Wanaharakati wa Somalia walaani ujumbe wa “mapenzi juu ya kifo cha kishahidi” kutoka kwa mke wa Zawahiri

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Juni 25, 2012

  • 66 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wanawake wa Somalia na wanaharakati wa haki za binadamu wamelaani ujumbe wa karibuni wa mke wa kiongozi wa al-Qaeda Ayman al-Zawahiri ambao anatoa wito kwa akina mama wa Kiislamu kuwakuza watoto wao kwa “mapenzi ya jihadi na kifo cha kishahidi”.

  • Wanaharakati kadhaa waliiambia Sabahi kuwa ujumbe wa Umaima Hassan unapingana na misingi na heshima ya Uislamu. Juu, Mama wa Kisomali na watoto wake wawili wakielekea hospitali mjini Mogadishu mwaka 2009. [Na Yasuyoshi Chiba/AFP]

    Wanaharakati kadhaa waliiambia Sabahi kuwa ujumbe wa Umaima Hassan unapingana na misingi na heshima ya Uislamu. Juu, Mama wa Kisomali na watoto wake wawili wakielekea hospitali mjini Mogadishu mwaka 2009. [Na Yasuyoshi Chiba/AFP]

Umaima Hassan Ahmed Mohammed Hassan alitoa ujumbe hapo tarehe 8 Juni katika tovuti yenye mahusiano na al-Qaeda.

“Ushauri wangu kwa nyinyi dada zangu kuwakuza watoto wao juu ya mapenzi ya jihadi na kifo cha ushahidi na kuwajenga mapenzi juu ya dini na kifo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,” Hassan aliandika.

“Ujumbe huu ulitolewa kwa dhamira ya kutia sumu akili za watoto kwa ajili ya kuwaandikisha na kuwatumia katika shughuli za kigaidi na matendo ya kigaidi,” alisema mwanaharakati wa haki za watoto Anab Mohamed Omar.

“Kulea watoto katika utamaduni wa vurugu, kujiua na kumwaga damu isiyo na hatia sio sahihi na kunapingana na misingi ya Uislamu,” Omar aliiambia Sabahi.

“Akina mama na walezi wenye dhamana ya kuwalea watoto lazima wawalee katika mapenzi na hisia zinazopingana na misingi ya misimamo mikali,” alisema. “Lazima wawalinde watoto kutokana na dhana potofu. Pia lazima wawe imara kupambana na utetezi wa ugaidi na itikadi za al-Qaeda ambazo zinahamasisha kumwaga damu ya watu wasio na hatia.”

“Inaeleweka kuwa mashirika ya kigaidi yanafanyakazi bila kusita ya kuwalaghai watoto na vijana kwa vile wao ni rahisi na wanaovutika na mawazo mapya bila ya kujua matokeo yake,” Omar alisema. “Kwa hivyo tunawataka wanamama wa Somalia kuungana na kufanyakazi pamoja ili kupambana na wazo hili la siasa kali katika nchi yetu.”

‘Utamaduni wa chuki na vurugu’

“Magaidi wanajaribu kuwashawishi baadhi ya akina mama kuingiza kwa watoto wao utamaduni wa chuki na vurugu ili wawe mabomu ya kibinadamu na wanaojiua kwa kujitoa muhanga,” alisema Amina Abukar, mwalimu mwanaharaki wa haki za wanawake.

“Akina mama lazima wawe na dhamana kamili katika malezi ya watoto wao. Lazima wafuate taratibu sahihi wakati wa kuwalea watoto wao kwa sababu siasa kali na msimamo mkali havina nafasi katika Uislamu,” aliiambia Sabahi.

Abubakar ametoa wito wa kutokomeza kutojua kusoma na kuandika pamoja na ujinga miongoni mwa wanawake na watoto wa Somalia ili wasiangukie katika siasa na misimamo mikali.

Kupitia vita vya kupambana na kutojua kusoma na kuandika, tunaweza kupigana na mawazo ya siasa kali,” alisema. “Tunatoa wito kwa akina mama na masheikh kufanya kazi pamoja ya kueneza dhana halisi ya Uislamu na kufuata njia iliyonyooka ya kuwalea watoto wao ili waweze kupambana na siasa kali kwa njia zote tulizo nazo.”

Abukar alisema akina mama wana wajibu mkubwa sana wa kupambana na siasa kali na ugaidi.

“Uislamu ni dini ya kuvumialiana na inapingana na misimamo mikali ya dini na siasa,” alisema.

Kutumia watoto kama “mafuta katika vita”

Su'di Mohamed Ali, mkurugenzi tawala katika Wizara ya Wanawake na Masuala ya Familia, aliwataka akina mama wa Somalia kuwakuza watoto wao katika misingi ya wastani, uraia na uzalendo.

“Njia ambayo mke wa al-Zawahri anawataka akina mama kuwalea watoto wao juu ya vurugu na ugaidi hakuhusiani na Uislamu,” alisema. “Tunatoa wito kwa akina mama wa Somalia kuwalea watoto wao juu ya uvumilivu na udugu na kuwafunza njia sahihi ya Uislamu, mbali na siasa kali na vurugu. Itikadi ya al-Qaeda haiwakilishi njia sahihi ya Uislamu na kwa sababu hii tunawataka akina mama wa Somalia kutomsikiliza mke wa kiongozi wa al-Qaeda.”

Ali alisema ujumbe huu ni ushahidi kuwa al-Qaeda wanataka kuwatumia watoto kama mafuta katika vurugu na vita.

Fartun Yusuf Ahmed, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 24 alisema, “Kitu muhimu zaidi katika malengo ya elimu -- ya zamani na ya sasa – ni kuwatayarisha raia wa kuigwa watakao kuwa na faidia kwa wao wenyewe, taifa lao na dini yao. Uislamu unapingana na aina yoyote ya msimamo mkali au ung’ang’anizi katika itikadi na matendo.”

“Uislamu ni dini inayohusika na kutoa ushauri na msimamo wa wastani na siku zote inakuwa na msimo wa kati katika kila kitu,” aliiambia Sabahi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 44)

Dislike_icon(22)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • C/rashiid karate
    September 4, 2012 @ 02:40:54PM

    Tumeamrishwa kupigana vita vitakatifu na Mungu Mwenyezi, na hatuwezi kupinga au kujadili kitu chochote tulichoamrishwa na Mungu kwa sababu Yeye ndiye Ambaye aliumba kila kitu kinachoishi ulimwenguni na vyote ni waja Wake. Matokeo yake, mtu yeyote ambaye ana shaka au anayejadili kuhusu vita vitakatifu basi nafikiri anatenda dhambi. Kwa hivyo, ikiwa wewe ni Muislamu wa kweli, usipinge au kujadili kuhusu kile ambacho uliamrishwa na Mungu kwa sababu wewe ni mja Wake.

  • mohamed
    September 4, 2012 @ 09:43:32AM

    Amani iwe juu yenu. Sio vibaya kuishi kwa dini. Ni lazima lakini kujilipua kwa mabomu ya kujitoa muhanga ni vibaya kweli kweli. Muogopeni Mungu wakati wote.

  • ismaaciil mahamed osman
    September 2, 2012 @ 04:24:47AM

    Naaminikuwa neno ‘Jihadi’ maana yake ni kujitolea nafsi na juwajulisha wengine kuwa wanatakiwa kuchukua juhudi kujifunza jinsi ya kupambana na makafiri na wasaidizi wao.

  • zakariya
    September 2, 2012 @ 02:02:52AM

    Amani iwe juu yenu. Kama Muislamu, popote unapoishi duniani ni wajibu kuwalea watoto wako kwa mujibu wa mafunzo na misingi ya dini ya Kiislamu. Pia inatakiwa kuwafundisha jinsi ya kupigana vita vitakatifu na ambao wameruhuswa kupigana vita vitakatifu. Lazima wafunzwe kuwa Muislamu hapaswi kumshirikisha Muislamu mwengine katika vita vitakatifu. Asanteni. Karibuni.

  • Basbaas
    September 1, 2012 @ 08:52:46AM

    Kwa maoni yangu, yeyote yule anayeendelea kuzungumzia suala hili anashiriki katika kueneza maoni haya. Mungu, Mwenye Uwezo, ameweka wazi na haihitaji matangazo yanayofanywa na mtu katika dunia ya leo kwa sababu hakuna kitu kipya kinachoweza kuongezwa katika dini. Watoto wana dhamana? Hapana. Kuwalea watoto kwa kuwafundisha jinsi ya kupigana ni wazo baya. Waleeni watoto kwa njia za amani kwa kuwafundisha dini na mambo mengine mazuri.

  • abdirashiid osmaan
    August 30, 2012 @ 09:39:03AM

    Mada mnayoitolea maoni iko dhahiri. Mkoje?

  • ismaaciil cadami
    August 30, 2012 @ 07:04:21AM

    Jihadi ni haki ambayo imefanywa kuwa ya lazima kwa kila Muislamu ambaye anaweza kuilinda dini yake lakini hii iliyopo Somalia sio Jihadi au kitu kinachokaribiana nayo. Ikiwa nitamuua Muislamu ambaye ni wa taifa moja na dini moja na sisi kwa jina la Jihadi, nitakuwa nimefanya dhambi tu na sitozawadiwa na Mungu. Hatupaswi kuwalea watoto wetu kwa kuwafunza aina hii ya jihadi ya Somalia. Tunapaswa kuwaelimisha ili waweze kutofautisha mabaya kutoka mema.

  • BINU LADEN
    August 30, 2012 @ 02:31:30AM

    Mungu ni mkubwa. Ni nzuri kweli kwa sababu watu wote waliotoa maoni katika makala hii wanaonekana kujua umuhimu wa mafunzo yanayofundishwa na dini yetu nzuri. Tunamuomba Mungu kuwaondosha makafiri. Lakini kibaya zaidi ni wale ambao kwa sababu ya kuwaunga mkono makafiri wanasema vibaya kuhusu Uislamu huku wanatafuta umaarufu, heshima na pesa kutoka kwa makafiri. TUNATAKA KUWAAMBIA KUWA HESHIMA NA HADHI VINAPATIKANA KATIKA DINI YETU NZURI: UISLAMU.

  • Mohamed Abdullahi
    August 28, 2012 @ 08:09:06PM

    Msifuni Mungu. Mshukuruni Mungu. La pili, Mungu atuongoze kufuata dini na kutusaidia kuifahamu.

  • farhan muhamad xasan
    August 27, 2012 @ 04:55:59AM

    Mimi ni raia wa Somalia. Kwa kweli sielewi ni nani atakayejali haki za watu ikiwa Wasomalia wamegawanyika wenyewe katika vyama vya kisiasa.

  • BISHAAR
    August 26, 2012 @ 10:31:29AM

    MKE WA MWANAJIHADI SHEIKH AYMAN (MUNGU AMLINDE) YUKO SAHIHI NA WATOTO LAZIMA WALELEWE KWA MUJIBU WA DINI YA KIISLAMU NA MAWAZO YA KUHUSU JIHADI. WANAWAKE HAWA WANAODAI KUWA WANAHARAKATI WA KIJINSIA WAMETOKA NJE YA DINI. JE, NI UGAIDI KUWALEA WATOTO KUIPENDA DINI YAO NA KUWA WANAJIHADI?

  • oday jacayl
    August 26, 2012 @ 03:18:43AM

    Mapenzi katu hayafi kutoka kwa kila mmoja na haimuachi mmoja pekee.

  • muhaajir
    August 20, 2012 @ 09:33:03AM

    Mungu ni mkubwa. Chukueni fursa ya dini na nendeni katika vita vitakatifu, enyi Waislamu. Piganeni vita vitakatifu dhidhi ya wasioamini.

  • Cabdulaahi Cabdi
    August 20, 2012 @ 02:34:14AM

    Amani iwe juu yenu. Ni haki kuwalea na kuwafundisha watoto juu ya Uislamu ili waweze kukusaidia hapa duniani na akhera. Ninaleta ujumbe huu kwa kila mama na baba lakini siungi mkono kunandikishwa kwao kama askari kwa sababu watoto hawajui chochote. Kupigania dini ni lazima kwa watu wazima, sio kwa watoto.

  • kululecke
    August 18, 2012 @ 10:14:31AM

    Tunamuomba Mungu atujaalie amani.

  • kululecke
    August 18, 2012 @ 10:10:15AM

    Uko sahihi ndugu. Unapaswa kulinda usalama popote ulipo dunia hii, kwa sababu hilo lina maslahi kwako na kwa ndugu zako.

  • cabdifataax
    August 17, 2012 @ 06:06:41AM

    Ningependa kuwaambieni kuwa hamko sahihi. Hamwezi kutoa maoni yenu kuhusu dini lakini mnaweza kuwauliza wanazuoni pale mnapokuwa na shaka kuhusu dini. Tusivuke mipka kwa sababu ya chuki kwa mtu au kikundi.

  • wadani muslin ah oo dadki iyo dalka jecel
    August 15, 2012 @ 09:04:29AM

    Amani na baraka za Mungu ziwe juu ya Waislamu wote popote pale walipo. Kama nitazungumzia juu ya vita vitakatifu, naweza kusema kuwa sisi hatuelewi maana yake vizuri kwa sababu mnadhani vita vitakatifu ni lazima kwa nani? Ni kwa nani vita vitakatifu hupiganiwa? Na ni wakati gani vita vitakatifu vinakuwa lazima? Kama tumemuua mtu ambaye ameshuhadia kwamba hakuna Mungu wa kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni mjumbe wake wa kweli, hatutakuwa tumepigana vita vitakatifu bali tutakuwa tumepotelea mbali ya njia ya Mwenyezi Mungu na tutakuwa tumekiuka haki ya Waislamu wasio na hatia. Kama unamuita mtu kutoka msikitini kuwa ameasi kutoka Uislamu, utakuwa muasi katika changamoto hiyo. Wale vijana wenu ambao walihadaiwa wanapaswa kutumia akili zao vizuri na kujishughulisha wenyewe na mawazo ya ndani. Kipande hiki cha ushauri kinatoka kwa ndugu yako katika Uislamu. Naomba Mungu atusaidie tufuate njia yake ya haki.

  • salmaan cali
    August 14, 2012 @ 06:59:04AM

    Makafiri wako katika vita na dini yetu na Koran, kwa hivyo ndugu zangu eleweni kuwa makafiri wanachokiita ugaidi ni vita vyetu vya haki vya Jihadi. Ndugu zangu, msikubali kupotoshwa mkaamini hilo na lazima tufanye vile Mwenyezi Mungu alivyotuamrisha kufanya.

  • nagma osman
    August 13, 2012 @ 05:25:53AM

    Nawahimiza mumuogope Mungu na muache kuanzisha chuki baina ya watu. Kueneza chuki sio kuzuri. Pia ningependa kuwaambia al-Shabaab kuwa mmeshaasi kutoka kwenye dini na lazima mtubu kwa Mungu na kuacha kuua Waislamu wasio na hatia. Na pia muache kuwapotosha vijana na watoto wasio na hatia. Ikiwa kweli mnapigana vita vitakatifu kwa nini basi hamuongozi kwa kuwa mfano katika uwanja wa vita?

  • Mohamed
    August 12, 2012 @ 03:19:31AM

    Fungueni macho yenu na mjifunze elimu, ndugu zangu. Kinachotokea Somalia sio vita vitakatifu kwa sababu kuua, kulemaza, kuiba, kupiga mabomu, kuchapa viboko, kusambaratisha watu na kuwakata vipande vipande na kutoroka majeshi ya wasiokuwa Waislamu kwenye uwanja wa vita hivo sio vita vitakatifu. Ni wajibu wa kila Muislamu kujifunza dini ya Mungu na kusema nimesikia kutoka Sheikh fulani haitakuwa sababu ya kujitetea akhera.

  • cabdikarim Awes
    August 11, 2012 @ 04:10:07PM

    Ni maelezo kuhusu ukweli wa mambo.

  • Jamaal
    August 11, 2012 @ 08:50:30AM

    Baada ya maamkizi ya heshima, ningependa kusema kuwa sio vizuri kuwapotoa watoto na tunapaswa kutowaamini watu kama Zawahiri na mke wake tuliooneshwa kwenye televisheni na wale Wasomali wengine ambao nyuso zao daima hazionekani. Wazo la kuwalea watoto kwa kuwafundisha kujilipua mabomu ya kujitoa muhanga ni kitu kilichoundwa na mke wa mtu tuliyeoneshwa kwenye televisheni na Wasomali lazima wawe na tahadhari wasipotoshwe.

  • sanka
    August 9, 2012 @ 12:23:57PM

    Haki iko wazi wakati wote, kwa hivyo acheni kulumbana na fuateni Sharia kama ilivyo.

  • saalixu bukhaadir
    August 8, 2012 @ 06:50:11PM

    Amani iwe juu yenu. Ningependa kuwaambia wasomaji wetu wapendwa kuwa kuandikisha watoto kama askari ni marufuku.

  • mukhtar
    August 2, 2012 @ 11:24:15AM

    Ninataka

  • diiriye canbuur
    August 2, 2012 @ 05:15:07AM

    Bado kuna wanawake wanaowahimiza watu kujilipua! Tunatakiwa tuelewe dini ya Kiislaamu vizuri sana, ili tuishi kwa amani hapa duniani na akhera. Utafaidika nini kumuua kiongozi Muislamu wa maombi wa msikiti na kuwalipua watoto wadogo? Madhara gani uliyoifanyia Marekani na nchi za magharibi? Uislamu haihimizi kuweko kwa shida lakini wachache walio na matakwa yao kufanya hivo.

  • mogihiolina
    August 1, 2012 @ 03:53:24AM

    Kwa kweli, nadhani vita vitakatifu vipo na vimeelezwa katika Koran Tukufu na Mweneyezi Mungu...lakini vimetafsiriwa vibaya au kutofahamika na hawa binamu zangu, hasa wale wanaong’ang’ania itikadi potofu za kigeni. Dini yetu haiwalemezi watu mizigo ya matatizo lakini sheria hizi za kumuita Muislamu anayeasi kutoka Uislamu au asiyekuwa Muislamu sio sahihi. Ndugu zangu, ni lazima kwa kila Muislamu kujifunza Sharia (Sheria) ya Kiislamu lakini tusijifunze kuitafsiri vibaya. Binamu zangu, mimi ni Muislamu ambaye ni raia wa Ujerumani lakini ambaye ninataka kujifunza lugha ya Kisomali na ambaye ninailewa zaidi lugha hii kuliko nyinyi. Ninamuomba Mungu atuongoze katika njia iliyonyooka na ninashukuru kwa maoni yenu, ndugu zangu.

  • jibriil maxamud jibriil
    August 1, 2012 @ 03:03:57AM

    Al-Qaida hawajaumba pepo na dini yao wenyewe. Sielewi kuhusu itikadi hii ya kupotosha watoto kujilipua wenyewe. Itikadi hii ambapo Waislamu wanashauriwa wajilipue wenyewe haina msingi wa kidini wala haiko karibu na mafundisho ya dini yoyote.

  • samiir hussein
    July 31, 2012 @ 01:34:11PM

    Vita vitakatifu ni kitu ambacho kipo.

  • Saadaal Weynr
    July 31, 2012 @ 01:05:16PM

    Lazima mzingatie juu ya kile mnachowaandikia watu kwa lengo la kuwachochea akina mama ambao ni waumini.

  • Mohamed Ali
    July 24, 2012 @ 07:02:01AM

    Kwa kweli nimefurahi sana kuwa watu wanajifunza kuhusu matatizo yanayoletwa duniani na watu hawa wanaoitwa al-Qaida ambao nina hakika hawasemi ukweli kuhusu Uislamu bali uongo na kuonesha picha mbaya juu ya Waislamu. Hakuna popote ilipoelezwa kwa dini ya Kiislamu kuwa wanawake na watoto wauliwe kwenye misheni ya kulipiza kisasi huku wakilipiza kisasi cha watu wanaodai kuwa ni wapiganaji wa vita vitakatifu. Nashangaa kwa sababu katu sijawahi kusikia kulipiza kisasi kwa mtu aliyekufa kwa ajili ya Menyezi Mungu.

  • Garaad
    July 23, 2012 @ 10:07:54AM

    Amani iwe juu yenu. Kwanza, ninamuomba Mungu, amlinde mke wa kiongozi Ayman al-Zawahiri ambaye ni mpiganaji wa vita vitakatifu. Pia ninamuomba Mungu awaumbe wanawake wengi wa aina yake. Pia, inaonekana kuwa wanawake waliotoa maoni kuhusu Umeyma Hassan Ahmed hawana elimu ya dini au hata mila za Kiislamu. Uislamu ni dini ya haki, dini ya amani na subira lakini kwa nani???. Ni kwa ajili ya Waislamu au wasiokuwa Waislamu? Pia wao ni vipofu na viziwi kuhusu vita vitakatifu kama nguzo ya Uislamu ambao wanadai kuulinda….!!!!! Ningependa kuuliza swali; vipi mtu atalinda dini wakati anachukia vita vitakatifu au anaviona kama chuki au vita tu? Sitaki kusema sana kuhusu wanawake hawa wanaotoa maoni yao kuhusu elimu yao kwa sababu hii inaweza kuonekana kutoka kichwa cha habari ‘Wanaharakati wa haki za binadamu na kama wao’ wanavumilia lugha hii inayosemwa na wasiokuwa Waislamu ambao hawajui chochote kuhusu Uislamu...Uislamu kama dini hulinda haki na haihitaji mwanamke mzee kuilinda au mwanamke kuitetea... Ningependa kumalizia kuwa nyinyi mmepotea ikiwa hiki ndicho mnachoamini na ningependa kuwataka mtubu kwa Mungu kabla wakati haujaisha.

  • Hamaam
    July 22, 2012 @ 09:26:35AM

    Ningependa kutuma salamu zangu kwa dada yangu Umeyma na wapiganaji wote wa vita vitakatifu. Ningependa kuwaambia waendelee kupigana vita vitakatifu kwa vile adui anakaribia kufa. Ujumbe wangu kwa wanafiki ni kuwa karibuni wataadhibiwa kwa uhalifu wanaofanya dhidi ya Uislamu. Naapa tutawamalizeni ikiwa tutapata fursa, Mungu akipenda.

  • nuur adiin cabdulaahi
    July 22, 2012 @ 05:17:32AM

    Vita vitakatifu ni moja ya matendo yanayosifiwa na Mungu lakini ni vipi hasa vita vitakatifu? Vita halisi vitakatifu ni vile vinavyoendeshwa kwa kuulinda Uislamu kama dini dhidi ya uchokozi wa wasiokuwa Waislamu kama ilivyoelezwa katika dini. Wasomali wamegawika katika makundi mawili linapokuja suala la vita vitakatifu: wale wanaotafsiri vita vitakatifu kama vita vinavyopiganwa dhidi ya Waislamu wenzao na wale wanaochukia kabisa vita vitakatifu na ni marafiki wa wasiokuwa Waislamu. Mungu awaunganishe Waislamu wote katika vipengele vya itikadi. Nur Abdullahi co. wa Burro.

  • X.A.Sadiiq
    July 21, 2012 @ 08:44:03AM

    Mtume wetu Mohammad (Amani Iwe Juu Take) hakuwapeleka watoto katika vita vitakatifu. Kwa hivyo, vipi tuwaambie akina mama ambao ni Waislamu kuwafundisha watoto wao kuhusu vita vitakatifu? Umayma hakuweza kutofautisha baina ya vita vya kisiasa au vita vitakatifu kwa kuelezea kile kinachoendelea nchini Somalia kama vita vitakatifu. Nadhani hatupaswi kusema uongo kuhusu dini na tusijenge uadui miongoni mwa watu kwa jina la mapenzi ya dini.

  • mubarik (suldan xadari)
    July 20, 2012 @ 01:28:57PM

    Kufa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mapenzi kwa Mwenyezi Mungu si kitu kimoja. Kufa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kunahusisha mtu kujitolea nafsi yake katika kulilinda dini.

  • hassan ali awil
    July 19, 2012 @ 12:02:25PM

    Hii ni ripoti nzuri isiyopendelea upande wowote ambayo haiungi mkono kikundi chochote au kukisema vibaya kwa kikundi chochote na ningependa kuifanyia kazi tovuti hii. Mimi ninaishi Burro na ninaleta ombi langu la ajira kwa unyenyekevu, kkkkkkkkkkkkkkkkkk.

  • amina ummu amiira
    July 19, 2012 @ 04:31:49AM

    Nadhani, kulea watoto katika njia sahihi na kwa kumuogopa Mungu ndio jambo zuri. Vita vitukufu vipo na vitaendelea mpaka siku ya mwisho. Nafikiri wakati umefika kusisitiza woga kwa Mungu na chuki kwa wasiokuwa Waislamu kwa watoto wetu kwa sababu chuki kwa wasiokuwa Waislamu sio vibaya kwa vile imeelezwa wazi katika dini – Uislamu, lakini ni dhidi ya Uislamu kuwapotosha watoto kiitikadi na kuwahusisha na vita. Asante sana.

  • mumtaz
    July 19, 2012 @ 04:28:49AM

    Katili anaewataka watu wawashambulie wenzao kwa mabomu na milipuko na ambae anajisifia vifo vyao hastahiki msaada wowote.

  • Mr. Jacalsame
    July 19, 2012 @ 12:34:39AM

    Maisha ni upendo……………………………

  • lovedoc
    July 17, 2012 @ 07:43:20PM

    Mimi ni kijana kutoka Tanzania ambaye asili yangu ni Somalia

  • Cuud Qaboobe
    July 17, 2012 @ 06:44:44PM

    Si sahihi kwa Wasomali kuichukua dini ya Kiislamu kama Waarabu waliokuwa wakimsumbua mtume (Amani Iwe Juu Yake.) Wasomali wanapaswa kuuchukua Uislamu kama inavyoelezwa katika Koran na mila za Mtume kwa mujibu wa tafsiri zilizotolewa na wanazuoni wa Kiislamu wa Somalia ambao hawafuati itikadi potofu. Tulikuwa tunajifunza Uislamu kutoka kwa wanazuoni waliokuwa wakiongoza kwa haki. Pia tunajua kuwa wanawake lazima wafuate amri za mume zao kitu ambacho wanakipinga siku hizi. Hii ni ishara ya wazi yakupotea kwa heshima binafsi na heshima kwa dini ya Kiislamu.

  • moh
    July 12, 2012 @ 07:57:13AM

    Asanteni nyote. Mwenyezi Mungu awabariki kwa wingi. Wale wanaomjua MUNGU wafanye lililo la haki.

  • shaafici
    July 8, 2012 @ 04:41:41AM

    Ni uchambuzi mzuri.

  • oday404
    July 8, 2012 @ 01:15:56AM

    Kwa kweli ni ujumbe mbaya ambao utawatenga watu na kuanzisha uadui miongoni mwao. Ninependa kuwaomba watu wasifuate itikadi za kigeni zenye kupotosha ambazo zitawaharibia mustakabali wao.

  • axmed tayo
    July 7, 2012 @ 08:46:54AM

    Ningependa kuwaombeni muwalinde wanawake wa Somalia kutoka kwa maadui kwa sababu wao ndio msingi wa kuwepo kwetu sote.

  • muwaxid jooga hargiesa
    July 7, 2012 @ 07:39:32AM

    Chuki zetu kwa wapiganaji wa vita vitakatifu na mapenzi kwa wasiokuwa Waislamu wanaoipiga vita dini yetu na ndugu zetu Waislamu, ni ishara ya wazi juu ya ujinga wetu kwa kile kinachoendelea ulimwenguni leo. Kuweni na tahadhari na wasiokuwa Waislamu, hawatawaokoeni.

  • c/risaaq
    July 7, 2012 @ 03:00:17AM

    Inasikitisha kwetu kuwa tunawafundisha watoto wetu wapigane. Na hii ndio sababu kwa nini Somalia imo ndani ya maafa. Nadhani ni sahihi kwetu kuwafundisha watoto wetu dini na tabia nzuri. Wale wanaoshikilia dhana ya kuwa tuwafundishe watoto wetu kupigana lazima wapigwe vita kwa sababu wanaingiza mila ambazo hazina mizizi katika dini yetu ya Kiislamu. Itikadi hii iliyoletwa na maandishi yasiyokuwa ya Kiislamu kwa sababu baadhi ya mambo yanayofanywa na al-Qaeda hayana mashiko katika Uislamu.

  • maxamuud
    July 7, 2012 @ 02:19:33AM

    Ni vizuri sana kwa wanawake watu wazima kufuata itikadi za kimagharibi na za wasiokuwa Waislamu na kuzikataa baadhi ya mila za Kiislamu. Ningependa kuwaomba wanawake kutubu kwa Mola wao kwa sababu ni vibaya sana kuidhihaki dini.

  • hibaaq husein barre
    July 4, 2012 @ 03:22:44AM

    Jina langu ni Hibaq Hussein Yarre na nina hasira kweli kweli kuwa sisi kama Waislamu tumefikia hatua ambapo hatuwezi kujua tofauti baina ya kile tunachofanya na kile ambacho dini yetu inatutaka tufanye au tusifanye hasa kuhusu vita vitukufu (Jihadi), ambacho ni kitu kinachotupeleka karibu ya Mwenyezi Mungu lakini tunapaswa kutambua kuwa umwagaji damu wa Waislamu wengine si sehemu ya Jihadi na tunapaswa kuona haya kutokana na mambo hayo; zaidi, ni kuwa wale wanaofanya hivyo wanadai kuwa hiyo ni kazi ya dini. Ndugu zangu, ninawaomba mrejee kwa Mwenyezi Mungu hasa wale wanaodai kuwa ni al-Qaeda. Chochote unachofanya ulimwenguni hapa utatakiwa kujibu mbele ya Mungu na unahitajika kuifikiria adhabu inayokusubiri akhera.

  • mohamed
    July 4, 2012 @ 12:55:53AM

    Mungu ni mwema, hii sio vyema.

  • ام عاشة
    June 28, 2012 @ 12:29:13PM

    Tumefurahi sana kuhusu ujumbe huu, tunawaambia maadui: Kufeni na mfundo!

  • naciimo
    June 28, 2012 @ 12:23:49PM

    Nimefurahi sana kwa wimbi jipya la kujilinda wenyewe kutoka kwa maadui wetu, jambo litatuletea mafanikio ambayo ndiyo yanayotakiwa na Wasomali wote.

  • khadar
    June 28, 2012 @ 11:17:57AM

    Kuwa Muislamu maana yake nini? Je, kuwa Muislamu kunajihusisha na itikadi maalumu au kufuata mafundisho ya Koran Tukufu na mila za Mtume? Ikiwa jawabu ni kufuata Koran Tukufu na mila za Mtume, hivyo hupaswi kufuata itikadi ya kikundi au sekta yoyote na kila kinachojulikana kama demokrasia inayopingana na dini ya Kiislamu. Ningependa kuwaambia akina mama kujifunza dini kwanza na kulea watoto wao kwa mujibu wa dini. Vita vitakatifu ni lazima kwa kila Muislamu mwanamke na mwanamme wakati ambapo dini ya Kiislamu inakandamizwa.

  • Cabdi
    June 28, 2012 @ 05:42:34AM

    Amani iwe juu yenu. Mlichoandika ndugu zangu ni dhambi tupu. Mmeonesha vita vitakatifu kama ni fujo ambazo hazipaswi kufundishwa kwa watoto wadogo. Hili ni kinyume na dini yetu na hampaswi kuzungumza vibaya kuhusu dini yetu kwa sababu ya chuki kuhusu kikundi fulani. Tubuni kwa Mungu ndugu zangu wapendwa. Mimi siungi mkono wala sijiainishi na kikundi chochote wa sekta lakini ninapinga kuzungumzwa uovu juu ya Uislamu na vita vitakatifu.

  • nawaal
    June 28, 2012 @ 02:43:32AM

    Wazazi wanaowaruhusu watoto wao kujilipua wenyewe kwa mabomu ya kujitoa muhanga ni wapuuzi na ninamuomba Mungu kuwaongoza katika njia sahihi, Mungu akipenda.

  • KHADAR
    June 27, 2012 @ 11:18:15PM

    MKE WA MPIGANAJI WA VITA VITAKATIFU ZAWAHIRI NI MPIGANAJI MWENYE BUSARA WA VITA VITAKATIFU ANAYEIPENDA DINI YAKE NA KUFANYAKAZI KWA AJILI YA MWANAMKE HUYU WENGINE ANAYEJULIKANA KWA KUWA MKRISTO MKALI NA ANAYEPINGANA NA YEYOTE AKIFANYAKAZI KWA AJILI YA MUNGU.

  • geesiga magabade
    June 27, 2012 @ 10:30:52PM

    Mungu apishie mbali. Mwanamke huyu anayejiita Anab ameasi kutoka dini ya Kiislamu kwa kudhihaki sharia ya Kiislamu na kupinga mmoja miongoni ya minara inayozawadiwa watu peponi hasa wale wanaokufa katika vita vitakatifu. Aliisema vibaya moja ya misingi ya sharia ya Kiislamu wakati akitumikia shirika lisilo la Kiislamu. Mwisho lakini sio yote, ningependa kumshauri Anab kutubu kwa Mwenyezi Mungu asiutaje vibaya Uislamu, ikiwa anashindwa kutubu kuhusu dhambi aliyofanya atasafishwa na wapiganaji shijaa wa vita wasiogopa yeyote isipokuwa mwenyezi Mungu, Mungu akitaka.

  • mohamed abdullahi carey
    June 27, 2012 @ 11:55:41AM

    Mpiganaji wa vita vitakatifu ni yule anayekufa kwa ajili ya Mungu na msaliti ni yule anayepigana dhidi ya vita vitakatifu.

  • Bernard
    June 27, 2012 @ 07:30:49AM

    Tangiaumaarufu wake kwamba watoto na vijana ni shabaha mpya ya magaidi kwa vurugu, wakati umefika kwa akina mama somali na viongozi wa kukuza maadili mema kwa watoto na vijana. kutokujua kusoma na kuandika miongoni mwa makundi haya mawili ambayo ni baadaye ya nchi somali na zaidi hivyo, kujaribu na kuingiza mwao upendo kwa ajili ya amani na kukuza maisha. Kitu kingine, serikali inapaswa kuzingatia kuondoa umaskini ambayo inaweza kuwa sababu nyingine vijana wako shabaha magaidi haya.

  • Mubashir Hayow Ahmed
    June 27, 2012 @ 06:51:29AM

    Ni wajibu wa kila baba na mama na kuleta watoto wao kulingana na Uislamu na kuwafundisha juu ya vita vitakatifu lakini sio kuwadhuru Waislamu wengine na wasiokuwa Waislamu kwa sababu hii ni kinyume kabisa na Uislamu. Uislamu hufundisha kuhusu kuwa na huruma kwa viumbe hai wote. Ningependa kuwaambia wanawake wa Somalia wanaojiita wanaharakati wa haki za binadamu au wanaotetea usawa wa kijinsia kwamba Uislamu umeeleza wazi haki za wanawake kwa kiasi kwamba wanaruhusiwa kushiriki katika vita takatifu na kwa sababu hii hoja yako ziwe na msingi juu ya dini.

  • muuna cabdiraxmaan xasan xaaji
    June 27, 2012 @ 04:32:26AM

    Ningependa kusema kwamba wametugusa mioyo yetu kwa kuwaachia huru wanawake wawili. Nadhani al-Shabaab wanapaswa kukumbuka nini wanafanya kwa sababu wao pia na watoto na wasiwaue au kuwateka watoto wa wengine na akina mama. Napenda pia kuwaambia kuwa haki iko njiani na wataadhibiwa kwa ajili ya makosa wanayofanya dhidi ya jamii. Nchi yetu itakuwa ya amani hivi karibuni, Mungu akitaka.

  • Hamid samer
    June 26, 2012 @ 01:46:20PM

    Unafikiri nini? Huyu ni kichaa kama mume wake. Wanawataka watu wafanye ugaidi na wao wanajificha kama panya. Mungu awaapize na kikundi chao cha kigaidi. Al-Zawahiri amefilisika na hawezi kufanya chochote na kitu pekee anachoweza kufanya ni kujionyesha katika vyombo vya habari kama kwamba bado ni imara na kikundi chake kilichoporomoka bado kina uwezo wa kutisha watu. Al-Zawahiri wewe ni kichekesho tu!

  • Jsam
    June 26, 2012 @ 05:40:17AM

    Kwa kweli ningekuwa na uwezo...... hawa magaidi wanastahili kifo hata kabla hawajatungiwa mimba..... Hakuna MUNGU wa vurugu na kujitoa muhanga kwa kisingizio cha kumtetea mungu... hivi ni MUNGU gani huyo asiye na nguvu hadi kuhitaji mwanadamu mdhaifu kama gaidi amtetee? Hamuoni kwamba huyo siyo MUNGU bali ni mwnadamu tu? MUNGU ninaemjua mimi haitaji msaada wa kiumbe chake katika kupambana na uovu maana yeye akitamka tu mambo yanakuwa. Kama kweli MUNGU wa magaidi yupo,... wamwambie atamke mambo yatokeee..... MUNGU wangu anaweza kufanya hayo kama alivyotamka kila kitu kikawepo duniani na sayari zote. Hata sasa anaweza kutamka chochote kikatokea....

  • KAMGISHA
    June 26, 2012 @ 01:30:01AM

    Uislam ikiwa ni diniya haki ni wajibu kila muslims awe tayari kulinda fikra, uhuru, na amani, kwa sababu huo ndio msingi wa UISLAM hajalishi ni eneo gani ulilopo mithali upo katika ulimwengu wapaswa kusimamia haki Haieti picha kama baadhi ya watu wanaua wenzao kwa misingi ya kuleta Amani, kisha wengine wakitenda matendo hayo hayo waitwe MAGAIDI, Naamin umefika wakati sasa Waislam wote ulimwenguni kushikamana na kupinga dhuluma zidi yao . Jamii ya kiislam popote ilipo ni ndugu hakuna mipaka ya kijoglaph katika uislam ujumbe wa mke wa ZAWAHIR ni mhim sasa kuzingatiwa na jamii nzima ya Waislam kuwajenga watoto katika TAWHD sio kosa na TAWHD ndio msingi wa kuikataa Dhuruma, siku zote haki haichangamani na Batwil ni lazima kimoja kishinde aidha HAKI au BATWIL na siku zote haki uishinda batwili na Amin hata SOMALIA ipo siku haki itashinda hao mujahidi na hao wanao ua Raia na kubaka Wanawake kwa kisingizio cha kulinda Aman watashindwa tu .

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo