Siku ya Wakimbizi Duniani yagubikwa na hali ya kutokuwa na usalama katika kambi ya Dadaab

Na Bosire Boniface, Wajir

Juni 22, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Hali ya kutokuwepo na usalama katika makambi ya Dadaab Mkoa wa Kaskazini Mashariki ya Kenya ndio wasiwasi mkubwa miongoni mwa wale wenye dhamana ya ustawi wa wakimbizi, serikali na maafisa wa misaada waliiambia Sabahi.

  • Wasomali katika kambi ya Dadaab kaskazini mashariki mwa Kenya wakihudhuria sherehe za kuadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani mwaka huu hapo tarehe 20 Juni. [Na Abdullahi Mire/AFP]

    Wasomali katika kambi ya Dadaab kaskazini mashariki mwa Kenya wakihudhuria sherehe za kuadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani mwaka huu hapo tarehe 20 Juni. [Na Abdullahi Mire/AFP]

Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa Kenya Emmanuel Nyabera alisema tishio la usalama limeathiri vibaya sana usambazaji wa dawa na msaada wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi 500,000 katika makambi ya Dadaab yenye makambi ya Hagadera, Ifo, Ifo II na Dagahaley.

“Kila mmoja miongoni mwa wakimbizi, wafanyakazi wa misaada, vyombo vya kuimarisha sharia na jamii za wenyeji zinaathiriwa na shughuli za kigaidi za wanamgambo wa al-Shabaab na vigenge vingine vya kigaidi katika makambi,” Nyabera aliiambia Sabahi.

Alisema wakati wafanyakazi wa misaada wanakabiliwa na mandhari ya utekaji nyara, mabomu ya kuzika ardhini na mashambulizi ya mabomu kutoka kwa washirika wa al-Qaeda, kikundi cha al-Shabaab, mambo yanayoathiri morali katika kambi.

Mwaka jana, al-Shabaab waliwateka nyara wafanyakazi watatu wa misaada ambao ni Madaktari Wasio na Mipaka makambini. Hili lilifuatiwa na wimbi la mashambulizi ya mabomu ya kuzika ardhini na maguruneti ambayo yaliua maafisa kadhaa wa usalama wa Kenya na mauaji ya kutumia silaha ya viongozi wa wakimbizi.

Hapo tarehe 15 Juni, watu watatu, akiwemo kiongozi mwanamke wa wakimbizi, walijeruhiwa wakati kifaa cha mlipuko cha kutengeneza kilipolipuka katika kambi ya Ifo.

Nyabera alisema kuwa mashambulizi ambayo hayachagui yameeneza hofu makambini na kuzidisha changamoto za usambazaji wa misaada.

Alisema Siku ya Wakimbizi Duniani mwaka huu, iliyoadhimishwa hapo Jumatano (tarehe 20 Juni), ilifanyika huku kukiwa na hisia za “mashaka na woga" katika makambi yote ya wakimbizi ya Dadaab.

Siku ya Wakimbizi Duniani ina lengo la kupeleka mwamko wa kimataifa juu ya hali mbaya za wakimbizi na hali ilivyo makambini. Kauli mbiu ya mwaka huu, “Kila mtu mmoja anayelazimishwa kukimbia ni mmoja katika wengi zaidi”, inadhamiria kuonesha mazingira yanayosababisha watu kuwa wakimbizi na kuhamasisha njia za kuwalinda, alisema.

“Siku iliadhimishwa katika makambi yote kwa maonesho ya kitamaduni, lakini msemaji baada ya msemaji alilalama kuhusu hali ya kutokuwepo kwa usalama,” alisema.

Kuhakikisha usalama makambini

Hata hivyo, Nyabera alisema UNHCR inafanyakazi pamoja na viongozi wa Kenya ili kuleta hali ya kawaida makambini, Alisema UNHCR ilitoa magari ili kusaidia doria za polisi na kuweka vifaa vya usalama vya mawasiliano ili kuwepo na hatua za haraka pale panapotokea wasiwasi juu ya usalama.

Viongozi wa Kenya waliiambia Sabahi kuwa wanafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kuwa kila mtu makambini yuko salama.

Afisa mwendeshaji wa polisi huko Dadaab George Kingi alisema si chini ya mipango 10 ya mashambulizi kutoka kwa washukiwa wa al-Shabaab yalizimwa mwezi uliopita. Alisema maafisa wa polisi wamejitolea maisha yao ili kurejesha utulivu makambini.

“Ni dhamana yetu kuimarisha sharia na kanuni na jamii ya wakimbizi wametekeleza wajibu wao katika kutoa habari muhimu sana ili kuzuia uhalifu,” Kingi aliiambia Sabahi.

Alisema idadi kubwa sana ya wakimbizi makambini inaleta changamoto kubwa za usalama, ambapo baadhi ya watu wenye dhamira za kihalifu wanajifanya kama wakimbizi. Kingi alisema viongozi wanafanyakazi na jamii ya viongozi wa wakimbizi ili kuzuia udanganyifu.

Alisema doria za usalama na kuwepo kwa wanaintelijensia kumeimarishwa makambini.

Mkimbizi aliyezungumza na Sabahi alisifu juhudi zinazofanywa na maafisa wa usalama. Fatuma Hussein Ali mwenye umri wa miaka 47 anayeishi katika kambi ya Ifo, alisema wakimbizi wenyewe wanakuwa walinzi dhidi ya wakorofi.

“Nina imani kuwa, kwa ushirikiano baina ya wakimbizi na maafisa wa usalama, al-Shabaab watashindwa,” alisema. “Hii ni kwa manufaa ya wakimbizi na kila mtu hapa Dadaab.”

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 7)

Dislike_icon(3)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Ahmed Kaafi
    June 26, 2012 @ 11:03:38AM

    Umoja wa Mataifa umekuwa mstari wa mbele nchini Somalia ili kusukuma ufumbuzi kwa njia ya amani miongoni mwa koo tofauti na juhudi zao zinazaa matunda. Umoja wa Matiafa pia umekuwa dhamana kwa kuomba uingiliaji kati kijeshi ili kusaidia kuwapiga al-Shabaab. Umoja wa Mataifa uliweza kuhamasisha vikosi kutoka mataifa kadhaa ya Kiafrika na sasa ni suala la wakati tu kabla ya al-Shabaab kushindwa moja kwa moja. Umoja wa Mataifa pia umezihamasisha taasisi yasiyo ya kiserikali kusaidia chakula na matibabu kwa watu wa Somalia wanaoteseka. Vilevile Umoja wa Mataifa imefanya juhudi za kuleta wawekezaji ili kuwekeza nchini na kuboresha uchumi wa nchi. Halikadhalika, Umoja wa Mataifa umejihusisha na serikali ya shirikisho na imekuwa ikitoa ushauri na njia nyingine za misaada. Pia, Umoja wa Mataifa imefanya juhudi kubwa sana na watu wa Somalia wanawadaiwa Umoja wa Mataifa kwa baadhi ya mafanikio waliyopata.

  • moses ikere
    June 25, 2012 @ 08:47:34AM

    Kinaendelea nini?

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo