Julai 11, 2012
Viongozi wa ngazi za juu wa al-Shabaab pamoja na wanachama wa kawaida walio kwenye milima ya Galgala wanajiengua kutoka kundi hilo kwa kasi, kwa mujibu wa Msaidizi Mkuu wa Polisi wa Puntland, Luteni Jenerali Muhidin Ahmed Muse.
Muse alikataa kutaja ni wanachama wangapi wa al-Shabaab waliokwishakulisaliti kundi hilo hadi sasa, lakini alisema tayari polisi imeshawaonesha hadharani baadhi ya wale ambao wako kizuizini na itawatangaza hivi karibuni.
Katika miezi ya karibuni, baadhi yamapigano yamekuwa yakitokea huko kati ya wanajeshi wa Puntland na wapiganaj wa al-Shabaabkatika milima ya Galgala, umbali wa kilomita 60 kusini magharibi ya Bosaso.
Katika mahojiano na Sabahi, Muse alisema kwamba serikali inafanya kila jitihada kuleta amani katika mkoa huo na itaendelea kufanya kazi ya kufikia utulivu wa Puntland.
Sabahi:Kwa nini unaamini kuwa watu hawa sasa wanahatarisha maisha yao na kujiengua na al-Shabaab?
Luteni Jenerali Muhidin Ahmed Muse:Sababu ya msingi iliyopelekea uasi huo wa wanachama wa al-Shabaab dhidi ya kundi lao ni msamaha wa Rais Abdirahman Mohamud Farole wa Puntland alioutoa kwa mtu yeyote anayetaka kuachana na al-Shabaab. Wamekuwa wakihakikishiwa kwamba hawatabebeshwa dhamana ya kitu chochote kama watajisalimisha.
Sababu nyingine mbali ya hiyo ni kwamba vijana hawa [wa al-Shabaab] wameng'amua kwamba walikuwa wakimezeshwa uongo katika mafunzo waliyokuwa wakipewa. Wamefahamu sasa kwamba hakuna uhalali wa kidini, kwamba watu wanauliwa ovyoovyo na kuchinjwa kwa makusudi. Wameona watu wakiuawa wakati wakitoka misikitini na sasa vijana hao wana uelewa wao wenyewe.
Tumegunduwa kwamba sio tu kwamba wanakuja kwetu [viongozi wa Puntland], bali wengine wanapanga hata kuwatoroka [al-Shabaab] kujiunga na familia zao, wengine wanakwenda kwingine.
Sabahi:Kuna mipango yoyote kwa wapiganaji hao waliojiengua mara tu wakiwa mikononi mwenu?
Muse:Mpango wa serikali ni kwamba yeyote anayejiengua na kundi hilo na akawa tayari kujiunga na jeshi atakaribishwa jeshini. Yeyote anayetaka kufanya kazi mwenyewe, au anayetaka kusafiri pia yuko huru kufanya hivyo. Hakuna atakayelazimishwa kwa lolote lile.
Kuna uvumi mkubwa kwamba yeyote anayetoka makabila ya nje ya Puntland ataua [mara akikamatwa], na huo ni uzushi usio mashiko. Watu wengi ambao hawatoki kwenye eneo hili wameomba msamaha, wapo hapa na wamesalimisha silaha zao. Yeyote [awe wa asili ya kabila lolote] anaweza kujitokeza. [Wakijiengua tu na kundi hilo] watachukuliwa kwenye sehemu maalum au eneo watakalochagua wenyewe.
Sabahi:Kuna kivutio cha fedha munachokitumia kuwavuta wapiganaji wanaojiengua?
Muse:Kuna ukweli fulani katika hilo - yeyote anayejileta mwenyewe na kusalimisha silaha yake atafidiwa. Wale wanaohitaji kusafiri (kurudi kwenye maeneo yao ya asili) watasaidiwa na watashughulikiwa. Tutatoa huduma bora kabisa tunayoweza kwa wale wanaochagua kujiengua na kundi hilo.
Tunawatolea wito wale wanaume ambao wamepewa mafunzo ya kupigana kwa kupotoshwa lakini wanaendelea kusalia nyuma, kwamba bado wanayo nafasi na wanastahiki kupokea msamaha wa rais. Hawatashitakiwa mara tu watakapoachana na al-Shabaab. Kile wanachopaswa kufanya ni kuwajulisha maafisa wetu wa usalama tu, ili watayarishe kuwasindikiza kutoka maeneo husika na kuwahakikishia usalama wao.
Sabahi:Wangapi wameshajiengua na kundi la al-Shabaab hadi sasa?
Muse:Kuna wengi ambao wamejitokeza, lakini sitakutajia idadi kamili kwa sasa. Kuna majina ambayo bado hatujayatambua wakiwemo maafisa wa ngazi za juu wa al-Shabaab. Mungu akipenda, tutayaweka majina hayo hadharani muda utakapokuwa muafaka kufanya hivyo.
Sabahi:Kuna uvumi kwamba wapiganaji hao waliojiengua na al-Shabaab wanatumia msamaha huo wa rais kama njama ya kusababisha madhara. Unasemaje kuhusiana na hilo?
Muse:Huo ni uongo. Wapiganaji vijana wanaikimbia al-Shabaab kwa wingi, hapa Puntland na pia katika maeneo mengine ya nchi kwa sababu wamefunuliwa na ukweli sasa. Tuna maafisa wa usalama waliofunzwa kuwafuatilia, na hatuna shaka [ya kupangwa njama yoyote].
Sabahi: Munawafikiaje wapiganaji waliojiengua?
Muse: Tuna timu ambayo ina dhamana ya operesheni hii tu. Baadhi ya vijana walioasi wanatusaidia, bado wanawasiliana na baadhi ya marafiki zao ambao bado wamejificha na wanatusaidia katika jitihada za uratibu. Wanatuhusisha kila wakati juu ya pale mambo yalipo, [kama vile] wangapi wako tayari kuja na vipi wanaweza kufikishwa.
Sabahi: Mtachukua hatua gani baada ya hapa?
Muse:Tuna matarajio kwamba tutapata ushindi mkubwa dhidi ya [al-Shabaab].
Ama kwa watu tunaowachukua, wana sehemu ya kuwapokea. Umma na jeshi wako tayari kuwapokea. Tunawakaribisha hata wale wanaopenda kuondoka, na tutachukua hatua za haraka dhidi ya wale wanaobakia.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Hatuwezi kudanganywa na taarifa kama hizo za uongo kwa vile sisi si wageni kwa yale yanayofanyika nchini. Ninawahakikishia nyote kuwa karibuni mtasikia kitu ambacho kitawahangaisha wanafiki na kuwafanya Waislamu wafurahi.
Hizi ni habari za jukwaa zilizopangwa na hakuna mpiganaji wa al-Shabaab aliyejisalimisha. Puntland inajidai kucheza na vyombo vya habari kwa kuzungumzia kuhusu matatizo ili ipatie fedha. Ni waroho na wanapaswa kuacha kujipinga wenyewe.
Mchezo umekwisha kwa al-Shabaab na mataifa ya kweli ya Kiislamu ya Somalia, Somaliland na nchi zingine zinazofanana.
Viongozi wa jamii ya Kiislamu wanapaswa kurudufu jitihadi zao ili kuhakikisha hawa wenye siasa kali hawawezi kupoteza akili za vijana. Hatua ya kwanza dhidi ya wale wenye siasa kali ni kuwa viongozi wa Kiislamu kujiunga kupambazuka itikadi sahihi ya uislamu. Hakuna mahali palipoandika kuwa dunia inapata amani kwa kuhatarisha maisha ya watu wengine. Kama inawezekana, vikundi hivyo lazima wahakikishe watoto wao wafundishwe katika madrasa zao kuhusu hali njema ya jamii yao, na wanachama fisadi wa ondolewa kutoka kwa uongozi wa jamii.