Afgoye imerudi katika maisha ya kawaida baada ya kuwa chini ya udhibiti wa al-Shabaab kwa miaka kadhaa.

Na Adnan Hussein jijini Mogadishu

Juni 22, 2012

  • 3 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wakazi wa Afgoye kwa mara nyingine tena wanafurahia utulivu wa mji wao baada ya vikosi vya Somalia na vikosi shirika kuwaondoa al-Shabaab mwezi uliopita.

  • Kamanda wa kikosi cha Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM)  luteni Jenerali Andrew Gutti akihutubia askari huko Afgoye mapema mwezi huu baada ya kuukomboa mji huo kutoka kwa al-Shabaab. [Stuart Price/AU-UN IST/AFP]

    Kamanda wa kikosi cha Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) luteni Jenerali Andrew Gutti akihutubia askari huko Afgoye mapema mwezi huu baada ya kuukomboa mji huo kutoka kwa al-Shabaab. [Stuart Price/AU-UN IST/AFP]

Wakati wa kipindi cha miaka mitano ya al-Shabaab kuidhibiti Afgoye, wakazi waliishi katika hali duni na wakulima walikuwa katika shinikizo kubwa, linaloshuhudiwa na kudidimia kwa uzalishaji wa kilimo. Wakulima hawakuwa tayari kutoa nusu ya mazao yao kwa al-Shabaab kama “kodi”.

“Mji wetu ni mzuri kwani unaweza kuona mabwawa ya maji ya kuchimbwa, ndizi na miti ya maembe ya kijani muda wote inayoongeza zaidi uzuri na fahari ya sehemu hii ya kuvutia,” mkazi wa Afgoye Bakar Omar aliiambia Sabahi. “Tuna Mto Shabelle unaotiririka maji wakati wote, bila kusahau chemchem zilizotawanyika na hewa mwanana. Kila mahali unapokwenda, utaona pazuri na patulivu”.

Afgoye ni mji wa kihistoria ulio kilometa 30 Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu. Kuna madaraja mawili ambayo yanawezesha uvukaji wa mto Shabelle, ambao unakatiza katikati ya mji na boti mbili za kutengenezwa kwa mbao zinazobeba abiria kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. Wakulima humwagilia mashamba yao kwa maji yanayotokana na vijito na msimu wa mvua.

Watu wanaoishi katika mji huu wanakadiriwa kuwa 250,000 na wakazi wake wengi wanafanya kazi za kilimo na uwindaji. Afgoye ni kituo muhimu cha biashara kwani upo kando kando ya barabara ya kuelekea Kismayo, Baidoa, Marka na Mogadishu.

Bille Ahmed Abdullahi, mfanyabiashara wa ndani ambaye amebobea katika uzalishaji wa malimao yaliyokaushwa, alisema Afgoye unajulikana kwa mazao mbalimbali, yakiwemo ndizi, maembe, limau, nyanya, machungwa machungu, kiazisukari, bamia na matango. Mji huu pia unajulikana kwa mbegu za ufuta zinazogandamizwa na mashine kutoa mafuta ya alizeti.

Wanakijiji wa ndani ambao wanategemea wanyama wafugwao kama vile ngamia, kondoo, ng’ombe na kuku wanawapatia wageni maziwa na mtindi kama ishara ya ukarimu, kwa mujibu wa desturi, alisema.

Serikali ya Somalia yaongeza msaada kwa Afgoye.

Kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa kilimo, serikali ya Somalia inapanga kuwapa wakulima mbegu, mbolea na viuavidudu visivyo na kemikali, alisema Kamali Abdullahi Abdi Ahmed, Mkuu mpya wa Afgoye.

“Tunasaidia moyo wa ushirikiano kati ya [wakulima] ili kuwa na hisia ya jamii wakati wanapoadhimisha matukio ya furaha na mabaya ya kijamii na kuvuna mazao kama vile ngano na ufuta” Ahmed aliiambia Sabahi.

Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alikaa usiku kucha katika shamba huko Afgoye wiki iliyopita, wakati alipokutana na viongozi wa kikabila wa ndani kuunda bodi ya wakurugenzi kwa ajili ya manispaa hiyo. Hii itafanya Afgoye kuwa mji wa kwanza kukombolewa kutoka kwa al-Shabaab kufurahia utawala wa ndani uliochaguliwa, kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya kisiasa Jamila Hanafi.

Hanafi aliiambia Sabahi kuwa kamati ya fedha itawajibika katika kukusanya kodi za mji huu na kuzifanyiakazi ya kurejesha huduma za kijamii kama vile shule na hospitali na kukarabati mitaa mikubwa ya mji huu.

Mohamed Baraako, mkazi wa Afgoye, aliiambia Sabahi kuwa watu wa ndani wanatokea katika makabila mbalimbali lakini wameunganishwa na maadili makubwa kama vile ukarimu, uthubutu, upole, huruma na uaminifu.

Pasipo al-Shabaab, watarudia njia yao ya kwanza ya upendo na amani, hawatachukua silaha, alisema.

“Wakazi wa Afgoye kwa ujumla wana amani na maisha yao yametiwa alama ya urahisi na umaskini, lakini hatakufa njaa kwa sababu ardhi yao yenye rutuba inazalisha matunda mengi na mazao,” Barako alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 48)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • abdi dheere
    June 26, 2012 @ 11:20:56AM

    Al-Shabaab wamekuwa wakiendesha uhalifu wa mauaji dhidi ya ubinadamu nchini Somalia pamoja na uharibifu wa mali. Uhalifu wao unazidisha ukali tu, kwanza walianza na utekaji nyara wa watoto na kuwapa mafunzo ya uaskari. Hili ni kinyume na kanuni za haki za binadamu, hawa ni watoto hao wanaopelekwa mstari wa mbele wa vita na wanaotumia kama walipuaji mabomu ya kujitoa muhanga. Al-Shabaab pia wamekuwa dhamana kwa mauaji ya wananchi wao wenyewe na watu wasio na hatia katika nchi jirani. Kikundi hiki cha kigaidi kimekuwa dhamana wa uharibifu wa mali kwa kupiga mabomu maduka, hoteli na majengo mengine makubwa. Hili limepelekea upotevu wa mamilioni katika uharibifu wa mali. Pia kikundi kinahusika na uharamia ambapo wanateka nyara meli za mizigo katika bahari kuu na kutaka pesa nyingi za kukombolea ili waziachie huru meli hizo. Vile vile, al-Shabaab wamesababisha mateso kwa famili nyingi kwa sababu ya kuvunjika kwa viungo vya familia na kuzilazimisha kuwa wakimbizi.

  • muse
    June 25, 2012 @ 01:59:15AM

    Ikwa al-Shabaab watamalizwa, Somalia itapata amani kwa baraka za Mungu.

  • abdiqadir
    June 24, 2012 @ 04:47:51AM

    Tangazo kwa wanaohusika. Mimi ni Msomali, mwanamme, niliyezaliwa Kaskazini ya Somalia ambayo sasa inaitwa Somaliland, ninayependa Somalia iungane kama ilivyokuwa kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza. Hata hivyo, kurejea katika muungano wa Somalia ni vigumu. Nahisi tungejaribu tunavyoweza kufanya ili kuiunganisha tena Somalia. Ndugu zangu wapendwa, tusiweke maslahi yetu kabla ya maslahi ya nchi na hebu tufikiri vipi tunaweza kuilinda nchi yetu kutoka kwa maadui zetu. Tusijaribu kurejea mazingira mabaya ambayo tumekuwemo, kutoka vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kujitenga ni njia pekee inayowezekana katika nchi ambayo ina mafanikio lakini kwa hali yetu ni tofauti kabisa kwa sababu tumeharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeua akina baba, akina mama, dada, kaka wengi na kuacha mayatima wengi nyuma. Tusijigawe kwa misingi ya makabila na majimbo. Sisi sio ndugu? Tusahau kila kitu na kujikusanya pamoja na kuwa jamii moja. Vipi tutaweza kuungana? Mchakato wa kutuunganisha unaendelea, tuutakie kila la heri.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo