Wapiganaji wa kigeni wa al-Shabaab waonekana huko Shabelle ya Chini

Na Adnan Hussein, Mogadishu

Juni 19, 2012

  • 27 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wakati majeshi ya Somalia na washirika wake wanaendelea kuwasukuma al-Shabaab nje ya ngome muhimu kusini ya Somalia, wanavijiji wanasema wapiganaji wenye mafungamano na al-Qaeda wameonekana huko Shabelle ya Chini.

Wapiganaji wa kigeni wameonekana katika miji ya Barawe na Marka, ambayo bado viko chini ya udhibiti wa al-Shabaab, kwa mujibu wa mvuvi wa eneo hilo Adaawe Mataan.

Mataan aliiambia Sabahi kwamba aliona kundi la wapiganaji wa kigeni katika siku za karibuni wakiwasili katika migahawa chini ya ulinzi nzito wa usalama. Alisema walitumia magari ya magurudumu manne na kuficha wasifu wao kwa kujifunga vilemba au tovinyago vyeusi.

Makadirio yanatofautiana, lakini baadhi ya vyanzo vya habari vinasema kiasi cha wapiganaji 500 wa kigeni wako pamoja na al-Shabaab nchini Somalia.

Usakaji wa al-Shabaab huko Shabelle ya Chini

Jeshi la Somalia limeahidi kuwasaka wanachama wa al-Qaeda nchini Somalia na kufanya kazi ya kuvunja mipango yao ya kuhatarisha usalama wa Somalia na nchi jirani.

Jenerali Ali Araaye Osoble, mkuu wa operesheni katika jeshi la Somalia, aliiambia Sabahi kwamba wanachama wa al-Qaeda wanatafuta maficho katika misitu na mashamba ya Shabelle ya Chini, na kwamba vikosi vya usalama vya Somalia ni kazi bila kusita ya kuwasaka kwa kutumia njia zote iwezekanavyo.

Alitoa wito kwa wananchi wa Somalia kushirikiana na vikosi vya askari ili wakuzuia al-Qaeda wasifanye vitendo vyovyote dhidi ya viongozi wa kidini na kikabila, vikosi vya usalama, viongozi wa serikali au wananchi wa kawaida.

Gavana wa Shabelle ya Chini Abdiqadir Mohamed Nur alisema serikali yake itachunguza kwa karibu harakati za wapiganaji wa Somalia na wa nje ili kuwaleta chini ya ulinzi na kuwashitaki.

"Tutaendelea kuwasaka [wahuni] hawa kwa njia ya uvamizi na usafishaji wa usalama baada ya kuichukua miji ya mkoa na vijiji ambako waasi bado wanatembea kwa uhuru, kwa kutumia fursa ya maeneo ya wazi ya pwani," aliiambia Sabahi.

Duru za kiintelijensia zinaonyesha kuwa wanachama wa al-Shabaab walipita katika kijiji cha Kuunya-Baroow na kukaa huko kwa muda wa siku tatu, alisema, akaongeza kuwa operesheni ya usalama itawakamata wazee wa kikabila wanaoshutumiwa kwa kutoa maficho salama na makazi kwa ajili ya wapiganaji.

Wapiganaji wakimbilia Yemen

Kamanda wa al-Shabaab alithibitisha uwepo wa wapiganaji wanaojulikana, viongozi waandamizi wa kigeni wenye uhusiano na al-Qaeda na al-Shabaab katika Shabelle ya Chini. Alisema wapiganaji wengi wamekuwa wakikimbia Yemen kwa vile majeshi ya pamoja ya Somalia na Umoja wa Afrika wanasonga mbele ndani ya eneo hilo.

Kamanda huyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliiambia Sabahi kuwa kiasi cha wapiganaji 80 na Kiarabu na Magharibi wamekimbilia Yemen kutoka Kismayo zaidi ya miezi miwili iliyopita kutumia boti ndogo, iliyotengenezwa Yemen.

Baada ya kuwasili Yemen, wapiganaji hao walijiunga na Ansar al-Sharia, kundi linalohusishwa na al-Qaeda katika Ras ya Arabuni ambayo wanapigana na jeshi la Yemeni.

Kamanda huyo alisema Wasomali na wageni wamekuwa wakionekana wakiishi katika miji mikuu katika sehemu za mashariki na kusini mwa Yemeni.

Hapo mwezi Machi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Yemeni walikituhumu kikundi cha al-Shabaab kwa kupeleka wapiganaji wapatao 300 kupambana sambamba na al-Qaeda dhidi ya jeshi la Yemeni na vikosi vya usalama.

Katika mwezi huo huo, Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema vikosi vyake vya usalama viliwakamata Wasomali wanne wanaotuhumiwa kuwa ni al-Shabaab kando ya barabara inayounganisha mikoa ya Lahj na Abyan.

Wizara ya Ulinzi ya Yemeni ilithibitisha tarehe 18 Juni kwamba raia wa Somalia alilipua yake fulana yenye mabomu, na kumuua Jenerali Salem Ali Qoton, kamanda aliyekuwa anaongoza jitihada za Yemeni ya kuwashindwa al-Qaeda katika mikoa ya kusini mwa nchi.

Al-Shabaab katika ‘shida kubwa’

Fatima Sheikh Abdilatif, mwenye umri wa miaka 25, alisema yeye alitoroka kutoka al-Shabaab baada ya vikosi vya serikali kuuteka mji wa Afgoye mwezi uliopita. Alisema walikuwa anafanyakazi kwa ajili ya kikundii za kuwapikia chakula chao na kuosha nguo zao kwa mkono.

"Baada ya kutambua kwamba kikundi kilikuwa katika shida kubwa na kwamba hatima yangu ilikuwa haijulikani, niliamua kutoroka kutoka kambi yao huko Elasha Biyaha na kukimbilia katika maeneo ya amani," alisema. "Mimi sasa navaa niqab ili kuficha sura yangu."

Abdilatif alisema wapiganaji kadhaa wa kigeni walikuwa wanakuja kila wiki kufuliwa nguo zao na kuhudhuria mihadhara misikitini na katika maeneo makubwa ya umma karibu na maeneo ya makazi ya watu waliokimbia makazi yao nje ya mji mkuu. Vikosi vya Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia na Umoja wa Afrika viliidhibiti Mogadishu mwezi Machi.

Abdilatif alisema baadhi ya wapiganaji wamefunga ndoa na wanawake wa Somalia na wanao watoto.

Vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika viliudhibiti mji wa Afgoye terehe 25 Mei katika shambulio kubwa la kusafisha eneo la al-Qaeda na wafuasi wao wa Somalia ambao walikuwa kudhibiti mji huo kwa takriban miaka minne.

Al-Shabaab walilazimishwa kuondoka kutoka ngome zake katika Afgoye na Afmadow kutokana na kusonga mbele kwa askari wa Somalia na vikosi vya Umoja wa Afrika vya kulinda amani.

Ingawa al-Shabaab bado wanadhibiti sehemu kubwa ya kati na kusini mwa Somalia wanakabiliwa na mashambulizi ya ardhini na hewani kutoka kwa vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Kenya ambalo sasa linafanyakazi chini ya uongozi wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).

Al-Shabaab wametishia kulipiza kisasi kutokana na kupoteza kwa miji hiyo.

Vikosi vya Umoja wa Afrika na Somalia vyasonga mbele

Jenerali wa AMISOM, Ugadi Kiki alisema shambulio linalofuata ni kuuteka mji wa Balad.

"Baada ya kuuteka ushoroba wa Afgoye, ambao wanaishi kwa watu waliokimbia makazi yao, tunaandaa kuanzisha mashambulizi mengine makubwa dhidi ya wanamgambo waliobaki katika mkoa wa Shabelle ya Chini," Kiki alisema katika mkutano na waandishi wa habari hapo tarehe 8 Juni.

Tuko katika maandalizi ya kuanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa al-Shabaab kwa sababu mpango wetu ni kuunga mkono jitihada za kuyakomboa maeneo ya kando ya Mto Shabelle," alisema.

Naye Jenerali Abdullahi Ali Aanood, Kamanda wa Kikosi cha Kwanza cha jeshi la Somalia, aliiambia Sabahi kwamba jeshi, kwa msaada wa AMISOM, lipo tayari kwa hatua ya mashambulizi dhidi ya al-Shabaab huko Balad kutoka pande zote mbili. Alisema vikosi vya pamoja vinaukaribia mji kupitia barabara kuu inayounganisha na Mogadishu, pamoja na barabara nyingine inayokwenda eneo la kilimo katika eneo la Afgoye.

Aanood alisema vikosi vyake hivi karibuni vitaikomboa miji yote katika Shabelle ya Kati, na hivyo kukomesha utawala wa al-Shabaab katika eneo hilo, kama vile maeneo ya mkoa wa Hiran.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 94)

Dislike_icon(13)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Naitwa lugano
    December 18, 2012 @ 11:21:35AM

    Nawasalimu masomaji enyi alshababi endeleeni na moyo huo huo wa kujituma wala msiludi nyuma mtashinda tuu na kumiliki somalia mungu yuu pamoja nanyi

  • Bonnie Keago
    September 13, 2012 @ 04:56:11AM

    Nzuri sana, lakini tafuteni njia ya kuwaweka pahali baada ya kushindwa. Kama sio hivyo, wataibuka tena.

  • daxon omari
    July 26, 2012 @ 04:03:27AM

    BAINA YA MWENYEZI MUNGU WA MOHAMMED, AL-QAIDA, AL-SHABAAB NA YAWHEH MUNGU WA KWELI WA MTUME ELIJAH ... NDIYE WA HAKI WA KUABUDIWA NA KUTUMIKIWA...

  • wilfas
    July 3, 2012 @ 08:17:00AM

    Tumechoshwa na al-Shabaab na vikundi vingine. Tafadhaleni yeyote aliyeko Somalia amechoshwa wakati anapoamka na kuona miili ya maiti ambazo al-Shabaab wameua. Tafadhaleni TFG na KDF, tafadhaleni hakikisheni mtakapomaliza vita hivi hakuna yeyote aliyebaki nyuma kwa jina la al-Shabaab au al-Qaeda katika Somaliland.

  • cumar
    June 30, 2012 @ 03:12:38PM

    kkkkkk watu wanaomiliki tovuti hii wanashangaza hasa wakati wanaposisitiza kuwa hawapendelei upande wowote. Ahkkkkkkk. Nyinyi someni tu jinsi gani wanajieleza wenyewe:- (Tovuti inayoitwa Sabahi inagharimiwa na utawala wa Marekani huko Marekani hasa idara ya ulinzi ambayo ni dhamana wa kurejesha amani na mafanikio katika eneo hili.)

  • Muse Wariiri
    June 29, 2012 @ 07:35:20AM

    Kwa kweli, nimeshawishika na habari hii, hii ni kwa sababu kila mtu anajua kikundi potofu cha al-Shabaab kimekuwa kikichukua wake zao kwenye makazi huko mkoa wa Shabelle ya Chini. Licha ya hayo, wakati nguvu zao zitakapokwisha, na wao watamaliza. Hiyo maana yake ni kuwa Somalia itapata tena amani.

  • Kaamil
    June 26, 2012 @ 01:12:36PM

    Vijana wa Kiarabu na wa Kisomalia kwa hakika wanakabiliwa na matatizo kuhusiana na ugaidi na itikadi za al-Qaeda zinazoenea haraka na makosa mengine yanayoyafanywa dhidi ya jamii. Vijana wanashiriki katika shughuli hizi za uhalifu kwa sababu ya ukosefu wa ajira, kwa hiyo wanafanyakazi kwa ajili ya al-Qaeda ili kujipatia fedha. Wazazi wanatarajiwa kuwashauri watoto wao hasa vijana ambao akili zao zinaweza kubadilishwa kwa urahisi na kuwa magaidi. Kama wazazi wanashindwa kuwatunza watoto, wao basi watapoteza watoto wao kwa magaidi.

  • DEQA ADEN
    June 26, 2012 @ 10:12:54AM

    HABARI ZENU HAZIFAI NA HAMTHIBITISHI RIPOTI ZENU. HABARI ZENU ZINAONESHA KUWA NYINYI MNAPENDELEA UPANDE MMOJA KWA HIVYO NINAWAOMBA MSAHIHISHE MAKOSA YENU ILI MAONI ZAIDI YA WASOMAJI YAWAKILISHWE AU MTAWEZA KUUZA HABARI ZENU KWA KIASI CHA ASILIMIA 40 YA WASOMAJI.

  • Prof. Geedow
    June 26, 2012 @ 07:13:48AM

    Huu ni mfululizo wa maandishi kuhusu uchambuzi wa mabadiliko yanayotokea kusini ya Somalia, ambako waandishi wa habari wanajaribu wanavyoweza kutosheleza mahitaji ya habari kwa wasomaji wote. Ni muhimu kuwapatia wasomaji ripoti sahihi kuhusu matokeo ya kila siku ambapo mwandishi haelekei upande wowote bali kati na kati. Nimekuwa nikisikia kuwa vyombo vya habari havipendelei popote. Nafikiri mwandishi amesahau maadili ya uandishi habari. Ningependa kuwashauri waandishi wa habari kufungamana na sheria zinazotawala vyombo vya habari na kuwapatia wasomaji habari sahihi zisizo na alama za uongo.

  • MOSES MURIUKI
    June 23, 2012 @ 05:16:59PM

    Hongera majeshi ya Somalia na AMISOM. Hapa Kenya tunataka kuona amani nchini Somalia na serikali nzuri, watu wa Somalia ni dada na kaka zetu, hatutaki kuwaona wanateseka katika mikono ya AL-SHABAAB.

  • mulili
    June 21, 2012 @ 08:34:34AM

    Endeleeni.

  • martin kim
    June 21, 2012 @ 08:07:28AM

    Wekeni habari za mwisho... tunataka kuwamaliza al-Shabaab na kuwapa watu wa Somalia fursa ndogo ya kuwa huru na fursa kwa watu kufanikiwa na kuendelea pamoja na kaka na dada zao wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Dua zetu daima zipo pamoja na kaka yenu wa Somalia Martin Nairobi.

  • saleban ali
    June 21, 2012 @ 07:25:23AM

    Ningependa kuwasalimu nyote ..... Bila shaka, tunataka kuona al-Shabaab wanatokomezwa kutoka Somalia na nchi nyingine lakini swali ambalo mtu anapaswa kujiuliza ni, mapambano dhidi ya watu hawa ambao hatujui wanatoka wapi vitaendelea.......au ni mkataba ambao umeanza na kusitishwa tena ili kuendelea kwa miaka mingi?

  • Eng. Joshua Nyamai
    June 21, 2012 @ 06:32:17AM

    Mungu atawasaidia watu wake nchini Somalia.

  • wanyama evans
    June 21, 2012 @ 05:02:15AM

    Sio suala la mwisho wa vita dhidi yao, bali kutafuta suluhisho ili kubadilisha nia za uovu.

  • sorhe benson
    June 21, 2012 @ 02:55:15AM

    Itabidi walazimishwe kutoka nje ya Somalia ikiwa hawako tayari kujisalimisha.

  • cumar samaale geeddi
    June 21, 2012 @ 02:23:40AM

    Baada ya salamu napenda kuuliza, nani ambaye atachukua nafasi ya Al-Shabaab baada ya kuondolewa?

  • chumoanderschumo
    June 20, 2012 @ 03:11:23PM

    Inaonesha mafanikio na njia sahihi kuelekea kuhakikisha usalama wa Wasomali na serikali yao kwa vikosi vya KDF pamoja na kukuza morali wa kikosi cha KDF. Ongezeni juhudi KDF.

  • Hazim
    June 20, 2012 @ 02:58:52PM

    Mara tu al-Shabaab watakaposhindwa ndio hapo somalia itakapokuwa na amani na Wasomali wataweza kusonga mbele kuijenga nchi yao. Nchi nyingine za Afrika ya Mashariki pia zitakuwa katika amani kutokana na uharamia na zitaweza kufanya biashara ya kimataifa.

  • hassan fatah
    June 20, 2012 @ 02:00:42PM

    Kusitisha shughuli za ugaidi wa Al-Shabab kunapaswa kuwa kipaumbele cha juu cha serikali ya Somalia ili kuokoa maisha na kurejesha amani Somalia.

  • mimimimim
    June 20, 2012 @ 10:56:48AM

    Ua kikundi chote cha magaidi.

  • justine kimonge
    June 20, 2012 @ 09:22:15AM

    IKIWA SERIKALI YA YEMEN HAITAKUWA MAKINI, ITAKUWA ZAMU YAO

  • Alla yaqaan
    June 20, 2012 @ 08:22:41AM

    Amani iwe juu yenu. Kama utoaji wa taarifa hausimamiwi vizuri, ni dhahiri utakuwa na sifa na taarifa za uongo na zisizothibitishwa na njia bora ya usimamizi unapatikana katika kitabu kitukufu (Koran) cha Mwenyezi Mungu. Ningependa kuwaomba waandishi wa habari kuandika ukweli ili wasiuze habari za uongo kwa wasomaji. Kumbuka, siku moja mtaulizwa mbele ya Mungu kwa kile mnachoandika. Mcheni Mungu na thibitisheni mnachoandika.

  • DANIEL
    June 20, 2012 @ 06:20:47AM

    WASAMEHENI

  • mahamou
    June 20, 2012 @ 03:56:19AM

    Nimefurahi kwamba umenishawishi na ninakushuru kwa jambo hilo.

  • Kimwole Kiptiness
    June 20, 2012 @ 03:56:13AM

    Ninavipongeza vikosi vya kanda kwa juhudi zao kubwa za kuwavunja nguvu al-Shabaab. Siku za kikundi cha ugaidi nchini Somalia zimekwisha, Hawana chochote cha kutoa kwa watu wa Somalia. Sasa ninaliomba jeshi la AMISOM/Somalia kuwaendea magaidi huko miji ya mwambao ya Barawe na Marka na wale wanaokimbia wazuiwe kwa sababu kuwaruhusu kukimbia itakuwa kuahirisha tatizo. Watarejea na kuanzisha tena vita visivyoisha, Wale wanaojaribu kutoroka kwa baharini pia wazuiwe na jeshi la maji la Kenya na Umoja wa Ulaya nje ya mwambao wa Somalia. Endelea, endelea AMISOM ENDELEA.

  • yaxye
    June 20, 2012 @ 02:58:56AM

    Ninasikitishwa sana kuhusu madai ya mapambano yaliyoripotiwa na mtandao wa habari wa Sabahi Online wakati wote. Achaneni na utegemezi wa tetesi na thibitisheni taarifa zenu.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo