Julai 19, 2012
Serikali ya Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo baada ya meli iliyokuwa imebeba abiria 290 kuzama katika bahari yenye mawimbi makali siku ya Jumatano (tarehe 18 Julai) baada ya kuondoka Dar es Salaam ikielekea Zanzibar.
Boti ya MV Star Gates ilizama karibu na Kisiwa cha Chumbe kiasi cha saa 7:50 mchana, kwa mujibu wa Mwinyihaji Makame Mwadini, waziri wa dola katika ofisi ya rais na mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
"Tumepeleka waokoaji na boti tano katika eneo la tukio ili kusaidiana na waokoaji wengine," alisema. Jeshi la majini na Msalaba Mwekundu ni miongoni mwa waokoaji katika ajali hiyo.
Kwa mujibu wa orodha ya wasafiri, abiria 290 na mabaharia walikuwa katika boti hiyo, ikiwa ni pamoja na watoto 30 na baadhi ya watalii, AFP iliripoti.
Mpaka sasa miili 38 imeshaokolewa, wakati 114 bado hawaonekani, maafisa walisema.
Boti katika eneo hilo mara nyingi hubeba abiria zaidi ambao hawakuandikishwa katika orodha rasmi, kwa hivyo idadi ya watu waliokuwemo ndani -- na miili itakayohesabiwa hatimaye -- inaweza kuwa kubwa zaidi.
Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein alisema siku tatu za maombolezo zitaanza Alhamisi, huku bendera zikipepea nusu mlingoti.
"Hili ni janga la taifa na ninatangaza siku tatu za maombolezo ili kuwafariji jamaa na marafiki wakati tunafanya kila linalowezekana kujua ukweli," Shein alisema katika mkutano na waandishi wa habari.
Naye Spika wa Bunge la Taifa Anna Makinda aliahirisha Bunge siku ya Alhamisi, ili kuwapa wabunge nafasi ya kushiriki katika msiba na shughuli za uokoaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi aliomba mwongozo wa kusitisha kikao cha bunge kilichokuwa kinajadili bajeti ya wizara yake ili kutoa wakati kwa wabunge kutoka Zanzibar kuungana na familia zao.
Nchimbi aliiambia Sabahi kuwa alimpeleka Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema kuimarisha shughuli za uokoaji huko Zanzibar.
Kaimu Katibu wa Bunge John Joel aliiambia Sabahi kuwa ofisi yake ilitoa ndege kutoka Dodoma kwenda Zanzibar kwa ajili ya wabunge wa Zanzibar.
Miili iliyookolewa itapelekwa katika Viwanja vya Maisara vya Zanzibar, ambako ilipelekwa miili mengine, wakati Spice Islander, iliyozama mwezi wa Septemba 2011, ambapo karibu watu 200 walifariki na kuacha mamia ya majeruhi. Zaidi ya watu 600 walinusurika katika ajali hiyo.
MV Star Gates ni meli ya pili inayomilikiwa na kampuni ya Sea Gull Sea Transport Ltd. kuzama, baada ya MV Fatih kuzama katika bandari ya Malindi huko Zanzibar mwezi Mei 2009, na kuua watu sita.
Jamaa wa abiria waliokuwa bado hawajaonekana walikusanyika katika bandari ya Dar es Salaam.
"Kama unavyoonana hapo, tumechanganyikiwa. Hatujaonyeshwa ofisi za meli ambako jamaa zetu walinunua tiketi, na wahusika hawatoi habari zozote na hatuna njia ya kufika kulikotokea tukio," Salum Ahmad Salum aliiambia Sabahi huku anatokwa machozi.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu William Lukuvi alisema kuwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam itatumika kama kituo cha kuwajulisha jamaa habari za abiria waliopotea na wakazi wengine wa jiji.
Aisha Mwinyikai Salum, aliyefika kutoka Zanzibar kwa boti siku ya Jumatano, aliiambia Sabahi kuwa bahari ilikuwa na mawimbi makubwa kutokana na upepo mkali, ambapo anafikiri kuwa hiyo ndio ilikuwa sababu ya ajali.
Msemaji wa polisi ya Zanzibar Mohamed Mhina alisema upepo ndio uliokuwa sababu. "Hali ya hewa ilikuwa mbaya sana," aliiambia AFP, na kuongeza kuwa hali hiyo ndiyo iliyosababisha shughili za operesheni kusimamishwa usiku.
Kawaida, kiasi cha boti 12 husafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kila siku, kila moja ikifanya safari nne za urefu wa maili 39 za baharini.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Ni aibu kuwa tumekuwa na ajali 3 kama hizi ndani ya muda wa miaka mitatu. Najiuliza ni lini serikali itakuwa makini kuhakikisha usalama wa watu wake? Upepo si sababu ya kufanya meli izame, bali ni kupakia kupita kiasi. Tunahitaji kuchukuliwe hatua madhubuti dhidi ya wale wanaohatarisha maisha kwa ajili ya pesa. Mabomu yatalipuka kwa mfululizo, meli yatazama na kitu pekee utakachosikia ni "poleni sana jamani, lilikuwa kosa kubwa" au hiki au kile, lakini hakuna yeyote ambaye atalaumiwa na maisha huendelea.
mahumahubtaa
Ni huzuni kwa serikali, imetokea kwa mara ya pili, inapaswa kuboresha ulinzi wa mwambao. KHAMIS KUTOKA ZANZIBAR.
Wakati umefika kwa watu hawa kujua kuogelea ili waweze kutoroka; wakati hatari kama hizo zikitokea serikali pia ihakikishe kuwepo kwa boti nyingi kwa ajili ya watumiaji wa bahari.
Hizi ajali zimekuwa too much, na ukifuatilia zaidi unagundua kuwa meli /magari yalikuwa makuu kuu...tumekuwa dampo la vitu vibovu kwa kutafuta unafuu wa bei, na matokeo yake yatatuangamiza wenyewe...Ni msiba mkubwa sana kwa taifa, poleni sana wafiwa, na mungu azilaze mahala pema peponi roho za marehemu! http://miram3.blogspot.com/
Mungu awape moyo wale wote waliopoteza wapendwa wao, jamaa na marafiki kutokana na janga la boti, hiki ni kipindi cha majaribu kwao.