Juni 27, 2012
Barabara inayounganisha Hargeisa na Ina Guha katika mpaka wa Ethiopia inawekwa sawa na kuboreshwa, kwa kushukuru juhudi za kukusanya fedha za jamii ya Somaliland.
Ujenzi huo wa barabara ya kilomita 80 ulianza rasmi mwanzoni mwa mwezi huu huko Hargeisa, na inatarajiwa kuinua uchumi wa na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma baina ya Somaliland na Ethiopia.
Mradi wa ujenzi, ambao utagharimu dola milioni 4.2, unafadhiliwa na jamii zinazoishi Hargeisa na Salahley pamoja na msaada wa wananchi wa Somaliland wanoishi nje, kwa mujibu wa Sheikh Mohamed Ali Gedi, naibu mkurugenzi wa bodi ya kamisheni ya barabara.
Gedi alisema barabara ya Hargeisa-Ina Guha mwanzo ilijengwa nchini Somalia na serikali ya Italia miaka ya 60 ili kuunganisha Hargeisa na Ethiopia na miji mengine ya mipakani na miji ya Somalia.
Alisema jamii inayoishi katika eneo hili ilikuwa na wazo la barabara ya lami miaka kadhaa iliyopita.
“Wakati pesa ya ujenzi ilikadiriwa kuwa zaidi ya dola milioni 4, watu walifikiria kuwa hilo haliwezekani, lakini sasa wamegundua kuwa inawezekana,” Gedi alisema katika hotuba yake ya sherehe za uzinduzi wa ujenzi huo hapo tarehe 6 Juni.
“Ni furaha kubwa kwetu kuanzisha ujenzi mpya wa barabara hii muhimu sana,” alisema. Nchi zinazoendelea hazipata mafanikio kwa kitu walichopelekewa, bali kwa hamu za wananchi wao za kuziendeleza nchi zao.”
Gedi alisema pesa kwa ajili ya kazi za barabara zilifadhiliwa na mashirika ya ndani, wafanyabiashara, wanaume na wanawake wanaoishi Hargeisa na Salahley, pamoja na jamii inayoishi uhamishoni. “Mtu yeyote anaweza kuchangia kwa hari yake katika mpango huu,” Gedi alisema.
Alisema barabara hiyo itajengwa kwa awamu kadhaa, katika sehemu za kilomita 13 kila moja.
Guled Osman, mjumbe wa kamisheni ya barabara, alisema jamii ilianza kuchangisha fedha za mradi huu hapo Disemba 2011. Mpaka sasa wameshakusanya dola milioni 1.7, wakati vifaa na zana zenye thamani ya dola milioni 1.4 vilitolewa na mfanyabiashara wa Hargeisa Omar Aided.
Meya wa Hargeisa Hussein Mohamud Jiir alisema serikali ya mtaa imechangia dola 20,000 za kuanzia mradi, na iko tayari kuchangia zaidi. Alisema Mamalaka ya Barabara ya Somaliland pia imeahidi kushiriki katika maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Hargeisa-Salahley-Ina Guha.
Abdirahman Aden Aar, mhadhiri wa uchumi katika Taasisi ya Utumishi wa Umma ya Hargeisa, alisema barabara itarahisisha maingiliano baina ya jamii na ubadilishanaji wa bidhaa na huduma baina ya Somaliland na Ethiopia, na itatoa nafasi za kazi kwa watu wengi.
“Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa eneo hili, mzunguko wa watu na ubadilishanaji wa bidhaa na huduma,” Aar aliiambia Sabahi. “Ninaweza kusema kuwa barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wa Somaliland.”
“Biashara za wenyeji zitafaidika kutokana na uuzaji wa lami, mafuta na vitu vingine vinavyohitajika katika ujenzi wa barabara," alisema.
Mbunge wa Somaliland Abdirahman Osman Alin, anayewakilisha Kusini ya Hargeisa na Salahley, alisema serikali ya mtaa itamualika Rais wa Somaliland Ahmed Mohamed Silanyo baada ya kilomita 13 zitakapokamilika ili kuwahamasisha watu kutoka maeneo mengine kutoka Somaliland kuunga mkono mradi huu.
Alin alisema ujenzi wa barabara hii utaongoza maendeleo na kupambana na umasikini, na mara awamu ya mwanzo itakapokamilika, tutaihamasisha jamii kusaidia mradi ili kumaliza sehemu iliyobakia ya barabara.
Gedi, naibu mkurugenzi wa bodi ya kamisheni ya barabara, alisema ujenzi wa barabara utakamilika mwaka huu. “Ikiwa pesa zitakusanywa, inaweza kumalizika kasoro ya miezi sita,” alisema.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Ni kazi nzuri sana kuona kwamba watu wa Somaliland wanafanya kazi ngumu na kwa kweli hii inaonesha jinsi gani watu wa Somaliland walivyo tayari kwa kuliendeleza taifa hili. Nina hakika kuwa ikiwa tutaendelea na kazi kama timu tunaweza kuwa sawa na mataifa yaliyoendelea.
Mungu ni mzuri, haya ni maendeleo mapya ambayo yanaleta furaha. Ikiwa watu wa Somalia wangekuwa wanafanya lolote kwa njia ambayo wamelishughulikia hili, nchi ingeweza kutatua matatizo na njaa ambayo yanaikabili. Pia ingekuwa imeshapita vita vya kawaida. Nimefurahi kuwa watu wa Hargesia na Salahley wamekuja na maendeleo makubwa kiasi hicho.