Julai 12, 2012
Mpango wa kadi za vitambulisho vipya vya taifa nchini Tanzania umeanza mwezi uliopita jijini Dar es Salaam katika jitihada za kuimarisha usalama na kuongeza mapato ya serikali, kwa mujibu wa Naibu Mkuu wa Polisi, Issaya Mangulu.
Mpango huo unawataka raia wa Tanzania na wa kigeni wanaokaa nchini humo kwa angalau miezi sita kujisajili na walio na umri wa kuanzia miaka 18 kujisajili na kutembea na kitambulisho.
"Kimsingi, vitambulisho hivi vitasaidia mfumo wetu wa kuwafuatilia wahalifu," Mungulu aliiambia Sabahi. "Taarifa kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) zitatumika (wakati wa uchunguzi) kujua historia ya mshukiwa, ambayo inajumuisha anapoishi au kufanya kazi na mengine kama hayo."
Alama za vidole na picha za wenye vitambulisho hivyo zitachukuliwa kurahisisha utaratibu wa kuwatambua watu hapo baadaye. Kuwatambua watu wanaoishi na kufanya kazi nchini Tanzania ni jambo la msingi katika kuhakikisha usalama, hasa kutokana na idadi isiyojulikana ya wakimbizi ambao wameingia kutoka nchi jirani zenye vita na migogoro, alisema.
Kwa zaidi ya miaka 40, Tanzania imepokea wakimbizi kutoka Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na baadhi ya wahalifu wanaweza kuja kupitia njia hiyo hiyo, alisema Mungulu.
Kutokana na wimbi hilo la wakimbizi wanaoingia nchini, kuwa na mfumo wa kutambua utaifa wa mtu, hadhi ya kisheria na taarifa nyingine kunakuwa muhimu kwa juhudi za jumla za usalama, alisema.
Taarifa za vitambulisho vya taifa zitaunganishwa na mifumo mingine ya kitaifa, kama vilemfumo wa namba za posta, Mamlaka ya Mapato ya Tanzania, taarifa za polis,i na mashirika ya usalama ya kimataifa kama vile Interpol. Mafungamano ya mashirika kadhaa, ya ndani na ya nje, yatasaidia kufikia lengo la muda mrefu la usalama na uchumi, alisema Mungulu.
Hadi sasa, waajiriwa wa serikali na wataalamu wanaofanya kazi kwenye mabenki wamepewa kipaumbele na kusajiliwa, alisema Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu, katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mpango huo ulioanza Septemba, utasambaa sehemu zote za nchi. Usajili unatarajiwa kukamilika mwaka 2014, lakini utaendelea hata baada ya hapo kuwasajili raia ambao wanafikia umri wa kulazimika kuwa na kitambulisho. "Usajili utakuwa utaratibu wa kuendelea," alisema Maimu.
Kwa ajili ya kujiandaa vyema na hatua hii, Maimu alisema NIDA ilifanya programu ya majaribio mwanzoni mwa mwezi Juni katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. Zoezi hilo liliisaidia mamlaka hiyo kuyagundua na kuyapatia ufumbuzi mapungufu yaliyoonekana kwenye mchakato huo, alisema.
"Kama unavyojua, Dar es Salaam ndio mji mkubwa kabisa nchini. Tukifanikiwa kutoa vitambulisho Dar es Salaam, mradi huu utafanikiwa nchi nzima," Maimu aliwaambia waandishi wa habari.
Vitambulisho vitatolewa bure kwa Watanzania wote, ambapo Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) litalipia gharama za vitambulisho vya wakimbizi.
Chini ya mpango huo mpya, itakuwa ni lazima kwa raia wa Tanzania kujisajili na kutembea na kitambulisho cha uraia. Kuvunja sheria hiyo kunaweza kupelekea kifungo cha hadi miezi sita, alisema Meneja Mahusiano wa NIDA, Thomas William.
"Baada ya yote, kitambulisho hicho kitakuwa kinaunganishwa na mifumo ya huduma za kijamii. Ukikataa kujisajili au kutoa taarifa za uongo, hilo litakuwa na athari kwako mwenyewe. Utakuwa hustahiki kupata huduma nyingine za kijamii hadi utakapokuwa na kitambulisho hicho. Kwa hivyo, watu lazima wawe navyo," William aliiambia Sabahi.
Vitambulisho hivyo vitatolewa na kampuni ya Malaysia iitwayo Iris Corporation Berhad, ambayo imeshinda zabuni ya kutoa vitambulisho milioni 25. Mradi huo utagharimu shilingi bilioni 200 (dola milioni 124) na unafadhiliwa na serikali ya Tanzania.
Joseph Bwakyayo, 55, mfanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara jijini Dar es Salaam, aliiambia Sabahi kwamba kuwatambua wakopaji kutawasaidia wakopeshaji kutathmini hatari na gharama za mtu binafsi na kuamua juu ya uwezo wa kukopesheka wa kila mkopaji, ambako kutaifanya mikopo iwe rahisi zaidi kufikiwa na raia.
"Watanzania hawakusajiliwa na ni gharama kubwa kuwatambua waombaji wote wa mikopo kuhakikisha kuwa benki zinawakopesha watu wanaostahiki. Ni kama kucheza kamari," alisema Bwakyayo.
Bwakyayo alisema mara kwa mara wakopeshaji hulazimika kuthibitisha mambo mepesi kama eneo la makaazi kwa kutembelea nyumbani au kwenye biashara ya mkopeshwaji, na ambako pia huweza kukutana na utapeli wa wale wanaojifanya kuwa ni wamiliki wa biashara fulani. "Kufidia hatari kama hizo, tunaweka kiwango kikubwa cha riba," alisema.
Pamoja na kuziweka gharama za kuthibitisha juu ya wakopaji, baadhi benki hulipisha hadi asilimia 40 kuepuka hatari ya kufilisika, alisema.
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
ni pongezi kw taifa letu. Kw hatua muhimu kama hiyo. Je usajili w vitambulisho hivyo arusha itaanza lini?n inachukua muda kiasi gani mtu apate kitambulisho hicho?
nataka kufahamu vitambulisho vya uraia vitaanza kutolewa ini tangu siku ilipozinduliwa pale karemjee
Wasomalia wanapaswa kusaidiwa wawe huru kutoka kwa mashetani hawa wa al-Shabaab.
Serikali ya Tanzania inapaswa kujua ya kwamba watapata mapato lakini haitawazuia wahalifu kupitia vitambulisho ukiangalia operesheni ya utaratibu ya watu wa Afrika Mashariki wanapovuka mipaka. Italazimu ukarimu wa watu wa Afrika Mashariki kusimamisha uhalifu na ugaidi na wala sio kutundika vitambulisho shingoni mwao au mifuko zao za fedha zilozopigika kiuchumi, begi za mkono na mapochi.
Mimi ni Mtanzania mwenye asili ya Somalia, kitu kinachonisikitisha ni jinsi gani watu wanavyoniona kama mkimbizi wakati kamwe sijawahi kuiona nchi yangu ya asili. Tatizo ni kubwa kwa sababu tunajiona wenyewe kama Watanzania kwa rangi, au asili ya Kibantu au kwa kuzaliwa? Ninastaajabu jinsi watu walivyo na wasiwasi juu ya wahamiaji wakati wanaweza kuleta maendeleo na mawazo mapya ikiwa wapo hapa kwa nia nzuri. Kitu nilicho na hakika nacho ni kuwa kama Obama angekuwa Mtanzania basi asingekuwa raisi kama watu wangejua kama baba yake alikuwa Mkenya, lakini taifa kubwa kama Marekani, lilijua hilo na kumfanya rais wao. Sina maana ya kusema kwamba watu waje kuhamia hapa na kuondoka kirahisi, lakini ubaguzi wa rangi ndio kitu tusichotaka miongoni mwa Waafrika. Tayari yanatosha yale tuliyopata kutoka kwa wazungu. Natumaini hii halitatokea katika utoaji wa vitambulisho.
Ni programu nzuri sana, lakini suala muhimu sana ni kuwa makini nayo hasa kwa kutoa elimu kwa umma ili watu waizowee programu hii.
tunaomba hii sera iendelee vizuri na ifanikiwe lakini wananchi tusiwe kikwazo tujitokeze kwa wingi na pia na viambatanisho vyote pia tuwafichue amabao tunamashaka nao. ''TANZANIA DAIMA''
nimepenada sana website hii mimi nina website yangu naweza kukopi habari kutoka kwenu mimi niko Tanzania
mi nasema ni mawazo mazuri sana yanayotolewa humu mi nimeyakubali, na vilevile nchi yetu itajengwa na sisi watanzania wenyewe, ni kufanya bidii tu
mi naona huu mpango ni mbaya kwa ile imani ya mpinga kristo ,wa kristo wa kweli hawataweza kuuza wala kununua bila kuwa na card hizi ,card hizi zina faida ya muda mfupi bali athari zake ni za maisha yote kwa maana nyuma ya mpango huu ni mpinga kristo amenza kusajili watu wake bila wao kujua ili iwe rahisi kwake kutawala dunia
Hili ni wazo zuri sana kwa Tanzania na hii ninaitoa kutoka ndani kabisa ya moyo wangu. Ninaipenda nchi yangu na daima nitaipenda. Endelea Tanzania.
Ni wazo zuri sana, lakini wasiwasi wangu hautaondoka kwani raia wa kigeni na wakimbizi watatumia nafasi hiyo kujipatia uraia kirahisi ukizingatia nchi yetu ilivyokuwa na huruma pia karibu karibu nyingi na kutaka kuonekana ina amani, upendo na msaaada katika nchi zisizopenda kusaidiwa.
Mpango ni mzuri, nionavyo mimi katika hili ni kutoa kwanza vitambulisho vya muda. Baada ya hapo kila atakayekuwa amepewa kitambulisho hicho afuatiliwe kwa makini ili kuona kama taarifa alizozitoa ni sahihi. Hii itakuwa ni pamoja na kufuatilia pale alipozaliwa iwapo kweli anafahamika na pia pale alipoishi kwa muda mrefu iwapo anafahamika. Vinginevyo tutatoa vitambulisho hata kwa wasiostahili. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.
Ninaukaribisha mpango huu mpya wa kitambulisho cha taifa kutolewa Tanzania na ningependa kuwa mshirika wa mpango huu na pia kukumbuka kuwa mimi ninatoka nchi nyengine kwa hivyo tafadhalini mnisaidie kadi moja tu. Asanteni sana.
Ni hatua nzuri kwa serikali ya Tanzania. Kwa kweli uwajibikaji unahitajika ili kufanya mambo yaende vizuri, kwa faida ya wote.
ZOEZI HILI LIFANYWE KWA MFULULIZO NA SERIKALI MARA KWA MARA KAMA LINAVYOFANYIKA NCHINI KENYA WAKATI MTU ANAPOFIKA UMRI WA MIAKA 18. MFIKIRIE HILO WATANZANIA WENZANGU.
Ni nzuri, na naipenda! Lakini bado nina wasiwasi kwamba kutokana na uwezekano wa kuwepo rushwa, ufisadi, uchakachuaji etc. kupitia wale wanaoshughulikia uandikishaji. Inawezekana wenye kufanana na sisi, Watanzania, ambao si wazawa asilia wakapatiwa vitambulisho vya uraia kwa kuzaliwa, ikiwa hakutakuwepo kazi ya ziada na madhubuti ya uhakikisho thabiti kwenye maeneo waliyoonyesha wametokea/wamezaliwa!
Ya! ni jambo zuri kwa nchi yetu sababu ni njia rahisi itakayotuwezesha kuwapata wahalifu, hasa kutoka external country, isipokuwa cjaupenda utaratibu wake kwani watu wanakaa mda mrefu ktk vituo vya kujisajili, serikali iongeze wahudumu.
Nchi yangu ya asili – moja ambayo Watanzania wengi wanataka waende au kuhamia, imefanikiwa kuendelea bila ya kadi za utambulisho katika vita viwili vikuu vya dunia, na idadi kubwa ya wataokuwa wahamiaji tangu wakati huo. Kule kwa kawaida watu wana maoni kuwa vitambulisho ni aina ya “Kaka mkubwa anakuangalia”. Kwa ujumla, hamtakiwi tu kutoa alama zenu za vidole na vitu kama hivyo iwapo utakamatwa – na kushitakiwa kwa uhalifu. Vyenginevyo kila mtu anaruhusiwa awe na faragha – cheti chako cha kuzaliwa kinatosha isipokuwa tu unahitaji paspoti au leseni ya udereva – hatua nyengine huchukuliwa. Kwangu mimi hili linaonekana kuwa na mtazamo hasi uliopitiliza kiasi kuhusu wahamiaji nchini Tanzania. Idadi ya watu nchini Tanzania ni kidogo ikilinganishwa na nchi za Ulaya, na serikali haina mpango wowote wa maana wa mafao ya uzeeni au pensheni ambao wahamiaji wataumaliza. Kwa hivyo kuna madhara gani wahamiaji wanafanya kwa nchi – haielekei kama kutamwagika kwa rasilimali nyingi. Jiulize mwenyewe kwa makini – Unapata nini kutoka kwa taifa ikiwa unamiliki kitambulisho ikilinganishwa na wale ambao hawana? Kwa mimi inaonesha zoezi lenye gharama ndogo zaidi litafanya hii kazi. Wapewe wale Watanzania ambao hawana vyeti vya kuzaliwa. Utaratibu uliobakia- leseni za udereva, paspoti, n.k., tayari vipo ikiwa unacho cheti cha kuzaliwa. Habari zilizobakia za kadi ya utambulisho – ikiwa ni raia unayefuata sheria – ni serikali tu kutaka kujua zaidi kukuhusu kuliko wanavyohitaji kujua.
Kitambulisho kitasaidia kupunguza mlolongo wa taratibu nyingi zenye usumbufu wakati wa kutoa huduma kama kitatumika kwa malengo yaliyowekwa, kama vile kupata mkopo, kutambulisha utaifa nchi za nje, lakini nadhani vingegaiwa kwa watanzania tu, pia wazawa kwani nchi yetu bado haitambui uraia wa nchi mbili.
Wakati umefika tuwe na kitambulisho ambacho ni muhimu kwa wananchi wote watu wazima. Wasiwasi wangu pekee, kama walivyo wengi wetu, tutahakikisha vipi hatutoi kadi hizi kwa wasiokuwa raia?
Ni wazo zuri sana lakini watu wanajichanganya baina ya masuala ya kisiasa na masuala ya kiserikali. Elimu zaidi inahitajika kuhusu vitambulisho vya taifa.
Ni vyema Taifa lilivyo fikiri kufanya kitu kama hiki, kwani maisha yanakwenda yakibadilika na watu wanaongezeka katika Duni nafikiri ipo siku watu wataishi popote pale kama hakutakuwa na ulinzi wa kutosha. Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania.
Tutumaini kuwa suala zima linakwenda kama lilivyopangwa. Wazo zuri sana.
Ufunguzi mzuri kwa fursa ya kibiashara...kwa Wakenya...
Napendekeza iwepo njia ya kujisajili kwa njia ya mtandao kwasababu wengine unakuta muda uliopangwa Dar kwa zoezi hili yeye yuko safarini,akirudi anakuta zoezi limepita kwa dar es salaam kwa hiyo anakosa kitambulisho.
NINAIPENDA HII, MIMI PIA NINASUBIRI KUKIPATA WAKATI UTAKAPOFIKA KWA SISI WA ARUSHA, TANZANIA.
Kwa jumla hii ni hatua nzuri ya kushughulikia masuala yanayohusiana na uhamiaji haramu, lakini vipi wataweza kuhakikisha kadi hizo hawapewi watu wasiokuwa Watanzania, kwa vile tuna uzoefu wa paspoti za Tanzania kupewa watu wa mataifa mengine?
Hii ni hatua nzuri sana kufikiwa hadi sasa, Tuiunge mkono serikali ili ifanikiwe.
Hii ni njia ya vipi baadhi ya watu wanaweza kuiba fedha za umma. Sioni umuhimu wa kitambulisho kwa nchi yenye ufisadi kama hii...mabilioni hayo yangefaa kuelekezwa kwa kilimo Kwanza
Wazo zuri. Ninaipenda Tanzania, nitakuja Mbezi karibuni, Afrikana
Hii ni habari nzuri kwa Watanzania. Wasiwasi wangu ni kuhusu utolewaji wa vitambulisho kwa watu wasiostahiki. Uongozi lazima uwe na tahadhari juu ya suala hili. Nakumbuka mwaka 2003 nilikuwa ninapita katika uwanja wa Amsterdam huko Uholanzi. Nilifurahi kumuona mtu ana paspoti ya Tanzania. Nilidhani nilikutana na ndugu yangu. Nilimwakia, Mambo? Akapiga kelele kwa sauti ya Kinaigeria, “kijana, shughulika na yanayokuhusu”. Saa chache baadaye nilimwambia kuwa nitapiga simu Ubalozi wa Tanzania Uholanzi uje kuthibitisha urai wake. Alikuwa tayari kunipa hongo ili nimsaidie. Mwisho akaniambia ukweli. Nilishangazwa kuwa alipata paspoti ile kwa dola 600.
Lazima tuwe na tahadhari kuwapa watu kutoka nje hadhi sawa na watu wa Tanzania ni hatari. Ninapinga programu hii ikiwa wanasema Watanzania sio wazuri lakini wanajumuisha wageni, hili ni balaa. Hili si kwa ajili ya HATIMA YA TANZANIA ni kwa ajili ya watu wachache kama ( Wanaigeria, Wakongo, Marekani, Waarabu, Sudani, Afrika Kusini, kenya, Uganda, Lebanon, Urusi, Uchina, Korea, Ujapani, Taiwan) na hao wote watakuwa Watanzania! Lazima tuliangalie hili. Mimi bila ya kulazimishwa na mtu au shirika lolote, makala hii siipendi.
Sijaridhika sana na njia ya zoezi hili linavyofanyika. Baadhi ya watu wanalalamika kwa nini hawapigwi picha wakati wa kujiandikisha, wanachofanya ni kujaza fomu tu na kuondoka. Ndio lote hilo linalohusika na kitambusho? Au ni ujanja ujanja tu? Hatutaki pesa zetu za kodi kutumiwa mara nyengine tena kwa masuala hayohayo. Tafadhalini, wale wanaofanyakazi wahakikishe kuwa masuala yote muhimu yanayohusu kitambulisho yafanywe ipasavyo na kwa elimu yote.
Nimepeleka habari zote kuhusiana na kadi ya utambulisho, itachukua muda gani kuipata kadi yenyewe?
Mimi ni mwanafunzi ninayesoma nje ningependa nipate kitambulisho cha taifa, nitakipataje? Kuna mpango gani kwa wale walioko nje ya nchi? Ninaweza kukipata kwenye Ubalozi wa Tanzania?
Mimi ninaishi Tanzania na ni mgeni, ni kazi nzuri. Endeleeni.
NI NZURI, LAKINI WANAOENDESHA USAJILI LAZIMA WACHUKUE TAHADHARI ZOTE ZILIZOWEKWA, KWA MAANA YA KUWA MTU YEYOTE ASIDAIWE MALIPO KWA SABABU KITAMBULISHO NI BURE. MWENYEZI MUNGU ALIBARIKI ZOEZI HILI LIFANYIKE IPASAVYO.
Ni mfumo mzuri sana, kila mtu anayeishi Tanzania anatakiwa awe nacho.
Wapeni hongo wanawake watakuja kukujazia fomu au subiri kwenye foleni kwa masaa na hilo sio jambo la kawaida katika sehemu hizi za dunia. Tunaneemeka kwa zao hili la biashara ya rushwa, ukilipa mambo yanafanyika, hulipi simama na subiri zamu yako kwa masaa. Ninakushukuruni, Firozali A. Mulla DBA.
Hili ni zoezi zuri lenye mwelekeo mzuri kwa serikali ya Tanzania na nchi kwa jumla.
Hili ni jambo zuri sana. Ili kupunguza wahamiaji haramu kila Mtanzanaia lazima awe anatembea na kadi yake ya utambulisho. Itakuwa ni salama zaidi kumtambua mtu wakati atapokuwa anahitaji huduma yoyote ya kijamii na atajulikana kirahisi bila ya misukumano. Hata hivyo, ni muhimu kwa nambari katika vitambulisho zikawekwa vizuri katika msimbo ili kuepusha hatari za wanaoghushi.
Teknolojia ya alama za vidole karibuni itapitwa na wakati. Ninashauri kadi ziweze kuingiza na kuhifadhi Alama za DNA ili kuokoa gharama baadaye kwa vile hili litakuja karibuni hivi.
Nadhani ni wazo zuri lakini serikali lazima iwe na tahadhari katika kipindi hiki.
kwasababu za kiusalama wa kitaifa international ID ni muhimu sana hivyo kwa watanzania wote tujitokeze katika zoezi hili
Ni wazo zuri.
Mungu ibariki Tanzania, tuko pamoja na pamoja tunaweza. Ninajivunia Tanzania na Kitambulisho kinanitambulisha mimi ni nani. Hongera.
Nimefurahishwa kujua kuwa hatimaye serikali imeanza mradi huu ghali sana. Hata hivyo, rekodi ziwe si za kawaida kiasi gani, kutakuwa na sehemu ya ukweli ndani yake. Watu hawataweza kujiandikisha kwa majina tofauti kwa vile alama za vidole hazitaruhusu hilo kufanyika. Hapo ndipo tutakapoweza kumripoti “yeyote” anayejidai kuwa “mtu mwengine” kwa kuandika nambari zake za kitambulisho. Hilo litawaogopesha wadanganyifu pamoja na wahamiaji haramu, ambao kabla waliwadanganya Watanzania wasiojua chochote. Endeleeni na kazi nzuri
Kwa kweli wazo ni zuri lakini tatizo langu ni, litaweza kusalimishwa na kusimamiwa vipi kwa sababu Tanzania ni nchi mama ya Afrika, nchi ambayo huwezi kujua nani ni raia, nani mhamiaji au mwananchi halali. Hata hivyo, hongera Serikali yangu kwa kuja na wazo hilo kwa sababu sasa tutaweza kuhesabika, nchi jirani yetu ya Kenya wanafanya vizuri juu ya hilo na acheni niwaambieni, ndio kwa nchi yangu ninayoipenda, ambayo ninajivunia, nchi ya Mlima Kilimanjaro.
Kadi ya utambulisho ni wazo zuri LAKINI changamoto kubwa zinakuja kutoka watu wa nje, kuna wageni wengi. Siku hizi wageni hao wana vyeti vya kuzaliwa, wameolewa na Watanzania, walisoma Tanzania, wanafanyakazi TZ, wanajua Kiswahili vizuri sana, UTAWEZAJE KUMTAMBUA MTU WA AINA HII KATIKA JAMII YETU???
Wale wote waliopewa kazi hii ya heshima lazima wawe wazalendo na kuhakikisha kuwa hakuna mtu ambaye sio Mtanzania anapata kadi ya utambulisho. Kila mtu lazima awasilishe asili ya wazazi wake na hili lithibitishwe na kamati maalumu ili kuwang’oa wale wanaodanganya. Kila atakayekamatwa anadanganywa afungwe. Kusiwe na faini, tafadhali. Hilo litaifanya nchi yetu kuwa na usalama zaidi.
Nadhani, hatua iliyochukuliwa haina maana, ni kuhasarisha fedha za Serikali na hapa imelazimishwa na sheria kuelekea wakati uliowekwa, kwa vile watu wengi ni wa daraja la wafanyakazi na kwa kupata fursa kutoka kwa kampuni katika mazingira ya sasa ni vigumu sana ili tu kufanya uandikishaji.
Juu ya Muharam Mchume, pendekezo langu ni kuwa moja ya kibali kinachohitajika kutambua utaifa wa mtu ni cheti cha kuzaliwa kiwe ni lazima na nyaraka nyengine ziwe ni ziada tu ijapokuwa ni muhimu pia. Kwa sababu tuna wageni wengi wanaoishi isivyo halali na wengine ni wanyang’anyi.
brilliant idea kudos the government of Tanzania
Ni zoezi muhimu lakini ni kujirudia kwa juhudi na kuhasarisha fedha za umma. Miaka michache iliyopita, kulikuwa na juhudi za kukusanya rejista la wapiga kura, watu hao hao wanaoulizwa kujiandikisha leo (miaka 18 na zaidi) walitakiwa kupitia kwenye mchakato huo na kupata kadi zao za kura. Kama tungekuwa wazalendo na wenye kufahamu vema pesa za umma, data zilizokusanywa wakati ule zingeweza kutumika kupata habari ambazo sasa watu wanaulizwa kwa ajili ya kadi za utambulisho. Nina hakika baadhi ya mafisadi vigogo walifanyia kazi vipi asilimia 10 wakati huo na asilimia 10 nyengine wakati huu wa zoezi hili, litaongezeka kuwa rushwa mara mbili na kushauri serikali yetu ya kifisadi wasijali kuyaunganisha mazoezi haya mawili ili kuokoa pesa za umma.
Kwa upande wangu sidhani kama ni jambo zuri! Kwa sababu watu lazima wawe na vyeti vya kuzaliwa na Watanzania wengi wenye umri zaidi ya miaka 45 hawana vyetI vya kuzaliwa kwa hivyo hii itatoa nafasi kwa wasiokuwa Watanzania kughushi matakwa tofauti. Kwa hivyo serikali lazima iwe na tahadhari!
Hii ni nzuri sana. Ninatoa hongera zangu kwa serikali yetu. Hii ni kusema kuwa, kabla ya wazo hili la vitambulisho mtu hakuweza kusimama na kuulinda utaifa wake. Lakini sasa, kwa kuja vitambulisho, tunaweza kujivunia kweli na Tanzania yetu na kuizungumza mbele ya yeyote na popote ulimwenguni. Sifa tele kwa serikali ya Tanzania na shirika lake kwa moyo wao wa kutekeleza mradi huu.
Nchi yetu imekuja na wazo zuri, tushirikiane kwa hili.
Kwa maoni yangu kuhusu uandikishaji, tunapaswa kuongeza muda kwa Watanzania hasa Dar es Salaam ambapo uandikishaji umeanza, kwa sababu watu huenda kazi mapema kwa hivyo watakuwa na muda mdogo wa kujiandikisha na pia kufungua vituo vya kujiandikisha. Vituo ziwe mapema kidogo ili wafanyakazi wafike mapema kiasi cha saa 1 asubuhi na vituo kufungwa saa 12 jioni. Hili lingerahisisha kazi.
Wazo la kuwa na vitambulisho vya taifa ni zuri lakini utawala lazima uwe na tahadhari katika zoezi zima hasa katika kuandikisha wasiokuwa Watanzania.
Huu mpango unaonekana ni mzuri au pengine unaweza kufanyika, lakini sina hakika vipi wakimbizi wataondolewa katika mchakato wa uandikishaji, isipokuwa tu tukubaliane kama taifa, wale wageni watakaofanikiwa kutojulikana wawe Watanzania wa kiasili kutokana na werevu wao.
Mimi ni mgeni na ningependa nipate kimoja, vipi na wapi ninaweza kujiandikisha?
Sawa, hili ni wazo zuri lakini kiasi cha pesa zilizowekwa kwa ajili ya kazi hii ni kikubwa sana na nyinyi vijana mliopewa kazi hii kuifanya mtajinufaisha sana.
Ndio! Ni wazo zuri lakini wengi wa Watanzania wanaishi vijijini, na wengi wao hawana habari ya kuhusu mpango huu. Kwa hivyo mpango na mkakati mzuri lazima uundwe ili mradi huu ufikie malengo yaliyopangwa. Mnaweza kwanza kufanya utafiti rahisi kwa kutoa vitambulisho vya muda.
GOOD GOVERNMENT FOR ID,NOW TUTAKOPA KIULAINI,HATA KUWEKEANA BOND.a
Kama kweli mpango huo utafanjika kwa haki na usawa itakua vizuri sana.Na ningependekeza waanzie kwenye wilaya na vijiji vilivyopo mipakani.Kwani mambo kama haya mnapenda sana kuyaanza DSM,hiyo ni tabia mbaya sana kuona huko ndio Tanzania. Acha mara moja:
Nzuri lakini kwa mimi inaelekea kama wahamiaji haramu wana matatizo mengi.
Wazo zuri.
Ndio! Makala nzuri lakini sielewi nini kitatokea kwa wageni kupewa vitambulisho sawa na wenyeji.
Sidhani kama kutakuwa na mafanikio yoyote katika hili, kwa vile tumeshaahidiwa mambo mengi lakini serikali yetu imeshindwa kuyatimiza, hata hivyo ni wazo zuri.
Kwa kweli tunahitaji VITAMBULISHO VYA TAIFA lakini KWA NINI PIA WASIO KUWA RAIA WANATAKIWA WAJAZE FOMU. Tuwe makini hivi ni VITAMBULISHO VYA TAIFA SIO VITAMBULISHO KWA wanaoishi TANZANIA
HONGERA!!!!, HII ITALETA UFANISI KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUPATA MIKOPO.
Huu ni mwanzo wa alama ya ushetani (666). Kumbuka kuwa alama ya ushetani itafanyakazi kupitia mfumo wa utambulisho ambao una data zako katika mfumo huo, na ikiwa hukubaliani nao, unazuia kupata mahitaji ya lazima kwa maisha.
Ninapendezwa na mpango huu lakini nina kitu kimoja cha kuukumbusha uongozi – kuna idadi kubwa ya taasisi za elimu ya juu zitakazoukosa mpango huu kutokana na siku za mapumziko kwa sababu baadhi yao watakuwa hawapo mahali pao pa kuzaliwa na mahali pa kusoma kwa wakati huo huo. Njia nzuri kwa watu hawa kuweza kuandikishwa ni kuwapo mahali pa masomo ikiwa habari zote zitapatikana.
SAFI SANA! KAZI MUDA MREFU...TUNAHITAJI VITAMBULISHO...NA NDIO HILO LITAKUWA JAMBO ZURI!
Wazo zima linaelekea kuwa zuri lakini wasiwasi wangu ni kuwa mradi huo unaweza uwashirikishe watu ambao hawachaguliki kama wasio kuwa raia. Kenya, kwa mfano, ilianza mradi huu tangu mwaka 1923 na ndio sasa unaendelea vyema. Habari zilizotolewa zinachunguzwa na hata kuangalia katika kizazi kimoja au viwili vya watu walioandikishwa. Huko Sinza na Kinondoni Hananasif, kwa kutaja chache, tuna idadi kubwa ya Wamalawi, Wanaijeria na Wakongo na wote wanajiitwa Watanzania. Kuna wengine wanazo hata kadi za kupigia kura. Ushauri wangu ni kuwa kuwe na tahadhari ya ziada katika zoezi zima.
Makala hii ni nzuri.
Hii ni nzuri sana. Tunaomba kila kitu kitaenda vizuri kama kilivyopangwa. Asanteni kwa wazo zuri. Hongera.