Wakazi wa Mogadishu waikaribisha Ramadhani kwa utulivu mkubwa huku Mogadishu, lakini wasiwasi bado unaendelea

Na Adnan Hussein, Mogadishu

Julai 20, 2012

  • 4 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wakazi wa mjini Mogadishu wanaukaribisha mwezi wa Ramadhani katika mazingira ya utulivu mkubwa na hali ya usalama iliyoimarika, lakini wengi bado hawana njia za kujikimu wenyewe na famiia zao wakati wa mwezi huu mtukufu.

  • Wanunuzi wakijaza katika masoko ya Mogadishu kununua mahitaji ya Ramadhani. Juu, mteja ananunua tende kwenye Soko la Hamar Weyne. [Na Adnan Hussein/Sabahi]

    Wanunuzi wakijaza katika masoko ya Mogadishu kununua mahitaji ya Ramadhani. Juu, mteja ananunua tende kwenye Soko la Hamar Weyne. [Na Adnan Hussein/Sabahi]

  • Wakazi wa kambi ya Bosnia ya watu wa ndani waliokimbia makazi yao mjini Mogadishu wanasema wako katika mahitaji makubwa ya msaada ili waweze kuendelea na Ramadhani.  [Na Adnan Hussein/Sabahi]

    Wakazi wa kambi ya Bosnia ya watu wa ndani waliokimbia makazi yao mjini Mogadishu wanasema wako katika mahitaji makubwa ya msaada ili waweze kuendelea na Ramadhani. [Na Adnan Hussein/Sabahi]

Kabla ya vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika (AMISOM) kuwafukuza al-Shabaab kutoka jijini na maeneo ya karibu mwezi Agosti 2011, kwa miaka mingi Ramadhani ilikuwa imekumbwa na mzozo kwa vile kikundi chenye mafungamano na al-Qaeda mara kwa mara kilikuwa kikishambulia maeneo ya wakazi jijini na makazi ya raisi.

Farah Aweys, baba wa mtoto wa miaka mitano anayeishi huko mtaa wa Hamar Jadid katika Wilaya ya Wardhigley alisema, "Ninaukaribisha mwezi wa Ramadhani nikiwa na mtoto na mke wangu nyumbani kwetu baada ya kukimbia vichwa vya mizinga na vita baina ya al-Shabaab na vikosi vya Ethiopia mwaka 2007."

"Wakati ule, tulikwenda eneo la Elasha Biyaha, ambalo lililochukuwa nusu ya wakazi wa mji ulioharibiwa," alisema. "Tuliamua kurejea nyumbani wiki nne zilizopita baada ya serikali kuchukua udhibiti wa milango yote ya kuingilia inayoelekea Mogadishu."

"Hii ni mara ya kwanza tunaweza kuikaribisha Ramadhani bila ya vurugu mjini Mogadishu, jambo linalotufurahisha kwa sababu vikosi vya serikali vimeweza kuvifukuza vikosi vya waasi kutoka Mogadishu na miji ya jirani kama vile Balad na Afgoye kaskazini na kusini," aliiambia Sabahi.

Safiya Enow, mwenye umri wa miaka 51, mmiliki wa duka katika Soko la Bakara, alisema makundi makubwa ya wanunuzi wanajazana sokoni siku za karibuni, na watu wananunua kiwango kikubwa cha chakula kwa ajili ya kufuturu, na daku inayoliwa kabla ya sala ya alfajiri.

Hatahivyo, aliambaia Sabahi kuwa kupanda kwa bei zachakula kama vile mchele, unga, tambi, tmafuta ya kupikia, maziwa ya unga, juisi, mboga mboga na kuanguka kwa kiwango cha kubadilisha dola dhidi ya shilingi ya Somalia. Gharama hizi zimesababishwa na matatizo ya kifedha kwa familia za Kisomalia ambazo zinapokea fedha kutoka kwa jamaa zao walioko nje, na kuwalazimisha wakuu wengi wa familia kuingia mitaani na kuomba ili waweze kukidhi mahitaji ya familia zao.

Watu wa ndani waliokimbia makazi yao 'wanahitaji msaada mkubwa sana'

Wakati vita vikipamba moto baina ya jeshi la Somalia na al-Shabaab katika maeneo ya kati na kusini ya nchi, makumi ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao jijini wanakabiliwa na matatizo kuhusu chakula na makazi, na wateseka kutokana na upungufu wa misaada ya kibinadamu.

Kambi ya Bosnia kwa watu wa ndani waliokimbia makazi yao katika Wilaya ya Hodan ya Mogadishu inazihifadhi familia 72 zilizokimbia kutoka maeneo ya Bay na Bakool kusini magharibi mwa Somalia. Wanakabiliwa na hali za maisha magumu huku mwezi wa Ramadhani ukikaribia, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa chakula na msongamano wa watu.

Naibu Mkurugenzi wa Kambi, Nur Ali Abdulle, alisema msaada wa kifedha na masuala ya ndani wanaoupata kutoka Baraza la Wakimbizi la Norwei hautoshi, na kuyataka mashirika ya misaada kuwapelekea misaada ya kibinadamu ili kusaidia kupunguza mateso na huzuni.

"Tunanyoosha mikono yetu kwa wafanyabiashara wa Somalia na mashirika kutupatia misaada kwa njia ya chakula, madawa na mahitaji mengine. Tunatarajia kuwa mashirika ya misaada ya Kuwait na Uturuki yatatuletea vifurushi vya chakula na mgao wa chakula kwa ajili ya kufungulia saumu na kupambana na njaa na mahitaji ya msingi," aliiambia Sabahi.

Mariam Ali Hassan, mwenye umri wa miaka 39 na mama wa watoto sita, alilazimika kukimbia kijiji chake cha Goof Guduud karibu na Baidoa na kufika Mogadishu kutafuta mahali pa kukaa katika kambi ya Bosnia wakati mume wake alipofariki miaka minne iliyopita. Alisema alikuwa amekata tamaa kutokana na hali ngumu ya kifedha ambayo watoto wake wanakumbana nayo katika kipindi hiki wanapoikabili Ramadhani wakiwa mikono mitupu na bila chakula.

Aliiambia Sabahi kuwa yeye ndie mchumi pekee wa kulisha familia yake na kwa miezi mitano iliyopita ameshindwa kupata kazi hata moja. "Nitawezaje kutimiza majukumu yangu ya kidini mwezi huu ambapo wanawake kama mimi tunakumbwa na ukosefu wa ajira, njaa na ufukara?" alisema.

Naye Madina Hassan Abdi, mwenye umri wa miaka 32 na mama wa watoto saba ambaye mume wake ni mzee na mgonjwa, alikimbia na familia yake kutoka Hudur huko mkoa wa Bakool miaka miwili iliyopita wakati watu wenye siasa kali walipoyafukuza mashirika ya kimataifa ya misaada.

"Ninauza ndizi tu na maembe na mara nyingine huosha nguo kwa matajiri na familia zenye kipato cha kati ili kumsaidia mume wangu na watoto," aliiambia Sabahi. "Wafanyakazi wa misaada hawawezi kutimiza mahitaji yetu yote ya msingi."

"Ramadhani ndio inakuja na tuko na mahitaji makubwa sana ya msaada. Mifuko yetu ni mitupu na hatuna pesa za kutosha ili kumudu mahitaji yetu ya kila siku," alisema. "Hali inayosikitisha ya uchumi inaonekana wazi katika shughuli za manunuzi kwenye masoko ya ndani. Bado tunajaribu kuepuka njaa na makazi yetu hayana kitu."

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 63)

Dislike_icon(2)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • fatima
    July 31, 2012 @ 03:57:55AM

    Mimi ni msichana wa miaka 23 na nina elimu kwa hivyo ninatafuta kazi.

  • abdirahman
    July 27, 2012 @ 05:18:24AM

    Ningesema kuwa hii ni nzuri.

  • Fatah Maaxaay
    July 25, 2012 @ 03:57:40PM

    Al-Shabaab imekuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Somalia kwa sababu imekuwa chanzo cha kuanguka kwake. Hakuna mwekezaji wa kigeni au wa ndani atakayetaka kuhatarisha pesa zake nchini Somalia ndani ya mashambulizi ya kigaidi na ukosefu wa usalama. Hii imeifanya serikali kukosa mapato, pia serikali haiwezi kuanzisha maendeleo ya kiuchumi au miundo mbinu kwa sababu kwanza lazima ihakikishe usalama wa wafanyakazi. Al-Shabaab wameulemaza uchumi zaidi kwa kuteka nyara meli zinazobeba bidhaa katika bahari. Hii imefanya biashara ya kimataifa kuwa karibu haiwezekani na hii imekuwa na athari hasi kwa uchumi wa nchi. Matendo ya al-Shabaab pia yamesababisha isiwezekane kwa watalii kutembelea nchi, na kuikosesha serikali kiwango kikubwa cha mapato na faida ambazo yangeweza kuiendeleza nchi.

  • siciid
    July 24, 2012 @ 02:10:12PM

    Hakuna shida, tutatoa sadaka kwa watu wanaoishi makambini.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo