Juni 13, 2012
Timu ya Abaarso Tech iliishinda Prison Corps kwa vikapu 36-25 katika mchezo wa mwisho wa mashindano ya mpira wa kikapu ya wiki mbili ambayo yalimalizika Jumatatu (tarehe 11 Juni) huko Somaliland.
Mashindano hayo yaliandaliwa na Wizara ya Vijana, Michezo na Utamaduni na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Somaliland, na kudhaminiwa na Mercy Corps kwa ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Marekani kwa ajili ya Maendeleo (USAID).
Waziri wa Vijana, Michezo na Utamaduni wa Somaliland Ali Said Raygal alisema mashindano hayo yalikuwa sehemu ya juhudi za wizara za kuimarisha michezo Somaliland na kusaidia kujenga uwezo wa vijana kimwili na kiakili.
Mashindano hayo yalikuwa ya kwanza ya aina yake Somaliland tangu serikali kuu ya Somalia kuanguka miongo miwili iliyopita, kwa mujibu wa mkurugenzi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Somaliland, Mohamed Abdullahi Qodah.
Alisema mashindano hayo yalikuwa na “umuhimu mkubwa kwa sekta ya michezo ya Somaliland”.
Timu sita zilishiriki mashindano katika Uwanja wa Timo Adde: Abaarso Tech, Prison Corps, SOHASCO (shirika la ndani lisilo la kiserikali), Chuo Kikuu cha Alpha na timu mbili zilizowakilisha vijiji vya Mohammad Moge na Jigjiga-yar huko Hargeisa.
“Lengo la mashindano ilikuwa ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika michezo kwa sababu kujumuika ni muhimu kwa kukuza kiwango cha michezo [katika jamii],” Qoodah alisema. “ Tutajaribu tuwezavyo ili kuwahamasisha vijana kushiriki katika michezo ili kuwaepusha na kujihusisha na vitendo vya kigaidi na matumizi ya madawa, vitu ambavyo ni tatizo kwa Somaliland.”
Sherehe za ufungaji zilihudhuriwa na Waziri wa Vijana, Michezo na Utamaduni, Kamishna wa Magereza Mohamed Hussein Farah, Katibu Mkuu wa Wizara ya habari ya Somaliland Mohamed Hussein Farah, Mkurugenzi Mkuu wa Waziri wa Vijana, Michezo na Utamaduni Mustafe Mohamed, na mkurugenzi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Somaliland na mashabiki wa mpira wa kikapu.
“Katika mashindano yoyote, moja ya timu mbili hushinda, na huifanya timu iliyoshindwa kujaribu zaidi ili kushinda katika mashindano yajayo,” Raygal alisema katika hotuba yake wakati wa maadhimisho ya ufungaji.
Naye kamanda wa timu ya Prison Corps aliipongeza timu ya Abaarso Tech kwa ushindi. “Tutajaribu kadri tuwezavyo kushinda katika mashindano ya mwaka ujao na nitaimarisha timu yangu,” Farah alisema.
Raygal alikabidhi kombe la ushindi kwa timu ya Abaarso Tech na kuwapongeza. Pia alikabidhi sare za michezo kwa wachezaji wawili, mchezaji aliyeshinda vikapu vingi wakati wa mashindano na mchezaji bora katika mashindano.
Raygal alisema wizara inapanga kujenga viwanja zaidi vya michezo ili kuwapa vijana fursa ya kushiriki katika aina tofauti za michezo na kuwahamasisha wapende michezo zaidi.
“Ninapenda kuyaomba makampuni binafsi na mashirika ya ndani na ya kimataifa kutusaidia kutekeleza mipango hii,” alisema.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Ninaipongeza timu ya Abaarso kwa kushinda kombe.
Nimefurahi kweli kwa Abaarso kushinda kombe na wakati huo huo kuwataka waendelee na moyo huo huo.
Ningependa kuipongeza timu ya Abaarso Tech ambayo ilishinda mashindano hayo. Kwa kweli wamefanya vizuri sana. Naamini kuwa haya ni maendeleo mazuri ambayo yanawapatia fursa vijana kuondokana na kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya na dhidi ya wale wanaowapa sumu ya itikadi za kupotosha.
Inahamasisha kusikia habari kuwa vijana wa Somalia mnajishughulisha na michezo ili kujiepusha na uovu wa kutumia madawa ya kulevya au shughuli za KIHALIFU.