Makabila ya Kisomali yakataa wito wa al-Shabaab kufadhili vita vyake

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Julai 03, 2012

  • 3 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Viongozi wa makabila ya Somalia na maafisa wameulaani wito wa karibuni wa al-Shabaab wa kuyataka makabila kujiunga na vita vya kundi hilo na kugharamikia shughuli zake za kigaidi.

  • Wakiwa wamepungukiwa na fedha, wapiganaji wa al-Shabaab wamekuwa

    Wakiwa wamepungukiwa na fedha, wapiganaji wa al-Shabaab wamekuwa "wakiwarubuni" raia wa Somalia kugharamikia operesheni zao. Pichani juu, wapiganaji wa al-Shabaab wakisimama kulinda mkutano karibu na Mogadishu mwaka 2009. [Mustafa Abdi/AFP]

"Makabila ya Somalia yameteseka kwa ukatili na vitendo vya kihalifu vya al-Shabaab na sasa makabila yote yamejua vizuri kwamba al-Shabaab ni maadui wao na adui wa amani, maendeleo na ustawi," alisema Mohamed Hassan Haad, kiongozi wa kabila la Hawiye, moja ya makabila na lilitopakaa sana katika maeneo ya kati ya Somalia.

"Makabila hayo pia yametambua kuwa al-Shabaab wamekuwa kikwazo wa watu wa Somalia, na ndio maana makabila ya Kisomali hayawezi kuwa washirika wa kundi hili au kukubali wito kutoka viongozi wake," alisema.

Hapo Juni 18, kiongozi wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane, ajulikanaye pia kama Mukhtar Abu Zubair, aliyataka makabila ya Kisomali kujiunga na kile alichokiita Jihadi. Baadaye, hapo tarehe 23 Juni, kiongozi wa al-Shabaab katika mkoa wa Shabelle ya Kati, Yusuf Sheikh Isse, anayefahamika pia kama Kaba-kutukade, aliwataka viongozi wa makabila ya Kisomali na wafanyabiashara kuchangia uwezo wa kujilinda na juhudi zake za kuyalinda maeneo yaliyo kwenye udhibiti wake.

Haad aliiambia Sabahi kwamba wito wa viongozi wa al-Shabaab kuunga mkono na kufadhili harakati zao za kijeshi si kitu kipya. "Tunayataka makabila ya Somalia kutokutoa aina yoyote ya msaada kwa makundi yenye misimamo mikali yaliyokataa amani," alisema. "Kinyume chake, tunayahamiza makabila hayo kupigana dhidi ya al-Shabaab."

Kiongozi wa kikabila, Sultan Mohammed Saeed, pia aliwataka wananchi kusimama dhidi ya kundi hilo lenye mafungamano na al-Qaeda.

"Tunawataka raia wanaoishi kwenye maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa waasi kuanza wimbi la upinzani na kukataa matendo ya kikatili ya kundi hilo la siasa kali," aliiambia Sabahi.

"Tunayahimiza makabila haya kuanzisha mapinduzi dhidi ya al-Shabaab, wakifuata mfano wa mapinduzi katika nchi za Kiarabu. Tuna hakika kwamba makabila haya yanaweza kuliondosha kundi la siasa kali la al-Shabaab kwenye maeneo yao, ikiwa wana nia ya kweli na madhubuti ya kufanya hivyo," alisema.

Saaed alisema makabila yanaweza kutekeleza jukumu muhimu katika vita dhidi ya al-Shabaab kwa kuisaidia serikali kuwafurusha wanachama wake katika maeneo yao na kupenyeza taarifa kwa vyombo vya usalama kuhusiana na harakati za kundi hilo.

Al-Shabaab wawabughudhi wenyeji

Hussein Mohamud Osoble, kamanda wa wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wa Ahlu Sunna wal Jamaa, alisema al-Shabaab daima "imekuwa ikiwaghilibu na kuwafanyia matendo ya kigaidi wananchi".

"Wamekuwa wakitoza kodi kubwa kwa makabila yanayoishi kwenye maeneo wanayoyadhibiti katika mkoa wa kati wa Galgadud," alisema. "Wanamgambo wameweka faini kwa koo na wenyeji kuanzia dola za Kimarekani 6,000 hadi 9,000 kwa mujibu wa ukubwa wa ukoo, katika sehemu ya mashariki ya mkoa wa Galgadud, kwa lengo la kugharamikia shughuli zao za kigaidi."

Osoble alisema wenyeji hawana hiari ila kulipa fedha hizo kwa kuhofia matokeo mabaya.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Abdiqadir Muse, anasema al-Shabaab inayatoka kodi makabila kwa sababu vyanzo vyao vya kifedha vimekauka kutokana na kupoteza udhibiti wa miji na maeneo muhimu yaliyolipatia mapato kundi hilo.

"Kwa kuwa al-Shabaab imepoteza maeneo na miji mingi muhimu kwa miezi michache ya hivi karibuni, kundi hilo liko kwenye hali ngumu na haliwezi kuwalipa wapiganaji wake kwa sababu ya upungufu wa fedha," Muse aliiambia Sabahi.

"Kwa kuanza kukauka kwa vyanzo vyake vya fedha, kundi hilo limeanza kutumia njia ya kutoza kodi na faini kubwa kwa makabila.

Kuutafsiri vibaya Uislamu kuhalalisha wizi

Mbunge Mohamed Omar Gedi alisema al-Shabaab imeanza kuiba mifugo kutoka kwa wananchi huko Juba kwa kisingizio cha Zakkat.

"Wanamgambo hao wa siasa kali huiuza mifugo sokoni kwa kugharamikia mashambulizi yao ya kigaidi dhidi ya watu wa Somalia," alisema. "Tabia hii ni ushahidi wa wazi kwamba matendo ya wanamgambo hao wa siasa kali hayana uhusiano na Uislamu kwa sababu Uislamu unakataza kuiba mifugo kutoka kwa watu masikini na kutumia fedha kugharamikia vita dhidi ya watu."

Gedi alisema al-Shabaab yametumia njia nyingine kadhaa kugharamikia shughuli zake za kigaidi, kama vile kuteka nyara wageni kwa ajili ya kupata fedha za kikomboleo na kushirikiana na maharamia wa Kisomali.

Sheikh Ahmed Dhiisow, anayeongoza Baraza la Maulamaa la Somalia, alisema al-Shabaab haina madaraka ya kidini ya kukusanya Zakkat. Alisema al-Shabaab inautafsiri vibaya Uislamu na ni waasi wa kiitikadi, na ndio sababu wanachama wake wamekuwa wakijivunia kutangaza kwamba wao ni tapo la al-Qaeda nchini Somalia.

"Kile kinachofanya al-Shabaab nchini Somalia hakiweza kuitwa Jihadi. Dhana ya Jihadi ni kuwapa nguvu wanyonge, kuwalinda Waislamu na kueneza Uislamu - sio kuwadhalilisha Waislamu na kuwalipua kwa mabomu watu wasiokuwa na hatia," Dhiisow aliiambia Sabahi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 24)

Dislike_icon(7)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Osman Xaaji
    August 17, 2012 @ 09:46:04PM

    Ugaidi unaonesha tabia ya watu wanaoabudu shetani na kuumwa wendawazimu, na hii ndio sababu moja inayoongoza kwa umuhimu wa mashirikiano katika kushughulikia ugaidi na aina zake zingine. Kwa sababu hii, umuhimu wa mazungumzo ya kidini katika jamii ili kuwaamsha watu kutokana na hatari za ugaidi na kuushughulikia kiakili. Suluhisho sio kupambana na ugaidi katika uwanja wa vita tu, bali pia kufanya juhudi za pamoja kwa jamii nzima rasmi na vyombo vya habari ili kufikia fikra potofu na kuonesha na kutambua uongo kwa vizazi. Aina nyingi za ugaidi zinatupelekea kupambana nao kwa nguvu sana, kwa kina na uaminifu bila ya kupumua au unafiki.

  • jeremiah jeremy
    July 6, 2012 @ 06:48:03AM

    Tuwang'oe al-Shabaab moja kwa moja.

  • kenn mutuma
    July 4, 2012 @ 04:45:45AM

    Hali inapwaya.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo