Julai 16, 2012
Wapiganaji wa al-Shabaab wanajiondoa kutoka maeneo yao katika mkoa wa Lower Shabelle huku wanajeshi wa Somalia wanaoungwa mkono na kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Afrika nchini humo (AMISOM) wakielekea kwenye mji wa pwani wa Marka, umbali wa kilomita 90 kusini mwa Mogadishu, maafisa wa serikali na wa usalama wameiambia Sabahi.
"Majeshi ya ushirika yanawasaka wanamgambo wa al-Shabaab waliobakia katikati ya msitu na pia kwenye mashamba na vijiji vya mkoa wa Lower Shabelle," alisema gavana wa mkoa wa Lower Shabelle, Abdulqadir Mohamed Nur.
"Vikosi vya ushirika vinaendelea kusonga mbele kuelekea maeneo yaliyo bado chini ya udhibiti wa al-Shabaab katika mkoa wa Lower Shabelle kuhakikisha udhibiti kamili kwa mkoa mzima na kuwasaka wapiganaji wa al-Shabaab waliotoroka kambi yao ya mafunzo ya Laanta Buuro, baada ya kutawaliwa na majeshi ya ushirika," aliiambia Sabahi.
"Wapiganaji wa al-Shabaab sasa wanatafuta maficho kwenye misitu, mashamba na vijiji, lakini Jeshi la Taifa la Somalia limeapa kuwasaka popote walipo na kuhakikisha udhibiti kamili wa eneo hili huku likiwafyeka kabisa mabaki ya kundi hilo la kigaidi," alisema Nur.
Hapo tarehe 11 Julai, vikosi vya Somalia na AMISOM viliishika kambi muhimu ya mafunzo ya al-Shabaab ya Laanta Buuro, umbali wa kilomita 40 magharibi mwa Mogadishu, katika mashambulizi yaliyopelekea vifo vya wapiganaji 11 wa al-Shabaab na mateka wanne, kwa mujibu wa msemaji wa AMISOM, Kanali Ali Aden Hamud.
"Laanta Buuro ni moja ya maeneo muhimu ambalo al-Shabaab walilitumia kutolea mafunzo na kufanyia mashambulizi dhidi ya Mogadishu, na pia kilikuwa kituo muhimu cha mafunzo kwa kundi hilo," alisema Hamud.
"Kulitia mikononi eneo hili muhimu la Laanta Buuro kutaimarisha usalama wa mji mkuu, Mogadishu, na barabara ya Afgoye, na pia kutasaidia juhudi za kutoa huduma za kibinaadamu kwa watu wanaoishi eneo hilo," Hamud aliiambia Sabahi. "Hili pia litaweka mazingira salama katika viunga vya magharibi na kusini mwa mji mkuu, kwani inawakatia magaidi vituo vyao walivyokuwa wakitumia kufanyia mashambulizi."
Pamoja na kukamata vifaru na silaha za kijeshi, AMISOM ilifanikiwa pia kuokoa zaidi ya magunia 500 ya chakula cha msaada ambacho kilikuwa kimeibwa na al-Shabaab kutoka mashirika ya misaada na wakaazi wa huko, alisema Hamud. Alisema kwamba al-Shabaab ilikuwa ikiiba chakula hicho kwa lengo la kuwalisha wapiganaji wake. AMISOM ilisema kwamba msaada huo wa chakula, uliokuwa umekusudiwa kuzisaidia familia zilizoathiriwa na ukame, kingelirejeshwa kwa watu hao wenye mahitaji makubwa ya chakula.
"Kulichukua eneo la Laanta Buuro kutawazuia wanaitikadi kali wa Kiislamu kufanya mashambulizi kwenye mkoa huo," alisema kamanda wa AMISOM, Luteni Jenerali Andrew Gutti.
Maafisa wa usalama wanasema kwamba kuichukua Laanta Buuro kunafungua njia ya kuukomboa mji wa Marka, ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Lower Shabelle.
"Adui sasa anakimbia na vikosi vya washirika havijakabiliana na upinzani mkali hadi sasa," alisema Abdullahi Osman, mmoja wa makamanda wa kampeni ya kijeshi katika mkoa huo. "Tutakamilisha misheni yetu ya kuukomboa mkoa wa Lower Shabelle haraka sana, Mungu akipenda."
Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, vikosi vya jeshi la Somalia na vya washirika vimewalazimisha wapiganaji wa al-Shabaab kukimbia kutoka mji mkuu na kundi hilo limepoteza udhibiti wa maeneo kadhaa muhimu katika maeneo ya kusini na katikati ya nchi.
Endapo vikosi hivyo vya washirika vitafanikiwa kuidhibiti Marka, itakuwa ni mji mkuu wa nne wa mkoa kukombolewa kutoka mikononi mwa al-Shabaab mwaka huu -- baada ya Beledweyne, Baidoa na Hudur.
Maafisa wa serikali wanasema kuupoteza Laanta Buuro ni pigo jipya kwa kundi hilo ambalo katika miezi sita iliyopita tayari limeshapoteza maeneo mengi, ikiwemo miji ya Afgoye, Balad na Afmadow.
"Al-Shaabab waliutumia Laanta Buuro kama kituo cha kutayarisha mashambulizi yao dhidi ya vituo vya serikli na vya AMISOM mjini Mogadishu na vitongoji vyake, kwa hivyo kuukamata mji huu ni ushindi mkubwa kwa vikosi vya washirika na pia ni pigo kubwa kwa waasi," Osman aliiambia Sabahi.
"Sasa tupo umbali wa kilomita 30 kutoka Marka, ambako wapiganaji wa al-Shabaab wanakimbia wakiogopa vikosi vya Somalia na AMISOM vinavyoelekea huko," alisema. "Tunatarajia kuuchukua mji huo hivi karibuni."
Wakaazi wa Marka walisema viongozi wa al-Shabaab wameanza kutelekeza sehemu zao kwenye mji huo baada ya kuwasili kwa wanajeshi wa serikali na AMISOM kwenye eneo la Laanta Buuro.
"Wapiganaji wa al-Shabaab wamekuwa wakipita na magari madogo wakielekea Baraawe, ngome yao nyingine katika mkoa wa Lower Shabelle," mkaazi wa Merka, Abdullahi Ghuri, aliiambia Sabahi.
Gavana Nur alisema kwamba operesheni ya kuwamaliza al-Shabaab katika mkoa wake inakusudia kuongeza orodha ya mafanikio na ushindi uliopatikana na majeshi ya Somalia na AMISOM, na pia kuwanyima al-Shabaab fursa ya kujikusanya tena. Kampeni hiyo inakusudia pia kuwapata viongozi wa al-Shabaab wanaoaminika kujificha katika misitu ya mikoa ya kusini.
"Msamaha uliotolewa na serikali ya Somalia kwa wapiganaji wanaojisalimisha wenyewe hauwajumuishi viongozi wa kigaidi wanaoshukiwa kuwa na mafungamano na al-Qaeda," alisema Nur.
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Maas, samahani; unaweza kuendelea kuota. Afrika haitakusubiri hadi uamke!
Mungu Mkubwa! Waislamu wengi wametoa mawazo hasi licha ya kuwa na majina mazuri.....Muhammad, Rashid, Abdulwahad.....niruhusuni niiweke wazi...AL-SHABAAB si magaidi wala si watu Wasomali...ni Waislamu wanaopigana ili kuiokoa dini...ya UISLAMU. MWENYEZI MUNGU ANASEMA; MNAJARIBU KUWAPENDA (WAKRISTO) WAKATI WAO KWA KWELI HAWAWAPENDENI...Tafadhalini, shikamana na dini yako na usiogope kusema kama wewe ni MUISLAMU...Unaielewa historia ya marehemu Osama bin Laden? Ah! Al-Shabaab ni wapiganaji wa vita vitakatifu na Mungu akipenda Koran itachukua nafasi yake....Salaam.
Nilikuwa ninaiunga mkono sana al-Shabaab ingawaje ilishindwa. Kwa kweli ninasikia vibaya kuhusu hilo. Ninamuomba Mungu awasaidie wapiganaji wa vita vitakatifu.
Acha liwe funzo gumu kwao, pengine litawafanya wabadilike tabia zao, lakini AMISOM lazime isiwadhuru watu wasio na hatia
Ukombozi wa nchi yote ndilo ninalohisi litakalothibitisha kuwepo kwa AMISOM ndani ya Somalia. Itakuwa wepesi kwa vile wananchi wa kawaida ndio wanaobeba makali ya vita hivi.
Serikali lazima ishirikiane na makampuni yote ya usalama ili kupata mafunzo yanayohitajika ya walinzi ambao wana sifa kwa sababu wanatakiwa waweko kila mahali. Ni kweli kusema kuwa kikundi cha al-Shabaab kimekuwa dhaifu kuliko wakati wowote kabla, na kwa kweli wako katika kitanda cha kifo, na ni suala la wakati tu kabla ya kusikia mwisho wa kikundi hiki. Kuwepo kwa vikosi vya Somalia na vikosi vya Misheni ya Umoja wa Afrika kutoka mataifa kadhaa ya Afrika, vikosi vyote hivi vina lengo moja - harakati ya al-Shabaab. Mawazo ya watu wa Somalia kwa sasa yako katika kuijenga nchi yao, na hawana uhusiano wowote na kikundi hicho.
Kila mtu anataka Somalia pawe pahala pa amani pa kuishi, na kwa lengo kama hilo, Wasomali wote lazima waungane dhidi ya maadui zao. Amani nchini Somalia itategemea aina ya uongozi ambao utaongoza nchi hiyo. Mpaka sasa hali zinakwenda vizuri, kila mmoja anataka majeshi ya Misheni ya Umoja wa Afrika na Jeshi la Taifa la Somali kuendelea na juhudi hizo za hali ya juu.
Vizuri, kama ikiwa kuna ukweli hata nukta katika makala hii (ambapo ninaamini ni kweli) basi kuikomboa Somalia kutakuwa mafanikio makubwa kabisa wa AMISOM katika historia ya OAU/AU. Dunia haiwezi kusubiri zaidi kuona Somalia iliyo huru na yenye amani. Jumuiya ya Kimataifa (IC) iliangalia kwa miongo miwili ikiwa na hisia chache wakati Somalia iliponyongwa na kukabiliana na ukosefu wa utawala wa hali ya juu. Kwa vile sasa Jeshi la Taifa la Somalia, AMISOM na Kenya (inastahiki kupongezwa kwa hatua yake ya ujasiri mwezi Oktoba mwaka jana) sasa wamefika umbali huu, je jumuiya ya kimataifa haiwezi kuingilia na kutoa msaada unaohitajika sana ili kung'oa siasa kali ambazo zimekuwa zikiikanganya na kuitawala nchi kwa miongo sasa? Ninashauri kuwa dirisha hili la fursa lisiwachwe kupotea kutoka mikono ya Jumuiya ya Kimataifa. Tunahitaji kuona utawala wa Marekani na nyota inayoinuka ya China kujitokeza Somalia zote zikifanya kazi ya kwa dhamiri njema ya mamlaka ya nchi hii. Au mafuta ndio suala hapa?
Biblia inasema katika Mwanzo 6, yule anayeua kwa kumwaga damu, yeye mwenyewe atauliwa kwa kumwaga damu. Al-Shabaab mumewaangusha Waafrika.
Kwa nini kuwafanyia watu ugaidi kwa jina la dini? Wakati umefika wa Somalia kukombolewa. AMISOM, wasakeni. Mungu ibariki Somalia.
Ni bahati mbaya sana kuwa al-Shabaab wanasakwa kama mbwa baada ya kuikatili jamii ya Somalia kwa muda mrefu. Hongera AMISOM na KDF kwa kuwatoa nje hao wauwaji wa halaiki.
HONGERA KWA VIKOSI VYA WASHIRIKA. TAFADHALINI WASAFISHENI WATU HAO NJE YA SOMALIA NA SERA ZAO MBAYA, ILI WATU WA SOMALIA WAWE HURU NA HURU DAIMA.
Somalia imechukua hatua katika kujaribu kuinyanyua nchi kutoka majivu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeisabababishia nchi maumivu makali kwa zaidi ya miongo miwili. Shirikisho linafanya kila kitu kuhakikisha kuwa watu wa Somalia wako salama na wanalindwa; imewapa mafunzo maelfu ya polisi na askari ili kuwalinda watu wake na pia inawataka wafadhili kuja kusaidia na kuhakikisha wanaweza kuwalisha watu wake. Serikali ya Shirikisho ya Somalia pia imefanyia mageuzi sheria zake za mahakama na sheria nyengine ambazo ziliwakandamiza wanawake na makundi ya wachache. Haya yamewapa wanawake nafasi ya kuongea katika bunge na kushiriki katika kutoa maamuzi muhimu kuhusu watu wa Somalia. Serikali ya Somalia inaijenga upya nchi kwa kujenga barabara na miundombinu mengine. Kuna shule zinakuja katika sehemu kadhaa za Somalia na hospitali ili kuhudumia ustawi wa watu wa Somalia. Kile ambacho serikali ya Somalia imefanya ni kizuri lakini hakitoshi na ikiwa itaweza kupata usaidizi zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa itaweza kufanya mengi zaidi nakuanza upya kwa wananchi wake wote.
Msivunjike moyo wanaume, shughulikieni kuwamaliza. Al-Shabaab ni kama mbu tu mbele ya tembo katika uwanja wa vita. Endeleeni vijana.
Al-Shabaab lazima ishughulikiwe sana mara moja ili kuwapa watu wa Somalia mazingira ya kuishi kwa amani.
Waacheni wahisi joto. Hatuwezi kuishi muda wetu wote kwa woga kwa sababu ya majambazi wachache ambao hawafuati hata haki za msingi na kanuni za ubinadamu. Kwa njia moja au nyengine, upuuzi huu wa al-Shabaab lazima usitishwe.
AMISOM tafadhalini wauweni panya hao.
TUNAHITAJI VIONGOZI WANAOMUOGOPA MUNGU AFRIKA, TUNAENDA KUMUWEKA KIONGOZI NCHINI SOMALIA LAKINI NA ITIKADI ZILE ZILE ZA AL-SHABAAB, TABIA YA KUWAMALIZA WAPINZANI WAKE. KWA NINI VIONGOZI WA AFRIKA HAWANA HURUMA KABISA? KWA NINI NI MAFISADI NA WANAKWAPUA KARIBU KILA KITU KILICHOMO NCHINI MWAO? UKABILA? UDUGU? UONGOZI KATIKA AFRIKA LAZIMA UBADILIKE KUTOKA MTINDO WA KIHITLER KUELEKEA DEMOKRASIA. NAKUSUDIA KILA MTU ANATAKA KUISHI NA KUISHI VIZURI. KUNA MASWALI MUHIMU LAZIMA TUJIULIZE WENYEWE: NI KITU GANI KILIZAA AL-SHABAAB? 2. WALIKUWA NA SABABU ZA KWELI AMBAZO ZILIPUUZWA? KENYA KUWENI NA TAHADHARI KUNA KITU KINATOKOTA HUKO MWAMBAO. 3. TUNA VIKOSI VYA NJE VINAVYOVURUGA AMANI BARANI AFRIKA? JE, UONGOZI WA AFRIKA UNAFAA KWA MAHITAJI YA KIDEMOKRASIA? NINAVYOFAHAMU AL-SHABAAB WALIKUWA WANAANDIKISHA WANACHAMA KUTOKA NCHI JIRANI! NCHI HIZI ZITAFANYAJE KATIKA KIPINDI CHA BAADA YA AL-SHABAAB? MTANDAO WA AL-SHABAAB UTAFUMULIWA MOJA KWA MOJA? MIMI SIUNGI MKONO AL-SHABAAB, LAKINI DHAMIRI YAO INAACHA MENGI YA KUTAMANIKA! TUSUBIRI TUONE!
Al-Shabaab itokomezwe kabisa.
LAZIMA WAULIWE WOTE, KWA NINI KUUA BINADAMU WASIO NA HATIA?
hongera majeshi ya AMISOM FANYENI BIDII KUIKOMBOA NCHI YENU ILI MUISHI KWA AMANI
Kwa kweli ninahusudu vitendo vya wanajeshi wa Kenya ili kuimaliza AL-SHABAAB.
Hongera kwa wanajeshi ya AMISOM na Kenya na TFG; Mungu awabariki na awape ushindi dhidi ya panya wa al-Shabaab. Dada na kaka zetu wa Somalia wanawaangalieni nyinyi. Siku zote tupo miguuni mwenu kuomba ili Bwana awalinde. Tuko nyuma yenu kwa asilimia 100. Kwa mara nyengine tena hongereni.
Nadhani kuna mambo zaidi nchini Somalia kuliko kile tunachoambiwa. Sielewi kwa nini nchi nyingi zinajidai kutaka amani ya Somalia na bado wakati al-Shabaab wanapooneshwa kwenye TV wamebeba bunduki nzito, tafadhalini, silaha zile hazikutengenezwa Somalia. Inawezekana baadhi ya mataifa makubwa yako katika biashara ya silaha au kuna kitu nchini Somalia ambacho wanakitaka.
Al-Shabaab wanapambana na bado wanasimamia Uislamu na utawala wa Kiislamu. Msiwaruhusu wapuuzi hao kuwazuwieni.
Natakata kuthamini juhudi zilizofanywa na vikosi vya AMISOM ili kurejesha amani na utawala wa kidemokrasia nchini Somalia.
HAKUNA MTU MWENYE AKILI ZAKE TIMAMU KAMWE ATAKAYE IONESHA HURUMA KWA AL-SHABAAB IWE NDANI YA SOMALIA AU POPOTE ULIMWENGUNI. LUGHA IWE NI “WAMALIZENI KABISA.”
HAKUNA KUWAPINGA WATU NANCHI YAO
Ninaipenda hii! Kama majeshi ya Kenya yangeliingia Somalia miaka kumi na tano iliyopita, tungekuwa tumeiokoa sana nchi hii kubwa kutokana na kuanguka ambako kwa bahati mbaya imeteseka kwayo. Endeleeni mbele AMISOM. Tumalize kile ambacho tumechelewa kukimaliza.
Mungu siku zote yuko upande wa haki. Endeleeni na kazi nzuri, AMISOM. DAIMA AMISOM, DAIMA AFRICA!
HONGERA AMISOM, ENDELEENI KUWAKAMATA NA/AU KUWAUA PANYA NA FUKO HAWA!!!
Kila mtu katika dunia hii ana haki ya kuishi kwa uhuru na kuwa na sauti ya kupanga hatima yake. Mwenyezi Mungu aliwaumba binadamu sawa na lazima wagawane mafanikio, utawala na rasilimali zake sawa sawa. Nashangaa kusikia kifungu cha 4.5. Moja kwa moja ni kwa ajili ya kikundi kinachojitenga. Wasomali, futeni maneno hayo na mheshimu haki za ndugu zenu, Natumai mabadiliko tunayotarajia yatagusia nyanja zote na lazima kila kitu kiwe kipya (raisi mpya na baraza la mawaziri jipya), kwa misingi ya ujuzi, elimu na uzoefu.
Mimi nataka niwe mwanachama wa al-Shabaab.
Al-Shabaab waoneshwe kuwa watu wa Somalia pia wanahitaji amani. Hili lifanywe na AMISOM kuwapiga al-Shabaab na kuhakikisha kuwa wanatolewa nje ya ardhi ya Somalia ili dada na kaka zetu waweze kupata amani na kuishi kwa raha.
Hongera Jeshi la Somalia, AMISOM na wananchi shupavu wa Somalia kwa vile mnapigana tena kwa juhudi kuikomboa nchi yetu iliyobakwa (Somalia) kutoka mikono ya wahuni wasio na haya, wanaoua na kuwaacha watu vilema kwa jina la MWENYEZI MUNGU. Kwa hakika mtazawadiwa kwa ukarimu na MWENYEZI MUNGU mwenyewe.
Al-Shabaab ni watu ambao dunia yote ingeungana na kuwamaliza moja kwa moja kwa sababu wamepoteza eneo la dada na kaka zetu wa Somalia na kwa nchi nzima.
Al-Shabaab inahitajika kutokomezwa kwa haraka kutoka Somalia.
Hongera AMISOM. Tunajivunia nyinyi, watimueni hadi mtu wa mwisho. Hawa ni watu wa Jehannam.
Rafiki zangu! Al-Shabaab wanapaswa wafikirie zaidi juu ya kile wanachokifanya, kuhusu athari hasi na pia athari chanya kwa jamii. Vyenginevyo waache kufanya hivyo kwa sababu muda wao wa kuishi ni mbaya sana.
Kwa kweli mimi siungi mkono hilo, kuwa vita viwe ni chaguo kwa hali yoyote ile, Kwa hivyo ningependekeza kuwa, pande zinazohusika zije na suluhisho zuri zaidi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa janga. {Mazungumzo}ni chaguo zuri zaidi kuliko vita.
Hongereni sana majeshi ya umoja wa africa na yale ta somalia umefanya kazi kubwa sana ya kuwarudishia amani ndugu zetu wa somalia
Ni vizuri kuwang’oa makafiri hawa kutoka uso wa dunia. Wajiunge na baba yao shetani ambaye wanamtumikia na waungue motoni milele au watubu na kuwa tena binadamu.
Pumzikeni katika Maumivu (R.I.P) wanamgambo wa al-Shabaab. Mmekuwa wasumbufu kwa amani ya Wasomali na Wakenya pia. Shetani asiye na Maadili awachome katika JEHANNAM ya milele!!!!!
TUTAWEZAJE KUWA HURU KUTOKANA NA AL-SHABAAB IKIWA VIONGOZI WANAWAIBIA WATU WAO? MP KUTOKA BANADIR NA WATU WA MARKA WANAIBIWA NA RAISI NA BABA MKWE WAKE SULTAN MUSTAF, KIONGOZI WA JADI OSMAN YAROW ILI WAWEZE KUTOA FURSA KWA SULTAN MUSTAF AMBAYE HATOKEI MARKA. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NAMI KUPITIA NAMBARI HII YA SIMU
AMISOM inafanya kazi nzuri, watoeni al-Shabaab nje ya Afrika, lakini wang’olewe pia wafuasi wao nchini Kenya na sehemu nyengine za duniani.
Tuone mambo haya yataishia wapi na tuone mafanikio ya kweli ya vita vinavyoendelea.
Ninapendezwa na juhudi za serikali ya Kenya kwa al-Shabaab.
Nafurahi sana kuona hatimae ndugu zetu Wasomali mnaelekea kupata ushindi dhidi ya magaidi wanaolisumbua taifa lenu chini ya kivuli cha dini yenu tukufu ya kiislamu. Mimi si muislamu, lakini naamini mtaitendea haki dini yenu kwa kutoihusisha na siasa jambo ambalo linatoa mwanya kwa magaidi kulivuruga taifa lenu. Jifunzeni kuweka sheria za kujitawala hapa duniani nyinyi wenyewe. Kwa kuwa nyinyi ni waislamu bila shaka mola wenu atawaongoza kutunga sheria nzuri kwa karne ya leo. Msifanye makosa kuwanyanyasa wanawake kwa kisingizio cha dini. Inshalah kwa mapenzi ya mungu mtapata amani na utulivu katika nchi yenu.
Mwisho wa kifo cha ugaidi wanaodhani wanaweza kutembea kote na kuiweka chini ustawi na uhuru wa watu wengine.
Al-shabaab lazima wamalizwe nchini Somalia.
UJUMBE KWA AL-SHABAAB: WAKATI UMEFIKA WA KUNYANYUA BENDERA NYEUPE-msalimu amri au mfe.
Wanaowahurumia al-Shabaab waelewe kuwa siku zao zimehesabika nchini Kenya; waelewe kuwa tuna Shirika la Upelelezi lenye nguvu sana.
Ni ujinga kuwa mtu yeyote mwenye hisia kuweza kuwahurumia hawa, achilia mbali kuunga mkono kikundi cha kipuuzi kama hiki.
KWA KUWA AL-SHABAAB HAITHAMINI HAKI YA BINADAMU KUISHI NA UHURU, KWA NINI NA WAO WAISHI? WANAHITAJI KUKATWAKATWA NA KUTUNDIKWA DAIMA.
WASAKENI, WASAKENI NA KUWAUA (AL-SHABAAB).
Vikosi vya washirika lazima vifanye haraka ili Wasomali waufurahie uhuru wa nchi yao.
Nadhani siku za al-Shabaab zinahesabika na tuna hakika kabisa kuwa wanachimba mahandaki na mashimo ya kujificha, lakini tunawafuatilia na nina hakika kuwa watajaribu kubadilisha mbinu zao kama vile kukimbilia maeneo ya raia. Tendo lao lililopita la kigaidi lilikuwa Kenya ambako waliua watu wengi waliokuwa wanaabudu, wasio na hatia katika kanisa kwenye ibada za asubuhi.
Katika mlipuko wa jana huko Dagahaley kwenye kambi ya Dadaab nilivunjwa moyo kweli kwa kile magaidi walichoifanyia polisi ya Kenya ikiwa ni pamoja na kumlemaza rafiki yangu. Hii mambo ya alshabab lazima imalizwe
Wakati siku hiyo itakapofika na tutakuwa tunaangalia kwenye TV zetu na habari katika vyombo vyote vya habari kuwa KISMAYU IMEANGUKA, nitajivunia sana kwa vile yote hii ni kutokana na uwezo wa KDF na bila ya shaka majeshi ya AMISOM na nchi zilizoungana nasi. Kitu kimoja zaidi, katu sitalichukulia tena jeshi letu kuwa la bure bure tu.
Kidole cha gumba juu kwa AMISOM.
Vizuri sana AMISOM. Al-Shabaab lazima wasalimu amri kwa sababu tunaweza kuona mara hii watajisalimisha. Kazi nzuri AMISOM.
Kila mtu apeleke maombi yake juu ili kuviombea vikosi vyetu nchini Somalia.
Lazima washughulikiwe kwa sababu wao ndio chanzo cha mfumko wa bei nchini Kenya. Wanaiba na kujenga majumba Nairobi
Ninaipenda makala hii, inakupa habari za wazi n.k.
Natumai tu kuwa Somalia patakuwa pahali pa amani kwa kuishi. Wasomali waungane dhidi ya maadui wao. Kuwepo au kutokuwepo kwa al-Shabaab, amani ya Somalia inategemea mtindo wa uongozi wanaotumia. Idumu Somalia
Al-Shabaab ni majambazi wa kawaida wanaopenda waonekane kuwa ni shupavu. Kwa kweli ni waoga wa hali ya juu. Viongozi wao wanakufa kwenye mapango na mashimo bila ya kufyatua risasi hata moja huku wakijikojolea. Kama AMISOM itaendelea kwa mwendo huo, majamaa hao watabakia katika vitabu vya historia vya daraja la tatu ifikapo mwisho mwa maka huu.
Kifo kwa al-Shabaab.
Endeleeni jeshi la Kenya.
Waasi hawa sio tu wanavuruga amani nchini Kenya bali dunia nzima. Wangefanya busara na kujisalimisha kwa KDF. Hongereni askari wetu ambao mmeamua kumaliza udhibiti wao kusini ya Somalia. NINAWATAKIENI USHINDI MKUBWA.
MSIMRUHUSU ADUI KUDHIBITI ENEO LENU. NINAVISALIMU VIKOSI VYETU. MUNGU AWAPE NGUVU KILA SIKU. ENDELEENI, DUA ZANGU NI KUENDELEA NA KUPATA USHINDI WOTE. MUNGU YUPO PAMOJA NANYI. MUNGU AVIBARIKI VIKOSI VYA KENYA NA WENGINE WOTE WALIOBAKIA AMBAO WANAVIPA USAIDIZI.
Mpaka sasa ni nzuri sana. Endeleeni na moyo huo AMISOM na jeshi la taifa la Somalia. Kumbukeni kuwa uovu hauwezi kushindana na wema hata kidogo.
Hii ni hisia yangu, serikali ingeshirikisha kampuni zote za kibiashara za usalama, wape mafunzo walinzi ambao wana sifa kiasi kwa sababu wanapatikana kila mahali. Al-Shabaab hawataweza kufanya chochote.
Ni kweli kusema kuwa sasa al-Shabaab ni dhaifu kuliko mwanzoni na kwa kweli wapo katika kukata roho na ni suala la wakati tu kabla ya kusikia mwisho wa kikundi hiki chenye sifa mbaya nchini Somalia. Sababu ya hilo ni kuwa wanayadhibiti miji michache tu na kwa hakika mji pekee walio na udhibiti kamili ni Kismayu. Sababu nyengine inayokifanya kikundi hiki kudhoofika ni kuwepo kwa nguvu kubwa za kijeshi kutoka pande zote; vipo vikosi vya Kenya, vikosi vya Somalia na vikosi vya AMISOM vinavyotoka nchi tofauti za Kiafrika. Vikosi vyote hivi vina lengo moja tu nalo ni al-Shabaab. Idadi ya askari katika kikundi chao pia ni ndogo sana; hii ni kwa sababu hawawezi kuandikisha watu zaidi kwa sababu ya miji michache wanayoyadhibiti. Watu wa Somalia sasa wanashughulikia kujenga upya taifa lao na hawana chochote cha kufanya na kikundi hiki. Kikundi pia kinapungukiwa na fedha kwa sababu hawawezi kuteka nyara meli au kufanya shughuli nyingine za kigaidi ambazo zilikuwa zinawapatia fedha. Na ni kwa sababu hii hawawezi kununua silaha.
@maas, wewe ni mmoja wa al-Shabaab na unapaswa kupondwapondwa!
Wakati umefika wa kuwashirikisha Waethiopia, wao wanajua jinsi ya kudhibiti watu kama al-Shabaab. Tuwasaidie wana wa watu wakubwa ili tuweze kumaliza tishio hili la al-Shabaab.
DISEMBA IKO MBALI KWA AL-SHABAAB ISIPOKUWA?
Hongera AMISOM, Al-Shabaab lazima wasalimu amri!
Al-Shabaab ni kitu kidogo kinachotishia maisha ya watu wasio na hatia na ndugu zetu wamethibitisha hilo. Amani ni ya umuhimu mkubwa kwa ubinadamu na ninawaomba wapiganaji wetu wenye uwezo kushinikiza na katu wasitake muwafaka hasa na magaidi. Heshima, watu wenye uwezo. Tunawatakieni ushindi.
AL-SHABAAB ni hatari kubwa na wanataka kuiua dunia yote.
hakuna anayeweza kuwashinda al-Shabaab kwa sababu tunapigana mmoja mmoja na tunaogopa ya kuwa tunaweza kufa na kuziacha familia zetu nyuma lakini wao wanapigana kwa msaada wa Mungu... wao wana dhamiri, sisi tuna fahari, wao wanapigana mpaka kufa, sisi tunapigana kwa ajili ya ushindi... Idumu al-Shabaab.
ITAWABIDI AMISOM WATAFUTE FEDHA ZAIDI KUTOKA KWA JUMUIYA YA KIMATAIFA ILI IWAPE MAFUNZO MAAFISA ZAIDI WATAKAOPELEKWA SOMALIA BAADA YA KUKAMATWA KWA MIJI AMBAYO NI NGOME ZA AL-SHABAAB.
NINAWACHUKIA AL-SHABAAB, WAO NI TATIZO KWA ULIMWENGU. LAZIMA WAMALIZWE.
umakini uongezeke kwa wanajeshi wa AMISOM !
Kwa mawazo yangu, nadhani al-Shabaab watahamia Kenya na kusababisha fujo kwa miaka 25 ijayo au zaidi.
Al-Shabaab watakwenda Kenya kutoka Somalia, watabakia kule kwa miaka 25 na kuendelea.
Tunawatakieni mafanikio katika kinyang’anyiro na tuna hakika kuwa tutawaua al-Shabaab wote.
Hawa wanamgambo wako kila mahali ikiwa ni pamoja na Nairobi na maeneo ya vijijini wakiwa katika harakati za kuandikisha watu, nani kasema watamalizwa?
Kenya isikate tamaa, tunavitakia mafanikio vikosi vyetu.
Al-Shabaab hawawezi kuogopwa tena, lazima watolewe ndani ya Somalia.
Kwa wale wanaowaunga mkono Wakenya kwa hili, Mungu awabariki nyote ndugu zangu wa Kenya, ninawatakieni maisha marefu ufaidike matunda ya kazi yenu nzuri. Kwa kikundi cha AMISOM, kama isingekuwa kujiunga na kuwezesha, tusingekuwa tumepiga hatua hii. Sote TUUNGANE PAMOJA NA KUOMBA DHIDI YA WATENDA WAOVU. Ninawatakia wanaotutakia mema wakati mzuri na wa amani. Kwa moyo mkunjufu, hili ni jambo zuri, kwa vile ninaamini kuwa AL-QAEDA wanafuatia – Amin. Mpaka watu watambue kuwa iko haja ya kumwamini Mungu na sio binadamu wala mawazo yao.
“Usalama unatolewa na imani kwa imani itakayopatikana mwishoni; lakini mwisho wa yote, maadui hawa lazima watengwe kutoka Kenya. Ninaliomba jeshi letu na WAKENYA wengine, lazima kuwepo na KAZI KAMA TIMU kwa sababu kufanya kazi kama timu ndio siri ya mafanikio ya timu. Wakati wanachama wa timu wanapokuwa wamoja, huwa rahisi kutimiza KAZI yao. Kwa hivyo, tuwafanye WAPUUZI HAWA WAELEWE KUWA sisi WAKENYA HATUTARUDI NYUMA mpaka tuibuke MASHUJAA.
AL-SHABAAB LAZIMA WAMALIZWE KABISA KABISA
Kikundi hiki cha magaidi kinagharamiwa kutoka karibu na mbali. Juhudi zifanyike ili kuligundua hilo. Heshima kwa watoto hawa wadogo wa AMISOM.
Kikundi cha al-Shabaab lazima king’olewe mara moja. Ninapenda maendeleo yanayofanikiwa na AMISOM, lakini tunahitaji habari za siku hadi siku kutoka kwa vyombo vya habari vya mataifa yetu.
Kila kitu kilichopangwa kwa ajili ya al-Shabaab, kitafanikiwa na karibuni hivi watamalizwa na askari wetu wenye nguvu na mbinu. Hatimaye watafanikiwa kuyakamata maeneo wanayojificha. Kila la heri askari wetu.
AL-SHABAAB wamekuwa maumivu ya kichwa kwa serikali ya Somalia, ikiwa kuna njia kwa watu hawa wanaojiita al-Shabaab kufutiliwa mbali ndani ya Somalia litakuwa jambo zuri kwa watu wa Somalia ili waweze kufaidi matunda ya amani kama nchi nyingine ulimwenguni.
Wayne: Kwa vikosi kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya kuliepusha eneo hili na vitisho vya vurugu: Ninasema, tunawapongezeni! Endeleeni na kazi mnayofanya na msirudi nyuma hadi kundi hili limeangamizwa kabisa. Kwa kikundi cha watu wenye siasa kali kuendelea kuwakatili wananchi wasio hatia kwa jina la dini, hilo halikubaliki, kwa vile sio jambo jema. Wabanjeni kama wanyama waharibifu, kwani ndivyo walivyo. Mko katika mawazo na maombi yetu.
Al-Shabaab lazima watolewe nje ya Somalia.
Al-Shabaab wamekuwa tishio kubwa, shukurani kwa washiriki wote kwa kuwang’oa. Kwa kweli ikiwezekana iwe ndani ya muda mfupi sana kadiri inavyowezekana.
NINAZISHAURI TAAZSISI ZA SERIKALI ZIWE MAKINI NA ZIFANYE KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA NA ZIACHE KUANGALIA WATU MACHONI HICHO NDIO KINACHOTUKWAMISHA KUFIKIA MAENDELEO YA TAIFA LETU LA ZANZIBAR PIA TUACHE KUWAKUMBATIA WATU NA KUWAPA NAFASI ZA KAZI AMBAZO HAWANA SIFA ZA KUZITENDEA KAZI NA MWISHO NI LAZIMA TUWASHIRIKISHE WATAALAMU KIKAMILIFU NA KAMA NI WACHACHE SERIKALINI BASI NINAISHAURI SERIKALI IWAAJIRI WATAALAMU KWA HARAKA KWANI TUPO WENGI AMBAO TUMEMALIZA VYUO NA TUKO MITAANI (NASI NI WATU MUHIMU SANA KATIKA TAASISI ZA SERIKALI )
Ninawapongeza Jeshi la Taifa la Somalia na AMISOM kwa kazi zao nzuri. Ninatarajia kutembelea Somalia karibuni kwa ajili ya utalii.
Sipendezwi na uamuzi huo
Hongereni! Tunajvunia kwenu. Dua zetu ziko nyuma yenu. Wasafisheni hawa wanamgambo wenye vichwa maji.
Waoga! Iweje kikundi cha watu wenye akili timamu wasababishe taabu kwa binadamu wenzao! Nakusudia, sielewi kabisa! Watu hawa watafaidika kwa lipi kutokana na yote hayo? Mifuko iliyojaa? Wakiwa na makosa au bila makosa? Vipi mtakwenda kufaidi pesa hizo?
Kwa nini AMISOM hamalizi jehanum yote ya al-Shabaab kwa ajili ya uhuru wa Somalia.
Hongera wasichana na wavulana wetu.
Inatosha, zaidi ya miaka ya 20 ya matatizo, njaa, uharibifu mkubwa. Wasafisheni, wakati umefika dai letu la amani na mapatano kusafisha njia. Idumu Somalia.
Hongera kwa Jeshi la Taifa la Somalia na AMISOM kwa kazi nzuri. Natarajia kuitembelea Somalia kwa utalii karibuni. Tafadhali endeleeni hadi muikomboe Somalia na sisi tuombe kwa Mungu ili nchi yetu ipate amani na tuungane kama mtu mmoja, nchi moja.
Al-Shabaab wanakuwa ni tishio kubwa kwa Wakenya na lazima washughulikiwe kwa usalama wa nchi yetu.
Huu ni ushindi kwa watu wa Somalia na kwa Pembe ya Afrika kwa jumla. Wadumu askari wetu na Mungu awabariki nyinyi na familia zenu.
Kwa ajili ya maendeleo na busara ikiambatana na kurejea kwa maadili, wanahitaji kung’olewa katika ardhi ya Somalia. Msamaha na huruma visiahidiwe kwa hatari ya kuwa wanamgambo wanawatishia wananchi wasio na hatia na nchi jirani. HONGERA MAJESHI YA AMISOM.
Kukimbia kwao sio suala, suala ni wapi wanakimbilia, isiwe Kenya. Serikali ifanye chochote kuhusu suala hilo.
Nimeipenda
Ninawatakieni mafanikio.
hivi kwanini sehemu nyingi waislamu wanauwa watu sheria au utaratbu wa kuuwa wanajifunza tok a maandiko gani, angalia somalia nigeria, na kwingineko . naomba kufahamu kwanini maana naelewa kuwa waislamu watu wa amani lakini kukicha vikundi vya ugaidi kwa jina la waislamu vinaongezeka. tanzania nako kuna kundi linachoma makanisa kwa kusngizia kueneza uislam. jamani amani in muhimu na kuuwa watu wasio na hatia si mapenzi ya mungu ndg zangu waislamu kemea vitendo hinvyo vyaa vikundi vya kuijua eti umejitoa mhanga wakati unapokufa unauwawengine wasiohusika, sijui kama mtume aliuwa maana angekuwa wa kwanza kujilpua , au kutega mabomu kuchoma makanisa , makanisa aliyakuta na akayaacha.
Kwa kuwa magaidi wanatoroka, hasingekuwa jambo la kushangaza, kwa vile ni kama panya na siku zote wamo katika kukimbia. Wao ni kama viongozi wao waoga, miongoni mwao akiwemo mbwa najisi, Osama bin Laden. Alikuwa anawatuma walio chini yake kuua watu wakati yeye alikuwa anaishi katika nyumba kinyaa kama alivyokuwa yeye mwenyewe, mbali sana na uwanja wa vita vya “Jihadi.” Uislamu haina uhusiano vyovyote na mtu huyu mmoja kinyaa au anayemfanana kama vile wanachama wa al-Shabaab. Mimi sina tatizo na kuuawa kwa Osama: tatizo la uharibifu lingetoa. Nina wasiwasi kuwa maiti yake iliyooza inaweza kuiharibu Bahari ya Arabia iliyo nzuri. Ikiwa mtajaribu tena kuua mdudu au panya mwengine, naomba msimtupe baharini, maji yanaweza kuharibika. Karibuni mtasikia kuwa watu wawili hawa wamekimbia chini kwa kutumia pasipoti ya kughushi, na kesi itafungwa. Ni huzuni kwenu, watumwa wa dirham na dinari.
Inahuzunisha kusikia uongo mwingi kama huu. Al-Shabaab bado wapo Mogadishu, Ceelaasha, kabla ya Lanta Bur na mbele zaidi ya huko.
AL-SHABAAB WANAPASWA KUMALIZWA ULIMWENGUNI KOTE.