Eastleighwood yatumia sanaa kupambana na kutiwa kasumba na mambo mabaya ya kuiga

Na Sargajan bin Kadii, Nairobi

Julai 20, 2012

  • 3 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Akivutiwa na hisia kali ya wasanii waigizaji vijana, Burhan Iman, mwenye umri wa miaka 23, aliuza biashara yake na kuwekeza katika dira yake ya kutoa burudani kwa jumuiya ya Wasomali wenye huduma duni nchini Kenya na kupambana na mambo ya kuiga hasi dhidi ya makabila ya Wasomali.

  • Mpigapicha Abuker Yusuf katika eneo wakati wa kuchukua picha na waigizaji wa Eastleighwood tarehe 7 Mei huko Nairobi. [Tony Karumba/AFP]

    Mpigapicha Abuker Yusuf katika eneo wakati wa kuchukua picha na waigizaji wa Eastleighwood tarehe 7 Mei huko Nairobi. [Tony Karumba/AFP]

  • Burhan Iman ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Eastleighwood, kikundi cha vijana waigizaji na waimbiaji Wasomali-Wakenya. [Sargajan bin Kadii/Sabahi]

    Burhan Iman ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Eastleighwood, kikundi cha vijana waigizaji na waimbiaji Wasomali-Wakenya. [Sargajan bin Kadii/Sabahi]

Hivyo, alianzisha Eastleighwood, kikundi cha waigizaji, washairi na waimbaji zaidi ya 200 wanaoishi Eastleigh, mtaa wa katikati ya Nairobi wenye msongamano wa watu na wengi wao ni Wasomali.

Sehemu kubwa ya mambo ya kikundi yanatangaza amani na kuwaelimisha vijana kuepuka kutekwa na kasumba za vikundi vya watu wenye siasa kali.

Eastleighwood inarekodi nyimbo na kutengeneza filamu, baadhi yake zinaweza kupatikana kwenye mtandao. Zaidi ya hayo, inaandaa michezo, matamasha ya vijana na shughuli nyingine za burudani jijini Nairobi.

Iman alizungumza na Sabahi kuhusu shughuli za Eastleighwood, changamoto na malengo ya baadaye.

Sabahi: Tueleze kuhusu wewe mwenyewe

Burhan Iman: Mimi ni mkurugenzi mtendaji na mwenyekiti wa Eastleighwood. Ingawa nilizaliwa Kenya, muda wangu mwingi nimekuwa katika nchi mbalimbali kama vile Falme za Kiarabu, Kuwaiti, Yemeni na Somalia. Ingawa kwa sasa ninaishi Nairobi, mara nyingi huwa nasafiri kwenda Mogadishu na sehemu nyingine duniani.

Sabahi: Kwa nini ulianzisha Eastleighwood?

Iman: Baada ya kuangalia vyombo vya habari vya Kenya kwa miaka mengi, niligundua kwamba hakuna mmoja wa vyombo hivi vilitoa habari yoyote kwa ajilia ya Wasomali-Wakenya, licha ya jambo la jamii hiyo inajumuisha idadi kubwa ya watu wa nchi.

Hili lilinichochea kujiuliza ni jinsi gani ninaweza kuendeleza maudhui ya burudani ya Somalia. Kwa kuwa muundo wa sanaa ya Somalia kimsingi umekuwa katika ufasaha wa kusema, niligundua kwamba majukwaa ya kusikia na kuona yangekuwa ndiyo sehemu ya kuanzia.

Nilithibitisha hili kwa utafiti niliyoufanya huko Eastleigh nilipowauliza wakazi wa kawaida kuhusu wanachokipendelea kati ya kusikia, kuona au kuandika [vyombo vya habari]. Hapo ndipo wazo la kuanzisha Eastleighwood lilipojitokeza.

Baada ya hapo, niliungana na kikundi cha marafiki na tuliandaa Utafutaji Vipaji Eastleighwood huko Eastleigh mwezi Julai 2011. Vijana walikuja kutoka maeneo ya jirani kuonyesha vipaji vyao vya kuigiza sanaa. Tulichagua wale tuliyohisi wanaweza kuendelea na mwaka mmoja baadaye, hawakutuangusha. Waliimarika kwa kiasi kikubwa mno.

Baadhi wamesharekodi nyimbo na kuigiza katika filamu zetu. Kwa kuvutiwa na shauku yao ya kufanikiwa, niliuza biashara yangu ili kuwekeza nguvu zangu zote na rasilimali katika ndoto ya Eastleighwood.

Sabahi: Tueleze kuhusu kundi na uigizaji wako.

Iman: Kwa sasa tuna waigizaji wa kike na wakiume, waimbaji, watayarishaji 200. Mpaka sasa, tunaandaa filamu mbili, "Mapenzi ni Upofu" na "Bahati", ambazo ziko katika hatua ya kutayarishwa.

Pia tumefanya michezo mingi jukwaani na uigizaji ambao umejikita katika mapenzi, amani, biashara haramu ya watu, ushirikiano na masuala mengine ya kijamii.

Sabahi: Unafikiri sanaa inaweza kutumiwa kuhubiri amani miongoni mwa vijana?

Iman: Bila shaka. Na hicho ndicho Eastleighwood inadhamiria kufanya tangu mwanzo. Kwa kweli nimefungua ofisi ya Eastleighwood katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Aden Adde huko Mogadishu jirani na Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, kwa madhumuni pekee ya kusambaza filamu na nyimbo zetu miongoni mwa vijana wa Mogadishu.

Wasomali wana bahati sana kwa sababu wanatumia lugha moja, utamaduni, mtindo wa maisha na wengi wetu ni waumini wa dini moja, ambako kunafanya iwe rahisi kutumia miundo ya sanaa katika mshikamano na kujenga amani miongoni mwetu wenyewe. Njia pekee ya kushinda vita dhidi ya kasumba ya vijana wetu inayoletwa na vikundi vya ugaidi ni kupitia utoaji taarifa, ambao unaweza kufanikiwa kupitia sanaa. Kwa hiyo, Kama Jeshi la Ulinzi la Kenya linavyoongoza mstari wa mbele jeshini, Eastleighwood inadhamiria kupeleka mbele ajenda kupitia sanaa.

Sabahi: Ni shughuli zipi za kijamii umekuwa ukizifanya ili kuhakikisha kwamba unafanikisha lengo la kutokomeza mambo ya kuiga dhidi ya Wasomali na kuhubiri ujumbe wa amani?

Iman: Licha ya majukwaa mengi ambayo Eastleighwood inatoa kwa vijana kutoka katika mazingira ya makabila mbalimbali kukutana pamoja na kuonesha vipaji vyao, pia tunapiga picha ya filamu za matukio halisi inayoitwa "Midnimo" (Umoja), ambayo itakuwa na matukio kutoka Eastleigh, Mandera, Garissa na Minnesota huku Marekani.

Filamu ya matukio halisi inapaswa kuonesha jitihada ambazo Wasomali wa kawaida wanafanya kushirikiana na watu wengine ili kujenga amani na umoja. Pia nilikuwa Mogadishu mwezi Aprili kufungua ofisi za Eastleighwood ambako nilitoa muhadhara kuhusu "Weka chini Silaha, Chukua Kalamu".

Pia tunapanga kuandaa usiku wa Somalia huko Nairobi ambapo watu wa nyanja zote watakuja na kufurahia chakula cha Somalia, muziki na utamaduni mwingine ambavyo tunaamini vitasaidia kupambana na mambo ya kuiga. Licha ya hayo, pia tuna filamu kadhaa na nyimbo zilizo mitamboni, vyote vinalenga kuleta mabadiliko mazuri ya kijamii.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 13)

Dislike_icon(1)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • ........gf.................................
    January 27, 2013 @ 01:03:00AM

    Wazo ni zuri la kupendeza, lakini jina sio zuri na wala haliko wazi, sio Somalia.

  • Dominic
    October 3, 2012 @ 09:11:10AM

    Kazi nzuri Walaal. Hizi ni akili tunazozihitaji kwa wakati huu ili kuwajenga watu wetu na kuimarisha kuishi pamoja kama jamii moja. Mafanikio.

  • freeman
    August 12, 2012 @ 10:59:39AM

    Makala hii hakuna maneno itakayoieleza. Unayo barua pepe yake au anuani ya jina analotumia FB kwa sababu nilijaribu kumtafuta FB lakini sikumpata. Kwa hivyo tafadhali fanya njia za kuwasiliana naye kwa vile mimi ni mtengeneza filamu pia wa Somalia na ninao uzoefu mkubwa.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo