Wakimbizi wa Somalia huko Yemeni waendelea kuhisi mjeledi wa al-Shabaab.

Na Adnan Hussein jijini Mogadishu

Juni 29, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Maelfu ya raia wa Somalia walikimbilia Yemeni kwa miaka kadhaa iliyopita kuepuka vurugu za al-Shabaab na utawala wenye msimamo mkali uliowekwa na harakati za al-Shabaab.

  • Wakimbizi wa Somalia wakitembea katika  mtaa wa ovyo wa Basateen karibu na mji wa bandari wa Aden kaskazini mwa Yemeni  2010. [AFP]

    Wakimbizi wa Somalia wakitembea katika mtaa wa ovyo wa Basateen karibu na mji wa bandari wa Aden kaskazini mwa Yemeni 2010. [AFP]

  • Wayemeni wakiangalia gari iliyoharibika katika shambulio la kujitoa mhanga katika mji wa bandari wa Aden ambalo lilimuua  Meja Jeneralli  wa jeshi la Yemen Salem Ali Qoton tarehe 18 Juni. [AFP].

    Wayemeni wakiangalia gari iliyoharibika katika shambulio la kujitoa mhanga katika mji wa bandari wa Aden ambalo lilimuua Meja Jeneralli wa jeshi la Yemen Salem Ali Qoton tarehe 18 Juni. [AFP].

Wakimbizi hawa hawakujua kuwa mjeledi wa al-Shabaab na itikadi yao inayounga mkono al-Qaeda ingewafuata hata baada ya kuvuka bahari.

Mwezi Februari 2012, wakati al-Shabaab walipoungana rasmi na al-Qaeda na waliapa kuwa watii kwa kiongozi wao Ayman al-Zawahiri, kundi hilo lilitangaza kuwa wanachama wake wangejiunga na kaka zao wa Yemeni katika jihadi”

Miezi iliyofuata baada ya kuungana , al-Shabaab walikuwa katika kukimbia, wakipoteza udhibiti wa miji muhimu kadhaa na kukumbana na vikosi vya mstari vya mbele vya majeshi yaliyoungana ya majeshi ya serikali ya Somalia na Misheni ya Umoja wa Afrika kwenye vikosi vya Somalia.

Matokeo yake, wanachama wa al-Shabaab wamekuwa wakiripotiwa kukimbia Somalia ya kusini wakiwa katika boti ndogo kwenye fuko za Yemeni katika jaribio la kuepuka kile kinachosemwa na wachambuzi wengi kuwa ni kushindwa kusikoepukika kwa kundi hilo.

Mariam Said wa kituo cha mawasiliano ya jeshi cha Somalia jijini Mogadishu alisema idadi kamili ya wapiganaji wa al-Shabaab huko Yemeni haijulikani.

“Hakuna yeyote anayeweza kutoa idadi hasa kuhusiana na idadi ya wapiganaji wa Somalia ambao wameunganishwa katika kundi la Ansar al-Sharia, ambalo linapigana na vikosi vya Yemeni. [Hatahivyo] hii ni hali ya hatari sana, “ aliambia Sabahi.

Uwepo wa wapiganaji wa al-Shabaab wanaopigana upande wa Ansar al-Sharia,tawi la Yemeni la al-Qaeda katika rasi ya uarabuni, na ukweli kuwa raia wa Somalia wamekuwa wakiunganishwa na operesheni za kigaidi huko Yemeni umeleta ugumu mwingine zaidi kwa wakimbizi wa Somalia ambao sasa wako katika kushukiwa.

Mlipuaji bomu la kujitoa muhanga Msomali amuua kamanda wa Yemeni.

Tarehe 18 Juni katika jiji la Aden, mlipuaji bomu la kujitoa muhanga alijirusha mwenyewe kwenye gari la meja jenerali Salem Ali Qoton, kamanda wa mkoa wa kaskazini wa Yemeni, na kulipua mkanda wake uliokuwa na milipuko.

Vyanzo vya matibabu vilisema Qoton alikufa mara alipowasili katika hospitali ya Sabir.

Saa chache baada ya tukio hilo, Wizara ya Ulinzi ya Yemeni ilieleza katika tovuti yake kuwa mlipuaji bomu alikuwa raia wa Somalia.

Tarehe 21 Juni, al-Qaeda walidai kuhusika na shambulio hilo.

Tulisikia taarifa za awali kuwa mkosaji wa shambulio hilo la kiuhalifu ni raia wa Somalia, lakini uchunguzi bado unaendelea kutafuta utambulisho wake halisi ,” balozi mdogo wa Somalia huko Aden Ahmed Abdi Hassan aliiambia Sabahi.

Hassan alielezea jinsi tukio hilo litakavyoathiri maisha ya Wasomali wanaoishi Yemen.

Tunashawishika kwamba watu wa Yemeni wanajua vizuri sana kwamba wakimbizi hawajawasili nchini Yemen kwa hiari yao, lakini ni kutokana na vita vinavyoendelezwa na kikundi cha al-Shabaab kinachoaminiwa kwamba hakitokani na taifa moja lakini kwamba ni dunia nzima ndiyo nyumbani kwao," alisema.

"Polisi walikuwa sawa kuchukua hatua kadhaa za tahadhari kuzuia uvunjifu wa usalama, lakini tunauliza kama wanatofautisha kati ya wale waliokuja Yemen kwa kukimbia vita nchini Somalia na wale ambao wanaleta vurugu," alisema Hassan.

Kamati ya usalama katika jimbo la Dhamar huko Yemen ya kati ilithibitisha tarehe 19 Juni kampeni ya kuwatia mbaroni wakimbizi ambao wako kwa makundi katika jimbo hilo kwa idadi ambayo haijawahi kutokea. Kamati iliwaonya dhidi ya hatari za kuingia kwa wingi kwa wakimbizi wa Somalia katika jimbo, maendeleo yanayosemwa kuwa yangeweza kutishia amani kutokana na matatizo ya usalama, kijamii na kiuchumi ambayo yanaweza kutokea, hususan wakati ambapo matukio ya kigaidi yanatokea.

Alipoulizwa kuhusu kampeni ya al-Shabaab kuunga mkono na Ansar al-Sharia, Hassan alisema, "[Al-Shabaab] walitangaza awali wangeenda Yemen na kujiunga na kile walichokiita ndugu zao wa Yemen katika Jihad, na hivyo tunatoa wito kwa mamlaka za Yemen kusimamia kikamilifu pwani na mipaka yao yote ili kundi hili lisiweze kujipenyeza nchini kwao na kuvuruga ulinzi na usalama wao.

Wasomali wengi nchini Yemen ‘hawasababishi tishio’

"Ninauhakika kwamba Wasomali wengi hawasababishi hatari yoyote katika ulinzi na usalama wa jirani zetu, Yemen, sawa na namna jamii ya Yemen ilivyokuwa ikiishi nchini Somalia kwa miongo iliyopita," balozi aliendelea.

"Tunajua kwamba watu wa Yemen wanawapenda Wasomali kama walivyokubali kushirikiana nao na serikali yao imewahakikishia uhuru wa kuzunguka kutafuta kazi ndani ya Yemen, bila kutaja ufadhili wa elimu kwa wanafunzi [Wasomali]wahamiaji," alisema Hassan.

Faisal Mayow, mwenye umri wa miaka 37, mkimbizi ambaye ameishi huko Aden kwa miaka 12, aliiambia Sabahi kwamba Yemen inakubaliana na ushirikiano wa kindugu, kidini na ushirikiano na majirani wa Somalia

Imekuwa ni nchi ya pili baada ya Kenya kuwakaribisha wakimbizi wa Somalia, na Sanaa wasingewakubali wananchi wa Somalia wanaofadhiliwa na al-Qaeda na madalali wa Wasomali wa al-Shabaab na washiriki wengine wageni," alisema ,"Tutawapa taarifa wanajeshi wa usalama wa Yemen kuwawinda na kuwashikilia wale wote ambao wanapenyeza katika kambi za wakimbizi kwa lengo la kuwapata vijana wadogo ili washirikishwe katika migogoro ndani ya nchi ambazo hata sio zao. Tutapambana na maadui wa amani katika kila mtaa na kila kichochoro.

Kuwazuia wapiganaji baharini

Mkuu wa Jeshi la Uanamaji Farah Ahmed Omar Qare, kamanda wa Jeshi la Baharini la Somalia, ameiagiza Yemen kutoa tahadhali na uangalifu kuhusiana na vikundi vya maharamia ambavyo vinajaribu kuwaumiza watu wasio na hatia.

"Tunatoa wito kwa serikali ya Yemen kutoa msaada zaidi kwa Wasomali ambao wameikimbia jehanamu ya al-Shabaab na kuwasaidia katika njia yoyote ile inayowezekana kwa chakula, dawa, mavazi na mahali pa kulala," aliiamba Sabahi. "Tunawaomba wasiwadhuru [Wasomali]wanaopita mitaani, wanaofanya kazi au hata wale wanaojaribu kuingia nchini."

"Hata hivyo, wale wote waliojihusisha na vitendo vya vurugu na kuwasaidia al-Qaeda wanapaswa kupewa adhabu," aliongeza.

"Hii ni hali tete sana na tutashirikiana na serikali ya Yemen kuwalenga maharamia wakati bado wakiwa baharini, kabla hawajatia nanga katika pwani za nchi zote, kwa sababu hili sio tatizo la Wasomali peke yao lakini litasambaa hadi Yemen na eneo zima," alisema Qare.

"Kunapaswa kuwa na ushirikiano halisi wa kimataifa ili kumaliza ukereketwa wa kupindukia na ugaidi nchini Somalia na Yemen," alisema. "Hali hii inachukulia watoto wasio na hatia na kutojua kwao chochote kuwaingiza katika dunia yenye chuki na mauaji

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 45)

Dislike_icon(1)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo