Somalia yajiandaa kwa uchaguzi wa kwanza wa urais jijini Mogadishu

Na Adnan Hussein jijini Mogadishu

Julai 12, 2012

  • 7 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kampeni za uchaguzi wa rais nchini Somalia zimeanza kwa dhati zikiwa na wagombea 21 wanaogombea Villa Somalia -- kasri ya rais jijini Mogadishu.

  • Spika wa bunge Sharif Hassan Sheikh Aadan akizungumza wakati Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali (kulia) na rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed (katikati) wakiangalia jijini Mogadishu Juni 2011. [Stringer/AFP]

    Spika wa bunge Sharif Hassan Sheikh Aadan akizungumza wakati Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali (kulia) na rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed (katikati) wakiangalia jijini Mogadishu Juni 2011. [Stringer/AFP]

Kufanyika kwa uchaguzi jijini Mogadishu kutakuwa ushindi wa kihistoria kwa watu wa Somalia, alisema Abdirashid Abdi Ahmed, msimamizi wa programu wa Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa yenye makao yake Nairobi.

Aliiambia Sabahi kuwa uchaguzi huu ni muhimu mahsusi kwa sababu kwa miaka kadhaa iliyopita serikali ya mpito iliundwa nje ya nchi. Kwa mara ya kwanza kutoka kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, mabunge yote mawili ya bunge na rais yatachaguliwa kutoka ndani ya jengo la bunge jijini Mogadishu.

Ajoos Sanuura, mshauri wa usalama kwa kamanda wa polisi wa Somalia, alisema kuwa kufanyika kwa uchaguzi wa rais jijini Mogadishu ni jambo la kuvutia na chanzo cha motisha kwa vikosi vya usalama kufuatilia  jitihada za kueneza utulivu na usalama nchini kote Somalia.

"Mogadishu inashuhudia shughuli za kisiasa zisizo na mfano na mikutano mikubwa kati ya rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed na viongozi wa kikabila kuwaleta katika kuelekea kwenye uidhinishaji rasmi wa katiba na kuwachagua wajumbe wa bunge la shirikisho," Sanuura aliiambia Sabahi.

Wagombea

Ahmed alitangaza ugombea wake kwa kipindi cha pili kama rais tarehe 25 April kuendelea kutekeleza programu za usalama na siasa ambazo alisema zimethibitisha mafanikio katika kuwaangusha al-Shabaab. Pia aliahidi kufanya taasisi za serikali na mahakama kufanya kazi kikamilifu, zikitoa njia kwa jitihada za ujenzi upya nchini kote kuinua uchumi.

Hata hivyo, Ahmed alisema anakaribisha ushindani kwa urais. "Nina furaha kabisa kuona wagombea wakifika katika mji mkuu kushiriki kwa ukaribu na kinyanganyiro kikubwa cha ushindani kwa kiti cha urais, kwani kila mgombea alitangaza programu yake ya kisiasa kwa kujiamini kama uadilifu na usawa wa uchaguzi unavyostahili," Ahmed alisema Juni.

Baada ya wajumbe wa Bunge la Katiba kuchaguliwa na rasimu ya katiba kuidhinishwa, wajbunge watamchagua spika wa bunge na manaibu wawili ifikapo tarehe 4 Agosti na rais ifikapo tarehe 20 Agosti, kwa mujibu wa orodha iliyopo..

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa na wanasiasa wanasema uamuzi wa Ahmed kutaka awamu ya pili ya miaka mitano umebadilisha nguvu ya kinyang'anyiro cha jamii. Viongozi wengi wana mawazo kwamba Ahmed, na Spika wa Bunge Sharif Hassan Sheikh Aadan, watakuwa na faida kwani wanatafuta kushika madaraka na kuendelea kuiongoza serikali.

Abdirahman Abdishakur Warsame, mjumbe wa bunge la mpito na mwenye matumaini ya urais alisema rais ana faida muhimu kwani yupo madarakani.

Zaidi ya Warsame, rais wa sasa, spika na Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali, wafuatao ni kati ya idadi ya wagombea wa nafasi ya urais: waziri mkuu wa zamani Mohamed Abdullahi Farmaajo, mwanadiplomasia mzoefu Abdullahi Mohamed Adow, mwanajeshi wa zamani na muislamu wa msimamo wa kati Abdirahman Mohamed Badiyoow, profesa Ahmed Mumin Warfa, mfanyabiashara Hajj Mohamed Yasin, profesa Ahmed Ismail Samatar, mwanataaluma na mwalimu wa zamani wa katika chuo kikuu huko Mogadishu Hassan Sheikh Mohamud, mbunge na waziri wa zamani Mohamed Mohamud Guled, na mbunge Mohamed Qanyare Afrah.

Rais wa Somalia alisema kwamba kila mgombea anapaswa kujua kwamba atashughulikia nchi ambayo imeharibiwa, ina uchumi dhaifu, na taifa lenye majeraha ambalo limekuwa likikerwa kwa vita na ukame.

"Siasa sio tu kugombea nafasi ya urais peke yake wakati ukiiacha nafasi nyingine za kisiasa za kuihudumia nafasi za nchi," alisema.

Mwanaharakati wa masuala ya Kijamii Zeytoon Ibrahim alisema wanatakiwa kuwa wazi katika uchaguzi ili kuzuia wagombea kulipia kura, hali itakayosababisha wagombea wengine kutolewa nje ya kinyang'anyiro.

Alitoa angalizo kwamba jumuiya ya kimataifa ilikuwa ikihitaji kipindi cha mpito kumalizika kwa amani na kidemokrasia, kikisogea kuelekea utawala thabiti wa shirikisho ambao utashirikisha matabaka yote ya jamii ya Somalia.

Intaneti yatoa ushawishi katika kampeni

Mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Somalia anasema baadhi ya wagombea wanaoishi nje ya Somalia wanatumia intaneti kusaidia kusambaza mawazo yao na ajenda, ambazo pia zimewafikia idadi kubwa ya wagombea muhimu.

Profesa Ahmed Ali, mtaalamu wa masuala ya siasa na usuluhishi wa migogoro, aliiambia Sabahi kwamba awamu hii ya uchaguzi wa rais ina wagombea wengi mara mbili ya uchaguzi wa rais wa kipindi cha mpito mwaka 2000, 2004 na 2009, ambavyo kila kipindi kilihusisha wagombea si zaidi ya 15.

Dahir Mohamud, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii, alisema intaneti inawaruhusu wagombea kueleza maoni yao kwa watu wengi zaidi, mawazo na shauku yao, ambayo haikuwezekana wakati wa uchaguzi uliopita wa rais wa Somalia nchini Djibouti na Kenya.

"Kinachofurahisha sasa ni kiwango cha uelewa kuhusiana na siku zijazo za taifa na wasiwasi wake, kwani watu wengi wa Somalia walieleza matakwa yao ya kufanya kazi kwa uaminifu kuelekea katika Somalia ya kidemokrasia na ya shirikisho," Mohamud aliiambia Sabahi. "Hili linaongeza kujiamini katika siku zijazo za Somalia, bila kujali ni nani atachukua madaraka makubwa ya Somalia au [mwelekeo] wake wa kisiasa."

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 35)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Suujino
    August 16, 2012 @ 07:39:15PM

    Wananchi wa Somali wameishi kipindi cha mpito kigumu sana ambacho kilikuwa kirefu kiasi cha miaka mingi lakini kila kilicho na mwanzo kina mwisho na huu ndio mwenendo wa ulimwengu ambao Mungu kaumba maisha juu yake kila kitu kina mwanzo na kila kitu kina mwisho na kwa hivyo yamaisha mateso ya wananchi wa Somali kwa kuwekwa katiba mpya ya nchi baada ya mkutano wa wajumbe wa tume ya uanzilishi inayo karibia kufikia wajumbe 823 au zaidi kidogo baada ya jitihada kubwa wamepata katiba mpya inayowahakikishia maisha yenye utulivu na amani yasiyokuwa na utumiaji nguvu na vitisho au vita japokuwa baadhi ya wapingaji walidhaniwa huenda wangelipua sehemu ya tume ya uanzilishi wakati wa mkutano wake lakini rehema ya Mungu ipo juu ya kila kitu katiba mpya ilitoa mwangaza na wakasherehekea wajumbe wa tume ya uanzilishi pamoja na wananchi wote wa Somali kwa jumla kwa mafanikio haya makubwa ambayo yatanukuliwa kwenye kumbukumbu kwa maneno yenye nuru.

  • DBA Hussein Ibrahim Amey
    August 3, 2012 @ 06:20:51PM

    Ningependa kuwaomba ndugu zangu katika bunge jipya la Somalia kumchagua Profesa Ahmad Ismael Samatar kuwa raisi wa Somalia kwa sababu ni mtu aliyeonesha uzalendo kwa miaka 20 wakati nchi ikiwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na uharibifu. Sina uhusiano kwa kidamu wala urafiki na sijawahi kumuona lakini nimeshamsikia akielezea maoni yake kwa uzalendo wa hali ya juu. Ndugu zangu, msipoteze fursa hii ambayo hamtaipata tena. Fikirieni vyema fursa hii na mumchague Profesa Ahmad Ismail Samatar kuwa raisi wa Somalia. Ahmad Ismail Samatar anastahiki urais wa Somalia. Msipotoshwe na mambo mengine yasiyokuwa ya lazima na mtakuja kujuta baadaye. Kuiokoa Somalia kunawahitaji mumchague Profesa AHMAD ISMAEL SAMATAR KUWA RAISI WA SOMALIA.

  • Doctor of Business Administration Hussein Ibrahim
    August 3, 2012 @ 05:59:13PM

    Ninawaomba wabunge wa Bunge jipya la Somalia wasipoteze fursa hii adimu ya kuchagua mtu anayefaa wakati ukifika kwa ajili ya Uraisi wa Somalia. Mgombea anayefaa na mzuri zaidi kwa Uraisi wa Somalia ni Profesa Ahmed Ismail Samatar. Ndugu zangu wabunge wapya, lifikirieni hilo, na msitumie vibaya uwezo mliopewa. Sina uhusiano naye wa kikabila,kirafiki au wowote ule. Yeye alizaliwa katika pembe moja ya Somalia na mimi nilizaliwa upande mwengine wa Somalia. Naamini anaweza kutuokoa kutoka miaka 21 ya majanga ambayo tumekuwa tukiishi nayo. Chukueni wakati kumsoma na dira yake kuhusu Somalia.

  • علي جبريل الكتبي
    July 16, 2012 @ 12:45:21PM

    Sheikh Sharif anaweza kushinda urais kwa sababu ya msimamo wake wa kati; anajenga daraja baina ya Wanaharakati wa Kiislamu na Wasekula. Wagombea wengine hawana fursa hii.

  • xaynuuf
    July 15, 2012 @ 08:40:21AM

    Uchambuzi huu ni mzuri sana, lakini kwa njia iliyowekwa katika maandishi ni aibu tu. Habari ingepaswa kuwekwa wazi. Asante sana.

  • zeytun mohamed
    July 14, 2012 @ 02:51:54PM

    Somalia imekuwa uwanja wa vita kwa zaidi ya miaka 20. Ninapendekeza kwa Sheikh Sharif kuachia ngazi yeye na wenzake ili kufanyika uchaguzi safi na angerahisisha upokezanaji wa utawala na uongozi kwa njia ya amani ili kuwaruhusu wananchi kushiriki na kuunga mkono mchakato wa wazi wa kidemokrasia. Hilo litaimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa. Ikiwa mchakato huu utakuwa wa amani ndipo tutakuwa tumerejesha imani kwa Wasomali walioko uhamishoni ili waweze kurejea nyumbani na kuanza mchakato wa ujenzi mpya na maendeleo ya taifa.

  • Ahmed
    July 13, 2012 @ 04:59:34AM

    Mchakato wa wagombea wengi kuliko uchaguzi wa raisi uliopita wa mwaka 2004 kutokana na teknolojia ya kisasa inayotawaliwa na intaneti ambayo wagombea wanawavutia watu wao kwa kampeni za uchaguzi wa rais mpya tarehe 20 Agosti mjini Mogadishu. Wagombea hao miongoni mwao ni rais wa sasa Ahmed na waziri wake mkuu pamoja na spika wa bunge Sharif Sakiin na wanataka kurejea ofisini kwa kipindi cha pili. Somalia inakaribia enzi mpya baada ya miaka 21 ya migogoro, vita vya wenyewe kwa wenyewe, njaa, ukame pamoja na itikadi mpya ya ugaidi ambayo kabla haikuwa maarufu kwa watu wa Somalia na kupelekea kuundwa kwa kikundi kinachoitwa al-Shabaab ambao katika miezi ya hivi karibuni kilijiunga na al-Qaeda kama ilivyoelezwa wazi na vyombo vya habari.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo