Vikosi vya usalama vyaisafisha Mogadishu mabaki ya al-Shabaab

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Julai 13, 2012

  • 3 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vikosi vya usalama vya pamoja vinafanya operesheni ya kiwango cha juu ya kusafisha mabaki ya al-Shabaab kutoka Mogadishu na maeneo inayoizunguka kulekea mkutano wa katiba unaokuja.

Operesheni hiyo iliyoanza tarehe 7 Julai, tayari imepelekea kukamatwa kwa zaidi ya wanachama 500 wa kikundi hicho na kutaifishwa kwa idadi kubwa ya silaha na milipuko.

Katika operesheni hiyo ya pamoja, polisi, jeshi na Misheni ya Umoja wa Afrika (AMISOM) vilielekeza maeneo ambako washukiwa wa al-Shabaab walijichanganya na washirika au wapenzi wa al-Shabaab kujificha huko. Maeneno yaliyopekuliwa ni pamoja na mashariki, kaskazini, na magharibi ya mji pamoja na karibu ya mji wa Afgoye, ambao kabla ulikuwa ngome imara ya al-Shabaab na vikosi vya serikali na AMISOM kuuchukua hapo Mei.

"Dhamiri ya kampeni hii ya usalama ni kuisafisha Mogadishu na mabaki ya al-Shabaab ambao wanakataa amani," alisema Khalif Ahmed Irig, kamanda wa kikosi cha usalama katika mkoa wa Banadir.

Vikosi vya pamoja vinafanya msako wa hali ya juu katika majumba, wanaotembea kwa miguu na magari, aliiambia Sabahi. Pia waliweka sehemu za ukaguzi kwenye maeneo ya kuingilia au kutoka katika maeneo yaliyopangwa kudhibiti watu wanaoingia na kutoka.

Kampeni hii ya usalama itaendelea hadi siku kadhaa zijazo na kuyajumuisha maeneo yote ya Mogadishu pamoja na maeneo yaliyokombolewa hivi karibuni ili kutokomeza maficho na mabaki ya al-Shabaab ili kuzuia vikundi vyenye silaha kuibuka upya. "Vikosi vya usalama vimeandaa mpango wa kutekeleza katika maeneo yaliyokombolewa karibuni ili kuimarisha usalama nchini kote," Irig alisema.

Baada ya kuhakikisha usalama wa barabara, viwanja vya mraba vya umma na masoko, operesheni italenga kuwanyang'anya silaha wananchi na kufanya uvamizi wa polisi majumbani katika mji na viunga vyake, hasa katika maeneo ambayo yanashutumiwa kuwa silaha zimefichwa huko, Irig alisema.

Hii ni operesheni kubwa kabisa kufanywa na vikosi vya pamoja mjini tangu Serikali ya Mpoto ya shirikisho kuidhibiti Mogadishu na maeneo ya jira baada ya al-Shabaab kutolewa nje ya mji mkuu mwezi Agosti 2011.

Vikosi vya usalama pia viligundua maficho ya silaha za al-Shabaab katika eneo la Suuqa Hoolaha kaskazini ya Mogadishu. Maficho hayo, ambayo vikosi vya usalama vilisema ni ya al-Shabaab, yalikuwa na vichwa vya mizinga mikubwa, misili na mapipa yaliyojaa milipuko.

"Vikosi vya usalama vimepokea taarifa kuwa mabaki ya al-Shabaab yamekuwa yakijipenyeza [katika maeneo yenye watu wengi] na kujidai ni wananchi baada ya maficho yao kwenye miji ya Afgoye na Balad kuharibiwa," Kapteni wa Polisi Ahmed Ali Hassan aliiambia Sabahi, na kuongeza kuwa operesheni hii ya pamoja ina dhamiri ya kuwafukuza watu hawa wanaojipenyeza.

Kuhakikisha usalama wa mkutano wa katiba

"Lengo la operesheni hii ni kuifanya Mogadishu kuwa iko salama kwa asilimia 100 na tayari kwa kuendeshamkutano wa katibana uchaguzi mkuu unaokuja," alisema mkurugenzi mkuu wa Wizara ya mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa, Jama Mohamed.

Mohamed alisema kuwa wizara imetoa maelekezo ya kuzidisha usalama jijini na maeneo yanalizunguka kabla ya kuanza kwa mkutano wa katiba, ambao ulisitishwa moja kwa moja.

Kamati ya Somali ya Usalama wa Taifa pia imetangaza kuwa itafunga baadhi ya barabara za Mogadishu wakati wa mkutano wa Bunge la Taifa la katiba.

Hassan Mohamed, mkazi wa Mogadishu mwenye umri wa miaka 38, alisifu utendaji wa vikosi vya usalama. "Tumefurahi sana; utendaji wa vikosi vya usalama umezidi matarajio yetu," aliiambia Sabahi.

Mohamed aliwataka wananchi kuvisaidia vikosi vya usalama na polisi ili kuufanya mji kuwa salama. "Kuufanya mji kuwa salama si dhamana ya upande mmoja pekee, bali ya Wasomali wote," alisema.

Naye Fatima Omar, mwenye umri wa miaka 46 na mmiliki wa duka katika eneo la Suuqa Hoolaha, aliviomba vikosi vya serikali ya Mpito ya Shirikisho kuongeza juhudi zake za kuulinda mji. "Hali ya usalama Mogadishu imeimarika vya kutosha ikilinganishwa na miezi kadhaa iliyopita, kutokana na juhudi zinazoendelezwa na serikali," aliiambia Sabahi.

Omar alielezea kuridhishwa kwake na utendaji wa jeshi na polisi katika kutekeleza dhamana yao ya usalama na utulivu mjini, kuwasafisha al-Shabaab na kuwakamata watu mmoja mmoja wanaoharibu usalama wa umma.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 15)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • KO'KORE OMINGLI
    July 17, 2012 @ 06:43:52AM

    NINAISIFU TIMU YA AMISOM, KWA KWELI INAFANYA VIZURI. TUNAHITAJI BUSARA NCHINI SOMALIA. INAKUWA HAINA MANTIKI WAKATI BINADAMU ANAPOFURAHIA KUWAONA BINADAMU WENZAKE WANAKUFA OVYO KWA SABABU YA UROHO WA UTAJIRI TU. ULIMWENGU UMEFIKIA PAHALI AMBAPO WATU WANAHUBIRI AMANI. HAKUNA ANAYETAKA KUPOTEZA MAISHA YAKE BILA YA SABABU.

  • بارك الله بل من يقاتل الارهاب
    July 17, 2012 @ 06:12:50AM

    Kuanguka kwa itikadi ya siasa kali nchini Somalia kulichochewa na vikundi vya kigaidi ambavyo viliwalazimisha wawafuate kwa kutumia vurugu na kuwatisha. Ikiwa tabia hii iliwapa utawala wa nguvu, Wasomali walibakia wakiwa waoga na wasiwasi wa vurugu, unyama, kukosa maadili, ukatili na ukandamizaji wa kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab. Baadhi ya matendo yao hayawezi hata kufikirika na kukubalika. Hawa si chochote bali magengi yanayoua watu. Kwa hivyo, vikosi vya usalama lazima viudhibiti ugaidi na kuwatokomeza magaidi ambao hawakufanya chochote zaidi ya kuvunja majumba, kulazimisha wanavyotakata wao kwa wengine na kuivuruga nchi. Zaidi ya hayo, hawawatakiwi watu jema lolote, wao ndio sababu ya kukosekana kwa utulivu nchini Somalia. Magaidi hawa ni washenzi; wanaua watu bila ya kuchagua wawe wanawake, vijana au wazee. Watu hawa wasiotenda haki lazima wamalizwe; hawana huruma, kwa hivyo lazima waukuzwe, wakimbizwe, wakamatwe na kutokomezwe ili watu wa Somalia waweze kuishi kwa uhuru, amani, utulivu na usalama.

  • Tayab Ibarim Sayyad
    July 17, 2012 @ 05:58:57AM

    Katika nchi kama Somalia na Iraki, umasikini umekuwa sababu ya kuibuka kwa makundi mawili makubwa kabisa ya ugaidi ulimwenguni. Tukichukua hali ya kawaida huko Somalia, vijana wanaojiunga na al-Shabaab ni vijana wasio na ajira na wanaotoka maeneo yenye umasikini wa kutisha. Wanajiunga na vikundi vya kigaidi kwa sababu ya ahadi ya kupata pesa. Kuna mkakati unaoweza kutumiwa na serikali ili kusaidia kupambana na ugaidi nao ni kwanza kupambana na umasikini. Umasikini unaweza kuwasukuma watu kufanya kila aina ya mambo maovu katika juhudi za kujipatia pesa kidogo. Serikali ya Somalia inaweza kufanya kazi ya kuhakikisha kuwa misaada yote inaopelekwa kwa ajili ya njaa katika maeneo yaliyokumbwa na umasikini, na kujaribu kuboresha hali za maisha ya watu. Wanaweza kuandaa shughuli za ajira kwa vijana ili kuwaepusha na kujiunga na vikundi vya kigaidi.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo