa Mungu awalinde na afanye ngao kupitia damu yake na mtaibuka washindi . Hongera.

  • Kasuku
    July 30, 2012 @ 06:37:20AM

    Itakuwa habari nzuri ikiwa Kismayo itaanguka kwa AMISOM.

  • wambulwa wafula wambulwa
    July 30, 2012 @ 04:55:47AM

    Al-Shabaab wanaoishi kwa upanga waachwe wafe kwa upanga, mafundisho ya Biblia yanaonesha hivyo.

  • Ben
    July 30, 2012 @ 03:27:07AM

    Mungu wabariki wanawake na wanaume wa KDF kwa vile wanapambana kufanikisha kazi hii ya heshima.

  • MOHAMED ABDI
    July 30, 2012 @ 03:18:32AM

    Tuwaombeeni Luteni Shukri Mohamed Abdi na wenzake wa KDF na TFG: na wale wote wanaojali kuhusu Somalia. Mwenyezi Mungu awalinde vijana wetu wa ulinzi katika kuelekea kwao Kismayo na hata Mogadishu. Amin, amin, amin, Ewe mwenyezi Mungu.

  • nakusi
    July 29, 2012 @ 11:38:55AM

    Tabaka la watu wa juu kutoka Somalia wanaoishi Kenya lazima wachangie katika mchakato wa amani kwa kuisaidia Kenya kuwatambua wahalifu wanaowalenga watu wetu katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab na sehemu nyengine za nchi.

  • Daud
    July 29, 2012 @ 08:46:21AM

    ni makala nzuri

  • Nandwa Peter
    July 29, 2012 @ 07:29:28AM

    Endeleeni AMISOM, iliyo kuu na imara, ninawaombeeni dua kutoka alfajiri hadi jua kutua.

  • J.kipaipai
    July 29, 2012 @ 01:00:56AM

    Kazi nzuri, Mungu akusaidieni.

  • GEOFFREY KUBAI MUTIGAH
    July 28, 2012 @ 05:34:14PM

    Vidole vya gumba juu kwa KDF na AMISOM. Ni wakati kwa nguvu za giza nchini Somalia kusagwa mpaka kusalimu amri. Mungu Ibariki Kenya, Mungu Ibariki Somalia, Mungu Ibariki Afrika. Al-Shabaab ipotelee mbali. KDF na AMISOM tumesimama pamoja na nyniyi na Mungu awape ushindi.

  • martin
    July 28, 2012 @ 08:06:01AM

    KDF tuko nyuma yenu, endeleeni.

  • Machogu
    July 27, 2012 @ 10:52:17AM

    Kwa kuwa kazi nzuri inatendeka katika operesheni hii, tuwashukuru na kuwapa moyo na ari KDF wetu pamoja na askari wa AMISOM ambao wamejitolea kuilinda nchi yetu (Kenya). Hata hivyo, ninasumbuliwa na kituo cha habari kinachoendelea kutangaza, mipango ya AMISOM na KDF pamoja na maendeleo yaliyofikiwa. Ndio! Wanatujuza habari moto moto, lakini wawe na tahadhari habari hizi zisitumiwe na al-Shabaab kujipangia mikakati au kuifanya mipango hii kuwa migumu. Tafadhali, tafadhali, tafadhali” Bwana (majina yako yote yanazingatiwa) msemaji, simamia habari inayotumwa kwa watu wa habari, wawe wa kitaifa, kikanda au wa kimataifa. Ikiwa inawezekana, toeni habari baada ya mashambulizi kwishafanyika. Yeyote anayetaka kuona kile kinachoendelea au kile mnachofanya, watakeni wawe wavumilivu. Kwa hali yoyote ile, walikuweko wapi wakati al-Shabaab ilikuwa ikiwachinja watu. Mashirika ya kiraia hawafai kutoa maoni zao za kipuuzi. Tuwasaidie pale inapowezekana lakini tusilaani kazi nzuri ya AMISOM na KDF. Vyenginevyo, KDF na AMISOM, asanteni kwa kazi yenu. Endeleeni vijana, wanawake na wanaume. Mwenyezi Mungu awe pamoja nanyi katika hali zote.

  • shus
    July 27, 2012 @ 10:27:02AM

    Aha! Acha nisubiri matokeo. Mnaunga mkono uvamizi shaghalabaghala na usiopangwa nchini Somalia ambapo wageni ni chakula moto. Kismayo si pahali maalumu kwa KDF, askari wa kukodiwa wa Museveni na Burundi ambao ni watafuta maisha. Baada ya Kismayo tuhesabu upotevu wa wachokozi hawa.

  • Momanyi
    July 27, 2012 @ 09:49:03AM

    Vikundi vya KDF na AMISOM, kazi nzuri! Ukombozi kamili unakuja kwa Somalia na nchi Jirani. Mko mioyoni mwetu na tunawaombea. Hatimaye mtashinda vita hivi. Mungu yuko nyuma ya juhudi zenu kwa vile mnapigania amani. Awajaalieni Ushindi wote. Momanyi.

  • Devis Op
    July 27, 2012 @ 08:27:02AM

    Hawa al-Shabaab ni mbwa wa ngono. Ni lazima waishi kwa kulamba vidonda vya waliokufa. Hakuna kurudi nyuma kwa TFG na AMISOM. Watawakomboa Wasomali ambao ni watu wema ili wafaidi matunda ya nchi yao. Operesheni Linda Nchi inaendelea. Wapigeni maadui wa watu wa Somalia. Wasafisheni katika choo.

  • moses ole keshe
    July 27, 2012 @ 07:44:30AM

    Kwa nafsi yangu, nimefurahia sana na mwendeleo ambao AMISOM imefika mpaka leo. Mungu aliye na nguvu awe na jeshi letu katika wakati huu mgumu.

  • Kiboi
    July 27, 2012 @ 07:07:35AM

    Vikosi vya KDF, TFG na AMISOM mpo katika nafasi nzuri ya kuiteka Kismayo kwa usiku mmoja na nadhani mmeshapitiliza muda zamani. Ikiwa naweza kuuliza, kwa nini mnawaacha viongozi wa al-Shabaab kukimbia kutoka Kismayo? Pili, bado mnashawishika kuwa viongozi wa kikundi hiki hawaishi Kenya na kufanya shughuli zao pamoja na viongozi wetu? Kwa nini sisi (wananchi wa kawaida) tuendelee kuteseka mikononi mwa al-Shabaab wakati “viongozi wetu" wanafaidi pesa za uharamia. Ili kuwapa al-Shabaab pigo la mwisho, vita vingeanzia na Eastleigh – Nairobi kabla ya kupelekwa Somalia.

  • obur eva
    July 27, 2012 @ 04:57:30AM

    Kurejeshwa kwa uhuru wa fikira kupo karibu. Shikilieni hapo hapo.

  • Benjamin
    July 27, 2012 @ 04:52:50AM

    Kazi nzuri jeshi letu. Endeleeni.

  • joseph
    July 27, 2012 @ 03:42:59AM

    Al-Shabaab inaishi zama za kale na wanahitaji kusasisha itikadi yao

  • abel ojwang'
    July 27, 2012 @ 02:34:39AM

    Ninaunga mkono operesheni hii kwa vile ni vyema kuwa na serikali kwa ajili ya watu wa Somalia. Hili litawasaidia kuiendeleza nchi yao na kuwa na uhuru wa kuishi kwa mtindo wa maisha yao wenyewe.

  • wekesa
    July 27, 2012 @ 01:25:55AM

    Endeleeni na kazi nzuri, waacheni watu wa Somalia wafurahie uhuru, daima tunamuomba Mungu awape watu wa Somalia amani na waweze kuendeleza nchi yao.

  • david anyanzwa
    July 26, 2012 @ 08:59:46AM

    Nimefurahi kwa venye KDF ilichukua muda kuwashambulia al-Shabaab huko Kismayo, kwa sababu wanamgambo wamewashikilia raia kwa usalama wao wenyewe kama ngao yao. Walitaka kujificha wenyewe kwa haki za binadamu za UN, kwamba KDF imewaua raia, lakini sasa hawatawalaumu KDF, watawalaumu AMISOM na hawa wanalindwa na UN. Jeshi la Ulinzi la Kenya limepewa mafunzo mazuri na litawashughulikia al-Shabaab bila huruma. Watajuta kuishambulia Kenya. Upelelezi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya imekamilika, kwa sasa al-Shabaab wako kimya kwa vile hawaelewi mpango wa Kenya.

  • Benjamin
    July 26, 2012 @ 08:30:27AM

    Nadhani hili ni jaribio la kukusudia ili kudharau juhudi za KDF. Maoni yangu ni kuwa hii sio haki, AMISOM ni nini, walikuwa wapi wakati KDF walipoleta amani maeneo makubwa yaliyokuwa yanakaliwa na al-Shabaab? Kwa vyovyote vile, enyi mashujaa wa KDF, endeleeni na kazi nzuri. Hongera

  • vera
    July 26, 2012 @ 02:23:54AM

    Mubarikiwe kwa kazi ya mikono yenu na mpewe nguvu za kuwashinda watu hao mpaka mwisho.

  • abdulahi iiman
    July 25, 2012 @ 02:01:02PM

    Al-Shabaab imewaua watu wa Kisomali na yanayofanyika hayawezwi kufanywa na mtu Msomali, lakini ni matokeo ya itikadi ya unyama ambayo imejificha chini ya mambo ya dini. Watu wa Kisomali watakuwa imara na kupumzika siku moja bila ya kujali shida ambazo wanapitia kama mauaji, wizi na uporaji wa mali zao na vikundi hivi. Vikosi vya serikali isishambulie maeneo ambayo wengi wanoishi ni raia kwa sababu hii italeta vifo vya watu zaidi hii ikifanyika. Serikali lazima iwe na hadhari ya hali ya wananchi wake.

  • TOILI
    July 25, 2012 @ 11:00:06AM

    AMISOM wawe na tahadhari wasiwadhuru wananchi wasio na hatia. Ni hatua nzuri, endeleeni.

  • Dmanga
    July 25, 2012 @ 10:28:20AM

    Hiyo ni kweli meja...Bila ya KDF operesheni haitafanikiwa.

  • Noah Tanui
    July 25, 2012 @ 07:25:07AM

    Ninajivunia na kile kinachoendelea Somalia mpaka sasa. Kinachohitajika sasa ni mpango mzuri na taratibu za mkabala wa kimbinu. Ni suala la wakati tu, Kismayo itakuwa katika ukanda unaomilikiwa na jeshi. Ndio, kunaweza kutokea vifo huko. Kitu muhimu ni kuusafisha mji wote na wananchi wafurahie kuliko wakati waliokuwa wametekwa nyara na al-Shabaab. Chukueni wakati, lakini lazima mshinde vita hivi. Mbele daima, nyuma mwiko. HONGERA, sisi tunawaangalieni na tunawaoombeeni dua nyinyi na Somalia siku moja itafurahia AMANI - Mlinda Amani wa Zamani, Timor ya Mashariki Mstaafu C.I. Noah Tanui.

  • abdille
    July 25, 2012 @ 06:45:49AM

    Ni makala nzuri, sio sahihi kumuua kijana ambaye bado hajaoa hadi kufa hata kama amefanya tendo la zinaa, hii ni kwa mujibu wa Koran Tukufu

  • runsheeg
    July 24, 2012 @ 08:04:14AM

    Hii ni hadithi ya watu walio katika hali ya ulevi. Mtu huyu anayepigwa huko Qoqani na Kolbiyo na kudang'anya umma afanye anavyoweza...Kuiweka nchi chini ya utawala wa watu waliofunikwa ni bora kuliko kuiweka chini ya utawala wa kikoloni wa Afrika.

  • major(RTD) Sila Mutungi
    July 24, 2012 @ 04:29:22AM

    Ingawa nimefurahishwa na habari nzuri ya maendeleo ya mpango wa TFG kuikamata Kismayo, na kama kuna sababu nzuri ya kutotaja nani aneyehusika na maendeleo haya, nadhani ni makosa kutoitaja KDF ambayo imechukua uongozi wa kuikamata Kismayo kutokana na ukweli kwamba wana nguvu ya kuwatoa al-Shabaab Kismayo na kuwakomboa watu wa Somalia. Meja (Mstaafu) Sila Mutungi.

  • m.amiin
    July 24, 2012 @ 12:35:21AM

    Amani iwe juu yenu. Tunamuomba Mungu kuwafanya al-Shabaab wamezwe na ardhi.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo