Kenya yashutumu al-Shabaab kwa mashambulio ya makanisa, yaapa kuongeza usalama

Na mfanyakazi wa Sabahi

Julai 02, 2012

  • 5 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kenya haitaondoa majeshi nchini Somalia mpaka usalama utakaporejea, Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga alisema Jumatatu (tarehe 2 Julai) siku moja baada ya watu 17 kufariki katika shambulio la hatari mno ambalo Kenya imeshuhudia kwa mwongo huu.

  • Mwathirika wa shambulio la kombora la tarehe 1 Julai katika makanisa mawili huko Garissa alisukumwa katika kiti cha wagonjwa kuingia kwenye gari la wagonjwa baada ya kusafirishwa kwa ndege kwenda Nairobi kwa matibabu. [Tony Karumba/AFP]

    Mwathirika wa shambulio la kombora la tarehe 1 Julai katika makanisa mawili huko Garissa alisukumwa katika kiti cha wagonjwa kuingia kwenye gari la wagonjwa baada ya kusafirishwa kwa ndege kwenda Nairobi kwa matibabu. [Tony Karumba/AFP]

Akizungumza akiwa Garissa, ambako watu waliovalia barakoa Jumapili walirusha makombora katika makanisa mawili kabla ya kurusha risasi katika mkusanyiko huo, Odinga alitoa ujumbe wa ukali kwa harakati za al-Shabaab walio shirika na al-Qaeda, ambapo aliilaumu kwa shambulio hilo.

Kujisalimisha siyo uchaguzi kwetu, kwa sababu iwapo tutaiacha Somalia, utawala huria utapelekwa ambapo utagawanya mipaka, kwa mujibu wa AFP.

"Kenya itasimama kwa umoja hata kama al-Shabaab watafanya vitendo vya kukatisha tamaa.... al-Shabaab wanapinga maendeleo yanayofanywa na vikosi vyetu nchini Somalia," alisema. " Tutasimama kwa umoja na kwa ushirikiano."

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limeweka idadi ya vifo vya shambulio la Jumapili kuwa 17 na kusema si chini ya watu 40 walijeruhiwa, wakiwemo watu saba ambao bado hali zao ni mbaya. Watatu kati ya waliojeruhiwa vibaya wamesafirishwa kwa ndege jijini Nairobi kwa matibabu.

Watoto watatu wameripotiwa kuwa miongoni mwa waliokufa.

Al-Shabaab hawajadai kuhusika na shambulio hilo, ingawaje tovuti ya Al-Kataib ya Twitter inayounga mkono al-Shabaab ilisifu operesheni yenye mafanikio huko Garissa.

Mkuu wa Jimbo James Ole Serian alisema polisi wa Kemya waliahidi kuimarisha usalama katika jimbo la kaskazini Mashariki kufuatia shambulio hilo.

Operesheni za usalama zimeanzishwa huko Garissa, Wajir na Mandera, na mkutano kati ya viongozi wa ndani huko Garissa umepangwa kufanyika wiki ijayo, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti Jumapili.

Serian alituliza hofu ya wakazi ya mashambulio ya baadaye. " Mji huu ni tulivu na hakuna mashaka," alisema usiku wa Jumapili.

Msemaji wa polisi Eric Kiraithe alisema polisi walikuwa wakipanga Jumatatu operesheni kubwa ya usalama kuwakamata wakosaji na kudai silaha zilizotumika, ambazo watu wenye silaha waliziiba kutoka kwa maofisa usalama katika makanisa baada ya kuwaua.

Usalama makanisani huko Mombasa utaongezeka pia, pamoja na waumini kukaguliwa kabla ya kuingia makanisani, Ofisa wa Jimbo la Pwani Aggrey Adoli aliliambia gazeti la The Standard la Kenya siku ya Jumapili. .

"Tumewasambaza maofisa wa usalama makanisani, hususani siku ya Jumapili, na hakutakuwa na sababu ya kuogopa," alisema.

Vatican wameyaita mashambulio "ya kutisha na yanayotia wasiwasi".

"Woga wa vurugu dhidi ya watu wasiokuwa na msaada wanaokutana kwa amani kwa ajili ya maombi hauzungumziki," msemaji Federico Lombardi aliiambia Redio Vatican.

Waislamu maarufu nchini Kenya pia zimeshutumiwa kwa mashambulio hayo, na zimeitwa mbele ya sheria haraka kwa ajili ya uhalifu.

"Mahali popote pa ibada panatakiwa kuheshimiwa na watu wote," alisema mwenyekiti wa Baraza la Juu la Waislamu la Kenya Abdulghafur El-Busaidy, haya yalielezwa katika gazeti la The Standard la Kenya. "Uislamu na Waislamu wasijihusishe na matukio hayo ya uhalifu na mawakala wa usalama wa nchi zinazohusika wanalazimika kwenda kwa kasi kuwakamata wahalifu."

Mkurugenzi mkuu wa Umoja wa Mashirika ya Kiislamu nchini Kenya Fazul Mohamed pia amekana mashambulio hayo, ambayo alisema yanadhihirisha ukosefu wa maadili wa wahalifu.

"Kama itatokea kwamba waumini wa Kiislamu wamefanya mashambulio hayo, watapaswa kuchukuliwa kama wahalifu na sio [kama] Waislamu," alisema. "Uhalifu ni uhalifu tu. Uislamu haufundishi mtu yeyote kuua wananchi wasiokuwa na hatia."

Mohamed alitoa wito kwa viongozi wa dini kuzungumza dhidi ya mashambulizi ya magaidi na kuwalinda vijana kujiingiza katika makundi ambayo yanakimbilia katika ugaidi na vurugu.

"Tunapaswa kuwalinda vijana wetu dhidi ya kuingizwa katika makundi ambayo yanabadilisha mafundisho ya dini na kufanya vitendo vya uhalifu," alisema. "Hilo linasaidia tu kueneza jina zuri la dini."

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 9)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • haybe yare
    July 4, 2012 @ 10:15:00AM

    Nitatoa mawazo yangu ambapo mimi siungi mkono mabomu ya kujitoa muhanga kwa sababu yoyote ile.

  • Diana G. Keneth
    July 4, 2012 @ 03:29:32AM

    Ninathamini juhudi zinazofanywa za kuanzisha operesehni za usalama katika miji iliyotajwa na usalama katika makanisa. Hata hivyo, ni bora kuanzisha operesheni za usalama kila pahali, kila wakati. Tusizingatie hoja zetu kuhusu dini kwa sababu washambulizi wanaweza kulenga kikundi chochote cha watu. Nadhani tungepaswa kuungana kama wananchi na kufanyakazi pamoja kama timu ili kuhakikisha upatanifu na usalama nchini mwetu. Pamoja na hayo, makala ni nzuri na inatia matumaini kwa sababu wasemaji kadhaa wanaweka maneno yao.

  • wilson
    July 3, 2012 @ 04:37:59PM

    Ninataka kuihamasisha tu serikali ya Kenya kupeleka maofisa wengi zaidi wa polisi kadri iwezavyo mipakani, ili wahalifu waasiweze kutoka ndani ya Kenya.

  • snichchisky
    July 3, 2012 @ 10:05:18AM

    Ninasikitika kwa serikali ya Kenya. Mwenyezi Mungu alete amani miongoni mwa mataifa yanayopakana na Kenya.

  • snichchisky
    July 3, 2012 @ 09:57:31AM

    Kuna uwezekano kuwa shambulio hilo lilifanywa na al-Shabaab pengine wakati wakijaribu kujipenyeza nchini.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo