Juni 18, 2012
Awamu ya kwanza ya mradi wa reli za abiria jijini Nairobi iko njiani kuanza kazi ya kuchukuwa abiria mwezi ujao.
Mradi huo unadhamiria kupunguza msongomano katika eneo la Nairobi na kurahisisha upatikanaji wa usafiri wa umma kati ya eneo la kibiashara la kati ya mji na maeneo ya ng’ambo ya mji mkuu huo wa Kenya.
Kwa mujibu wa wizara ya usafirishaji ya Kenya, mradi huo unaogharimu shilingi bilioni 24 (dola milioni 283) umegawanywa katika awamu nne, ukiunganisha wilaya ya kati na miji ya Syokimau, Ngong, Kiserian Kikuyu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, kwa mujibu wa Wizara wa Uchukuzi.
Mradi huo unajumuisha kuzitengezea njia za reli zilizopo, kuboresha vituo, alama za barabarani na vifaa vingine, ununuzi wa magari mapya ya reli na utanuzi wa huduma za reli mpaka uwanja wa ndege.
Awamu ya kwanza ya mradi – barabara ya kilomita 2.2 kuunganisha kituo cha reli Syokimau na kituo kikongwe cha Embakasi – ilikamilishwa tarehe 30 Mei.
Reli ya Syokimau-Wilaya ya Kati inatarajiwa kuanza shughuli zake za kibiashara mwishoni mwa mwezi Julai, ikigharimu jumla ya shilingi milioni 200 (dola za Kimarekani milioni 2.4) na ikitegemewa kuchukua abiria 10,000 itakapokamilika.
Waziri wa Uchukuzi wa Kenya, Amos Kimunya, alisema kituo cha reli cha Syokimau kitafika mpya kuondosha msongamano mjini na kuimarisha sekta ya usafirishaji.
“Tutahakikisha kuwa kuna kiwango cha juu cha treni zinazofanya kazi kila siku kukidhi matakwa ya wasafiri,” alisema baada ya kuchagua kituo hicho hapo Mei, kwa mujibu wa gazeti la The Star la Kenya.
“Hutalazimika tena kuganda tena kwenye foleni kwa masaa mengi,” alisema.
Reli hiyo ya Syokimau-Wilaya ya Kati ni reli ya mwanzo kujengwa nchini Kenya tangu Vita vya Pili vya Dunia. Njia ya mwanzo ya reli iliyojengwa na Waingereza kati ya mwaka 1896 na 1901, inatoka mji wa bandari wa Mombasa hadi Kisumu kupitia fukwe za Ziwa Viktoria. Nyongeza mpya itaunganisha barabara mpya katika kituo cha treni cha Nairobi katika wilaya ya kati.
Meneja Mkurugenzi wa Shirika la Reli la Kenya, Nduva Muli, aliwaambia waandishi wa habari mwezi uliopita katika safari ya mwanzo ya uzinguzi kutoka Syokimau kwenda mji mkuu, kuwa ujenzi wa awamu nyingine tatu zilizobakia utaanza mwakani.
Serikali inafikiria kuupa fedha uwanja wa ndege kufadhili sehemu iliyobakia ya mfumo huo wa usafiri wa treni, baada ya mpango wa dhamana wa shilingi bilioni 17 (dola milioni 20) kushindwa kufanya kazi, kwa mujibu wa gazeti la The Standard la Kenya.
Mara tu utakapofanikiwa mfumo mzima wa reli utakuwa na uwezo wa awali wa kuwasafirisha abiria 170,000, kwa mujibu wa InfraCo Africa, ambayo imekuwa ikifanya kazi na shirika la reli la Kenya kwenye mradi huo tangu mwaka 2009.
InfraCo ilisema mradi huo utafungua fursa mpya kwa ajili ya ajira na makaazi na utatoa usafiri wa uhakika kwa wakaazi wa mji huo na wageni. Wafanyabiashara wanaosafiri watafaidika na huduma ya usafiri wa moja kwa moja kutoka uwanja wa ndege hadi kitovu cha mji.
Mtandao wa reli wa kisasa ni sehemu ya mpango wa maendeleo wa Dira 2030 wa Kenya, na sehemu ya juhudi za sasa za serikali kuiimarisha huduma ya usafiri katika nchi. Miradi mingine mikubwa ya hivi karibuni inajumuisha barabara kuu ya Thika, barabara kuu ya Nairobi-Mombasa na utanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Martin Gateri, mhandisi na mshauri kwa makampuni binafsi na serikali juu ya miradi ya miundombinu, anasema mradi huo wa reli utaufanya mji wa Nairobi kuwa wa kisasa, akiufananisha na miji mikubwa ya kimataifa ambako usafiri unafanyika kupitia treni zinazotembea kwa kasi.
“Mradi huu ni muhimu sana kwani unakusudiwa kuondosha msongomano barabarani na kuupa mji taswira nzuri kwa kuanzisha njia rahisi na yenye ufanisi ya usafiri kwa ajili ya mji huu unaokuwa haraka.” Gateri aliiambia Sabahi.
Ingawa kumekuwa na wasiwasi kuhusu uhamishwaji wa watu wanaoishi katika eneo litakalotumia kujenga njia mpya ya reli, Gateri alisema kujitolea sadaka ni lazima kwa kupatikana maendeleo.
“Ujenzi wa reli nchini Uingereza mwaka 1880 uliifungua nchi na kuweka msingi wa kuifanya jamii yao kuwa ya kisasa,” alisema. “Kujenga njia mpya ya reli nchini kote ni moja ya hatua za kwanza ya Kenya kuinua [watu wenye kipato cha kati] taifa,” alisema.
Mwanauchumi Tiberius Barasa alisema kuwa treni mpya zitasaidia kupunguza msongamano jijini, lakini faida za uchumi hazina uhakika sana.
“Faida ya njia hii ni kuwa itapunguza msongamano katika barabara kuu zinazoelekea ndani na nje ya mji, pamoja na kupunguza wakati ambao waendeshaji hukaa katika msongamano wa barabarani,” alisema. Hata hivyo, kiuchumi, faida zitakuwa kidogo, kwa vile njia za reli zitakuwa fupi sana kwa kasoro ya kilomita 30.”
Kwa mujibu wa Wizara ya Uchukuzi, njia ya Kituo cha Reli reli cha Syokimau-Nairobi kitakuwa na urefu wa kilomita 20.
Kuzalisha faida za maana aa kiuchumi, Barasa alisema mfumo wa reli inahitaji kufika miji ziliko mbali ya mji mkuu, kama vile Eldoret, Nakuru na Machakos, ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na kukuza biashara.
Francis Gichuki, mhandisi wa sayansi ya kimazingira katika Chuo Kikuu cha Nairobi, alisema njia mpya za reli zitaleta baadhi ya mafanikio ya kimazingira.
Gichuki aliiambia Sabahi kuwa reli ambazo Shirika la Reli la Kenya zinatumia ni za zamani na si rafiki wa mazingira kuliko treni mpya kabisa katika soko. Hata hivyo, alisema athari za kimazingira za treni kongwe bado ni kidogo kuliko matumizi ya gari.
Mradi huu utafanikiwa zaidi ikiwa nchi itamudu kuweka injini za kisasa zenye kutoa hewa chafu kidogo, Gichuki alisema. Alisema hii itasaidia maendeleo ya kimazingira, kwa vile mfumo mpya ulio safi na wenye uwezo ni muhimu katika kupunguza hewa chafu na matumizi ya mafuta.
Wizara ya Usafiri wa Anga ya mkoa wa Somaliland siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni) iliikataza ndege...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata makamu wanne wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Ma...
Watu wenye silaha kwenye Kaunti ya Wajir walimuua polisi mmoja wa akiba wa Kenya siku ya Jumanne ...
Japan inaipa Tanzania dola milioni 49 (shilingi bilioni 80.4) kama msaada na mkopo kwa ajili ya k...
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo yeye pekee yake amewateua na kuwapangia kazi maafisa wa...
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumanne ilimkubalia Makamu wa Rais wa Kenya Willia...
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Tusubiri na kuona. Pengine ni matangazo zaidi kuliko kile kilichoko uwanjani. Pesa lazima zipatikane na tayari zimeshatumia vibaya. Angalieni eneo hili.
Kenya ni nchi mabayo ina uwezo mkubwa na mustakabali wake unaonekana kung’ara kwa sababu ya mambo yafuatayo. Katiba yao mpya imegawanya madaraka na kuwawezesha watu ili kufanya chaguo juu ya vipi waongozwe. Hii itawafanya wawakililishi wao kuwa wakali zaidi katika kupatiwa huduma kwa watu. Karibuni Kenya imegundua mafuta kaskazini ya nchi na wakati mafuta haya yatakapoanzwa kuchimbwa Kenya itakuwa msafirishaji mkubwa wa mafuta kwa nchi jirani na hili litakuza uchumi mara kumi zaidi. Sasa wawekezekaji zaidi na zaidi wanakuja nchini na kujihusisha na shughuli kubwa za kiuchumi kama vile kuanzisha miji ya Konza na Tatu. Kumekuwa na uboreshaji mkubwa katika miundo mbinu kama vile barabara na reli. Kenya pia imewekeza katika uboreshaji wa kilimo chake na kugharimia elimu bila ya malipo kwa wote. Serikali ya Kenya imeanzisha shughuli nyingi za kuwakaribisha wafadhili kugharimia miradi mikubwa ambayo itaongeza fursa za ajira na uchumi.
Kuna treni mpya ya abiria ambayo uko njiani na itaunganisha miji kadhaa na mji mkuu na hii itakuwa na athari za moja kwa moja kwa uchumi wa Kenya na hatimaye itaimarisha njia ya maisha ya watu. Treni ya abiri itakuwa rahisi kuliko njia yoyote ya usafiri kwa maana ya kuwa watu wataweza kutumia pesa kidogo zaidi wanapokwenda kazini. Reli hazisababshi msongamano kwa hivyo watu wengi wataweza kufika kazini kwa wakati na watatumia wakati wao kwa ufanisi. Treni ya abiria pia zitawawezesha wafanya biashara kusafiri miji tofauti ili kufanya shughuli ambazo zitakuwa na faida kwa uchumi wa Kenya. Treni zitatoa fursa za ajira kwa mamia ya watu wasio na ajira nchini, jambo ambalo badala yake litakuza uchumi. Pia kutakuwa na majengo yatayojengwa katika vituo vya reli na kupatikana kwa fursa nyingi za biashara.
Makala nzuri, hakuna mbadala wa ufanisi ulioundwa na mfumo mpana wa reli. Sehemu nyingi za vijijini ziko nyuma kwa sababu thamani ya viwanda haiwezi kuondoshwa kutoka kule liliko soko kubwa la walaji, na huko ni Nairobi na Mombasa. Reli itakuwa suluhisho la mwisho la suala hili, na hata masuala ya uchimbaji viwanda vyingine vikubwa, reli inatoa fursa nyingi katika masula ya uchumi mkubwa. Mchango mwingine muhimu ungekuwa katika uwekezaji wa usafiri wa reli za kasi, na kasi tunayozungumza hapa ni kilomita 120 kwa saa ambayo itafanya vizuri sana. Kwa hivyo mnaweza kufika hadi ndani sana na kuruhusu kazi kuendelea haraka na kwa ufanisi panapohitajika. Kwa hivyo, mimi ninayeishi Nakuru au eldoret na kusafiri kwenda Nairobi au Nyeri au Namangana na Biashara siku hiyo hiyo. Ikikamilika tu kila mmoja atafaidika, tofauti zitakuwa ndogo sana hapo mwanzo lakini kuendelea mfululizo kunajenga faida kubwa.
Kimunya lazima ajifunze namna ya kufanyakazi kwa ufanisi katika wizara yake na kufanya chochote, kutopata malipo na kutofanya kazi hakuwezi kupunguza ajali?