Jimbo la Kaskazini Mashariki laungana dhidi ya al-Shabaab

Na Bosire Boniface, Garissa

Julai 17, 2012

  • 3 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wafanyabiashara, wakaazi, wachungaji na maafisa wa usalama wa mji wa Garissa wanasema hawatatishwa na wimbi la hivi karibuni la mashambulizi ya katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Kenya.

  • Wafanyabiashara na wakaazi wa Garissa wanasema hawatarudishwa nyuma katika harakati zao za kila siku baada ya mashambulizi katika mji huo. [Bosire Boniface/Sabahi]

    Wafanyabiashara na wakaazi wa Garissa wanasema hawatarudishwa nyuma katika harakati zao za kila siku baada ya mashambulizi katika mji huo. [Bosire Boniface/Sabahi]

  • Wamiliki wa nyumba wanasema wanapokea maombi ya watu wanaotaka milango ya kufanyia biashara, jambo linaloashiria kuwa biashara imebakia kuwa madhubuti. [Bosire Boniface/Sabahi]

    Wamiliki wa nyumba wanasema wanapokea maombi ya watu wanaotaka milango ya kufanyia biashara, jambo linaloashiria kuwa biashara imebakia kuwa madhubuti. [Bosire Boniface/Sabahi]

"Mashambulizi kama haya yanaweza kuwakimbiza wawekezaji mara moja, hasa kwa sisi ambao Garissa si mji wetu wa asili. Lakini hakuna anayekimbia," alisema James Chege, ambaye asili yake ni Jimbo la Kati na ambaye sasa anamiliki hoteli ya Holiday Inn mjini Garissa, ambayo ililengwa na mashambulizi ya bomu la kutupwa na mkono Novemba 2011 yaliyopelekea vifo vya watu wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa.

"Nimekuwa nikifanya biashara yangu hapa kwa zaidi ya miaka minne sasa," aliiambia Sabahi. "Biashara hii ndiyo ambayo imekuwa ikiikimu familia yangu ya watu wanne na sina tatizo na mtu. Bado ninapata wateja licha ya mashambulizi."

Chege alisema jamii ya wafanyabiashara inashirikiana pamoja kufanya kazi kwa karibu sana na vikosi vya usalama.

"Mara kwa mara polisi hutushauri hatua za usalama za kuchukua kama vile kuwakagua wateja wetu kwa vifaa maalum," alisema. "Wateja nao wanashirikiana vyema kwa sababu ni kwa maslahi ya kila mmoja. Pia tuna nambari za simu za mkononi za maafisa kadhaa wa jeshi la polisi kuwajulisha kuhusiana na mambo yanayotilia shaka."

Likiwa karibu na Somalia, Jimbo la Kaskazini Mashariki ni shabaha rahisi kulengwa na al-Shabaab katika mashambulizi dhidi ya raia, wafanyakazi na maafisa wa usalama.

Hata hivyo, wakaazi wanasema matatizo ya sasa ya usalama hayahusiani kabisa na migogoro ya kibabe na kikabila iliyowafukuza wafanyabiashara katika miaka ya 1990.

Hussein Mohammed Adow, mwenye umri wa miaka 45, mmiliki wa nyumba mjini Garissa, alisema vikosi vya usalama na wananchi wa huko wamekuwa wakifanya kazi pamoja kurudisha amani. Alielezea imani yake kwamba vitisho vya al-Shabaab vitashindwa kwa ushirikiano huo.

Aliiambia Sabahi kwamba katika siku nyuma hali ya kukosekana kwa usalama ilichangia katika kiwango cha chini cha maendeleo ya mkoa huo. Baada ya kuwa na amani iliyowavutia watu kwa maisha na biashara, alisema wakaazi hawatamruhusu yeyote kuuchafua utulivu uliopo.

Adow alisema hivi karibuni alipokea simu kutoka kwa watu watatu wa Nairobi na Jimbo la Kati wakiulizia ikiwa kuwa nafasi tupu za biashara ili waanzishe maduka ya simu za mkononi. "Wote walikuwa na hamu ya kushiriki kwenye ujenzi wa Garissa," alisema.

Mashambulizi dhidi ya makanisa yashindwa kuvuruga maisha ya kila siku

Zachary Gitonga, mwenye umri wa miaka 23, mhitimu wa hivi karibuni wa chuo cha afya cha Embu (Embu Medical Training College) aliiambia Sabahi kwamba aliomba kazi ya mkemia kwenye hospitali moja ya binafasi mjini Garissa siku mbili tu baada ya al-Shabaab katika makanisa mawili hapo tarehe 1 Julai yaliyoua watu 17 na kujeruhi wengine zaidi ya 60.

Alisema ataripoti kazini mara moja ikiwa maombi yake yatakubaliwa. "Ninajua kuwepo kwa vitisho vya al-Shabaab, lakini hilo halitanizuia kama nitapata kazi huko," alisema.

Mkurugenzi wa Baraza la Biashara na Viwanda la Kenya katika Jimbo la Kaskazini Mashariki, Zeiban Sheikh Mohammed, alisema mashambulizi hayo hayajaathiri biashara.

"Maeneo ya kijamii bado yanajaa wateja. Teksi, Waombaomba, wachuuzi na wauza madukani wanaendelea kuwepo makazini mwao hadi usiku wa manane. Mafundi, fundi viatu na waashi wanaripoti kazini wakikaidi," aliiambia Sabahi.

Pamoja na hayo, vituo vikuu vya biashara katika barabara za Ngamia, Biashara na Miraa ziko kwenye pirika za kuuza vitu vya elektroniki, vyakula, nguo na vya nyumbani.

Meja Mstaafu Bashir Hajji Abdullahi, anayefanya kazi ya mshauri na mchambuzi wa masuala ya usalama nchini Kenya, aliiambia Sabahi kwamba mashambulizi ya al-Shabaab dhidi ya waumini kwenye nyumba za ibada ni jambo la hatari sana, lakini jamii na serikali wataweza kuyashinda. Alisema hamu ya watu kujikimu kiuchumi imewasaidia kuungana dhidi ya kundi hilo la kigaidi lenye mafungamano na al-Qaeda.

"Al-Shabaab wanajaribu kupandikiza vurugu za kidini kati ya Waislamu na Wakristo ili kutengeneza mazingira ya ghasia yanayowawezesha wao kuishi, lakini watu mashujaa na wenye moyo wa jimbo la Kaskazini Mashariki hawajaingia mtegoni," alisema, akiongeza kwamba kwa al-Shabaab kuchagua kuwashambulia waumini wasio na makosa kwenye nyumba za ibada kumewapotezea huruma yoyote iliyokuwa imebakia kwao.

Waumini wa dini zote mjini Garissa wameungana baada ya mashambulizi dhidi ya Kanisa la Afrika Inland na lile la Kikatoliki, huku maimamu wa Kiislamu wakiapa kuwaunga mkono ndugu zao wa Kikristo.

Wakaazi wa Kiislamu waapa kuwalinda majirani wa Kikristo

Sheikh Abdullahi Salat, mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Kenya mjini Garissa, alisema Waislamu wataunda ngome ya binadamu kuzunguka makanisa mjini Garissa wakati Wakristo wakiwa kwenye ibada zao.

"Ikiwa washambuliaji wanataka kuwaua ndugu zetu wa Kikristo, watapaswa kwanza kutuua na sisi Waislamu walio kwenye ulinzi," aliiambia Sabahi. "Mashambulizi dhidi ya waumini kwenye nyumba za ibada yamezidisha tu mshikamano wetu wa kuishi kwa ustahimilivu. Washambuliaji hao hawataweza kuwazuia watu kufanya shughuli zao za kila siku."

"Lazima tukemee mashambulizi kama hayo kwa sababu kama Wakristo ndio wanaolengwa, wanamgambo watawashambulia Waislamu. Wenye siasa kali hawana marafiki wa kudumu," alisema.

Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Kaskazini Mashariki anayemaliza muda wake, James ole Seriani alisema 10 kati ya watu 30 waliokamatwa baada ya mashambulizi hayo wako kizuizini wakiendelea kuchunguzwa, akiongeza kwamba mashambulizi kama hayo ya kigaidi yanakuwa na ajenda nyingine na ile ya kidini.

Seriani aliiambia Sabahi kwamba licha ya vitisho, serikali haitaweka amri ya kutotoka nje. Alisema wakaazi wa huko wametakiwa kurudi kwenye shughuli zao za kawaida, huku wakiendelea kuwa na tahadhari.

"Uchumi wa hapa unaongozwa zaidi na biashara ambazo hazina muda maalum wa kufungua na kufunga," alisema. "Kuweka amri ya kutotoka nje kutawafaidisha zaidi magaidi."

Maafisa wa usalama wenye silaha wamekuwa wakipiga doria mjini Garissa, wakijiweka kwenye maeneo ya nje ya makanisa na maeneo mengine ambayo al-Shabaab wametishia kuyashambulia, alisema Seriani.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 12)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • علي جبريل الكتبي
    July 19, 2012 @ 11:30:54AM

    Watu wanaoishi katika mikoa ya kaskazini mashariki ya Kenya wanajulikana kwa kupambana na Al Shabab kwa njia zote zinazowezekana. Lakini, eneo hilo ni makao ya wanaowaunga mkono Al Shabab kichini chini, na hawa hawawezi kudhibitiwa bila ya hatua kali kuanzishwa na serikali. Imedhihirika ya kuwa, kuna upungufu katika utekelezaji wa serikali kuhusu suala hili. Kwa mfano, kuna baadhi ya wanazuoni mjini Nairobi, kama vile (Hassan) ambaye huunga mkono waziwazi Al Shabab katika hotuba zake na mawaidha ya kidini. Anathubutu hata kutoa wito wa kuiunga mkono Al Shabab mbele ya vyombo vya upelelezi vya Kenya, jambo linalowafanya watu wengi kujiuliza kama kuna uhusiano wa siri baina ya Sheikh Hassan na vyombo vya usalama vya Kenya. Kuwaondoa watu hawa kunategemea umakini wa serikali katika kuishughulikia hali hii. Kwa hivyo, serikali lazima itafute msaada kwa viongozi wa kikabila wa Kenya katika maeneo hayo pamoja na maimamu wa misikiti.

  • nolascos usulle
    July 19, 2012 @ 01:51:29AM

    kwa kweli linaumiza na kukera kwa wenzetu kuhusiana na matatizo ya mauwaji yanayotokea kwa wenzetu juu ya alshabab me naomba mungu mkono wake ukae juu yao amen

  • Hassan Khan
    July 18, 2012 @ 02:14:38AM

    Kwa kweli Al Shabaab nafikiri kama hawana roho zabinadam,mambo wanafanya walah siwaukum ila Allah atawaukum.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo