Juni 29, 2012
Vikosi vya usalama katika uwanja wa ndege wa Berbera, Somaliland, mapema wiki hii viliwaokoa wasichana waliokuwa wakisafirishwa kwa njia haramu.
Wasichana hao wote wakiwa kati ya miaka minane na 11 walitolewa eneo la kusini ya Somalia, kama alivyosema meneja wa uwanja huo wa ndege, Omar Abdullahi Aden, kuiambia Sabahi.
Alisema watoto hao walikuwa wakisindikizwa na wanaume wawili watu wazima, waliodai kuwa mtu mwingine ndiye aliyewakabidhisha kwao katika wilaya ya Walla Weyn kwenye mkoa wa Lower Shabelle.
Wasafirihaji hao wawili wa binaadamu waliwaambia maafisa kwamba mtu mmoja aliwalipa kuwapeleka watoto hao kwa mtu mwingine aliye mjini Hargeisa, alisema Aden. “Watu hao wawili na wasichana hao walikuwa wakisafiri na ndege ya African Express ambayo waliipandia mjini Mogadishu. Watoto walionekana kama hawajui walikokuwa wakipelekwa na kwamba walikuwa wakisafirishwa kwa nguvu.”
Wasichana wote walikuwa wanaongea lahaja ya Kimai inayozungumzwa katika baadhi ya sehemu za kusini ya Somalia, alisema.
Aden alisema maafisa wa usalama waliwaweka ndani watu hao wawili na kuwakabidhisha wao na wasichana wote 12 kwa polisi wa uhamiaji wa Somaliland. Kwa sasa vikosi vya usalama vya Somaliland vinamtafuta mtu anayeshukiwa kuwasubiri wasichana hao mjini Hargeisa.
“Ni operesheni iliyopangwa vyema kuwaiba watu na tutamkata kila mshukiwa wa shughuli hizo. Hatuna shaka kuwa watoto hawa walikuwa wanatoroshwa ili wakadhalilishwe; ni wasichana 12 kutoka familia tofauti,” aliongeza.
Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji ya Somaliland, Mohammed Ali, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Hargeisa hapo Jumatano na kusema wasichana hao 12 walikuwa wanakwenda kuuzwa.
Alisema uchunguzi wa kesi hiyo umegundua kwamba wafanyabiashara haramu ya binaadamu walikuwa wanapanga kuwasafirisha watoto hao nje ya Somaliland kwa kupitia barabara na kuvuuka hadi Djibouti na kisha kuendelea nao kutoka hapo.
Kulinda haki za watoto ni muhimu sana kwa mashirika ya huduma za kijamii yaliyoko Somalinda na jumuiya za Umoja wa Mataifa kufanya kazi pamoja kuwalinda watoto wasiokuwa pamoja na watu wazima wakati wakivuuka mipaka, alisema Osman.
“Pia ni muhimu kwa serikali kuwapa mafunzo maafisa wa usalama wa uhamiaji na polisi kuwa waangalifu kwa watoto wanaosafiri bila ya wazazi wao,” alisema Osman.
Katika siku za hivi karibuni, Somaliland imeshuhudia kuongzeka kwa shughuli za usafirishaji haramu wa binaadamu unaowalenga watoto wadogo, Sahardid Mohamed Osman, ambaye ni meneja wa uendeshaji wa shirika la haki za watoto la Comprehensive Community-Based Rehabilitation Somaliland (CCBRS).
“Tangu Aprili kumekuwa na kesi mbili zinazowahusisha watoto wanaosafirishwa kwenye makundi, na inawezekana wengi zaidi wamekuwa wakitoroshwa nje ya nchi bila ya kujuilikana,” aliiambia Sabahi.
Katika mikasa mingi, watoto wanaotekwa nyara hutekwa kutoka nje ya Somaliland, alisema Bashe Yusuf Ahmed, mkurugenzi mkuu wa wizara ya kazi na masuala ya kijamii ya Somaliland.
Katika mkasa mmoja, hapo Aprili 28, watoto tisa wakiwa na mwaka kuanzia mmoja hadi mitatu waliokolewa kwenye bandari ya Berbera. Watoto hao walikuwa wakisafirishwa katika meli kutoka Yemen na Waethiopia wawili, ambao kesi yao sasa iko kwenye mahakama ya Berbera, alisema Ahmed.
“Watoto hao sasa wanatunzwa katika kituo cha Mayatima cha Hargeida, na hadi sasa hakuna aliyedai kuwa ni wake.”
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Ni bahati mbaya sana na balaa ambavyo vimeiangukia Somalia. Wengi wa watu wetu leo kwa hivyo hawana hisia za kupoteza dini yao na utaifa wao. Naomba Mungu awaoneshe Wasomali njia iliyonyooka.
Wewe si maarufu kwa uharamia wa baharini tu, bali katika biashara ya binadamu, biashara haramu ya silaha, utekaji nyara, kusafisha pesa na vita vilivyopo sasa. Hii sio njia ya kuikomboa Somalia kutokana na wimbi la umasikini na ugaidi. Tufuate mikabala ya kidiplomasia na nchi zetu jirani na kujitahidi kufanyakazi kwa kuimarisha uchumi.
Si jambo zuri kufanya biashara kama hii. Vipi wangelikuwa watoto wako au jamaa zao ndio waliouzwa, ungejisikiaje? Serikali iwe makini sana na watoto wanaotoroshwa kwa njia za haramu na waweke sheria kali za kuwafanya watekaji nyara hao waache biashara hii.