Julai 19, 2012
Watu wanne walijeruhiwa wakati maguruneti mawili yalipolipuka kwenye duka la kinyozi na hoteli mjini Wajir, tukio la mwisho katika mfululizo wa mashambulizi nchini Kenya, polisi ilisema.
Afisa Kamanda wa polisi wa Wajir James Mutungi aliiambia Sabahi kuwa maguruneti mawili yalirushwa katika duka la kinyozi la Ralph's Super Cutz na Roho Safi Hotel, ambazo ziko na umbali wa mita 50 tu.
"Mashabulizi hayo yaliratibiwa kwa vile yalitokea wakati mmoja, saa 2:30 usiku," alisema. "Uchunguzi wetu unaonesha kuwa hili ni shambulio la al-Shabaab. Ni shambulio lao la mfano hasa."
Mutungi alisema kumefanya ukamataji wa watu kuhusiana na tukio hili, lakini polisi wanafuatilia vielezo vingine.
Kuimarika kwa usalama na uangalizi wa jamii vimepunguza mashambulizi ya kikundi hicho chenye mafungamano na al-Qaeda, alisema.
"Hili ni tukio la mwanzo tangu tarehe 30 Mei, na tunatumai kuwa tutafanyakazi na jamii ili kuimarisha amani," Mutungi alisema.
Mmoja wa waathirika, Justus Lemeri, mwenye umri wa miaka 38, aliiambia Sabahi kuwa alikuwa nje ya duka la kinyozi akimsubiri rafiki yake wakati mlipuko ulipotokea.
"Kulikuwa na mchafuko pale watu waliporupuka kuelekea mlipuko na wengine walipokimbia," alisema.
Alisema kuwa kulikuwa na watu 10 waliokuwa wamekaa nje ya duka wakati wa mlipuko.
"Guruneti la mwanzo lililipuka karibu yetu na hatukujua tufanye nini. Halafu lingine likatua kwenye uwanja wenye mchanga na tulikimbia kabla halijalipuka," alisema. Lameri alisema huku ameshikilia majeraha yake katika vidole vitatu.
Shuhuda mwingine, Boniface Mbuvi, aliiambia Sabahi kwamba alikuwa mita chache na kikundi cha marafiki yake wakati waliposikia mlipuko. "Nilikuwa karibu na hoteli kwa muda mrefu na hakukuwa na chochote cha kutilia mashaka," alisema.
Alisema kulikuwa na watu wakakimbia baada ya mlipuko na ilikuwa vigumu kuwajua watu waliokuwa walifanya shambulio hilo.
Baada ya muda mfupi, watu walikimbilia palipotokea mlipuko ili kuwachukua majeruhi na kuwapeleka hospitali. Alisema, polisi walifika baadaye, wakalifunga eneo hilo na kuwahoji mashuhuda.
Afisa wa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Wajir Mohamed Hussein Abdikadir aliiambia Sabahi kuwa waathirika wawili wamelazwa hospitali, ambapo wawili wengine waliruhusiwa usiku huo huo.
Alisema watu waliolazwa wana majeraha mengi lakini hali zao ni nzuri.
Mlipuko hiyo ilitokea kiasi cha mita 100 kutoka Star Restaurant, ambapo shambulio la bomu la tarehe 30 mei liliua mtu mmoja na kujeruhi wengine wanne.
Pia, ni kasoro ya mita 500 kutoka Dubai Hotel and Lodging, ambayo ilishambiliwa kwa guruneti tarehe 26 Mei, na kujeruhi watu watatu.
Kenya imekabiliwa na mfululizo wa mashambulizi ya maguruenti, upigaji risasi na milipuko ya mabomu tangu ilipopeleka majeshi yake nchini Somalia mwezi Oktoba ili kupambana na al-Shabaab.
Hapo tarehe 1 Julai, watu wenye bunduki waliua kiasi cha watu 16 na kujeruhi madazeni katika mashambulizi pacha yaliyolenga makanisa huko Garissa .
Licha ya mfululizo huo wa mashambulizi ya kigaidi huko Wajir na maeneo mengine ya Mkoa wa Kaskazini Mashariki, Wakenya wanasema wameungana dhidi ya vitisho vya al-Shabaab .
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
Sampuli ya DNA iliyochukuliwa kwenye mswaki uliokuwemo kwenye begi lililokuwa na risasi lililopat...
Wakenya kumi na wasaba wameshtakiwa kwa kuvunja amani, kufanya ghasia na ukatili dhidi ya wanyama...
Al-Shabaab imedai kuhusika na urushwaji wa makombora kwenye kasri ya rais mjini Mogadishu siku ya...
Wanajeshi wa Uganda wa Kikosi Namba 9+ wanarudi nyumbani baada ya kukamilisha miezi 13 ya ziara y...
Kikosi cha polisi cha Kenya kitaanza uhakiki wa kina wa maofisa mwezi ujao, kikianza na kusaili w...
Ujambazi ulizuiwa katika ofisi za usalama za Wells Fargo huko Mombasa ulisababisha kifo cha watu ...
Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliahidi msaada wa nchi yake katika kipindi cha ujenzi mpya wa ...
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Mimi ni mvulana mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki. Ningependa kutangaza hadharani kuwa rais wa Puntland ni muongo kwa sababu hakutimiza kile alichoahidi wakati wa kampeni. Kwa kufanya hali kuwa mbaya zaidi. Alitumia pesa za umma na kuiuza nchi kwa kampuni za kimataifa zinazomilikiwa na wezi. Ningependa kuwataka wananchi wamwajibishe rais.