Kushindwa kwa al-Shabaab kwarejesha usalama huko Hiran, Bay na Bakool

Na Adnan Hussein, Mogadishu

Julai 03, 2012

  • 26 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Hali ya kawaida imerejea katika majimbo ya Hiran, Bay na Bakool baada ya vikosi vya Somalia na washirika wake kuwasafisha al-Shabaab kutoka maeneo hayo miezi ya karibuni.

  • Duka la wakazi katika soko huko Beledweyne inayojitawaliwa badala kuwa chini ya udhibiti wa al-Shabaab. [Na Adnan Hussein/Sabahi]

    Duka la wakazi katika soko huko Beledweyne inayojitawaliwa badala kuwa chini ya udhibiti wa al-Shabaab. [Na Adnan Hussein/Sabahi]

  • Wakazi wakizungumza nje ya jengo lililojaa matundu ya risasi huko Beledweyne. [Adnan Hussein/Sabahi]

    Wakazi wakizungumza nje ya jengo lililojaa matundu ya risasi huko Beledweyne. [Adnan Hussein/Sabahi]

Gavana wa Hiran Abdifatah Hassan Afrah alisema jeshi limeondoshwa katika mitaa ya Beledweyne, na watu sasa wanaweza kwenda kazini bila ya woga wa vurugu.

Afrah aliiambia Sabahi kuwa wafanyabiashara wanaona ongezeko kubwa la wateja na mauzo mpaka saa nyingi jioni. Alisema mzunguko wa watu baina ya miji jirani umekuwa ukiongezeka, na migahawa mipya imefunguliwa mjini kote.

Alisema shughuli za biashara na elimu zilisita wakati wa udhibiti wa al-Shabaab, kwa vile kikundi hicho kililazimisha kodi zisizo za haki na kuwalazimisha wakaazi kujiunga na safu zao.

"Milango yetu sasa iko wazi na biashara inaendelea kama kawaida," alisema mfanyabiashara mwenyeji Nur Dhaqane. "Tunatarajia kuanza upya kutokana na hali ya wasiwasi na ukosefu wa usalama tuliyoishi nayo kwa muda wa miaka mitatu ya utawala wa siasa kali wa al-Shabaab."

"Waliwataka wenyeji kususuia nguo zilizoagizwa kutoka nje tulizokuwa tunauza kwenye duka letu. Mauzo yalipungua na karibu kila kitu kusimama wakati wa udhibiti wao. Lakini sasa, watu wengi wanakuja kuuliza mitindo ya mwisho iliyoingia, hasa linapokuja suala la nguo za wanawake, vifuasi na viatu," aliiambia Sabahi.

Vikosi vya Somali na Ethiopia viliukamata Beledweyne mwezi Disemba 2011 baada ya kuwafukuza waasi nje ya Matabaan, Mahaas ana vijiji jirani. Mwezi Juni, askari 100 wa Djibouti walifika Beledweyne, kuungana na vikosi vya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).

Al-Shabaab bado wanashikilia maeneo mengine ya Hiran, kama vile miji ya Buulobarde, Jalalaqsi na Buqda.

Hashi Malin, mwendesha shule binafsi wa zamani huko Beledweyne, alisema wanafunzi wanarejea shule baada ya wengi kwishakimbia kutoka mjini hapo kwa kuogopa kulazimishwa kupigana kwa ajili ya al-Shabaab.

"Mkutano wa wanafunzi ulitawaliwa na huzuni, kwa vile walipoteza wapendwa wao waliouawa kutokana na vita na utupianaji risasi," alisema. "Pia kulikuwa na hisia za furaha kutokana na watu kuonana tena baada ya muda mrefu. "Machungu waliyoachiwa ni kumbukumbu ya pamoja ambayo haiwezi kufutwa kwenye akili zao."

Mwanafunzi Ali Mohammed Wasighi alisema, "nilirejea shuleni kwangu, Mujama Um al-Qura huko Beledweyne, miezi minne iliyopita mimi na wanafunzi wenzangu ili kuendelea na masomo yetu. Maisha yangu yamerejea kuwa ya kawaida, baada ya dhiki nyingi kutokana na vita vinavyochosha, na wengine kama mimi ambao tulilazimika kuchukua silaha na kuingia vitani. Tulikuwa hatuna mtu wa kutuangalia wala kutushughulikia. Wengine waliuliwa, wakati wengine walijeruhiwa na mustakbali wao bado haujulikani."

Hudur yarejea katika hali ya kawaida

Isaac Yarow Mohammed, mzee wa kikabila wa Hudur katika jimbo la Bakool, alisema mji taratibu unarejea katika maisha baada ya vikosi vya Somali na Ethopia kumaliza udhibiti wa miaka mitatu wa al-Shabaab katika eneo hili.

"Tuna mahitaji makubwa sana ya kazi na tunataka kufunga ukurasa huu wa vita," aliiambia Sabahi. "Tunahitaji kuendelea na ujenzi mpya na tungependa serikali ya mpito kugharamia miradi zaidi ya maendeleo ili kuwaokoa vijana na tatizo la ukosefu wa ajira na ugaidi, wakati tunafufua uchumi."

Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitatu, zahanati inayoendeshwa na Shirika la Afya Duniani, (WHO) imefunguliwa mjini, ikishughulikia vipimo na kutoa maelezo ya matibabu.

Dk. Omar Salah, mratibu wa WHO kwa misaada ya dharura, aliiambia Sabahi kuwa kituo kinapokea wagonjwa kati ya 100 na 150 kwa siku. katika miezi miwili iliyopita, maelezo ya matibabu 34,000 yametolewa kwa wagonjwa, alisema.

Kamishna wa mji wa Hudur Mohamed Mualim alisema WHO imetoa maabara ya tiba bure ili kusaida maelezo ya madawa yanayohitajika na tiba.

Mualim aliyaomba mashirika ya Somalia na ya kimataifa kurejea kusaidia kuimarisha hali za kibinadamu. Aliiambia Sabahi kuwa kuna baadhi ya msaada ya kibinadamu inakuja katika jimbo la Bakool, wanawake wengi na watoto wamedhoofika kwa njaa, magonjwa na utapiamlo.

Hospitali ya Baidoa inakosa dawa, vifaa vya kutosha

Baidoa, mji mkuu wa jimbo la Bay, ulikamatwa na vikosi vya pamoja vya Somali na Ethiopia mwezi Februari. Hapo Aprili, AMISOM ilipeleka askari 100 huko Baidoa, wakiwa ni wa mwanzo kupelekwa nje ya Mogadishu. Katika uwanja wa ndege wa Baidoa, helikopta zinakuja kutoka Mogadishu zikiwa zimewaleta majeshi wa AMISOM, maafisa wa Somali na wajumbe kutoka mashirika ya kimataifa ya afya na misaada.

Hata hivyo, hospitali ya eneo hilo, ina ukosefu wa madawa ya msingi, kwa mujibu wa viongozi wa eneo.

Amin Osman, mjumbe wa kamati ya wakaazi wa Baidoa ambayo inaendesha hospitali hiyo, alisema ukosefu wa dawa umepelekea kuahirisha kazi za upasuaji kwa wagonjwa kadhaa waliojeruhia. Alisema kuna upungufu mkubwa wa mahitaji kama vile dawa za ganzi na ukosefu wa maabara ya tiba ili kupima na kuhifadhi damu.

Osman aliiambia Sabahi kuwa hospitali inayo gari moja pekee ya kubebea wagonjwa ambayo haina vifaa vya msaada wa kwanza.

Mbunge Fawzia Mohamed Sheikh alisema wagonjwa wanaofika hospitali kuu ya Baidoa wanashindwa kupata dawa za kuwatibu. Pia kuna upungufu wa fedha na muundombinu ufaao wa maji taka, alisema, jambo ambalo linasababisha janga la kiafya kwa wagonjwa.

Aliiomba serikali ya mpito na mashirika ya kimataifa kuisaidia hospitali ya Baidoa.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 93)

Dislike_icon(4)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • علي جبريل الكتبي
    July 19, 2012 @ 12:47:05PM

    Ili kujibu maoni ya Um Aish, ninasema: ni aina gani ya usalama ambayo kikundi cha al-Shabaab inaleta, wakati watu wanaoishi katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao wanaishi kwa vitisho na woga?

  • Kareithi Benjamin Mwangi
    July 18, 2012 @ 05:53:36AM

    Huu ni mpito mkubwa uliofanywa nchi Somalia hasa kwa kusikia kuwa wananchi wanathamini kila siku ya kuwepo kwa katika ardhi ya Somalia. Shirika la Afya Duniani lisifiwe kwa wazo lake lakuona Wasomali wanapatiwa matibu ya lazima ili kuwezesha maisha katika nchi yao. Asante kwa serikali zote ambazo zinahusika huu kufanyika kwa mpito huu.

  • Mmmaa
    July 17, 2012 @ 05:37:25AM

    Asanteni kwa habari za karibuni. Ni ishara tu ya siku njema na Mungu yuko upande wa Wasomali. Karibuni watafurahia kuwepo katika dunia hii kama wengine.

  • Geoffrey Chege
    July 16, 2012 @ 07:27:05AM

    Wakati inaporipotiwa kuwa hali ya kawaida inarejea Somalia, huo ni muziki masikioni mwa Wakenya kwa vile tunahusika katika vita ambavyo havikutarajiwa kuwa vyetu. Tunaishi katika woga wa mashambulizi ya kigaidi na wenzetu wamekuwa wakiuliwa kwa sababu ambazo hawawezi kuzielezea. Kwa bora amani irejee Somalia na eneo hili lirejee katika hali yake ya kawaida ya maisha. Wavuvi watarejea baharini, na wakulima hawataangalia tena pembeni na maisha yatarejea kuwa ya kawaida kwa sote.

  • Mpenda Amani
    July 16, 2012 @ 07:06:12AM

    Somalia inahitaji amani. Nchi za Afrika zinataka kufanya biashara na watu wa Somalia. Tunahitaji kuona maendeleo katika muongo ujao, maendeleo ambayo yatakuja ikiwa tu amani itadumishwa. Hongera kwa nchi zote zilizopeleka askari wao Somalia kupambana na magaidi!

  • Kinya
    July 16, 2012 @ 06:36:29AM

    Ikiwa kitu fulani ni kizuri....tena kwa nini kuwaweka watu katika woga na vitisho...?? Ikiwa mtu ni ndugu yako, kwa nini akutese, akufanye mkimbizi katika ardhi nyingine? Mara nyingine hutaka niangalie tu na kuona... Maombi yangu yanahusu Kenya na Somalia yote…

  • sailes maine marashi
    July 16, 2012 @ 03:06:36AM

    Ndio, hii ni nzuri lakini ni kweli kwamba UA unaweza kudumisha amani nchini Somalia na kuwadhibiti al-Shabaab kikamilifu?

  • ESOLOM NGARI KARIUKI
    July 16, 2012 @ 01:37:18AM

    Wakazi wengi wa mikoani wanataka kujua dini ya kweli na dhamira yake. Wameona waziwazi mambo ambayo dini zao zinayataka. Kama isingekuwa ni kuwaunga mkono kwao tangu mwanzo, hatua zao za mwanzo zingekuwa ni kuzikimbia na kwa hivyo maisha yangekuwa bora. Hii ni fursa nzuri kuwaambia watu juu ya Mungu wa kweli anayepaswa kuabudiwa. Wangepewa fursa ya kufikiria kwa kina kuhusu dini yao ya Kiislamu na tabia zake. Ninawatakia kila la heri katika maisha. Wale ambao hawana chakula, Bwana wa wageni awajaalie uhai. Mungu akubarikeni ninyi pia.

  • joeliser
    July 15, 2012 @ 08:13:37AM

    Mimi nadhani kujadili imani ya mtu mwengine ni upotoshaji. Waislamu wanapaswa kufahamu kuwa katika sehemu zote za dunia Waislamu ndio wanaosababisha matatizo kwa wengine. Nchi kama Somalia, Nigeria n.k., Waislamu wanawaua Wakristo kwa kuwachomea makanisa. Sijawahi kusikia Mkristo kuchoma msikiti kwa sababu Ukristo unafundisha amani na upendo wakati Uislamu unaelewa kuwa ni imani yake tu iliyo sahihi na kwa kuwaua wasiokuwa Waislamu ataingia “peponi kwao”. Karibu vikundi vyote vya kigaidi vimejielekeza kwenye Waislamu. Tafadhaleni, rejeeni katika akili zenu na muufahamu ukweli. Waislau wengi wanawafundisha watoto wao Kiarabu katika madrasa na kwa hivyo kuwanyima watoto wao kupata elimu ya kawaida. Wakati watoto wao wanaposhindwa kufaulu wanawalaumu Wakristo. Unapochukua mambo mawili kwa wakati mmoja, lazima kimoja utakipoteza.

  • umikaltum ahmed
    July 14, 2012 @ 03:29:29AM

    Mimi ninachotaka ni Somalia tu kuwa na amani… na Mwenyezi Mungu akipenda watapata kila kitu.

  • bs.
    July 12, 2012 @ 10:00:49AM

    Sote ni wamoja katika mtiririko wa dunia na ni bora kwetu sote tusiwe katika vita. Hii ni zawadi kwa dunia ambapo amani inatawala. Kwa wale waliojeruhiwa au kuumizwa na wale waliopoteza wapendwa wao, maombi yetu ya dhati kabisa yako pamoja na nanyi nyote!!!

  • collins
    July 12, 2012 @ 06:33:03AM

    Ni rahisi kutoa kibanzi kutoka jicho la mtu mwingine kuliko lako mwenyewe, kwa vile binadamu, tangu anguko lililorekodiwa katika Mwanzo 3, ana hisia za kufanya uamuzi rahisi wa kutumia vurugu kwa kisingizio cha kujilinda mwenyewe. Kumekuwepo na vita vingi vilivyopiganwa ulimwenguni tangu mwanzo kwa jina la aina fulani ya Mungu. Binadamu wengi wamepoteza maisha yao na mali kuharibiwa. Hii imetokea ulimwenguni kote ila ya kujali fungamano la dini, iwe ni ya Kibudha, Kikristo, Kiislamu, Kihindu n.k. Ni njia gani ya kushughulikia vurugu imemwangusha binadamu? Imani ya Mungu kuwa ni mwenye uwezo wote, anayejua kila kitu, na yuko katika kila mahali katika itikadi za kisasa, ingeweza kutusaidia, na kumsaidia yeye kufanya kazi yake. Wazo sio ni nani yule anayetuchukia, au ni nani adui yetu. Tatizo liko katika kujifikiria wenyewe. "Hebu kila mtu asiangalie maslahi yake binafsi, lakini maslahi ya wengine.” Wafilipi 2:1-4. Vita ni matokeo ya kujaribu kuthibitisha kwa wengine kuwa sisi ndio wakubwa, wakubwa hata kupita Mungu. La pili, masha ya binadamu hayana uhakika hata kidogo. Vitu tunavyopigania vinamaliza, tunavipoteza, hasa baada ya kufa. Hakuna binadamu aliyefanikiwa kuchukua pamoja naye fedha zake, ardhi, nchi, au mali yake katika kaburi, au katika ulimwengu mwengine. Wamisri waliwazika wafalme wao pamoja na watumwa wao. Lakini kila kitu kilikwisha, kikaoza kwenye ardhi. Jambo bora ni “Kila nilichopata na kukihesabu lakini nikakipoteza, kwa utukufu wa ujuzi wa Yesu Kristo,” Filipo 3:7-11. Inaonesha kuwa kazi ya kulipiza kisasi dhidi ya maadui wetu wa kufikirika au wa kweli ni Mungu mwenyewe. Warumi 12:9-

  • falaag
    July 12, 2012 @ 03:53:28AM

    Unakaribishwa sana mjomba.

  • brian
    July 11, 2012 @ 01:50:29PM

    Kadiri mnavyoendelea kupigana ndani ya Somalia, ndivyo Wakenya wengi mtakavyokuwa mnawapoteza.

  • Ahmed Abdallah Albeity
    July 11, 2012 @ 01:06:32AM

    Nimefurahishwa sana na ripoti hizi,ikiwa ni marayangu ya kwanza kupata habari za uhakika kuhusu Somalia.Nawaomba mtupe na habari za Mataifa mengine.Nawakilisha.

  • Ben Kim
    July 10, 2012 @ 07:52:41PM

    Asante Hussein kwa taarifa za kuhabarisha. Kupiga marufuku al-Shabaab nchini Somalia sio suala la Ukristo dhidi ya Uislamu. Watu wanaoishi chini kunyimwa haki zao na kuuliwa ni Waislamu. Watendaji wa maovu haya pia ni Waislamu. Hakuna mtu yeyote atakayekuwa na ujasiri wa kudai uvamizi wa Kikristo au wanawashambulia katika misheni za tena na tena. Ukristo umejengwa kwa Upendo na Utu, kwa sababu hiyo Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote, wawe Wakristo au wasiokuwa Wakristo.

  • Meshaq Shackah
    July 10, 2012 @ 07:00:11AM

    Hongera kwa askari wote waliofanya amani iweko Somaliland.

  • Jeilani
    July 9, 2012 @ 02:12:17AM

    Serikali ya shirikisho kwa kweli imepiga hatua kubwa sana za kuimarisha usalama wa nchi na wamefanya hivi kwa kuwapiga vita al-Shabaab kwa nguvu zote. Serikali inaongeza idadi ya majeshi yao na vikosi vya polisi ili kusaida kuweka amani. Pia imeomba msaada kutoka Umoja wa Afrika na jumuiya ya kimataifa ili kuwagharamia katika silaha na mafunzo muhimu ili waweze kupambana na ugaidi nchini Somalia. Serikali pia imeungana na majeshi ya AMISOM yaliyomo tayari nchini kusaidia kuwasafisha al-Shabaab moja kwa moja. Njia nyingine ambayo serikali inafanya ni kujaribu kuandaa mazungumzo ya maelewano na koo zote zinazogombana na katika juhudi hiyo wataweza kuwaunganisha watu wa Somalia na kuwazuia wasijiunge na al-Shabaab.

  • Jane
    July 8, 2012 @ 09:22:21AM

    Why do muslims always say that they are hated by christians? Are they happy when thugs go killing in the name of their God. Allah s a strong God and needs no one to fight for him. Now that somalia is getting peaceful all the somalis should go back to their country and leave us alone. And for those youths who were recruited by alshabaab ,and now they claim they are back to kenya and want to settle down should be prosecuted accordingly because they did not inform anyone when they left to join the alshabaab.now that they want to be accepted as harmless citizens back in kenya they come pretending to be good citizens.kikulacho ki nguoni mwako.

  • DENNIS AWANDU
    July 7, 2012 @ 01:19:12PM

    Mnafanya vizuri KDF. Tunajivunieni nyinyi. Kituo kinachofuata ni Kisiwa cha Migingo.

  • Norbert Okumu
    July 7, 2012 @ 06:36:13AM

    Toreza Mussa, unabweka kwa mti usiohusika. Ukristo wa kweli unahubiri kuwa kuna Muungu mmoja, Jina lake ni Bwana Yesu Kristo. Mungu huyu ana kazi nyingi, kama vile kazi yake kama Babab; kwa maana ya kuwa Muumbaji wa kila kitu. Kazi yake kama Mwana. Hii ni pale alipochukua umbo la binadamu na kuja na kufa kwa ajili ya binadamu – kumbuka kuwa mwili unaweza kufa lakini Yule ambaye anayeishi katika mwili huo, Roho ya kudumu haiwezi kufa – Mungu yule mkubwa aliyeishi katika mwili hawezi kufa. Unayo Roho inayoishi mwilini mwako, wakati mwili wako unapokufa Roho haifi, inasubiri hukumu ya Roho Mkuu anayeitwa Bwana Yesu Kristo ambaye ana uwezo wa kuua ikiwa atagundua una madhambi. Tena, Mungu huyu mkubwa ana kazi ya Roho Mtakatifu, anayekuja kuishi ndani ya waumini, kwa hivyo inakuwa sio waumini tena wanaofanya kazi yao, bali yule Roho mkuu anayeishi ndani yako. Ili kufahamu ninachosema, mfano ni kwa mtu aliye na majukumu mengi; kwa mfano, Rais wa nchi anaweza kuwa Mbunge na pia Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya nchi husika, hilo linamfanya yeye kuwa ni watu watatu? HAPANA, ni mtu yule yule lakini mwenye majukumu tofauti.

  • علي جبريل الكتبي
    July 5, 2012 @ 03:09:10PM

    Hakuna shaka kuwa wakati eneo lolote la Somalia linapokombolewa kutoka kwa al-Shabaab, maisha yatarejea kuwa ya kawaida. Na hiyo ndio sababu kwa nini tunapaswa kuikomboa Somalia yote kutoka makucha ya al-Shabaab. Kwa matumaini makubwa, juhudi za kimataifa zinazokusudia kujenga nchi kamili ya Somalia, zitafanikiwa kwa sababu al-Shabaab wanatumia ombwe la usalama nchini, kwa hivyo jumuiya ya kimataifa ikiwakilishwa na Marekani na Uingereza, zinapaswa kuiunga mkono serikali inayokuja ya Somalia. Na nchi jirani, kama vile Ethiopia na Kenya, zinapaswa pia kuisaidia Somalia ili kuanzisha taifa lao kuondokana na sera zao kongwe za kuiogopa Somalia inapokuwa imara. Serikali imara ya Somalia itahakikisha usalama wa nchi jirani.

  • toreza mussa
    July 5, 2012 @ 11:30:00AM

    Ninataka kusema kuwa Waislamu ulimwenguni wanachukiwa na wasiokuwa Waislamu kutokana na ukweli kwamba wana imani ya kweli kuliko dini nyingine za ulimwengu. Maoni haya yanaonesha kuwa siku zote ukweli unauma kwa waongo. Kwa hivyo mitume wote wa Mungu walichukiwa na wale wasiokuwa Waislamu na sio sababu wanajidai kuwa Waislamu ni wabaya sana ili kila mtu awachukie. Waacheni, kuna njia moja sahihi ya maisha kuelekea peponi, Wachukulie wale wanaoamini utatu kuwa 1+1+1= 1. Hii ni falsafa ya kuleta elimu kwa yule ambaye akili yake imelela na hana fikra katika njia ya sasa ya maisha kuwa Mungu aliyeumba ulimwengu hawezi kufa. Kwa hivyo mfuateni Mungu wa kweli.

  • benjamin munyao
    July 5, 2012 @ 07:24:23AM

    Vikosi vya jeshi lazima viwe makini zaidi.

  • David O
    July 5, 2012 @ 06:12:42AM

    Hii ni kwa ajili ya Sabahi na waandishi wake wa habari. Hongereni kwa kuufahamisha ulimwengu juu ya Somalia na ninawahamasisha kuendelea kuripoti katika mazingira magumu. Endeleeni kutoa habari - mnathaminiwa!

  • أم عائشة
    July 5, 2012 @ 02:17:18AM

    Al-Shabaab ni moja wao ambaye ataleta utulivu na usalama. Ama kuhusu wahalifu na makafiri waliotuchukulia pesa zetu na kuua watoto wetu, Mungu atawashinda!

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo