Wito wa jihadi wa al-Shabaab ni kuungama kushindwa, wachambuzi wasema

Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Juni 20, 2012

  • 291 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Katika rekodi ya sauti iliyotolewa Jumatatu (tarehe 18 Juni) katika Redio Andalus, kipaza sauti cha al-Shabaab, kiongozi wa kikundi Ahmed Abdi Godane, anayejulikana pia kama Mukhtar Abu al-Zubair, aliwataka wapiganaji wake kusimama imara katika uwanja wa vita, na kuahidi pepo kwa yeyote anayekufa kwa kulinda dini yake.

  • Kamanda wa kikosi cha AMISOM Brigadia Paul Lokech (kati) akizungumza na askari kabla ya kusonga mbele kuelekea Afgoye hapo tarehe 25 Mei. Al-Shabaab kuipoteza Afgoye kunachukuliwa kama mojawapo ya mfululizo ya vipigo vya hivi karibuni kwa kikundi. [Na Stuart Price/AFP]

    Kamanda wa kikosi cha AMISOM Brigadia Paul Lokech (kati) akizungumza na askari kabla ya kusonga mbele kuelekea Afgoye hapo tarehe 25 Mei. Al-Shabaab kuipoteza Afgoye kunachukuliwa kama mojawapo ya mfululizo ya vipigo vya hivi karibuni kwa kikundi. [Na Stuart Price/AFP]

“Ushindi upo katika mikono ya mujahidina,” Godane alisema katika ujumbe wake. “Dunia inajikusanya ili kuitawala Somalia chini ya kisingizio cha kupigana na kikundi cha mujahidina wa al-Shabaab.”

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kiusalama ambao wamekuwa wakikisimamia kikundi cha al-Shabaab chenye uhusiano na al-Qaeda, wanasema kuwa ujumbe wa Godane ni jaribio la kunyanyua morali miongoni mwa wapiganaji wake, na ni aina tu ya kukiri kuwa kikundi kinakaribia kushindwa baada ya kupoteza ngome zao kadhaa muhimu kusini na kati ya Somalia.

Al-Shabaab wako katika ‘hali isiyotamanika’

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mtaalamu wa vikundi vya Kiislamu nchini Somalia Mohamed Hassan alisema harakati ya al-Shabaab ni katika "hali ya kuchanganyikiwa kabisa na inayokaribia kukata tamaa.”

"Ujumbe wa Godane ni kuungama kuwa wapiganaji wamekuwa wakishindwa katika vita vinavyoendelea nchini Somalia, kwa hivyo anajaribu kunyanyua morali miongoni mwa safu za waasi,” aliiambia Sabahi.

"Al-Shabaab wako katika hali ngumu na isiyotamanika, ambayo ni hatari sana wakati shinikizo la kijeshi kutoka pande zote, na ndio maana kikundi kinapambana ili kiendelee kuishi,” Hassan alisema.

Katika ujumbe wake, Godane aliyataka makabila ya Somalia kujiunga na kile alichokiita dhidi ya vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika na washirika wao.

“Tunayataka makabila yote ya Somalia kujiunga na jihadi na kusaidia juhudi za kuanzisha taifa la Kiislamu ambalo litawasilisha mwamvuli wa Waislamu wote katika eneo hili,” Godane alisema.

“[Mwaliko] huu utatua katika masikio ya viziwi na hautatiliwa maanani na makabila ya Somalia,” alisema mchambuzi wa wa masuala wa kisiasa aliyeko Mogadishu Abdinaasir Osman.

Makabila ya Somalia hayaungi mkono ugaidi na hakuna kabila linaunga mkono vikundi vinavyokataa amani,” aliiambia Sabahi. “Makabila yako pamoja na taifa na ushahidi wa hili ni mkutano uliowaleta pamoja Mogadishu viongozi wote wa makabila ya Somalia kutoka nchini kote ili kuchagua wajumbe wa Bunge la [Taifa] Katiba na wajumbe wa bunge jipya.”

Osman alisema watu wa Somalia, hasa wale wanaoishi katika maeneo yaliyo katika udhibiti wa al-Shabaab, wameshateseka na bado wanateseka kutokana na mkabala mgumu na hatua za kikatili, na ndio sababu kwa nini hakuna makabila yanayounga mkono wito wa kiongozi wa al-Shabaab.

Mzunguko unaoelekea chini

Ali Ahmed, mchambuzi wa masuala ya kiusalama na afisa mstaafu kutoka jeshi la Somalia, alisema mzunguko unaoelekea chini wa al-Shabaab unakabiliwa na kampeni za kijeshi dhidi yao.

“Ikiwa kampeni za sasa za kijeshi dhidi ya al-Shabaab zitaendelea na kasi yake, kwa hivyo inawezekana [sana] kuwa kikundi hiki kitaacha kuwepo kama jeshi lenye nguvu katika miezi michache,” Ahmed aliiambia Sabahi.

“Tunachokiona leo ni kuwa al-Shabaab imejikuta katika matatizo makubwa na kinakumbwa na upotevu mkubwa, bila ya kutaja kuwa wapiganaji wake wamekuwa wakijiondosha bila ya ushindani kutoka kila mji ambao vikosi vya Somalia na majeshi ya Umoja wa Afrika wanayoikabili,” alisema. Hii ni ishara kuwa uwezo wao wa kupigana umedhoofika.”

Katika miezi iliyopita, al-Shabaab wamepoteza miji kadhaa mikubwa na midogo, ya hivi karibuni ikiwa Afgoye na Afmadow. Wachambuzi wanasema kuwa ushindi huu uliopatikana na jeshi la Somalia, kwa msaada wa Misheni ya Umoja wa Afrika Somalia (AMISOM) na vikosi washirika wa kanda, kulikosababisha al-Shabaab kupoteza ngome na miji yake ya mikakati, kumeleta pigo kubwa kwa kikundi.

Wakati vikosi vya Somalia na vya Umoja wa Afrika vikisonga mbele, macho yote sasa yameelekezwa katika ngome yao iliyobakia, mji wa bandari wa Kismayo.

“Jeshi la taifa, kwa msaada wa vikosi marafiki, inakaza kamba katika mji wa al-Shabaab wa Kismayo," alisema Kanali Daahir Abdulqadir, mmojawapo wa makamanda wa Jeshi la Somalia huko Juba ya Chini.

“Tunatayarisha kuongeza shambulio la mwisho huko Kismayo kwa sababu kuukamata mji huu kunawakilisha pigo la mwisho kwa kikundi,” aliiambia Sabahi.

Abdulqadir alisema al-Shabaab hawana nguvu za kutosha za kuulinda mji na wanaelekea kukimbilia katika msitu mnene nje ya mji.

'Msumari wa mwisho katika jeneza la al-Shabaab'

Tangu Marekani ilipotangaza tarehe 7 Juni zawadi ya dola milioni 33 kwa viongozi saba wa juu wa al-Shabaab, vyombo kadhaa vya habari vimeripoti kuwa wamekuwa wakikimbia kutoka Kismayo. Wachambuzi wa masuala ya kiuslama wanasema kuwa zawadi hizi zitaongoza shinikizo kwa al-Shabaab.

“Ikiwa Kismayo itaanguka katika mikono ya vikosi vya serikali, kwa hivyo al-Shabaab imekuwa katika hali ya kuchanganyikiwa kisiasa, kifedha na kijeshi ambayo itagongea msumari wa mwisho katika jeneza la al-Shabaab,” Abdulqadir alisema.

Bandari ya Kismayo inafikiriwa kutoa mapato kwa al-Shabaab na unachukuliwa kuwa uti wa mgongo kwa kikundi katika masuala ya kifedha. Ili kuyafanya mambo kuwa mabaya zaidi kwa al-Shabaab, kuna migawanyiko ya ndani na tafauti kubwa miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab.

“Mgawanyiko ndani ya al-Shabaab unaongezeka kutokana na vikwazo vya sasa wakati kikundi kinapoteza ngome zake muhimu sana,” alisema mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwanaharakati Ahmed Aadan.

“Suala hili lilianza baada ya kikundi kutangaza kuwa litaungana na al-Qaeda mwezi Februari mwaka jana, na kuanzia hapo, kumekuwa kukiibuka migawanyiko ya ndani siku baada ya siku,” aliiambia Sabahi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 426)

Dislike_icon(58)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Stephen Odhiambo Ja Ugenya
    July 27, 2012 @ 04:14:39AM

    Al-Shabaab si watendaji tena. Na kama wao ni watendaji basi watuhakikishie.

  • Dheere
    July 23, 2012 @ 03:27:28PM

    Al-Shabaab imesababisha madhara makubwa na upotevu wa maisha nchini Somalia na hii imeathiri maisha ya vijana wengi. Kama tunavyojua vijana wana nguvu na wengi wao wanapenda kujishughulisha na michezo. Kwa ajili ya al-Shabaab, hii imekuwa haiwezekani kwa sababu vijana wanatekwa na kulazimishwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab. Hili limeua shauku lolote ya vijana. Kikundi cha kigaidi pia kimeifanya nchi kutokuwa na usalama na ni hatari sana kufanya shughuli yoyote ya kimichezo kwa sababu ya uoga wa kushambuliwa na waasi.

  • micheal kirui
    July 23, 2012 @ 09:39:00AM

    Suala hilo linaendelea vyema, shukurani kwa washirika wa majeshi ya Afrika kwa kuwashinda maadui wa dunia.

  • Joyce
    July 23, 2012 @ 08:38:57AM

    Ninakipenda

  • GIDEONS
    July 21, 2012 @ 03:16:37PM

    KUNA VISIMA VYA MAFUTA NCHINI SOMALIA? SOMALIA ITAKUWA MKOA WA TISA NA SIO JIMBO LA 48 YA KENYA. KAZI NZURI VIJANA.

  • Sawa SAWA
    July 21, 2012 @ 11:31:45AM

    NIMEIPENDA HII.

  • lily
    July 21, 2012 @ 11:20:32AM

    Alshabab wakwende huko their days are numbered how can they just kill innocent people in church ?what wrong did people at Garissa do ,infact they kill their own people too in the name of Jihad ...do they know the meaning of that in there religion.By the way do we have their debts?i wonder God will help Kenyan Troops in this battle am sure we gonna win the battle.Amen.

  • carol Mcckenna
    July 21, 2012 @ 05:32:42AM

    AL-SHABAAB are jus wasting time throwing stones whereas they will waste other times collecting them.............hahahahaha! hawa2wezi bwana hawa kdf en paramater soldiers r tough cheerz 2 them all as we w8t 4 da recruitment..................!

  • I. Andanje
    July 21, 2012 @ 05:18:42AM

    Daima niliamini juu ya uwezo wa askari (wa KDF). Fanyeni kazi vizuri kaka na dada zetu na Jah atawabariki. Hongera.

  • Mariam
    July 20, 2012 @ 02:43:01PM

    Msomali au Muislamu yeyote anayewaunga mkono al-Shabaab ama atakuwa kiopu au ni mgonjwa tu kama wale wahuni wanaijiita AL-KABAAB. Lazima tuwe na tahadhari katika kuchagua washirika wetu. Binafsi nimeshuhudia matendo yao ya kikatili na nimeelewa kutokana uzoefu ule ni kwa kiasi gani ni wagonjwa. Mtu yeyote anayetenda uhalifu dhidi ya ubinadamu hapaswi kuvumiliwa. Hili litumike pia kama onyo kwa askari wa TFG na vikosi vya AMISOM. Lazima waelewe kuwa kazi yao kubwa kwa sasa ni kushinda mioyo na akili za umma na kwa hivyo wabembeleze watu wa Somalia. Al-Shabaab wanashindwa vita kwa sababu umma wa Wasomali umechoshwa na uongo na ukatili wao, sio kwa sababu hawana nguvu za kutosha za bunduki. Katu huwezi kushinda vita bila ya msaada wa umma. Hawa watu wa kawaida, wawe wakulima masikini au wachungaji wenye njaa, ni watu hao hao wanaowapatieni habari nzuri za kiintelijensia kuhusu walipo maadui zenu kwa sababu nyinyi hamuwezi kuwepo kila pahali wakati wote. Tuiombee Somalia kwa sababu miezi michache ijayo ni muhimu sana kwa vile ni mwisho wa kipindi cha mpito kwa TFG na mwisho wa utawala wa Al-Shabaab. Kitakachotokea baadaye kitategemea sana vipi tunajidhibiti wenyewe leo, kesho na mwezi ujao, iwe katika uwanja wa mapambano au katika ulingo wa kisiasa.

  • Ibrahim Ahmed
    July 20, 2012 @ 11:24:15AM

    Uislamu utatawala tena ulimwenguni.

  • Prestige Camp
    July 20, 2012 @ 11:18:42AM

    Bila ya shaka wameshindwa lakini mashambulizi ya kigaidi yatakayokuja huwa KALI!!!

  • jacob Young KongKong
    July 20, 2012 @ 05:03:08AM

    Turuhusu amani irejee Somalia, tuachane na maoni kama hayo, nani anamshinda nani?

  • mbogo
    July 19, 2012 @ 05:15:43AM

    Ni mwenyezi Mungu tu anayejua kuhusu pepo na/au jehanum. Inawezaje binadamu kuwaahidi wengine kuwa wataenda peponi wakati yeye mwenyewe hajawahi kufika huko? Ndugu zangu amkeni! Al-Shabaab ni sawa na farasi anayekata roho na wamechanganyikiwa juu ya maisha yao wenyewe. Ndugu zetu wa Somalia wameshateseka kwa muda mrefu na sasa wanayo fursa ya amani katika nchi yao. Mwisho, nikija kwa kile kinachoendelea Somalia sasa, ni hakika kuwa matatizo ya Afrika yanahitaji ufumbuzi wa Afrika, iwe ni kijeshi au vinginevyo.

  • koech banyamulenge
    July 17, 2012 @ 10:44:09AM

    Kwa usalama wa Pembe ya Afrika, mwanamme yeyote asitoke nje ya Kismayu. Waruhusu wanawake na watoto tu, askari wetu wa majini wamezuia baharí zote. Kwa hakika wataangamizwa.

  • aden
    July 17, 2012 @ 02:31:24AM

    Kkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkk

  • ANTHONY NGANGA
    July 14, 2012 @ 09:36:24AM

    Magaidi wa al-Shabaab kuyashambulia Makanisa ya Kikristo ya Kenya ni ishara ya kushindwa. Kwa nini wawalenge wananchi wasio na hatia wanaoabudu na kumsifu Mungu? Kama wangekuwa wanaume vya kutosha, wangewalenga wanaume wenye sare ambao wanawalazimisha kukimbia miji mikubwa iliyo chini ya udhibiti wao. Kuwaambia watu wa Somalia wajiunge na jihadi dhidi ya AMISOM ni hatua ya kushindwa. Kamanda hawezi kuahidi watu pepo, angewaahidi moto wafuasi wake.

  • ibraahiim
    July 9, 2012 @ 08:53:51AM

    Al-Shabaab hawana heshima kwa wanawake na watoto. Ningependa kuwaomba dada na kaka zangu wa Somalia kuwa waangalifu kuhusu kikundi hiki hatari. Al-Shabaab si kikundi cha Kiislamu na kwa kweli ninaweza kuwahesabu kama makafiri.

  • KIPKETER ELVIS NGETICH
    July 9, 2012 @ 08:35:47AM

    Al-Shabaab lazima waelewe kuwa wanapoteza wakati na mali kwa sababu hali yao kifedha haiwezi kulinganishwa na walinda amani wa dunia. Wangepaswa kujisalimisha.

  • Alice Nyaga
    July 9, 2012 @ 08:16:15AM

    Al-Shabaab wangesitisha moyo huu wa uovu walionao...na kuwapenda dada na kaka zao ili Kenya nayo iweze kuacha kupoteza mali...

  • simon mwangangi
    July 9, 2012 @ 08:11:42AM

    let the al-shabaab face it rough.they have not yet faced the real kdf.wait until other boys ere added in kdf,they will cry.bravo para,rangers and the whole kdf soldires.recrute us tufanye hii kazi.

  • JUMA BIN JUMA
    July 9, 2012 @ 08:08:29AM

    WASOMALI WANAOLALAMIKA KUHUSU KDF KUWANG’OA AL-SHABAAB KUTOKA SOMALIA NI: 1. MAJAMBAZI WANAOFAIDIKA KWA KUTOKUWEPO KWA UTAWALA NA HAWATAKI AMANI IWEPO. 2. WAFUASI WA AL-SHABAAB WANAOJIFICHA NYUMA YA UISLAMU ILI KUENDELEA KUIKAMUA SOMALIA HADI IKAUKE. UISLAMU HAUKUWA NA WALA SI MAANA SAWA NA UUAJI NA KUKOSA UTAWALA. WALE WANAOUA NA KULEMAZA NA KUIBAKWA JINA LA DINI NI MAKAFIRI.

  • kokoyo
    July 9, 2012 @ 07:52:58AM

    Sasa al-Shabaab wanavifanya vita hivi kuwa vya tofauti za kidini. Hahahahahahaha....hii ni sawa na kisa cha mfamaji, hukamata japo ubua.

  • ERIC COLANDO
    July 9, 2012 @ 07:46:31AM

    HONGERA JESHI LA KENYA. Hii ndio njia ambayo Wakenya tumeonesha kuwa tunapenda amani. Unaweza tu kutatua tatizo kupitia makubaliano, mkishindwa mnatafuta msuluhishi. Ikiwa hilo nalo litashindwa njia pekee ya kufanya ni kutumia nguvu zako za mwili kama ambavyo Kenya ilifanya.

  • Maina
    July 9, 2012 @ 06:59:00AM

    Al-Shabaab wako katika kitanda wanakata roho.

  • paul muturi
    July 9, 2012 @ 06:42:53AM

    AMISOM-Endeleeni. Nendeni Kismayo na kadri itakavyokuwa karibuni, ni bora zaidi. Somalia lazima iwe na utulivu.

  • MYRA
    July 9, 2012 @ 05:44:21AM

    KAZI NZURI KDF HONGERA, MNASTAHIKI SIO KUWAPIGIENI MAKOFI KWA MKONO TU BALI PIA KUWAPIGIENI MAKOFI KWA MIGUU.

  • timo
    July 9, 2012 @ 05:29:06AM

    Kazi nzuri!

  • GEORGE OKUMU
    July 9, 2012 @ 04:50:24AM

    Kushindwa kwa al-Shabaab nchini Somalia kutaleta amani katika nchi yetu ya Kenya na Afrika ya Mashariki na Kati. Watu wa Somalia wanaoishi nchini Kenya katika kambi za wakimbizi watapata fursa ya kurejea kwenye nchi yao ya asili ambayo walihama miaka mingi iliyopita. Wataweza kujiwezesha wenyewe kiuchumi. Watoto watapata fursa ya kwenda shule katika nchi yao. Mungu awajaalie al-Shabaab washindwe kwa kudhalilika kabisa.

  • stephen
    July 9, 2012 @ 04:48:07AM

    Nadhani Uislamu hauna maana ya vita au ugaidi. Wakristo na Waislamu ombeni kwa aliyejuu zaidi ambaye ni MUNGU. Na yeye ndie pekee anayeweza kumaliza maisha ya kile alichokiumba mwenyewe. Piganeni kwa kutumia Biblia au Koran, sio na silaha za kuua mamia ya roho za binadamu. HONGERA KDF NA AMISOM. Tunasubiri kukombolewa kwa Somalia.

  • Christian
    July 9, 2012 @ 04:14:11AM

    Unaua na unatarajia uzawadiwe pepo na Mungu??????Ni dini gani hii. Haiingii akilini.

  • fatuma omar
    July 9, 2012 @ 01:52:33AM

    Karibuni tuliwaona al-Shabaab wakiwakumbatia al-Qaeda, hii ni hatua ya makusudi ya kikundi hiki kwa sababu wanataka wajihisi kuungana na kikundi chenye nguvu zaidi kutoka Mashariki ya Kati. Ombi la Al-Shabaab la muungano wao na al-Qaeda linaweza kuonekana kama hatua ya kuchanganyikiwa kwa al-Shabaab ili kujiimarisha na kuweza kuomba msaada wa kifedha na silaha kuwasaidia katika kikundi chao kilichochoka. Vikundi hivi pia viliungana kwa sababu vina itikadi moja na wanapigania dhamira moja. Al-Shabaab ni kikundi kichanga kwa hivyo kinahitaji kuwakumbatia wenzao wa Mashariki ya kati ili kuwatisha maadui zao. Wanataka kuzifanya nchi nyingine ziwaogope kwa sababu wameunganisha nguvu zao; tunaona kuwa al-Shabaab wanawataka al-Qaeda kwa sababu wao ni dhaifu.

  • ROBERT
    July 8, 2012 @ 05:20:49PM

    Hii, ninawakusudia Wasomali wote... Mmeteseka kwa muda mrefu. Isipokuwa tu mmeamua kwa uhakika kuwa haya ni mabadiliko. kwa hivyo fanyeni kazi kama kawaida. Na sio hata AMISOM wanaweza kufanya chochote. Hakuna mtu atakayewaamulia mustakabali wenu, ni nyinyi wenyewe tu mnaoweza kufanya hilo. Tafadhaleni, ifanyeni historia kuwa ni mwongozo wenu. Ziangalieni nchi kama Ujerumani, Italia na Japani...angalieni wale walioibuka kutoka katika majivu na kwa mara nyingine tena kuwa viongozi wa dunia. Viongozi wa Koo wa Somalia. Sasa mnayo nafasi, kamatieni muda huu. Ifanye iwe ya maana. Kwa muda wa miaka kumi ijayo, wafanyeni wote wazungumzie Somalia yenye amani iliyofanikiwa.

  • masterseed
    July 8, 2012 @ 03:33:18PM

    Kijana huyu anayeitwa Murphy, hebu tupe wasaa na natumai wewe sio mzungu. Makala hii inaendelea kutaja mafanikio ya AMISOM na inawaweka upande KDF. Kwa wazungu wengi hakuna kitu kizuri kinachotarajiwa kufanywana na KDF ambayo ilikuwa haijajaribiwa. Sasa wameanza kimkakati ili kuongoza uvamizi wa Kismayu, mzungu anataka kuona wengine na wala sio KDF. Lazima tuwaepuke viongozi tunaolazimishiwa na magharibi ili kuendeleza udhibiti wao kwa Waafrika kwa kutuambia sisi si watu wamoja. HESHIMA kwa KDF, askari wataalamu wanaomaliza misheni yao kwa dua ya kutoa shukurani na kutoa msaada kwa wanaohitaji wanaowakutia. Mungu awabariki.

  • babeba
    July 8, 2012 @ 03:30:35PM

    Ni Mungu tu anayejua kwa nini jambo hili limetokea. Tuombeni kwa ajili ya amani.

  • Wamumyai
    July 8, 2012 @ 02:37:36PM

    Naangalia mbele ambapo siku moja mtu anaweza kuitembelea Somalia na kuzungumza na ndugu zetu ambao watakuwa wameonja uhuru uliokuwa hautajwi. Tutachanganyika pamoja, kufanya biashara pamoja na kuheshimiana bila ya kujali imani za dini zetu.

  • Hadithi Adam
    July 8, 2012 @ 01:51:36PM

    Tunavishukuru vikosi vya TFG, AMISOM, Ethiopia pamoja na KDF ya Kenya. Al-Shabaab ni majambazi yasiyokuwa na dini yanayoua watu wasio na hatia kwa maumivu makali.

  • yusuf ali mustafa
    July 8, 2012 @ 01:29:56PM

    Mwenyezi Mungu alipize kisasi kwa dhambi zote zilizofanywa na al-Shabaab nchini Somalia. Mwenyezi Mungu atawaandama hadi wa mwisho aliyebakia wa al-Shabaab iwe nchini Kenya au Somalia. Somalia itafaidi amani kama zilivyo nchi zilizoendelea. Al-Shabaab waache kutumia jina la dini wakati wanafanya uhalifu.

  • Mugambi
    July 8, 2012 @ 11:59:08AM

    Kila siku inasemwa kuwa "Ikiwa huwezi kupigana nao, ungana nao".

  • james maghanga
    July 8, 2012 @ 11:32:27AM

    Kenya yenyewe ina matatizo. Tusiwalaumu al-Shabaab kila mara, hatuwezi kujiongoza wenyewe.

  • ibra
    July 8, 2012 @ 10:32:55AM

    Tawala kwa bunduki ufe kwa bunduki. KDF na AMISOM ninawatakia kila la heri katika kuwaokoa watu wa Somalia.

  • Jarule
    July 8, 2012 @ 09:27:49AM

    Kwa mimi kupigana kwa ajili ya amani hakuna maana yoyote na pia kuua ili kuokoa maisha. Ninachojua ni kuwa sote ni watu wa Mungu na tunatakiwa tuishi kwa amani na upendo. Inaumiza moyo wangu kuona ndugu zangu (Waafrika) wanauana wenyewe kwa wenyewe bila ya sababu yoyote. Mungu awape busara ya kuweza kujua jema na baya.

  • sikimb
    July 8, 2012 @ 09:16:56AM

    Al-Shabaab siku zenu zinahesabika, mmefanya ukatili, mmeua, mmewafanya watu walemavu, kwa miaka mingi, sasa huu ni msumari wa mwisho katika jeneza lenu. Nendeni mkajifiche chini ya Bahari ya Hindi.

  • mohamed
    July 8, 2012 @ 08:50:20AM

    Ningependa kuvipongeza vikosi vya Jeshi la Kenya, Serikali ya Mpito ya Shirikisho na AMISOM. Ningependa kuwaomba kukitokomeza kikundi hiki cha kigaidi kinachojiita “vijana” ili Wasomali waweze kutulia tena.

  • michael mbugua
    July 8, 2012 @ 07:23:19AM

    Kila kitu kitakuwa sawa kwa watu wa Somalia. Wakati umefika kwa Somalia kuwa huru na wale wanaojaribu kuiharibu watakumbana na ghadhabu za ulimwengu.

  • evance okoth
    July 8, 2012 @ 06:02:17AM

    Nafsi yangu inalia kwa wakati mdogo tu wa kuwepo hapa kutokana na kikundi hiki cha kishetani. Nguvu yoyote inayoelekezwa katika kukandamiza matendo yasiyokuwa ya binadamu bila ya shaka ni faraja kubwa. Asante MUNGU kwa kutoa mwanga wa matumaini. “Mungu wetu si Mungu aliyelala.” Bila ya shaka moto utawaangamiza watu waovu.

  • LAWRENCE GICHURU MURAGA
    July 8, 2012 @ 05:32:53AM

    Karibuni al-Shabaab watang'olewa na Wasomali watakuwa na kauli katika njia wanayotaka kuongozwa. Baadaye wale waovu na wachoyo wapenda vitu hawatakuwa na popote pa kwenda wala yeyote wa kumlilia kwa vile vitendo vyao vitawaandama hadi makaburini kwao. Roho za watu wasio na hatia ambao wamekufa katika mikono ya wauaji hawa wasio huruma zitalia kwa vizazi vingi vijavyo vya watu wa Somalia na wenyewe watasimamia amani na kuungana katika kujenga Jamhuri ya Somalia iliyoungana kwa maendeleo ya binadamu kama ilivyoelezwa katika Kitabu Kitakatifu.

  • Omache Peter
    July 8, 2012 @ 05:28:38AM

    Hebu washindwe mapema kama jana. Pumbavu!

  • michira wycliffe
    July 8, 2012 @ 04:22:39AM

    Tuombeni amani itawale, kujisalimisha kwao ni dhana ya pazia la moshi tu, kwa hivyo tuwe macho!

  • chris
    July 7, 2012 @ 11:56:38PM

    Tuko pamoja nanyi katika maombi yetu. Bwana awalinde kwa vile mnapigana kuilinda nchi yetu na watu wake. Endeleeni kuwamaliza al-Shabaab, mlete amani kwa watu wetu na kwa watu wa Somalia kwa jumla.

  • JOSEPH SUDHE
    July 7, 2012 @ 10:01:41AM

    THANK GOD ALSHABAB WAMESARENDER MAPEMA KABLA KDF & AMISOM WAJAVAMI KISMAYU

  • waithaka
    July 7, 2012 @ 09:49:18AM

    Heshima kwa majeshi ya Kenya. Mnafanya kazi nzuri. Ni jambo la uoga kweli kushambulia watu kanisani kwa jina la Mungu. Ni dini gani inayoruhusu kuua watu wasio na hatia?

  • mark kiprotich kirwa
    July 7, 2012 @ 08:53:14AM

    HONGERA kwa wapiganaji wa ustawi wetu nchini Somalia na nina hakika wakati wowote watarejesha utulivu.

  • PAUL MARWA
    July 7, 2012 @ 08:40:36AM

    Serikali ya Kenya isiondoke kwa sababu watu hawa wanajidai tu ili mara tu tutakapoamini kuwa wao wameshindwa, wataigeukia serikali yetu, lazima tuwe na tahadhari kubwa. Askari wetu wabakie kule ili kuweka usalama zaidi. Paul Marwa wa Chuo Kikuu cha Nairobi.

  • lucy
    July 7, 2012 @ 05:57:32AM

    Komredi wenzangu, endeleeni na kazi nzuri. Wakenya wako pamoja nanyi na Mungu yupo upande wenu. Mungu atahakikisha anazilinda familia zenu, kama nyinyi mnavyolinda taifa lenu. Hongera.

  • zax
    July 7, 2012 @ 05:05:28AM

    Nadhani njia bora zaidi ni mazungumzo na sio kwa nguvu za mtutu, kwa sababu huwezi kutatua tatizo kwa kuanzisha tatizo jengine.

  • phiriphiri
    July 7, 2012 @ 05:02:00AM

    Ninaipenda makala hii. Hayo ni mateke ya punda anayekata roho.

  • shadsmkenya
    July 7, 2012 @ 04:28:32AM

    Hawa maharamia ni watu waoga, kwa nini hawapigani na askari wenzao na wanaua raia wasio na hatia? Walianza kujishambulia wenyewe kwa kutumaini kuwa walipata mafunzo mazuri. Naamini siku moja watarejewa na akili zao na kuungana na serikali ya Somalia katika kujenga nchi yao. Mimi naamini kuwa wanashindwa.

  • Malik-al Islam
    July 7, 2012 @ 03:30:14AM

    Watu wa Somalia lazima wakubali kuwa dini haiwezi kuongoza siasa kwa sababu siasa haipaswi kuwa imani ikiwa inatakiwa kukidhi mahitaji yake ya kisiasa. Binadamu wanapaswa kuongozwa na sheria za kidunia ambazo kimaumbile zina nguvu. Al-Shabaab ni hatari na wakalI na wanachotaka ni kuleta tabu za kudumu kwa watu wa Somalia.

  • LISTONE OLOCH
    July 7, 2012 @ 02:30:41AM

    Natumai kuwa makala hii haina maana ya kuwafurahisha Wakenya lakini ni ukweli ulio wazi katika uwanja wa mapambano. Kila la heri askari wa Kenya.

  • kioko
    July 6, 2012 @ 07:12:06PM

    ALSHABABU WAONESHWE ADHABU!! KUDOS AMISOM AND KDF PARTICULARLY!

  • kuloba vk
    July 6, 2012 @ 12:05:25PM

    malisa hao wakora, let somalia be stable for the bettement of humanity , bombing a few grenades will not stop the advancement of those good forces. peace must be appreciated by all Amen

  • patrick
    July 6, 2012 @ 11:21:30AM

    Hii ni ishara ya woga kwa al-Shabaab kupeleka hasira zao kwa waumini dhaifu wasio na silaha. Hawa wajisalimishe kwa KDF ikiwa wanataka wapumue vizuri.

  • ZIGLA
    July 6, 2012 @ 11:17:10AM

    NADHANI KWA MUJIBU WA KORAN WAISLAMU WANASEMA WAKATI MTU ANAPOJIUA NA KUUA WATU WASIO NA HATIA, HUYU HUENDA MOJA KWA MOJA JAHANAMU NA NDIO MAANA AL-SHABAAB WAKAWA HAWAJALI JUU YA WATU.

  • Lexas
    July 6, 2012 @ 10:30:01AM

    Kazi nzuri KDF.

  • ALI MOHAMMED
    July 6, 2012 @ 09:37:37AM

    MWENYEZI MUNGU atawaadhibu makafiri yaani vikosi vya KDF, AMISOM, WAETHIOPIA na TFG. AL-SHABAAB watakuwa washindi na UISLAMU utatawala ulimwengu wote mpende msipende.

  • Lichina
    July 6, 2012 @ 08:48:23AM

    Wananchi wa Somalia wameteseka kwa muda mrefu. Hili genge la al-Shabaab wamefanya vibaya zaidi kwa kuanzisha jeraha kwa watu ambao tayari wanateseka. Nimefurahi Somalia itakombolewa kutoka kwa majambazi yasiyo na akili na kuacha watu wa Somalia kujenga nchi yao na kuabudu katika njia wanayoichagua wenyewe bila kulazimishwa kutoka ndani au nje. Ninaelewa pia kuwa Mwenyezi Mungu hahitaji mtu ili apigane kwa ajili yake. Yeye ni Muweza!

  • Misso Oljoro
    July 6, 2012 @ 08:34:42AM

    Al-Shabaab ni majambazi tu yaliyoamua kasumba ambao wanatumiwa kwa maslahi ya kiuchumi kutoka kwa watengenezaji wao bila ya kujijua. Tuzitoboe na kuzitoa bongo zao nje. Hongera Kenya, mnafanya kile mlichofanya kwa UGANDA. Moyo wa majirani zetu kujitolea kwa wengine uendelezwe wakati utakapofika wa kuitoa Rwanda nje ya Kongo.

  • Kamau
    July 6, 2012 @ 07:19:34AM

    Amani ni maadili, urithi ambao unapaswa kupendwa na wote na ndio maana TFG kwa kushirikiana na AMISOM lazima waende sambamba katika mapambano na kuleta AMANI.

  • Fredrick Chalinga
    July 6, 2012 @ 05:32:10AM

    Ni kwa sababu ya KDF ambao imewafanya al-Shabaab wawe kitu kilichopita. Mwandishi anaogopa kukitaja kikosi hiki muhimu katika vita dhidi ya kikundi kisicho halali. Kusingekuwepo na KDF, al-Shabaab bado wangekuwa hai, huru na wazima. Hongera kwa kikundi hiki chenye heshima na nidhamu ambacho kimejitolea sana kuokoa maisha ya watu wa Somalia. Kwa waoga ambao wanawashambulia raia makanisani na sehemu za kijamii, chukueni maneno yangu, siku zenu zinahesabika na mtakufa vibaya sana. Kumbukeni kuwa mnapoua kwa upanga, mtakufa kwa upanga na kwa hivyo hakuna chaguo jingine. Itakuwa siku njema wakati Somalia itakaposhikilia amani na umoja, wakati mauaji na uchinjwaji vitakuwa historia na wakati usalama kwa kila mtu utahakikishwa.

  • alex
    July 6, 2012 @ 05:24:50AM

    Tunahitaji amani, kupigana sio kuzuri.

  • stanley
    July 6, 2012 @ 05:04:10AM

    Wakubali tu kushindwa na waache kulipiza kwa nchi washirika. Kesi kadhaa za mashambulizi zinahusishwa na al-Shabaab yameripotiwa hasa huko Kenya.

  • Joseph Mwaura
    July 6, 2012 @ 03:17:44AM

    Timu iliyoungana, hao ndio askari WETU, Jeshi la Kenya. Endeleeni na kazi nzuri na Mungu Mwenye uwezo atayakabidhi maeneo yaliyobakia mikononi mwenu.

  • blasto bula.
    July 6, 2012 @ 03:01:47AM

    Hakuna umwagaji damu unaoishia bure. Wale wanaishi kwa upanga lazima wafe kwa njia hiyo hiyo.

  • KIPROTICH MUTAI ARAP TARE
    July 6, 2012 @ 01:35:17AM

    ASANTENI KDF KWA KAZI YENU NZURI, TUNAWAOMBEA.

  • patrico
    July 5, 2012 @ 01:26:45PM

    Wakati watu wajinga wanapodhibiti serikali yoyote hayo ndiyo matokeo ya mateso. Waende jehanam. Unaweza kuwapumbaza watu baadhi ya nyakati na Mujahidina lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote. Watu wa Somalia AMKENI, MUNGU NI UPENDO na sio gaidi, anajua namna ya kuadhibu bila ya kutumia binadamu. Jiulizeni wenyewe. Mnasali mara tano kwa siku na bado mnachukiana na mna lugha moja, ikiwa hamuwezi kuwapenda majirani zenu, mnatarajia Mwenyezi Mungu atawapenda? AMKENI, TUKO KATIKA KARNE YA 21. Binafsi ni nawapendeni, lakini ninawachukia wale wanaochukia kwa jina la dini.

  • Musee Himself
    July 5, 2012 @ 11:36:03AM

    Watoto wabaya, watoto wabaya, mtafanya nini, mtafanya nini wakati wanawajieni!!

  • justice cheruyot
    July 5, 2012 @ 11:19:52AM

    Ninaipenda, ni njia moja ya kuonesha kuwa al-Shabaab kuwa huu ni mwisho tu wa njia. Lazima wafikirie mpango wa pili ambao ni kujisalimisha kwa sababu baada ya yote ni kuwa hakuna lolote jema lililotokana na matendo yao zaidi ya kuwafanya watu wa Somalia wateseke bila sababu.

  • ASAGWILE N.N
    July 5, 2012 @ 10:46:05AM

    TAFADHALI serikali ya Kenya, sitisheni misheni yenu ndani ya Somalia dhidi ya al-Shabaab kwa sababu mnajitafutia matatizo ndani ya mpaka wenu, hili litatatuliwa na Wasomali wenyewe.

  • tame
    July 5, 2012 @ 10:05:19AM

    Inathibitisha vya kutosha kuwa kwa sasa Wakorea hawakuwa sahihi, nishati ya kale ya Somalia imo ndani ya Somalia na ni pigo kwa al-Shabaab. Wanapaswa waone aibu kwa wale wanaoitwa "nywele ngumu" wanawafundisha ubinadamu.

  • Mbuvi
    July 5, 2012 @ 09:41:40AM

    Endeleeni na morali wa hali ya juu askari wetu mlioungana ili kuwapiga hawa wanaojiita al-Shabaab...na kumbukeni kusali kwa ajili ya ushindi mwisho wa yote...tunajali na tunawapenda sana...Wakenya tunajivuna saa zote, saa zote, hata katika nyakati za al-Shaaab!!

  • argentdijango
    July 5, 2012 @ 08:55:43AM

    Kitu cha kipuuzi kabisa sio ujinga lakini kujaribu kutumia kitu kwa ajili ya ulinzi ambao ni dini. Kenya ni mwokozi. Mungu Ibariki Kenya.

  • Musyoki Muli
    July 5, 2012 @ 06:24:48AM

    Ni wakati kwa watu kunyanyuka na kupinga dhidi ya wauwaji wakandamizi ambao ni al-Shabaab. Ni wakati wa kujipanga wenyewe kuwa sehemu ya usafishaji wa mwisho. HONGERA AMISOM. Pamoja tutaikomboa Somalia.

  • David Ochieng
    July 5, 2012 @ 06:04:21AM

    Kila la kheri kwa ndugu zetu wa Somalia. Daima hawakustahiki adhabu ya al-Shabaab ambayo wamewasababishia kwa muda mrefu. Huu utakuwa ndio mwisho wao na fursa kwa kila raia wa Somalia kufurahia maendeleo yanayotokana na AMANI.

  • Geoffrey Tanui
    July 5, 2012 @ 06:01:32AM

    Tuwasaidie watu wa Somalia kwa kuondokana na al-Shabaab ambao wamewadanganya vijana kwa kuua wananchi wasio na hatia na kuwafanya wateseke kungemridhisha Mwenyezi Mungu, jambo ambalo sio kweli.

  • Audi Ali
    July 5, 2012 @ 05:37:45AM

    Kazi nzuri KDF. Kwa kweli mmewaangusha wale waliokuwa na wasiwasi nanyi. Watu kwa jumla waelewe kuwa hivi sio vita vya kidini...ni vita baina ya ulimwengu uliostaarabika wenye uvumilivu dhidi ya magaidi wendawazimu wa kale ambao kama wataachiwa bila ya kuangaliwa wanaweza kutupeleka katika majanga. Wakati umefika kwa Wakristo na Waislamu wa Kenya na ulimwengu wote kufanyakazi pamoja ili kuipinga kanuni hii inayoletwa na magaidi.

  • eunice mwaita
    July 5, 2012 @ 05:31:42AM

    everything that u do shall be judged accordingly siku ya kihama yaja kill pple as much as u want but remember one day u'll pay for it

  • ALVIN
    July 5, 2012 @ 05:07:58AM

    Mungu ametupeleka kote huko katika kupata amani na utulivu. Tunaomba sana kuwa al-Shabaab watatambua makosa yao kwa sababu bila ya shaka MUNGU hatawaruhusu kuondoka bila ya kuadhibiwa kwa kuharibu amani nchini kwetu.

  • muslim
    July 5, 2012 @ 05:05:59AM

    @al-islam nenda na ukasome.

  • Douglas Arot
    July 5, 2012 @ 04:31:07AM

    Kwa nini wapige mabomu kanisani, wangekubali tu kuwa wao ni waoga.

  • Mutere
    July 5, 2012 @ 04:20:06AM

    Hongera KDF na AMISOM na Mwenyezi Mungu awape nguvu na busara zaidi.

  • EMMANUEL
    July 5, 2012 @ 03:14:03AM

    Utukufu wote kwa Mwenyezi Mungu. Kwa nini kuua watu wasio na hatia katika makanisa na mitaa? Simameni kama wanaume na kukabiliana na AMISOM.

  • mohamed kadeo
    July 5, 2012 @ 02:48:55AM

    Tuiunge mkono KDF kwa kazi nzuri. Wachunguzeni wanaowapatia pesa al-Shabaab huko Eastleigh.

  • Erastus Kahunyo
    July 4, 2012 @ 11:50:06AM

    Majeshi ya Kenya endeleeni na moyo huo huo na BWANA WETU awe pamoja nanyi.

  • albert chomba
    July 4, 2012 @ 09:46:17AM

    Kilichobakia cha al-Shabaab ni ndege wa kufugwa tu kwa vile wameshapoteza kichwa, na baada ya muda watapikwa, kuliwa na kusahauliwa milele.

  • Mohamed
    July 4, 2012 @ 09:38:04AM

    Mungu ibariki KDF!!!

  • SANGA JILANI
    July 4, 2012 @ 09:19:23AM

    Sisi kama Wakenya tuendelee kuomba kwa wanajeshi wetu, MUNGU ISAIDIE NA IBARIKI KENYA.

  • Johnnyange
    July 4, 2012 @ 08:31:22AM

    SIO KWAMBA WANAPOTEZA VITA BALI WANATAKA KUVIBADILISHA KUWA VITA VYA KIDINI...HAHAHAAA. HAYA NI MATEKE YA MWISHO TU YA PUNDA ANAYEKATA ROHO. ENDELEENI, ENDELEENI KDF, AMISOM, UTURUKI, TFG NA VIKOSI VINGINE VYOTE VINAVYOPIGANA KWA AJILI YA SOMALIA YENYE AMANI. MWENYEZI MUNGU KWA HAKIKA ATABARIKI KAZI YA MIKONO YENU. NYINYI VIJANA NI HEKAYA KWETU..."WAUWENI WOTE NA SONGENI MBELE, IKIWA MTAKUFA LEO, ITAKUWA SHEREHE"

  • wewe
    July 4, 2012 @ 06:48:33AM

    NinachUkia ninapoona watu wanapouana wakati Mungu alituumba kuishi katika dunia hii na kila mtu atakufa kwa wakati wake. Ningetamani kuwa kusingekuwa na serikali, polisi au wauaji wa watu, tunaamka tu, kufanya kazi, kula, kulala na kufaidi maisha na kusubiri kifo, kwa sababu mwisho wa yote siku moja kila mtu atakufa. Kwa hivyo, kwa nini kuuana. Ni wazimu.

  • SALEH BIN RAWAH
    July 4, 2012 @ 06:21:50AM

    Amani iwe juu yenu. Wapiganaji wa AL-SHABAAB tafadhaleni pigeni kwa jina la MWENYEZI MUNGU, na pia MWENYEZI MUNGU uwe pamoja nao (MWENYEZI MUNGU NI MKUBWA).

  • antony koskey
    July 4, 2012 @ 05:49:12AM

    Mungu ibariki KDF yetu na askari wa AMISOM kwa vile wanaikomboa Somalia. Tafadhali ichukueni Kismayo kabla ya Agosti kama ilivyopangwa.

  • mole
    July 4, 2012 @ 05:08:47AM

    KDF imo ndani Ya Somalia ili kuulinda USHOROBA WA LAPSSET ambao unatishiwa na al-Kebaba... TuTatuondosha uongozi wao popote waendapo. DIRA 2030. HURRAY...

  • KIBE
    July 4, 2012 @ 04:37:04AM

    Mwisho wa al-Shabaab unakaribia siku hadi siku.

  • pujab
    July 4, 2012 @ 04:18:33AM

    Hata kama al-Shabaab mnajaribu kuua watu, sasa mmekwisha. Hata Osama alikufa akiwa amejificha ndani ya miguu ya mwanamke. Oooh, alikuwa muoga na namna alivyoua wengi...

  • kenn mutuma
    July 4, 2012 @ 03:28:31AM

    Viva majeshi ya Kenya. Hongera kitengo cha 12 cha ufundi... waueni moja kwa moja mende hao anaotia huruma......

  • jane
    July 4, 2012 @ 02:51:13AM

    Dada na kaka zetu kutoka Somalia tunawahurumia, hakuna kitu kinachoangamiza kuliko kulea watoto wasiojua nchi yao ya kuzaliwa iko wapi kwa sababu tu ya kikundi kilichoapa kutibua amani katika nchi ya Somalia. Tunamuomba Mungu na Uwezo Wake Mkubwa kuingilia kati katika vita hivi na kuleta ushindi kwa KDF na vikosi vyote kwa kuleta tena busara katika nchi hii. Hongera. Karibu mmeshafika. Muhoi Ngai.

  • MWENDA
    July 3, 2012 @ 11:46:36PM

    Kwa ndugu Waislamu wote, kwa uelewa wangu mdogo, MUISLAMU WA KWELI HAUNGI MKONO UGAIDI WALE WANAOHUBIRI NENO LA JIHADI NA KUDAI WANATETEA UISLAMU, NANI ANAUPIGA VITA UISLAMU? WAELEWE MAANA YA UISLAMU NA KWA TAARIFA YAO TU, NI KUWA UISLAMU NI DINI YA AMANI NA SIO UGAIDI. WASHINDWE AL-SHABAAB.

  • abby billz masini
    July 3, 2012 @ 08:52:19PM

    Al-Shabaab hawawezi kuwa majambazi kiasi hicho, kwa vile kila kitu hutokea kwa sababu, inawezekana al-Shabaab wana sababu nzuri ya kufanya wanachofanya.

  • Christopher A Mulama
    July 3, 2012 @ 05:06:41PM

    Kadiri watakavyosafishwa mapema, ndio bora kwa eneo hili.

  • AMOS WASWA
    July 3, 2012 @ 03:58:22PM

    Ni kitu kizuri sana kwa Kenya kulinda maisha ya wasio na hatia na kuondosha ugaidi ndani ya mikono ya watu wetu. Hongera Kenya, Idumu. Hakuna haja ya kusema kuwa kizazi hiki kilichostaarabika cha sasa inashangaza kuwa na mashambulizi ya kigaidi kiasi hicho na kwa kweli ni kurudi nyuma na upuuzi. Ingekuwa wazo zuri kwa wanachama wa al-Qaeda kuachana na upuuzi wao huu na kuacha kuwabugudhi ndugu zetu wa Somalia.

  • mtupoa
    July 3, 2012 @ 01:05:06PM

    Mambo! Al-Shabaab waoga! Kwa nini mnaua wale ambao si wapiganaji? Mmechanganyikiwa kiasi kwamba mnataka kujenga picha ya mzozo wa Kidini chini Kenya. Sisi tumestaarabika sana kwa ushamba kama huo wenu! Kenya ni taifa la dini nyingi na tunaishi kwa amani na mapatano. Daima hamtamuona mtu kupambana nawe kwa msingi wa dini yako. Nyinyi ni genge tu la wahalifu msio na hata elimu ya msingi kwa hivyo kukosa hisia za msingi. Hata hivyo, ni vyema kwenu ikiwa mtafikiri kuwa Mungu atawapa pepo kwa kuua wanawake wasio na silaha na watoto katika sehemu zao za ibada. Iendeeni pepo kwa mtindo huo. Inawasubiri! Hahahahahahaha! Kwa nini kiongozi wenu hajilipui yeye mwenyewe. Ikiwa kufa katika tendo la kuua wengine ni poa kwa mujibu wa imani zenu potofu, kwa nini Osama alijificha majabalini kama panya kwa muda mrefu? Kwa nini alikuwa anakimbia nyuma ya mwanamke wakati Wamarekani walipokwenda mafichoni kwake? Angeweza kufa huku anacheka akielewa kuwa pepo ni njia tu ya kufia! Naamini kuwa kila mtu anayeua kwa jina la dini hamjui Mungu. Mungu ni upendo. Upendo ni kuvumiliana (subira) na kupatana. Nyinyi si waislamu wa kweli. Nyinyi ni wajinga, Makafiri mliolaaniwa!!! Jilipueni wenyewe basi zaidi… na wakati mnafanya hivyo, tafadhalini muombeni Kiongozi wenu naye ajilipue pia. Baada ya yote ni kuwa pepo inawasubiri. Au sio?:-)

  • Emmanuel
    July 3, 2012 @ 12:27:28PM

    Huu ni wakati wa kuwa na polisi ya jamii na viongozi wanapaswa kuitikia wito wowote ule wenye mashaka haraka inavyowezekana!

  • Jimmy Kiilu
    July 3, 2012 @ 11:21:59AM

    Ndio, majambazi haya kwa jina la MWENYEZI MUNGU wako katika hali ngumu, wasagwe mpaka wasionekane. Ninaunga mkono vikosi vya pamoja nchini Somalia.

  • erastus njeru
    July 3, 2012 @ 11:00:44AM

    Kwa KDF, msisherehekee bado mpaka mawakala hao wa kifo watakapokamatwa.

  • ALEX ONSARE
    July 3, 2012 @ 10:56:07AM

    AMISOM? SEMA KDF TU, WAMETUFANYA TUJIVUNE.

  • Peris kitheka
    July 3, 2012 @ 10:13:06AM

    Ninaviombea vikosi vya KDF NA UA nchini Somalia kila siku kwa sababu Somalia inapaswa kuwa na amani ili Kenya iwe na amani kamili. Mungu akubarikini.

  • MKENYA DAMU
    July 3, 2012 @ 09:20:06AM

    NCHI YETU ILINDWE MUDA WOTE... ENDELEENI...KDF... ENDELEENI MKIWA MNAJIVUNA KWA KUJUMUISHWA NA NYINYI...MWENYEZI MUNGU ANAONA KUITIA MISHENI YENU...KAZI NZURI...HONGERA.

  • DENNIS RUNO
    July 3, 2012 @ 09:13:13AM

    AL-SHABAAB BADO WANAENDELEA KUTAFUTA SEHEMU LAINI ZA KUSHAMBULIA. WANASUBIRINI KUONA NINI KINAENDELEA NCHINI KENYA. WANAKUBALI KUSHINDWA ILI KUONA SHINIKIZO LINAPUNGUA NA BAADAYE WANASHAMBULIA TENA.

  • Wyclife omondi
    July 3, 2012 @ 09:01:12AM

    Ninavitakia ushindi KDF NA AMISOM. Mafanikio yenu ni fahari yetu. Kazi nzuri iliyofanyika vizuri.

  • Athuman
    July 3, 2012 @ 07:09:15AM

    Ninahamu ya kutoona au kutosikia habari za al-Shabaab.

  • Willie Malile
    July 3, 2012 @ 07:05:14AM

    Al-Shabaab, al-Qaeda na vikundi vingine vya kigaidi lazima visagwe kama mchanga kwa sababu wanaishi maisha ya kinyama.

  • Shirleen Bondo
    July 3, 2012 @ 06:31:20AM

    al shabaab hahahahhahah u guys r jst lunatics yaani u wanna destroy our country.....wen we decide 2 get bak at u.....MTAKOMA WENYEWE

  • elijah waituru
    July 3, 2012 @ 06:22:24AM

    Al-Shabaab na kikundi chochote cha wanamgambo duniani kisifikirie kuwa wao ndio binadamu pekee wanaoishi duniani humu,lazima wafahamu kuwa hakuna mtu anayeweza kuumiliki ulimwengu peke yake na tunahitaji kuishi pamoja na kuishi kwa mashirikiano kwa ajili ya maisha mazuri katika ulimwengu wa amani.

  • deafrica
    July 3, 2012 @ 05:34:18AM

    Ninachukia wakati watu wanapotumia dini kuficha matendo yao ya uoga. Ni wanajeshi wangapi wa KDF ni Waislamu? Vipi wanaweza kufikiri kuwa KDF inakwenda kueneza Ukiristo? Hivi si vita vya dini na ikiwa nyinyi AL-SHABAAB mngekuwa Waislamu wa kweli, msingekuwa mnafanya mnayofanya, kuua wasio na hatia, kuteka nyara, na kujiua wenyewe... Hakuna popote katika Koran Tukufu panaposemwa uweni watu wasio na hatia. Kujiua ni HARAM. Mwenyezi Mungu hatetei matendo hayo ya uovu na akili na mawazo ya kiakili yanayoletwa na al-Shabaab. Hivi sio vita vya kidini a.k.a JIHADI. Nendeni mkatafute maana ya Jihadi, hakuna popote panaposemwa kuwa ni mauaji. Vita vya Jihadi ni dhidi ya nafsi yako mwenyewe na msisababishe vita dhidi ya wengine. Mwenyezi Mungu Ibariki Somalia. Mwenyzi Mungu ibariki KDF na AMISOM.

  • Watata
    July 3, 2012 @ 05:18:33AM

    Al-Islam-Ninapenda maoni yako, hasa ile sehemu, “Hii si dini ya vita na ikiwa nyinyi al-Shabaab mngekuwa Waislamu wa kweli, msingekuwa mnafanya mnayofanya, kuua wasio na hatia, kuteka nyara, na kujiua wenyewe… Hivi sio vita vya kidini, a.k.a JIHADI. Nendeni mkatafute maana ya Jihadi. Hakuna popote panaposemwa kuwa ni mauaji. Vita vya jihadi ni vita dhidi ya nafsi yako mwenyewe na sio kuanzisha vita moja baada ya vyingine.” Vikundi vyote visivyo halali vinavyoua watu wasio na hatia siku baada ya siku kwa jina la jihadi wanaharibu imani nzuri ya Waislamu. Watu wengi wanaweza kuamini hivyo ni vita vya Kiislamu wakati sivyo. Nadhani wakati umefika kwa viongozi wa Kiislamu kuwa imara dhidi ya kikundi hiki na kwa kuueleza umma maana ya maneno kama JIHADI kupitia magazeti na vyombo vyingine vya habari vya kijamii kama vile Facebook, Twiter n.k. Nina hakika mia kwa mia kuwa viongozi wa kikundi hiki hawajaui sana kuhusu Koran, hudonoa tu baadhi ya naneno kutoka Koran yanayofaa kwa madhumuni yao. Mimi sio Muislamu lakini sipendi njia ambayo dini nyingine zinafanya kuamini kuwa Waislamu wako dhidi yao (kama kwamba kuwa Muislamu maana yake ni kuwa katili).

  • awilo
    July 3, 2012 @ 03:44:28AM

    Maneno mazuri na muweke Nchemuya. Mungu Ibariki KDF na watu wa Somalia wakati wanachagua serikali yao mpya.

  • George
    July 3, 2012 @ 03:09:55AM

    Al-Shabaab, kimbieni kwa maisha yenu mnayoyapenda wala msitazame nyuma. Kimbilieni gereza lililo karibu yenu na mjipeleke wenyewe huko. Hii ndio njia pekee mnayoweza kuokoa ngozi zenu kwa siku chache kidogo, vinginevyo mama wa operesheni zote anakuja na sioni kama mtapona.

  • Ba` Mtumishi -Hombolo dodoma
    July 3, 2012 @ 01:13:55AM

    mi nadhani lazima ifike hatua ubinadamu uthaminike leo alshabab wakisota wengine hawatarudia unyama kama wao

  • Kathy Kaytes
    July 2, 2012 @ 09:42:56PM

    Mungu awalinde KDF. Wanafanya kazi nzuri.

  • Black Owl
    July 2, 2012 @ 09:11:35PM

    Watu wa Kenya, na hasa Wakristo, hawana watakachopata kutoka kwa mashambulizi ya kijeshi kwenye ardhi ya Somalia kwa kueneza Ukristo kama al-Shabaab wanavyodai. Sisi Wakenya hatupendi vita. Kwa ujumla vita havilipi na katika hali nyingi - ni upuuzi mtupu. Babu zetu walipigana na Waingereza wakati wa kuikalia Kenya kwa mara ya mwisho. Ni kutokana na kile walichojifunza ndicho kilichowafunza wazazi wetu kuwa vita lazima viepukwe kwa gharama zote isipokuwa tu kama ni lazima. Hivi ndivyo wazazi wetu walivyotufunza. Kwa hivyo, madai yao kuwa Kenya iliivamia Somalia ili kueneza Ukristo ni upumbavu na uovu. Kwa jumla, Ukristo katika ulimqengu wa leo haushambulii eneo lolote ili kueneza dini. Kenya haina haja ya kuvunja heshima, majivuno na dini ya watu wa Somalia. Hata hivyo, sisi tunasisitiza kuwa Wasomali wapate haki ya uongozi wao ili iweze kuwadhibiti kwa ufanisi watu wenye siasa kali ndani ya mipaka yao baada ya AMISOM kumaliza operesheni zake. Sisi Wakenya hatutaki tena kuvumilia kipigo cha Somalia inayovumilia, na vita vyake vinavyoenea hadi nchini kwetu. Tunathamini amani, maelewano na umoja. Ni pale tu watu - ndani na nje ya mipaka yetu - wanatishia hiyo, hapo tena tuko tayari kuifurisha ardhi yetu kwa damu yetu wenyewe ili kulinda nchi yetu. Kenya sio Marekani. Ni heshima kufa kwa ajili ya nchi yako. Kwa upande mwingine. hatufuati mchakato unaotakiwa na watu waoga wanakwenda kueneza fujo. Sisi tutawakata vichwa tu, ili mafisi na matai wafanye sherehe.

  • Okeno a.k.a Chile
    July 2, 2012 @ 08:12:34PM

    KUWA GAIDI NI KUPOTEZA WAKATI NA AKILI. WAAMBIENI AL-SHABAAB KUWA SIKU HIZI VITA NI UPUUZI SASA WAANGALIE JUU YA KUISHI KATIKA SAYARI HII ILI KUFAIDI MAISHA KWA VILE HAKUNA ANAYEJUA IKIWA MAISHA YAKE BAADA YA KIFO KWA SABABU HAIJAWAHI KUTHIBITISHWA BADO NA KWA HIVYO YEYOTE ANAYEJALI KUHUSU MAISHA NZURI BAADA YA KIFO NI MJINGA. KUUA WATU WASIO NA HATIA LAZIMA KUADHIBIWE KWA KUWAUA WAUWAJI. HONGERA ASKARI WA KDF NA SASA NINAWEZA KUJIDAI KUWA MKENYA. KWA WALE ASKARI WA KDF WALIOKUFA KWA AJILI YA NCHI YAO WAKUMBUKE KUWA VIFO VYAO VINATHAMINIWA ZAIDI NYUMBANI KWA KUVIKUMBUKA VIFO VYAO KAMA ASKARI WA KWELI NA SIO WAOGA WANAOOMBA MAISHA ZAIDI ULIMWENGUNI WAKATI MUDA WAO WA KUFA UMESHAFIKA. KENYA HOYEH!

  • kayorodoi
    July 2, 2012 @ 05:11:22PM

    Kiasi cha asilimia 99 ya wale wanaotoa maoni ni Wakristo. Mmmmmmh, nafikiri kitu fulani hakiko sawa, kuna baadhi ya ukweli kuhusu al-Shabaab. Lazima nikitafute. Mwenyezi Mungu wanyanyue.

  • sophia
    July 2, 2012 @ 01:02:42PM

    Mambo! Timu ya Kenya, Mshusheni Goliath kwa jina la Bwana. Tunaomba bila kuchoka kwa ajili yenu na Mungu atawapeni USHINDI!!!!

  • newton lugogo
    July 2, 2012 @ 11:55:32AM

    Endeleeni na kutenda mema, al-Shabaab na vikundi visivyo na maana lazima vishindwe, na sote tuombe kwa ajili ya amani kwa watu wa Somalia.

  • wilson Letuati
    July 2, 2012 @ 11:52:15AM

    Huu ni mziki mzuri kuusikia. Shukurani kwa Mungu watu hawa wasio na huruma wanashindwa. Nimefurahi kuwa hatimaye Waislamu wanaomuogopa Mungu wanaikomboa nchi yao. Tunamuomba Mungu kuzifunga njia zote za kutorokea viongozi hawa makatili wa kikundi.

  • K E Mwaniki
    July 2, 2012 @ 10:26:50AM

    Ninaipenda hii.

  • margaret wairimu
    July 2, 2012 @ 09:06:56AM

    Vita vya mwili kwa mwili ni chaguo la mwisho? Itakuwaje kama tungejaribu diplomasia? Mengi ya vitendo vyetu vinasukumwa na kiwango chetu kidogo cha elimu, pengine tungeongeza elimu yetu nchini Somalia. Elimu ni msingi wa mwamko wa haki zetu za binadamu. Ikiwa tutajua umuhimu wa heshima ya binadamu, hakuna mtu angejaribu kuingilia kati utaratibu wa mfumo wa kimataifa. Upungufu wa nyenzo na umasikini visichukuliwe kuwa ni sababu ya mizozo na kupoteza maisha ya watu wasio na hatia. Kila mtu ana haki ya kuishi. Tutatue mizozo yetu kidiplomasia na kuepuka umwagaji damu kwa jina la mipaka yetu.

  • Peter Gunja
    July 2, 2012 @ 08:29:38AM

    Al-Shabaab wangejifunza kutoka kwa uzoefu mchungu waliowasababishia Wasomali. Siku zao zinahesabika na ninatamani zifikie mwisho karibuni.

  • tsarlove blaq amoh
    July 2, 2012 @ 08:09:46AM

    Mwenyezi Mungu ni Mkubwa!!! [God is Great!!!]

  • KEVINE MARTINS
    July 2, 2012 @ 06:04:03AM

    Shukurani kwa Jeshi la Ulinzi la Kenya, TFG NA AMISOM KWA KUWAOKOA WASOMALI KUTOKA KWA WANAMGAMBO WA AL-SHABAAB - BWANA ABARIKI KAZI YENU NZURI

  • obadia kamau
    July 2, 2012 @ 04:51:42AM

    Ni vyema kujua kwamba licha ya kupoteza kaka na dada zetu, ni kwa dhamira ya haki. Kuweni na imani kwani ushindi upo karibu.

  • wambui chebbe
    July 2, 2012 @ 04:23:10AM

    Endeleeni KDF. Uonesheni ulimwengu kwamba mnao uwezo. Ninaona fahari juu yenu.

  • njeru mbae
    July 2, 2012 @ 03:07:50AM

    Kamwe hawakufikiria kwamba KDF lina uwezo mkubwa, kwa vile Kenya haijawahi kwenda vitani lakini hii ni kuonyesha uwezo wa KDF. Wacha al-Shabaab wajue kwamba tuko tayari kugharamikia kulinda mamlaka yetu na hawatotutisha kwa vitendo vyao vya kiwoga kama mashambulizi haya ya karibuni. Tunaamini kwamba kwa kuwa KDF linawashughulikia magaidi hawa, tutalimaliza suala hili. Hongera KDF.

  • wycliffe mutoro
    July 1, 2012 @ 07:31:25PM

    Mungu asiwe na wanyama hawa. Kwa nini wanapigana vita wanavyoshindwa? KDF ni sawa na watu wenye uwezo kupita kiasi.

  • FRANCI NDUNGU FROM MWEA MAKUTANO
    July 1, 2012 @ 07:07:24PM

    NINATAMBUA HAPA JITIHADA AMBAZO KDF IMEFANYA. JITIHADA ZAO ZIZAE MATUNDA.

  • stephen
    June 30, 2012 @ 04:42:35PM

    Mungu wetu mwema aliye mbinguni wape ushindi KDF.

  • francis katana
    June 30, 2012 @ 11:24:09AM

    Watu wa Somalia wameteseka kwa kipindi kirefu. Majeshi ya AMISOM na SOMALIA lazima wawatoe makatili hawa Kismayu. Na kwa mapenzi ya MUNGU, ushindi upo njiani. Kuua watu kwa jina la Mungu ni kosa. Inanitia kichefuchefu kuona wanawake na watoto wakiteseka kila siku.

  • DK
    June 30, 2012 @ 07:47:48AM

    Utukufu na heshima yote ni kwa MUNGU aliyetupa ushindi huu. Jina lake litukuzwe. Hongera kwa majeshi ya Kenya, TFG na AMISOM. Kwa hakika tunahitaji dunia salama na tunahitaji kuishi kama ndugu kwa sababu sisi sote ni wa Mungu.

  • tony
    June 30, 2012 @ 07:28:15AM

    Hongera jeshi la Kenya. Kazi nzuri. Ninajionea fahari kwenu.

  • Alphonse
    June 30, 2012 @ 07:00:40AM

    Nawaheshimu watu wa Somalia wanaojua haja ya kupigania amani na wasioamini propaganda. Mungu ibariki Somalia.

  • samiir
    June 30, 2012 @ 06:53:03AM

    Al-Shabaab ni kikundi cha kigaidi kilicholetwa ili kuwakatili watu wa Somalia. Mwenyezi Mungu anaona yote kwa wale wanaokosea kujificha nyuma ya dini Yake. Natumai Somalia siku moja itadai nafasi yake katika Afrika na sisi wa Somaliland tunaomba kwa Mwenyezi Mungu tuione siku hiyo. Pia ninawaonya al-Shabaab ambao wamekuwa wakitukatili kwa muda mrefu, wawe na tahadhari kwani hatuwezi kuvumilia zaidi.

  • LUCKYONE BONI
    June 30, 2012 @ 06:37:47AM

    MUNGU ANASEMA USIUWE KATIKA AMRI ZAKE SI WAISLAMU WALA WAKRISTO. ALIKUSUDIA KILA MTU. SASA KWA NINI MTU AITOE ROHO YA MWENZAKE. HUO NI UNYAMA.

  • ALOYS NYANG'AU
    June 30, 2012 @ 04:05:05AM

    Mungu awasadie wale wote wanaofanya kazi kubwa ya kuikomboa Somalia. Watu wa Somalia wapate amani.

  • michael onyango
    June 30, 2012 @ 03:49:00AM

    Majeshi ya Marekani yalishindwa lakini Jeshi la Kenya linaweza kwa uwezo wa Mungu. MUNGU IBARIKI KENYA.

  • AL-Islam
    June 30, 2012 @ 03:43:27AM

    Ninachukia sana watu wanapotumia dini kuficha matendo yao ya woga. Wanajeshi wangapi wa Kenya ni Waislamu? Wangapi wanaweza kudhani kwamba wanakwenda Somalia kueneza Ukristo? Hivi si vita vya kidini, na ikiwa nyinyi al-Shabaab ni Waislamu kweli, musingelifanya munachokifanya: kuwaua watu wasio na hatia, kuteka nyara na kujitoa muhanga. Hakuna popote kwenye Qur’an Tukufu panaposema “ua watu wasio na hatia”. Kujitoa muhanga ni haramu. Allah hapendelei matendo hayo ya kishetani na mawazo ambayo al-Shabaab wanapandikiza. Hivi si vita vya kidini, kama vinavyojulikana kuwa JIHAD. Nenda mukazinge maana ya Jihad. Hakuna popote inaposema kuwa ni kuua. Jihad ni vita dhidi ya nafsi yako mwenyewe, na sio kufanya vita dhidi ya wengine. Mwenyezi Mungu ibariki Somalia. Mwenyezi Mungu ibariki jeshi la Kenya na la AMISOM.

  • patrick Mitsanze Samson
    June 30, 2012 @ 02:51:13AM

    Hongera Kikosi cha Ulinzi cha Kenya, Jeshi la Taifa la Somalia na AMISOM. Kujitolea kwenu na kazi kubwa. Kupitia sala tumeona ushindi. Shukrani Mungu kwa kutupa usalama katika taifa letu, Kenya. Tunaiombea Somalia kuwa taifa TUKUFU, NCHI ya amani. Ewe Mungu, tusaidie!

  • SUDHE JOSEPH
    June 30, 2012 @ 02:15:35AM

    AMISOM wanatakiwa kufanya kazi kubwa zaidi kuhakikisha kuwa al-Shabaab na wanamgambo wake wanashindwa. Ningependa kuwashukuru wanajeshi wa Kenya kwa kazi nzuri wanayoifanya nchini Somalia. Mungu awabariki nyote!

  • Ogara
    June 30, 2012 @ 02:14:44AM

    Laiti ulimwengu uko salama, lakini mara nyingine unalazimisha watu kama KDF kuchukua hatua. Wakati nikipongeza ushindi dhidi ya al-Shabaab, ninataka kuwaomba Waislamu wasitumie uongo kuwapeleka wapendwa vitani, ili kuuliwa tu wakati bado maisha yao ni dhaifu. Wale wanaowatumia watoto kama hawa wajitokeze, ama kwa mazungumzo au kukabiliana na risasi. Kwa nini mnajificha ikiwa nyinyi ni wakweli?

  • Edwin Kemboi
    June 29, 2012 @ 03:33:58PM

    Kwa mara ya kwanza ulimwengu umegundua kuwa jeshi la Afrika ni zuri zaidi duniani. Ulimwengu wote umeishaachana na Somalia mpaka pale vikosi vya KDF vilipoamua kuwa sasa inatosha na kama askari wazalendo, wakaamua kuleta amani kwa majirani wao waliochanganyikiwa. Heshima kwa KDF. Marekani na kombora yao walikimbia na kuondoka Somalia na aibu, vikosi vyote vya Ulaya viliogopa Somalia. Wengine walikuja na kuondoka, lakini KDF imefanya kile ambacho mwaka mmoja tu uliopita kilifikiriwa hakiwezekani. Wanaokosoa walifikiria kuwa Kenya ilikuwa na wazimu lakini tumethibitisha kwa ulimwengu kuwa sisi ni kikosi bora zaidi ulimwenguni na hatumuogopi yeyote. Kwa hivyo yeyote yule asijaribu tena kuchezea mipaka ya nchi yetu. Tutampiga vibaya!!! Wakati vikosi vya KDF vilipoingia Somalia, karibu nijiandikishe jeshini ili kuwakomboa watu wa Somalia walioteseka kwa muda mrefu. HESHIMA KWA KDF, HESHIMA KWA KENYA, MUNGU IBARIKI KDF, MUNGU IBARIKI KENYA.

  • alex
    June 29, 2012 @ 02:19:09PM

    Kila la heri AMISOM. Tunaomba amani kwa majirani na ndugu zetu wa Somalia.

  • JOHN KASSAM
    June 29, 2012 @ 02:02:29PM

    Mungu ibariki KDF, Mungu Ibariki familia zao, watu wa Kenya, kwa msaada wao waliotoa kwa KDF tangu askari wetu shujaa walipovuka mipaka kuvitafuta vigenge vya kihalifu vinavyoitwa al-Shabaab. Majambazi hawa wamewaibia amani yao watu wapenda amani wa Somalia kwa miaka mingi. Fikiria raia wa Somalia wanavyofika kwa ukatili wa al-Shabaab kwa miaka yote hiyo. Ushetani wao sasa umeshindwa kabisa na wakati umefika kwao kukabiliana na hukumu ya Mungu. Kesi yao haina kukatiwa rufaa. Lazima washindwe kwani wataangamizwa na KDF. KDF imeuthibitishia ulimwengu kuwa si askari wa taaluma lakini ni hatari wakichokozwa. Kama unataka kujua zaidi juu yao, waulizeni al-Shabaab na washirika wao.

  • Muhsin
    June 29, 2012 @ 01:36:10PM

    Enyi mnaotaka utukufu kutoka kwa makafiri. Mnataka wakusifuni kuwa mnaandika mambo ya kuwasaliti waislam ili wakusifuni? Utukufu wote ni Allah naye atawadhalilisha wanafiki na makafiri na atawakusanya katika jahannam wote. Mnaungana na vyombo vya Kikafiri na kishetani vya Kimagharibiu kusema propaganda za uongo ili muhalalishe mauaji kwa waislam. Allah atawadhalilisha duniani na akhera.

  • mulu kilinga
    June 29, 2012 @ 10:19:42AM

    Hoyeeeee, ushindi uko mikononi mwenu, endeleeni kwa bidii!

  • JAMES KARANJA
    June 29, 2012 @ 09:39:20AM

    Al-Shabaab hamna nafasi huko Somalia. Hata kama mtaenda kwenye msitu mkubwa, lazima mtafutwa tu. KDF wanakuja kwa hivyo jitokezeni na mjisalimisheni.

  • islamic fellower
    June 29, 2012 @ 09:37:40AM

    Hakuna isipokuwa AL-SHABAAB. Mwenyezi Mungu atawalindeni na Mwenyezi Mungu akitaka atawajaalieni pepo. MAREKANI nyinyi ndio magaidi katika ngozi ya msaada.

  • REUBEN NJOROGE
    June 29, 2012 @ 09:30:38AM

    Majeshi yetu ya Kenya ndio hodari zaidi ulimwenguni kote na nina imani kubwa sana wataleta ushindi.

  • Sagero Zedekiah
    June 29, 2012 @ 09:29:29AM

    KDF yote inag’ara sio kwa Wakenya tu bali kwa wengine pia. Mungu awajaalie uwezo kwa hili.

  • Andrew Kamenju
    June 29, 2012 @ 09:13:16AM

    Kwa watu wa Somalia, ungeni mkono juhudi za vikosi vyenu na washirika wake ili kuikomboa nchi yenu. Tujenge eneo lililo salama, lenye amani, mafanikio na maendeleo ndani ya Mashariki na Pembe ya Afrika. Nyinyi ni nchi mnayofanya kazi ngumu, tunao nyinyi katika ukanda huu na tunaelewa jinsi mlivyo kwa eneo hili. Sisi ni kichekesho katika eneo hili. Nyinyi ni sehemu ya eneo hili. Tuna shughuli nyIngi za pamoja – kumbukeni kuwa kwenye mashindano ya mpira wa miguu ya Afrika ya Mashariki na Kati na shughuli nyingi za pamoja – sasa hamko tena kule – tunawahitaji mabibi na mabwana. Mungu awabariki nyote.

  • BILLY
    June 29, 2012 @ 09:08:33AM

    KILA LA HERI ASKARI, MMEIFANYA SERIKALI YA KENYA KUJIVUNIA NYINYI. MWENYEZI MUNGU AWAZAWADIE ZIADA KUBWA. KENYA OOYEE!!! KENYA YAAAA!!!!

  • baba junior
    June 29, 2012 @ 07:53:03AM

    Wakati amani inatakiwa kuwa muongozo wa mafundisho katika mioyo yetu, wakati unakuja wakati jicho linapochungulia, uovu, ulafi, upuuzi, ufisadi, uuaji, uoga, wazimu, uporaji, ushetani na magengi yasiyojulikana kama al-Shabaab, lazima yasimamishwe ili kuleta ustaarabu, na unyofu wa kitaifa. Ni hapo tu, ndio taifa litafikia ukuaji halisi wa kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwa nini basi mabwana wa vita wachache wasiojua kusoma wala kuandika wameachwa kwa muda mrefu na kuharibu maisha, kuharibu mifumo ya kijamii, kuua uchumi wa nchi yao na hata kuendeleza ujambazi huo huo kwa jirani yake mpendwa? .. Jirani ambaye amezichukua familia za Kisomali na kuishi nazo miongoni mwa dada na ndugu wengine wanaopenda amani na kuwachukulia kama ndugu. Aibu gani kwa jirani kuweza kuigeukia nyumba ambayo inawalisha watoto wa jirani yake? Al-Shabaab hawawezi hata kufikiria jinsi wanavyoiumiza Kenya! Ni kweli kuwa waathirika wachache wameteseka kutokana na KDF lakini kitu kimoja ni kweli, KDF isilegeze kamba hadi majambazi hawa ambao hawajui mzazi, kaka, dada, jamaa au jirani watakapolizwa chini na kufutwa katika vitabu vya historia. Vita vya kiakili vinavyooneshwa na KDF vinaonekana wazi kwa sababu wamewafuata majambazi hawa na sio kuwasumbua raia waliochanganyikiwa. Kutoka Afrika, wameuonesha ulimwengu namna gani vita vya kisasa vinaweza kupiganwa kupitia kuwahusisha wananchi, huruma, kuwavutia wahanga na kwa kutumia akili kutoa huduma za kidugu kwa wahalifu. Sio hadithi za kutunga za akina Swatzeneger au Rambo zinazofaa bali...

  • clement wambua
    June 29, 2012 @ 06:34:10AM

    WAAAW! Kenya ni nchi yenye nguvu…ninaipenda nchi yangu Kenya...

  • Towett joseah
    June 29, 2012 @ 06:25:23AM

    Al-Shabaab, walikuwa hawapigani kwa maslahi ya watu wa Somalia. Ni bora kwao kupumzika. Shukrani kwa KDF na AMISOM. Lakini Kenya lazima iwe uangalifu, kwa tahadhari tu kama huu utakuwa ni ujanja.

  • ben
    June 29, 2012 @ 12:44:06AM

    Lini Kismayo itatekwa? Imeishachukua miezi mingi. Waleteni sili wa majini wa Marekani!

  • MATHEWS MZALENDO
    June 28, 2012 @ 06:18:31PM

    DUA ZANGU NI KWA SOMALIA IWE NA AMANI AMBAKO WATOTO WATATEMBEA MITAANI BILA YA UOGA WA MWIBA WA AL-SHABAAB. KWA WATU WOTE, WANAUME NA WANAWAKE WA AFRIKA YA MASHARIKI AMBAO MNAPIGANA KUIKOMBOA SOMALIA, ‘HONGERA NA HEKO’. NI MUNGU PEKEE ATAKAYEWALIPA KWA MEMA MLIYOFANYA. VIDUMU VIKOSI VYA KDF NA AMISOM NA SERIKALI YA MPITO YA SOMALIA.

  • john
    June 28, 2012 @ 11:52:08AM

    Kweli kabisa! Wazazi wetu, ndugu na dada zetu, watoto wetu pia wameshateseka vya kutosha katika mikono isiyo huruma ya wahalifu, wauaji wa msululu, waliojulikana kama al-Shabaab, wanaojidai kuwa ni Waislamu LAKINI kweli Uislamu unatetea mauaji ya watu wasio na hatia? MUNGU ni MKUBWA. Ninachojua ni kuwa Uislamu ni dini ya amani na upendo na haitetei chochote zaidi ya amani, upendo, umoja. SHUKRANI ZA PEKEE KWA RAIS WA KENYA KWA KUWAKOMBOA WATU WA SOMALIA KUTOKA KWA NONDO HAWA al-Shabaab. HONGERA KIBAKI! MUNGU AKUBARIKI NA WATU WAKO.

  • simon peter
    June 28, 2012 @ 11:23:07AM

    Kila la heri KDF...Mungu akulindwa.

  • josphat mulei
    June 28, 2012 @ 10:48:45AM

    Heshima kwa KDF (askari wetu hawapigani vita, tunajua vita, hebu Wamarekani waelewe) lilikuwa jambo la kuchekesha wakati ule Oguna aliposema tutawapiga punda wote wanaokusanyika.

  • edu
    June 28, 2012 @ 08:05:41AM

    KDF songeni mbele…msijali hata kidogo kukosolewa. Kumbukeni kuwa mara tu ukishakuwa askari, daima utakuwa askari. Ushindi uko pamoja nanyi.

  • njuguna john
    June 28, 2012 @ 07:09:15AM

    Kiingie jahanamu kikundi ambacho hakitarajiwi kuwekwa kule.

  • CATE
    June 28, 2012 @ 05:29:38AM

    Mungu ibariki KDF na serikali ya Kenya kwa njia ambayo mmekuwa mkaidhibiti hali ya Somalia ambayo imekuwa tatizo kwa Afrika Mashariki na Afrika yote. Rambirambi kwa familia za askari shujaa waliopoteza maisha yao wakiwa katika jukumu lao la kulitumikia taifa lao lililopendwa. Bila kuwasahau watu wa Somalia na TFG ambao wameshirikiana vyema na KDF kwa maslahi ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu nchini Somalia. Watu wa nchi hii wameshateseka vya kutosha, hasa wanawake na watoto na hatuwezi kusubiri kuwaona kuishi kwa amani. Heshima kwa KDF na TFG!!! Na Mungu kuwa na utukufu wa ushindi huu kuwa ni ushindi wako.

  • KEVIN
    June 28, 2012 @ 05:11:51AM

    HONGERA KDF NA KARIBUNI MNAELEKEA KWENYE MSINGI MZURI AMBAO MMEANZISHA.

  • Benard Nyongesa Makokha
    June 28, 2012 @ 05:04:42AM

    Hii ni habari nzuri kwa eneo hili na kwa jumuiya ya kimataifa kwa jumla. Al-Shabaab ni genge la wahalifu. Vitendo vyao vimekuwa ni kuua na adhabu yao iwe kifo, ikiwa watapatikana.

  • Korir
    June 28, 2012 @ 04:56:53AM

    Kazi nzuri sana.

  • Patrice Lumumba Omolo
    June 28, 2012 @ 04:53:15AM

    Al-Shabaab wameleta hali isiyokuwa ya utulivu na wameonesha kutokukua katika uongozi wao. Dunia haiwezi kudhibitiwa na kikundi cha wakereketwa wa dini. Tunampenda Mungu na tunaipenda Somalia kufaidi amani yao. Watu hawa wamewakatalia Wasomali amani wanayoihitaji. Waacheni washindwe ili Wasomali waweze tena kufaidi amani yao. Tunaipenda Somalia na tunawataka waishi kwa amani pamoja na majirani zao. Somalia ni nchi nzuri ambayo ina watu mashujaa na wazuri, wakereketwa hawa wanatoa sura mbaya ya nchi.

  • jesse kariuki muiru
    June 28, 2012 @ 03:27:30AM

    Itabidi wachukue mikono yao wenyewe watake wasitake.

  • s.semera
    June 28, 2012 @ 02:30:09AM

    Mwanasiasa/mwanamuziki anayeitwa Munishi anatabiri maangamizi kwa jeshi la Kenya kwa kusema kuwa al-Shabaab ni kama mfupa ambao fisi hawawezi kuubanja, sasa nina hamu ya kuona utabiri wake wa maangamizi.

  • onesmus maritim
    June 28, 2012 @ 01:57:10AM

    Hii ni makala isiyo ya upendeleo na iliyojaa maana. Hakuna nafasi katika ulimwengu wa kisasa kwa ushabiki wa kidini. Uislamu ni ya amani – watu kama al-Shabaab na al-Qaeda wamejenga taswira mbaya kwa vikundi vyengine visivyodhuru na vya amani vya makabila ya Somalia. Kwa mtazamo wako juu ya Pepo – watakutana na muasisi wa uovu, na zawadi yao ni moto wa kudumu jehanamu – na kuwa sehemu ya kuni za moto!!!

  • Kimwaki Kiririmbi
    June 27, 2012 @ 01:40:13PM

    Shukurani zote ziende kwa Mwenyezi Mungu! Al-Shabaab wanajaribu sana kuhalalisha kupigana kwa jina la Uislamu. Uislamu hauruhusu kuteka nyara mali za watu wengine. Uislamu hauruhusu kuua watu wasio na hatia. Al-Shabaab waliwapiga mabomu mahafali katika Chuo Kikuu ambako waahitimu wa udaktari waliuawa. Huo ni Uislamu gani? Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni hakimu wa matendo yote, chochote ambacho al-Shabaab waliwafanyia watu wa Somalia ni ushahidi kuwa ni dhidi ya mafunzo ya Uislamu. Walizuwia misaada ya tiba na ya kibinadamu kwa watu wa Somalia misaada ambayo kikundi chao hawakuweza kutoa, watoto walikufa kwa njaa na maradhi. Haya si mafundisho ya Kiislamu!

  • alshabab
    June 27, 2012 @ 12:04:26PM

    hahahaha

  • hassan
    June 27, 2012 @ 10:40:52AM

    Al-Shabaab ni adui wa watu wa Somalia, wanatumia vibaya dini ili kuwadanganya vijana kwa ajili ya dhamira yao. Natumai kila Msomali atagundua kuwa mustakbali wa nchi yao mama uko mikononi mwao. Hatimaye al-Shabaab watakwenda, lakini amani itashinda? Wanahitaji amani ili kujenga nchi moja iliyoungana chini ya utawala wa Kiislamu...

  • NYAEMA NYALIK
    June 27, 2012 @ 10:19:33AM

    Kwa kweli heshima ya binadamu imepungua kwa muda mrefu kutokana na viongozi wa al-Shabaab na vijana kwa sababu mtu hawezi kulinda dini kwa kuua watu wa dini yake kinyama. Nashangaa ni dini gani wanayoilinda. Tunahitaji turejee ubaoni ili kuelezea maana ya kupigana kwa ajili ya dini. Hii ni ishara ya wazi ya kushindwa kwa al-Shabaab.

  • abu-salem
    June 27, 2012 @ 09:30:41AM

    Jeshi la kitaalamu la Kenya liko kazini. Kwa kweli ninapenda namna wanavyoendelea. Mungu wabariki.

  • Gicharu
    June 27, 2012 @ 09:03:55AM

    Mungu wabariki watoto wetu katika KDF kwa kazi yao nzuri sana. Tunawaombea watu wa Somalia wapate amani.

  • ALI HIREY
    June 27, 2012 @ 08:45:26AM

    Makala nzuri sana, Mwenyezi Mungu alete amani kwa somalia. Tuishukuru UTURUKI, KENYA, UGANDA, RWANDA,na AMISOM. Mwenyezi Mungu awabariki wote. Tunaelewa kuwa KDF wanapigana kukiwa na vifo kidogo sana vya raia sio kama Vikosi vya Marekani BLACK HAWK . Vikosi vya Ethiopia vinajulikana kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika jimbo la Somalia la Ogaden ambalo ni sehemu ya Ethiopia. Natarajia dunia itaikomboa Somalia baadaye kuiokomboa Ogaden na kumuondosha dikteta Miles Zinawi. Ethiopia inataka kutibua amani nchini Somalia kwa maslahi yake ya kichoyo. Heshima kwa Uturuki, KDF, AMISOM

  • james
    June 27, 2012 @ 08:43:33AM

    Askari wetu wanaielewa vyema kazi ya. Heshima kwao. Mungu awalindeni vijana.

  • freedom fighter
    June 27, 2012 @ 08:15:30AM

    Ujumbe huu ni ishara ya udhaifu wa al-Shabaab, wameshapoteza takriban ngome zao zote nchini Somalia. Wamekuwa wakiwatisha watu kwa miaka mingi. Tunazithamini TFG na AMISOM

  • omosh
    June 27, 2012 @ 07:42:25AM

    Hongera KDF kwa kazi nzuri mnayoifanya. Endeleeni kufanyakazi na kuwa waangalifu. Wanaweza wakawa wanapanga kitu cha kipuuzi lakini sisi tuna imani mtaweza kuwasambaratishwa vibaya sana.

  • cornelius mokaya monari
    June 27, 2012 @ 06:56:03AM

    Natumai sasa tuko sawa. Asante Mungu kwa yote.

  • Majani Tyson
    June 27, 2012 @ 06:45:48AM

    Ukosefu wa amani popote pale ni tishio la usalama kila pahali. Wakati umefika kwa ulimwengu wote kuziunga mkono KDF, TFG na AMISOM…

  • anthony kimilu
    June 27, 2012 @ 06:44:59AM

    Hii yote ni kwa ajili ya uovu katika Pembe ya Afrika. Amani, amani, amani, ndio kitu pekee tunachotaka ndani ya Afrika. Kazi nzuri KDF.

  • abud said
    June 27, 2012 @ 06:30:17AM

    Hii inaonyesha namna gani Magharibi umeleta morali dhidi ya wapiganaji lakini kwa hakika Mungu atahakikisha nani ni mshindi na dini gani ni ya kweli……………….

  • Leima
    June 27, 2012 @ 04:56:12AM

    Somalia, kama taifa lolote linahitaji serikali inayofanya kazi, yenye usalama imara na mfumo wa uchumi uliotulia. Wasomali hawastahiki njaa na vifo katika mikono ya magaidi. Heshima kwa Kenya na AMISOM.

  • jiiri
    June 27, 2012 @ 04:00:10AM

    Mababu zetu walipigania uhuru. Philipson, wewe babu yako ni nani? Kwa nini huzungumzii juu ya Kenya yenye amani? Vipi kuhusu wale ambao babu zao hawakupigania uhuru? Kwa hivyo unakusudia wasiachwe peke yao. Wewe ni mjinga.

  • MUSAU
    June 27, 2012 @ 03:31:21AM

    MTU YEYOTE ANAYETAKA KUWEPO NA VITA VYA JIHADI LENGO LAKE NI KUWATOA MUHANGA WATOTO WA SOMALIA NA VIJANA WETU KWA AJILI YA FAIDA ZAO ZA KIBINAFSI. SOMALIA YENYE AMANI NI FAIDA KWA ULIMWENGU WOTE, KENYA, WATU WA SOMALIA NA ZAIDI KWA MUNGU WETU. WADUMU WATU WA SOMALIA HODARI WA KAZI. MUNGU AJAALIE AMANI NA MAFANIKIO YAWE PAMOJA NASI DAIMA MILELE. KIFO KWA AL-SHABAAB NA AL-QAIDA NA MAADUI WA SOMALIA. WATU WA SOMALIA AMKENI NA MSIMAME KWA AJILI YA AMANI NA MAFANIKIO. WALE WANAOWAANDIKISHA ILI MPIGANE WENYEWE KWA WENYEWE KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU, MUNGU WETU, WANAFANYA HIVYO KWA FAIDA ZAO BINAFSI KUPITIA DAMU ZA WATOTO WA SOMALIA AMBAO WALIPASWA KWENDA SHULE. JESHI LA KENYA NA WENGINEO. ENDELEENI KUWAFUATA NA KUWATOKOMEZA MAADUI WA WATU WA SOMALIA. KUMTUMIKIA BINADAMU NI KUMTUMIKIA MUNGU.

  • Lian Aviela
    June 27, 2012 @ 03:29:23AM

    Ninataka kuona tu watu wanaofanyakazi nchini Somalia. Ninataka kuwaona wasomali wanaenda shule na kushindana na ulimwengu wote. Ninataka kuiona Somalia ambapo maisha yanaheshimiwa kuliko chochote, kwa yeyote aliye hai awe Muislamu au asiyekuwa Muislamu (msome Mungu) ambaye alipuliza uhai ndani yetu hakuwa mpumbavu kutuwekea maisha ndani yetu na wewe binadamu huna haki ya kuyaondoa kwa misingi ya kuwa unamsaidia Mungu. Muogope Mungu na kile anachoweza kufanya na kile unachoweza kukifanya kwake. Mungu ni mkamilifu anayeweza kujilinda mwenyewe. Ninataka kuiona Somalia ambapo wanawake wanaishi kwa furaha na kufaidi haki zao. waweze kuimba na kucheza katika harusi za watu wazima sio za watoto. Ninataka kuiona Somalia ambapo majirani wanaweza kutembelea na kukaribishwa na kuondoka bila ya kudhuriwa, kama ambavyo tumewafanyia Kenya wa miaka sasa. Kuiombea Somalia kwa MUNGU WANGU MUWEZA ndio mradi wangu.

  • collins were
    June 27, 2012 @ 03:28:42AM

    Wakati vita vitakapomalizika tutakuwa watu wenye furaha zaidi nchini Kenya. Wazazi wetu watarejea nyumbani na ardhi ya Somalia hatimaye itakuwa huru.

  • naftaly
    June 27, 2012 @ 03:25:14AM

    Uwezo wa Mwenyezi Mungu ushinde mikononi mwa jeshi la Somalia na AMISOM. Somalia yenye amani ndio dua zetu.

  • lexas
    June 27, 2012 @ 02:31:42AM

    KDF mnafanya vizuri sana. Endeleeni.

  • peter mwaura
    June 27, 2012 @ 02:28:25AM

    Watu wowote na akili zao timamu hawatangulizi ajenda ya kidini kupitia vitisho, ugaidi, matendo yasiyo ya kibinadamu kwa watu wao, kutokuwa na heshima miongoni mwa matendo mengine ambayo hayampendezi Mungu, ikiwa wanaamini Mungu katika dini yao.

  • kennedy
    June 27, 2012 @ 02:27:25AM

    TUMEVIJUA VITA KUWA NI KITU CHA KUPIGA CHOCHOTE KINACHOTEMBEA,KINACHOKAA , NA WAMAREKANI, WAETHIOPIA, WAINGEREZA NA WAFARANSA WOTE WAMEONYESHA KUWA NI VITA HIVYO. Lakini katika karne ya 21 vita vimekuwa hivi wanavyofanya KDF. Sehemu ngumu…kupigarisasi chochote kinachotembea ni rahisi lakini ubinadamu wenu je? Natumaini Watu wa Somalia watanyanyuka na kujenga nchi yao na kumbukeni Kenya kwa mafanikio yao yanayotarajiwa.

  • maureen
    June 27, 2012 @ 02:02:45AM

    Hizi ni dalili za mwisho kwa hivyo tuwe na tahadhari sana wakati tunapoona mambo kama haya na daima tumwombe Mwenyezi Mungu kutulinda.

  • OPOSH
    June 27, 2012 @ 01:29:32AM

    Ni aibu kweli ikiwa hii ndiyo wanayoiita Jihadi Tukufu, Kuua dada na kaka wasio na hatia, inatisha kuona watoto wanavyokufa katika kambi za wakimbizi. Mungu awaonyeshe njia watu wake.

  • michael odewa Amollo
    June 27, 2012 @ 01:15:17AM

    Hongera KDF kwa kuleta amani Somalia.

  • G nyaboga
    June 26, 2012 @ 07:49:50PM

    Heshima kwa KDF, siku zote tunawaombeeni. Endeleeni na moyo wenu, tunawapa heshima. Malizeni kazi yenu na mrejee nyumbani.

  • victor osiro
    June 26, 2012 @ 04:01:17PM

    Tumechoshwa na hawa al-Shabaab. Mungu iokoe Kenya.

  • MBECHA
    June 26, 2012 @ 03:46:26PM

    Ni wazi kabisa kuwa kile kinachotokea Somalia ni jihadi, katika historia ya ya Uislamu vita hivi havina mwisho...na mwisho kabisa KENYA NA WASHIRIKA WAKE watashinda, Mwenyezi Mungu akipenda.

  • Gabriel
    June 26, 2012 @ 03:35:54PM

    Hiyo ni nzuri kwa sababu ni mbaya kwa kikundi cha watu kuwakandamiza wengine kwa ajili ya kulinda haki zao na baada ya wote wale waliozikiuka mwanzo.

  • MILLY WERE
    June 26, 2012 @ 02:07:25PM

    So Al-Shabaab can also admit defeat......?You know somehow i thought they would finish us all.Kenya na hii army yetu tuko juu tu yaani.Na haturingi imagine.NAJIVUNIA KUWA MKENYA.

  • vera
    June 26, 2012 @ 01:59:58PM

    nilijua kenya iko mbele.bravo our army

  • Pete A.
    June 26, 2012 @ 01:53:23PM

    Somalia ni nchi tajiri yenye watu wenye juhudi ya kazi, wafanyabashara werevu wanawake na wanaume. Amani nchini Somalia itachochea uwekezaji na fursa za biashara kwa Afrika ya mashariki na nchi nyingine duniani. Al-Shabaab lazima waelewe kuwa watu wa Somalia wamechoshwa na uchoyo wao.

  • Amos Marube
    June 26, 2012 @ 12:16:33PM

    Al-Shabaab waliua askari 500 wa AMISOM kutoka Uganda, Burundi na Ethiopia baadaye wakatembeza miili yao katika njia isiyo ya kibinadamu na kuisulubisha Biblia. Tena Mungu aliamua kulipiza damu ya makomredi waliouawa na Wasomali wasio na hatia kwa kupeleka KDF. Kutoka pande zote (ardhini na baharini), na wameifanya dunia kujivunia kwa kuwaponda al-Shabaab. Mungu amepigana kwa ajili yao na daima Hatawaacha. Kismayo itaanguka karibuni ikiwa tutawaunga mkono watu hawa wenye thamani kwa kuomba sana.

  • waltr kodipo
    June 26, 2012 @ 11:09:16AM

    Kwa nini msemaji anawaambia wapiganaji kuwa watazawadiwa pepo ikiwa watakufa katika uwanja wa vita? Baada ya kufa unatarajia kupata nini wakati maafunza ndio wanakuwa godoro na blanketi lako?

  • george ndole
    June 26, 2012 @ 10:05:00AM

    Mungu aijaalie Somalia amani ambayo wamekuwa wakiihitaji kwa muda mrefu.

  • Martin
    June 26, 2012 @ 09:29:39AM

    Al-Shabaab Pumzikeni Kwa Amani.

  • henry
    June 26, 2012 @ 08:56:43AM

    Mungu ibariki KDF. Nyinyi ni Mashujaa kwa watu wengi. Asanteni kwa kuwakomboa dada na kaka zetu wa ardhi ya Somalia. Askari, nyinyi ndio Musa wa zama hizi.

  • ken
    June 26, 2012 @ 08:35:12AM

    Al-Shabaab lazima wakubali kushindwa, na kuzungmza kwa ajili ya amani na pengine kujiunga na serikali ya mpito na kuendesha uchaguzi miaka mitano ijayo. Jicho kwa jicho huwafanya nyote muwe vipofu. Mguu kwa mguu utatufanya sote tuwe vilema. Al-Shabaab....Amani... Amani.

  • Prof.Musa Lenana & William Mulwa
    June 26, 2012 @ 05:17:49AM

    Mkuu ya Haki za Binaamu na mkurugenzi mtendaji (wa Masuala ya kanda ya Afrika) ya Tume ya Kimataifa ya haki za binadamu na Demokrasia (ICHRD) […] wanatoa wito kwa serikali zote ulimwenguni kuunganisha juhudi zao pamoja na vikosi vya serikali za Umoja wa Afrika nchini Somalia kuweka mipango ya mikakati ya kiintelijensia ambayo itawang’oa Wanamgambo wote waliobakia wa al-Shabaab wanaojikusanya nchini Somalia na kukusanya vifaa vyao vya kijeshi, kuwakamata wanamgambo wenye silaha ambao wamesalimika na silaha za Umoja wa Afrika kwa kutafutwa kutokana na mauaji, utumiaji nguvu, kwa kuwa wanachama wa kikundi cha wanamgambo wenye silaha ambacho kimekuwa kikifanya uhalifu dhidi ya ubinadamu. Kamisheni ya ICHRD inamtaka kiongozi wa al-Shabaab AHMED ABDI anayejulikana kama Mukhtar Abual-Zubair au Godane kujisalimisha kwa hiari yake sasa kwa vikosi vya Umoja wa Afrika na kuacha kujipotosha wenyewe kuhusu jihadi kwa vile jihadi hutumika na Waislamu kuhusu imani ya Kiislamu pekee kama inavyoelekezwa na Koran Tukufu na muanzilishi wa imani ya Kiislamu Mtume Muhammad. Vitendo vya al-Shabaab vimekuwa vya kigaidi, kinyume na Mungu, uhalifu wakiwango cha juu unaoeneza mauaji, utumiaji nguvu, kuzinyanyasa haki za jamii za Wasomali na uhalifu dhidi ya binadamu, kuteka nyara watoto na kuwafunza kupigana kama watumwa na kupigana bila kutaka. Makabila yote ya Somalia yameshajua haki zao na hawatajiunga na kikundi haramu cha Al-Shabaab kinachojikusanya chini ya kikundi cha mujahidina wa al-Shabaab.

  • papara mukanda
    June 26, 2012 @ 05:11:50AM

    Tunaendelea kwa kasi kubwa ya kusitisha mateso ya watu wa Somalia ndani ya mikono ya wezi {al-Shabaab}. LENGO LETU ni kuwakamata viongozi wao na kuwafungia magerezani mwetu ili kaka na dada zetu waache kuteseka mara moja.

  • carmichael
    June 26, 2012 @ 04:08:32AM

    Al Shabab ni lazima iangamizwe kwa sababu ya maafa iliyowasababishia wananchi wa Somalia kwa watu wasio na hatia wakiwamo wanawake na watoto - ni lazima wafyekwe. Sitaki kuamini kama kweli kuua watu wasio na hatia ndiyo Uislamu mbona tunaishi miongoni mwa waislamu ambao ni wema na wacha Mungu? Ama kweli hizi ni siku za mwisho ambazo upendo wa watu umepoa.

  • Nyambura Njuguna
    June 26, 2012 @ 02:08:48AM

    Mungu libariki KDF letu na washirika wake. Idumu amani.

  • Grace
    June 26, 2012 @ 01:27:19AM

    Habari nzuri. Dua zangu kwa askari wote wa Somalia. Hatutaki vikosi vya uovu.

  • joana
    June 25, 2012 @ 03:32:04PM

    Kila la heri Somalia. Amani inahitajika kweli kabisa.

  • muthee
    June 25, 2012 @ 09:49:36AM

    GOD IS THE ONLY ONE GOD AND HIM ONLY WE MUST FEAR AND RESPECT ALL THAT HE CREATED.HE IS THE ONLY ONE WHO GIVES AND TAKES AWAY OUR LIFES.YOU AL-SHABAAB USIDANGANYIKE KWAMBA UTAPATA VIRGINS IN HEAVEN,LAKINI UNABEBA CHAKULA CHA FUNZA-WORMS

  • PHILIPSON JRN
    June 25, 2012 @ 08:47:29AM

    Tunataka kufaidi amani katika ardhi yetu ya Kenya ambayo mababu zetu walipigana kwa ajili ya uhuru. Al-Shaaab, tuacheni peke yetu.

  • Kihara
    June 25, 2012 @ 08:24:52AM

    Al-Shabaab washindwe,ni jambo zuri kwa watu wa Somalia. Watu wa Somalia wasiteseke kwa uhuni.

  • Gilbert M
    June 25, 2012 @ 07:48:55AM

    Makala hii ni nzuri. AMISOM lazima wawafuate al-Shabaab hadi maficho yao ya mwisho. Ulimwengu umeshateseka sana na hatuna huruma hata kidogo. hongera kwa wapiganaji wazuri wa AMISOM.

  • tosh
    June 25, 2012 @ 07:13:42AM

    Murphy, kwa taarifa yako ni kuwa vikosi vya Kenya vinakaribia Kismayo kuliko vikosi vyovyote vilivyomo Somalia. Kwa kweli Kenya haipigani na majirani zake bali kwa sababu ya mkataba wa IGAD wa kutopeleka mejeshi katika nchi mnazopakana. Uganda haina mpaka na Somalia, Ethiopia ilikuwa na mambo yake na Eritrea ambayo inajilipizia kwa Somalia lakini Kenya hatukua na lolote na hawako vitani na Somalia bali ilitumia kifungu cha 51 cha Usalama cha Umoja wa Mataifa kinachowaruhusu kuwafuata wanamgambo hadi mafichoni kwao na kwa hivyo Somalia sasa ina amani katika maeneo yote waliyoyakamata. Lazima ujifunze na kukubali ukweli kuwa mwenendo wa vita sio kuuliwa bali kushinda kukiwa na idadi ndogo au kutokuwepo na vifo kabisa.

  • Godfrey Ojiambo
    June 25, 2012 @ 06:49:07AM

    Somalia iliyotulia ni amani kwa Kenya, hakutakuwa na biashara ya silaha ndogondogo ambazo zinaishia katika mikono ya wahalifu ambao wanawaua wafanyakazi wazuri wa kenya.

  • anonymous
    June 25, 2012 @ 06:41:27AM

    Tunawatakia ushindi KDF NA AMISOM. Ushindi wenu fahari yetu. Kazi nzuri, hongereni.

  • Derrick Israel
    June 25, 2012 @ 06:02:14AM

    Inaelekea kuwa kweli na ni bora iwe hivyo na tunatumai sana kuwa tishio la Al-Shabaab halihusiani na chochote na shambulio la guruneti huko Mishimoni.

  • KISASI
    June 25, 2012 @ 05:50:11AM

    Hongera KDF, TFG na AMISOM kwa kazi nzuri sana, Kumbuka kauli mbiu ya kupigana, "Mbele daima, nyuma mwiko" Wapigeni na kuwasaga hadi dakika ya mwisho. Ulimwengu wote na hasa raia wasio na hatia wa Somalia ambao kwa sasa wanateseka watafurahi kuona Somalia inakombolewa kutoka mikononi mwa genge la kigaidi lisilo na huruma, AL-SHAABAB.

  • Ullembe Nyahera
    June 25, 2012 @ 05:24:34AM

    Its sweet melody.Finally Al-Shabaab is perilously close to losing .Never again will they perceive Kenya as a sitting duck 'washindwe na walegee kila sehemu ya mwili'

  • kenyan
    June 25, 2012 @ 05:21:53AM

    Siasa na uwezo ndilo viongozi wanalolitaka kwa sasa...vita lazima visimamishwe!!!!!

  • bingi
    June 25, 2012 @ 03:39:49AM

    Kama Muislamu imara naamini kuua watu wasio na hatia kwa jina la jihadi sio sahihi hata kidogo, bila ya shaka wote au wengi wa watu wa Somalia ni Waislamu na wanapigana wao kwa wao. kwa hivyo hii ndio mnaiita jhadi? Hamna aibu.

  • joan
    June 25, 2012 @ 03:29:17AM

    Heshima kwa jeshi la Kenya, mmetufanya tujivunie.

  • joel
    June 25, 2012 @ 03:22:58AM

    Viongozi lazima siku zote wajaribu kuleta amani kwa migogoro yote iwe kwa hali ya chini au ya juu kwa sababu mwisho unaweza kuona kinachowatokea majirani zetu kutokana na kutoelewana kidogo, kwa hivyo lazima aina fulani ya kusikiliza mazunguzmozo ya pande zote mbili kwa ajili ya faida ya pamoja kwa wahusika wote hasa wale walio dhaifu na wasio na ulinzi. Kikubwa kiko kwa wale wenye nguvu na wale wasio na nguvu kwa sababu kuwa mtu mmoja kwangu mimi ni kuwa na nguvu, na wale wanaochukua dhamana ni lazima wawalinde watu kuliko kutangaza vurugu. Mazingira ya amani huleta utajiri kwa raia na pia afya zao zinakuwa nzuri kwa vile wana uchumi nzuri. Inasikitisha kuona mataifa yote ya Kiafrika yamefanywa yawe ya kijeshi na wale wanaothamini uwezo kuliko ustawi wa wanaowatawala.

  • tonny
    June 25, 2012 @ 02:51:35AM

    Heshima kwa KDF, iangushe ngome imara ya mwisho ya al-Shabaab- bandari ya Kismayo. Vijana wetu wanahitaji kurejea nyumbani.

  • edward
    June 25, 2012 @ 02:46:45AM

    Inawezekana al-Shabaab wanatumia mbinu. Ni lazima tuwe uangalifu zaidi.

  • daxon omari
    June 25, 2012 @ 02:27:47AM

    DAMU YA YESU KRISTO ALIYESULUBIWA KWA MAPENZI YAKE KWETU IMEMWAGIKA,IMEIFUNIKA SOMALIA NA KUPELEKA NGUVU IMARA ZA MAPIGANO NA UJASIRI WA VIKOSI WASHIRIKA ILI KUWAKOMBOA WATU WA SOMALIA KUTOKA MAKUCHA YA SHETANI ANAYEITWA AL-SHABAAB. NA MAMA YETU MTAKATIFU NA BIKRA MARIA MWENYE USHINDI ANALETA AMANI KWA NGUVU KWA KUZIKOMBOA NA KUZIUNGANISHA FAMILIA. MUNGU MWENYE UWEZO AMALIZE KAZI ALIYOIANZA. HURUMA ZA YESU NA MARIA TUNATUMAINI KATIKA ROHO ZENU ILIYOKOMBOKA, MADHUBUTI. AMINA, AMINA, AMINA.

  • muregi moses
    June 25, 2012 @ 02:24:40AM

    Wakati amani ni lazima katika mioyo yetu, unafikiwa muda ambao kuchungulia jicho, uovu, ukorofi, ulafi, upuuzi, utundu, uuaji waoga, uporaji kichaa, maoni ya ushetani kwa magenge yasiyojulikana kama al-Shabaab lazima kusimamishwa ilikuleta ustaarabu, na unyofu wa kitaifa. Ni hapo tu, ndio taifa kufikia ukuaji halisi wa kiuchumi kisiasa na kijamii ukuaji. Kwa nini basi mabwana wa vita wachache wasiojua kusoma wala kuandika wameachwa kwa muda mrefu na kuharibu maisha, kuharibu mifumo ya kijamii, kuua uchumi wa nchi yao na hata kuendeleza ujambazi huo huo kwa jirani yake mpendwa? .. jirani mabaye amezichukua familia za Kisomalia na kusishi nazo miongoni mwa dada na ndugu wengine wanaopenda amani na kuwachukulia kama ndugu. Aibu gani kwa jirani kuweza kuigeukia nyumba ambayo inawalisha watoto wa jirani yake? Al-Shabaab hawawezi hata kufikiria jinsi wanavyoiumiza Kenya! Ni kweli kuwa waathirika wachache wameteseka kuokana na KDF lakini kitu kimoja ni kweli, KDF isilegeze kamba hadi majambazi hawa ambao hawajui mzazi, kaka, dada, jamaa au jirani watakapolazwa chini na kufutwa katika vitabu vya historia. Vita vya kiakili vinavyooneshwa na KDF vinaonekana wazi kwa sababu wamewafuata majambazi hawa na sio kuwasumbua raia. Kutoka Afrika, wameuonesha ulimwengu namna gani vita vya kisasa vinaweza kupiganwa kupitia kuhusika kwa wananchi, huruma, kuwashinda wahanga na kwa kutumia akili kutoa huduma za kidugu kwa wahalifu. Sio hadithi za kutunga za akina Shwartzenegger au Rambo zinazofaa bali akili!

  • b. j.massawe
    June 25, 2012 @ 01:56:03AM

    Al-Shabaab waende jehanamu. Dini nzuri ya dada na kaka zetu Waislamu imekuwa ikipotoshwa na wauaji hawa wanajidai mabalozi wa uislamu. Kwa hakika wataangamia.

  • bonyi evans
    June 24, 2012 @ 04:51:04PM

    Ni jeshi letu lililofanya juhudi za kuanza kuwakomboa Wasomali kutoka jehanamu katika ardhi yao wenyewe, nchi nyingine za Afrika zisingeshiriki vinginevyo askari wetu endeleeni, MUNGU WETU yuko pamoja nanyi, Amina!

  • N. N. Y.
    June 24, 2012 @ 04:26:38PM

    Tunataka Somalia na Afrika ziwe na amani.

  • carlos omamo
    June 24, 2012 @ 03:31:34PM

    Askari wa Kenya mnafanya vizuri.

  • tadman
    June 24, 2012 @ 02:05:53PM

    Huu si wakati wa kujipiga kifua na kuchukua sifa zote. Uganda, Ethiopia, Kenya, Uturuki na Burundi zote zimechangia katika mafanikio ya Somalia na hakuna nchi yoyote inayostahiki kudai sifa zaidi.

  • alvin
    June 24, 2012 @ 12:38:37PM

    Tafadhali endeleeni kuomba kwa ajili ya taifa ambalo linazaliwa upya.

  • Fredrick were mulago
    June 24, 2012 @ 12:05:30PM

    Amani safi hatimaye itakuja kwa ndugu zetu kwa njia ya Moto. Natamani ingekuja kwa njia yaPeponi, ingedumu milele. Kwa njia gani mtu huko anajitayarisha kwa amani ya kudumu na utulivu nchini Somalia? Kwa vyovyote vile, hawa wanaoshindwa wanakimbila wapi? Ni Kenya au katika kambi za Dadaab kama wakimbizi? Mipaka yetu iko salama kiasi gani leo? Wamepeleka wapi silaha zao? Huko wanakokwenda wanapeleka amani? Tutumaini kila kitu kiende sawa. Mungu Ibariki Kenya. Mungu Ibariki Somalia.

  • kioko
    June 24, 2012 @ 11:08:09AM

    Hongera majeshi yetu ya Kenya, Hongera.......

  • freddy gooner
    June 24, 2012 @ 10:33:58AM

    Vikosi vya AMISOM vimekuwepo Somalia kwa muda mrefu sana bila ya mafanikio makubwa. Ukweli ni kuwa KDF ndiyo iliyokata kichwa cha al-Shabaab na kudhoofisha operesheni zake kusini ya Somalia. Kujiunga kwa KDF katika AMISOM kulikuwa jambo zuri ili kuvipa nguvu vikosi vya AMISOM ambavyo kwa muda mrefu vilikuwa vinapigana na wanamgambo mjini Mogadishu ukiachia mbali miji muhimu ya kusini ya mikakati kwa al-Shabaab . Tuwapeni sifa wanazostahiki na kuwapa moyo majeshi ya KDF na AMISOM kwa kuwasafisha majambazi hawa moja kwa moja, Wasomali wanahitaji amani na maendeleo. Heshima kwa KDF na AMISOM.

  • Kenya Juu
    June 24, 2012 @ 09:39:29AM

    @ Murphy unazungumza upuuzi mtupu na wewe unalijua hilo.

  • abdirshid jama
    June 24, 2012 @ 06:36:13AM

    Tunahitaji amani katika Pembe ya afrika.hakuna kingine bora zaidi kuliko amani...Somalia inahitaji amani zaidi kuliko yeyote mwengine dunia hii... tafadahlini, ipeni amani fursa, somalia nyingine inawezekana sana.

  • Sylvanus
    June 24, 2012 @ 02:03:33AM

    Murphy, nimesikitishwa sana na maoni yako. Uliposema kuwa Jeshi la Kenya liko kilomita 60 tu ndani ya Somalia.....Kumbuka hili, vita hivi ni kuhusu kuleta utawala wa sheria na busara kwa nchi ile. Sijui unatoka wapi, LAKINI JAMBO MOJA NI MUHIMU. Katu hatutofanya kosa ambalo jeshi la Marekani lilifanya wakati lilipoingia Somalia. Soma na uelewe historia yako vyema. Tukija kwa jeshi la Kenya, ikiwa utakuwa umeangalia vyema, JESHI LA KENYA HALIKIMBILII kuiteka Somalia. Lengo lake la msingi ni kuteka kilomita mia kadhaa, kuanzisha muundo wa utawala unaofaa, machifu, wakuu wa wilaya, polisi katika eneo hilo n.k. Jeshi la kenya KATU halitafanya makosa yaliyofanywa na jeshi la Marekani.

  • hamisi
    June 24, 2012 @ 12:47:47AM

    Murphy, sijui wewe uko sehemu gani ya dunia lakini Nchemuya alieleza ukweli ambao wale wanaojiita wenye nguvu kubwa wanaiona ni ngumu kuikubali. Kitendo cha Kenya kilikuwa ni kulipiza kisasi kwa "tabia chafu" za mtoto mdogo. Wakati ndugu mdogo anapovunja kioo cha kompyuta huhamaki na kumfunga jela, Umekosea kujua maana ya maneno ya Nchemuya. Wameweza kupambana na kikundi cha kigaidi kwa mpango uliopangwa vyema, intelijensia... Wazo langu katika maneno yake ni kuwa tofauti na wenye nguvu kubwa ambao dhamiri yao ni kuvifuta vkundi kama hivyo vya waasi, Kenya inaamini katika heshima ya maisha, iwe ni wahalifu au wengine, Katika kutekeleza mashambulizi saambamba, watu wengi wasio na hatia wanakufa na kulemazwa - KD na TFG wasingependa kuona mandhari kama hayo, na ndio maana maendeleo yanaonekana pole pole. NI VITA VINAVYOHESABIWA NA KUTEKELEZWA KIINTELIJENSIA NA USO WA BINADAMU.

  • Peter
    June 23, 2012 @ 07:19:59PM

    Mpendwa Nchemuya, hujui unachokisema kuhusu suala zima. Hili si suala la nani anawashinda al-Shabaab dhidi ya jeshi la Kenya. Watu wengi wamejitolea sana kabla ya Novemba 20, hasa watu wa somalia wenyewe. Natamani ungekuwa somalia kabla (kama mtu binafsi)halafu. Jeshi linajua zaidi bila ya shaka na ndio sababu wao hawasemi sana.

  • Ali Said Mohamed
    June 23, 2012 @ 03:45:12PM

    Endeleeni KDF, mnafanya vyema kwa heshima ya ubinadamu, kitu mnachofanya ni cha heshima na tendo ambalo litakumbukwa katika historia. Tunajivunia nyinyi na familia zenu kila siku.

  • ALLY SWALEHE
    June 23, 2012 @ 02:46:33PM

    AL SHABABU WATETEA HAKI YAO, WAACHWA KUONEWA, SOMALIA NI NCHI YAO WAJIBU WAO KUCHAGUA SERIKALI WAIPENDAO

  • mitcol3
    June 23, 2012 @ 02:34:57PM

    Umesema vizuri Nchemuya, KDF imeweza kuishi na maoni kama hayo yasiyo na msingi hata kutoka kwa mkuu wa nchi wa kanda na zaidi kutoka kwa sehemu ya watu wake wenyewe. Ninajivunia kile wanachofanya nchini Somalia. Wakati umefika hata kwa watu wa Kenya wenyewe kuthamini kwa kutokuwepo kwa vita nchini na amani wanayofaidi mpaka sasa ni kwa ajili ya kizuio kilichofikiwa na KDF. Ninajivunia.

  • wilbroda wanyama
    June 23, 2012 @ 10:51:34AM

    Al-Shbaab pia wangejifunza kuwa licha ya tofauti za kidini, sote tunatokana na MUNGU MMOJA, muumba wetu ambaye hapendi kuua kwa njia wanayofanya na kubadilisha njia ya tabia zao kwa kujua kuwa siku moja watajibu kwa matendo yao.

  • liban
    June 23, 2012 @ 09:12:27AM

    Mimi kama kijana wa Kenya mwenye asili ya Kisomalia kwa kweli ninawashukuru watu wa Kenya na serikali yao kwa sababu wamenipa elimu na amaani ambavyo nchi yangu ilishindwa kunipa, waliheshimu haki yangu. Nafikiri Kenya ina haki ya kulinda watu wake na uchumi wake na dini yetu haimruhusu yeyote kuwakera majirani zake. Kenya ni nchi jirani yetu na tuliikosea kwa kuteka nyara watalii wake hakuna mtu ambaye angekubali hivyo, kwa hivyo, walichofanya ni kwenda Somalia na kwa kweli nimefurahi kwa hatua hiyo kwa sababu al-Shabaab sio tu ni adui wa Kenya bali pia adui wa Somalia na ninataka kuliombea jeshi la Kenya kuwatokomeza kutoka nchini kwetu ili tuishi kwa amani na maelewano katika nchi yetu na majirani zetu.

  • zakayo
    June 23, 2012 @ 08:45:44AM

    Genge hili limesabababisha maisha ya wengi wasio na hatia kuteseka. Hebu wasafishwe kutoka uso wa wengine na kikundi kingine chochote kama wao lazima kifuate mkumbo. Lazima amani utawale duniani na hakuna maisha ya yeyote asiye na hatia yatapotea kwa sababu kuna vikundi vilivyojipanga vya wauaji.

  • DON CORLEONE
    June 23, 2012 @ 07:12:42AM

    Hakuna nafasi kwa magaidi katika Somalia ya sasa. Imeshateseka vya kutosha. Hatutaki al-Shabaab ambao hawajui maana ya jihadi, jihadi si kundi la majambazi na mazimwi.

  • Randiga E O
    June 23, 2012 @ 05:57:46AM

    Wananchi wa Somalia ni binadamu. Wao ni viumbe wa Mungu. Mungu yule yule aliyeumba kila kitu, vyote tunavyoweza kuviona na kuvigusa, na vyote vilivyoko mbali na ufahamu wa mwanadamu. Wameteseka vya kutosha. Wanastahili amani, uhuru na kila kitu chema ambacho Mungu ametukusudia sisi wote. Hebu sote tuchangie katika utekelezaji wa amani ya kweli kwa ajili ya Somalia.

  • osogo odhiambo
    June 23, 2012 @ 05:49:31AM

    Nimeipenda hii

  • P.MEEME
    June 23, 2012 @ 05:08:25AM

    Sisi nchini Kenya tunafurahi sana kwamba hivi karibuni ndugu zetu wa Somalia watakuwa na amani. Ikiwa hakuna amani nchini Somalia hakutakuwa na amani nchini Kenya. Tuna furaha sana kwa kazi nzuri inayoendelea nchi Somalia.

  • samuel kavoo
    June 23, 2012 @ 04:53:09AM

    let ma country Kenya work hard to tackle thi terroristic group since it has led us to enter into alot of troubles tuungane pamoja tumalize AL-SHABAAB.

  • DAVID KARANJA
    June 23, 2012 @ 04:52:41AM

    NINAAMINI kuwa Somalia ni hivi karibuni itatulia. Mungu azisaidie KDF na AMISON kwa kuipa amani nchi hii ya heri.

  • mike
    June 23, 2012 @ 03:45:25AM

    HI. FUNDISHO KWA AL-SHABAAB na wengine wenye akili kama zao, kwa hakika watu hawa watakiri na kujisalimisha na kuacha kupambana na kufikia makubaliano na KDF ya Kenya ili kuokoa maisha ya watu wengine wasio na hatia.

  • Devis
    June 23, 2012 @ 03:10:43AM

    Hii ni hatua nzuri kwa watu wa Somalia. Wanapaswa kusifiwa kwa kurejea nyumbani lakini shetani Al-Shaabab waliwafukuza. Kenya imewapa makazi wahamiaji. Baadhi yao kwa udanganyifu wamejipatia hati za uraia wa Kenya. Si kwamba walizihitaji bali kupata mahali pa kupaita nyumbani. Walitaka kufanya biashara, kuingiliana na watu na kulisha familia zao. Misaada ya wafadhili ilikuwa haitoshi kwa kulisha wote. Tabasamu katika uso wa Kenya inaonekana. Nchi ambayo ilikuwa inaitwa "Jeshi la sherehe" likawa la amani halisi na jeneza la Al.Shaabab. Kama Kenya isingetuma vikosi vyake nchini Somalia, vikosi vya Uganda na Rwanda visingewaweza al-Shaabab. Sasa inaitwa AMISOM, lakini waliharakisha mipango yao ya mwisho kama KDF- Operesheni Linda Nchi. Tuna furaha sasa, kwamba Wasomali watakuwa nyumbani kwao. watoto watakuwa wakiona kuona nchi ya mababu zao kwa mara ya kwanza. Mungu isaidie KDF. Mungu isaidie AMISOM.

  • MARTIN MBATHA KIVINDYE
    June 23, 2012 @ 01:26:05AM

    Ninawaaminieni vijana, nina hakika al-Shabaab watakimbilia mbali.

  • Richard Boit
    June 22, 2012 @ 04:45:56PM

    Bwana Mungu aliliambia Jeshi la Ulinzi la Kenya {kupitia kwa Mtume wake, Dk David Edward Owuor} kwamba yeye {Mungu} anajua kuwa {KDF} wanapambana na mabaya na wao watashinda vita----! Asante Bwana Yesu! Wewe ni mwaminifu!

  • Murphy
    June 22, 2012 @ 09:50:03AM

    Nchemuya unasema nini? Jeshi la Kenya limepata mafanikio katika Somalia lakini bado liko kilomita 60 ndani ya Somalia na mpaka sasa hawajamshinda yeyote. Kenya ilijiingiza tu kwa vile al-Shabaab walikuwa wanaharibu sekta yao ya utalii. Kama hakukuwepo na Mzungu yeyote aliyetekwa, Kenya ingekuwa ni mtazamaji tu. Kenya inatakiwa iheshimu nchi nyingine za Afrika ambazo zimeongoza na kupoteza idadi kubwa ya askari katika shughuli hii. Kenya haiko pekee na si haki kuipa sifa kama hiyo. Tutumaini mzozo huu umalizwe haraka na Wasomali waweze kusonga mbele, itakuwa manufaa kwa kila mtu.

  • mutiria ccharles
    June 22, 2012 @ 08:59:00AM

    Tunataka kuifanya dunia isiyokuwa na vita.

  • danny diesel
    June 22, 2012 @ 08:07:57AM

    Bado haijashindwa.

  • yusuf ngunyi
    June 22, 2012 @ 07:46:42AM

    Watu wa Somalia wanahitaji amani. Tutumie dini zetu kwa kujitukuza wenyewe, Kenya ni kimbilio salama kwa Wasomali, wanajihadi na wengineo. Wanajihadi walifanya kosa kubwa kwa kujaribu kuipiga Kenya. Kenya siku zote ilikuwa daima ni chanzo cha wao kujipatia riziki. Nafikiri bora wangeondoka Kenya kwa usalama wao. Nafikiri watu wote wapenda amani wanaomba ili siku moja kuwepo na amani Somalia ambako wataachana na ukabila.

  • george kalah
    June 22, 2012 @ 05:22:27AM

    Waacheni watu wa Somalia wawatoe wale wanaoitwa wapiganaji wa al-Shabaab wanaowajua kwa viongozi ili wakabiliane na sheria. kama watu wa Somalia wanahitaji amani kwa serikali yao, nchi na watu wa Somalia. Watu wa Somalia ni muhimu zaidi kuliko mtu mmoja mmmoja.

  • Frederick N Chege
    June 22, 2012 @ 05:01:59AM

    Makala hii inavutia sana. Ninaipenda, AMISON endeleeni, juhudi zenu zinazaa matunda katika taifa la Somalia.

  • roy
    June 22, 2012 @ 01:57:35AM

    Heshima kwa KDF, TFG na AMISOM...muwamalise hawa wanojiita al-Shabaab au kwa jina lolote lile na kuleta busara ndani ya Somalia.

  • STEVE
    June 21, 2012 @ 01:32:22PM

    Mungu awasaidie wale wanaopigana ili kuikomboa Somalia. Watu wetu wameteseka kwa muda mrefu. Kifo kimekuwa ratiba ya kila siku na amani ni kiu inayounguza katika roho za Wasomali. Al-Shabaab wanapaswa kufikiri mara mbili, kujisalimisha na kuwaacha Wasomali waishi maisha ambayo Mungu aliwataka waishi.

  • peter kagiri
    June 21, 2012 @ 08:56:31AM

    majeshi wa kenya mko kwenyewe tu sana xo keep up tu na msupport

  • nchemuya
    June 21, 2012 @ 06:12:27AM

    Somo kwa al-Shabaab na wengine wenye akili kama zao...kwa sababu tu baadhi ya nchi hazitaki kupigana haina maana kuwa haziwezi kupigana. Kwa miaka mingi Kenya ilikuwa inatoa onyo kwa al-Shabaab na kujaribu kuwahamasisha waishi maisha ya kistaarabu, maisha ya maendeleo, lakini wema wa watu wa Kenya ulichukuliwa kitu cha bure. Baya zaidi, kwa sababu siasa ya nje ya amani ya Kenya ya kuepuka migogoro kwa gharama zozote, al-Shabaab waliichukulia Kenya sawa na mbwa dhaifu asiye meno. Kwa sababu ya uroho wa al-Shabaab wakaanza kushambulia meli za Mombasa na hata kuvuka mpaka na kuwashambulia watalii. Kuna mazungumzo kuwa hata walitaka kuwauwa maafisa waandamizi wa serikali huko Kenya. Basi... sasa wanapata walichokuwa wanakitaka. Nina hakika jeshi 'lisilojaribiwa wala kupimwa' la Kenya limekuwa kifurushi cha kushangaza. Tofauti na majeshi ya Marekani, Uganda na Ethiopia ambayo yanapiga mabomu chochote kinachotembea, jeshi la Kenya limetekeleza mkakati wawajanja, kuwasumbua na hatimaye kuwakomesha kabisa kundi la kigaidi katika kila hatua. Hakuna anayethubutu kusema jeshi hili (karibu wote walioingizwa Somalia waliwapa lile jeshi 'dogo lisilojaribiwa wala kupimwa' la Kenya hakujna fursa yoyote mwezi Novemba wakati lilipoingia Somalia), lakini ukweli ni kuwa hakuna jeshi jingine katika siku za karibuni ambalo limeweza kupambana na kikundi cha kigaidi kwa mpango imara, intelijensia na mafanikio ya haraka kama haya ya jeshi la Kenya.

  • ali deeqsi love
    June 21, 2012 @ 04:16:27AM

    al shabab alah aa madhiyo

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo