Majadiliano kati ya Somalia na Somaliland yafunguliwa huko London

Adnan Hussein jijini Mogadishu na Barkhad Dahir huko Hargeisa wamechangia katika ripoti hii

Juni 21, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mkutano maaalumu wa siku mbili kati ya wawakilishi kutoka Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia (TFG) na Somaliland ulianza Jumatano (tarehe 20 Juni) huko London, ukizindua majadilianao ya moja kwa moja kati ya pande mbili hizi kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20.

  • Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed (kushoto) na Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali wakiwa katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu Somalia huko London mwezi Februari uliopita. [Matt Dunham/AFP]

    Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed (kushoto) na Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali wakiwa katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu Somalia huko London mwezi Februari uliopita. [Matt Dunham/AFP]

  • Rais wa Somaliland Ahmed Mohamed Silanyo (kushoto) akizungumza huko Hargeisa tarehe 7 Machi wakati wa matembezi ya tathmini  yaliyofanywa na wawakilishi wa Umoja wa nchi za Ulaya kwa Somalia Georges-Marc Andre. [Na Simon Maina/AFP]

    Rais wa Somaliland Ahmed Mohamed Silanyo (kushoto) akizungumza huko Hargeisa tarehe 7 Machi wakati wa matembezi ya tathmini yaliyofanywa na wawakilishi wa Umoja wa nchi za Ulaya kwa Somalia Georges-Marc Andre. [Na Simon Maina/AFP]

Mkutano huu uliotarajiwa sana ulikidhi moja ya mapatano yaliyofikiwa na TFG na Somaliland katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu Somalia mwezi Februari, na kuazimia kuanza mazungumzo kati ya pande mbili hizi kutafuta suluhisho kwa masuala ya kudumu, ikiwemo umoja wa kitaifa na usalama wa kikanda.

Mazungunmzio hayo yaliongozwa na wawili hao, kamati ya watu watano walioiwakilisha TFG na Somaliland, ambayo iliteuliwa na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed na Rais wa Somaliland Ahmed Mohamed Silanyo

Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa wa Somalia Abdisamad Maalim Mohamud aliongoza kamati hii ya TFG iliyojumuisha Waziri wa Elimu Ahmed Aydid Ibrahim, balozi nchini Djibouti Abdi Hussein Gulwade na wabunge Hussein Hassan na Mohammed Hassan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Somaliland Mohamed Abdullahi Omar aliongoza kamati yake iliyojumuisha Naibu Spika Bashe Mohamed Farah, Mwenyekiti wa Haki na Ustawi wa Chama Faisal Ali Warabe, Waziri katika Ofisi ya Rais Hirsi Ali Haji Hassan na Waziri wa Kazi na Masuala ya Kijamii Mohamud Ahmed Barre.

Waheshimiwa wa Kimataifa pia walihudhuria mkutano huu, ambao ulifadhiliwa na serikali ya Uingereza na Umoja wa nchi za Ulaya.

Iwapo wajumbe watafanikiwa katika awamu hii ya kwanza, Ahmed na Silanyo wanatarajiwa kukutana baadaye mwezi huu kwa mkutano wa awamu ya pili katika Umoja wa Falme za Kiarabu, kwa mujibu wa Redio BBC Somalia.

Kufikia makubaliano

Licha ya umuhimu wa mkutano huu, ambao ulizileta pamoja pande mbili hizi kwa mara ya kwanza kutoka Somaliland kujitenga kutoka Somalia 1991, baadhi ya wachambuzi wamebakia na mashaka kuhusu matokeo yake.

Nasra Dhuuh Malin, mhamasishaji wa chama cha kiraia jijini Mogadishu, alisema majadiliano kati ya TFG na Somaliland yataendelea bila kikomo ispokuwa pande zote mbili zimeonyesha kubadilika kulingana na hali.

Hadi sasa, Somaliland imeendeleza nafasi yake maalumu ya kubaki imara katika kutafuta uhuru utambuzi wa kimataifa. Kabla ya kuondoka kwenda London, waziri wa mambo ya nje aliwaambia waandishi wa habari kuwa ujumbe wake utawaelezea washirika wenzao wa TFG uamuzi ambao Somaliland ilifikia 1991 wa kujitenga kutoka Somalia.

“Ni lazima tudumishe hadhi yetu kama taifa huru, linalostahili heshima ya kimataifa. Uhuru wetu wa kuamua mambo haujadiliki,” Omar alisema.

Lakini Bihi Iman, mchambuzi wa mambo ya kisiasa huko Hargesia alisema wakazi wa Somaliland siyo wote waliofikia makubaliano kuhusu suala hili.

Ingawaje Somaliland ilifanya kura ya maoni 2001, na asilimia 97 ya wapiga kura kuidhinisha kujitenga, alisema kura hiyo haikuwa ya uwakilishi wa watu kwa sababu ni watu wachache zaidi ya milioni moja walishiriki kati ya wapiga kura waanaostahili milioni 2.5. Zaidi ya hayo, kura hiyo ya maoni ilikuwa na mipaka kwa wakazi wa Somaliland, ikiwaacha Wasomali wengine nje ya mchakato, alisema.

Iman alisema ili kujua Wasomali wanataka nini, kura nyingine ya maoni itapaswa kupigwa. "Sasa hivi hatuwezi kusema kwamba tunajua mahitaji ya watu … tunaweza kujua tu kama tutawauliza na kupiga kura," alisema.

Aliagiza pande zote kuacha kutangaza nafasi zao wakati mazungumzo bado yanaendelea, na kusema bado kuna nafasi ya aina fulani ya makubaliano inayoweza kufikiwa katika awamu hii ya mkutano.

"Watu wamechoka na hali isiyo na utulivu waliyokuwa nayo kwa muda wa miaka 21 iliyopita, kunatakiwa mabadiliko," alisema akiongeza kwamba ile ni hisia moja iliyowapata Wasomali wote.

Kusonga mbele

Mohamed Haruun Bihi, mjumbe wa chama cha upinzani cha Haki na Ustawi, alisema kwamba mazungumzo na TFG yaliongeza morali katika matumaini ya kusuluhisha migogoro inayoendelea.

Bihi aliiambia Sabahi kwamba wazo la kujitenga na Somalia halikuja kirahisi na kwamba wananchi wake wanataka suluhisho la kisiasa la haki na linalokubalika. Alisema kama hawatapokea pendekezo la ndugu zao wa kusini kama ni la haki, wataweza kuendesha kura ya maoni kuamua siku zao zijazo.

TFG wameendelea kurudia tena kusudi lao la kufanya mazungumzo na nchi ya Somaliland na kuhimiza umoja wa kitaifa kwani utatatua matatizo yote yaliyobaki.

Akizungumza na Redio Mogadishu inayoendeshwa na serikali siku ya tarehe 11 Juni Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali alisema serikali yake imejiandaa vya kutosha kwa mazungumzo na ina amini moyo wa kushiriki wa uzalendo utawasaidia pande zote kufikia mwafaka.

"Watu wetu wanasimama pamoja kwa umoja na wanaungana katika sura ya maadui kuhifadhi uhuru wetu, fahari na kiu yetu ya amani na maisha ya mafanikio," alisema.

Sawia na hilo, Rais Ahmed ametoa wito kwa wazee wa makabila ya Somalia kusaidia kutunza umoja na uthabiti katika nchi kwa kuendeleza mazungumzo ili kufikia makubaliano ambayo yatairidhisha Somaliland.

"Ninawaomba muingie katika mazungumzo kati yetu na ndugu zetu kutoka katika serikali ya Somaliland ili tuweze kutatua matatizo. Ningependa ninyi kuzingatia jitihada zenu mlizoziheshimu kwa kuwasukuma kuelekea katika umoja wa kitaifa ulio thabiti ili kuzuia kusambaratika kwa nchi," Ahmed aliwaambia wazee wa makabila katika mkutano uliofanyika mapema mwezi huu.

Wazee wa makabila ya Somalia wamekuwa kati ya michakato ya siasa ya nchi. Wamepewa jukumu la kuchagua wajumbe katika Bunge la Taifa la Katiba Somalia, ambalo litaboresha rasimu ya katiba mpya. Wazee watachagua wabunge ambao watakuwa wakimchagua rais wa Somalia ajae, kuanzia mwisho wa kumaliza kipindi cha mpito ifikapo tarehe ya mwisho, tarehe 20 Agosti.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 22)

Dislike_icon(4)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • mohamed
    June 24, 2012 @ 01:09:47PM

    Upuuzi.

  • Ahmed Dhegaweyne
    June 22, 2012 @ 05:10:09AM

    Sidhani kama ni haki kwa Somaliland kuwa mustakabali wao na amnai waliyoipata kwa nguvu na utulivu wa kidemokrasia utathibitishwa na sauti ya watu wa Somalia na serikali yake ambayo wanapigana vikali kwa zaidi ya muongo kabla ya kushinda vita na kuvunja muungano baada ya Somalia kuingia katika mfumo usio na serikali tayari ni miaka 20 imepita ambapo Somaliland imekuwa ikifaidi amani. Jawabu ni kuwa hapana, lakini vyombo vya sheria vitatumika na jumuiya ya kimataifa itaingilia kati kwa utengano wa amani.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo