Tanzania yajiandaa kufufua mpango wa Jeshi la Kujenga Taifa

Na Deodatus Balile, Dar es Salaam

Juni 21, 2012

 • 17 Maoni
 • Chapisha
 • Panga upya Punguza Ongeza

Tanzania inajiandaa kurejesha mpango wa taifa wa jeshi la Kujenga Taifa, ambao ulisitishwa miaka 20 iliyopita, kufuatia wito wa kufufuliwa kwa shughuli hizo kama chombo cha mshikamano wa kijamii.

 • Vikosi vya ulinzi vya jeshi la Tanzania wakicheza gwaride Dar es Salaam. Serikali ilitenga pesa katika bajeti ijayo ili kurejesha mpango wa taifa wa Jeshi la Kujenga Taifa. [Na Mwanzo Milinga/AFP]

  Vikosi vya ulinzi vya jeshi la Tanzania wakicheza gwaride Dar es Salaam. Serikali ilitenga pesa katika bajeti ijayo ili kurejesha mpango wa taifa wa Jeshi la Kujenga Taifa. [Na Mwanzo Milinga/AFP]

Mpango huo ni mafunzo ya kijeshi ya mwaka mmoja ambapo Watanzania watatakiwa kushiriki kabla ya kujiunga na taasisi za elimu ya juu.

Mpango wa jeshi la Kujenga Taifa ulianzishwa mwaka 1963 na rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere. Ulisitishwa mwaka 1994 baada ya ukosefu wa fedha.

Pamoja na mafunzo ya kijeshi yenye kiwango, mpango huu pia hutoa mafunzo juu ya haki za binadamu, elimu ya uraia, na historia ya Tanganyika na zanzibar, na pia unakusudiwa kuamsha hisia za umoja na uzalendo kwa wanafunzi.

Waziri wa Fedha wa Tanzania William Mgimwa aliliambia bunge wiki iliyopita kuwa kisasi cha shilingi bilioni 7.5 (dola milioni 4.7) zitatengwa katika bajeti ijayo ili kufufua mpango wa Jeshi la Kujenga Taifa.

Kwa kuanzia, wanafunzi 5,000 tu wahitimu wa elimu ya juu watachaguliwa kushiriki katika mpango huo.

Wabunge wanatarajiwa kupigia kura bajeti ya nchi siku zijazo.

Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa aliukaribisha uamuzi wa kuanzisha mpango huu, kwa kusema Jeshi la Kujenga Taifa liliwapa wanafunzi kutoka matabaka tofauti fursa ya kukaa pamoja kabla ya kujiunga na chuo kikuu na kujifunza kuhusu uzalendo na maadili ya Tanzania.

Nimefurahishwa sana na uamuzi huu. Ninayachukulia mafunzo ya jeshi la Kujenga taifa kama moja ya nguzo za taifa zetu,” Lowassa aliiambia Sabahi. “Jeshi limekuwa chombo muhimu cha kuwaunganisha Watanzania tangu kuanzishwa kwake mwaka 1963.” Lowassa alisema umuhimu wa mpango huu haupaswi kudharauliwa.

Alisema baadhi ya majirani wa Tanzania wameshindwa kufikia makubaliano katika nchi zao, jambo ambalo limechangiwa na kutokuwa kwao na utulivu. Tanzania imeweza kujitofautisha katika hilo kutokana na Jeshi la Kiujenga Taifa, alisema.

“Amani yetu haiwezi kutenganishwa na Jeshi la Kujenga Taifa,” Lowassa alisema.

Kujenga kujiamini na kuimarisha umoja

Simon Mokiwa, mwenye umri wa miaka 42 na mkazi wa Dar es Salaam, ambaye alitumikia Jeshi la Kujenga Taifa katika kambi ya Bulombola Kigoma mwaka 1991, alisema shughuli hizo zilisaidia kujenga moyo wa ushindani na mtu kukabiliana na utofauti wa Tanzania.

Alisema vikwazo ambavyo kuruta walikabiliana navyo wakati wa kutumikia viliwasaidia kukua na kujitarajisha vyema kwa kazi na kuishi popote Tanzania. “Vikwazo tulivyokabiliana navyo wakati wa Kujenga Taifa ndivyo vilivyotukuza," Mokiwa alisema.

Mokiwa aliiambia Sabahi kuwa jeshi la Kujenga Taifa liliwasaidia vijana kujiamini wakati huo huo kujenga hisia za umoja.

“Liliwaunganisha Watanzania wa asili mbali mbali,” alisema. “Wahindi, weupe na weusi walikwenda kambini, kufunzwa, kulima mashamba pamoja, bila ya kujali asili za familia zao. Nafikiri ni kitu kizuri kwa kizazi kipya na kwa taifa letu pia.”

Luteni kanali Hashim Mzava, afisa wa jeshi mstaafu, aliiambia Sabahi kuwa kufufuliwa kwa mpango wa Jeshi la Kujenga Taifa kutasaidia kuwajenga vijana na maadili mema ya kazi.

“Kujenga Taifa si mazoezi ya kiwiliwili tu, kunafanya mengi zaidi ya hilo. Kunaingiza nidhamu katika kizazi hiki kipya,” Mzava aliiambia Sabahi. “Watafunzwa mambo mengi kuhusu Tanzania na maslahi ya taifa. Haya hayafunzwi katika mtaala wa kawaida wa shule.”

Ikiwa serikali iko makini kuhusu kuugharimia mpango huu, lazima itenge pesa zaidi, alisema mwanauchumi Honest Ngowi.

Ngowi, ambaye anafundisha katika Chuo Kikuu cha Maumbe, alisema wanafunzi 5,000 ambao sasa serikali imeshawapangia bajeti, ni sehemu tu ya wanafunzi 700,000 wanahitimu elimu ya juu kila mwaka.

Ikiwa Watanzania wote watahitajika kushiriki katika mpango huu kabla ya kujiunga na chuo kikuu, lazima pesa nyingi zaidi ziingizwe ili kuuendeleza, alisema.

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

 • kibaha sec school
  July 5, 2014 @ 04:30:32PM

  Inabidi wanafunzi wafuatiliwe.kwa umakini.zaidi ili wasigeuze jeshi kama danguro yaan kufanya vitendo vya.zinaa

 • sophie
  May 17, 2014 @ 12:03:52AM

  Ni wazo zuri kwa kujenzi wa taifa imara.

 • Lenard shelembi
  April 15, 2014 @ 11:47:31PM

  Mim naishukulu sana serikar kwa maamzi hayo maana tupo vijana wengi ambao tunapenda kujiunga na mafunzo lakn tunakosa namna naiomba serikar itusaidie kwa hilo.

 • renus ferdinand kitego
  October 18, 2013 @ 04:00:49AM

  Jeshi ni wito na sio ajira hivyo umefika wakati wa jeshi kuangalia utayari wa mtu kuliko vyeti na umri ili tupate wazalendo...tuachane na utumwa wa kuangalia makaratasi(vyeti)bali utendaji wa mtu hiki ndo cha msingi jeshini.

 • Peter
  July 18, 2013 @ 10:37:34AM

  Kwa maslahi tu, nchi nyengine nyingi hazina jeshi la kujenga taifa lakini vijana wao wanajiamini kweli......

 • Aggrey Kigodi
  June 28, 2013 @ 06:11:17AM

  Naipongeza sana serikali kwa uamzi mzuri kwasababu hii itawafanya vijana wajiamini na kuwa wawajibikaji na hasa kujitambua,naipongeza sana serikali kwa kurudisha mfumo huo mzuri. Mimi napenda sana jeshi lakini sasa nashindwa nifanyaje kwaani umri wangu unaniruhusu nina umri wa miaka 23,na nimehitimu kidato cha sita mwaka huu...naombeni sana msaada wenu.

 • dismas .s. kimario
  June 24, 2013 @ 02:29:01AM

  mi naona n bora maana vijana wa darasa la saba tunapata shida sana tuna bakina vipaji vyetu huku tukiwa tunapenda sana maswala ya kujiunga na jeshi

 • Baraka nassoro said
  May 9, 2013 @ 10:48:58AM

  N mpango mzur ambao serikali inao lakini je kuna malipo yoyote ambayo mtakuwa mnatupatia maana wengine familia zetu zinategemea tumalize form six tuanze kuzisaidia kwa matatzo madogomadogo kabla hatujaenda chuo,so me nilikuwa naomba yawepo malipo kidogo ambayo yatatusaidia kuzikwamua familia zetu. Ahsante

 • Seche loulo
  March 26, 2013 @ 05:41:07PM

  Ninaona maana katika hili....maoni ya wananchi yanapendekeza kwamba badala ya kupoteza pesa chache tulizonazo juu ya hili!!! Serikali inapaswa kufuata mpango mkubwa wa kuboresha kiwango cha elimu ya Tanzania na ifanyie kazi kuimarisha vikosi vya usalama vya nchi!!! Serikali isilazimishe wasomi wa kabla ya chuo kikuu juu ya hili. Baada ya yote, sioni tafauti iliyopo miongoni mwa walewaliipata nafasi ya kujiunga na jeshi la kujenga taifa na wale ambao hawakufanya baada ya fmupi...vitabu vya kuandika....vitabu vya kusoma kamamvile gwa marufuku mwaka 1994...tafadhalini, tumieni fedha vizuri...serikali imekaa kama haiwajibiki katika uamuzi wake wa. Inasikitisha kwamba viongozi wewtu wenyewe walilifikiria hilia nahawakutoa vitu vya lazima kama vile ....vitabu...watu masikini....masikini na miundombinu

 • Juma Mpangule
  March 16, 2013 @ 04:23:27PM

  GOLI LA MBALI HILO,HAKUNA WA KULALAMIKA! CHA KUJIULIZA NI 1.JE WOTE WANAOENDELEA WANALAZIMISHA WATU KWENDA JESHINI? 2. WALIOENDA JESHINI WAKATI HUO NI WANASIFA TUNAZOZITEGEMEA JESHINI? 3. KWENYE UTAIFA,NINI TOFAUTI YA ANAEPITA JESHINI NA ASIYEPITA. WENGI WAPE, MIMI SIKUBALIANI NA KULAZIMISHA WATU KWENDA JESHI, SERIKALI IBORESHE TU MAJESHI YAWEZE KUAJILI WATU WENGI BASI NA KUWAWEZESHA KUCHANGIA KATIKA TAIFA. Yaani, majeshi yawe sehemu ya kupita na kubaki kwa anayependa basi. Peleka bajeti yote hiyo kwenye kununua matreka na kulima masamba makubwa,siku chache kilimo cha mkono historia.

 • JOFREY A.JOHN
  March 1, 2013 @ 01:29:31PM

  HONGERA SERIKARI YA TANZANI KWA KURUDISHA "National service program" NA MIMI NI MMOJA WA WAHUSIKA TOKA LINDI HIGH SCHOOL-JOFREY JOHN

 • oscar stuart
  February 24, 2013 @ 01:59:17AM

  yani baada wa jadili wasomi watafanye ktk taifa.wa na zungumza upumbavu.

 • Rebacca Kurubai
  January 28, 2013 @ 06:07:35AM

  Bila ya kuwa na uzoefu wa jeshi la kujenga taifa nisingekuwa hivi nilivyo leo. Ninapendekeza lifufuliwe na litasaidia jamii yetu kuweza kujilinda wenyewe na maisha ya kujitegemea. Kumbukeni tu kuwa kizazi hicho cha wale waliokwenda Jeshi la Kujenga Taifa bado kipo.

 • Dr. Emmanuel Kandusi
  January 1, 2013 @ 09:58:40AM

  Tafadhali naomba procedure nahitaji kijana wangu ambaye kamaliza Form 6 na kufaulu Div. 2. Nahitaji apitie NS kabla hajaendelea na masomo ya juu. Ahsante. Dr. Kandusi

 • Isaya Yonamu Ngao
  July 30, 2012 @ 12:51:57AM

  Ndio! Ni wazo zuri. Kurejesha Jeshi la Kujenga Taifa ni jambo lenye masilahi makubwa. Mtu anayepitia JKT ana uwezo wa kuishi popote, mimi mwenyewe nilipelekwa Ruvu katikati ya mwaka 1982 kama kuruta na baadaye Buhemba kama mtu wa huduma kwa miezi sita. Siku hizo hakukuwa na njia ya kuaminika kuelekea Kilwa (Lindi) lakini niliweza kusafiri na iliyokuwa MV Lindi kwenda Kilwa kwa siku tatu na kubakia huko kwa raha. Nina hakika kile nilichokiona kule haiwezekani kukishughulikia bila ya uzoefu wa JKT. Napendekeza wafanyakazi wote wa kuanzia mwaka 1995 wajiunge na JKT, waripoti makambini kupatiwa mafunzo. Hii ni kwa sababu wengi wao ni wavivu na msingi wa migomo katika nafasi za kazi. Ndio, hili ni kweli.

 • Laurenti Masui
  June 24, 2012 @ 02:06:16PM

  Jamani hapa ndipo ninapopata shida sana kuelewa kwa nini watu hatujui tunafanya kitu gani; hebu tujiulize hilo jeshi tunalotaka kurudisha lina tija ipi? achilia hoja viza ya uzalendo inayotangulizwa kila kukicha> Hao tunaowalaumu kwa kutokuwa wazalendo wote walipitia jeshi hilo hilo. Jamani hiyo pesa tuitumie vizuri kutoa elimu nzuri na bora kwa wanafunzi wa shule za sekondari kama vile kuwapatia mabweni na chakula. pamoja na mambo mengine sisi tuliokuwa jeshini nyakati zile tunajua kuwa ndio kwanza wanaanzisha mgodi mwingine wa kula na kutafuna pesa. Hebu tutafakari tuache ushabiki!

 • Kazaura Isdori
  June 23, 2012 @ 06:14:33AM

  Mpango huu ni mzuri ambao ulichelewa kurejeshwa kwa maslahi ya nchi. Faida zake ni pamoja na kujenga maadili mema ya kitaifa kwa vijana, kuondoa tofauti za kikabila, kidini, na hata za kipato kwani ndani ya kambi nyote hujiona wamoja. La muhimu kwa serikari ni kuhakikisha mpango huu unaandaliwa vyema ili kuleta tija kijamii, kisiasa kiuchumi na kiutamaduni. Ni jambo jema kuwa na taifa lenye vijana wakakamavu, wavumilivu, wabunifu na wenye uzalendo na kujivunia ustawi wa nchi yao. KUJIANDAA VYEMA NI KUJIANDAA KUSHINDA. 34

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo